Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA : ALEX WAMILLAZO
Simulizi : Kijiji Cha Wachawi
Sehemu Ya Tatu (3)
Baada Mzee baluguza kupotea maeneo Yale..muda huo huo alitua Mzee kinono akiwa sambamba na ungo wake..Mzee kinono alionekana kumfukuzia Mzee baluguza lakini kwa bahati mbaya hakumkuta..”Daah huyu Mzee baluguza anauchawi wa nchi gani!? ila ipo siku tutakutana tu”
Alisema Mzee kinono…Mzee ambae alikuwa na bifu kali na baluguza…hivyo kwisha kusema hatimae,nae alipotea.
Asubuhi ilipopambazuka ngoma ya kuashilia msiba iliskika kijijini bhonde…Masikio ya wanakijiji yalitega vizuri ili waweze kuskia jina la mtu aliefariki kutoka kwa mtoa tangazo…nae mtoa tangazo la msiba hakuweza kusita kumtaja…nae hakuwa mwingine ni mama chiku.
Hakika wanakijiji walio isikia hiyo taarifa walionekana kustaajabu lakini kwa wale ambao walikuwa wachawi hawakuweza kushangazwa na kifo cha mama chiku kwani walijua sababu iliyomsababishia umauti.
Wanakijiji walijazana nyumbani kwa mama chiku kwa niaba ya mazishi..lakini kabla mwili wa mama chiku haujapelekwa kuzikwa,,mala ghafla alitokea Bi kileleganya ambae ni kiongozi…Na kitu ambacho alikifanya Bi kileleganya ni kuuzuia ile mwili wa mama. chiku usizikwe badala yake ukawe kitoweo kwa familia ya kichawi pamoja na misukule.
Hivyo Bi kileleganya kwa nguvu kubwa ya kichawi aliunyakua ule mwili wa mama chiku,,kisha akaweka mti wa mgomba..mti ambao kama huna macho ya kichawi huwezi kuugundua.
Mazashi yalifanyika..wanakijiji baadhi wakijua wamemzika mama chiku na wengine ambao walikuwa wachawi walijua dhahili shahili wamefukia mgomba wa ndizi.
Hivyo baada ya mazishi kumalizika…walionekana vijana watano wakikaa kikao cha muda mfupi..kikao hicho ambacho walijadili kufanya upelelezi ili kumpata mtu aliehusika na mauaji ya mama chiku…Hakika vijana wale ambao nao kiuchawi walikuwa si haba walikubaliana kulifanyia kazi hilo suala..na kisha wakashikana mikono wote kwa pamoja,wakawa wamepotea mfano wa taa izimikapo gizani.
Wakati vijana wale watano wakipanga kufanya upelelezi wa mauaji ya mama chiku…upande mwingine,,Wazee wateule wakishirikiana na serikali yakijiji walikaa pamoja kujadili mauaji ya kikatili yaliyofanyika kijijini kwao..ambapo walikubaliana kumuunguza ndani ya nyumba mtu atakae bainika kuhusuka na mauaji ya mama chiku.
Taarifa hiyo iliweza kumfikia chinichini Mzee baluguza ambae ndio muhusika…cha ajabu baluguza alicheka kwa dharau kisha akasema..”hii tayali imeshakuwa VITA ..sikutaka kumfundisha uchawi mjukuu wangu Makongoro lakini imebidi la sivyo Nitamkosa…ngoja leo usiku nimpeleke gambosh…hakuna namna”
Alijisemea maneno hayo Mzee baluguza huku akiungojea usiku kwa ham ili ampeleke mjukuu wake gambosh nchin Nigeria ili nae aweze kujilinda katika kijiji kile kilicho sheheni wachawi.
Hatimae usiku uliingia…ambapo siku hiyo familia ya Mzee baluguza…yaani Bi Mazoea ambae ni mke wa Mzee baluguza na mjukuu wao ambae ni Makongoro walilala mapema kwa sababu kijiji kilionekana kuchafuka baada kifo kile cha mama chiku ambae alikatwa shingo na Mzee Baluguza.
Hivyo saa Sita usiku ilipotimia..Mzee Baluguza alinyanyuka kutoka kitandani kwake,kisha akaingia uvunguni ambako alitoka na chungu chake alichokuwa akihifadhia mazagazaga ya kichawi…alikikamata kile chungu kwa mikono yake miwili..kisha akizipiga hatua kuelekea chumbani kwa mjukuu wake ambae ni Makongoro ,,wakati huo Makongoro alikuwa amelala fofofo.
Mzee Baluguza baada kuingia chumbani kwa Makongoro…alimwamsha nae Makongoro aliamka.
Baada Makongoro kuamka..Mzee Baluguza akimtazama mjukuu wake usoni kisha akasema “Nakuomba ufumbe macho yako..usifumbue mpaka nikuruhusu” Alisema Mzee Baluguza ,,wakati huo akimfunga hirizi mjukuu wake. Mara baada kumalizika zoezi lile,hatimaye Mzee Baluguza alimwambia Makongoro asimame.Makongoro alisimama huku akijiuliza babu yake anamaana gani kumkatisha usingizi na kisha kumfanyia Mambo Yale.
“nakuomba usifumbue macho…ukifumbua kabla sijakuruhu shauli yako…” Alisisitiza Mzee Baluguza akimwambia mjukuu wake.
Hivyo baada kumaliza hayo,,Mzee Baluguza alimwambia Makongoro amkumbatie..Makongoro alimkumbatia,ambapo punde si punde alijikuta wapo nje ya nyumba.
Mzee Baluguza alinyoosha mkono wake wa kulia,,ghafla kikatokea kibuyu chake kidogo ambacho ndani yake kilikuwa na damu, alikunywa damu ile iliyo kuwomo ndani ya kile kibuyu…Kisha akarudia kumwambia Makongoro “usifumbue macho macho,pia nikumbatie vizuri usiniachie” Makongoro alifanya hivyo.
Kwisha kusema hayo,walipaa angani…safari ya kuelekea gambosh ikawa imeanza.
Wakati walipokuwa angani…Makongoro alihisi baridi Kali pamoja na upepo mkali,,kitu ambacho kilimfanya kutaka kufumbua macho ili angalie yupo katika mazingira gani…lakini kabla Makongoro hajaifkia macho yake…ghafla alijikuta wametua aridhini…na hivyo Mzee baluguza alimruhusu Makongoro kuyafumbua macho yake.
Makongoro alishtuka baada kufumbua macho yake..kwani aliwashudia wachawi wapatao therathini ambao mavazi yao yalifanana na mavazi aliyoyavaa babu yake.
“Babu kwani hapa wapi” Alihoji Makongoro akimuuliza babu yake…Lakini cha kushangaza Mzee baluguza hakumjibu chochote mjukuu wake. Wakati huo ilisikika sauti kutoka ndani ya wachawi wale therathini ikisema “Jamani tuondokeni tayali tumetimia”
Ilisikika ikisema hivyo ile sauti,,ambapo iliweza kuungwa mkono na wachawi wote waliokuwa wamekusanyika pale rukwa kwa niaba ya safari y kuelekea gambosh.
Hivyo baada wazo hilo kuungwa mkono na jopo lile la wachawi…punde si punde alitokea mtokea Mzee mmoja ambae aliitwa mahulubila…ambapo baada kutokea Mzee yule..haraka sana alichukua kisu kidogo ambacho muda wote alikuwa nacho mfukoni…kisha akatia dam kile kisu,,,wakati huo huo akawaambia wachawi wenzake wafumbe macho.
Baada kumalizika Mambo yake,aliwaambia wafumbe macho..
“waoooo….ndege?..” Alisema Makongoro huku akitabasam baada kuiona ndege..
Ruksa ilitoka kwa Mzee Mahulubila..akiwaambia wachawi wenzake waingie ndani ya ndege ile ya kichawi,kwa niaba ya kuelekea gambosh kwenye chimi chimi ya uchawi…….Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,,wakazipiga hatua kuelekea ndani ya ndege..wakati huo Makongoro akionekana kuwa na shauku kubwa ya kuipanda ndege ile ambayo ilitokea kimazingala.
Hatimae ndege ile ya kichawi ilipaa angani..wakati huo ikiwa haina sauti yoyote……Na wakati ndege ile ilipokuwa bado ipo angani..Mzee baluguza alimgeukia mjukuu wake ambae msamaha wote alikuwa akitabasam kupanda…Mzee baluguza akasema “huku tunakokwenda…nakuomba uwe makini sana!! ukiona kitu usikikodolee macho sana pia maswali yako ya kipuuzi siyataki..vilevile chakula chochote au kinywaji ukipewa tumia..tofauti na havyo utafia huku huku”
Aliongea hivyo Mzee baluguza..maneno ambayo yalimnyong’onyesha Makongoro akiwa haelewi babu yake anampeleka wapi na pia kufanya nini na japo lile la wachawi..
Wakati Makongoro akiendelea kujiuliza bila kupata jibu,mala ghafla ndege ile ya kichawi ilianza kuyumba yumba..Na punde si punde nyuma ulizuka moto
Moto ule ulienea kwenye ile ndege ambayo ulikua imepakia jopo la wachawi…wakati huo Makongoro alikuwa akipiga kelele kuomba msaada…lakini kelele zake Makongoro zilifikia tamati baada Mzee baluguza kumziba mdomo..wakati huo huo mmoja wa wachawi waliokuwemo ndani ya ile ndege,alionekana kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza ambae alikuwa akihaha kumziba mdomo mjukuu wake ili asipige kelele.
“Mzee mwanzangu huyu nani yako??…maana anavyo onekana ni mgeni katika safari hizi..” alisema yule mchawi ambae alionekana kuwa na cheo frani katika kazi ile ya kichawi.
“Mmh huyu bwanaaa…ni mjukuu wangu..ila kwa kua kijijini kwetu wamecharuka kutaka kumuangamiza?? hivyo nimeona heri nije nae huku ili na yeye aweze kujilinda dhidi ya maadui zake..” Alijibu Mzee baluguza.
“Anhaa jambo jema Mzee mwenzangu,sina la ziada”
Kwisha kusema hivyo,,hatimae ndege ile ya kichawi ilitua chini…ampapo mkuu wa safari aliinyoshea kidole ndege..ghafla ikageuka kuwa kisu kama ilivyokuwa awali kabla ya kugeuka kuwa ndege.
Wakati huo huo walionekana binadam wawili wa kutisha,,ambao mmoja alikuwa na jicho moja katikati,na mwingine hakuwa na maskio…wote walikuwa wamevaa koti nyeusi ambazo zilikuwa na kofia zake..hivyo watu wale walipiga hatua kuelekea mahali walipokuwa Makongoro pamoja na jopo nzima la wachawi aliotua nao.
“Babu hao ni akinanani??..”
“Shiiiiiii kaa kimya” Alijibu hivyo kwa kunong’ona Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake baada kuulizwa kuhusu wale watu waliokuwa wakiwafuata.
“Karibuni” Wale watu walisema huku wakiambaa kuelekea kwenye jengo kubwa ambalo mlangoni ilionekana nembo ya kichawi..na chini ya hiyo nembo yalionekana maneno ambayo yaliandikwa kwa rugha ya ajabu ajabu…ingawa baada kuingia ndani zaidi,Makongoro aliliona jina gambosh katika koldo moja ndani ya ile nyumba..na hapo ndipo alipo faham kuwa tayali wametua katika ardhi ya gambosh.
Hivyo wale watu walionekana kutisha kwa upande wa Makongoro,walizidi kupiga hatua huku Makongoro na babu yake pamoja na wale wachawi wengine wakiwafuata nyuma…mwishowe walifika katika ukumbi mkubwa ambao ulikua umesheheni watu wa kila aina.
Makongoro walipigwa na butwaa baada kuwaona wachawi wale..alitamani kumuuliza babu yake kisa kilicho wafanya watu wale kufulika kiasi kile katika ile ukumbi,,lakini aliogopa kwa sababu babu yake alisha mkataza kuuliza uliza maswali….Wakati ule ule mbele yake Makongoro..alikiona kiti ambacho kilikuwa kiking’aa mfano wa almasi…Na katika kiti kile,alitokea mtu mmoja ambae kimwonekano alikuwa na jinsi mbili tofauti..kwani hata sauti aliyopasa ilisikika mala mbili,yaani ya kike na yakiume..vile vile yule mtu katika kifua chake alionekana kuvaa cheni zenye nembo ya mafuvu.
Aliogopa Makongoro baada kumwona yule mtu …alitamani kumuuliza babu yake kuhusu yule mtu,,lakini mwendo ule ule alisita baada kukumbuka kuwa babu yake hataki maswali.
Kimya kilitawala katika ukumbi ule..na ghafla ilisikika sauti ndani ya ule ukumbi,,ukumbi ambao ilikuwa umejaza wachawi mbalimbali pamoja na binadam wa kila aina..sauti hiyo ilisema..”Wote simameni na kisha tuungame kabla hatujaanza kuyadadavua masuala yaliyotukutanisha mahali hapa..” Ilisema hivyo ile sauti..sauti ambayo ilisikika katika jinsia mbili,ya kike na ya kiume…
Hivyo wachawi wale walifanya kama amli ilivyosikika…kasolo Makongoro ambae hakusimama ingawa nae alishikwa mkono na babu yake akimtaka asimame kama wengine walivyo fanya…
Baada kumalizika kuungama..wot kwa pamoja walikaa chini..na hiyo ikawa nafasi pekee ya Makongoro kutazama kila pande katika ukumbi..akiwa bado katika kutazama tazama,,mala ghafla alishtuka baada kumwona mwalimu wake wa hisabati ambae aliitwa shija..nae akiwa miongoni mwa wachawi waliokuwemo ndani ya ule ukumbi..Makongoro alijiuliza ni vipi mwalimu wake atoke Dar es salaam ambako anafanya kazi,moja kwa moja aonekane gambosh?? Na hapo ndipo Makongoro alipokumbuka kuwa mwalimu huyo alishahusishwa na tuhuma za kichawi,,ila zikawa zimeishia chini chini….na hivyo Makongoro akawa amefaham kuwa mwalimu shija ni mchawi kama alivyokuwa akituhumiwa na wanafunzi wa shule mwenge..shule ambayo mwalimu hiyo alikuwa akifundisha pia Makongoro nae akiwa miongoni mwa wanafunzi wa shule hiyo.
Makongoro aliduwaa huku akimtazama vizuri mwalimu yule…wakati huo huo shija nae aligeuka upande aliokuwa Makongoro…na hivyo wakawa wamekutana uso kwa uso…kitendo ambacho kilimfanya shija kurudisha uso wake kama awali baada kumwona Makongoro ambae alikuwa ni mwanafunzi wake “Mmh huyu Makongoro kafikaje fikaje huku??.. na bila shaka atakuwa kanijua…na kama kweli kanijuwa,,hakika nitafanya juu chini ili nimwangamize kabla unga haujazidi maji” Alisema shija baada kuingiwa na hofu kuhusu Makongoro.
Na wakati hayo ya Makongoro pamoja na mwalimu wake ambae ni shija…alipokuwa yakiendelea,upande wa pili nako yule mtu mwenye jinsi mbili tofauti…aliendelea kuzungumza Mambo mbalimbali kadha wa kadha..na katika mambo hayo ilikuwemo suala nzima la kugawa uchawi kwa watakao hitaji..kisha akaomba majina ya watu wanao hitaji na aina gani ya uchawi unaotakiwa.
Kwisha kusema hayo kengere ililia,,kuashilia kuwa umefika muda wa kula chakula…hivyo mtu yule ambae alikuwa akiendesha Mkutano ule wa kichawi..aliwaruhusu wachawi wake wakale Kwanzaa chakula kisha waendelee na Mkutano..ambapo Mzee baluguza alimshika mkono mjukuu wake,moja kwa moja walielekea kwenye chumba mahususi kwa kulia chakula..Chumba ambacho kila kona ilisikika harufu ya dam za binadam.
“Chochote utakacho letewa kula wala usiohope…na pia ukienda kuchukuwa uchawi kwa yule kiumbe,,Naomba uchukuwe uchawi wa kujilinda na kuua..Sarawak??..” Mzee baluguza alimwambia hivyo mjukuu wake kwa msisitizo… huku wakiwa tayali wameketi kwenye viti ambavyo vilitengenezwa kwa kutumia mifupa binadam pamoja na ngozi ya Chui..
Hivyo Makongoro baada kuambiwa vile na babu yake,aliitikia kwa kichwa..wakati huo huo alionekana binti mzuri ambae miguu yake ilikuwa kama mbuzi..binti yule akiwa na bakuli mbili mkononi,,alizipiga hatua kuelekea kwenye meza ambayo walikuwa wapo Mzee baluguza pamoja na Makongoro.
Hivyo binti yule baada kuifikia meza ile..aliwapa zile bakuli baluguza na mjukuu wake…ampako Mzee baluguza aliufakamia kwa pupa mchuzi uliokuwemo ndani ya bakuli yake….wakati huo Makongoro nae alipo ingiza kijiko chake kwenye mchuzi katika bakuli lake…ghafla alistisha baada kuona kiganja cha macho ya binadam yakielea kwenye ule mchuzi.
“Lazima ule la sivyo hutoki huku…”
Alisema Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake…baada kumwona akiogopa kuyala yale macho ambayo ni chakula maalum kilicho andaliwa kwa niaba ya wachawi watakao hudhulia Mkutano gambosh.
Makongoro aliyatazama yale macho yaliyokuwa yakielea kwenye mchuzi ndani ya bakuli..kisha akamtazama na babu yake ambae alionekana kula chakula kile bila wasiwasi…ghafla mate yalimjaa Makongoro mdoni,,akahisi kichefuchefu….na punde si punde alitapika..kitendo ambacho kiliwafanya wachawi wote waliokuwemo ndani ya chumba kile kusimama huku wakikodele macho meza ambayo alikuwa kakaa Mzee baluguza na mjukuu wake ambae ni Makongoro.
“Nani huyo ambae anafanya ujinga hum ndani??..” Mchawi mmoja mwenye ulemavu wa ngozi yaani albino..alisikika akisema hivyo kwa sauti kali..ambapo hapo hapo,alionekana mchawi mwingine alinyoosha kidole kuelekea kwenye meza ambayo aliketi Mzee baluguza nammjukuu wake.
Hivyo baada mchawi yule albino kuonyeshwa ,,haraka sana alizipiga hatua kuelekea kule alikokuwa Mzee baluguza…wakati huo Mzee baluguza akimwambia mjukuu wake kwa sauti ya kunong’ona..akisema “Unaona sasa tayali umeshavuruga…tangu awali nilikwambia chochote utakacho letewa we kula tu hata kwa kujikaza ili ufuzu zoezi la kupata uchawi !! Lakini wewe unajifanya mtoto wa mjini,,haya sasa kazi kwako..huyooo albino anakuja”
Alisema hivyo Mzee baluguza huku akiangalia jicho ngembe kule anakutokea mchawi albino.. Makongoro aliogopa,hima alinyanyuka kutoka kwenye kiti akitaka kumkimbia mchawi albino..lakini Mzee baluguza alimtuliza kwa kumwambia kuwa “endapo ukikimbia basi utakufa” Makongoro baada kusikia neno hilo kutoka kwa babu yake..woga ulizidi maladufu..akajikuta yupo Kati kwa Kati,kukaa alishindwa pia kukimbia alishindwa…Hivyo alisimama huku akitetemeka,na macho yake yakimtazama mchawi albino ambae nae alizidi kuzipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa Mzee baluguza na Makongoro.
Baada mchawi albino kufika katika meza ile ya Mzee baluguza..ghafla alimshika Makongoro kisha akavuta kwake kwa nguvu…huku akiongea rugha ambayo Makongoro na babu yake hawakuweza kuielewa…
Hakika Makongoro alipasa sauti ya kilio..akiomba msaada asaidiwe..lakini cha ajabu wachawi wote waliokuwemo ndani ya kile chumba akiwemo Mzee baluguza..hakuna aliejitolea kumng’atua Makongoro katika mikono ya yule mchawi albino ambae alionekana kutaka kumuua Makongoro.
Hivyo wachawi wote waliishia kutazama tu..wakati huo minong’ono mbili mbili ikisikika kwa chini chini..minong’ono ambayo ilisikika ikimsifu mchawi yule albino kwa uhodari aliokuwa nao wa kupigana kichawi….wakati huo Mzee baluguza yeye alikuwa ameweka mikono kichwani akitazama jinsi mjukuu wake alivyokabwa na mchawi albino…kwa hakika alimwonea huruma sana,,alitamani kwenda kumwokoa..lakini Mzee baluguza akajikuta kuwa nguvu alizo nazo hawezi kupigana na mchawi albino..mchawi ambae alibarikiwa nguvu aina Saba za giza.
Lakini wakati mchawi yule albino,alipokuwa akiendelea kukazana kutaka kumtoa roho Makongoro..mala ghafla katika wachawi wale therathini waliosafiri na Makongoro kutoka sumbawanga mpaka gambosh..alijitikoze mmoja ambae alifahamika kwa jina gwimo..ambapo gwimo kwa kutumia kiganja chake aliunyoosha mkono wake kisha akampiga moto mchawi albino..nae baada ule moto kumpata,haraka sana alimwachia Makongoro..kisha akamgeukia yule aliempiga moto wa kichawi.
Hivyo akionekana kughadhibishwa na kitendo kile..mchawi albino aliongea tena maneno yasiyoeleweka..lakini hakujibiwa na mtu..zaidi gwimo alijitokeza na kisha kusemama “Mimi hapa gwimo mwana wa gwimo” Kwa kauli ya kishujaa kabisa mchawi gwimo alijigamba mbele ya mchawi albino..ambae alikuwa si mchezo katika shunghuli nzima ya kupigana kichawi.
Wakati Mzee baluguza akimnyoosha mjukuu wake shingo baada kutoka kwenye imaya ya mchawi albino…upande mwingine nako walionekana wachawi baadhi wakisogeza meza kando ili kuwaachia nafasi mchawi gwimo na mchawi albino..ambae tayali alikuwa amesha badilika uso kutoka katika umbile la kibinadam..na kuingia katika umbile lingine tofauti..maskio yake yalipotea huku macho yake nayo yakionekana kuwa kama ya nyoka.
Wakati huo gwimo yeye hakubadilika kitu chochote..zaidi aliikaza vizuri kiunoni vazi lake nyeusi..kisha akasimama katikati ya uwanja..ambapo mchawi yule albino aliasama mdomo wake..ghafla ulitoka moto mkali uliomfuata gwimo ..lakini kwa kuwa gwimo nae hakuwa haba..hivyo aliweza kuukwepa moto ule.
Hakika shangwe za kumshangilia gwimo..zilisikika baada kupangua moto ule .na pia ziliongezeka maladufu baada gwimo kujibu shambulizi ambalo moja kwa moja lilimkuta mchawi albino..ambapo alianguka chini mfano wa mzigo wa kuni utokapo kichwani.
Kwa hasira kali mchawi albino alinyanyuka akata kujibu shambulizi..lakini ghafla kengere ililia kuashilia kuwa muda wa kurudi ukumbini umewadia..na hivyo mchawi yule albino alirudi katika hali yake ya ubinadam..kisha wakaelekea ukumbini..wakati huo Mzee baluguza akiwa sambamba kabisa na mjukuu wake Makongoro..ambae nae baada kunusurika kifo kutoka kwa mchawi yule katili albino,alitamani akalipe kisasi kwanza pindi atakapo pewa uchawi.
Hivyo mala baada kufika ukumbini..ghafla ilisikika sauti ya mkuu wa wachawi ikiwata wale wachawi waliokuwa wakipigana watoke nje wakalishe misukule..mpaka pale kikao kitakapo kitakapo malizika..ambao watu hao ni mchawi albino pamoja na mchawi gwimo.
Wote walinyanyuka kila mmoja akimtamani mwenzie,,kisha wakapotea pale kwenye kikao..ambapo baada kupotea kwa hao wachawi..punde punde mkuu yule wa wachawi gambosh..aliwataka chipkizi wanao hitaji uchawi…….Hivyo haraka sana Mzee baluguza alirudia kumkubusha Makongoro..akisema “Tafadhali nakuomba uchague uchawi wa kuua na kujirinda dhidi ya maadui sawa sawaa” Aliaisitiza Mzee baluguza..wakati huo Makongoro akiwa tayali kanyuka..hivyo alizipiga hatua kuelekea kwa mkuu wa wachawi,,hakuwa peke yake bali alikuwa na chipkizi wengine mbalimbali wiliotoka mataifa tofauti tofauti ndani na nje ya bara la Africa.
Na baada Makongoro na wenzake kufika kwa mkuu yule wa wachawi..hatimae aliondoka nao moja kwa moja mpaka kwenye chumba cha kiapo..ambapo katika chumba hicho zilisikika sauti mbalimbali za wafu pamoja na harufu mbaya iliyoenea chumba kizima..Hakika Makongoro aliogopa sana,,ila aliamua kupiga moyo konde,na hivyo punde si punde ilisikika sauti nzito ndani ya kile chumba cha kiapo..saut ambayo ilisikika ikisema “kabla ya kuapa..lazima ule kwanza nyama mbichi ya binadam pamoja na kikombe cha damu..kwani hicho ndicho chakula chetu stahiki kama ilivyo wali kwa mwanadam wa kawaida”
Kwisha kusema hivyo..ghafla mbele yake Makongoro alitokea mtu alievaa koti jeusi kuanzia juu mpaka chini,,,,akamkabidhi Makongoro bilauli kubwa lililokuwa limejaaa ulimi na sehem ya Siri ya mwaume pamoja na moyo bila kusahau kikombe kikubwa kilicho sheheni damu nzito ya binadam.
Makongoro alizitazama zile nyama..ambazo zilikuwa zikitoka dam wakati wote..Hakika alijutia kwanini aliamua kwenda kumtembelea babu yake kijijini..maana laiti kama ningebaki zake mjini,basi hayo mambo yote yasingemkuta…Hivyo Makongoro akiwa ameyafumba macho yake..alikula zile nyama mbichi moja baada ya nyingine..na baada kumaliza alishushia na damu nzito iliyokuwa kwenye kikombe..wakati huo huo kwa mbali zilisikika sauti za watoto wakishangilia,,,sauti ambazo Makongoro hakuweza kutambua mahali zinapotokea.
Na Makongoro alipokuwa akiendelea kustajabishwa na zile sauti za watoto..mala ghafla mbele yake alitokea mkuu wa kichawi huku akiwa na jungu kubwa lililokuwa likifuka moshi mweusi…mkuu yule alitabasam baada kumwona Makongoro kafuzu mtihani wa kula nyama mbichi..hivyo moja kwa moja alimwamlisha anyooshe mkono wake,,nae Makongoro alifanya hivyo hivyo…ambapo mkuu yule wa wachawi alimshika mkono,kisha akasema
“Unaitwa nani..??”
“Makongoro..”
“Anhaa jina nzuri sana kijana..pia nikupe pongezi ya kufaulu huu mtihani mzito,,kwa Hakika wewe ni jasiri kupita kipimo na nakutabilia kwa siku za usoni wewe utatisha bala nzima la Africa….Lakini yote kwa yote..napenda Nikuulize maswali tofauti tofauti..na katika kujibu tamka neno..ng’onilo sawa kijana??..”
“Sawa” Aliitikia Makongoro hivyo huku akijifuta baadhi ya mabaki ya damu katika mdomo wake.
Na hapo ndipo mkuu yule wa wachawi alipo anza kumuuliza maswali mbalimbali Makongoro…na kati ya maswali hayo aligusia jinsi gani kijana ataweza kuilinda na kuiheshim kazi yake ya kichawi…nae kwa kujiamini Makongoro alijibu “Ndio nitailinda na kuiheshim”…Baada Makongoro kujiibu vizuri,ghafla kilitokea kitabu kikubwa kwa mkuu yule wa wachawi..na muda huo huo ulitokea msukule..msukule ule ulizipiga hatua mpaka kwa mkuu wa wachawi kisha akainama chini..ambapo uliweza kugeuka kuwa meza.
Hivyo mkuu yule wa wachawi akawa amekiweka kitabu juu ya mgongo wa msukule ambao umegeuka kuwa meza..kisha akamwita Makongoro ili asaini..Makongoro nae kwa kua kila kitu kigumu alikuwa ameshakivuka,,Hakika hakusita kwenda kusaini..alisaini kwa kujiamini kabisa..kwani baada kuinywa damu ile ya binadam nafsi yake iliingia dosari kidogo..dosari ya kutokuogopa kitu.
Na wakati hayo yakiendelea..upande mwingine nako..alionekana mchawi albino na mchawi gwimo wakizozana…badala ya kufanya kazi waliyopewa ya kulisha misukule kama moja ya adhabu waliyopewa na mkuu wao wa wachawi,,baada kuonekana wamegombana kinyume na sheria ya gambosh…hatimae walijikuta wakirudia kupigana..ambapo mchokozi alikuwa ni mchawi albino ambae hapo awali alionekana kuzidiwa uwezo na gwimo licha ya yeye kusifika kwa uhodari wa kupigana kichawi zaidi…hivyo lengo la mchawi albino ni kutaka kumnyoosha gwimo ili atunze heshima yake katika kijiji kile cha gambosh.
Hakika patashika nguo kuchanika mapigano ya nguvu yakiendelea katika nyumba ile ya kutunzia misukule..wakati huo misukule nayo ikilia njaa kiasi kwamba ilivunja milango na madirisha..kisha ikasambaa sehem mbalimbali..Huku ugomvi wa mchawi albino na gwimo bado ukiendelea kupamba moto,pasipo kujuwa kuwa wamesababisha balaa la misukule kutoroka.
Na ugomvi ule ilipokuwa ukiendelea…Kwingineko nako..mkuu wa wachawi alionekana kumkabidhi Makongoro hirizi tisa zenye ukubwa tofauti tofauti kisha akaondoka nae moja kwa moja mpaka kwenye Mkutano..ambapo alikuta maongezi mbalimbali yakiendelea katika ukumbi ule wa wachawi..na hivyo baada mkuu kutokea,hatimae kimya kizito kilitawala huku wachawi wale wakijiuliza chipkizi wengine wako wapi mpaka mkuu arudi na chipkizi mmoja ambae ni Makongoro..lakini maswali yao kabla hawajayapatia majibu,,mala ghafla mkuu yule wa wachawi alipasa sauti akisema “Kwanza kabla ya yote,,ebu mpongezeni kijana huyu Mdogo kwa kile alicho kifanya..kwa Hakika huyu ni kijana jasiri natumai siku za karibuni atatisha sana” Alisema mkuu yule wa wachawi..ambapo hapo kelele za wachawi wakimpongeza Makongoro zililindima kila kona ya ukumbi..ila kasoro mtu mmoja tu hakuweza kumpongeza Makongoro..ambae nae si mwingine ni mwalimu shija…
Hivyo mala baada pongezi kumfikia Makongoro..hatimae mkuu yule wa wachawi alielezea aina ya chakula alichopewa Makongoro kama moja ya mtihani.. Hakika wachawi wote walibaki midomo wazi…wakati huo Mzee baluguza akimtazama mjukuu wake na kisha kusema “Inaamna supu ya macho mbaya..ila nyama mbichi tena ya sehem ya Siri ndio tamu??…Hahahaaaaa kweli mjukuu ninae..pole yao Mzee mwakipesile” Hakika Mzee baluguza alisema hivyo huku akiachia tabasam pana.
Hivyo baada ya hayo mkuu wa wachawi..alitaka kufunga kikao..lakini kabla hajafunga,ghafla Bibi mmoja alietokea nchini Congo ambae nae alimpeleka mjukuu wake gambosh ili apewe uchawi..alisimama na kisha kuhoji mahali alipo mjukuu wake pamoja na wenzake..
“Wameshindwa mtihani..kwahiyo sheria yetu inasema mtu yeyote akiferi mtuhani..hastahili kurudi katika jamii ya watu wa kawaida kwa maana atavujisha Siri” Kwa sauti Kali…mkuu yule wa wachawi alimjibu bibi kizee…ambapo nae baada kusikia maneno hayo aliangua kilio kikubwa huku akilitaja jina lamjukuu wake..
Wakati huo huo mkuu yule alifunga kikao kisha akatoweka..
Na baada mkuu wao kuondoka!?..Mzee baluguza alizipiga hatua kumfuata mjukuu wake alietunukiwa jopo la hirizi na uchawi wa kutosha…hivyo moja kwa moja walijikusanya pamoja kama walivyotua katika ardhi ya gambosh..lakini kati yao alipungua mmoja ili watimie therathini …ambae ni gwimo..kwahiyo haraka sana harakati za kumtafuta zilifanyika..lakini hakuweza kumpata..na hivyo mkuu wa msafara alichukua kisu chake kidogo..ambapo kufumba na kufumbua kiligeuka kuwa ndege..wote walipanda hatimae safari ya kurudi Tanzania ikaanzaa baada kukaa gambosh kwa siku mbili……Hivyo ndege ile ya kichawi baada kufika sumbawanga ilitua chini..ambapo walishuka Mzee baluguza na mjukuu wake kisha kila mmoja akachukua ungo..na safari ya kurejea kijijini bhonde iliendelea,,wakati kijiji kilikuwa kimechafuka wakimtafuta Mzee baluguza kwa udi na uvumba ili wamuuwe baada kugundulika kuwa yeye ndio alie husika na kifo cha mama chiku..mama muuza pombe alieuwawa kikatili kwa kukatwa shingo na Mzee baluguza..wakati huo huo Mzee kinono nae alikuwa akimuwinda Makongoro ili amteketeze.
Mzee baluguza akiwa na mjukuu wake ndani ya ungo wakirudi kijijini baada kutoka gambosh..ghafla walishtuka walipoona moto ukiwaka kwa mbali katika kijiji chao cha bhonde…hivyo moja kwa moja Mzee baluguza Alimtazama mjukuu wake ambae alikuwa pembeni yake kidogo,kisha akasema “Makongoro jiandae,,maana moto ule unao uona si bure”
Alisema Mzee baluguza huku akijifunga vizuri hirizi yake kwenye mkono wake…ambapo nae Makongoro alifanya hivyo hivyo…na baada ya dakika kadhaa,walitua chini nje kidogo na nyumba yake Mzee baluguza…ambapo baluguza na mjukuu wake,kwa pamoja walichuchumaa style ya kupiga magoti mfano ya wanariadha,,punde si punde walipotea nje,wakatokea ndani.
Hakika kitendo kile kilimfrahisha sana Makongoro…akajikuta akitabasam huku akimtazama babu yake,ambapo nae Mzee baluguza aliachia tabasam kama vile alivyofanya mjukuu wake,kisha akasema “Naam Makongoro kazi nzuri…Sasa kama wanajiamini wachokoze moto huu” Alisema Mzee baluguza akionekana kujiamini kabisa.
“Hahahaaa babu bwanaa sawa mimi niko sawa kila idara” Makongoro alijibu hivyo huku akipiga kifua chake kuonyesha kuwa yupo sawa kwa lolote kwa chochote.
“Sawa mjukuu wangu nenda kalale ila kumbuka kesho pasaka,,hivyo mchana tutajumuika pamoja kufrahia sikukuu,ila usiku tutaelekea buharamulo kwenda kula chakula chetu cha kichawi”
“Sawa babu nimekuelewa..usiku mwema” Makongoro alimjibu babu yake kisha akaingia chumbani kwake.
Wakati hayo yakiendelea,upande ule ambako ilionekana moto..walionekana wachawi wa kijiji cha bhonde wakiimbana kucheza huku wakiwa uchi,,wakati huo pembeni yao likionekana jungu kubwa lililokuwa limejaaa nyama za binadam likiwa juu ya mafiga…hivyo baada kuimba na kucheza kwa muda mrefu,hatimae mkuu wa hafra ile ya kichawi alistisha ngoma kisha akasema “Jamani tumefrahi vya kutosha..tukiimba na kucheza ila kwa sasa ni muda wa kula kitoweo kilicho andaliwa mahususi kwa siku ya leo” Kwisha kusema hivyo mkuu yule wa hafra ambae aliitwa Mzee dole tupu,,ghafla kelele na moyowe ya wachawi zilisikika kila pande…huku mirunzi kadha wa kadha nayo ikifuatia…bila shaka hiyo yote ilikuwa ni furaha ya kusikia jina kitoweo.
Mkuu wa hafra alimteua Mzee sule ndio awe mgawaji wa chakula…hivyo Mzee sule aliweza kuifanya kazi ile kwa umakini zaidi..nacho chakula kile zilikuwa ni nyama za binadam.
Baada wachawi wale walipomaliza kula chakula chao,,hatimae mkuu wa hafra aliwataka waondoke majumbani mwao…lakini kabla hawajasambaa,mala ghafla alikuja popo katika sherehe ile..popo huyo alitua moja kwa moja kwenye bega la Bi kileleganya ambae muda wote mwanzo mpaka mwisho wa sherehe alikuwa kakaa pembeni akiwatazama wachawi wake jinsi wanavyo frahia sherehe..
Hivyo baada popo yule kutua kwenye bega la Bi kileleganya….hima alisimama kisha akasema “Natumain wote kwa pamoja mmefurahi sana..lakini furaha yenu hii isiwafanye mjisahau kujilinda..” Alisema Bi kileleganya kisha akameza mate..lakini kabla hajaendelea,mala ghafla ilisikika sauti ya mmoja ya wachawi,,sauti hiyo ilisikika ikisema ” Unamaana gani mkuu” Kwisha kusema hivyo yule mchawi..wachawi wenzake walimtazama kwa jicho baya..huku kwa kunong’ona ilisikika sauti nyingine ikimjibu “We kaa kimya..usirudie tena kuongea wakati mkuu hajamaliza kuongea” Alionywa hivyo yule mtu..ambapo nae aliomba radhi huku akionekana kuwa na hofu..lakini Bi kileleganya,licha ya kuisikia ile sauti..ila hakuweza kudili nayo kwani alijuwa ni presha iliyomkamata mchawi wake…hivyo aliendelea na kitu alichotaka kuongea..” Jamani naombeni nisiwachoshe…ila ninacho wataka ni nyinyi kuwa makini..maana Mzee Baluguza karudi…” Alisema kwa msisitizo Bi kileleganya huku akiwakodolea macho wachawi wake..ambao nao walionekana kupigwa na butwaa baada kusikia jina Baluguza.
Na wakati wachawi wale wakiwa katika dimbwi la wasiwasi…mala ghafla Bi kileleganya alimwita Mzee mwakipesile,kisha akamwambia ” Mwakipesile fanya kazi yako sasa ya kutuletea yule mjukuu wa Mzee baluguza kwenye familia yetu..Sawa sawaa??..”
“Sawa mkuu…” Kizee mwakipesile alijibu kwa heshima..
“Haya mnaweza kurudi majumbani kwenu” Aliongeza kwa kusema hivyo mkuu yule wa wachawi kijijini bhonde..ambapo yeye ndio alikuwa wa kwanza kupotea maeneo yale,,kisha wengine wakafuatia..punde si punde wote walipotea.
Usiku uleule kabla hapajakucha…Gambosh nchini Nigeria..Mchawi albino na mchawi gwimo..walijukuta wakiwa katika wakati mgumu baada kukutwa wakigombana…wakati huo wakisababisha misukule kutoroka.
Katika chumba mahususi kwa niaba ya mateso..walipelekwa wachawi wale..lakini kwa kuwa mchawi albino alikuwa akijiamini kwa sababu ya kuwa na nguvu nyingi za giza,hatimae alipinga mateso ambayo angeyapata..kitendo kilicho mkera mkuu wa kitengo cha mateso..ambapo aliamulu kuwa mchawi albino abebe naaadhabu ya gwimo….hivyo gwimo nae alibadishiwa adhabu..ambapo alipelekwa shambani kulima.
Hakika gwimo alilima sana siku hiyo…istoshe alipokonywa nguvu zake za kichawi…hivyo akawa analima yeye kama yeye..
Wakati huo katika chumba kile cha mateso ilikuwa patashika nguo kuchanika,,ugomvi Kati ya mchawi yule albino na mkuu wa kitengo cha mateso…kwani mchawi albino alionekana kupinga mateso,,na hivyo ikawa imefikia hatua ya kupigana…..Lakini wakati wakiwa katika mapigano,,mala ghafla alitokea mkuu wa wachawi Africa nzima…Mkuu yule alionekana mifupa tu bila ngozi wala nyama za mwili..ambapo mkuu yule wa wachawi kwa kutumia rupia yake aliyokuwa nayo mkononi…aliizungusha kwa kuipitisha katikati ya vidole vyake…wakati huo mchawi albino alikuwa akiishiwa nguvu kila sekunde zilivyozidi kwenda…mwishowe kabisa akinyong’onyea kabisa..ambapo alifungwa nyororo kisha akavuliwa nguo mwili mzima..na punde si punde baada kufungwa mnyororo,ghafla alitokea mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitano..mtoto yule alizipiga hatua kuelekea mahali alipokuwa mchawi albino akiwa katika fundo za nyororo..Hivyo baada kumfikia…mtoto yule alinyoosha mkono wake juu..punde si punde Katika mkono wa yule mtoto ilitokea bakuli kubwa na mkasi mdogo mkali…..mtoto yule alicheka kwa sauti Kali iliyoambatana na mwangwi mkali,,na mala baada kumaliza kucheka,aliuchukua mkasi kisha akaanza kukata kiungo kimoja baada ya kingine kwenye mwili wa mchawi albino,,ambae nae alipasa sauti Kali ya kuhisi maumivu.
Wakati huo kijiji bhonde..wachawi wote waliingiwa na hofu baada kusikia habari za Mzee baluguza…lakini hali hiyo ilikuwa tofauti kwa Mzee kinono..kwani baada kusikia kuwa Mzee baluguza karudi,haraka sana alichukua ungo wake,kisha akapaa kumfuata nyumbani kwake kwa lengo la kwenda kumuuwa Makongoro..mjukuu wa Mzee baluguza..pasipo kujuwa kuwa Makongoro nae kapewa uchawi.
Angani saa za usiku..alionekana Mzee kinono akiwa ndani ya ungo akisafiri kumfuata Makongoro kwa nia ya kulipa kisasi…kwani ikumbukwe kuwa Makongoro alimpa paka jiwe,,pasipo kujuwa kuwa paka yule alikuwa ni mtoto wa Mzee kinono..Na Hivyo kitendo kile kilimkela sana Mzee kinono,,mpaka akaamuwa kujenga chuki dhidi ya Mzee baluguza ambae ni babu yake Makongoro.
Lakini kabla Mzee kinono hajatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza,,mala ghafla ungo wake uliyumbishwa..Mzee kinono alishtuka baada kuona hali ile..Hivyo alichukua kibuyu chake kidogo alichosafiri nacho,pia akachukua na kipisi cha mkia wa ng’ombe..ambapo mkia ule aliuchovya kwenye kile kibuyu chake kilichokuwa na damu kisha akanyunyuzia kila pande kuu ya dunia.
Na mala baada Mzee kinono kufanya hicho kitendo…haraka sana alifungua mkoba wake chakavu,kisha akatoa hirizi kubwa,,hirizi hiyo alijifunga kwenye mkono wake huku akiongea maneno ya kichawi….ambapo punde si punde ungo ulitulia.
“Mimi ndio mfalme wenu pumbafu zenu” Alijigamba hivyo Mzee kinono baada kufanikisha kuutuliza ungo wake kwenye ramani sahihi..wakati huo kwa mbali walionekana wachawi wengine wakielekea kule alikitoka Mzee kinono,,lakini cha ajabu wale wachawi waligeuka na kisha kumfuata Mzee kinono kwa kasi ya ajabu..
Kwa hakika Mzee kinono nae baada kujishtukia kuwa anafuatwa na wachawi nyuma yake..hima nae aliongeza kasi ili kuwakimbia wale wachawi ambao walionekana kuwa na uwezo mkubwa kuliko yeye.
Hivyo wakati hayo yakiendelea…upande mwingine nako Makongoro nae alipokuwa amelala kitandani..mala ghafla alishtuka kutoka usingizi baada kusikia sauti ikimwita…..sauti hiyo haikuwa ya mtu mwingine bali ilikuwa sauti ya mkuu wa wachawi..ambapo Makongoro baada kuifaham ile sauti aliondoa hofu mwili,alisimama kando ya kitanda chake kisha akakaa tayali kumsikiliza mkuu wake anasemaje,,
Na wakati Makongoro alipokuwa kimya,,akimsikiza mkuu wake ili aseme neno..ghafla chumbani kwake ulitokea mwanga mkali…mwanga huo kabla haujatoweka mle chumbani..ulitokea mkono bila kiwiliwili,mkono huo ulikuwa umeshikilia hirizi ukimpatia kijana Makongoro.
Makongoro bila wasiwasi aliizipiga hatua kuifuta ile hirizi…Na mala tu alipo ishika ..sauti ya mkuu wa wachawi ilirudia kusikika ikisema “Makongoro hiyo ndio kila kitu kwako..Sema kitu chochote cha kichawi utakipata…Hivyo itunze itakusaidia” Kwisha kusema hivyo..ile sauti ilipotea,na mwanga ule mkali nao ulizimika..ambapo Makongoro nae alijifunga vizuri ile hirizi kwenye mkono wake kisha akarudia kitandani kulala..
Ils la kabla usingizi haujamkamata..ghafla ile hirizi aliyokuwa ameivaa mkononi ilianza kumbana kiasi kwamba akashindwa kulala..akawa amekaa kitandani tu….Na wakati huo huo. Mzee kinono tayali alikuwa ameshatua kwenye nyumba ya Mzee baluguza..ambapo baada kutua..Makongoro akiwa chumbani kwake alisikia mshindo,hivyo alisimama kutoka kitandani kisha akachukuwa nguo yake nyeusi ambayo alijifunga kiunoni..na moja kwa moja alizipiga hatua kuelekea kwenye kona ya chumba chake kisha..punde akawa amepotea akatokea nje.
Mzee kinono baada kumwona Makongoro alicheka sana kwa dharau na kejeli,,na baada kumalizika kucheka alisema “Eti na wewe unatuiga sisi??..sasa acha nikionyeshe ili utambue kuwa uchawi na ugolo ni vitu viwili tofauti” Alisema Mzee kinono akimaanisha kuwa Makongoro hana uchawi,bali anaugolo kwa sababu ugolo na uchawi vinafanana.
Hivyo Mzee kinono baada kusema hayo alirusha kombola moja la kichawi kuelekea mahali alipokuwa Makongoro..lakini cha ajabu Makongoro alipotea akatokea nyuma yake Mzee kinono..kitendo ambacho kilimshangaza sana Mzee kinono kwa uwezo ule aliouonyesha kijana Makongoro.
Ila licha ya Mzee kinono kushangazwa na uwezo ule wa Makongoro..kwa Hakika hakutaka kushindwa,,zaidi aligeuka nyuma yake alipokuwa amesimama Makongoro ambae nae alikuwa akicheka mfano wa mtu anaetekenywa.
Na mala baada Mzee kinono kumgeukia Makongoro..safari hiyo hakumrushia kombola,bali alimrushia moto wa kichawi..lakini moto ule kabla haujampata Makongoro..ghafla Makongoro aliunyoosha mkono wake wa kushoto uliokuwa na hirizi aliyopewa gambosh…punde si punde moto ule alio urusha Mzee kinono uliganda kisha ugeuzwa ukawa maji.
“Mmmh” Mzee kinono aliguna asiamini kama kweli Makongoro ndio anaeyafanya Mambo yale..wakati huo akijiandaa kumkimbia kabla kijana hajajibu mashambulizi.
Na haikuchukuwa muda Mzee kinono alipotea akatokea nyumbani kwake. ..ambapo baada kufika,moja kwa moja alichukua jungu lake lililokuwa na makorokoro ya kichawi kisha akaenda nalo mpaka sebleni kwake huku akijiuliza “mtoto yule uchawi mkali vile kautoa wapi??..Daah hapana mimi kinono bwana miaka dahali nipo kwenye uchawi,sasa iweje mtoto mdogo kabisa anishinde??…
ITAENDELEA
Isikupite Hii: Dalili za Kuonyesha Mwanamke Anataka Umpeleke Chumbani
Kijiji cha Wachawi Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;