CHOMBEZO

Ep 01: Kitunguu Saumu

SIMULIZI Kitunguu Saumu
Kitunguu Saumu Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA: CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo: Kitunguu Saumu

Sehemu ya Kwanza (1)

“Kama bahati ni kuwa na bwana mwenye hela mimi sina bahati aisee. Najua bahati imegawanyika mara mbili; kuna bahati nzuri na bahati mbaya; kwa hiyo kwa usahihi kabisa niseme kuwa sina bahati nzuri ila nina bahati mbaya.

“Bora huyo bwana awe ananihonga vihela vya kusuka kama mabwana wa mwenzangu Adellah maana mabwana ninaopata mimi ni makapuku balaa, hata hela ya pedi na losheni sipati.

“Najiuliza nashindwa kujua sababu yangu kuwa hivi, kwa sababu kwanza mie sio mbaya kama Adellah, lakini mwenzangu anahongwa balaa, na ndoa anazikataa mwenyewe. Wakati mie hizo ndoa nazitafuta kwa tochi tangu nilipokata tamaa na harakati zangu za Umiss na ndiyo nilijuana Adellah huko kwenye harakati za ulimbwende.

“Muone namsema lakini amelala tulii, hapo ameachiwa namba na tip za laki laki kutoka kwa mabwana zake, mie hata kupewa tip za wanja loh!” aliwaza Naima akimvua Adella sare zake za hoteli na kumsaidia kumlaza kitandani shoga yake aliyelewa tilalila kwa ofa za bia kutoka mwanaume wake.

Naima alikumbuka alivyojifanya ana tabia njema mbele ya mwanaume wa Adella, tena akinywa soda tu lakini mwenzake Adella alikunywa Konyagi akishindana glasi na bwana ake, tabia mbaya kwa mwanamke kuwa mlevi lakini Adellah alipendwa hivyohivyo.

Ona Naima alikumbuka alivyoongea kwa staha na utaratibu, lakini Adella aliongea mbele za huyo bwana ake kwa mitusi na kupayuka, lakini Adellah alipendwa hivyohivyo na alihongwa na mihela na bila bwana wa Adella wangepanda daladala usiku huo kutoka Gongola Mboto hadi Moshi Bar kwenye chumba chao walichopanga, lakini kwa sababu ya bwana ake Adellah aliwapa hela ya bajaji na zaidi.

Basi Naima aliumwa kwa wivu, akamaliza kumvua shoga yake nguo na kumlaza vizuri kitandani, kisha akamtazama vizuri kumkagua vizuri kujilinganisha kuwa anazidiwa nini yeye na Adellah hadi bahati imchezee shere. Wote walikuwa weusi; mzigo wake ni namba nane na Adellah kajaliwa hipsi kavu na hana wowowo la kutisha. “Au kisa mimi nimezaa?” Aliwaza Naima akijikagua kama anamichirizi ya tumbo.

KITUNGUU SAUMU 2

(mr x part 3)

Wakati akiwaza hayo ghafla simu iliita, akashtuka na kugundua kuwa siyo Techno yake bali ni ya Adellah. Akaipuuza na kuvua nguo zake na akaenda kuoga kisha akarudi tena kitandani kujiegesha kiubauvu ubavu pembeni ya Adella aliyekuwa akikoroma kilevilevi.

Mwenyewe Naima akasoma dua na kumuomba Mungu ampatie mwanaume aolewe na kupunguza makali ya maisha yaliyomfanya awe muhudumu wa hoteli badala ya bosi mahali fulani.

Akiwa amemaliza dua lake na kuanza kulala, ghafla mlio wa simu ya Adella ulianza kusumbua ngoma za sikio ya Naima, akavumilia, ikaita tena na tena zaidi ya mara tisa kisha ikakatwa tu na milio ya meseji mbili za harakaharaka ukaingia.

Naima akajiuliza ni nani aliyekuwa akipiga simu ya Adella vile, isije kuwa ni taarifa mbaya kutoka kijijini kwao huko Mwanza, maana Adellah na yeye ndugu zake hawakawii kulia matatizo.

Basi Naima kwa shauku akafungua simu ya Adellah kwa vile pattern yake aliijua akaifungua na kuona missed calls kuwa za namba ngeni yaani mpya kabisa.

