LYRICS

Dizasta Vina – Waridi Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Waridi Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Waridi, a number eight song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Hatia V

Waridi Lyrics by Dizasta Vina

Waridi na baba yake hazikuiva
Mzee alimtia hofu waliweka distance
Waridi alificha yaliyonisibu kwenye kichwa
Tension kubwa mfano wa maadui baada ya vita

Na alishazoea mzee kumkemea
Ilikuwa adimu sana kuona baba anamchekea
So, kila mzee wake aliporudi alijificha
Kwani mtoto kumwogopa baba ilikuwa sifa

Alipopata shida alikaa kimya alitunza
Alikosa jibu alivunga
Hakuwa na mtu wa kuzungumza
Alisema siku… nitakuwa mkubwa nitahama nyumba

Maswala ya shule ndio yalikuwa maongezi pekee
Alipewa ada ilipofika tarehe
Simu za mdingi yake ziliharibu sherehe
Binti aliukosa upendo wa mzee, ilikuwa ni wazi

Waridi alihama nyumba kwenda kuanza chuo
Akawa huru kula kunywa kuchangua nguo
Ndipo akagundua milango mipya ya ulimwengu
Akafurahi, walimwengu wakampa funguo

Akapiga picha Dar nzima
Akaijua Posta, Sinza Palestina
Akajua kuna zaidi ya kupika na kufua
Mzazi alimficha dunia ikamfundisha asiyojua

See upcoming rap shows
Get tickets for your favorite artists

You might also like
Tribulation
Dizasta Vina
Lose Yourself
Eminem
Mockingbird
Eminem

Akatokea Baba mwenye fedha msitu
Akamjali, akawa anamsikiliza kila kitu
Akamkumbatia kusema Waridi I miss you
Naye akafurahi kwakuwa ana daddy issues

Huyu mzee hakumfukuza sebuleni
Hakugomba alipofeli aliyofunzwa shuleni
Alimwacha huru kuvaa mapambo ya mwambao
Akamnunulia simu mixer bando za mtandao

Akamwacha huru baada ya nyumbani kuwa mtumwa
Alimgawia sehemu ya matunda aliyoyachuma
Waridi alilala bila kurushiwa stimu
Mzazi alivuta waya hakupokea simu

Mazoea yakawa tabia, tabia ikawa hali
Akamupa mwili na hisia kila aliyemjali
Amani ya kitu kidogo ikamvuta
Hakuzuga, Waridi hadi masomo akavuruga

Waridi aliruka na wazee
Waridi alishazuzuka na bazee
Aliukumbuka sana ule ukali wa mzee wake
Alighafirika sana na hakutaka uendelee

Hakurudi nyumbani wazazi walipata homa
Alifata kumbatio Mwanza na Dodoma
Wazee walimpa Chips Mayai na Nyama Choma
Akamnunulia gari akamwambukiza ngoma

Mimba juu binti akageuka Single Mother
Dunia ikamwonyesha Waridi jinsi ilivyo fasta
Cycle ikaendelea, trauma juu ya trauma
Drama juu ya drama na Depression ikam-mendea

Muunganiko wa huu upepo ukaleta tufani
Sababu ya upendo mdogo alioukosa nyumbani
Baba jinyoshee kidole mtoto akikosea
Mpende akuheshimu akikuogopa tu amepotea

Dizasta Vina – Waridi Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment