Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Kwanza
KICHAWI

Ep 01: Kijiji cha Wachawi

Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA : ALEX WAMILLAZO


Simulizi : Kijiji Cha Wachawi

Sehemu Ya Kwanza (1)

Ulikuwa usiku wa manane,ambapo katika mbuyu mkubwa kuliko yote kijijini Isegeye walikutana wachawi wakubwa kwa wadogo,ambapo katika ule mkutano walijadili jinsi gani ya kumuunganisha kijana Makongoro katika familia ya kichawi. Makongoro ambaye ni kijana mgeni hapo kijijini aliyekwenda kuwasabahi bibi na babu yake baada kuhitimu Elimu ya msingi.

Hivyo kwa kuwa ulikuwa ndio utaratibu katika hicho kijiji kuweza kumfanyia vitibwi mgeni anae ingia lada zao,ndio maana mapema sana wachawi wa kijiji hicho wakaamua kumuwekea kikao Makongoro ili wamjaribu.

Naam! kikao kilidum ndani ya masaa mawili,ambapo uliweze kupatikana mwafaka kwamba wamwache kwanza Siku mbili au tatu makongoro ayazoee kwanza mazingara ya kijiji cha hicho,Na bada ya hapo ndipo waanze kufanyia mambo yao kama walivyo zoeleka.

Siku zilisonga,wakati huo kijana Makongoro akiendelea kuyafurahi maisha ya kijijini..Haswa jinsi alivyokua akijidekeza mbele ya bibi na babu yake,pasipo kujuwa nini kitakacho mtokea siku za usoni…Na hivyo baada Makongoro kuzoeleka kijijini,hatimae Wachawi walirudia tena kujikusanya muda uleule mahali pale,sehem ambayo baadhi ya wanakijiji walikuwa wakiigopasana kukatiza hasa pindi giza liingiapo.

“Habari zenuu..wana wanzego”…Ni sauti ya mkuu wa kikao aliyosikika akiwa salimia wachawi wenzake,mara tu wote walipokuwa wametulia kwenye ule mti mkubwa kuliko yote kwa niaba ya kusikiliza kipi kitajiri baada kikao cha kwanza kumalizika bila kufanya mambo makuu kwa kijana mgeni aliyeingia kijijini kwao,nae si mwingine ni Makongoro.

Wachawi hao baada kusalimiwa na mkuu wao wa kikao,wote kwa pamoja waliitikia..Wakati huo sauti mbalimbali za ndege wa ajabu zikisikika kwa mbali,pamoja na upepo uliokuwa ukivuma polepole ili kuwasaidi kupata taarifa za hatari nao vilevile ulikuwa ukivuma. Baada kuitikia salamu hiyo,ndipo mkuu wao alipo sema.

“Nadhani kila mmoja anatambua kwamba siku kadhaa zilizopita,kuna mgeni kaingia hapa kijijini kwetu…Na sisi kama wanakijiji wa hiki kawaida yetu ni lazima tumjaribu mgeni yoyote yule aingiae kijijini kwetu..Hivyo basi..Mzee mwakipesile nakuomba ufanye hiyo kazi kwa vyovyote vile lazima yule kijana aungane na sisi..Sawaaaah”

“Sawaaaaa..Bi kileleganya” Aliitikia Mzee mwakipesile,baada mkuu wa mkutano kumteua kuifanya kazi ya kumvuta kijana makongoro ili ajiunge kwenye jamii ya kichawi,wakati huo babu yake makongoro ambaye aliitwa Mzee Baluguza,nae alikuwa ni mchawi aliye jitegemea.

Hivyo mkuu yule wa kikao kwisha kumteua mtu,hatimae waliagana kisha kila Mchawi akapotea pale chini ya ule mti ambao ulikuwa kama ukumbi wa mikitano ya wachawi.

Mara baada ya hayo kupita,hatimae kesho yake asubuhi Makongoro aliamshwa na bibi yake ili waende shamba,lakini kwa ukarimu na adabu aliyokuwa amejaliwa kijana Makongoro..Alimtaka bibi yake abaki nyumbani ili shamba aende yeye peke yake,kwani alimuonea huruma bibi yake ambaye tayali ameshakwishakula chumvi nyingi. Lakini Makongoro alipomwambia hilo suala bibi yake, alikataa kwa kudai kuwa nibora waende wote.Kitendo hicho kiliweza kuzua ubishi fulani kati ya bibi na mjukuu..Na kabla hawajapata jibu muafaka,ghafla alitokea Mzee Mwakipesile,moja kwa moja alikwenda mpaka mahali walipomesimama bibi na mjukuu waliokuwa wakiendelea kubishana.

“Habari za asubuhi jamani”..Ilikuwa ni salam ya Mzee mwakipesile,aliyoitoa mara tu alipo wafikia Makongoro na Bibi yake,kitendo ambacho kiliweza kusitisha ubishi wa Makongoro na Bibi yake.

“Bi Mazoea..Embu mwache kijana nae akajifunze maisha ya kufanya kazi peke yake bwanaa..utambania mpaka lini??Eee sio vizuri kiukweli”

Mzee mwakipesile ambae ndio aliyeteuliwa na wachawi wenzake kufanya kazi ya kumwingiza Makongoro kwenye familia ya kichawi…Alimwambia hivyo Bi mzoea ambae ndio bibi yake Makongoro,kwa sauti ya upole.

Na hapo ndipo Makongoro alipo muunga mkono Mzee mwakipesile,Bi mazoea akawa amekosa nguvu ya kumkataza Makongoro..Alimwacha aende akafanye kazi shambani huku akimtaka arudi nyumbani mapema,Makongoro alicheka kwanza kisha akasema

“Sawa mke wangu we usijali, ila niandalie ugali na mlenda maana hiyo mboga ndio inayo nifanya nipasahau mjini”

Alisema Makongoro huku akitupia na utani uliomfanya Bi mzoea kuyaanika mapengo yake nje kwa furaha ya kufurahishwa na utani wa mjukuu wake.Baada Makongoro kuondoka shambani,hatimae Mzee mwakipesile aliweza kukaa kitako na bibi yake Makongoro huku akionekana kumdadisi maswali mengi kuhusu Makongoro,kweli baadhi Bi mazoea aliyajibu lakini mengine alishindwa kwani alijua tabia ya wanakijiji hicho…lakini yote kwa yote baada ya mazungumzo,hatimae Mzee mwakipesile aliagana na bibi yake Makongoro kisha akaondoka zake..Mzee Mwakipesile alipoondoka,punde si punde Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro mume wa Bi mazoea aliingia Nyumbani kwake huku mkononi akiwa na wanyama fulani aina ya ndezi…Cha ajabu kabla hajaingia ndani Mzee Baluguza alihamaki kwa hasira kali akimuuliza mke wake ambae ndio Bi mazoea”Nataka uniambie,huyu Mzee mwakipesile kafuata nini hapa nyumbani kwangu” Bi Mazoea hakimjibu zaidi aliomba msamaha Kwa maana alishindwa kumtimua kwa sababu yeye na Mzee Mwakipesile ni kundi moja katika uchawi..Lakini Mzee Baluguza licha ya kuombwa samahani,hakutaka kuelewa na zaidi alicharuka baada kuuliza wapi alipo kwenda mjukuu Makongoro na kujibiwa kuwa kaelekea Shambani.

Kwa hakika Mzee Baluguza alizidi kuchanganyikiwa,huku akimtolea mke wake maneno makali ya kiruga alielekea chumbani kwake kuchukua kibuyu chake cha kichawi ili apate taarifa kuhusu mjukuu wake huko shambani.

Jasho la kutosha likimtoka Mzee baluguza akihofia usalama wa mjukuu wake,hatimae alichukua unga mweusi aliouchanganya na dam chache iliyokuwemo kwenye kile kibuyu…kisha akaongea maneno yake ya kiruga huku mkono wake ulioshikilia kibuyu ukiwa juu mfano wa mtu anae tafuta Network kweny simu yake…Punde si punde alitokea bundi ambae moja kwa moja alitua kwenye bega la Mzee baluguza,ambapo Mzee baluguza alimchukua yule bundi kisha akamtwaa kwenye mikono yake alafu akaongea kiluga tena..Na ghafla yule bundi aliruka akayeyukia angani,ipatayo nusu saa akawa amerejea tena moja kwa moja alitua kwenye ungo mahususi ambao Mzee baluguza alikua amesha uandaa..Wakati huo Bi mazoea nae alikuwa akiombea yule bundi alietumwa kuchukua taarifa kuhusu Makongoro aweze kuja na taarifa njema ili amalize siku kwa amani.

Hivyo baada yule bundi kutua kwenye ungo wa Mzee baluguza,haraka sana Mzee balu alimchukua kisha akamtazama machoni kwa maana yule bundi wa kichawi wa Mzee baluguza alikua akinasa taarifa kwa kutumia mboni zake..Na mala baada Mzee baluguza kumtazama mala mbilimbili yule bundi kwenye macho yake..mala ghafla.

Ghafla alishtuka huku akimtazama mke wake jicho ngebe,wakati huo Bi mazoea akiendelea kuwadaa ndezi alioletewa na mume wake ambae ndio Mzee baluguza.

Hivyo Mzee baluguza baada kushtuka,alikohoa kidogo..kikoozi ambacho kilimfanya Bi mazoea kumgeukia mume wake…Na hapo ndipo alipo kutana uso kwa uso na mume wake.

“Unamtazama nani?? lione mapengo yake sasa,pumbafu mbwa koko wewe”

Alieyaongea maneno hayo alikua ni Mzee baluguza akionekana kukasilishwa na kitu alichokiona kwenye mboni za bundi wake wa kichawi…Lakini licha ya Bi mazoea kutukanwa,ila alikaa kimya kwani tangu enzi za ujana wao alimtambua vema kuwa mume wake ni mkorofi,na ndio maana aliondolewa kwenye kundi la wachawi wa pale kijijini kwao bhonde..


Basi shambani nako,baada makongoro kufanya kazi kwa muda mrefu.Hatimae aliamua kuanza safari ya kurudi nyumbani,ambapo alikuwa yupo njiani alikutana na Mzee mwakipesile…Mzee ambae alipewa majukum na mkuu wake wa kichawi kwamba aifanye shughuli ya kumuunganisha makongoro katika familia ya kichawi.

“kijana habali yako”

Mzee mwakipesile alimsalimia Makongoro..Makongoro alishtuka baada kuskia mtu akiongelea nyuma yake,kitendo ambacho kilimfanya ageuke nyuma haraka ili kumtazama mtu aliemsalimia.

“Aah Mzee shkamoo”

“Malakhaa ujambo kijana wangu”

“mimi sijambo mzee wangu sijui wewe”

Mzee mwakipesile akitabasam,alijibu.”Haswaa mimi pia niko vizuri…eeh wapi unaelekea sasa”

“Mda huu narudi nyumbani baada kumaliza kazi” Alijibu hivyo Makongoro huku akipiga hatua polepole za kuondokea..Lakini Mzee mwakipesile alimsimamisha.

“Simama basi mjukuu wangu..au unaskia njaa kali”Mwakipesile alimuhoji Makongoro.

“Ndio babu”

“Anhaa hilo sio tatizo..Ebu twende kuleee unakoona miti mingi ya miembe ..au hupendi kula maembe?…maana nyie watoto wa mujini bhana mnamaringo sana”

Mzee mwakipesile alimwambia hivyo Makongoro huku akimaliza kwa kicheko ambacho kilimfanya Makongoro nae acheke..”Hapana babu sio wote,mfano mimi nimeyapenda sana maisha ya hapa kijijini kwenu na wala sina mpango wa kurudi mjini”

“Teh teh teh sawa kijana..pita vizuri maana njia hii imejaa miba”

Naam!story mbili tatu ziliendelea kati ya Mzee mwakipesile na Makongoro,wakati huo wakiwa njiani wakielekea shambani kula maembe.

“Khaa babu hivi miembe hii yote ya kwako?..”

Baada kufika shambani na kukuta miti mingi ya miembe iliyoivisha kwa ustadi..hatimae Makongoro alipigwa na butwaa hivyo akawa amemuuliza hivyo Mzee mwakipesile.

“Ndio mjukuu wangu,kwani huko mjini hakuna miti ya miembe?..”

Makongoro alicheka kidogo baada kuulizwa swali lile na Mzee mwakipesile kisha akajibu..

“Haah babu acha kunivunja mbavu bhana..sasa mjini utalima wapi”

“Lakini naskia huko mjini wanawake wazuri wapo wengi..eti ni kweli rafki yangu?..”

“Ndio wapo wengi tu..ila pesa yako babu”

“Mmh kwahiyo mpaka hela?..”

“Ndio babu,siunajua kizuri ghalama?!..”

“Haya mjukuu wangu ngoja ipo siku na mimi nitaenda huko mjini nikawaone hao wanawake wazuri..”

“sawa babu karibu…ingawa mimi bado nipo nipo kwanza hapa bhonde”

Hakika yalikua ni mazungumzo marefu ambayo Makongoro alikua akizungumza na Mzee mwakipesile,wakati huo wakiendelea kula maembe.

Na baada kumaliza,hatimae Mzee mwakipesile alimwonyesha njia ya kutokea Makongoro ili arudi nyumbani kwa bibi yake…Hivyo baada Makongoro kutokome,ghafla ile miti ya miembe ilegeuka kuwa wachawi ambapo walimpa hongera mzee mwakipesile kwa kujenga ukaribu na kijana makongoro huku wakizidi kumpa moyo kuwa asikate tamaa bali aendelee nae kujenga urafiki mpaka pale atakapo vutwa kwenye familia ya kichawi.

Baada ya hayo,hatimae walijumuika pamoja wale wachawi kisha wakacheza na kuimba nyimbo zao asili..wakati huo kila mmoja akipotea baada ya dakika moja mpaka pale wote walipo kwisha akawa amebaki mzee Mwakipesile ambae nae alikua akijipanga kupotea ila alistisha huo mpango baada kutokewa na Mzee baluguza babu yake makongoro.

Alishtuka mwakipesile…huku Mzee baluguza akipiga hatua kumfuata alipo kuwa amesimama…Na baada kumfikia alimwambia kwa sauti ya polepole

“Cheza na watoto wa kijiji hiki, ila usicheze na mjukuu wangu…nadhani umenielewa…la sivyo mtataka vita kati yangu na nyinyi..”

Mzee baluguza alimwambia hivyo Mzee meakipesile..wakati huo mwakipesile akihemea juju…

Na baada Mzee baluguza kusema hayo aliyeyuka..akimwacha Mzee baluguza akijitafakali mala mbilimbili jinsi gani atampata kijana makongoro hali ya kuwa babu yake ameshamchimba mkwala.


Basi hatimae usiku uliingia..ambapo mala baada kumaliza kula chakula cha usiku.Mzee baluguza alikaa kitako na mjukuu wake kisha akamwonya Makongoro kuweka mazoea na yule Mzee mwakipesile..Hivyo Mzee balu alienda mbali zaidi akimwambia kwamba endapo kama hatokua mskivu basi atamrudisha mjini kwa wazazi wake..Kitendo ambacho kilimfanya makongoro kuomba msamaha,huku akijiuliza kwanini babu yake anamkataza kuweka mazoea na yule Mzee wakati ana roho nzuli??..Lakini yote kwa yote Makongoro alitii agizo…Na hivyo siku hiyo aliamua kwenda kulala mapema kwani alikasirika.

Hivyo basi baada saa saba usiku kuingia..wakati huo Makongoro akiwa kwenye dimbwi la njozi,ghafla alishtuka kutoka usingizini baada kuskia nyimbo za asili zikiimba jirani na nyumba ya bibi yake…Apapo aliinuka kisha akaenda kufungua mlango ili ashuhudie kilichokuwa kikiendelea…

“Yesu wangu..?”

Alishtuka Makongoro baada kufungua mlango,na kushudia kundi la wachawi wakicheza kwa kuzunguka huku wakiwa uchi…ila kwa kuwa mwanga wa mbalamwezi ulikuwa hafifu,hivyo Makongoro hakuweza kuziona sehem nyeti za wale wachawi.

Basi nyimbo na vigelele za wale Wachawi ziliendelea wakati Makongoro akiendelea kuwatazama bila wao kujuwa,lakini punde si punde wale wachawi walipotea..ila alisalia mchawi mmoja tu ambae nae alipiga hatua kuja mlangoni ambapo alipokuwa Makongoro.

Basi Makongoro alipomwona yule mchawi akija mahali alipokuwa amesimama,haraka sana alifunga mlango kisha akatimkia kitandani kwake…wakati huo akiwa bado hajamjuwa vizuri yule mchawi aliekuwa akimfuata,ingawa alikuwa na mashaka kuwa huwenda akawa ni bibi yake kwani mwendo wa bibi yake na mwendo wa yule mchawi aliemwona nje,wote walifanana…Lakini yote kwa yote Makongoro hakutaka kuyatilia maanani,kwa sababu hakuwahi sikia popote kwamba bibi yake akituhumiwa kwa uchawi.

“Daah hapa sasa naanza kukihofia hiki kijiji…maana haya mambo niliyoyaona sio powa kabisa”

Alijisemea maneno hayo ndani ya nafsi kijana Makongoro,wakati huo akilivutia kichwani blanket yake aliyopewa na bibi yake kwa niaba ya kujifunika muda wa kulala…Na punde si punde alipitiwa na usingizi…

Hivyo basi baada Makongoro kupitiwa na usingizi mzito..Ghafla upepo mkali ulivuma nje ya nyumba ya Mzee baluguza,wakati huo Mzee baluguza yeye akiwa ameshaondoka zake katika majukum yake ya kichawi..Naam!Baada upepo ule mkali kuvuma kwa kasi zaidi,punde si punde alitua chini na ungo Mzee mwakipesile ambae alipewa jukum la kumuunganisha kijana Makongoro katika familia ya kichawi.

Hivyo Mzee mwakipesile,akiwa na mkoba wake pamoja na hirizi mbalimbal..huku kiononi akiwa amevaa vazi jeusi na kichwani akiwa amejifunga kitambaa chembamba chenye rangi nyekundu..hima alichukuwa kibuyu chake kidogo kilicho chakaa,halafu akanyoosha mkono wake juu ulieshika kibuyu..kisha akaushusha….Ambapo alichukua kitu kama mkia wa ng’ombe mfupi,akawa anapitisha juu ya kile kibuyu mfano wa mtu anae fukuza nzi ili wasitue kwenye kibuyu..Hivyo baada kufanya hayo alikipuliza kile kibuyu kwa kutumi kinywa chake..kisha akacheka kidogo huku akikitazama kile kibuyu.

Na mala baada kumaliza kucheka,hatimae Mzee mwakipesile aliinamisha kichwa chini kidogo…punde tu akawa amepotea pale nje,ghafla akawa ameibukia ndani chumbani kwa Makongoro.

Hakika Mzee mwakipesile alitabasam kidogo baada kumwona Makongoro akiwa amelala kitandani hana hili wala lile…Na hapo ndipo alipopiga hatuwa kumfuata kitandani,ila kabla hajafanya jambo lolote kwa makongoro…Alimruka kwanza mala tatu kisha akasogea kando kidogo na kitanda alichokuwa amelalia Makongoro..Kwisha kufanya hayo,Hatimae Mzee mwakipesile alimwita Makongoro kwa ishara ya mkono,ambapo Makongoro aliweza kunyanyuka mwenyewe kutoka kitandani.Akiwa hajitambui alimfuata Mzee mwakipesile ambae nae alizidi kurudi nyuma mpaka alipo fika kwenye kona ya chumba..Hivyo akawa amepotea ambavyo ndivyo hivyo ilivyokuwa kwa Makongoro nae alipotea kama alivyopotea Mzee mwakipesile.


Basi mala baada Mzee mwakipesile kutoweka na Makongoro…hatimae alimpeleka kwenye milima mikubwa ya kijiji cha bhonde..ambapo huko kulikuwa na jopo kubwa la misukule iliyofugwa..Hivyo kijana Mkongoro akawa amekabidhiwa kazi ya kuilisha ile misukule..ambayo chakula chao kikuu ilikuwa ni ndizi mbivu pamoja na pumba za mahindi iliyochemshwa..kweli Makongoro aliifanya ile kazi aliyopewa na Mzee mwakipesile,kazi ya kuilisha misukule.Kazi ambayo Makongoro aliifanya akiwa hajitambui…kwa hakika Makongoro,kijana ambae alikuwa na mwili mdogodogo alipata shida kuilisha ile misukule,kwani kuna baadhi ya misukule ambayo ilikuwa na njaa kali ambapo ilimsumbua sana Makongoro.

Naam!Baada Makongoro kuhitimisha ile kazi,hatimae ile misukule ilipotea mmoja baada ya mwingine..mpaka pale yote ilipokwisha..hivyo punde si punde kundi kubwa la wachawi wakiwa na Nyugo zao(ungo)mfano wa kumbikumbi walitua katika ile milima ambapo waliwakuta Mzee mwajipesile pamoja na Makongoro..

Hivyo salam za kichawi ziliendelea pale,wakati huo Bi mazoea ambae ndio bibi yake Makongoro alionekana kushtuka baada kumwona mjukuu wake maeneo yale ambayo ni mahususi kwa niaba ya wachawi na misukule kulia chakula..Basi haraka sana Bi mazoea alimtafuta Mzee mwakipesile,kwani alijuwa kuwa dhahili shahili Makongoro atakuwa kaletwa na Mwakipesile na sio mtu mwingine.Kweli hatimae Bi mazoea alifanikiwa kumapata japo kwa mbinde kwa sababu wachawi walikuwa wengi mno.

“Habali bhabha”..Bi mazoea,mzee aliekuwa na mapengo alimsalimia kwanza Mzee mwakipesile huku akionekana kuwa na hofu…

“Salama tu kwema?..”Alijubu mwakipesile.

“Hapana sio salama…Hivi wewe ndio umekuja na mjukuu wangu?..”

Alicheka kwanza Mzee mwakipesile baada Bi mazoea kumuuliza hilo swali..kisha akamjibu.

“Ndio mimi..ila usihofu hapo alipo haelewi chochote,zaidi anahisi yupo kwenye ndoto tu kitandani”

“Mmmh wewe acha utani bhana..embu mtazame kwanza…eti eti etiii…mbona ananichekea ..Aaaa..We mzee mwakipesile usinisababishie matatizo mimi..onhooo”

“Acha woga basi..yani ulivyo kama sio nguli wa uchawi?..usiniabishe Bi mazoea mpenzi wangu wa zamani sawaeee”

Aliingiza utani kidogo Mzee mwakipesile,lakini Bi mazoea hakucheka wala kutabasam kwani alighazibishwa na kile kitendo alichokifanya Mzee mwakipesile.

“Haya??..ila nadhani unamjuwa vizuyi babu yake..mimi sina neno”

Hakika kwa sauti ya upole Bi mazoea alimwambia hivyo Mzee mwakipesile…Naam! Mzee mwakipesile baada kuambiwa hivyo,haraka sana aliandaa ungo wake kwa niaba ya kumrudisha Makongoro nyumbani kwaa maana alikuwa akimwogopa sana Mzee baluguza,yote kutokana na uchawi mkali aliokuwa nao Mzee baluguza ambae ndio babu yake makongoro..Basi wakati Mzee mwakipesile alipokuwa akifanya harakati za kuondoka ,ghafla alizuiwa asiondoke mpaka ale chakula kwa pamoja,chakula ambacho kilikuwa na nyama za binadam kinywaji kikiwa ni dam za binadam..Hivyo basi Mzee mwakipesile alilia hatimae alipewa ruksa ya kuondoka,huku wakimuhiza awahi kwa sababu watakuwa wakimsubili yeye pekee,kitendo ambacho kilimlazim Mzee mwakipesile kuahilisha kutumia nyia ya ungo,akawa ametumia njia ya kupotea kama mwanga uzimikapo.

Kweli punde si punde Mzee mwakipesile alitua kwenye uwanja wa nyumba ya Bi mazoea mke wa Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro…Faster alifanya mambo kama aliyoyafanya hapo awali wakati wa kumchukuwa Makongoro…Na hatimae akawa amemrejesha makongoro kitandani,lakini kabla Mzee mwakipesile hajaondoka chumbani kwa makongoro..ili asahi kula chakula na wachawi wenzake..Mala ghafla Mzee baluguza nae alitua mlemle chumbani kwa Makongoro..wakati huo Mzee baluguza na Mzee mwakipesile ni Maadui kama ilivyo maji na moto.

“Mwakipesile,hivi unanitafutia nini wewe mzee?..eeh nilishakwambia sihitaji upuuzi wako kwa mjukuu wangu mbona hunielewi?..$asa nadhani dawa yako moja kwanza lazima nikushkishe adabu mpumbafu”

Alikuwa ni Mzee baluguza…alisikika akiongea maneno hayo baada kumkuta mwakipesile chumbani kwa mjukuu wake,wakati huo nao Mzee mwakipesile alikuwa akijiweka sawa kwa niaba ya kupambana,kwani alijipa matumaini kwamba huwenda akafanikiwa kumshinda Mzee mwenzake baluguza ambae nae alikuwa si haba kwa mambo ya kichawi.

Kweli punde si punde walipotea mle chumbani kwa Makongoro..wakatua nje ya nyumba ambako kulikuwa na uwanja umpana….Hivyo haraka sana kila mmoja alifanya maandalizi yake ya kuvaa hirizi kwa ustadi wa hali ya juu..Na hatimae pambano likaanza…Aliekuwa wa kwanza kumuanza mwenzake alikuwa ni Mzee baluguza ambapo kwa kutumia mikono yake aliikunja kisha akaikunjua mfano wa mtu anae skuma gari…ghafla ulitokea moto ambao moja kwa moja ulimfuata Mzee mwakipesile…hivyo kwa kuwa Mzee mwakipesile nae alikuwa vizuri kwa yale mambo..Aliinama moto ule aliourusha baluguza ukawa umepitiliza………Alicheka Mzee mwakipesile halafu nae akajibu mashambulizi mawili ya haraka haraka…ambapo Mzee baluguza alitaka kujitahidi kulikwepa,lakini fataki moja ilimbabatiza.Fataki ambalo Mzee mwakipesile alilirusha kwa kutumia mdomo ambao uliweza kutema moto mkali malambili ya ule alio urusha Mzee baluguza…Hivyo Mzee balu akawa ameanguka Chini kama mzigo wa kuni..kitendo ambacho kilimfanya augulie maumivu kwanza kabla hajajibu pigo,huku Mzee mwakipesile akiendelea kujiweka sawa wakati huo akimwita Baluguza ili amkomeshe vizuri.

“Khaa uchawi huu kautoa wapi huyu mzee!..hakika leo nimeumbuka…ila ngoja nijitahidi la sivyo huyu mzee atamzoea mjukuu wangu”

Ni mzee baluguza alikuwa akiyaongea hayo maneno,wakati bado akiwa chini akiendelea kuugulia maumivu…ila mwishowe alisimama kisha akarusha moto kwa kutumia mkono wake wa kulia ghafla Mzee mwakipesile akaunasisha pamoja na moto wake,haraka sana Mzee balu alirusha tena moto kwa kutumia wa kushoto…hivyo kwa kuwa nguvu zote za mzee mwakipesile zilikuwa zikitumika upande mmoja ambao ni kuugandisha moto pamoja na mokono wa kulia wa buluguza…Hatimae ule moto uliorushwa na mkono wa kushoto ulifkia Mzee mwakipeslile……Alilalama kwa sauti kali kali huku akigagaa chini..Sauti hiyo iliweza kumfikia mkuu wake wa kichawi kule milimani ambako ndiko kulikokuwa na makazi maalum ya kulisha chakula misukule pia na wachawi kulia chakula.Hivyo mkuu yule baada kuiskia hiyo sauti ya Mzee mwakipesile alishtuka..hima alimwita mchawi mmoja kisha akamwagiza amletee chungu,kweli punde si punde yule mchawi alikileta..ambapo mkuu yule ambae jina lake ni Bi kileleganya alifanya mambo yake ya kichawi…ghafla ndani ya kile chungu kilichokuwa na mkojo wa mama mjamzito,walionekana Mzee baluguza na mzee mwakipesile wakipigana.Wakati huo Mwamipesile akionekana kushambuliwa sana.

“nyote kimyaaaa” Bi kileleganya ambae ndio mkuu wa wachawi pale kijijini bhonde,aliutuliza umati wa wachawi ulikuwepo pale milimani…kweli wote walikaa kimya

“Mnaongea ongea tuuuu…mnajuwa kinachoendelea muda hu?..”

Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi..ghafla wote walianza kutazamana.

“sijawaambia mtazamane…pumbafu zenu..haya haraka sana kila mmoja ajiandae,safari moja kwa moja mpaka nyumbani kwa Bi mazoea tukamwokoe mwenzetu…”

Amri ilimtoka kwa mkuu wa wachawi huku akionekana kukasilika…hivyo punde si punde wachawi wote walikuwa wameshakaa kwenye nyungo zao tayali kwa safari ya kwenda kumwokoa Mzee mwakipesile ambae alikuwa akipigwa vibaya na Mzee baluguza.


Mfano wa mbayuwayu warukavyo angani ndivyo ilivyokuwa kwa wale wachawi jinsi walivyopaa angani na nyungo zao…naam!punde si punde wachawi wale wakawa wanefika,ila walitua pembeni kidogo kisha wakapanga mikakati jinsi ya kumwokoa mwenzao..Hivyo wote kwa pamoja walikubaliana kumvamia Mzee baluguza kasoro Bi mazoea ambae ni mke wa mzee baluguza..Hakika patishika nguo kuchanika, ugomvi uliendelea pale lakini mwishowe wale wachawi walimvamia wote kwa pamoja baluguza..na kwa kuwa baluguza alikuwa ameshachoka alishindwa kujitete kwa kutumia mikono yake,hivyo aliita nyuki wa kichawi ambao alikuwa amewafuga…kweli punde si punde sauti za nyuki ziliskika wakija kwa kasi,kitendo ambacho kiliwafanya wale wachawi kutimka lakini hawakumwacha Mzee mwakipesile ambae alikuwa kapigika vibaya.

Baada ya hayo kupita,Mzee baluguza alirudi ndani kulala akiwa hoi bi taabani..wakati huo kabla hapajakucha Makongoro nae aliamka ili aende chooni kujisaidia..Alistaajabu baada kujikuta mwili umechoka bila kufanya kazi yoyote ngum,lakini hakutaka kujaji sana zaidi alishuka kitandani kisha akaelekea chooni kujisaidia…hakuna asiejuwa vyoo vya kijijini jinsi vilivyo..makongoro wakati anatembea kuelekea chooni ghafla alimwona paka mkubwa mweusi mbele yake,,alimfkuza lakini hakutoka…..Hivyo Makongoro akaamua kuchukua jiwe kisha akampiga yule paka mbae nae alilia kwa sauti kali kama mtoto huku akimfuata mbio makongoro.

“Bibi nakufaaaa”…Sauti ya makelele iliskika kutoka kwa Makongoro huku akikimbilia ndani..waakati huo yule paka aliepigwa jiwe alikuwa akimfukuzia nyuma..Lakini kabla yule paka hajamkalibia,ghafla alipotea…Hivyo hata mzee baluguza alipotoka nje kuangalia kilichomkuta mjukuu wake,hakuona chochote…Na hapo ndipo alipo mtuliza kumwondoa hofu,wakati ho tayali haja ya kwenda chooni kujisaidia ilikuwa imeshapotea kwa Makongoro.

Asubuhi ilipo ingia kabla Mzee baluguza na familia yake hawajaamka,ghafla mlango wa nyumba yake uligongwa…hivyo Mzee balu baada kuiskia hodi aliamka ili akamsikilize huyo mtu aliedamkia kwake..Baada kufungua mlango,alikutana uso kwa uso na Mzee mmoja ambae aliitwa kinono Mzee ambae pembeni yake alikuwa na kijana wake mdogo mwenye umri kama miaka kumi na nne…kijana huyo alikuwa ameshika kichwa chake ambacho kilikuwa kikitilisha dam.

“Habali za hasubui mzee baluguza”

“Salama tu sijui kwako!?..”

“Kwangu sio salama kiukweli…Kama unavyomwona kijana wangu jinsi alivyojileruhiwa na mjukuu wako..”

“Mjukuu wangu??..embu acha utani basi kinono..mjukuu wangu hajawahi kugombana na mtu yoyote hapa kijijini,kwahiyo wewe unapo niletea hizo tarifa zako naona kama unanichefua”

“Nakuchefua?..jana wakati kijana wangu alipokuwa kwenye matembezi yake,alipigwa jiwe na mjukuu wako,halafu leo hii unaniambia nakuchefua?..aaah wapi Mzee baluguza siku zote mimi huwa mstarabu lakini ukiniudhi na mimi ntakuudhi mala mbili ya ulivyo niudhi…hivyo basi mimi naondoka lakini nakuomba umkanye mjukuu wako,awe makini hapa kijijini la sivyo utamkosa…”

“Aaah mkwala huo..wewe mzee kinono huwezi kunitisha mimi wala mjukuu wangu,na kwa taarifa yako endapo kama mjukuu wangu akikutwa na tatizo lolote..hakika ntadili na wewe mpaka mwisho..mpumbaffu wewe”

ITAENDELEA

Isikupite Hii: Dalili za Kuonyesha Mwanamke Anataka Umpeleke Chumbani

Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment