E NEWS

Mjengo wa Christian Bella noma amedai msingi tu ni Milioni 100.

Mjengo wa Christian Bella noma amedai msingi tu ni Milioni 100.

Msanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva na Mbalax, Christian Bella, amezua gumzo mitandaoni baada ya kufichua kuwa msingi wa nyumba yake mpya umegharimu takribani shilingi milioni 100 pekee – na ujenzi bado unaendelea!

SIMILAR: Navy Kenzo kuja na Album Mpya Hivi Karibuni

NI Headlines za msanii kutokea kwenye muziki wa Dansi, Christian Bella ambae time hii ametuonesha mjengo wake na amedai kuwa msingi wa  nyumba hiyo ni Milioni 100,

Christian Bella, anayejulikana kwa vibao kama Nashindwa,” “Olla,” na “Yako Wapi Mapenzi”, ameendelea kuonyesha mfano wa msanii anayetumia kipato chake kwa uwekezaji wa maana.

Mbali na muziki, amekuwa akijihusisha na biashara mbalimbali, ikiwemo real estate na miradi ya familia.

Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa kupitia mahojiano na vyombo vya habari, Christian Bella amesema nyumba hiyo ni moja ya miradi yake mikubwa binafsi, akisisitiza kuwa hakupenda kutumia nguvu nyingi kwenye maneno, bali kwenye matokeo ya kazi na uwekezaji wa muda mrefu.

“Watu wengi wanapenda kuona matokeo, sio maneno. Nilianza kwa msingi, na mpaka sasa msingi pekee umenigharimu zaidi ya milioni 100. Ujenzi bado unaendelea, lakini najua itakuwa nyumba ya ndoto zangu,” alisema Christian Bella.

More hit song from Christian Bella;

Leave a Comment