Harmonize – Utanikumbuka Lyrics
High-rated Tanzania recording artist, multi-award winner, and Konde Music WorldWide serial hitmaker Harmonize released a new hit song titled Utanikumbuka, a number six song from Made for Us Album.
SIMILAR: Harmonize – Nitaubeba
Utanikumbuka Lyrics by Harmonize
Big Boy On The Beat
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Ooh Aah
Ooh Aah Aaah
Natamani kuimba
Pengine ukasikia
Maneno yangu ya mwisho
Ila sauti ndo inagoma
Yani kama inakwaruza
Huruma
Ukinitazama machoni yamevimba
Nimekesha nalia
Na sijui lini mwisho
Mwili wa joto na homa
Yani mpaka naunguza
Mapenzi hayana dhihaki
Mwenzako nishawaza hadi faraki
Ama niende kortini nikashitaki
Kwamba unadhulumu furaha yangu
Mdomoni una maji we samaki
Sa mbona hata kusema hutaki
Ama ndo unataka sitaki
Ina maana huzioni jitihada zangu
Pengine donda nililokupa
Limefuta upendo unajaribu kujilazimisha
Mengine unafanya kuniridhisha
Mwili umekonda umebaki mifupa
Kulilia upendo basi moyo rudisha
Kama umenisamehe na yameisha kinyonge
Ninajiuliza bila majibu
Wapi ninapoharibu
Kila ninachojaribu
Hakikupendezi
Utanikumbuka mpenzi uta
Utanikumbuka mpenzi uta
Maana wapo watakaokukosea(Utanikumbuka mpenzi uta…)
Na wasikiri kosa
Muda wote wanawaza kukuchezea
Hakuna wa kukuposa
Eeh eeh
Inaboa mapenzi yakishaisha
Licha ya kujitoa
Mwenzangu kumridhisha
Eti mara yupo bize yupo bize
Alipo hataki nimuulize
Anajua lazima iniumize
Imeandikwa samehe na usilipize
Huenda hata msamaha ulionipa ni kazi bure
Kama umeshindwa nifanya
Nijione kama yule Rajabu wa zamani
Rudi Ma unipe joto
Hili baridi kama Toronto
Si ulijiita Kurwa mi Doto na utanipa watoto
Sa mbona sikuoni
Ninajiuliza bila majibu
Wapi ninapoharibu
Kila ninachojaribu
Hakikupendezi
Utanikumbuka mpenzi uta
Utanikumbuka mpenzi uta
Maana wapo watakaokukosea(Utanikumbuka mpenzi uta…)
Na wasikiri kosa
Muda wote wanawaza kukuchezea
Hakuna wa kukuposa
Eeh eeh
Konde Boy Call Me Number one, Bakhresa
Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka
Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka
Na sikuombei mabaya(Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…)
Ooh Mabaya
Na sitakusema vibaya(Uuh Uuh Uuh Utanikumbuka…)
Uso umeumbwa na haya
Uncle Duke unipigie ukinikumbuka
Harmonize – Utanikumbuka Mp3 Download
More hit songs from Harmonize;