Mchina Akamatwa na Vifaa vya Staelink
E NEWS

Mchina Akamatwa na Vifaa vya Staelink

Mchina Akamatwa na Vifaa vya Staelink
Mchina Akamatwa na Vifaa vya Staelink

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na kikosi kazi maalum cha kuzuia na kupambana na matumizi ya makosa ya kimtandao kimeendelea na kazi ya ufuatiliaji na kufanikiwa kwa mara nyingine kuwakamata Claudian Makaranga (28) Mkazi wa Kawe, Kinondoni na Hongliang Yang (35) Mchina, Mkazi wa Kigamboni, kwa tuhuma za kuingiza vifaa vya mawasiliano ya intaneti Nchini bila kufuata utaratibu wa kisheria vyenye jina la STARLINK KIT/DEVICE.

SIMILAR: Manula azindua duka la vifaa vya michezo

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam akiongea leo amesema “Watuhumiwa hao wamekuwa wakijitangaza kuuza vifaa na kutoa huduma ya intaneti Nchini kupitia
Instagram kwa akaunti yenye jina la STARLINK, baadhi ya vifaa vilivyoingizwa Nchini imebaika vilishauzwa na kutumika katika baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam kitendo ambacho ni kosa na kinyume na sheria kwani havijaidhinishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)”

“Vifaa vilivyokamatwa ni Starline Dish 12 na Starlink Router 12 , Polisi Kanda Maalum ya Dar inatoa wito kwa Wananchi kuwa makini na matumizi ya vifaa vya
mawasiliano ambavyo havijaidhinishwa na mamlaka husika”

SIMILAR: Krystyna wa Czech ashinda miss world 2024

Itakumbukwa mwezi February mwaka jana Boss wa Makampuni ya SpaceX, Tesla na Twitter, Elon Musk alisema kilichobaki kwenye mpango wake wa kuuleta mradi wa Starlink Tanzania ni kibali tu kutoka kwenye Serikali ya Tanzania, hata hiyo Waziri Nape amesema walishajibiwa na watakapokamilisha documents wataruhusiwa kuingia Nchini.

Source: Millard Ayo

Leave a Comment