Dizasta Vina – A Confession of a Mad Man Lyrics
LYRICS

Dizasta Vina – A Confession of a Mad Man Lyrics

AUDIO Dizasta Vina - The Verteller Album MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – A Confession of a Mad Man Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled A Confession of a Mad Man, a number four song from his album titled The Verteller Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Tatuu ya Asili

A Confession of a Mad Man Lyrics by Dizasta Vina

Ah Nakumbuka aliniambia akiniona mimi anaona upendo
Anaona nchi ya ahadi anaona pepo
Anaona future ya maisha anaona lengo
Akiniangalia anaona kesho, n’kashangaa sana

She had her game tight
Kwani licha ya aibu, alionyesha feeling that she can’t fight
Alikuwa tayari hata kunipa game night
Akiuliza “don’t you believe love in a first sight

Nikamwambia “mbona una kasi ya jini?
Akacheka, akasema “brother wasi wa nini?” Akideka
“We ni handsome, na pia ni mpole
Mchizi ka’ wewe unahitaj manzi ka’ mimi” nikawaza

Alikuwa ana ‘summer body times two
Mi’ machoni nilimtamani ila ni nafsi tu
Ndo’ inagoma akanishika sikio akanong’ona
Kwa mahaba akisema “dude i love you

And then she called me names, mara ‘Babes
Mara ‘Boo boo
Akipitisha nails kwenye chuchu ah
Hata waungwana kwenye meza ya pembeni wakashangaa
Wakauliza “damn bro una juju

Akataka anibusu n’kakataa kimtindo akanuna
Akala mingo akanibusu kwenye shingo n’kaguna
Akauliza “we umeoa?” Nikasema “No
“Kwanini hunipendi!!?” Nikasema “dada nakuonea huruma

Akahamaki “huruma ya nini boy!? Una vibinti bar
Achana navyo ili niku-treat kama minister
Hivi jinsi navyokupenda hauhisi raha
Kwanini usikubali tuwe wote what’s so difficult

“Unaonyesha walakini unan’shangaza
Au pengine una ukimwi unaogopa kuusambaza
Nikamwambia “sikia, najua kunielewa sio simple
Mi’ nachinja watu nauza moyo na figo
Akacheka kwa mashauzi ya ‘kinafki’ ‘nafki
Ilikuwa ni wazi ali-doubt doubt
Akasema “labda bro’ hauna kazi
Hiyo mioyo na figo ukichinja unauza wapi

Nikamwambia “calls nyingi zinaingia
Kila pande za nchi hizi pieces wanazivia
Mtandao unakua kila pande za jiji napopitia
Na-expand treats mpaka India

Akacheka sana, mpaka akaniegemea
Wakati peke yangu kichwani najisemea
“Dada angejua kitachokwenda kumtokea
Angebeba pochi yake angetembea, angekwenda mbali

Nikamwambia “nenda nyumbani usigeuke nyuma
Kalale kesho nenda ibadani katoe ushuhuda
Nakupa nafasi ya kuishi ipokee uujuze umma
Kaandike kumbukumbu kuwa umenusurika kufa

Akasema “sio mbaya nzi kufia kwenye kidonda
Usiniache mimi maana nahofia kukonda
Nakupenda sana please niweke moyoni hapo
Ukiwa muuaji n’tafurahi kufa mikononi mwako

Hakutaka kusikia mambo mengi
Kama bidhaa ameshailipia na sasa anasubiria “change
Kwa lugha ya nje ya dunia macho sexy
Akanikaribia kisha akani-kiss passionately, ah

“Do you have a car or some’ brother
Translation akiuliza ka’ n’na gari labda
Nilipomwambia mi’ muuaji aligoma
Akaniambia twende home kisha akanidandia kifuani ghafla

Ile nafsi bado inanikemea
Najikuta peke yangu kichwani najisemea
“Binti angejua kitachokwenda kumtokea
Angebeba pochi yake angetembea angekwenda mbali

Kivivu tukazama kwenye Harrier
Safari kwenda home bila barrier
Baada ya nusu nikampa mvinyo wa baridi wa kiitalia
Na ndani yake nikaweka Valium

Akapiga fundo kisha akaweka glasi mezani
Akatabasamu akasogea hadi jirani
Akaweka mkono wake begani
Kisha kiudadisi akaniuliza honey hujaniambia
Unafanya kazi gani

Nikamuonyesha picha za mademu kama mia
Niliowachora akasema “baby we’ ni genius
Nikamwambia “niliowachora nishawachinja you’re the next one” akasema
“Baby haupo serious

Aliniimbia wimbo maneno yakikata kinywani
Ishara ya kwamba kimtindo dawa imeshapanda kichwani
Nikambeba kisha nikampeleka mpaka chumbani
Hakukuwa na kitanda zaidi ya meza nikamlaza mezani

Nikamchora, nikimtizama mwili wake wa mvuto
Huki nikiwaza “unapopenda ukubali majuto
Nikampiga busu zito kwenye paji la uso
Kisha nikatoa visu vikali na nyundo

Dizasta Vina – A Confession of a Mad Man Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment