CHOMBEZO

Ep 04: Kitunguu Saumu

SIMULIZI Kitunguu Saumu
Kitunguu Saumu Sehemu ya Nne

IMEANDIKWA NA: CHANDE ABDALLAH 

********************************************************************************

Chombezo: Kitunguu Saumu

Sehemu ya Nne (4)

*Harufu ya vita ikanukia! Na huko mbele siyo kuzuri!

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 35

Basi Naima hakuchelewa akarudi haraka pale bustanini, akimtazama Friday akielekeza dawa zake kwa kundi la wanaume wa kizungu waliomjalia, maana wengine ukute walikuwa na vibamia hatari.

“Naima, unajisikiaje?” aliuliza Jenny.

“ooh kichwa kimepungua sasa, Jenny hivi hapa kuna mtu wa maabara?” aliuliza Naima.

“Yah, kuna Mkemia, Madam Johan, yule pale,” alisema Jenny akimuoneshea kidole mwanamama Fulani aliyetulia tu bustanini akitazama wanaume wanavyozongana kumpampatikia Friday na vizizi vyake, lakini alipomuona Jenny akimuoneshea kidole, akasimama na kusogea upande wao.

Wakasalimiana na Naima na kutambulishana vizuri tena mama huyo akafurahi kupata muda angalau kuonwa na Naima.

“Mwambie, anaweza kuzihakikisha hizi dawa ili upate ushahidi kamili kuwa ni zina tiba hiyo kweli, pasipo na madhara kwa mtumiaji?” alisema Naima akimwambia Jenny amwambie kwa kiingereza Madam Johan.

Jenny akamnyooshea lugha, Madam Johan. Kweli akatikisa kichwa kuonesha kukubaliana naye.

“Jamani; mimi naitwa Madam Johan ni Mkemia, ningependa hizo dawa zote nichukue sampo kidogo nikazifanyie uchunguzi kuthibitisha kama hazina madhara kabla hamjaanza kuzitumia,” alisema Madam Johan kukawa kimya na hata wale wazungu walioshoboka wakazirudisha zile dawa kwa Friday, ili mtaalamu athibitishe.

“Kwa hiyo somo la dawa halitaendelea hadi yeye azithibitishe au?” Friday akiwa amepigwa na butwaa akamuuliza Madam Alexandrina.

“Ndiyo hakuna namna, unaweza kufundisha kitu kingine hizi dawa tumpe yeye azifanyie uchunguzi kwanza,” alisema Madam Alexandrina.

“uchunguzi unachukua siku ngapi?” aliuliza Friday akiwa amechukia kwelikweli maana hapo yeye hakuwa na kipya zaidi ya hizo mada za tiba za kunjunjana tu.

“unachukua hata mwezi, miezi au mwaka, ni utaratibu wa kawaida, kosa ni langu sikukwambia hapo kabla, ni kwa ajili ya usalama wa watu wa marekani si unajua mambo ya sheria na sera za nchi,” alisema Madam Alexandrina, Friday akalazimika kuvaa suruali yake na kulifungia limdudu lake humohumo kwa ndani maana alikatishwa somo.

Wakati akimalizia kuvaa vizuri ndiyo akamuona Naima akiwa amesimama na huyo mkemia Madam Johan.

Mh akajiongeza na kuhisi Naima kamfanyia Fitna. Akawa ameduwaa ubaoni asiwe na la kuzungumza.

KITUNGUU SAUMU 36

Ikabidi Naima asimame na kwenda mbele kama kawaida yake akijiamini mno.

“Jamani kama nilivyowaambia mwanzoni kabisa, kuwa mafunzo yetu yatakuwa kwenye mambo manne, urembo, mapishi, mapenzi na tiba. Kwa bahati nzuri kwenye kipengele cha tiba kwa kuwa tupo na mtaalamu wetu hapa Madam Johan itakuwa rahisi kuwathibitishia dawa tunazotumia Afrika ndiyo zinazotufanya tuwe hivi hadi leo bila kudhurika kwa chochote.

“binafsi nimekuja na baadhi ya tiba pia, nitaziwasilisha kwa Madam Johan kwa vipimo, kabla sijathubutu kuzileta kwenu, yote ni kwa ajili ya usalama wa afya ya kila mmoja wetu hapa,” alisema Naima akimpiga dongo Friday humohumo.

“Okey sasa, twende kwenye kipengele cha mapishi, hapa tungeweza kuzungumzia jinsi vyakula vinavyoathiri uwezo wetu wa kufanya mapenzi. Aidha kutushusha au kutupandisha. Lakini uzuri vyote mnavijua. Hivyo nimeamua kuja na kipengele kidogo tu kwenye mada hiyo ili muone maajabu ya Afrika.

“Kwetu tuna kiungo cha chakula kinachoitwa manjano; Mnakijua?” aliuliza Naima akifungua begi lake na kutoa kifuko Fulani hivi akionesha unga wa rangi ya njano ndani yake. Wote wakatikisa kichwa kuonesha hawajui chochote.

Akaanza kuelezea Naima, uzuri wake akifundisha Naima tu, darasa linakuwa sikivu na kila mmoja anaandikaandika, hiyo ikimaanisha kuwa ana karama ya ufundishaji.

Friday ndiyo akaona hivyo, roho ikamuuma zaidi, tena darasa zima akaliona likiwa bize na Naima, mtu pekee aliyekuwa akimtazama Friday kwenye kona ya umati ni Collins shoga peke yake.

Akaghadhibika. Akasikiliza jinsi Naima alivyofundisha faida za kiungo hicho na kushangaa eti akiletewa na jiko pale, akaanza kuonesha kwa vitendo manjano inavyopikiwa. Akatengeneza wali wa manjano na ndiyo kila mmoja akataka kupika kiwe ndiyo chakula cha mchana cha siku hiyo. Wanafunzi wakazidi kumpongeza Naima.

“kwahiyo, tiba zangu mpaka mkazitesti, hayo manjano walaa!” alikoroma Friday akimwambia Madam Alexandrina.

“manjano ni kiungo cha chakula Friday; sio kama tiba zako.. halafu naona kama huyu msichana anakupiku hivi kwa ubunifu!” alisema Madam Alexandrina, asijue anamtia moto Friday.

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 37

Alichukia Friday, lakini akajilazimisha kuambatana na Naima ili asije kuharibu kazi.

“Friday njoo uonje,” alisema Naima mbele za wazungu wa watu, hapana nimekosea mbele za wazungu wa Mungu. Basi Friday akaenda kuonja huo wali wa manjano. Akajilazimisha tabasamu kuwa ni mzuri.

Nafsini naye akashawishika afahamu faida za hayo manjano, maana yalimpita wakati Naima anafundisha kule ubaoni kwa sababu yeye alikuwa bize kupanga na kupangua majungu, fitina na visasi dhidi ya mwenzake.

Akarudi kuangalia ubaoni, akaona Naima akiwa ameandika:

KIUNGO TIBA

  1. MANJANO

Kubadili rangi ya vyakula kama mchuzi, Wali, samaki, nyama, ndizi, etc

Kitiba, husafisha damu mwilini, kutibu shinikizo la damu, kuondoa lehemu ndani ya mishipa ya damu, huzuia mtu kupata kiarusi, ikichanganywa na unga wa habbatt soda na asali mbichi ni dawa kurahishisha mfumo wa mmeng’enyo na pia huondoa vidonda tumbo.

Manjano mbichi na yai la kuku wa kienyeji , ukipakaa kwenye ngozi yako huilinda ngozi yako kuifanya kuwa laini bila chunusi. Ukijikata unaweka manjano kwenye jeraha,kuzuia damu.

Manjano hukuwezesha mfumo wako wa fahamu kuwa bora zaidi, hutibu mafua. Pia hufanya joto la mwili kuongezeka na NGUVU YA KUFANYA MAPENZI.

Alisoma Friday hasa hayo maneno ya mwisho, akajua tu kuwa lazima Naima amefundishwa hayo na Kungwi Ilham na siku ile alimfungashia vitu hivyo kwenye begi.

Wakati huo basi vyakula vilivyopikiwa manjano vikawa vimeandaliwa huko ndani kwa ajili ya kuliwa wanaume wakaitwa kwa chakula cha mchana, wakala na kusaza na darasa likaisha siku hiyo ya kwanza kila mtu akimsifu Naima. Naye akawahusia wakina mama kutumia kiungo hicho walau kwa siku mara moja.

“Adellah na Friday, mnaonaje hali ya hapa?” aliuliza Madam Alexandrina, baada ya kuwaita Naima, Friday na mtafsiri Jenny.

“ni nzuri sana,kwa kweli nimepapenda nimependa na watu wake,” alisema Naima, Friday akatikisa kichwa kiroho mbaya flani hivi lakini akionesha kusapoti alichokisema Naima.

“oh nashukuru sana, wanafunzi wamefurahi sana kwa ajili yako Adellah. Agh na Friday pia.

KITUNGUU SAUMU 38

“habari zimeenea vibaya mno na tunatarajia kundi jingine la wanafunzi kuongezeka kuanzia kesho, sasa tumepanga kuongeza malipo zaidi ya ule mkataba wa awali. Je, mnaweza kumudu kufundisha watu mia moja na zaidi?” aliuliza Madam Alexandrina.

“haina shida, tunaweza,” alijibu Friday. Madam akafurahi na kutoa mikataba yake mipya akawapa ili wakapitie, lakini wakati huo, akawaingizia hela ya siku hiyo moja ambayo ilikuwa kama laki tanotano hivi, doh! We kwa siku unaingiza laki tano kwa ajili ya kufundisha mapenzi, aisee watu wanathamini kazi za watu, aliwaza Naima akifurahi kama nini maana hela hiyo kwa mara ya kwanza iliingia kwake na siyo ile iliyoingia kwa Adellah kwa bahati mbaya.

Wakaondoka kila mmoja akishika njia ya chumba chake, lakini Friday akamuona Naima akichukua simu kutoka kwa Jenny, akawaza lazima Naima atakuwa anatumiaga simu ile kufundishwa usiku akiwa chumbani na Illham.

Basi akaona afanye kila fitina azuie mawasiliano ya Naima na kungwi nchini Tanzania maana bila hivyo, ataonekana yeye mjinga asiyejua kitu mbele ya Naima.

Lakini sawa je, akimharibia Naima yeye atafundisha nini? Aliwaza Friday, akajishuku na kuhisi huenda ndiyo ataharibu kila kitu na wataonekana hawajui kufundisha na kurudishwa Tanzania. Bora amuache Naima, lakini na yeye ajifunze bila hivyo itakula kwake.

Friday akaghairi kwenda kwake, naye akamfuata Naima chumbani kwake.

“sikia, Naima hela umeziona zinavyoanza kuingia, hapo cha msingi, tufanye kazi tuache majungumajungu,” alianza kusema Friday.

“sasa Friday mimi na wewe nani ana majungu? Uliwezaje kunitoa darasani kule mchana ukasingizia eti naumwa.” Alisema Naima.

“wewe haukuniachia hata pumzi, kila kitu unaongea wewe tu, na wewe ulinisemeleaje eti dawa zangu zikachunguzwe!” alisema Friday, Naima akashuka.

“cha msingi tuwe tunaandaa somo pamoja kabla usiku,” alisema Friday. Wakakubaliana usiku huo wote wawepo kumsikiliza kungwi Ilham kiroho safi.

Lakini Friday hakuwa amefanya kiroho safi. Bali alikuwa na lake moyoni. alipoenda chumbani kwake, akapiga simu kioo cha simu yake kikiandika: Adellah na safari hii simu iliita.

Itaendelea..

KITUNGUU SAUMU 39

Bila haya wala mshipa wa kiume, Friday alipiga simu, lakini alitaka asijulikane kama yeye ndiye Friday hivyo alikuwa makini kupiga kwa kutumia simu ya mtu mwingine na kurekebisha koo lake ili asikike tofauti.

“Hallow,Adellah!” alisema.

“Hallow, nani?” alijibu Adellah, Friday akagundua sauti ya Adellah ni ya usingizisingizi akakumbuka kuwa huko Tanzania ni saa kumi au kumi na moja alfajiri.

“Aar Adellah mimi naitwa Chriss nipo Marekani, ni rafiki wa Friday.”

“Eeee ndiyo!” alishtuka huko Adellah akasikiliza kwa makini nadhani hata kitandani aliketi kabisa baada ya kujua huenda ni dili la kuitwa Marekani limetiki.

“mbona haukuwa unapatikana kwenye simu?” aliuliza Friday akijifanya ndiyo huyo Chriss.

“aagh nilikuwa na matatizo na simu kwa siku mbili hivi, lakini nilikuwa naiwasha jioni,” alisema Adellah kwa wasiwasi akikumbuka alivyokuwa anazima simu na kutopokea kwa kuhofia Naima atamsumbua kuhusu hela zake.

“sasa sikia, nilikupigia sana simu baada ya Friday kunipa maelekezo ya kukutafuta; kitu kilichopo, kuna mtu anaitwa Naima nadhani alichukuaga simu yako sijui, akawasiliana na mimi akajifanya ni wewe, akanionesha na vitambulisho vyako, tukamtumia na hela akaja Marekani, mpaka sasa hivi tupo naye na anatumia jina lako.”

“nini?!” alihamaki Adellah.

“Ndiyo hivyo, Mimi nilimshtukia hivi karibuni na hata mwenyewe hafahamu, kikubwa mwenzako anapiga pesa badala yako. Na kuna hela alitumiwa lakini ni bahati nzuri tu ilifika kwako lakini ilikuwa inaenda kwa Naima hiyo,” alichonganisha Friday.

“weee! Acha utani bwana, sikia,, aagh! Sikuelewi? Nanyie mtamchukuaje mtu ambaye siyo mimi!?” aliwaka Adellah.

“we Adellah, mtu anakuja na vitambulisho vimeandikwa kabisa Adellah, na anapokea kwa simu yako, sisi tutafanyeje?” alidanganya Friday akiongeza na machumvi kabisa.

“simu yangu! lini?” alihamaki Adellah, Chriss alivyomfitini akamwambia awashe whatsapp kumtumia screenshot za simu alizopiga siku zile usiku na zilivyopokelewa.

Adellah akawaza na kukumbuka siku hiyo ndiyo alikuwa nzutu asijitambue kwa pombe na asubuhi yake ndiyo Naima alijifanya hataki kwenda kazini. Doh! ndiyo siku ambayo mchana wake alitumiwa milioni nne.

KITUNGUU SAUMU 40

Adellah alipokumbuka akajiona mjinga, maana hizo kimbia zote huku na huko kumbe amejiibia mwenyewe doh!

“sasa sikia, we sijui Chriss! Huyo Naima, mpe ujumbe wangu kuwa atanikoma.. nitam..” alikosa maneno Adellah maana mwenzake alikuwa mbali kinyama yaani kwa Trump hiyo atanikoma, sijui mikwara ya kumpiga itamfika vipi? Loh!

“Sikia, Adellah haina haja, hapa nakupa namba ya bosi wake, anaitwa Madam Alexandrina, mwambie kuwa kuna mtu anaitwa Naima amefoji vitambulisho vyako na wewe ndiyo Adellah! Mwenzako anapewa laki tano kwa siku huku, na kuanzia kesho nadhani itafika milioni moja na nusu kwa siku, sasa kama utaendelea kukaa huko masikini shauri yako,” alisema Friday mwanaume anayewakilisha roho za kikekike.

Baada ya kukata simu ile Friday akamtumia meseji ya namba Adellah aliyevimba kama kifutu kwa hasira. Akawaza ataanzaje kupiga simu na kuongea kiingereza na huyo sijui Madam sijui nani?! Akawaza kumfuata shoga yake jirani anayesoma chuo kikuu.

Basi Friday akiwa amemaliza yake sasa akatabasamu maana lengo lake ni kuwa, Adellah ampigie simu Madam amuelezee, Madam atamuita na kumuulizia kuhusu Naima na yeye atajifanya hajui kwa kuwa alizungumza naye kama Adellah na alimpa vitambulisho halisi, basi hapo alijua Naima atafukuzwa na Adellah ataletwa. Wakati hivyo vitambulisho feki ni yeye mwenyewe Friday ndiye aliyemtengenezea.

“Friday! Kungwi is on!” alisema Naima akiingia chumbani kwa Friday na simu yake akiiseti video chat. Umegundua kuwa Naima kaongea kiingereza eeh! Ndiyo hivyo tena si unajua ukiwa states. Hahaa! Kaanza kukipatapata na yeye. Hapo kamaanisha kungwi yupo kwenye simu.

Wakakaa Friday na macho yake ya kisungura wakapokea maelekezo kutoka kwa Kungwi Ilham.

Wakamaliza na wote wakaenda vyumbani kwao kulala. Naima akifurahia kuwa amepewa mada nzuri ya kuiongelea kesho, na Friday naye alipatiwa yake tena nzuri zaidi, nafsi ikamsuta kuwa kwanini alimwambia Adellah wakati mambo yanaonekana yameanza kwenda vizuri; lakini potelea pote.

Maskini Naima akalala asijue yatakayomkuta. Achecheee!

Madam Alexandrina alikuwa chumbani kwake, akifurahia mapato ya darasa lake ambalo amewaajiri Naima na Friday na kutarajia wanafunzi zaidi na zaidi kuja.

Akaandaa maji ya moto kwenye Jacuzzi na kuvua nguo zake kisha akajidumbukiza humo ndani akihisi maji ya moto yakimkanda mwili wake. Alitamani Friday angekuwa naye hapo ndani usiku huo, lakini aliona Friday atashindwa kufanya kazi vizuri, na hata yeye mwenyewe pia aliona ataweka hisia kazini na mwisho wa siku wataharibu kazi bure.

Hivyo akajiwekea nadhiri kuwa hatakutana kimwili na Friday hadi pengine darasa liishe.

Simu yake iliita wakati tu alipokuwa anatoka kwenye Jacuzzi na kwenda kitandani, akaitazama na kuona ni namba ngeni na ya nchi nyingine. Akaipokea.

“Hallow Madam, I am, Adellah, real Adellah not that one, is fake name is Naima, see go see, tell Friday, that me is real, she no no anything, me iz Kungwi,” ilisikika sauti ya Adellah akiungaunga kiingereza akiongea kwa panic, lakini alieleweka kabisa yaani na ashukuriwe aliyemfundisha huko Bongo.

“what!?” alishangaa Madam, Adellah akarudia vilevile tena kama kameza tepu.

“okey thanks I will call you, (sawa nitakupigia)” alijibu kwa kifupi Madam.

“mi come to America me, please no Naima, is fake me original” alikomaa Adellah, wakati huo Madam Alexandrina akikata simu yake akimpuuza huyo mtu akahisi ni muongo tu.

Lakini hata awe nani huyo Adellah wake aliapa hatamfukuza hata kidogo, maana kwake alikuwa ni dili kwa vile alipendwa na wanafunzi na kwa jinsi alivyofundisha vizuri. Alichotaka Madam Alexandrina ni kwa hao akina Adellah na Friday kusaini tu mikataba aliyowapa upesi ili wamalizane.


Usiku huo Jenny alienda chumbani kwa Naima baada ya Naima kumuita amsaidie kumuelekeza masuala ya mkataba maana hakuwa anafahamu vingereza vilivyoandikwa na mbaya zaidi hakumuamini sana Friday maana yeye ni mbongo mwenzake na ujinga wake alishaujua.

