250 Investigation Officer Jobs at PCCB (TAKUKURU) Inviting Applicants
E NEWS

250 Investigation Officer Jobs at PCCB (TAKUKURU) Inviting Applicants

250 Investigation Officer Jobs at PCCB (TAKUKURU) Inviting Applicants
250 Investigation Officer Jobs at PCCB (TAKUKURU) Inviting Applicants

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

1.0 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
(TAKUKURU) anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kuajiriwa katika
nafasi za kazi zifuatazo kujaza ofisi za Wilaya:

1.0 AFISA UCHUNGUZI (NAFASI 250)
1.1 Sifa za Mwombaji:

1.2 Sifa za Kitaaluma:

  1. Muombaji awe angalau na elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa
  2. na chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
  3. Tanzania katika fani zozote kati ya hizi: Sheria, Uhasibu, Kodi,
  4. Sayansi ya Kompyuta, Sayansi ya Uhalisia, Ununuzi, Uchumi,
  5. Mipango, Usalama wa Mitandao, Takwimu, Ukadiriaji wa
  6. Majenzi, Uhandisi wa Umeme, Usanifu wa Majengo, Uhandisi wa
  7. Ujenzi, Uhandisi wa barabara na Uhandisi wa Maji, Saikolojia,
  8. Ushauri na Unasihi;
  9. Muombaji awe na ufaulu wa kuanzia daraja la pili la chini (lower second class).
  10. Waombaji waliosajiliwa na Bodi za Kitaaluma watapewa kipaumbele zaidi.
1.3 Sifa zingine:
  1. Mwombaji ni lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri usiozidi miaka 30.
2.0 MCHUNGUZI MSAIDIZI (NAFASI 100)
2.1 Sifa za Mwombaji:

2.2 Sifa za Kitaaluma:

  1. Awe na cheti cha elimu ya Kidato cha nne (CSE) au Kidato cha sita
  2. (ACSE), Astashahada au Stashahada ya fani yoyote inayotolewa na
  3. Taasisi au chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya
  4. Muungano wa Tanzania, pamoja na fani kama vile Mafunzo ya JKT
  5. na stadi za ulinzi, Ufundi wa magari, uchomeleaji na upigaji rangi za
  6. magari, Umeme wa magari, Udereva, Usaidizi wa ofisi na Mapokezi,
  7. uhasibu wasaidizi, Katibu Muhtasi/Mwandishi Mwendesha ofisi.

2.3 Sifa zingine:

  • Mwombaji ni lazima awe raia Tanzania na mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 25.
3.0 MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI WOTE
  1. Waombaji wanapaswa kuwa waadilifu na wasiokuwa na rekodi ya uhalifu;
  2. Waombaji waambatishe nakala zilizothibitishwa za vyeti vya kitaaluma na
    nyaraka nyingine ikiwamo nakala za vyeti vya kumaliza masomo katika
    ngazi mbali mbali za masomo;
  3. Waombaji wawe wamepitia mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa.
  4. Waombaji wawasilishe nakala zilizothibitishwa za vyeti husika vikiwamo
    vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya elimu, vitambulisho vya Taifa (NIDA) au namba
    ya usajili wa vitambulisho vya Taifa, picha ndogo moja n.k;
  5. Shuhuda za walimu, wahadhiri au waajiri kuhusu uwezo wa muombaji
    kimasomo au kiujuzi ama uzoefu na ufanisi wake katika kazi, nakala za vyeti
    vya taaluma zisizokuwa kamilifu na slipu za matokeo ya mitihani
    hazitapokelewa;
  6. Vyeti vilivyotolewa na Bodi za Mitihani za nje ya Tanzania vya elimu ya
    Kidato cha nne (CSE) au elimu ya Kidato cha sita (ACSE) vinapaswa
    kuthibitishwa na Baraza la Mitihani ya Taifa la Tanzania (NECTA);
  7. Vyeti vilivyotolewa na Vyuo Vikuu vya nje ya Tanzania vilivyothibitishwa na
    Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) vitapokelewa;
  8. Waombaji wanapaswa kuambatisha Maelezo Binafsi (CV) kuhusu elimu,
    ujuzi na uzoefu wa kazi ya hivi karibuni na yenye anuani ya makazi, anuani
    ya posta, baruapepe na namba za simu za mkononi zinazofikika kwa
    mawasiliano;
  9. Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya waombaji watakaowasilisha vyeti
    vya taaluma vya kughushi na taarifa za uongo katika Maelezo Binafsi (CV);
    10.Waombaji wanatakiwa kuwasilisha majina matatu ya wadhamini na namba
    za mawasiliano zinazopatikana na nakala moja ya picha ya hivi karibuni ya
    kila mdhamini;
    11.Waombaji waliowahi kuajiriwa katika Utumishi wa Umma na kuachishwa
    kazi kwa sababu zozote zile wasiwasilishe maombi;
    12.Barua za maombi ziandikwe kwa mkono katika lugha ya Kiswahili au ya
    Kiingereza;
    13.Waombaji ambao ni waajiriwa katika Taasisi za Serikali wapitishe maombi
    kwa waajiri wao wa sasa.
    14.Waombaji watakaokidhi vigezo vya awali vya sifa na matakwa ya maombi
    ndiyo pekee watakaofuzu kuingia katika hatua nyingine za mchakato huu
    wa ajira.

ANGALIZO:

  1. Waombaji wote watambue kuwa ikitokea wameajiriwa watapangwa
    kwenye kituo chochote cha kazi kadri ya uamuzi wa Mkurugenzi
    Mkuu.
  2. Cheti cha uanachama wa Klabu ya Wapinga Rushwa kitakuwa na
    faida ya ziada.
4.0 JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI
  • Maombi yote yatumwe kupitia mfumo wa kielekitroniki wa ajira wa TAKUKURU ambao anuani yake ni: www.pccb.go.tz/ajira na si vinginevyo. Maombi yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kwa mkono hayatapokelewa.
  • Barua za maombi ya ajira ziandikwe kwa Anuanwi;
  • Mkurugenzi Mkuu,
  • Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa,
  • Mtaa wa Jamhuri,
  • S.L.P. 1291,
  • 41101 DODOMA.

MWISHO WA KUTUMA MAOMBI: Tarehe 20 Februari, 2024

Leave a Comment