Akaitazama meseji ya mtu huyo ili aweke hakika kuwa ni mwanaume tu au ni nani? Basi akafungua ile meseji ikasema hivi:

“Hallow Adellah, ile ishu siyo wiki ijayo tena, bali ni kesho kutwa. Yule mzungu ameshafika. Na sasa kinachotakiwa tukutane kesho Ocean View, kisha nikupeleke shopping na saluni na kukuanzia kukupa ile hela ya kianzio. Halafu nitumie picha zako ambazo hujaweka make up au kuziphotoshop kwa whatsapp ili na mimi nikujue kwanza hata kwa sura na kama Mzungu atakukubali. Ingekuwa nakujua tusingekuwa na usumbufu huu. Ni muhimu na ukipata meseji hii utume picha zako haraka. Tafadhali kama ratiba zako zimekaa vibaya niambie mapema nimtafute mtu mwingine mzungu hataki kusubiri.”

Loh Naima aliisoma meseji ile na kumtazama Adellah kisha akaisoma tena na kugundua kuwa huyo mtu na Adellah hawajuani hata kidogo, na hilo linaonekana dili kubwa mno.

“mh kwanini nisilichukue mimi?” aliwaza Naima.

Je, nini kitatokea..

KITUNGUU SAUMU 3

(mr x part 3)

Haraka Naima akakopi namba kwenye simu yake na kufuta zile missed calls kwenye simu ya Adellah kisha akatuma meseji haraka.

“Hi, samahani nilikuwa nimesinzia, mimi ni Adellah namba yangu kuanzia leo ninatumia hii, picha ninakutumia sasa hivi whatsapp.” Aliandika Naima akitetemeka na meseji ikadeliver.

Akaanza sasa kuangalia picha zake huko kwenye Gallery kuona ipi inafaa, akaiangalia moja baada ya nyingine kuanzia alizojibinua kuonesha makalio yake na zile alizopiga na viguo vya bichi, akaona hizo zafaa akazituma haraka.

Lakini hazikuwa zimeonwa wala meseji zake hazikujibiwa, ikabidi usiku ule apige simu kwa namba ile.

“Hallow,” aliongea Naima baada ya simu kupokelewa.

“eeh wewe nani?” ilijibu sauti ya pili.

“Adellah, nimeshakutumia picha zangu, nipo tayari kwa hiyo kazi kesho,” alisema Naima midomo ikimtetemeka, huyo mtu wa upande wa pili alizungumza kiofisi zaidi hata katika usingizi wake akasema: “sawa ngoja nizitazame na kuzifowadi hapa sasa hivi, kesho nitakwambia muda gani tuonane,” alisema.

“Okey asante,” alijibu Naima aliyejifanya Adellah na kukata simu yake.

Mara kidogo wakati huo simu yake ikaingia ujumbe wa whatsapp kutoka kwa huyo mtu wa ajabu aliyetoka kuongea naye ikisema: “waoh ni mzuri kama nilivyokuwazia, mzungu amefurahia kukuona.”

Naye Naima akajibu: “Asante.” Kisha wakaagana usiku mwema tena.

Naima akashindwa kulala moyo ukimuuma kwa kuchukua bahati isiyo yake. Lakini akajiapia kuwa kamwe hatofungua domo lake kusema chochote kwa Adellah.

Kesho yake asubuhi na mapema Adellah aliamka na mning’inio wa pombe za jana yake, haraka akakimbilia simu yake na kuangalia meseji na simu kadhaa alizozikosa jana yake. Uzuri hakukuwa na kitu chochote, akashusha pumzi kama vile alishukuru.

Wakati huo Naima alikuwa akimchungulia tu kwa kijicho pembe akimuona mwenzake kwa yote aliyokuwa akiyafanya.

Adellah akanyanyuka na kichupi chake na kama kawaida yake asubuhi zote, akaanza kujinyoosha shingo yake kisha akajinyoosha mgongo, akagusa mguu wake kwa mkono wa kushoto na akafanya hivyo kwa upande wa kulia, kisha akainama kabisa hadi chini kujinyoosha kiuno.

KITUNGUU SAUMU 4

(Mr X part 3)

Naima alishazoea ujinga huo wa Adellah kila asubuhi, na hapo hatua iliyofuata alijua tu ni lazima Adellah atawasha mziki, hivyo alijiandaa kujiziba na mto masikioni maana alikera mno lakini mwenyewe akiyaita hayo ni mazoezi.

Siku hiyo Adellah akijua atamuudhi mwenzake kwa makelele, akavaa earphone alizonunua jana yake akazivaa akisikiliza na kuanza kuucheza ule wimbo wa Dullah Makabila ule wa Hujauramba.

Basi Adellah akaanza kuzungusha kiuno, huko na huku, akakatika kwa staili zote, sasa ile mihemo na vishindo vyake akifuata stepu ndiyo vilimfanya Naima ashindwe kuvumilia. Akashtuka na kukaa kitandani.

“Oyaa! We Adellah?” alikoroma Naima.

Adellah asisikie kabisa, akaendelea na kucheza kisingeli chake tena akacheza staili mpya ya ajabu ambayo anapitisha mikono chini na kujinyanyua miguu kama vile chura, kisha kiuno na miguu ikiwa inasapotiwa na mikono akikatika kwa staili hiyo ngumu iliyoitwa kwa jina la chura panzi na wachache tu ndiyo walikuwa wakiweza kuicheza.

Adellah alipogeuka katika stepu zake, alishangaa kuona sura ya mwenzake akiwa amenuna akimtazama. Uzuri alikuwa ameshamzoea na gubu lake akavua foni moja ili amsikilize kwanza bila kuacha alichokuwa akikifanya.

“makelele bwana, hivi una nini lakini!” alilalamika Naima. Adellah akatazama saa jasho likiwa linamtiririka.

“we mida ya kazi hii jiandae,” alisema Adellah akiacha alichokuwa akikifanya na kujiandaa kuingia bafuni.

“leo siendi kuna sehemu nataka kwenda mara moja,” alisema Naima kichwani mwake akiwa amepanga kabisa kwenda kuonana na yule mtu wa jana yake.

“Oh haya usisahau kumuaga bosi,” alisema Adellah na kuingia bafuni kuoga akamaliza yake na kujiandaa kisha akaelekea huko hotelini kwake.

Wakati huo Naima naye akapokea ujumbe kuwa waonane na Yule mtu saa sita asubuhi. Akajipula kwa uhakika na kuanza safari ya kipofu asijue mbele kuna nini zaidi ya kujua tu kuwa kutakuwa na hela yakutosha na ishu inahusisha wazungu, hivyo kama si mapenzi basi matangazo ya urembo wa bidhaa Fulani na yeye kwa ukata ule alikuwa tayari kwa yote hapo.

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 5

Naima akapanda kibajaji, mwendo wa dakika thelathiniakafika hapo Ocean View Hotel, akapiga simu kumtaarifu huyo aliyemfanya asafiri.

“Hallow nimevaa shati ya bluu bahari, nimekaa huku restaurant kona ya mwisho kabisa,” alisema huyo mwanaume. Hapo Naima akatembea kwa shaka hadi akaona mtu huyo kwa mbali akimpungia mkono.

Alikuwa ni mvulana mzuri mtanashati sana, kama vile wale mamodo wa matangazo ya televisheni. Alivaa mavazi mepesi na kujazia mikono yake vizuri kwa mazoezi na hata ngozi yake iliwa laini ishara kwamba aliitunza vizuri ili imuingizie kipato chochote labda.

“mambo kaka!” alisalimia Naima akipima kama sauti yake inafanana na huyo mwanaume aliyekuwa akizungumza naye kwenye simu muda si mrefu.

“poa tu, bila shaka wewe ndiye Adellah,” alisema huyo mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Friday.

“sasa Adellah kama tulivyoongea siku za nyuma, kuwa nitakupigia simu na kukutaarifu kuhusu lile dili, kwa bahati mbaya au nzuri mzungu kawahisha haraka anataka ukutane naye, sasa mchongo umenyooka kama nilivyokwambia, kikubwa nikwambie tu tutasafiri hadi Alabama na kila kitu tutakifanyia kule kwa muda wa mwezi mzima mkataba ni wa dola laki moja kwa hela ya kitanzania ni zaidi ya milioni mia mbili na laki tatu na upumbavu. Aaar malipo ya kabla ya safari ni shilingi milioni nne, na mengine ni kulekule.” Aliongea Friday kila neno likimvuruga Naima vibayavibaya.

Sasa kwa vile huyo Friday alisema alishaongea na Adellah mwenyewe, ikawa ngumu kwa Naima kuuliza tena kuwa ni jambo lipi aendalo kulifanya huko Alabama maana asije akashtukiwa bure, tena alivyosikia hizo hela eti milioni mia mbili na laki tatu kama malipo ya mwezi tu akachanganyikiwa. Eti tena atapewa milioni nne kabla ya safari loh!

Akafikiria kuwa kama Adellah alikubali kufanya dili hilo maana yake hata yeye anaweza kulifanya kwa kuwa alijipa imani kuwa hakuna kazi anayoiweza Adellah yeye aishindwe.

“Enhee Adellah niambie, akaunti yako ya benki umekuja nayo?” aliuliza Friday.

“aah hapana au?” alijiumauma Naima akishindwa kujua kama aliambiwa aje nayo au lah!

KITUNGUU SAUMU 6

“kwa hiyo unataka kupatiwa cash?”

“hapana itabidi unitumie hata tigopesa haina shida, siku hizi si kuna huduma za simu banking?” aliongea Naima.

“aaanhaa okey!” alijibu Friday na hapohapo aakaanza kuchezea simu yake, kisha akatuma.

“Tayari nimetuma, umepata meseji?” aliuliza Friday.

“hapana, sijapata,” alijibu Adellah akipekua simu yake. Ghafla Friday akashtuka na kucheka.

“doh nitakuwa nimekosea na kutuma ile namba yako ya jana loh!”

Mamaa! Sura ya Naima ilimshuka kama kapigwa na shoti ya umeme. Maana yake hela yote imeenda kwa Adellah mwenyewe.

“Aisee piga basi mtandaoni warudishe utume tena,” alisema Naima.

“hapana ni ngumu watasema watarudisha baada ya masaa ishirini na nne, kwani ile laini yako tuliyokuwa tunawasiliana nayo ina tatizo gani?” aliuliza Friday akimshangaa Naima.

“Aaar ina matatizo ya tigopesa,” aliwaza haraka mno Naima maana aliogopa asije akaipiga akaipokea Adellah bure halafu ikazua tafrani.

“Sawa kama ina matatizo ya tigopesa karipoti tu wakurekebishie ni jambo dogo tu ukienda kwenye mtandao husika, sasa hapa cha msingi twende shopping na tukakate kabisa passport za kusafiria safari ni jumanne,” alisema Friday, wakati huo Naima alikuwa akijisikia ganzi tu akiiwaza ile hela maana alijua tu asipompanga Adellah kihela chote kitapigwa.

Akaomba kwenda msalani mara moja, akafika huko akapiga simu kwa Adellah haraka, simu ikapokelewa.

“We Adellah! Sikia kuna pesa hapo imetumwa kupitia benki, milioni nne, kuna danga hapa nimeliambia litume kwenye namba yako, mie yangu inasumbua shoga, nakuja kuichukua niki..” kabla hajamalizia kuongea simu ikakatwa. Naima akaipiga tena haikupatikana. Akaandika kwa meseji na kumtumia Adellah tena ili ujumbe umfikie.

Loh huko alipo Adellah kumbe alivyoiona mihela yote ile inaingia akahaha kuichomoa harakaharaka akiunganisha mawakala kwa mawakala hadi akaitoa yote na kuiweka takoni na hivii alikuwa akizima simu ndiyo Naima akamuwahi. Sasa alishajua imetoka kwa Naima akajiuliza asepe nayo au abaki nayo. Akapiga akili harakaharaka, akajisema moyoni: nina matatizo kibao, Naima nimekutana naye kimjinimjini nitaachana naye kimjinimjini.

Basi akarudi na kusafisha gheto akasepa kavukavu.

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 7

Wakati huo Naima na Friday wakaenda shopping wakazunguka huku na huko, Naima akanunuliwa miparo ya kila aina, akaijaza kwenye begi na wakapelekewa hotelini akikabidhiwa chumba chake, na Friday akamtaka Naima alete baadhi ya stakabadhi mfano kitambulisho cha kupigia kura au leseni ya udereva, au hata cheti cha kuzaliwa na akikosa basi hata kitambulisho tu cha kazi.

Lakini Naima hakuwa na amefikiria hilo awali, akajishtukia maana kila kitu chake kiliandikwa Naima Abdul na si Adellah Mbugani kama alivyojulikana, hapo sasa tumbo likaanza kumuuma.

“Sikia kaka Friday, mimi kwa bahati mbaya sina chochote kati ya hivyo, nisaidie tu tufanye hata passport ya kutengeneza,” aliongea Naima akijaribu. “Mh!” Friday aliguna kidogo na kunyanyua simu akaongea pembeni kiingereza, kisha akarudi Naima wakati huo wasiwasi ukamjaa.

“sawa mzungu amekubali atufanyia kila kitu, lakini ujue wewe ndiyo muhimu kweli, kwangu pia maana hilo dili mimi nisingepewa bila wewe, kwa hiyo jiandae nenda nyumbani kachukue vitu vyako uje kulala huku hotelini, beba kila kitu cha mkoleni na ya kumbuke ya unyagoni, tukifika kazikazi na hatutakiwi kukosea,” alisema Friday akili ya Naima ikalia; Ngriiiiiii! Aliposikia hayo maneno ya Mkoleni na Unyagoni.

Akatamani kuuliza maana yake nini maana hayo maneno lakini akajizuia maana alikuwa kama vile anayajuajua na kama vile hayajuijui.

Lakini kwa kuwa amepatiwa nafasi ya kwenda nyumbani kwanza alipanga akifika huko mtaani aulizeulize hata kwa majirani maana alianza kuogopaogopa, akajaza majina yake kamili kwenye karatasi, umri wake, mahali alipozaliwa kwenye karatasi na kuagana na Friday kwa muda kwanza hadi baadaye.

Akiwa njiani akampigia rafiki yake Witness mcharuko.

“Hallow shoga mambo?” alisalimia Naima.

“poa tu vipi Naima?” alijibu Witness baada ya kupokea.

“nauliza eti unajua maana ya Unyagoni ni nini? Maana kama nimewahi kukusikia kutoka kwako hivi!” aliuliza Naima.

“mmmh unyagoni hujui maana yake we shoga wa wapi?”

“bwana niambie bwana,” alilalamika Naima akijishtukia maana yeye ni Wa-arusha kabisaaa. Na arusha ndiyo hawajuagi mambo ya mahaba kabisaaa wao wanatafuta hela tu.

KITUNGUU SAUMU 8

“Unyagoni shoga ni kwenye mafunzo ya watoto wa kike kujifunza mambo ya kikubwa, staha na kuishi na wanaume na mambo kibao,” alijibu Witness, Naima akakumbuka loh!

“enhee na Mkoleni!” aliuliza tena.

“mkoleni ni kwa kizaramo au makabila ya pwani lakini ni unyago tu huohuo, kwanini unaniuliza mambo hayo leo hii vipi?” aliuliza Witness.

“anhaa basi tu, hebu niambie hivi huko mkoleni, ndiyo wanajifunza mambo gani kwa mfano yaani,”

“mengi tu, inachukua mwezi mzima we kwani leo vipi?” alizidi kuuliza Witness. Naima aliposikia hayo mambo kuwa ni mwezi mzima akaona Doh! Sasa yeye atawezaje kwenda kuyajua kwa siku moja na kwenda nayo huko Marekani hiyo kesho kutwa.

Akawa na wasiwasi kama nini, akaona bora asiumbuke nchi za watu, kama vipi achukue ile milioni nne hata akimgawia Adellah laki tano haina shida, halafu amkimbie Friday.

Sasa akiwa anakaribia nyumbani ndiyo akawaza; ina maana Adellah anafahamu mambo ya mkoleni na ndiyo maana aliitwa kwenye dili hilo au? Mh inawezekana kweli maana alikumbuka michezo ya viuno ya Adellah, akakumbukaga alimuona akivaaga shanga, akakumbuka hadi mambo yake ya kiswaziswazi, na wanaume kumgandaganda, loh!

Nafsi yake ikamsuta maana dili halikuwa lake halafu kalivalia njuga halafu haliwezi na analikimbia, sasa si ni bora tu angemuachia rafiki yake masikini. Lakini potelea pote.

Naima akarudi nyumbani na kupapasa ufunguo chini ya kanyagio la miguu pale mlangoni, akafungua ndani, hakuamini macho yake aliona chumba kikiwa cheupe zaidi tu ya mabegi yake na kitanda kikavu, lakini si godoro wala kitu chochote cha Adellah. Akampigia simu Adellah haikupatikana.

Akapiga simu ofisini kwao, akasikia tu Adellah aliondoka mapema asubuhi bila hata kuomba ruhusa, na alionekana akiwa na haraka fulani hivi. Moja kwa moja Naima akajua kalizwa.

Lakini hakulia zaidi alicheka maana alijiona mjanja aliyezidiwa kete.

Sasa hapo hakuwa na namna zaidi ya kurudi tu kwa Friday, tena afanye awezavyo siku hiyo ajifunze ajifunzavyo ili aende Marekani la sivyo atakufa masikini Dar.

itaendelea

KITUNGUU SAUMU 9

Naima akapanga vitu vyake roho yake ikimuuma. Akaweka makabrasha ndani ya bajaji na nauli ikiwa ni hela yake kabisa kutoka mfukoni maana ile hela aliyopewa hakuwa nayo kabisa ndiyo hiyo aliyoibiwa na Adellah.

Akasonya na kumtukana Adellah kikwao. Alipofika hotelini, sasa akawa amechanganyikiwa aanzie wapi amalizie wapi. Akaona ngoja ampigie simu tena Witness, maana hali yake haikuwa hali.

“Hallow, sikia witness, nina mwanaume hapa ananisumbua hatari, eti anataka nimfanyie mambo ya mkoleni, sasa na mimi nimeogopa kumwambia sijafundwa, ndiyo leo usiku tunakutana kitandani tatizo ana hela sana, naomba nisaidie wangu plizi nifunze hata viwili-vitatu!” alisema Naima akidanganya. Loh Witness akacheka na kumwambia laivu kuwa haiwezekani kwa kuwa kila kitu hufundishwa kwa vitendo na si kurupukurupu hivyo.

“Mh shoga hapo siwezi kukusaidia, ungesema nije nikuelekeze kidogo sawa, lakini sidhani kama tukiwa mbali hivi utaelewa chochote. Lakini kuna njia, hebu ingia mtandaoni pekenyua stori Fulani hivi inaitwa Mr X kuna mdada alikuwa hajui akajifunza na mafunzo yote yamo humo,” alisema Witness.

Hiyo ikawa ahueni kwa Naima akajiegesha kitandani kwa wasiwasi na kuchomeka chaji ukutani akaanza kutafuta hadi akaipata hiyo stori, maana alitajiwa akaunti halisi ya mwandishi wa huo mkasa.

Akaanza kusoma akiwa na mashaka tele, hakujua kama ataweza kujifunza chochote ndani ya stori hiyo maana ilikuwa kama kula gizani. Akaanza taratibu na taratibu ikawa anasoma na kunogewa, akaona mahali imekatishwa na inatakiwa kulipia.

Hakuwa na hela ikabidi akope tigo, akapatiwa shilingi elfu tano, akampigia mwandishi maana namba yake ilikuwa pale kwa juu, akatuma hiyo elfu mbili ya kuendelea na kuungwa akaimalizia ile ya Mr X part One, akaviweka akilini vipengele na alipomaliza akaanza sasa kufanya kwa vitendo maana alijijua kuwa alivyovipuuzaga ndiyo hatma ya maisha yake huko aendako.

Alipotaka kuweka simu yake chini, akashtuka kuwa eti kumbe kuna Mr X part Two, akaanza kuisoma na kusomana, loh! Hiyo ndiyo ilikuwa hatari ikawa na mambo ya mkole kabisa na kungwi.

KITUNGUU SAUMU 10

Mafunzo yalitolewa na bibi Gululi na ni kulipia elfu mbili mia tano na kuendelea na stori ni shilingi elfu mbili.

Naima akashusha pumzi na kuona hayo ndiyo aliyokuwa akiyataka, akapiga simu tena kwa mwandishi wake, Chande Abdallah, akapokelewa na alichoongea kilitia huruma.

“kaka yangu, naomba nipo chini ya miguu yako, hadithi yako ndiyo maisha yangu, nikiikosa naweza kudhalilika ndiyo maana nimelipia ile ya kwanza na kuisoma haraka, nataka kulipia ya pili, lakini nataka sana hayo mafunzo ya Bibi Gululi, naomba nisaidie naomba nipo chini ya miguu yako, nina elfu mbili tu tena nimekopa tigonivushe,” alilia Naima kilio chake kikamgusa huyo aliyeandika hicho kitabu mtandao (ebook) akamtumia yote tena bila malipo na kumtaka akiwa sawa amtumie hela.

Basi Naima akashukuru, kichwa chake sasa kikiwaza kwa kasi, akasoma asitoke nje ya kile chumba, jua likazama na usiku ukaingia; yeye akiwa amejifungia tu akisoma, asijisikie njaa wala nini, mafunzo na video za mfano zilimuwehusha, akasimama na kuiga, akafanya mazoezi ya kutosha haraka mno akaishia kuumwa kiuno na mwili kuchoka maana ng’ombe hanenepi mnadani.

Lakini akasikia kuhusu huyo msimuliaji aitwaye Mary kuwa anaishi Marekani. Akawaza akiwa na kihela kwanini asimtafute hukohuko Marekani ili amfunde walau! Akaweka akilini kuwa atamuomba mwandishi ampe namba ya Mary.

Wakati Naima akiwaza hayo tu ghafla alisikia mlango wa chumba chake ukagongwa, akasimama na kufungua. Ooh alikuwa ni Friday na kibukta chepesii mkononi akiwa na chakula kilichowekwa kwenye sahani za vitundutundu kila kitundu kikiwa na msosi wake.

“Mambo Adellah!,aar nimeona umejifungia ndani kimya, nimekuletea chakula, halafu leo ningependa tulale wote ili nijue ufundi wako na wewe uujue wangu,” alisema Friday.

“yaani nini sijakuelewa!” alihamaki Naima.

“Adellah cha ajabu nini wakati tukienda kule tutakuwa tunafanya kila siku!” Doh Naima akastaajabu na kujiuliza: “Ina maana huko niendako nitakuwa na sex na Friday ndiyo nilipwe hela zote hizo? Na haya ya Unyagoni nitamuonesha yeye au? Na huyo mzungu je?”

“Anhaa okey, usijali ni leo tu tumbo langu linaniuma hivi hata sijisikii vizuri sana,” alisema Naima akijaribu kumkwepa Friday.

“Ooh, halafu uliposema kuhusu kuumwa tumbo umenikumbusha, kesho asubuhi kuna daktari atakuja kutupima magonjwa yote, ikiwemo ya ngono na tutapewa matibabu ili kule tuendako tuwe na afya njema,” alisema Friday.

“Mtihani mwingine huu,” aliwaza akilini Naima wakati Friday akiondoka mle chumbani.

Sasa Naima akaanza kujiuliza akilini mwake akiweka wazo kuwa huko aendako lazima tu kutakuwa na mambo ya kuektishwa filamu za ngono, akaiwaza na ile mihela aliyotakiwa kulipwa akaona hata kama afanyishwe ngono na mbwa alikuwa radhi kuichukua na kurudi Tanzania kama milionea kwani nani atajua.

Kweli hiyo kesho yake ikafika usiku mzima wa jana yake akiutumia kusoma na kujifunza mambo ya makungwi, kichwa chake kikika riri nadharia ya mafunzo yote, ingawa kwenye matendo ndiyo alikuwa akipata wasiwasi kama ataweza kuyamudu au lah.

Mida ya saa nne asubuhi ilipofika Friday alimpigia simu Naima kwenye chumba chake na kumuitia kwenye chumba chake, Naima aliingia kwa wasiwasi na kumkuta kuna mzee wa makamo aliyevalia kistaarabu akiwa huko.

Huyo mzee akatoa vipimo Fulani kutoka kwenye begi lake na kuanza kuwapima mmoja mmoja akichukua kipimo cha damu kubwa, akawapima kinywani kwa kuwataka kila mmoja apanue midomo. Halafu akawapima presha. Kama haitoshi akawapima mkojo na choo kikubwa. Na mwishoni kabisa, akampa Naima kidude Fulani hivi cha pamba kama vile vile vipamba stick, na kumwambia akiingize sirini mwake akikizungusha kwenye kuta za sehemu zake za siri kisha ampe.

Daktari huyo akatoka na vipimo vyote hivyo na kuondoka navyo.

“Adellah, vipi mbona unaonekana una wasiwasi kwenye kila kitu, kama vile hatujawahi kuongea?” aliuliza Friday wakati daktari Yule akiwa ameondoka.

“mh hapana ni ugeni tu tatizo,” alijitetea Naima.

“sawa lakini, mbona kwenye simu unakuwa mjanja, lakini hapa unaonekana mpole sana kwanini? Au tuwe tunachati tu kwa simu na siyo kukutana laivu?”

ITAENDELEA

Kitunguu Saumu Sehemu ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment