Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Nne
IMEANDIKWA NA : ALEX WAMILLAZO
Simulizi : Kijiji Cha Wachawi
Sehemu Ya Nne (4)
“
Wakati Mzee kinono akifanya yake huku akijiuliza kuhusu Makongoro,ghafla mwanae ambae aliitwa Sudi aliamka..alishtuka baada kumwona baba yake akiwa bize na jungu lake la kichawi,kwani alihisi kuwa kimenuka kijiji.. maana Sudi alikuwa ameshakalili kuwa endapo akimwona baba yake ameshika chungu chake,basi lolote limetokea aidha litatokea.
“Sudi..” Aliita Mzee kinono kwa jazba.
“Naam baba.”
“Ebu kuja hapa”
Kwa wasiwasi wa hali ya juu,Sudi alitii wito wa baba yake.
“Mmmh unamfaham yule mjukuu wa Mzee baluguza??. ” Kinono alimuuliza mwanae kwa hisia Kali.
“Mjukuu wa Mzee baluguza??…Ee ndio namfaham si yule alienipiga jiwe siku ile”
“Eeeh huyohuyo…ambae anajifanya yeye mjanja eti kisa ametoka mjini…ila tuachane na hayo,nilichokuitia ni kwamba popote utakapo muona..Tafadhali usimchokoze sawa Sudi??..”
“Sawa baba” Aliitikia Sudi ili kumlidhisha baba yake,lakini ndani ya nafsi yake bado alitamani akutane na Makongoro ili amfanyie mambo.
Baada Mzee kinono kumwonya mwanae kwa Makongoro..hatimae aliendelea na kazi yake ya kuangalia kitu alicho nacho Makongoro…ambapo mwishowe Mzee kinono aligundua kuwa Makongoro anahirizi kubwa na yenye nguvu nyingi..Alicheka Mzee kinono kisha akasema “Mimi ndio kinonoooo..nimesha sema siwezi kusumbuliwa na mtoto mdogo…” Alisema hivyo Mzee kinono huku akipiga kifua chake.
“Sudi mwanangu..”
“Naam baba…”
“Njoo unafanya nini huko..”
“Nachimba mihogo hapa nyuma ya nyumba..ili nichemshe”
“Anha njoo kwanza..” Sudi alitupa jembe chini kisha akatii wito wa baba yake ambae nae alikuwa akiimba nyimbo za kirugha huku akiyumbisha kichwa chake akikipeleka kulia na kushoto..
“Ndio baba nimekuja..”
“Saw sawa…umesema unachimba mihogo kwani Bukulu hayupo??..” Alihoji Mzee kinono..Bukulu ni msukule ambao aliufuga mzee kinono.
“Yupo baba lakini…”
“Lakini nini???…..Acha ujinga Bukulu yupo hapa kutufanyia kazi sawa??”
“Sawa baba nimekuelewa..”
“Naam vizuri sana….pia nakupa taarifa kuwa kisho mimi naelekea mindu kuna dawa frani naifuatilia..Hivyo jukum lako ni kumlinda Bukulu asitolike pia kama nilivyo kwambia kaa mbali na mjukuu wa Mzee baluguza..”
Alisema hivyo Mzee kinono..ambapo aliamua kuanzisha safari ya kwenda mindu kufuata uchawi mwingine mkali ili aweze kumwonyesha Makongoro kuwa ukubwa dawa.
Na wakati hayo ya Mzee kinono yakiendelea..tayali palikuwa pamekucha,,sauti za ndege zilisikika…kijiji cha bhonde kilionekana kuwa tulivu…Na kwa mbali alionekana kijana Makongoro akiwa na bibi yake wakielekea shamba huku wakiongea maneno kadhaa wa wa kadha ..
Lakini wakati walipokuwa njiani,ghafla nyuma yao alitokea Mzee mwakipesile moja kwa moja Mzee huyo alizipiga hatua kuwafuata Makongoro na Bi Mazoea ambae ni bibi yake Makongoro.
Hivyo baada kuwafikia,aliwasalimia kisha maongezi yakawa yamezidi kunoga,ila mwishowe Mzee mwakipesile alimwambia Makongoro kuwa wapite shambani kwake ili akachukue maembe..kitendo ambacho kilimfrahisha sana Makongoro…asijue kuwa ile ilikuwa ni njama ya Mzee mwakipesile kumvuta Makongoro katika familia ya kichawi…hali ya kuwa Mzee mwakipesile nae asijue kuwa Makongoro tayali ameshakuwa mchawi.
“Bibi tangulia kidogo kidogo…ngoja mimi nikachume maembe kwa rafiki yangu…maana naona leo hujanibebea hata kipolo..”
Alisema Makongoro huku akizipiga hatua kuelekea kwenye shamba la mwakipesile,,wakati huo Mzee mwakipesile alikuwa tayali amesha piga hatua kadhaa za kutangulia.
“Leo lazima huyu mtoto aingie kwenye familia yetu..yaani inyeshe mvua liwake juwa lazima aitwe mwana nkulu”
Alisema hivyo Mzee mwakipesile kwa kujiamini ndani ya nafsi yake..huku wakielekea shambani..ambako huko walitokea wengine wachawi ambao walijibadilisha wakawa katika hali ya kawaida.
“Eeh niambie rafiki yangu..mbona ulipotea siku mbili hizi??..”
“Amna babu mimi mbona nipo tu. !!..
“aaah hapana bwana,ebu acha kunificha we niambie ulikua wapi.maana hata babu yako nae alipotea,,??..”
“Hahahaaa hofu yako tu ila mimi nipo siku zote”
Naam yalikuwa ni mazungumzo ya Mzee mwakipesile na Makongoro..ambapo Mzee mwakipesile alionekana kumpeleleza Makongoro ili aseme wapi alikoenda na babu yake,lakini Makongoro nae alipiga moyo konde kwa kutomwambia ukweli Mzee mwakipesile…licha ya kufaham kuwa siku moja nyuma alikuwa gambosh yeye na babu yake ambae ni Mzee baluguza.
Hatimae walifika shambani..kwa kuwa Makongoro alipinda sana maembe,hivyo alijikuta akitabasam huku kimoyomoyo akijisemea ” Hata kwa ndumba sirudi mjini..maana mjini matunda kama haya mpaka utumie pesa..” Na wakati Makongoro alipokuwa akijisemea maneno yale,punde si punde Mzee mwakipesile alisikika akisema “Rafiki panda juu angua maembe uyawezayo kisha tukae chini hapa ili tule,,au unasemaje??.” Makongoro akitabasamalijibu “sawa tu babu ila sitokaa sana kkwani natakiwa kumuwahi bibi kabla hajafika shamba..”
“aah sawa sawaa,,fanya haraka basi..”
Alijibu Mzee mwakipesile huku akiwatazama wale wachawi waliojigeza kuwa watu wa kawaida…na hapo hapo mwakipesile alitoa ishara ya kichawi,,ashara ambayo iliwafanya wale watu kujiandaa kwa kuzifunga vizuri hirizi zao.
Na mala baada Makongoro kulidhika na maembe aliyo yaangua,hatimae alitelemka kutoka juu ya mwembe..ghafla alishtuka kufika chini na kutokumwona Mzee mwakipesile..Hivyo haraka sana alipasa sauti ya kumwita lakini Mzee mwakipesile hakuitika..kitendo ambacho kilimjengea fikra Makongoro akidhania kuwa huwenda Mzee mwakipesile kaenda kujisaidia mbali na shamba lake.
Makongoro aliketi chini ya mwembe huku akiendelea kumsubili mwakipesile,,wakati huo akiendelea kula maembe hali ya kuwa macho yake yalionekana kuwa na hofu,,kwani muda wote yalikuwa yakitazama huku na kule.
Lakin baada Makongoro kukaa chini ya mwembe kwa muda wa dakika kama sita,ghafla hirizi yake aliyopewa na mkuu wa wachawi ilianza kumbana..ambapo Makongoro alikumbuka jana usiku jinsi hirizi yake ilivyombana na punde si punde akawa ametokea Mzee kinono kwa dhumuni la kutaka kumuua…Hivyo baada Makongoro kukumbuka hilo tukio,haraka sana alisimama kisha akatazama kila pande kwenye shamba lile la Mzee mwakipesile..Na punde si punde wale watu walirudi katika hali yao ya kichawi….Makongoro alishtuka baada kuwaona wachawi wale,kwa sauti Kali alimwita Mzee mwakipesile pasipo kufaham kuwa katika wachawi wale alikuwemo Mzee mwakipesile.
Na baada Makongoro kuona haitikiwi na Mzee mwakipesile,,hima alitimua mbio,cha ajabu hakuweza kuyaacha yale maembe alikimbia nayo…wakati wachawi wale nao walipoona Makongoro kakimbia,,walitazama kisha wakashikana mikono..punde si punde walipotea wakaibukia mbele ya Makongoro ambae alikuwa kasi kuwakimbia wale wachawi.
Hivyo wale wachawi wakiongozwa na Mzee mwakipesile,baada kumfikia Makongoro,,walijitwajanya kwa kumzunguka Makongoro ili waweze kumshambulia kwa pamoja..lakini kabla hawajaftua makombola yao ya kichawi ghafla Makongoro alipotea pale katikati yao kisha akaibukia sehem nyingi huku akicheka kwa dharau,,wakati huo akila embe akiwatazama .
Hakika wale wachawi baada kushuhudia kitendo kile alicho kifanya Makongoro,walipigwa na butwaa hasa Mzee mwakipesile ambae alipewa jukum na mkuu wake..jukum la kumuunganisha Makongoro katika familia ya kichawi.
“Mmh huyu nae tayali kafuata nyendo za babu yake..hivi nitamuweza kweli??..” Alijisemea Mzee mwakipesile huku akimtazama Makongoro ambae nae alikuwa bize akila embe akisubili aone watamfanya nini ili na yeye aweze kujibu mashambulizi.
“Mzee mwenzangu..mtoto huyu si wakawaida bwanaaa..mimi naona bora tukamuundie kamati ili tujuwe tutamzibiti vipi..” Alisikika mmoja ya wachawi waliokuwa wakimsaidia mwakipesile kumpata Makongoro.
“Haswaa sio Siri maana huu uchawi alionao huyu mtoto si wa nchi hii” Aliongeza kwa kusema hivyo mchawi mwingine.
Lakini licha ya Mzee mwakipesile kupewa huo ushauli na wachawi wenzake,hakutaka kulidhika mpaka amjaribu tena Makongoro..ambapo aliweza kumrushia kombola la kichawi..kombola ambalo Makongoro aliweza kulidaka kisha kulirudisha kule liliko toka..
“Unaona sasa Mzee ushalizua balaa…tatizo wewe mbishi..” Mchawi mmoja alisikika akisema hivyo kwa hasira baada kuona kombola likiwafuata..ila kabla hakijawafikia walipotea..ambapo nae Makongoro alipotea na kuibukia shambani kwa bibiyake…Na punde si punde bibi yake nae alifika..Hivyo Bi Mazoea ambae ni bibi yake Makongoro,alishangaa kumkuta Makongoro shambani hali ya kuwa Alimwacha nyuma akielekea shambani kwa Mzee mwakipesile kuangua maembe akiwa na mwenye shamba ambae ni mwakipesile.
“Mmmh wewe Makongoro..umefikaje hapa na umepitia wapi..?” Alihoji Bi Mazoea akitaka kufaham ukweli kutokakwa mmjukuu wake Makongoro.
“Bibi tufanye kwanza kazi…hayo mengine tutaongea tu..kwanza Leo sikukuu ya pasaka kwahiyo tutoke mapema ili niwahi kwenye banda la video”
“Video??..Utavionea wapi hapa kijijini??..”
“Hata kijiji cha pili mimi nitaenda tu” Alijibu Makongoro huku akiendelea kuchimba mihogo.
“Haya bwana nyie watoto wa siku hizi mnataabu sana..yaani mnaliwa hela zenu eti kisa kuwaangalia watu wasio waona wala kuwajuwa..” Bi Mazoea nae aliongeza kwa kusema hivyo,,maneno ambayo yaliweza kumfanya Makongoro kucheka.
Hivyo baada kumalizika shunghuli za shamba ..Makongoro na bibi yake walirudi nyumbani..ambapo Makongoro baada kufika alichukua ndoo kisha akaelekea kisimani kuchota maji ya kuoga ili ajiandae kwenda kijiji jirani kutazama movie.
Na baada Makongoro kujiandaa..Alipewa chakula na bibi yake..chakula ambacho kilikuwa ni Ugali na kumbikumbi walio kaangwa….ila kwa kuwa Makongoro hakukizoea kile chakula,hatimae alikula kidogo kisha akamuaga bibi yake kwa safari ya kwenda kijiji jirani kutazama movie na moja ya matembezi,,kwa maana siku hiyo ilikuwa ni sikukuu ya pasaka.
Lakini kabla Makongoro hajaanza safari yake.. Aliitwa na bibi yake..ambapo Bi Mazoea alimwambia mjukuu wake kuwa asile chakula kwenye nyumba ya mtu hatakama sikukuu..kwani licha ya asilimia kubwa ya watu wengi sikukuu hula wali na nyama..lakini hali hiyo ni tofauti katika kijiji cha bhonde..ambapo wanakijiji wa kijiji kile hula nyama za watu kutokana na asilimia kubwa ni wachawi.
Na wakati hayo yakiendelea..upande wa pili nyumbani kwa Mzee mwakipesile,,walionekana wazee wakijadili Mambo mbalimbali huku wakiwa na ndioo iliyosheheni pombe ya kienyeji.. bila kusahau pembeni walikuwa wakisikiliza muziki kwenye radio mbao iliyo chakaa kwa vumbi na nyuzi za buibui…Na katika majadiliano yale,,jambo moja kuu ni jinsi gani wataweza kumvuta Makongoro katika familia yao ya kichawi..hali ya kuwa Makongoro nae ameshakuwa mchawi??..
Kwa hakika waliumiza sana vichwa wazee wale ambao walionekana kumsaidia Mzee mwakipesile kwa namna moja ama nyingine ili aweze kumpata Makongoro.
Na wakati kila mmoja akiendelea kutafakali jinsi ya kufanya..mala ghafla Mzee mmoja alikohoa kisha akasema ..”Jamani wazee wenzangu,mimi nimepata wazo la kulinyia kazi..Na nina Hakika asilimia zote endapo tukilifanyia kazi,basi yule mtoto hatoweza kutupa shida..” Alisema hivyo yule mzee,,wakati huo wenzake wakionekana kumsikiliza kwa umakini.
“wazo gani hilo ebu tuambie mzee mwenzetu.” Alijibu Mzee mwakipesile huku akionekana kuwa na shauku ya kutaka kulijuwa hilo wazo…ambapo yule Mzee aliesema kuwa ana wazo,alikunywa pombe kidogo iliyokuwa kwenye kikombe kikubwa..kisha akasema…
“Jamani huyu mtoto kama mnavyo muona,,uchawi wake unatisha sio mchezo…Hivyo mimi nilikuwa napendekeza kwamba hakuna haja ya kumuunganisha kwenye familia yetu..maana uchawi alionao tu unamtosha..” Mzee yule kabla hajaendelea kutoa wazo lake,ghafla Mzee mwingine alidakia akisema..”Sasa unaongea pumba gani we Mzee..eeh au kuzeeka kwako na akili pia imezeeka??….Haya tusimuunganishe kwenye familia yetu halafu tumfanye nini sasa” Alidakia huyo Mzee akisema maneno hayo kwa hasira kali,,ambapo yule Mzee aliekua akitoa wazo lake alionekana kuwa mpole huku akimsikiliza Mzee mwenzake kile anacho kiongea kwa hasira.
Hivyo mala baada Mzee yule kumaliza kuongea kwa hasira akipinga wazo la mwenzake,hatimae alikaa kimya,,kisha yule aliekatishwe nae alisikika akisema “Tatizo wewe mwongeaji sana,,istoshe unafoka kama vile unaongea na watoto wako….Sasa kwa taarifa yako hiyo mipango yenu muifanye wenyewe mimi simo kwa kazi hii ni ya mwakipesile”
Kwisha kusema hivyo yule Mzee alinyanyuka kutoka kwenye kigoda chake..kisha akarudi nyumbani kwake huku akiongea njia nzima.
Hivyo baada yule Mzee kuondoka..wale wazee walio salia wote kwa pamoja walikubaliana kummaliza yule Mzee mwenzao,,ambae aliitwa mzee chande..kwani waliamua kufanya vile baada kuonekana kuwa Mzee chande huwenda akawa msaliti juu yao.
“Mizee mingine bwana..yaani sisi tunakaa makini kumsikiliza kumbe anacho kiongea chenyewe hata hakieleweki..eti zee lote lile miaka dahali lipo kwenye uchawi ..halafu Leo hii anamwogopa mtoto mdogo kama yule..??..” aliongea maneno hayo Mzee mwakipesile..maneno ambayo yaliwafanya wazee wenzake kuachia cheko kubwa huku wakinywa pombe yao iliyokuwa kwenye ndioo kubwa..Na kwa mbali wakisikiliza muziki kwenye radio mbao.
Baada wazee wale kumaliza kunywa pombe yao..hatimae waliagana lakini kabla hawajasambaa,,Mzee mwakipesile aliwakumbusha kuhusu suala la kumuuwa Mzee chande ambae alionyesha usaliti..ambapo wazee wale walitii na kisha wakakubalina wakutane saa tano usiku sehem malum ili wajue namna gani wataweza kumuuwa Mzee chande msaliti.
Wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako alionekana Makongoro akizipiga hatua kuelekea kijiji jirani kwenda kutazama movie…lakini wakati Makongoro alipokuwa akitembea hana hili wala lile..mala ghafla nyuma yake alitokea Sudi mtoto wa Mzee kinono…Sudi akiwa katika mavazi yake ya kichawi,alizipiga hatua kumfuata Makongoro..Na kabla hajamfikia,Sudi alimrushia kombola Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae hirizi yake aliyopewa na mkuu wa wachawi gambosh ilianza kumbana,,na hapo hapo alijuwa tayali kuna tatizo hivyo kwa kuhusi tu lipotea ndani ya nusu sekunde kisha akaonekana tena live…na lile kombola la kichawi alilorusha Sudi likawa halijampata.
Makongoro aligeuka nyuma akamwona kijana mdogo mwenye makamo kama yake akiwa katika mavazi ya kichawi…Hakika Makongoro alijikuta akicheka huku akiendelea na safari yake ya kuelekea kijiji jirani.
Lakin licha ya Makongoro kumpotezea Sudi kijana wa Mzee kinono..ila Sudi bado aliendelea kumchokoza Makongoro..akasahau onyo aliyopewa na baba yake kuhusu Makongoro mjukuu wa Mzee baluguza…Na hapo ndipo Makongoro uvumilivu ulipo mshinda,hivyo kwa kutumia mkono wake uliokuwa na hirizi alimnyooshea kidole Sudi,,na punde si punde Katika kidole chake Makongoro ulitokea moto mwembamba,moto ambao ulikwenda kumpata Sudi..haikupita dakika Sudi alidondoka chini akafa.
Baada Sudi kupoteza maisha..Makongoro aliogopa sana hivyo aliamua kuahilisha safari yake akawa amerudi nyumbani..moja kwa moja alipitiliza hadi chumbani kwake huku akionekana kuwa na hofu juu ya kile alicho kifanya..
Lakini kitendo kile cha Makongoro kupitiliza hadi chumbani kwake bila kumsalimia bibi yake ambae alikuwa sebleni akipika chakula cha usiku..kiliweza kumshtua Bi Mazoea bibi yake Makongoro..ambapo aliweza kumeita ili amwambie kilicho msibu,,ile Makongoro hakuitikia…Na wakati huo huo Mzee baluguza nae alifika nyumbani,hivyo ikabidi Bi Mazoea kumwambia mume wake akamuulize kinacho msibu Makongoro.
Mzee baluguza baada kuambiwa vile..haraka sana alizipiga hatua kuelekea chumbani kwa Makongoro..kwa sauti ya kunong’ona Mzee baluguza alimuuliza mjukuu wake kitu kinacho msumbua.
“Babu nimezusha balaa..kumbe uchawiwenu unauwa kabisa..”
Alisikika ikisema hivyo Makongoro huku kilio kifuatia,,na Mzee baluguza baada kuona hali ile,,hima aliongea maneno yake ya kirugha huku akisugua kiganja chake…Na punde si punde kwenye kiganja chake walionekana wachawi wa kijiji kile cha bhonde wakiwa wamekusanyika kwa nia kumtaka Makongoro na kisha kumuuwa Mzee baluguza ambae ndio babu yake Makongoro.
“unaona sasa mjukuu wangu??..Kwahiyo kaa ukijuwa kuwa tumezungukwa na madui wengi..Na kauli mbiyu yetu ni dawa ya moto maji..Na sio dawa ya moto moto..hahahaaaaa wao wanawasha halafu sisi tunazima..futa machozi mjukuu wangu hujakosea kumuuwa yule mtoto wa Mzee kinono kwani ukiona hivyo nae alikuwa akikuwinda ili akuue..” Alisema hivyo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake,,hali iliyomfanya Makongoro kujiamini juu ya kile alicho kifanya.
Na giza lilipo tanda katika kijiji kile cha bhonde…Mzee mwakipesile alipanda ungo wake na kisha kutua sehem ile waliyoahidina wakutane na wazee wenzake.Hivyo punde si punde wale wazee nao walitua,ambapo walikubaliana kwenda kumuuwa Mzee chande kisha waelekee tena kwa Makongoro kwenda kujaribu tena bahati yao.
Kumbe wakati wazee wale walipokuwa wakipanga mikakati ya kumuua Mzee chande..Mzee chande nae machale yalimcheza,ambapo alichukua ungo na kibuyu chake kidogo..kisha akapaa kuelekea Congo ili kuongeza uchawi zaidi wa kuweza kujirinda dhidi ya Mzee mwakipesile na wenzake ambao wamepanga kumuuwa kabisa.
Hivyo wakati anaiacha ardhi na kuliona anga tu..mwakipesile na wenzake nao walitua nyumbani kwa kwake chande,,ambapo walijikuta wamechelewa kumuwahi Mzee chande.
Hakika roho ilimuma sana Mzee mwakipesile ambae ndio alikuwa kiongozi wa msako..Lakini yote kwa yote aliwataka wazee wenzake waelekee nyumbani kwa Mzee baluguza kwenda kumfuata Makongoro..hali ya kuwa Makongoro nae ameshaambiwa kuwa amezungukwa na maadui,,hivyo kuuwa ni jukum lake.
Kikao cha muda mfupi walikaaa Mzee mwakipesile na wachawi wenzake watatu…ambapo Mzee mwakipesile alisikika akisema. “Jamani kwa kuwa tumemkosa huyu mzee chande,,sasa safari hii tuelekee kwa Mzee baluguza,kwenda kumfuata mjukuu wake..lakini napenda kukumbusha kuwa tuwe tayali kwa mapigano maana nadhani kila mmoja hapa Kati yetu ameweza kushuhudia uwezo wa yule mtoto..je,kweli si kweli??..”
“Kweli kabisa..” waliitikia wale wachawi wengine baada Mzee mwakipesile kusema maneno hayo akiwaasa wenzake wawe makini pindi watakapo elekea nyumbani kwa Mzee baluguza.
Na mala baada kuelewana,,Mzee mwakipesile na wachawi wenzake walijifunga vizuri hirizi zao,kisha wakanywa damu ya binadam iliyokuwa kwenye kibuyu chao…Na hapo hapo safari ya kwenda kwa Mzee baluguza ilianza,,ambapo walipaa angani kwa kutumia ungo.
ITAENDELEA
Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Tano
Isikupite Hii: Dalili za Kuonyesha Mwanamke Anataka Umpeleke Chumbani
Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;