Kitumbua cha Kihindi Sehemu ya Nne
IMEANDIKWA NA : KIZARO MWAKOBA
*********************************************************************************
Chombezo : Kitumbua Cha Kihindi
Sehemu ya Nne (4)
“Wewe unafanya biashara ya vitumbua lakini sio kitumbua cha kihindi” Zawadi naye akazungumza kwa msisitizo kwa kujitapa.
“Na kwa nini mara unasema vitumbua, mara kitumbua?”
“Nasema hivyo kwasababu hicho kitumbua kimoja kinaweza kufanya maisha yako yabadilike kabisa” Zawadi aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
“Mnh!” Ashura aliguna huku akiamini rafiki yake yule alikuwa akizungumza kwa mafumbo mafumbo nab ado hakuwa amefahamu maana kamili ya hicho kitumbua cha kihindi.
“Usigune, unachotakiwa kuniambia ni kwamba upo tayari ama haupo tayari kwa biashara” Zawadi alihoji huku akijitingisha tingisha na mikono yake kifuani.
Ashura alijiinamia kwa muda akitafakari juu ya jambo lile. Moyo wake ulikuwa tayari kabisa kwa kufanya biashara lakini nafsi yake ilisita kwasababu hadi kufikia muda ule alikuwa hajaifahamu biashara yenyewe kiundani.
“Nasubiri jibu, mbona umeinama kama kobe?” Zawadi alimgutusha Ashura
“Hapana Zawadi mie naona sipo tayari kwa biashara hiyo” Ashura alijikuta akitoa jibu pasipo kujielewa.
“Kuzaliwa masikini ni bahati mbaya, lakini kufa masikini ni uzembe wako mwenyewe” alizungumza Zawadi kwa kebehi.
“Unamaanisha nini Zawadi?” Ashura akahoji baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa shoga yake kipenzi.
“Utakufa na uimasikini wako mama” Zawadi alizungumza kwa msisitizo ulio mfanya Ashura kujutia jibu lake alilolitoa kwamba hakuwa tayari kufanya hiyo biashara ya kitumbua cha kihindi. Hata hivyo bado moyo wake haukuwa tayari kufanya hivyo biashara ambayo ilikosa maelezo ya kueleweka.
Sauti ya kengere ya mlango wa kuingilia ndani ndiyo iliyowagutusha na kuwatoa mle jikoni. Walipofika sebleni Ashura alikwenda kuketi kwenye kochi na Zawadi akaelekea mlangoni kufungua mlango.
“Woow! Karibu sana Mr. Nakeshwar” Alisema Zawadi baada ya kufungua mlango na kumuona mgeni wake.
“Thaks toto zuri” Mgongaji alijibu baada ya kukaribishwa na kuingia ndani.
Mgeni yule alikuwa ni mwanaume wa makamo mwenye umbo kubwa ambaye alikuwa na asili ya kihindi. Hakuwa mwingine bali kama alivyotajwa na Zawadi, alikuwa ni yule yule Mr. Nakeshwar mume wa Bi. Fahreen yule mama aliyekuwa anachepuka na Magosho kaka wa Ashura.
Mr. Nakeshwar aliingia ndani kwa Zawadi na kwenda moja kwa moja kuketi kwenye sofa pasipo kukaribishwa na mwenyeji wake. Zawadi naye alifunga mlango na kwenda kujiunga na mgeni wake.
“Your most welcome Boss” Zawadi alizungumza huku akijiweka kwenye kochi lililokuwa karibu na mgeni wake mpya.
“Sante sana toto zuri, vipi iko problem?” Mwanaume yule alizungumza kwa lafudhi ya kihindi huku macho yake yakiwa kwa Ashura.
ENDELEA….
Mr. Nakeshwar alionekana kuwa na mashaka juu ya uwepo wa Ashura pale ndani. Nafikiri hakuwa ametegemea kumkuta binti yule ndani ya nyumba ile ya Zawadi. Aliketi kwenye kochi lakini ndani ya nafsi yake hakuwa na Amani kabisa.
“Hakuna tatizo, huyu ni rafiki yangu anaitwa Ashura” Zawadi alijaribu kumtoa wasiwasi Mr. Nakeshwar kwa kumtambulisha Ashura.
“Oh Sura!” Nakeshwar alisema kwa bashasha.
“Ashura, huyu ni bosi wangu anaitwa Nakeshwar. Ndio yule niliyekueleza kuwa nafanya naye biashara” Alisema Zawadi.
“Nashukuru kukufahamu boss” Ashura alijibu huku akimtazama kwa woga mzee yule wa kihindi.
“Mimi iko furahi zaidi, iko zima veve?”
“Ndio, mimi ni mzima kabisa”Ashura alijitahidi kuficha wasiwasi wake juu ya mzee yule wa kihindi.
“Ok, good”
“Vipi bosi unaniambiaje” Zawadi alihoji kukatisha zile salamu za Ashura na Mr.Nakeshwar ambazo zilionekana kukosa ukomo.
“Yeah, Lete tumbua bhanaaa” alisema Mr.Nakeshwar huku akiweka mezani brifkesi yake ambayo alikuwa ameketi nayo kwenye kochi kwa kumhofia Ashura.
Ashura aliinuka na kuelekea chumbani huku akiwa amewaacha sebleni Mr. Nakeshwar na Ashura.
“Your so beautiful girl” alizungumza Mr. Nakeshwar huku akiachia tabasamu lililozibwa na midevu.
“Abee” Ashura aliitika huku akionekana hakuwa ameelewa alichokizungumza mzee yule wa kihindi.
“I mean, veve iko zuri sana” Mr. Nakeshwar akafafanua.
“Asante” Ashura alijibu kwa aibu huku akitoa tabasamu la kujilazimisha.
Baada ya dakika kadhaa Zawadi alirejea na Brifkesi nyingine kutoka chumbani na kuiweka mezani ambako kulikuwa na briefcase ile aliyokuja nayo Mr. Nakeshwar.
“Good work” alisema Nakeshwar baada ya Zawadi kuweka brifkesi ile juu ya meza. Ashura alikuwa ametulia akiutazama mchezo ule. Alikuwa na hamu kubwa ya kupata kujua ukweli juu ya kitumbua cha kihindi alichokuwa anakiimba rafiki yake Zawadi pasipo kutoa ufafanuzi kamili.
Zawadi alifungua ile brifkesi na kuiwacha wazi. Ilikuwa imejaa vitumbua, kwa mahesabu ya haraka hara vilikuwa takribani vitumbua hamsini hivi. Mr.Nakeshwar aliokota kitumbua kimoja na kukimega kisha akakikodolea macho kwa makini na kukionja halafu akaachia tabasamu la matumaini.
“Vizuri Zawadi” alisema huku akifunga ile briefcase iliyokuwa imejaa vitumbua na kuvuta brifkesi yake ambayo ilikuwa mezani na kuifungua.
Noti za kitanzania zilizokuwa na thamani ya Elfu kumi zilikuwa zimefungwa kwenye maburungutu na kujaa ndani ya brifkesi ile aliyokuwa ameifungua Mr.Nakeshwar.
Ashura alihisi mapigo ya moyo wake yakidunda kwa kasi baada ya kuona ile minoti ndani ya briefcase ile. Akazidi kuchanganyikiwa na kuto kuelewakabisa juu ya biashara ile ya vitumbua. Akapiga moyo konde na kutulia kuendelea kuusoma mchezo ule.
“Poa bosi” Zawadi alisema na kuvuta ile brifkesi ya pesa, na Mr.Nakeshwar naye akavuta ile iliyokuwa na vitumbua. Walizifunga brifkesi zile kisha kila mmoja akawa amebaki ameshikilia ya kwake yaani wakawa wamebadilishana. Walitazamana kwa sekunde kadhaa kisha kila mmoja aliinua kidole cha mwisho juu kama ishara yao ya ushindi.
Pasipo kuzungumza neno lolote Mr.Nakeshwar alijiinua kutoka pale kwenye kochi na kutoka nje. Zawadi akawa amebakia na Brifkesi yake iliyokuwa imejaa maburungutu ya pesa.
Wakati wote huo Ashura alikuwa ametulia kwenye kiti akiutazama mchezo ule waliokuwa wakiucheza zawadi na mwanaume yule wa kihindi.
“Vipi shost” Zawadi alimgeukia Ashura baada ya kuondoka kwa Mr.Nakeshwar.
“Yaani ndio mmenichanganya kabisaaaa” alisema Ashura huku akikuna nywele zake.
“Kipi kilichokuchanganya sasa?” Zawadi akahoji kwa umakini.
“Hizo pesa ni za nini?” alihoji Ashura kwa umakini mkubwa.
“Ashura bwana maswali yako mwenzangu!”
“Nauliza kweli Zawadi namaanisha” Ashula akazungumza kwa msisitizo zaidi.
“Si umeona nimeuza vitumbua jamani au umeona kuna kitu gani kimetokea hapa?” Zawadi alijibu kwa kumalizia na swali.
“Vitumbua vile haviwezi kuwa na thamani ya pesa yote hiyo” alisema Ashura huku akioneshea kidole ile brifkesi iliyokuwa na pesa.
“Ulivipika wewe?” Zawadi akahoji kwa mkato baada ya kumuona rafiki yake yule hataki kukubaliana na ukweli.
“Mimi sio mgeni wa biashara ya vitumbua Zawadi” Ashura aliendelea kubishana na ukweli ule aliokuwa ameushuhudia.
“Lakini Ashura sijui kwanini umeng’ang’ania kuto kuelewa”
“Kwasababu sielewi!” Ashura akajibu kwa msisitizo.
“Unasema unajua biashara ya vitumbua, umeshawahi kupika vitumbua vya kihindi wewe?” alihoji Zawadi kwa msisitizo.
“Hata kama view vya kihindi au vya kisukuma, bado haujanishawishi”
“Shauri yako, mjini shule” alisema Zawadi na kuingia chumbani na Brifkesi yake iliyokuwa na pesa alizoziacha Mr.Nakeshwar.
*****
Taarifa za ujio wa Rachna binti wa kwanza wa Mr.Nakeshwar na Bi.Fahreen zilipokelewa kwa furaha sana na wazazi hao wawili. Walikuwa wakiwapenda sana watoto wao ambao walikuwa wawili tu kama mboni za macho yao. Watoto hao walikuwa ni Rachna na mdogo wake wa kiume Natal.
Kitendo cha Rachna kusoma mbali na nyumbani kilizidisha mapenzi kutoka kwa wazazi wake ingawa alikuwa binti mkubwa.
Macho ya Magosho hayakuweza kuamini pale alipomuona Rachna na Bi.Fahreen wakitembea maeneo ya Airport kuelekea pale alipokuwa amepaki gari. Akiwa amesimama huku ameegemea gari na funguo amezining’iniza mkononi, alimkazia jicho Rachna binti wa kihindi aliyekuwa amevalia suruali ya jinzi ambayo ilikuwa imembana ipasavyo na kupelekea umbo lake kuonekana vizuri zaidi, na juu alikuwa amevalia T-shirt nyeupe iliyokuwa na michirizi myeusi kwenye ukosi na kwenye pindo za mikono.
“Mungu wangu!” Magosho alitamka kwa sauti ya chini kisha akazunguuka nyuma ya gari na kufungua buti kwaajili ya kuweka begi la msichana Rachna.
“Gosoo kuje pokea geni bhanaa!” Bi.Fahreen alipaza sauti kumwambia Magosho ambaye alikuwa amesimama nyuma ya gari akiwasubiri.
Magosho hakuwa na kipingamizi zaidi ya kufanya vile ambavyo mke wa bosi wake alimuamuru. Mzigo wenyewe ulikuwa ni begi dogo tu la nguo tena lilikuwa likiburuzwa na matairi yake. Magosho akatembea kwa haraka hadi pale walipofika Bi.Fahreen na binti yake.
“Karibu sana dada Rachna” Magosho alizungumza na kupokea begi lililokuwa likivutwa na Bi.Fahreen.
“Thank you brother, sante sana” Rachna alijibu kwa sauti ambayo ilipenya kwenye masikio ya Magosho na kumfanya ahisi hali fulani tofauti kwenye ubongo wake.
Magosho alipokuwa akiliweka sawa lile begi ili aweze kulivuta vizuri, Bi.Fahreen na Rachna walitangulia na kumuacha nyuma.
“M a m a y a n g u!” Magosho aliendelea kutaharuki baada ya kuona jinsi Rachna alivyokuwa amezawadiwa kamzigo ka uchokozi huko nyuma.
Magosho alivuta begi taratibu kwa kuwafuata nyuma huku macho yake yakiwa yameganda kwa mtoto wa bosi wake. Jamani nyie mwacheni tu Magosho wawatu apagawe, maana huyo Rachna jinsi alivyokuwa mnh!
“Mtoto nyonga!” alisema Magosho kwa sauti ndogo kusifia jinsi hipsi zilivyomfanya binti yule wa kihindi avutie zaidi. Na ukizingatia alikuwa amevaa suruali basi umbo lilikuwa limejichora sawia kiasi cha mtu yoyote yule kuweza kushuhudia baraka alizokuwa amependelewa binti yule wa kihindi, nakwambia utafikiri toto la kisukuma jinsi lilivyoumbika.
“We nimalize tu!” Magosho aliendelea kuzungumza pekeyake hasa alipoona jinsi kale kamzigo ka Rachna kalivyokuwa kakitikisika kwa midundo ya hatua zake. Jamani nyie loooh!
Magosho alisahau kabisa kuangalia lile zigo zito lililokuwa likimvutia siku zote kwa Bi. Fahreen. Pamoja na kwamba Bi. Fahreen alikuwa akidondosha kwa kuyachanganya manyanga lakini kijana Magosho hakuona kabisa siku hiyo. Macho yake yote yalikuwa kwa Rachna.
Bi.Fahreen na Rachna walifika pale kulipokuwa na parking na kufungua milango ya gari kisha wakaingia tayari kwa safari ya kuelekea nyumbani. Rachna aliketi siti ya nyuma na Bi.Fahreen akaketi siti ya mbele kama ilivyokuwa kawaida. Alikuwa akipenda sana kukaa siti ya mbele ili kuwa karibu na kiburudisho chake.
Magosho alipakia begi kwenye buti kisha akaelekea ndani ya gari ambapo aliyekuwa ameachiwa jukumu lake la kuendesha.
“Pole kwa safari mgeni wetu” alizungumza Magosho huku akikunja kona kuiweka gari sawa kwa safari ya kurejea nyumbani Kariakoo.
“Thanks my brother, am home now” alisema Rachna huku akitabasamu.
Magosho alimtupia jicho Rachna kwa kupitia kioo kidogo kilichokuwa pale mbele kwa juu. Tabasamu la binti yule lilizidi kummaliza kijana wawatu wa kibantu. Ulipita ukimya wa dakika kadhaa ndipo Bi.Fahreen akaamua kuvunja ukimya ule.
“Gosoo” aliita Bi.Fahreen pasipo kumuangalia Magosho
“Naam mama” Magosho aliitika kwa heshima na utulivu mkubwa huku akibadilisha gia kwa kupanga na kupangua.
“What! umeniitaje?” Bi.Fahreen alihoji kwa hamaki baada ya kusikia Magosho amemuita mama. Siku zote Bi. Fahreen alipendelea kuitwa majina ya kimahaba na sio mama. Sasa siku hiyo Magosho alimuita mama kutokana na uwepo wa Rachna mle ndani ya gari. Hata hivyo mwanamke yule mtu mzima alionekana kutokujali uwepo wa binti yake na kutaka kuleta masuala yao ya mahaba.
Magosho aligeuza shingo yake kumtazama Bi.Fahreen ambaye siku zote alikuwa anapenda amuite mpenzi, au baby hasa wawapo wenyewe wawili. Na alichukia sana kuitwa mama. Kosa hilo ndilo ambalo Magosho alikuwa amelifanya.
“Usinitazame, umeniitaje?” Bi.Fahreen alisisitiza swali lake huku ametoa macho.
“Basi Bosi nisamehe” Magosho ilimbidi atunge jibu la kumpa mama yule aliyekuwa na balaa.
“Enhee iko namna hiyo, mimi bosi yako bhanaa” Bi.Fahreen alijibu huku akitingisha kichwa kujifanya kuwa alikuwa anataka Magosho amuite Bosi. Kumbe alikuwa amejisahau kama walikuwa na mtu mwengine mle ndani ndani ya gari.
“Iko ona toto yangu vhevhe?” alihoji bi Fahreen kwa kujibaraguza.
“Ndio bosi nimemuona, mmefanana sana” alisema Magosho huku akipangua gia na kukata kona.
“Kweli?”
“Kweli bosi. Inaonekana na wewe kwenye ujana wako ulikuwa moto” Magosho alizungumza na kukanyaga mafuta huku akipishana na magari mengine.
“Kwanini iko sema ivo vhevhe Goso?”
“Kwa kweli dada Rachna ni mrembo sana” alisema Magosho huku akimtupia jicho Rachna kupitia kwenye kile kioo kidogo. Alimuona Rachna alivyo vutiwa na kauli ile kiasi cha kumfanya aachie tabasamu zito la furaha. Magosho akajikuta akifarijika sana baada ya kumona binti yule akitabasamu kutokana na maneno yake.
Kwa upande wa Bi.Fahreen kauli ile haikuwa imembariki kabisa. Alishindwa kujizuia kuonesha kukasirika kwake.
“Veveee! hiyo toto yangu chezea mimi, hapana chezea toto yangu” alizungumza Bi.Fhreen huku akimuoneshea kidole cha onyo Magosho. Magosho alimtupia Bi.Fahreen jicho la wizi, alipoona mambo yameharibika ikammbidi awe mpole.
“Kama mama alikuwa mkali hivyo kwa binti yake, je huyo Mr.nakeshwar angekuwaje?” alijiuliza Magosho alipokuwa akikatiza mitaa ya kariakoo.
****
Ashura akawa ameduwaa pale kwenye kochi akishindwa kutafakari kale kamchezo ka rafiki yake na yule mwanaume wa kihindi. “Shauriyako, mjini shule” aliyakumbuka maneno ya Rafiki yake Zawadi alipokuwa akiingia chumbani na brifkesi iliyokuwa imejazwa pesa.
“Ni nani ambaye hapendi utajiri hapa duniani?” Ashura alijiuliza pale alipokuwa amekaa. “Hakuna ambaye hapendi utajiri, kama ni hoja ya kupika vitumbua hata mimi naweza kupika, sasa kwanini naichezea bahati hii? Haiwezekani” Ashura aliendelea kujiuliza maswali na kujijibu mwenyewe.
Baada ya Ashura kujiuliza maswali na kujipatia majibu yaliyomridhisha, akafanya maamuzi ambayo mwenyewe aliyaona yalikuwa na busara.
“Shost….” Sauti ya zawadi ilimgutusha Ashura kutoka kwenye lindi la mawazo. Ashura aliinua macho kumtazama rafiki yake ambaye alifika pale sitingrum na kuketi kwenye kochi la jirani na pale alipokuwa ameketi yeye.
“Mkataa pema pabaya panamuita” alizungumza Zawadi huku akijiweka vizuri kwenye kochi.
Ashura ahakutia neno lolote zaidi ya kutulia na kumsikiliza kwa umakini rafiki yake yule muuza vitumbua vya kihindi.
“Unayakumbuka vizuri maisha yangu ya nyuma?” alihoji Zawadi huku akiwa amemkodolea macho shoga yake. Ashura akaitikia kwa kichwa huku akimtazama Zawadi kwa umakini wa hali ya juu.
“Kama ningekuwa mgumu wa kuelewa kama wewe, kamwe nisingefikia hapa nilipo” alizungumza Zawadi kwa kujiamini.
Ashura aliinamisha kichwa chini kwa sekunde kadhaa kama vile alikuwa akiyapima yale maneno ya Zawadi kumbe jibu alikuwa nalo kitambo tu.
“Zawadi” aliita Ashura alipoinua shingo kumtazama Zawadi.
“Nakusikiliza”
“Nimeamua kufanya biashara pamoja nawe” alisema Ashura.
Zawadi hakuzungumza neno lolote baada ya kusikia maneno yale kutoka kinywani kwa Ashura. Hakutegemea kama binti yule mwisho wa siku angetamani kuthubutu kuungana naye katika biashara yake ya kuuza vitumbua vya kihindi. Akabaki ameduwaa akimkodolea macho rafiki yake yule.
“Ndio, nimeamua kufanya biashara ya kitumbua cha kihindi” Ashura akazungumza kwa msisitizo huku naye akimkodolea macho Zawadi.
“Kwanini unanitania zawadi?” alihoji Zawadi kwa mashaka ya kauli ile ya Ashura.
“Zawadi, unafahamu mimi siomtu wa kona kona, kama sitaki kitu nakuchana. Sasa nikuongopee ili iweje” Ashura alizungumza kwa msisitizo huku akilini mwake
“Kweli shost?” Zawadi alionesha kuhmaki baada ya kuthibitisha ukweli wa maneno ya Ashura.
“Amini nakwambia shoga yangu” Ashura alijibu kwa kujiamini.
“Wooow! umasikini tupa kuleee!” Zawadi alipaza sauti kushangilia huku akipaga makofi kwa furaha.
Ashura akawa anacheka kwa jinsi ambavyo shoga yake huyo alivyo onekana kuwehuka kutokana na majibu aliyo yatoa.
“Aaah! Jigiji!-Jigiji! Jigiji-jigiji-jijgiji” Zawadi alikuwa akiimba huku akikata viuno na mkono mmoja ameubandika kichwani na mwingine kiunoni.
Ashura alikaukia kucheka kiasi cha kushika mbavu zake kutokana na maumivu aliyo yapata kwa kucheka kwake.
“Zawadi shoga yangu kumbe bado hujakua wewe!” Ashura alizungumza huku akiendelea kucheka.
“Nimefurahi sana kuona shoga yangu unauaga umasikini”
“Jamani Zawadi asante kumbe unanipenda hivyo?”
“Alaaa! kwanini uteseke wakati najua jinsi ya kukusaidia? Haya nifuate nikuelekeze kazi mama” alizungumza Zawadi huku akipiga hatua kuondoka pale sebleni.
Waliingia kwenye chumba kimoja kilichokuwa na ukubwa wa wastani. Ndani ya chumba kile hapakuwepo na kitu kingine zaidi ya meza moja tu katikati iliyokuwa na ukubwa wa wastani. Juu ya meza ile iliyokuwa imetandikwa kwa kitambaa kisafi cheupe palikuwa na vitabu viwili. Walivua viatu na kuingia peku.
Mazingira ya chumbani mle yalimtatanisha sana Ashura. Alichokuwa anakifahamu yeye kazi ile ilikuwa ikifanyika jikoni. Sasa akashangaa analetwa kwenye chumba kilichokuwa kisafi kupita maelezo.
“Tunapikia humu hivyo vitumbua?” alihoji Ash ura baada ya kuona mambo hayaelewiki.
“Kuwa mpole shost, simama hapo geukia kule mbele” Zawadi alitoa maelekezo.
Ashura alifanya kama ambavyo mwenyeji wake alivyokuwa akimuamuru.
“Ok, unaona nini hapo mezani?” Alihoji Zawadi kwa umakini mkubwa.
“Vitabu” Ashura akajibu kwa ufupi.
“Unavifahamu?”
“Ndiyo, ni Biblia na Msahafu” Ashura alijibu baada ya kuviangalia vitabu vile kwa makini.
“Wewe unaamini katika kitabu gani kati ya hivyo?” Zawadi alihoji.
“Mimi ni muislamu, unadhani nitaamini kitabu gani?” Ashura alitoa jibu kwa kuuliza swali.
“Haya kichukue” alisema Zawadi.
Ashura alishituka kidogo baada ya kupewa yale maelekezo na rafiki yake yule. Akatulia na kukiangalia kitabu kile kwa kitambo kisha akamgeukia Zawadi na kumtazama kwa makini.
“Vipi mbona unasita? Chuku kitabu cha Quran hicho nikwambie cha kufanya” Zawadi akazungumza kwa msisitizo.
“Siwezi” Ashura aligoma kufanya vile alivyoagizwa na zawadi.
Jibu lile halikumridhia kabisa Zawadi. Hakutegemea kama angekumbana nalo kutoka mdomoni mwa Ashura. Akahisi kupandwa na ghadhabu dhidi ya tabia na mienendo ya rafiki yake yule.
Zawadi alikunja uso kwa hasira baada ya kusikia Ashura amegoma kugusa kile kitabu cha Quraan tukufu.
“Kwanini huwezi kukigusa?” Zawadi alihoji huku amekunja sura.
“Sipo tohara.” Ashura akajibu kwa upole.
Kauli ile ya Ashura kwamba hakuwa tohara ilimfariji Zawadi kwa kiasi fulani. Wasiwasi na hofu dhidi ya uamuzi wa Ashura vikapungua.
“Unaweza kujitoharisha, au unakikwazo?” Zawadi alihoji kwa umakini mkuwa.
“Sina kikwazo chochote naweza kujitoharisha”
“Ok njoo huku” Zawadi alizungumza na kutoka mle chumbani.
Waliingia chumba cha jirani ambacho kilikuwa na mabomba mengi ya maji. Ashura alipoyaona hakujiuliza afanye nini kwasababu alikuwa anafahamu wajibu wake. Alijitoharisha kisha wote wawili wakarejea kwenye kile chumba kilichokuwa na vitabu. Ashura alikichukua kile kitabu cha Quraan na kukishika kwa unyenyekevu.
“Kishike kwa mkono wa kulia na ukiinue juu” Zawadi aliagiza.
Ashura akafanya kama alivyoagizwa na shoga yake huku akiwa haelewi kilichokuwa kinataka kuendelea pale.
“Fuatisha maneno haya nisemayo” Zawadi aliagiza.
“Sawa” Ashura ilimbidi akubali tu ingawa hadi kufikia wakati ule alikuwa amekwisha poteza matumaini ya kufanya shughuli ile ya kuuza vitumbua kutokana na mfumo wake kuwa mrefu.
Hivyo vitumbua vya kupika kwa kutumia vitabu vya dini ni vitumbua vya aina gani? Akajipa moyo na kufuata maelekezo aliyokuwa anapewa na yule mwalimu wake wa kmfundisa mapisi ya kitumbua ca kihindi.
“Sema Emwenyezi mungu” Zawadi alizungumza.
“Ee Mwenyezi Mungu” Asura akafuatia.
“Mimi Ashura Machaku”
“Mimi Ashura Machaku” Ashura akamfuatisha.
“Nikiwa na akili yangu timamu, naapa kwamba nimeingia katika biashara hii kwa hiyari yangu mwenyewe, pasipo kulazimishwa wala kushurutishwa na mtu. Nitatenda yale yote ambayo kazi hii itanitaka kutenda pasipo ubishi wala kusita. Naahidi kuwa nitatunza siri zote za kazi hii. Nitakuwa tayari hata kutoa uhai wangu ili kutunza siri hii. Ee Mwenyezi mungu nisaidie” Ashura alifuatisha maneno yote hayo kama ambavyo Zawadi alimtaka kufanya na mwisho alirejesha mezani kile kitabu cha Quraan.
“Sasa shost utajiri ni wako” alisema Zawadi huku akitabasamu.
“Lakini shoga biashara yenyewe ndiyo ina mlolongo mrefu hivi?” Ashura akahoji kwa mashaka.
“Ah si unajua tena kila kazi ina kanuni na taratibu zake”
“Na hizi ni kanuni za kupika hivyo vitumbua?” alihoji Ashura kwa umakini.
“Sio vitumbua bali sema Vitumbua vya kihindi” Zawadi alimsahihisha Ashura.
“Sio vitumbua vya kihindi, bali sema Kitumbua cha kihindi” Ashura naye akamsahihisha Zawadi.
“Woow! umekwishaiva, sasa twende zetu huku” Alisema Zawadi na kutoka mle chumbani. Waliingia kwenye kile chumba kilichokuwa na mabomba mengi ya maji.
“Vipi tunajitoharisha tena?” Ashura alihoji baada ya kuona anarudishwa tena chumbani mle.
“Hapana” Zawadi alijibu huku akisogea pale kwenye bomba ambalo alilitumia Ashura kujitoharishia. Alilikamata bomba lile na kulivuta kwanguvu huku Ashura akiwa amesimama pembeni akimtazama. Shughuli ile iliendelea kwa sekunde kadhaa na mwisho pale kwenye lile bomba pakafunguka kama vile mlango pakawa pana pango.
“Heee!” Ashura alihamaki baada ya kuona tukio lele.
“Twende zetu” Zawadi alizungumza kisha akajichomeka kwenye lile pango lililofunguka.
Moyo wa Ashura ulisita kuingia kwenye pango lile ambalo ndani kulikuwa hakuonekani kitu kutokana na kiza kinene kilichokuwa kimetanda. Zawadi akiwa ndani ya lile pango aligeuka na kumchungulia Ashura ambaye alikuwa bado amesimama pale nje.
“Vipi wewe! twende” Zawadi alisisitiza kwa kutumia kiganja chake cha mkono.
Ashura huku akiwa na wasiwasi aliingia ndani ya pango lile kisha Zawadi akaufunga mlango wa pango lile.
Kwakuwa kiza kilikuwa kinene Ashura alishindwa kujua pa kuelekea. Zawadi alimtangulia na kumwambia amshike blauzi na kumfuata kwa nyuma.
Safari ile ya Zawadi na Ashura kwenye lile pango iliwachukua takribani dakika kumi hivi kwa mwendo wa kutambaa na magoti. Ashura alikuwa akitambaa kumfuata Zawadi lakini hofu ya kupoteza uhai wake ilikuwa imemjaa moyoni mwake. Hata hivyo hakukata tamaa na kuendelea kusonga mbele kuzama zaidi ndani ya pango lile.
Walitokea sehemu moja iliyokuwa na chumba kipana kilichokuwa na ukuta uliokuwa umepakwa rangi nyeupe sana. Ndani mle kulikuwa kumezunguukwa na makabati ya ukutani. Chumba kile kilikuwa na mwanga wa kutosha ukilinganisha na kwenye lile pango walimokuwa wakipita.
“Zawadi” Ashura aliita huku akizunguusha macho yake kuangalia mazingira yale.
“Niambie shost” Zawadi aliitika kwa sauti ya upendo pasipo kuwa na tabasamu lolote.
“Hizi ndio kanuni na taratibu za hivyo vitumbua vya kihindi zinaendelea?” Ashura alihoji kwa sauti iliyokuwa imekata tamaa.
“Baada ya dhiki faraja” Zawadi alijibu huku akifungua moja ya kabati lililokuwa mle ndani.
Hadi kufikia wakati ule kitumbua cha kihindi bado kilikuwa ni fumbo kubwa sana kwa msichana Ashura. Pamoja na kwamba alijiingiza kushiriki katika biashara ile tena kwa viapo vya vitabu vitukufu lakini bado hakuwa na mwanga wowote.
“Mungu wangu!” Ashura alihamaki baada ya kuona kilichomo ndani ya lile kabati lililofunguliwa na Zawadi.
Ashura aliweza kushuhudia idadi kubwa sana ya pesa za kitanzania zikiwa zimepangwa ndani ya kabati lile.
“Kawaida sana, Mungu akupe nini tena?” Zawadi alizungumza huku akilifunga kabati lile na kuendea kabati lingine lililokuwa jirani na kulifungua.
“We Zawadi!” Ashura alizidi kuhamaki baada ya kuona mabunda ya noti za dola ya kimarekani yamepangwa kwenye kabati lile.
“Vipi kuna tatizo?” Zawadi alihoji huku akimgeukia Ashura
“Pesa zote hizo ni za nani?”
“Zakwangu mimi na wewe” Zawadi alijibu kwa mkato.
“Kwa lipi hasa?”
“Kitumbua cha kihindi” alijibu Zawadi huku akitabasamu.
“Mnh!”
“Huna sababu ya kuguna njoo uone” alisema Zawadi huku akifungua kabati lingine.
Kilichokuwemo ndani ya kabati lile kilikuwa kigeni machoni mwa Ashura. Kulikuwa na pakiti nyingi sana zilizokuwa zimejazwa vitu vilivyofanana na unga wa ngano.
“Unafahamu hii?” Zawadi alimuuliza rafiki yake huku kimuoneshea zile pakiti.
“Sio ngano hii kweli?” Ashura alijibu huku akibonyeza bonyeza pakiti zile.
“Usijali utafahamu tu”
“Ni kitu gani?”
“Hii ndiyo pesa yenyewe sasa”
“Kwahiyo huu ndio unga wa kupikia hivyo vitumbua vya kihindi?”
“Naweza nikakwambia ndio au hapana”
“Kivipi sasa?”
“Njoo hapa” Zawadi alizungumza na kusogea kwenye kabati jingine refu kuanzia juu hadi chini lililokuwa karibu na lile pango waliloingilia.
Zawadi alipolifungua kabati lile Ashura akabaini kuwa kumbe halikuwa kabati kama alivyo dhani bali ulikuwa ni mlango. Yani kila hatua waliyokuwa wakipitia Ashura alijikuta akipatwa na mshangao. Bado alikuwa kama vile yupo usingizini kwasababu hakuna ambacho aliking’amua juu ya kile kitumbua cha kihindi.
“Twende zetu tajiri wangu” alisema Zawadi huku akiingia kwenye mlango ule aliokuwa ameufungua.
Kama ilivyokuwa kawaida Ashura alimfuata nyuma Zawadi. Walipoingia kwenye mlango ule, wakatokea sehemu moja ambayo ilikuwa na mashine nyingi ambazo Ashura hakuwahi kuziona katika maisha yake tangu alipokuwa amezaliwa.
“Sasa hapa mama ndipo jikoni kwetu” Zawadi alimtambulisha rafiki yake ambaye muda wote alikuwa ni mtu wa kushangaa shangaa. Ashura aliangaza kila kona mle ndani lakini hakuona jiko wala flampeni za kukaangia hivyo vitumbua.
“Jiko lenyewe liko wapi?” alihoji Ashura huku akijaribu kulitafuta mwenyewe.
“Hapa ndipo kila kitu” Zawadi alijibu huku akiwa ameweka mkono wake kwenye moja ya mashine zilizokuwemo mle ndani.
Ashura alisogea na kuishangaa ile mashine aliyoambiwa kuwa ndio kila kitu. Kusema kweli mashine ile ilikuwa haifanani na jiko la aina yoyote ile ambalo alikuwa anayafahamu yeye.
“Sasa hapa ndio unafanyaje?” alihoji Ashura huku akiikagua kwa makini mashine ile.
“Tulia mama” Zawadi alijibu na kuvuta hatua hadi sehemu moja ambayo ilikuwa na vitu kama matanki ya kuhifadhia maji. Aliingiza mkono na kuchomoa pakiti moja iliyokuwa na unga.
“Huu mama ni unga wa kawaida unatokana na mchele” Zawadi alizungumza huku akimuonesha Ashura ile pakiti ya unga aliokuwa ameutoa kwenye moja ya tanki lililokuwemo mle chumbani. Ashura alitulia kama kawaida yake akimsoma kiongozi ama mwalimu wake wa kazi.
****
Magosho alipaki gari kisha akateremka na kuzunguuka kwenye buti la gari ambapo alifungua na kutoa mzigo wa Rachna. Wakati huo Rachna na Bi.Fahreen walikuwa wamekwisha teremka na kuanza kuelekea ndani.
Magosho aliutoa ule mzigo kisha akauweka chini huku macho yake akiwa ameyagandisha kwa mgeni Rachna ambaye alikuwa ameongozana na mama yake.
“Haki ya mungu wallah” Magosho alijikuta akizidi kuchanganyikiwa na mtoto yule wa bosi wake. Alitikisa kichwa kusikitika kisha akavuta pumzi na kuzitoa kwa nguvu. Alimsifu Muumba kwa ustadi mkubwa aliouonesha kwa kumtengeneza Rachna pasipo kumfanyia choyo wala hasira hata chembe.
Bi. Fahreen na binti yake walipokuwa akikaribia kuingia ndani, yule mama wa kihindi aligeuka nyuma na kumfuma Magosho amesimama akiwakodolea macho. Mama yule alikunja sura yake kisha pasipo kuzungumza neno lolote alivuta hatua kurudi nyuma alipokuwa magosho.
Magosho aliisoma hali ya hatari kwenye sura ile ya mwanamke wa kihindi ambayo tayari alikuwa amekwisha kuizoea vya kutosha. Alichofanya yeye ni kuinua begi na kuvuta hatua kuelekea ndani. Wakakutana na Bi. Fahreen njiani.
“Vhevhe Goso, hiyo macho yako mbona hapana tulia leo?” alihoji Bi.Fahreen huku akiwa amemkazia macho Magosho.
“Kwanini unasema hivyo mama?” Magosho alihoji kwa wasiwasi.
“Pumbaaaa, yaani nazidi tibua mimi?”
“Mnh!” Magoshio aliguna kwa msahngao.
“Fyee nini? Iko tamani toto yangu halafu naita mimi mama?” Bi.Fahreen alizungumza kwa hasira huku akiwa amemtolea macho Magoso wa watu.
“Nisamehe kwa kukuita mama, lakini kuhusu kumtazama Rachna hilo sio kweli Bi.Fahreen” Magosho alijaribu kujitetea.
“Shut up! sasa ole yako sikia veve iko chukua toto yangu” Bi.Fahreen alizungumza na kuchukua lile begi kwa hasira kisha akaondoka na kumuacha Magosho ameduwaa kwa mshangao.
****
Onyo alilokuwa amepewa Magosho na Bi.Fahreen lilimfanya kuwa makini wakati wote. Hata hivyo tabia za Rachna zilimfanya Magosho kuwa katika wakati mgumu sana. Rachna alikuwa ni msichana mcheshi na mwenye upendo na watu wote pasipo kujali rangi wala jinsia. Kwa kipindi kifupi sana alikuwa tayariamekwisha kumzoea Magosho kutokana na tabia yake hiyo.
Mara nyingi sana Rachna alikuwa anapenda kuketi pamoja na Magosho hasa anapokuwa nyumbani. Alifanya hivyo pasipo kufahamu kuwa kitendo kile kilikuwa kikimtia hatarini kijana wawatu.
“Gosooo!” ilikuwa ni sauti mwanamke ikimuita Magosho ambaye alikuwa chumbani amepumzika.
“Vhevhe Gosooo!” Sauti ile iliita tena.
Magosho alikurupuka kutoka chumbani akiamini kuwa mtu aliyekuwa akimuita alikuwa ni Bi.Fahreen. Alipotoka tu akakutana na Rachna amesimama hatua kadhaa kutoka mlangoni kwake.
“Ooh! dada Rachna kumbe ni wewe?” Magosho alitamka huku akionekana kuishiwa nguvu.
“Vipi iko lala vhevhe?” alihoji Rachna kwa sauti ya upole.
“Hapana sikuwa nimelala, nilipumzika tu” Magosho alijibu huku akifikicha macho yake kwa vidole vya mikono.
“Kuje huku” Rachna alizungumza huku akivuta hatua kuelekea chumbani kwake.
Magosho alibaki akimkodolea macho binti yule wa kihindi aliyekuwa akitembea kwa nyodo na kudondosha mojamoja.
“Nije wapi sasa dada Rach?” Magosho akahoji kwa mashaka kidogo.
“Kuje kwa chumba yangu” alijibu Rachna pasipo kugeuka nyuma na kuingia chumbani mwake.
Magosho alivuta pumzi ndefu na kuzitoa kwa nguvu. Akajipa moyo kuwa Rachna hakuwa na tabia kama za mama yake Bi.Fahreen kwasababu binti yule alikuwa anajiheshimu sana kuliko mama yake. Hivyo hata kama angekwenda huko chumbani kwake pasingetokea baya lolote.
Tatizo lilikuwa ni kwa Bi.Fahreen ambaye mapema sana alimuonya Magosho kumzoea binti yake huyo ambaye mwenyewe alikuwa ni mcheshi. Hivyo Magosho alikuwa anahofia sana kukutwa na Bi. Fahreen chumbani mle mwa Rachna.
“Gosoooo!” Rachna alipaza sauti kuita.
Magosho akatazama kulia na kushoto kama kulikuwa na mtu anamuona. Baada ya kuhakikisha kuwa hakuwa anaonekana, alivuta hatua hadi pale kwenye mlango wa chumba cha Rachna na kugonga taratibu huku akisikiliza kwa makini kuruhusiwa kuingia.
“Ingia bhanaaa!” Rachna alipaza sauti kutokea ndani ya chumba kile.
Magosho alikamata kitasa cha mlango na kukinyonga tayari kwa kuingia chumbani mle. Sauti ya mtu aliyekuwa anajikohoza ilimgutusha na kumfanya ageuke. Macho yake yalikutana na macho ya Bi.Fahreen ambaye alikuwa ameegemea ukuta huku akimtazama jinsi alivyokuwa amekikamatia kitasa cha mlango wa chumba cha binti yake Rachna.
Magosho akabaki ameduwaa, alishindwa kufungua mlango kuingia na pia akashindwa kuachia kitasa cha mlango ule. Aibu na woga ndivyo vilikuwa vimemtawala kwa wakati ule.
“Gosooo” Rachna alizidi kuita kule chumbani pasipo kuelewa kitu kilichokuwa kikiendelea nje ya chumbani kwake.
Magosho hakuitika bali aliinua macho yake na kumtazama Bi.Fahreen ambaye alionekana kuvimba kwa hasira pale alipokuwa amesimama.
Magosho aliachia kitasa cha mlango wa Rachna kwa aibu huku akitazama chini na kuachia tabasamu ambalo halikuwa na ulazima.
“Shikamoo mama” akasalimia kwa haya huku akikutanisha viganja vya mikono yake na kuvisugua sugua.
Bi.Fahreen aliachia msonyo huku akimtazama Magosho kwa dharau na hasira.
“Dada Rachna aliniita” Magosho alijaribu kujitetea
“Nani iko mama yako?”
“Nisamehe mpenzi, hakuna kinachoendelea kati yetu” alizungumza Magosho kwa sauti ya chini ili Rachna kule chumbani asisikie maneno yale makali.
Rachna baada ya kuona Magosho anachelewa kuingia alifungua mlango na kuchungulia nje. Alimkuta mama yake amesimama hatua chache akitazamana na Magosho.
“Mom, mimi iko sida na Goso huku kwa chumba yangu” Rachna alizungumza pasipo kufahamu kitu kilichokuwa kikiendelea kati ya watu wale wawili.
“Ooh! No problem my daughter” Bi.Fahreen alijikakamua na kuzungumza huku kwenye uso wake akiwa amevaa tabasamu la bandia. Alimruhusu Rachna kuendelea na shughuli yake na Magosho. Rachna alimshika mkono Magosho na kuingia naye chumbani.
Kule nyuma Bi.Fahreen alipandwa na hasira zilizokuwa zimechanganyikana na wivu. Alikwenda kwenye kochi na kujitupa kama vile mgonjwa mahututi. Akajikuta akichukia sana uwepo wa Rachna ndani mle. Aliona wazi asali yake ilikuwa inaelekea kudokolewa nab inti yake kipenzi.
Rachna alipofika chumbani kwake aliketi kwenye kitanda na kumkaribisha Magosho kwenye kochi.
“Karibu kwa chumba yangu Goso” alisema Rachnakwa ile sauti yake nyororo iliyokuwa ikimmaliza Magosho.
“Kwanini tusiende kukaa sebleni dada Rachna?” Magosho akazungumza kwa sauti iliyokuwa imejaa hofu na mashaka. Wasiwasi wake wote ulikuwa kwa Bi. Fahreen ambaye alimtisha kwa kumtazama kwa jicho kali la onyo na tahadhari kubwa.
“Kae kwa sebule kwani sisi iko geni bhana!” alizunumza Rachna huku akirembua macho yake meupe yaliyokuwa yamepambwa kwa kope ndefu nyeusi.
“Kwahiyo wanaokaa sebleni ni wageni tu?” alihoji Magosho huku akijaribu kukwepesha kidogo macho yake kumtazama mrembo yule aliyekuwa mbele ya macho yake.
“Yes. Iko ivo” alisema Rachna huku akijiweka vizuri pale kitandani.
Kusema ukweli hapakuwepo na jambo lolote baya lililokuwa likiendelea kati ya Rachana na Magosho kule chumbani. Stori za hapa na pale ndizo zilizokuwa zikiendelea. Ucheshi wa Rachna ulimfanya Magosho kuondokewa na uwoga ingawa awali alikuwa na wasiwasi.
Walizungumza na mara kwa mara walikuwa wakiangua vicheko vya sauti huku wakigongeana mikono. Moyo wa Magosho ulijawa na amani baada ya kupata nafasi ya kuzungumza na mrembo yule wa kihindi ambaye alionekana kuwa mcheshi kuliko kawaida. Alisahau kabisa habari na vitisho vya yule mama mtu mzima wa kihindi.
Zile sauti za vicheko vya Magosho na Rachna kule chumbani zilimfikia vizuri sana Bi. Fahreen ambaye alikuwa ameketi kwa gadhabu sebleni. Alijikuta hasira zikimzidi kila alipokuwa akiwasikia watu wale wakicheka kwa furaha kule chumbani.
“Hii Goso iko bure kabisa!” alizunumza Bi. Fahreen kwa hasira huku akijiinua kutoka kwenye kochi na kusimama wima huku ameshika kiuno na midomo ya chini akiiuma kwa meno yake ya juu.
Mwanamke yule wa kihindi alizunguuka zunguuka pale sebleni huku akikuna kichwa chake kwa ghadhabu. Alikuwa akiamini kuwa binti yake alikuwa anaelekea kupora penzi lake kutoka kwa Magosho.
Uvumilivu ulimshinda Bi.Fahreen na kuvuta hatua kuelekea kwenye mlango wa chumba cha Rachna. Alisimama na kutega sikio kusikiliza kilichokuwa kikizungumzwa na wawili wale waliokuwa wamejifungia chumbani mle.
Pale mlangoni Bi. Fahreen aliambulia kusikia sauti za vicheko tu, maneno yaliyokuwa yakizungumzwa hakufanikiwa kuyasikia kwasababu yalikuwa yakizunumzwa kwa sauti ya chini. Hilo ndilo lililozidi kummaliza Bi.Fahreen pale mlangoni na kuhisi tayari binti yake alikuwa ameshafanya mapinduzi ya huba.
Wivu ulizidi kumtafuna mama yule wa kihindi na mwisho uzalendo ukamshinda. Kijana ambaye alikuwa akimpatia huduma takatifu anaona dalili za kumpoteza. Mbaya zaidi alikuwa anampoteza kwenye mikono ya binti yake mwenyewe.
“Haiwezekani” Alisema na kugonga mlango wa chumbani mle.
Mlango ulifunguliwa na Rachna ambaye alikuwa akifuta macho yake kutokana na mchozi yaliyokuwa yamesababishwa na kucheka sana. Bi.Fahreen alipomuona binti yake anafuta macho akajikuta akizidi kuchanganyikiwa na kujawa na wivu zaidi akiamini Magosho alimpa dozi binti yake hadi kumtoa machozi.
****
Zawadi alichukua paketi ya ule unga wa vitumbua alioutoa kwenye tanki na kuupasua kisha akauingiza kwenye karai la mashine moja lililokuwa likifanana na lile la mashine ya kukobolea mahindi lakini lenyewe lilikuwa na mfuniko. Baada ya hapo alichukua maji kutoka kwenye tanki jingine na kuyamimina mle kwenye mashine. Alichukua sukari kiasi cha kilo moja na kuimimina pamoja na yale maji kisha akabonyeza kitufe chekundu kwenye mashine ile na baada ya muda ikasikika ikiunguruma kwa sauti ya chini.
“Ama kweli ni vitumbua vya kihindi” Ashura alizungumza kwa mshangao.
Zawadi hakumjibu kitu chochote bali alikwenda kule kwenye kile chumba walichopita na kurejea na zile pakiti za unga uliokuwa umefanana na unga wa ngano uliokuwepo kwenye kabati.
“Unakumbuka vitu hivi?” alihoji Zawadi huku akimuonesha Ashura paketi zile.
“Sana tu” Ashura alijibu kwa kifupi.
Zawadi alifungua mtambo mwingine uliokuwa pembeni na mashine ile aliyokuwa ameiwasha awali.
“Unaona mashine hii?”
“Ndio…” alijibu Ashura huku akisogea pale alipokuwa amesimama Zawadi.
“Kwanza unaiwasha, halafu unachukua pakiti hizi, unazitumbukiza na nailoni zake” Zawadi alizungumza huku akifanya na vitendo. Kitu kilichomshangaza Ashura ni kile kitendo cha kutumbukiza pakiti za unga ule pamoja na nailoni zake.
“Sasa mbona hutoi hizo nailoni?” Alshura alihoji,
“Unga huu huwa hautolewi kwenye pakiti” Zawadi alizungumza huku akizitumbukiza pakiti zile moja moja mtamboni.
“Kwanini?” Ashura akahoji kwa mshangao.
“Kwasababu hii ndiyo mali yenyewe”
“Kwani ni unga wanini huo?”
“Hii ni COCAIN”
“Cocain!” Ashura alitamka neno lile kwa mshangao.
“Unacho shangaa ni kipi sasa?”
“Cocain si ni madawa ya kulevya?” alihoji Ashura kwa mshangao huku akihisi mwili wake ukiingiwa na baridi ya woga.
“Sasa kama ni madawa ya kulevya wasiwasi wako wewe ni nini?” Zawadi alihoji huku akimalizia kutumbukiza pakiti ya mwisho kwenye mtambo. Alisogea kwenye mashine ya kwanza na kuifunua kama vile kutazama maendeleo ya unga wa awali uliokuwa umechanganywa na maji.
“Njoo uone huku” Zawadi alimuita Ashura ambaye alikuwa ameduwaa kwa mshangao baada ya kuambiwa kuwa unga uliotumika ulikuwa ni madawa ya kulevya.
Ashura alisogea hadi pale na kuchungulia kwenye karai lile. Hapakuwepo na kitu chochote. Akageuza shingo yake na kumtazama Zawadi usoni kwa jicho la udadisi huku moyoni mwake akiwa bado amejawa na hofu
“Ukishaona karai limekuwa tupu unazima mashine” Zawadi alizungumza huku akibonyeza kitufe cha kuzimia kilichokuwa na rangi nyekundu.
akili ya Ashura ilikuwa imehama kabisa kiasi cha kuto kuzingatia kile alichokuwa anaelekezwa. Taarifa ile ya unga wa cocain ilikuwa imemchanganya kabisa.
“Sasa Zawadi…” aliita Ashura kwa sauti ya chini.
“Enhee….”
“Watu wakila hivi vitumbua si watalewa?”
“We wacha maswali bwanaaa, njoo mtamboni” Zawadi alimvuta mkono Ashura hadi kwenye mashine ya pili ambayo ilikuwa bado ikitoa mlio wa muungurumo kuashiria kuwa ilikuwa inaendelea kufanya kazi. Alibonyeza kitufe kingine na mashine ikabadili sauti na kutoa muungurumo mzito lakini nao pia haukuwa wa sauti ya juu.
“Ukisha washa hapa unasubiri dakika kama tano hivi” Zawadi alitoa maelekezo kisha akachukua sinia kubwa na kuliweka mbele ya mashine ile ambako kulikuwa na tundu dogo. Ashura alibakia kimya akimtazama rafiki yake yule ambaye alikuwa akishughulika vilivyo.
“Sasa tayari unaweza kubonyeza hapa” alitoa maelekezo huku akibonyeza mahali alipokuwa anapazungumzia.
Baada ya sekunde kadhaa vitumbua vilianza kudondokea kwenye lile sinia alilokuwa ameliweka kwenye tundu la mashine ile.
“We Zawadi!” Ashura alijikuta akihamaki na kusogea pale kwenye sinia lililokuwa likidondokewa na vitumbua.
“Vipi?” alihoji Zawadi huku akiachia tabasamu la matumini.
“Mbona mchawi hivyo?” Ashula alisema kwa kuhamaki.
“Mambo ya kihindi hayo” alisema Zawadi na kwenda kuzima mashine.
“Imekuwaje hapa?”
“Hapo mambo tayari kwa biashara” Zawadi akaeleza.
“Na ile Cocain imekwenda wapi?”
“Imo humo humo”
“Wapi?”
“Kwenye kitumbua”
“Lakini zawadi una dhambi wewe!”
“Dhambi za nini?”
“Sasa watu wa watu si watalewa wakila hivi vitumbua?”
“Hivyo vitumbua sio vya kula”
“Kumbe?”
“Vya biashara”
“Sasa ukifanya biashara ya chakula maana yake si kitaliwa?”
“Kikate katikati uone” Zawadi alizungumza kwa kujiamini.
Kwa hamasa kubwa Ashura alikimega kitumbua kile kilichokuwa mkononi mwake na kukikodolea macho. Hakuweza kuamini, pakiti ya Cocain ilikuwa ndani ya kitumbua kile.
“Hee!” Ashura alihamaki kwa mshituko.
“Sasa kazi ya vitumbua vyetu ni kusafirisha mzigo huwo” Alizungumza zawadi kwa kujiamini.
“Kuupeleka wapi?” alihoji Ashura
“Tunaupeleka katika nchi mbalimbali za hapa duniani, kama vile China na Afrika Kusini” alisema Zawadi.
Ashura aliposikia maneno yale alishituka sana. Akakumbuka matukio kadhaa yaliyotokea siku za hivi karibuni jinsi serikali ilivyotilia mkazo katika suala la madawa ya kulevya. Akakumbuka taarifa alizozipata za watu kufungwa jela kifungo cha miaka 30 kwa sababu hiyo hiyo ya biashara ya madawa ya kulevya.
Wasiwasi na hofu vilizidi kumtawala Ashura na taratiibu akajikuta akiingiwa na majuto ya kujiingiza kwenye shughuli kama ile pamoja na kwamba ilikuwa na dalili zote za kumtajirisha kwa muda mfupi.
****
Rachna alikuwa akiendelea kufuta macho yake huku akiwa ametawaliwa na tabasamu. Wakati huwo Bi.Fahreen ambaye alikuwa amejawa na hasira juu ya binti yake huyo alikuwa bado amesimama mlangoni pale.
“Karibu mom” Rachna alimkaribisha mama yake.
“Itia mimi Gosoo” alizungumza Bi.Fahreen kwa sauti kavu ambayo haikuwa yakwake kutokana na hasira alizokuwa nazo.
“Mnh! Mom, Goso iko furahisa mimi bhanaa” Rachna alizungumza kwa sauti ya kudeka pasipo kufahamu kuwa mama yake alikuwa amejawa na hasira juu yake.
“Veve iko chizi sana! mimi iko sida na Goso halafu veve leta jhinga jhinga yako hapa!” Bi.Fahreen alishindwa kuizuia hasira yake na kujikuta akimfokea binti yake ambaye alikuwa akimpenda kuliko kawaida.
“Basi mom, samehe mimi” Rachna alijikuta akiwa mpole ghafla. Aligundua kuwa mama yake alikuwa amekasirika.
“Hapana chelewesa mimi tena, itia Goso bhanaa” Bi.Fahreen alizungumza kwa hasira zaidi.
“Gosooo!” Rachna alipaza sauti kumuita Magosho ambaye alikuwa chumbani kwake akisikiliza majibizano yale kati ya Rachna na mama yake.
“Naam” Magosho aliitika kwa sauti ya chini iliyokuwa imajaa woga na wasiwasi.
“Kuje huku mom iko sida” alisema Rachna huku akiwa amegeukia chumbani kwake ambako Magosho alikuwemo.
Magosho alikurupuka na kutoka nje kwa wasiwasi akihofu kukutana na sura ya Bi.Fahreen. Rachna aliingia chumbani na kuwaacha mama yake na Magosho wamalizane.
“Naam mama” Magosho aliitika mara tu alipofika pale nje
Bi.Fahreen alimtazama kuanzia chini hadi juu kisha akatoa pumzi ndefu kuashiria kuwa alikuwa amejawa na hasira ndani ya moyo wake. kengere ya hatari ikagonga kwenye ubongo wa Magosho, akafahamu wazi kuwa alikuwa amekwisha zua balaa.
“Kuje huku” Bi.Fahreen alizungumza huku akiondoka kuelekea nje.
Pasipo kujishauri Magosho alimfuata mke wa bosi wake nyuma.
Bi.Fahreen alifika nje na kusimama barazani huku akionekana dhahiri kuwa alikuwa na hasira.
“Hivi veve Goso iko taka kufe?”
“Kwanini mpenzi”
“Iko naanza lini hiyo tabia?” alihoji Bi.Fahreen
“Tabia gani?”
“Hapana uliza mimi swali! veve iko toa penzi kwa toto yangu?” alihoji Bi.Fahreen huku sura akiwa ameikunja kwa hasira.
“Hapana mpenzi, tulikuwa tunapiga stori tu” Magosho alijaribu kujitetea.
“Napiga stori kwa chumba ya toto yangu?” Bi.Fahreen alihoji kwa hasira.
Swali la Bi.Fahreen lilimfanya Magosho kutulia kimya na kutafakari cha kujibu. Wakati huo Rachna alitoka chumbani na kusimama mlangoni. Alikuwa akiwatazama mama yake na Magosho walivyokuwa wakiangaliana kama majogoo. Bi.Fahreen alipomuona mwanae akajikuta akishiwa pozi.
“Hapana leta tena jhinga yako, nenda shule kachukue toto yangu” Bi.Fahreen alibadilisha maongezi mara tu alipobaini kuwa Rachna alikuwepo jirani na mahali pale.
“Sawa mama” Magosho alijibu na kuingia ndani kuchukua funguo za gari.
Alipokuwa anatoka aliwakuta Rachna na mama yake bado walikuwepo pale nje wakizungumza mambo yao ambayo yeye hakuyafahamu.
“Gosooo” Rachna alimuita Magosho alipokuwa anatoka nje.
Magosho alisimama na kugeuka nyuma kumtazama Rachna ambaye alikuwa anamuita.
“Ngoje mimi twende vote” alizungumza Rachna huku akivuta hatua kumfuata.
Magosho aliposikia maneno yale akajikuta akiishiwa na nguvu. Alimtazama Bi.Fahreen
ambaye alikuwa akimkata jicho la kumuonya kufanya kile ambacho Rachna alikuwa anakitaka.
“Lakini dada Rachna we ungepumzika tu, ngoja mimi nikamchukue mtoto” Maosho alizungumza kwa tahadhari baada ya kubaini kuwa Bi. Fahreen hakuwa amebariki safari ile.
“Goso taka nyima mimi safari veve?” alizunumza Rachn huku akimuelekeza kidole Magosho.
“Hapana Rachna my baby veve pumzike bhanaaa, hii Goso ipo hapa kwa kazi hiyo” alizungumza Bi. Fahreen kwa msisitizo ili kumshawishi binti yake asiongozane na Magosho.
“No Mom, mimi iko penda sana Goso, acha sindikize yeye” Jamani nyie binti yule alizungumza maneno makali kwa mama yake pasipo kuelewa kama alikuwa anautesa mtima wa mwanamke wa watu.
“Veve Rachna iko bisi sana mashiku izi” alizungumza Bi. Fahreen kwa ukali kidogo.
“Gosooo leo mimi endesa motukaa, vhevhe kae pembeni ya mimi” alizungumza Rachna na kumshika mkono Maosho kumvuta kuelekea kulipokuwa kumepaki gari.
Magosho alisita kuondoka lakini kutokana na lazima na machachari ya Rachna akajikuta akivuta hatua kuelekea kwenye gari huku wakimuacha Bi. Fahreen akiwakodolea macho kwa mshangao.
Kitendo kile cha Rachna kutaka kuondoka na Magosho kilizidi kumchanganya Bi.fahreen. Wivu ukamjaa na kuanza kutetemeka kwa hasira. Alibakia akiwatazama vijana wale wawili jinsi walivyokuwa wakiondoka.
Ndugu msomaji laitani Rachna asingekuwa mtoto wake wa kumzaa, nafikiri siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa maisha yake binti yule. Kijasho chambaamba kilikuwa kikimtiririka masikini mama wawatu. Kumbe wivu ni kitu hatari kiasi kile, Duuh! Ndugu msomaji omba sana katika maisha yako ugonjwa huu hatari wa wivu usije ukakupata mana unaweza ukafa kibudu ilhali unapumua.
Kwakuwa Rachna alikuwa ni mtu wa matani muda wote, alizidi kummaliza mama yake kwa kumshika kiuno Magosho wakati wanatembea.
“My God! Hii toto kuwe setani sasa!” alihamaki Bi. Fahreen huku akipeleka mkono wake kifuani kushika mapio ya moyo wake.
Masikini ya Mungu Rachna hakuwa na maana yoyote ile mbaya, tabia yake ya ucheshi na kupenda utani ndiyo iliyokuwa ikimmaliza mama yake kipenzi. Hakufahamu kabisa kama Magosho alikuwa ni baba yake wa mpango wa kando.
Magosho alielewa hali halisi aliyokuwanayo Bi. Fahreen kwa wakati ule, lakini angefanya nini sasa wakati Rachna hakuelewa kitu na ndiye aliyekuwa akifanya vituko mbele ya mama yake. Magosho akajikaza na kujichekesha mbele ya macho ya Rachna lakini ndani ya moyo wake kulikuwa na hofu na mashaka makubwa dhidi ya Bi. Fahreen.
Wakitembea huku wakicheka na kugongeana mikono Magosho na Rachna waliingia kwenye gari ndogo na safari ya kuelekea shuleni kwa mtoto Vashal ikaanza.
Kule nyuma Bi.Fahreen alizidi kuishiwa nguvu, na kwambaali akajikuta akimchukia binti yake Rachna ingawa alikuwa akimpenda kuliko maelezo.
Magosho aliendesha gari huku akilini mwake akiwaza namna ambavyo angekuja kujitetea kwa Bi.Fahreen mwanamke ambaye alikuwa ametawala uhuru wake. Kwa kiasi fulani alianza kujihisi mtumwa wa mapenzi. Kidogokidogo akaanza kujutia maamuzi yake ya kukubali kulala na mwanamke yule ambaye alikuwa sawa kabisa na mama yake mzazi.
Rachna ambaye alikuwa ameketi pembeni mwa Magosho alikuwa akimtazama dereva wao jinsi alivyokuwa akibadili gia na kukanyaga mafuta. Hakika aliridhika kabisa na kumsifu kimoyomoyo mwalimu aliyemfundisha kuendesha gari kijana yule hodari wa kuongoza gari lile.
Rachna aliinua macho yake na kumtazama usoni Magosho kwa makini ili kuendelea kuthibitisha umahiri wa dereva wa mama yake. Lakini Rachna alibaini hali tofauti kwenye sura ya Magosho.
“Gosoo” aliita Rachna kwa sauti ya chini.
Magosho hakuitika wala hakugeuza shingo kumtazama binti yule wa kihindi. Alikuwa amesikia vizuri wito ule lakini moyo wake ulisita kutoa ushirikiano wowote ule. Alihofia sana kupoteza kibarua chake kwa mambo ya kipuuzi kama yale aliyokuwa ameyafanya Rachna.
“Vhevhe Gosoo!” Rachna aliita tena kwa sauti.
Magosho hakuitika bali aligeuza shingo yake na kumtazama Rachna kisha akarudisha macho yake kutazama mbele.
“What is the problem?” (Tatizo nini) Rachna alihoji kujua kama kulikuwa na tatizo.
Magosho alitingisha kichwa kuonesha kuwa hakukuwa na tatizo lolote ambalo lilikuwa likimkabili.
“Sasa mbona iko ivo, au Mom iko kosea vhevhe?” Rachna akahoji kwa sauti iliyokuwa imejaa mashaka.
“Hapana dada Rachna nipo sawa tu” Magosho alizungumza huku akibana mafuta na kubadilisha gia kwenye tuta la barabarani.
****
Mawazo ya woga yalimjaa Ashura kila lipokuwa anakumbuka kesi za vijana wa kitanzania kuvuma kukamatwa na madawa ya kulevya nje na ndani ya nchi. Alimtazama Zawadi kwa hasira kwasababu ndiye aliyekuwa anamshawishi kufanya biashara ile.
“Haiwezekani” alisema Ashura kwa sauti ya msisitizo.
“Kipi kisichowezekana?” Zawadi alihoji huku macho yake akiwa ameyafinya kidogo kuonesha umuhimu wa swali lake.
“Mimi siwezi kufanya biashara haramu” Ashuara alizungumza kwa msisitizo
“Nahisi una wazimu we binti”
“Kama ningekuwa na wazimu ningekubali kufanya biashara za ajabu ajabu kama hizi” alizungumza Ashura kwa kujiamini.
“Kwahiyo unachokitaka hasa ni kipi?” Zawadi alihoji kwa sauti iliyojaa kiburi
“Nahitaji kutoka humu kwenye hili pango lenu” alisema Ashura.
“Pango la nani?” alihoji Zawadi kwa mkazo.
“Sijui mimi, ninachotaka ni kutoka humu” Ashura aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
“Umechelewa Ashura, tayari umeshafahamu ziri za kitumbua cha kihindi. Hivyo hili pango linakuhusu kwa namna moja ama nyingine” Zawadi akaeleza kwa msisitizo.
“Thubutuuu!, Zawadi kumbe hunifahamu vizuri wewe!” Ashura akazungumza kwa vitisho ili kumshawishi Zawadi aweze kumuacha Huru.
“Kwahiyo unataka kusemaje Ashura?” Zawadi akahoji kwa msisitizo mkubwa huku akijitikisa na macho yake akiyachezesha kwa dharau na kebehi.
“Naondoka, wewe endelea na vitumbua vyako vya kihindi” alizungumza Ashura kwa msisitizo.
“Okay, unaweza kuondoka” Zawadi alijibu taratibu lakini kwa sauti iliyokuwa imejaa gadhabu.
Ashura alibinua midomo yake kwa hasira kisha akavuta hatua kuanza safari ya kurudi kule walipotokea. Ni kweli kabisa pesa alikuwa anazihitaji lakini anaufahamu vizuri mziki wa watu wanaokamatwa kwa uhalifu wa madawa ya kulevya.
Zawadi alisimama huku mikono yake ameikumbatia kifuani na kumtazama jinsi ambavyo Ashura alivyokuwa akiondoka kwa kiburi. Aliachia tabasamu na kutikisa kichwa kwa masikitiko.
Ashura alitembea kwa haraka sana ili kutoka ndani ya pango lile ambalo alikwisha baini kuwa lilikuwa ni pango la uhalifu. Ndani ya moyo wake alipanga kwenda kutoa siri ile kwa jeshi la polisi ili kutokomeza shughuli zile.
Alipofika kwenye kile chumba cha kwanza walichoingilia alikuta makabati yako wazi na pesa zikiwa zinaonekana. Alisimama kwa sekunde kadhaa akizitazama pesa zile ambazo Zawadi alimueleza kuwa zilikuwa ni za kwao wawili. Alikumbuka hali halisi ya maisha yake yeye na kaka yake Magosho, akajiona ni upunguani wa akili.
Pamoja na kwamba hali ya woga ilikuwa imemtawala juu ya biashara ile iliyokuwa inapigwa vita kila kulipokucha na serikali pamoja na vyombo vya dini lakini maburungutu ya pesa yaliyokuwa yanamtazama kwa tabasamu la bashasha akajikuta akipatwa na tamaa ya kumiliki pesa zile.
“Potelea mbali bwana! kwani mie ndio nitakuwa wa kwanza kufanya biashara hii?” alijiuliza mwenyewe moyoni. Aligeuka na kurudi kule alikokuwa amemuwacha Zawadi amesimama.
“Zawadi” aliita Ashura kwa sauti ya upole na unyenyekevu.
“Vipi umesahau nini?” Zawadi alijibu kwa jazba huku akimtazama Ashura kwa jicho la dharau na kebehi.
“Hakuna nilichokisahau shoga”
ITAENDELEA
Kitumbua cha Kihindi Sehemu ya Tano
Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;
- Aisha Mapepe – Msamalia Mwema Alivyonila Utamu
- Aisha Mapepe – Ingiza Popote Bosi
- Aisha Mapepe – Binamu Alivyonionja Sebuleni
- Aisha Mapepe – Shemeji Usimwagie Ndani
- Aisha Mapepe – Mmh Dereva Bajaji Usiingize Huko
- Aisha Mapepe – Muuza Bra
- Aisha Mapepe – Afande Alivyonila Utamu Kituoni
- Aisha Mapepe – Mganga na Utundu Wake
- Aisha Mapepe – Baba Ake Martha Alivyonitafuna Kwenye Gari