Diamond Platnumz kulipia familia 500 kodi za nyumba miezi 3.
E NEWS

Diamond Platnumz kulipia familia 500 kodi za nyumba miezi 3.

Diamond Platnumz kulipia familia 500 kodi za nyumba miezi 3.
Diamond Platnumz kulipia familia 500 kodi za nyumba miezi 3.

Kupitia account yake ya Instagram, Star wa muziki wa kizazi kipya anayetamba kwa wimbo wake mpya “Jeje” Diamond Platnumz ametangaza rasmi kwamba shida za watu wa jamii yake ni zake.

Katika post hiyo Diamond Platnumz amefunguka kuhusu janga la Corona ambalo linaikumba dunia kwa sasa na yuko tayari kulipia kodi za nyumba ya miezi mitatu kwa familia 500.

Alisema japo kuwa na yeye ni miongoni ya walioathirika na janga hilo lakini bado yuko tayari kusaidia jamii yake katika kile kidogo ambacho Mungu amempa.

Utarituba wa namna ya kupata misaada hiyo utatolewa rasmi jumatatu hii..

Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara…. nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…

Ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…

Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….

Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba….🙏🏼 HiliNaloLitapita #ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona – Aliandika Diamond Platnumz

Leave a Comment