Hivyo akamuita Jenny, maana alisikiaga mtu akijibana kwenye mkataba, ataharibu kila kitu na atakosa hela.

KITUNGUU SAUMU 42

“Hapa mkataba unasema kwamba utalipwa milioni tatu za kitanzania kwa siku, na mahitaji yote ya kibinadamu utapatiwa bure na mwajiri.

“mkataba unasema, utawafundisha watu hadi mia tatu, na kujitolea kwa uwezo wako wote kuwasaidia kwa ushauri,”

“Utafundisha kwa vitendo, hata ikibidi kusex na patna wako mbele ya darasa ili somo lieleweke,” alisoma Jenny, vipengele vikawa vingi zaidi lakini vilivyomgusa Naima ni hivyo vya juu.

Hasa kwenye malipo na idadi ya wanafunzi. Akakumbuka aliambiwa kuwa wanafunzi watakaoongezeka ni hamsini tu, kama wataongezeka hadi miatatu si darasa litakuwa kubwa mno doh! Kwanini wasijadili malipo zaidi kwa kila kundi la watu hamsini? Aliwaza Naima. Lakini pia akaona aombe ushauri kwa Jenny.

“Mh Naima, makubaliano yako ni jambo binafsi,” alisema Jenny akionekana mzito kuzungumzia chochote.

“Nini anachofaidika Madam Alexandrina na hili darasa? Nataka kujua kwani hao wanalipia shilingi ngapi?” aliuliza Naima.

“Sipaswi kukwambia Adellah, lakini ada ya kila mwanafunzi hapa kwa thamani ya shilingi, kila mmoja analipia ada ya mwezi ya shilingi milioni 20,” alisema Jenny na kumuomba Naima asithubutu kusema kama yeye ndiye amemwambia.

Doh! wakati huo Naima akashtuka kusikia mihela yote hiyo akapiga hesabu kwa wanafunzi waliopo pale akaona hapana, mbona Madam anapata hela nyingi zaidi kuliko anazowalipa wao wanaofundisha?

Akaona kabla ya kusaini mkataba huo, amfuate Friday washauriane na ikiwezekana wamwambie Madam Alexandrina aongeze kidogo malipo hata angalau ifike milioni tano kwa siku.

Asubuhi ilipofika tu, Naima akaenda chumbani kwa Friday.

“sikia Friday, hapa tukomae apandishe hadi tano, hizo tatu ni ndogo bado, we unaonaje?” alisema Naima.

“Nini! Wewe umeandikiwa unalipwa milioni tatu? Mbona mimi moja na nusu!” alihamaki Friday.

“oh!” alishtuka Naima na kuona ameharibu bora asingesema chochote kumwambia Friday. Ona kumbe Friday alipewa mkataba wa peke yake, Loh! Basi akaripuka kwa hasira na akimfuata Madam Alexandrina chumbani kwake. Kisa ni kudai kwanini azidiwe mshahara na Naima, kwanza siyo Adellah shenzy! Ngoja akamnyee vya kutosha.

itaendelea

KITUNGUU SAUMU 43

“Madam,what is this!?” alisema kwa kufoka Friday akiwa na mkataba wa Naima na wake mkononi, akionesha kipengele cha malipo.

Lakini Madam Alexandrina akamjibu tu kikawaida: “ooh hiyo ni kutokana na kazi kubwa anayofanya Adellah, labda na wewe uongeze juhudi kidogo, nitakuongezea na kama hautaki! Upo free kwenda nitamchukua mwanaume mwingine.”

Friday akafura midomo ikatatizana akashindwa hata kuongea masikini, kumbe ndiyo kadharaulika hivyo; Loh!

Basi akajizoazoa kujipanga kumnyea Naima maana aliona yule Adellah pengine amechelewa kupiga simu; ile anataka kufungua tu mdomo wake kulikuwa na hodi mlangoni. Madam Alex akaenda kufungua.

Ni Naima! Akamkumbatia na kumbusu kisha amkaribisha ndani. Naima akaingia kwa tahadhari akimtazama Friday aliyesimama akitetemeka kama mashine ya kusaga.

“Friday saini mara moja kisha utupishe,” alisema Madam Alexandrina, Friday nyodo zikimuisha akachukua peni juu ya meza na kusaini kwa kukubali hiyohiyo milioni moja na nusu. Kisha akaondoka akiwa ameshika adabu yake.

Pale mezani akaacha mkataba wa Naima, nadhani Naima aliingia huko kuufuata ule mkataba wake pia na si vinginevyo maana kiingereza hakuwa anakijua sana hivyo alijiepusha kinoma kukaakaa na hao wazungu bila kuwa na Jenny.

Akataka kumuita Jenny, lakini Madam akamkatisha maana mazungumzo hayo ni ya binafsi sana, iwe kwa kiingereza au kigiriki hapo kuelewana lazima.

“Adellah! Mkataba wangu no sign? Wewe Vipi iko tatizo kama Friday?” aliuliza Madam kwa Kiswahili cha kuungaunga.

“hapana Madam, niliona hiki kipengele. Nikaona unaweza kuniongeza hata milioni tano kidogo maana ni watu wengi sana hao mia tatu,” alisema Naima akioneshea lile karatasi na kuchora pembeni alama ya Tano milioni ili mradi iwe rahisi kwa Madam Alexandrina kuelewa.

“sikia, Adellah.. au nikuite Naima?! Nakujua wewe ni nani? Ni feki, so listen, utafanya hivyo au hutaki!” alisema Madam Alexandrina akiweka uso wa mbuzi. Naima kusikia maneno hayo alipigwa na baridi yabisi akajua kimeshanuka hana nyimbo wala singo.

KITUNGUU SAUMU 44

“ina maana Friday amemwambia kuwa yeye ni Adellah feki! Kwanini?” aliwaza Naima akitetema hadi akishindwa kusimama vizuri maana aliona kazi ileee inapepea.

Madam Alexandrina akamsogelea na kumshika bega na kumkabidhi peni.

“Wether You’re Naima or Adellah, I like you and I’m determined to keep you; so do me a favor by signing the contract, or off you go.” ( iwe wewe Naima au Adellah, nakupenda na nimeamua kuendelea na wewe, kwa hiyo lipa fadhila kwa kusaini mkataba, au kwenda!), alisema Madam Alexandrina Naima akaelewa tu bila hata kutafsiriwa maana sura ya Madam ilikuwa ya usiriaz mno.

Akasaini mwenyewe na kuondoka ameloa.

Lakini alishaona kuwa Friday ni nyoka, nyoko, nyuku,nyiki na yote huko mbele, kwa maana hafai. Akamfuata kwa kumuogopa maana alijua aina hiyo ya wanaume ukiharibu ukuta wao wanamaliza hadi msingi wenyewe.

“sikia Friday, mimi sikujua kama Madam ameweka mishahara tofauti, cha msingi tupige kazi ataongeza tu, halafu kama hela mimi nitakuongezea laki tano kwenye kila mshahara wangu,” alisema Naima akimpoza moyo Friday aliyejiinamia ndani kabisa kwa kisirani.

“we rahisi tu kuongea hivyo kwa sababu una mshahara mkubwa si ndiyo? acha unafki!?” alilalamika Friday.

“Friday, acha ujinga, mbona umeenda kumwambia Madam kuwa mimi siyo Adellah ni Naima, na nimekaa kimya! Wewe ndiyo uache unafki, nimejitolea kukupa laki tano yangu kila mshahara kama hutaki basi?”

“we mimi mbona sijamwambia kama wewe si Adellah!?” alikana Friday.

“sasa kama si wewe ni nani?” alihamaki Naima.

“aisee atakuwa ni Adellah mwenyewe! Duh!” aliwaza Friday kimoyomoyo.

ITAENDELEA

Kitunguu Saumu Sehemu ya Tano

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment