CHOMBEZO

Ep 01: Mrembo Mcharuko

SIMULIZI Mrembo Mcharuko
Mrembo Mcharuko Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA: LATIFA

*********************************************************************************

Chombezo: Mrembo Mcharuko

Sehemu ya Kwanza (1)

“Hodiiii fundi, shikamoo! Sketi yangu hii ya shule nataka huipunguze maana ni ndefu sana”

Nilifika tu kwa fundi cherehani nikaanza kuongea bila kumpa nafasi.

“Duh we binti sijui nikujibu nini”

Alisema uyo fundi akiniangalia.

“Sio lazima kujibu wewe ikate apo ishone mie nakungoja sababu kesho ni shule naenda”

Nilimwambia.

“Lakini hii sketi mbona ipo vizuri ndefu ya heshima inafaa”

Aliongea akiangalia.

“Sketi ndefu kama naenda msikitini kuswali akuu sitaki we ikate ifike juu ya magoti”

“Mtumee we mtoto unalaana eeh”

“We babu usitafute kichambo nakwambia kama kazi uwezi sema”

Nilichukia uyu fundi anamaneno mengi.

Nikachukua nguo yangu nakuondoka nikaenda kwa fundi mwengine uyo hakuuliza sana akanipunguzia Sketi ikawa fupi nilifurahi nikarudi nyumbani sasa, njiani nikakutana na shogayangu ninaesoma nae Nasra.

“Hee mambo”

“Poa shost unatoka wapi?”

Aliniuliza nikamwambia nimetoka kupunguza Sketi yangu

“Bora mwezangu maana ilizidi lefu kama kuimba kwaya loh”

Nasra akanisapoti

“Umeona eeh shogayangu adi nilikuwa natia aibu”

Basi tukajazana ujinga apo kisha tukaagana yeye alikuwa anaenda dukani namimi nikarudi nyumbani.

Wazazi wote walitoka nyumbani nikabaki mimi na kakayangu Gedion yeye yupo secondary kidato cha pili namimi nipo darasa la saba.

Tofauti mie mcharuko balaa ila kakangu mpole adi wazazi wanampenda mimi sina ata anipendae kutwa napigwa tu kwa umapepe wangu.

Baba ni mwanajeshi alafu mama yeye ni daktari muhimbili.

Familia yetu kidogo inajiweza, kama kakayangu Gedion anasoma shule ya kulipia na akili anazo ila mimi nilipelekwa shule ya serikali.

“Wewe Lisa unatoka wapi?”

Nilipoingia tu kaka Gedion akaniuliza.

“Aah umekuwa mumewangu adi uniulize ebu nipishe mie”

Nilimwambia nikampita nakuingia chumbani kwangu, ananijua akili zangu ovyo hakuniuliza tena, baada ya muda mfupi baba alirudi Gedion akatoka kumpokea mimi nilimsikia lakini sikutoka nikabaki chumbani maana mimi na baba haziivi kabisa nikikaa karibu nae lazima anipige kutokana na ujeuri wangu.

Ghafla nikasikia mlango wangu unagongwa,

Gedion akaingia

“Unaitwa na baba uko”

“Anataka nini mwambie nimelala”

Mara nikamsikia baba anaongea mlangoni

“We Lisa ivi unajua kesho shule, nenda jikoni kasaidie kupika uwahi kulala”

Alisema nikaanza kujifanya naumwa nikajikamua machozi ya uongo sipendi kupika kilasiku nakimbia jikoni.

“Baba tumbo linauma uwiiii mamaaa weeee nakufaaaa”

Nilipiga kelele nikigalagala kitandani adi wakashtuka, Mara mama nae akarudi kelele zangu alizisikia akaja mbio chumbani nakuuliza kunanini kwakuwa yeye Daktari anajua akawaambia watoke nje anipime nini tatizo.

“Upo kwa siku zako kwani?”

Aliniuliza nikakubali wakati sipo akanambia ndo mana naumwa nisijali nitapona kisha akatoka nakuelekea chumbani akaniletea vidonge nimeze kupunguza maumivu nikapokea alipotoka nikavitupa uvunguni mwa kitanda.

Basi chakula kiliiva tukala pamoja kisha nikaingia ndani kulala.


Asubuh kulikucha nikaamka nakujiandaa kuelekea shule, nilipotoka wote walinishangaa Sketi ya shule imekuwa fupi sana.

“Hee we mtoto”

Mama alisema akitoa macho mi ata sikumjali, baba nae akapigwa na butwaa

“Ivi we Mtoto nikufanyaje mimi? Lisa utanipa kesi nitakukata shingo wewe”

Baba alipandwa na hasira ila nilimzoea ata sikuogopa kupigwa nilishazoea nakuona kawaida tu.

“Alafu nina wasiwasi we mwanamke uyu mtoto ulimuiba hospital sio mwanangu”

Baba alisema nakumgeukia mama, niliangua kicheko kwa sauti,

“Heheh haloooo”

Baba alianza kunisogelea anipige lakini mama akamzuia

“Muda wa kazi huu mumewangu ebu wahi kazini mwanao mzoee tu utamuumiza bure mtu mwenyewe haelewi”

“Unamtetea uyu chizi ipo siku nitamuua mimi”

Baba alitoka uku anafoka akapanda gari na kuondoka na kakayangu mie anaenipeleka shule mama basi tukatoka nje tukaingia kwenye gari akuniongelesha kitu akanifikisha shuleni nakuniacha.

Mamayangu mpole sana mwenye huruma lakini mtoto aliemzaa sasa majanga.

Basi shuleni kila mwanafunzi ananiangalia mimi na kimini changu sababu nimejaaliwa shepu ya maana makalio makubwa alafu nina miguu minene ya bia basi Sketi ilinipendeza adi raha.

“Apana chezea Lisa wowowo yani unatuua tu wenzio”

Mashoga zangu walianza kunisifia nimependeza.

Darasani hakukukalika wavulana wakaanza kunisumbua.

“Lisa mapumziko nitafute nina zawadi yako”

Alisema bakari

“Akaa unikome usinipake shombo mie zawadi kampe bibi yako”

Japokuwa nilikuwa mcharuko lakini sikujihusisha na mapenzi shuleni.

Basi ghafla mwalimu mkuu akaingia darasani alikuwa anafundisha hisabati akaanza kuandika akielezea mi ata sikumuelewa analofundisha ndo kwanza nikainamia dawati nakulala.

“Pumbavu nani alielala uko nyuma aje mbele apa”

Mwalimu alifoka, nilishamzoea baba mkali anasauti kubwa kama anaongea kwenye spika ata sikuogopa nikazidi kulala tu.

Wanafunzi wenzangu wakageuka kuniangalia uku wakicheka maana shule yetu wengi wamevulugwa, wapo wavulana wanamademu zaidi ya wawili, wasichana pia wanamabwana adi walimu, kuna wavuta bangi humo wezi wapo yani tafrani ata walimu hatuwaogopi.

Basi mwalimu mkuu akazidi kufoka nikainuka uku nimejishika tumbo nakusogea mbele.

“Mwalimu naumwa”

Nilisema nikiwa mnyonge uku nikijikamua machozi.

“Wewe mwanafunzi hii Sketi mbona fupi mno”

Aliongea akinitolea macho

“Mwalimu unanionea mbona wengi wanavaa sio mimi tu”

Nilijitetea lakini ni kweli wasichana wengi wanavaa nguo fupi ila tatizo mimi umbo langu kubwa tofauti na wengine wao maumbo yao madogo

“Unajitetea poyoyo wee nenda ofisini nikukute uko”

Alisema mwalimu nikageuka kuelekea ofisini kwake.

Aliendelea kufundisha alipomaliza akaja ofisini nakunikuta nimekaa mapaja yote nje na yalivyonona nikamuona ametoa macho anayaangalia

“Ivi unaitwa nani wewe binti?”

Aliniuliza

“Naitwa Lisa Charles”

“Unajina zuri kama wewe mwenyewe! Unajua Lisa unaweza kuponza mwanaume akafungwa kwaajiri yako?”

Mwalimu aliongea kwa upole adi nikashangaa wakati ni mkali balaa akainuka nakufunga mlango! mapigo ya moyo yalienda mbio Mwalimu mkuu akanisogelea karibu.

Nilianza kujuta kwanini nilipunguza sketi yangu nakuwa fupi iliyoniacha wazi, basi nikaanza kuishusha chini lakini haikusaidia. Mwalimu akasogea nakusimama mbele yangu akiniangalia.

“Lisa ukitoka shule naomba unione sawa”

Alisema nikamuitikia tu basi akaniruhusu kutoka.

Nikashukuru mungu maana sikutegemea kama ningeachwa salama, nilirudi darasani nakumkuta mwalimu wa sayansi anafundisha, uyu mwalimu kijana mdogo tu ni kipenzi cha wanafunzi micharuko maana akijua unademu anakupongeza sana kuna mmoja anaitwa saidi uyo anamademu watatu shuleni mwalimu alimfuma amekumbatiana nje ya darasa alimpongeza nakumpa pesa.

“Huo ndo ulijari sasa”

Alimwambia akicheka nakuwaacha apo.

Somo la sayansi linahusu mengi wanaelezea mwili wa binadamu nayeye alifundisha matusi matupu yani wanafunzi ndio wanampenda balaa.

“Mrembo wa shule karibu”

Aliniambia akiniangalia nilikuwa nimenuna apo yaliyonikuta kwa mwalimu mkuu sikusahau.

“Mbona umenuna? Yani umeamua utumalize kabisa na kimini chako”

Aliongea mwalimu akinitazama kwa matamanio makubwa.

Darasa zima walicheka wakinitazama, sikutaka kuongea nikarudi kwenye dawati nakukaa kimya.

Mwalimu alifundisha adi alipomaliza akasema

“Lisa nifate ofisini”

Nilijikuta nanuna zaidi adi nilijuta

“Sivai tena hii sketi mimi”

Niisema uku nikitamani kulia, mwalimu alitoka namimi nikaanza kujishauri niende au nisiende wezangu wakanza kunitania

“Lisa leo unamajanga kuitwa na walimu ofisini mbona utakoma”

“Mwezangu iko kimini chake kimezua tafrani leo”

Mashoga zangu Tina na Nasra walinichokoza

Maneno yao yalinikera nikatoka nikiwa nimenuna sana.

Nilifika ofisini nakumkuta mwalimu amekaa alinitazama juu adi chini uku akitabasamu.

Nikajisikia aibu niliinamisha kichwa chini sikutaka kumuangalia usoni.

“Lisa mtoto mzuri mbona muoga sana ila umependeza leo”

Alisema akionekana amenitamani, nilitetemeka uku jasho likinitoka mwilini.

Ghafla mwalimu Deo akanisogelea nilipo nakunishika.

“Mwalimu usiniguse”

Nilimwambia lakini akusikia akazidi kushika mapaja yangu nilitetemeka moyo ukienda mbio sana.

Nilijikuta namsukumiza kisha natoka mbio mule ofisini adi darasani nikihema sana. Sikutaka kubaki tena shule nilichofanya nikabeba begi langu nakutoka kurudi nyumbani.

Nilikuwa na pesa nikapanda bodaboda iliyoniwahisha nyumbani kwetu nilishuka nakuingia ndani nikashangaa namuona kaka Gedion amekaa sebuleni anatizama tv

“Wow mrembo mcharuko uyo kulikoni leo mapema?”

Aliniuliza sikumjibu nikampita tu nakuingia chumbani kwangu nikavua nguo za shule nakuvaa gauni nikatoka nje nimenuna balaa ata kakayangu aliponiona akuniuliza kitu alinitazama tu.

Mkononi nilishika ile sketi ya shule nikaingia jikoni nakumkuta dada wa kazi sikumsalimia wala hakuniuliza anaujua mcharuko wangu sichelewi kumchamba basi nikatafuta kibiriti nakutoka nje ya nyumba nikaiweka nguo chini nakuwasha moto, moshi mwingi uliingia ndani nakufanya kaka Gedion aje aone nachoma nini

“Haaa wee Lisa unachoma sketi ya shule?”

Alisema kwa mshangao sikumjibu kitu.

“Si naongea nawewe yani baba katoa pesa zake wewe unachoma nguo kweli”

Alizidi kunipandisha hasira zangu nikatoa msonyo wa nguvu adi alibaki kanitolea macho

“Sikia wewe kinyago usinizoee tena niache kama nilivyo”

Nilimwambia

“Yani Lisa mimi kinyago sawa tu”

Aliongea akitoka nakuingia ndani akachukua simu nakumpigia baba akamwambia nimechoma sketi moto.

Basi nilipomaliza nikaingia chumbani kwangu nakujifungia mlango sikutaka kuongea na mtu yeyote.

Nilipitiwa na usingizi adi niliposikia mlango unagongwa nikainuka kiuvivu nakuufungua nikamuona mama kumbe ilikuwa jioni imefika.

“Shikamoo mama”

Nikamsalimia

“Marahaba mwanangu, unaumwa au na umekula leo?”

“Apana uchovu tu wala sijala”

“Aya pole oga basi upate nguvu uje mezani nakuandalia chakula”

Nikamuitikia alitoka nikaingia kuoga nilipomaliza nikatoka kwenda mezani nilikuta chakula tayari nikaanza kula adi nilipotosheka.

Mara kaka Gedion akaja

“Mama uyu mwanao leo kachoma sketi ya shule moto”

Alinichongea nikamkata jicho baya.

“Wee Lisa kwaninii umechoma moto Sketi?”

Mama aliniuliiza

“Fupi imenipa usumbufu”

“Nani alikutuma ukate sasa? We sindo ulipeleka kwa fundi lakini”

“Mama bwana kaninunulie sketi ndefu”

Niliisema Gedion akacheka sana

“Mrembo mcharuko kapatikana anataka sketi ndefu”

Alisema akiinuka alinikera,

Basi nilimaliza kula nikaingia chumbani nakupiga pasi nguo zangu za shule nilichukua sketi yangu ya mwanzo ndefu kidogo ila haifiki chini kabisa.

Nikaziandaa nakulala zangu, siku iyo baba aliichelewa kurudi akanikuta nimelala.

Hatimae Asubuh ilifika wakashangaa nimevaa sketii ya mwanzo

“Wewe mjinga umenikera kuchoma moto nguo ya shule yani nakungojea maliza ilo la saba lako nakutafutia mwanaume akuoe sitaki kabisa kukuona apa”

Baba alifoka kwa hasira

“Mumewangu lakini maneno gani unamwambia mtoto uyo mume atampa nini uyu bado mdogo”

Mama alinitetea

“Lisa ni mtu mzima hana utoto wowote na ataolewa tu pumbavu! Gedion twende”

Alimaliza kufoka akamuita kaka nakupanda gari wakaondoka. Mama nae akanishika mkono tukapanda gari letu akanipeleka shuleni.

“Leo jioni nitakuletea Sketi mpya mwanangu”

Aliniambia kwa upole

“Sawa mama nashukuru”

Namimi nikajifanya mwema tena

“Lisa mwanangu jitahidi kusoma ufauru nikupeleke shule nzuri yakulipia ukiferi ndoa inakuhusu si umemsikia babayako leo eeeh?”

Maneno yake yaliniogopesha sana nikajikuta nakuwa mnyonge nikaitikia tu.

Basi nilifikishwa shuleni akaniacha nakuondoka ile naingia tu darasani wezangu wote macho kwangu adi nikaogopa imekuwaje ikabidi niwaulize

“Mwalimu mkuu anakutafuta jana ukaondoka bila kuaga hee utakoma leo”

Alisema mwanahawa shogayangu uyo nae kabla sijakaa sawa naona mwalimu amefika darasani akaita

“Lisa Charles nifate ofisini”

Akasema nakutoka nikaangua kilio kikubwa darasa zima wakacheka

Nilijiisi kama nina mikosi vile, basi nikaacha begi langu nakutoka kuelekea uko ofisini kwa mwalimu.

“Shikamoo mwalimu”

Nilimsalimia nilipofika

“Marahaba”

Alijibu uku akiniangalia juu adi chini, nikamuona anatabasamu nakusema

“Afadhari leo umevaa kiheshima ile nguo jana Mmmh haikumuacha wanaume salama”

Alisema nikajikuta natamani kucheka ila nikajizuia.

“Alafu jana kwanini uliondoka bila kuja kuniaga wakati nilikwambia ukitoka unione”

Alisema nikaona iki ndo alichoniitia.

“Mwalimu jana tumbo lilikuwa linauma sana”

Basi nilijibu kiunyonge ili aniamini.

“Oh pole sana mpenzi wangu”

Nilitoa macho ayo ili baba kuniita mpenzi nilishangaa.

Mara nikamuona kaingiza mkono mfukoni nakutoa wallet yake akahesabu noti tano za elfu kumi nakunipatia.

“Za nini izo mwalimu?”

Niliuliza kabla yakupokea isiwe ananipa ili nilale nae namimi sipo tayari.

“Zako Mrembo zitakusaidia chukua”

Alisema

“Sawa asante”

Nikazopokea nakuweka kwenye mfuko wa sketi yangu.

“Alafu mwalimu mwenzio baba kasema nikiferi ataniozesha naomba niende darasani nikajisomee”

Niliona ananichelewesha tu nikamwambia ivyo kwanza alicheka sana.

“Yani we binti mdogo ivyo kuolewa si vichekesho uyo baba yako anachekesha sana ila usijali nitakusaidia utafaulu sawa”

Basi nilifurahi nikamuitikia akaniruhusu nirudi darasani.

“Enhee shogayangu umekuwaje umepigwa au?”

Kufika tu marafiki zangu wakaniuliza.

“Akuuu mnipishe nina mwili wa Mapenzi sina mwili wakupigwa mie”

Niliwajibu wakaangua kicheko chakishambenga

“Hehehhee halooooooo”

Nikawatolea pesa nakuwaonyesha wakashangaa

“Kwaiyo mwalimu bwanako?”

Sauda akaniuliza yani nina mashoga kibao.

“Ilo jibu pigia mstari”

Nilimjibu wakazidi kucheka

“Chezea zigo wee mwalimu kapagawa nalo”

“Ila mwezangu unabahati mie mwalimu sudi bahiri ata pesa anipi akitoa nyingi elfu kumi”

Alisema Naomi, mara mwanahawa akadakia

“Mwezangu nimepata bwana kondakta wewe ananihonga usipime”

Basi tukaanza kuadithiana ujinga apo kila mtu akimtaja bwanake wengine wanao zaidi ya watano.

Mara mwalimu akaingia wa kike uyo anaitwa Samia akaanza kufundisha apo adi alipomaliza akatoka.

Walingia walimu wengine wakafundisha adi muda wakutoka shule ukafika tukaondoka.

Shule yetu haipo mbali sana na nyumbani napandaga bodaboda kurudi sipendi kutembea kwa miguu kuna umbali kiasi chake.

Basi nilifika nyumbani nikavua nguo za shule nakuvaa kanga nikaelekea jikoni.

“Chakula kipo wapi Leah?”

Nilimuuliza dada wa kazi

“Lisa mdogo angu ata salamu jamani”

Alisema kiunyonge mwenyewe.

“Yani mijitu iliyotoka kijijini utaijua tu wewe ulimuona nani anasalimiana mjini? Salamu vijinini uko apa mjini akuna salamu chakula kipo wapi nile mie?”

Alikoma mwenyewe kuniongelesha akabaki kimya, nikachukua chakula nikala nilipomaliza nikaenda chumbani kwangu nikabeba begi langu adi chumbani kwa kaka Gedion nikafungua mlango nakuingia nilimkuta kalala kitandani uku laptop ipo mbele anatizama movie.

“Mambo”

Nikamwambia

“Poa ndo nini unaingia bila hodi?”

“Gedion nawewe usharithi akili za babayako”

“Lisa nitakupasua kwanza umefata nini chumbani kwangu?”

“Bwana nifundishe kusoma ujue mitihani inakaribia nikiferi baba kasema ananiozesha”

Nilimwambia Gedion alicheka sana

“Bora uolewe tu”

Alijibu nikamtizama tu,

Basi nikatoa madaftari akaanza kunifundisha hesabu mimi mwenyewe kichwa panzi sielewi ata moja ilimradi tu.

Mara akainuka nakwenda chooni ni humo humo ndani, simu yake ikaita kakayangu kanunuliwa simu na laptop mie ndo sina chochote ila mama alinihaidi ataninunulia nikifauru kuingia secondary.

Basi nikapokea ile simu jina iliandikwa Clara

“Haloo my love”

Alisema nikashtuka

“Wewe nani unamuita kakayangu ivyo ivyo?”

Nikamuuliza

“Ooh mie Clara ni girlfriend wa Gedion”

Alisema

“Mfyuuuuuu sura imekukomaa kama ndimu mbovu, kakayangu mdogo anasoma umejitongoza unataka kumuharibu nyau wewe tena ukome usimzoee”

Nikiwa namchamba Mara kaka akatoka bafuni nakushangaa naongea na simu yake akanipokonya.

“Haloo sorry baby mdogo wangu uyu kichaa….nilikuwa toilet sorry mamy”

Basi akaongea nae akakata simu nakunitizama kwa hasira Alainogelea akiwa amevimba balaa

“Nani kakutuma upokee simu yangu unamtukana wifi yako kwanini?”

Alianza kufoka

“Ata siamini yani Gedion nawewe unademu kweli dunia imeisha”

Nilimwambia

“Kwaiyo unanidharau mimi sio rijali au?”

“Wewe bado mdogo baba anakutetea mpole kumbe bora mie mcharuko ila sina mwanaume”

Nilwambia akazidi kupandwa hasira nakunifata, niliogopa nikataka kukimbilia mlangoni maana niliisi atanipiga apo nilikuwa nimekaa kitandani akaniwahi nakunipiga kofi nikadondoka kitandani bahati mbaya kanga ikafunguka na ndani sikuvaa kitu zaidi ya chupi tu.

“Haaa Lisa”

Alipigwa mshangao kuona mapaja yangu makubwa hasira zote zilimuisha nikamuona akanikodolea macho uku nina maumivu kibao alichonipiga kiliniingia sana nikaanza kulia akasogea karibu

“Pole Lisa nisamehe kukupiga”

Alianza kuomba msamaha

“Lakini kwanini unakuja kwangu na kanga moja tu unazani mimi sina hisia au alafu jione ulivyo Lisa lakini mipaja yote hii na ilo zigo lako daah?”

Aliongea akinitolea macho ya mahaba kabisa nikamuona anaweka mkono nakushika mapaja yangu nilipomtizama sehemu zake zimeinuka niliogopa sana

“Gedion mimi dadayako lakini”

Nikajitetea lakini akunisikiliza akainama naku

Akainama nakulamba mapaja yangu nilishtuka nikaruka nakumsukumiza akadondokea kitandani nikavaa kanga yangu uku nikimtukana sana

“Sasa unanitukana nini unaniona mi sio rijali au adi uje na kanga moja uku?”

Akasema

“Mjinga wewe nitamwambia baba umetaka kunibaka”

“Namimi nitamwambia ulikuja na nguo ya ndani tu chumbani kwangu kwanza toka nje sitaki kukuona”

Basi nikatoka nakuelekea chumbani kwangu kulala.

Yani mimi mvivu kufanya kazi muda wote nalala tu ata kuosha kijiko sijui.

Basi nikalala adi jioni mama aliporudi akaja kugonga mlango nikaenda kufungua alafu kanga nilisahau kuvaa nikainuka mwenyewe tu.

Mama aliponiona akashtuka

“Wewe Lisa ndo nini unakaa mtupu bila nguo je angekuwa ni babayako”

Alisema akinishangaa

“Mama bwana nimeisahau kanga kitandani”

Niliongea apo nina usingizi bado.

“Lisa wewe utakuwa lini jamani loh”

Aliongea mama nakuondoka nikafunga mlango nakuendelea kulala.

Saa mbili usiku nikashtuka mlango unagongwa tena nikainuka kwenda kufungua kumbe ni kaka Gedion.

“Unaitwa ukale chakula tayari”

Alisema akiwa mlangoni akashangaa aliponiona na nguo ya ndani bado apo alikuwa mlangoni akaingia nakufunga mlango.

“Sasa umefata nini ndani si ushasema nimekusikia”

Nilimwambia

“Yani Lisa bado ujavaa nguo tu?”

Akaniuliza

“Si chumbani kwangu nipo inakuhusu nini?”

Nikajifunga kanga nakukaa kitandani.

“Ivi Lisa kweli huna boyfriend wewe?”

Aliniuliza akinitazama

“Sina bwana adi nimalize shule”

“Ngoja nikutafutie rafiki yangu mmoja handsome uwe nae sawa”

Alinambia kaka

“Alafu Gedion sipendi ujinga wako ujue”

“Sasa upendi nini mbona mi nina mademu watatu”

Hee nilishtuka sikuamini yani kakangu mpole uyo adi wazazi wanampenda kumbe ni muhuni balaa nilimtazama sikumpatia jibu mwisho nikainuka nakumwambia twende tukale.

“Vaa nguo basi baba yupo uko”

“Bwana kwani nipo uchi si nimejifunga kanga atajua ndani nimevaa nini ebu twende”

Basi tukatoka adi sebuleni nikawasalimia nakukaa tukaanza kula.

Tulipomaliza kila mtu akaingia chumbani kwake kulala.

Asubuhi kulikucha nikajiandaa kwenda shule.

Siku zilizidi kusonga adi tukafika mwezi wa tisa tukafanya mitihani yakumaliza darasa la saba nilishukuru sana maana nilikuwa sipendi kuvaa uniform za shule.


Kwasasa nikawa nipo tu nyumbani nikingojea majibu.

“Lisa mwanangu nataka nikupeleke ukasomee pre form one”

Mama alinambia nilinuna sipendi shule nitaenda kuzurura saa ngapi sasa.

“Mama jamani sasa kama nitaferi je?”

Nikamuuliza

“Utafauru mwanangu mungu atakusaidia sawa eeh”

Nilizidi kuchukia nikamkubalia tu.

Basi kesho yake akanipeleka uko shule ni buguruni na kwetu ni ubungo external.

Nikaanza masomo rasmi nilishukuru atuvai nguo za shule zaidi t-shirt yao iloandikwa jina chini unavaa nguo yoyote mimi nikawa navaa suluali maana iyo ndo nguo ya heshima kwangu na baba alinikataza kuvaa vimini.

Siku moja mwalimu mmoja anaefundisha hisabati akaniita muda wakuondoka huo nikaenda ofisini kwake.

“Ujambo Lisa?”

Alinisalimia

“Sijambo tu”

Namimi jeuri simwamkii mtu.

“Ivi Lisa unaboyfriend?”

Akauliza uyo mwalimu

“Mi bado nasoma boyfriend wa nini?”

Nikamjibu nikiwa nimechukia

“Waoo vizuri sana, ila nimekupenda sana natamani niwe mpenzi wako”

Aliongea uyo mwalimu ambae ni mkubwa hakuwa kijana alinichefua

“Mfyuuuu lione babu zima ovyo ujana wako ule na nani uzee uniletee mie ukinifia kifuani je unataka kunipa kesi tena unikome usinizoe”

Nilimchamba uyo mwalimu adi aliona aibu

“Basi Lisa basi yaishe”

“Siku nyingine ukirudia nakujazia watu apa”

Nilimwambia nikainuka nakuondoka kurudi nyumbani.

Basi nikafika nakuweka begi ndani nikaenda mezani kula.

Mara nikasikia mdundiko nje unapita matarumbeta yanarindima wazimu ukanipanda nikaingia chumbani kuvua ile suluali nikavaa taiti fupi na kanga juu nikatoka mbio getini nikapishana na baba alierudi kazini sikumjali nikaongeza mbio adi kwenye mdundiko nikaingia kati nakuanza kukata mauno mara nikawaona mashoga zangu husna na mwaija wee nilifurahi

“Shogayangu umekuja nawewe babayako ajakukataza?”

Aliuliza Husna

“Anikome babu yule akamkataze mkewe asinichunge mie sio n’gombe”

Niliwajibu apo tu ndo walinipenda kwa mcharuko wangu basi nikaendelea kuzungusha kiuno kama sina akili nzuri kanga ikadondoka sikujali adi chini nikalala nakata mauno ya nguvu

“Haloooo apana chezea Lisa zigo weweeeee

Watu wakaanza kushangiria mie ndo bichwa linakuwa kubwa kama tv ya chogo nazidisha miuno ata harusi sijui ya nani, nilicheza wee adi nikachoka mdundiko ulienda mbali toka ubungo external adi ubungo maziwa mbali karibu na stand nilichoka hoi nikaamua nirudi apo kanga sina nipo na tait fupi na umbo langu balaa sasa akili zikanijia nikakumbuka getini nilipishana na baba na tangu nitoke nyumbani saa kumi sasa ivi saa kumi na mbili giza limeanza kuingia kibaya zaidi kanga sijui nimetupa wapi

“Mamaaa weee leo baba atanipika supu mimi”

Nilisema nikiisi miguu haina nguvu nikakaa chini mara nikasikia naitwa kugeuka ni

Mwaija yule shogayangu akanisogelea,

“We Lisa umecheza adi kanga imevuka huna habari hii apa niliokota mie nikaishika”

Alisema nilimshukuru sana

“Mwezangu sijui ningeendaje nyumbani asante mwaya”

Basi akanipatia tatizo giza lishaingia kurudi mbali nikamuomba kama anabuku aniazime nitamlia nipande bodaboda

“Ata sikuazimi chukua tu shogayangu”

Nilimshukuru zaidi tukaagana nikasogea mbele kidogo kijiweni, nikapanda bodaboda moja ikanipeleka karibu na nyumbani nikashuka nakutembea kidogo nikaingia ndani apo moyo unajidunda balaa najua kipigo leo lazima.

Basi ile kuingia tu nikakutana na baba sebuleni kavimba balaa alinisogelea nakuanza kunitandika na mkanda wake wa kijeshi nilipiga kelele nililia adi mama akatokea kunigombelezea.

“Utaua baba Lisa msamehe mtoto”

“Acha afe shenzi uyu mtoto asikii kama kalambishwa mavi sijui ameniona narudi kanipita mbio kaenda kucheza ngoma muone ananuka jasho balaa apo Lisa utanipa kesi nakwambia nitakuua wewe”

Nilitoka mbio nikaingia chumbani nakujifungia nalia uku baba alizidi kufoka tu Mama akamtuliza nakuingia chumbani

Nililia adi nilipotosheka nikaenda kuoga nilipomaliza nilisikia njaa inauma sana, Mara Ghafla mlango wangu ukagongwa

“Nani wewe?”

Niliuliza kabla sijaenda kufungua.

“Mimi Leah”

Nikamfungulia namuona kabeba sahani ya chakula.

“Lisa mdogo wangu pole chakula iki kula mwaya”

Mwenyewe alikuwa anahuruma namimi nikamshukuru nakuanza kula uku amekaa ananitizama.

“Wewe huendi kulala kwani?”

Nikamuuliza

“Nakungoja wewe umalize nibebe vyombo”

Nikamuangalia sikumjibu nilikula adi nilipomaliza nikampa vyombo.

“Lakini mdogo angu punguza mcharuko ona kilasiku baba anakupiga”

Akajifanya ananipa ushauri

“Bibi wee koma ushauri pelaka Angaza tafadhari sijakuita apa kunipa chakula isiwe nongwa nitakitapika chote uondoke nacho unajifanya mwema ngoja ugeuzwe msukule”

Nilimpa maneno mabaya adi alikoma mara mama nae akaingia chumbani.

“Nimekusikia mtoto unamaneno machafu wewe lione kama zimwi”

Mama nae yumo kwa maneno nikabaki namtizama sijui nimjibu nini

“Wewe Leah ungeliiacha lilale na njaa ili halina shukrani kabisa”

Mama aliongea uyo adi basi Leah akatoka zake nakumuacha

“Alafu mi naisi kweli mliiiba hospital si mtoto wenu mimi maana hamnipendi kabisa naishi kama nipo utumwani na nitajiua mbaki wenyewe”

Nilimwambia mama akashtuka na maneno yangu

“Lisa mimi ndo mamayako mzazi niliekuweka tumboni miezi tisa nakukuzaa kwa uchungu unaanzaje kusema nimekuiba si tunakuchukia tabia zako mbaya”

Mama alisema

“Tabia mbaya nimejikojolea kitandani?”

Nilishtukia kofi la uso nimepigwa,mama akatoka nje nakuniacha nikafunga mlango nakulala.

Asubuh ilifika sikuamka adi mchana nikaunganisha kulala iyo siku ilikuwa wikiendi wote wapo nyumbani wakashangaa kwanini nimelala sana wakaja kugonga mlango ndo nikashtuka saa nane mchana mwili wote unauma kwa kipigo cha jana.

Mama ndo alikuja kuniamsha nakuniuliza najisikiaje nilipomambia naumwa akaniletea dawa yakupunguza maumivu ila nikaenda kula kwanza.


Siku sikazidi kusonga adi majibu yalipotoka nikaonekana nimefaulu hakuna alieamini kama Lisa mie nimefaulu kuingia secondary.

Tatizo likaja nimechaguliwa shule mbali tegeta uko si nilichukia sana

“Boea ningeferi tu ndo nini kupelekwa kijinini uko?”

“Lazima ukasome uko uko kwanza sijui kama ujawapa rushwa wakufaulishe”

Baba akaingilia

“Mi nina wazo mumewangu tumuhamishe Lisa shule anayosoma kakayake”

Mama akasema nakumfanya baba achukie sana.

“Unasemaje? Yani nitoe pesa zangu kwaajiri ya uyu kichaa nina wazimu au?”

Alifoka kwa hasira nakuinuka akaondoka nakutuacha.

“Ngoja nitakufanyia mpango nikupeleke ata Yusuph makamba ukasome apo”

Alisema Mama iyo shule ipo karibu na kwetu basi nikamkubalia, nikiwa pekeyangu nililaani kufauru nilitamani nifeli tu basi nilichukia.

Hatimae siku yakuanza masomo ikafika Mama akafatilia uhamisho adi yalipokamilika nikapelekwa shuleni kuanza.

Basi siku ya kwanza tu kufika nikapigana na mwezangu ambae alikaa kwenye kiti changu nilimdunda adi akatoka damu puani alikuwa msichana anaitwa mwamtumu.

Basi tangu siku iyo shule nzima nikajulikana Lisa ni nani nikapata mashoga wengi micharuko wenzangu adi nyumbani wakawa wanakuja tunapiga story mwisho wanaondoka.

Kaka Gedion akanichongea kwa baba ambae alipogundua naleta marafiki zangu akanipiga stop kuwaleta nyumbani alinikera.

“Alafu uyu atakuwa si babayangu sio bure”

Nilijisemea nikapanga nimuulize mama vizuri ambapo aliporudi tu nikamuwahi bila salamu

“Mama kanionyeshe babayangu mzazi alipo”

Nilimwambia akashtuka kwanza nakusema

“Babayako wakutokea wapi tena na uyu unaeishi nae apa ninani?

“Uyu si babayangu namtaka babangu wa kweli nasema”

Nilichachamaa nikimlazimisha anionyeshe babayangu

“Wewe mpuuzi usinisumbue mimi nimechoka”

Mama alisema akanipuuza nakuondoka.

Asubuhi ilifika kama kawaida nikajiandaa kuelekea shuleni sikuacha mcharuko wangu nilizidisha adi nilipofika kidato cha pili siku moja tunatoka shule rafiki zangu wawili wakanifuata

“Shosti leo ijumaa twende zetu coco beach wikiendi ishaanza ivyo”

Alisema Salma na mwezake Diana akadakia

“Ndio twende mwezangu tukaogelee”

Mi niliogopa tutachelewa kurudi na baba namjua atanipa kipigo nikawakatalia

“Twende Lisa atuchelewi bwana wendo mrembo wetu tunakutegemea”

Alinishawishi Diana basi nikakubali tukaondoka nakupanda gari la msasani, tulishuka macho tukachukua bodaboda adi coco.

Ilikuwa bado mapema shule tulitoka saa sita hakukuwa na foreni saa saba na nusu tukawa coco tayari.

Basi wezangu walikuwa na pesa tukakodisha nguo zakuogelea apo kila mmoja akachagua yake tukavaa nakuvua nguo za shule tukaogelea adi tulipochoka tukaanza kukimbizana kwenye michanga tulifurahi siku iyo adi saa kumi jioni tukaanza kujiandaa kuondoka. Mara nikasikia naitwa na mwanaume nikageuka nimsikilize ni mbaba mkubwa

“Ujambo Mrembo?”

“Sijambo shikamoo”

“Asante”

Alijibu uku anatabasamu alinichefua sana nikataka nianze kumchamba maana sicheleweshangi gafla wakaja mashoga zangu nakumsalimia kwa furaha yule mbaba.

Kumbe wenzangu walikuwa na mabwana tayari mie ndo nilikuwa mgeni sina mpenzi na mwanaume akinitokea nampa matusi adi anakoma

“Sisi tunaelekea ubungo tupeleke basi”

Salma akamwambia yule baba akakubali basi tukajiandaa nakuvaa nguo zetu za shule tukapanda gari lake nakuanza kutupeleka

“Nimempenda sana Lisa natamani awe mpenzi wangu”

Alisema uyo mwanaume ambae alitwambia anaitwa Mr Antony

“Lisa muoga uyu ila usijali utampata tu”

Diana alidakia kusema nikataka kuongea akaniwahi kuniziba mdomo maana ananijua nipoje.

Basi alipitia njia ya shekilango akakatiza makaburi ya ufi nakutokea shungashunga ndo maeneo ya kwetu walianza kunipeleka mimi kwanza lakini hatukifika nyumbani ila tulipo nyumba yetu inaonekana basi nikaagana nao nakutelemka ile nashuka tu kwenye gari naona gari la baba limesimama pembeni ameteremka nakuja nilipo ata kabla lile gari alijaondoka akanifikia

Baba alipofika akaninasa kofi moja bila kuongea akasogea adi kwenye gari nakugonga kioo

“Fungua mlango toka nje”

Alimwambia yule mwanaume aliekuwa ndani ya gari, ambae alifungua kioo kumsikiliza baba aliekuwa amevaa magwanda yake yakiwanajeshi nilijua muda huo ndo alikuwa anatoka uko kambini kwake Lugalo.

“Habari yako muheshimiwa?”

Alianza kusalimia Mr Antony,

“Salama, samahani nimeona binti yangu akishuka kwenye gari lako unaweza kunambia umemtoa wapi leo ijumaa shuleni wanatoka saa sita mchana na sasa ivi ni saa kumi na moja niambie umetoka nae wapi”

Aliongea baba akiwa siriazi zaidi alikuwa anakunja mikono ya nguo yake yakijeshi nakuifanya iwe fupi mikononi akionyesha hana masihara anaweza kumpiga uyo mwanaume anaeongea nae nilipomuangalia alionyesha anauoga kwa mbali ila alijitahidi kujikaza.

“Oh kumbe ni binti yako mimi nilimkuta coco beach akiwa na rafiki zake wawili wapo humu kwenye gari ngoja niwaite”

Akawaita wale mashoga zangu ambao waliteremka watoka nje nakumuona baba alivyo uoga uliwajaa walitetemeka ovyo.

“Ndo hawa marafiki zake niliwaona coco nikawachukulia kama watoto wangu nikaamua kuwasaidia niwapeleke majumbani kwao ndio nimeanza na uyo ulosema binti yako bado ninasafari yakuwapeleka hawa weninge majumbani kwao”

Alijitetea Mr Antony nakumfanya baba awageukie wale wenzangu Diana na Salma

“Aliyosema uyu baba ni kweli au?”

Aliwauliza akiwakazia macho wote wakatingisha kichwa kukubali,

“Mlipoenda uko coco mlitoa ruhusa majumbani kwenu na wewe Lisa unaanzaje kwenda bila kuaga nyumbani mlifata wanaume uko eeh?”

Baba aliwauliza akawashushia makofi wezangu wote waliobaki wanalia kisha akamwambia yule mwanaume awapeleke kwao kesi ikabaki kwangu sasa alinibutua adi tunafika nyumbani

“Ole wako siku nyingine utoke bila kuaga shenzi wewe”

Yani nilikuwa napigwa sana ila sikomi nikaingia chumbani nikalia nakumlaani baba bora afe kabisa.

Mama aliporudi akaambiwa ata hakuniuliza yeye alishachoka kuongea.

Basi siku zikazidi kusonga adi nikaingia kidato cha tatu bado niliendelea kuwa mtukutu baba ananipiga tu adi nikamaliza kidato cha nne nilishukuru mungu apo nikajiona nishamaliza masomo tena nilizidi kutanuka nakuwa mkubwa nilifikisha miaka kumi na nane basi nilijiona mtu mzima kabisa, sifai kupigwa sikutaka ata kungojea majibu nikaomba nipelekwe kwa bibiyangu Songea nikakae nimkimbie baba maana shule nimemaliza ningekuwa nazurura kilasiku ningedundwa na baba muhimu kuondoka kwake.

Siku moja usiku tunakula nikaanza maongezi.

“Nimemkumbuka bibi yangu mimi nataka nikamuone tena nikake uko adi majibu yakitoka”

Niliongea kiunyonge mwenyewe

“Ila bora ukakae kijijini labda utajua kazi umelegea kama mlenda vile”

Mama alisema baba akaniangalia Alisema

“Najua unanikimbia sawa nenda kule kuna babayako mdogo nitamwambia akulinde ukitoka tu akupige”

Nilichukia maisha gani yakupigwa kilasiku nikajikuta namchukia babayangu kuliko shetani nilimuangalia nikatamani nimuwekee sumu afe.

“Sawa anipige tu nishazoea si mnanifanya mie ngoma”

Nilimjibu baba

“Katulie mwanangu hatokupiga babayako mdogo usijali”

Mama alisema sikumjibu nayeye nikainuka nakuelekea chumbani kwangu.

“Jiandae kesho safari Asubuh na mapema”

Baba alisema nikaondoka zangu nimenuna.

Basi nilifika nikapanga nguo zangu vizuri nakuweka nikaingia kulala.


Asubuh kulikucha nikajiandaa nakutoka baba nikawaaga wote baba ndie alinipeleka adi stand ya mkoa ubungo akaniacha nimepanga gari nayeye kuondoka.

Basi saa mbili Asubuh safari ikaanza nilikuwa na simu apo tayari mama alininunulia, nikaanza kuchat na mashoga zangu nikiwaaga naenda kijijini

“Loh shosti umeishiwa na urembo wote ukaishi kijijini aibu”

Alinambia Nasra

“Mwezangu babayangu kazidi kunipiga nimeona niondoke tu”

Nikachat adi saa nane sijui tumefika wapi pale nilichoka nakulala zangu kwenye kiti.

Nikaja kushtuka imefika saa kumi na mbili giza limeanza kuingia.

Ghafla tukatokea porini barabara haionekani kila mtu akashangaa

“Tumefikaje uku wewe dereva vipi?”

Watu wote walishangaa tukamsogelea dereva tumuulize tukamkuta amelala uku damu zinamtoka na kondakta ajulikani wapi alipo apo wote tulijawa uoga kila mtu akatoka kwenye gari nakukimbia ovyo mie begi lilikuwa zito nilitupa uko nakutoka mbio nisijue wapi naelekea, kila mmoja alikimbia njia yake gari likabaki na dereva aliekufa tu.

Usiku ulishaingia, nilikimbia nikiwa pekeyangu nikatokea porini zaidi kunatisha uku milio ya wadudu inasikika

“Mama wee nakufa mimi uuuhh”

Nikaanza kulia giza limetanda sioni mbele wala nyuma natetemeka kwa uoga nikasogea kwenye mti mkubwa nakukaa chini nimejikunyata apo hofu imenijaa sina tumaini lolote

“Mungu ipokee roho yangu”

Apo ndo nilikumbuka kuna mungu kumbe wakati mama alipokuwa ananiambia niende kanisani nilikuwa nagoma leo yamenikuta sasa nilijuta bora ningebaki tu nyumbani safari yakijijini imekuwa ndo mwisho wangu.

“Nakufa mimi leo”

Nilizidi kutetemeka mara kwa mbali nikaona miale ya moto watu wanaimba nakuja kule nilipo nikatamani nikimbie ila nguvu nilikuwa sina hatimae wakanisogelea wakinishangaa sana walikuwa wanatisha niliisi wachawi walivaa kaniki chini juu vifua wazi ni wanaume watatu

Walizidi kunishangaa uku wakinimulika na ile miale ya moto usoni, hatimae mmoja akaongea nakuniuliza

“Unaitwa nani?”

“Naitwa Lisa”

“Umetoka wapi umefata nini uku kwenye ufalme wa Odinya?”

Aliuliza lakini sikumuelewa

“Mimi nimetoka Dar es salaam nilikuwa naelekea Songea kwa bibi yangu kuna sehemu tulifika ni porini akuna aliejua tupo wapi tukamsogelea dereva tumuulize tumemkuta amekufa wote kwenye gari tukatoka nakukimbia ndio mimi nimefika apa”

Nilijielezea nakuangua kilio kikubwa wale wanaume wakaangaliana nakusema wanisaidie

“Tumpeleke kwa Mfalme uyu”

Wakasema nilishtuka nikajua napelekwa kuzimu sasa.

“Kwani nyie ni wachawi au?”

Nikawauliza nakuwafanya wacheke alafu mmoja akanijibu

“Sisi ni watu kawaida ila tunaishi kiutamaduni yani kiasili pia tunamilikiwa na mfalme usiogope sisi watu wema twende tukusaidie”

Basi waliposema ivyo kidogo uoga ukanipungua nikainuka nakuongozana nao, walikuwa wanaimba nyimbo zao zakushangilia sijui ata sikuwaelewa.

Tulipita maporini humo uku ile miale ya moto ikitusaidia kuona mbele hatimae nikaanza kuona kwa mbali nyumba baadhi uku moto umewashwa kwa nje. Tulizidi kusonga adi tulipofika kwenye iko kijiji chao moja kwa moja nikapelekwa kwenye nyumba kubwa nje wamesimama walinzi walioshika mikuki mikononi mwao tukawasogelea.

Basi wakasalimiana nakuomba waingie ndani kuonana na mfalme ambapo walikubaliwa tukaingia wote.

Alitwa kijakazi mmoja akatumwa amwambie Mfalme kuna wageni wake nje ambapo baada ya muda mfupi alitoka nikamuona mwanaume wa makamo tu si mtu mzima sana alikuwa amevaa nguo za kijadi kama mganga vile

“Uishi miaka mingi ewe mfalme wetu”

Walisema uku wameinamisha vichwa vyao chini namimi nikawageza nikainama.

“Karibuni”

Alisema uyo mwanaume ambae ni Mfalme kisha akasogea kwenye kiti cha ngozi nakukaa.

“Ewe Mfalme wetu mtukufu uyu binti tumemkuta porini usiku huu amesema kapotezana na wenzake tumeona kuliko kumuacha msituni auliwe na wanyama tukaamua kumleta mbele zako ili umsaidie”

Aliongea mwanaume mmoja kati ya wale walionikuta porini kule.

“Kwasasa ningependa apumzike adi kesho ndio niamue nini kifanyike juu yake! Somoiyeee njo haraka”

Aliisema Mfalme nakumuita kijakazi mmoja jina lake Somoiye ambae alikuja nakuinamisha kichwa kwa adabu zote.

“Naam mtukufu Mfalme”

Alisema akiwa ameinama bado.

“Mchukue uyu msichana kampeleke chumba cha wageni mpe chakula ashibe na maji aoge kisha mbadirishe nguo izo”

Alisema Mfalme

“Sawa mtukufu Mfalme”

Aliitia uyo binti Somoiye akanishika mkono tukaondoka apo nakunipeleka kwenye nyumba moja iliyokuwa ya udongo imezungushwa na nyasi.

Tukaingia ndani ambapo kulikuwa na mkeka chini uku pembeni kuna kitanda cha kamba na shuka juu.

“Unaitwa nani?”

Aliniuliza

“Naitwa Lisa”

“Ooh Lisa liene”

“Sio ivyo ni Lisa tu”

“Yani nimeongeza maana yake umekuja mwenyewe”

Alisema ila sikumuelewa

“Ngoja nikakuletee chakula kwanza”

Alisema akainuka nakutoka umo ndani kulikuwa na kibatari kinawaka ndo mara ya kwanza naingia nyumba ya nyasi kwani ata kwa bibiyangu sio kijinini ni songea mjini nyumba yake ya tofari na kuna kilakitu ndani adi maji yapo, sasa uku nilipokuja leo ndo mara ya kwanza kilakitu kigeni kwangu.

Baada ya muda mfupi Somoiye akaja na sinia limefunikwa juu

“Karibu Lisa liene”

Alisema nikamshukuru nilifunua nakukuta ugali na nyama yakuchoma nilikuwa na njaa nikaufakamia wote adi nilipotosheka alinipa maji ya kunywa matamu ayo kama ya mvua

“Kuishi uku adi raha jaman”

Nilijisemea kimoyomoyo.

“Asante Somoiye”

“Usijal mrembo wangu”

Alikuwa mcheshi uyo mdada ambae kiumri yeye mkubwa kwangu basi akatoka na vyombo aliporudi alishika vitenge viwili na tait fupi moja akanipatia

“Njo nikuonyeshe bafu uoge kisha ukapumzike”

Alinambia nikatoka nakuingia kuoga adi nilipomaliza akanisaidia jinsi yakujifunga izo nguo

Kitenge kikubwa nilijifunga chini kiunoni na kingine kidogo kama kitop nikajifunga juu nikafanana na mavazi aliyovaa yeye sasa.

Baada ya apo nikarudi kulala ndani.

“Usiku mwema kesho asubuhi nitakuja kukuona sawa eeh”

Alinambia akaondoka nakuniacha nimejawa na mawazo siamini maisha yangu yamekuwaje.

Kulala kwenye kitanda cha kamba niliogopa nikalala kwenye mkeka chini, usingizi haukuja mapema nilikuwa na mawazo sana ata sijui muda gani nilipitiwa nikaja kushtuka asubuhi kumekucha

“Lisa liene amka”

Ni Somoiye ndie alikuja kuniamsha nikashtuka nakutoka nae nje ambapo alinipeleka kwa Mfalme aliniitaji.

Sasa niliweza kuona iki kijiji kilivyo madhari yake ilivutia kulikaa kiasili sana nakupendeza.

Nyumba nyingi za udongo na kuezekwa kwa nyasi zilienea maeneo mengi uku kukiwa na miti ya matunda mbalimbali na mboga za majani walizopanda nilizidi kushangaa sababu sikuwahi kufika vijijini nakujionea zaidi hii ni milki ya kifalme ambayo wanaishi kiutamaduni nilipenda sana kulivyo nikawa naangaza macho sehemu nyingi nakuangalia.

Basi nikafikishwa kwa Mfalme nakumsalimia ambapo nilimkuta na mkewake Malkia Tamara alikuwa mwanamke mzuri sana mwenye haiba ya upole.

“Unaitwa nani binti?”

Aliuliza uyo Malkia

“Naitwa Lisa”

“Ooh basi tutakuita Lisa liene maana yake umekuja mwenyewe”

Alisema akitabasamu nikamkubalia sawa.

Baada ya apo wakaanza kunihoji nimefikaje kijijini kwao, nikawaelezea ilivyokuwa wakanipa pole nakuahidi watanisaidia jinsi yakuondoka kurudi nyumbani

“Ila nimepapenda sana uku kwenu kuzuri naomba nikae ata mwezi mmoja”

Nikawaomba ili niendelee kujifunza mengi basi walikubali nakusema nitaishi nao apo kwao nilifurahi sana.

“Inabidi lipigwe baragumu nakuwaitwa wanakijiji watambue uwepo wa mgeni apa kijijini”

Alisema Mfalme na mkewe akakubali.

“Mashable kapige ngoma wanakijiji wakusanyike”

Aliamliwa kijana mmoja ambae aliondoka mbio nakwenda kupiga ngoma.

Mara vijakazi wakaja na kifungua kinywa wakaweka kwenye meza moja iliyokuwa humo ndani tulipokaa ambapo Malkia akanikaribisha chai, Mara ghafla akaja kijana wa kiume umri wake kama miaka ishirini na tano ivi alikuwa amevaa mavazi yakifalme pia

“Muishi miaka mingi Mfalme na Malkia”

Alisalimia baada ya apo akakaa nakujumuika nasi

“Lisa uyu ni kijana wangu nina watoto wawili wakike ambae ametoka yupo kwa shangazi yake na wakiume ndo huyu “

Alisema Malkia

“Muthan uyu anaitwa Lisa ni mgeni wetu apa kijijini”

Alimuelezea mtoto wake ambae alimuelewa utamburisho ukaisha apo tukaanza kula pamoja, nilipata bahati sana yakukaa na kula na Mfalme na familia yake.

Uko nje wanakijiji walikusanyika wengi uwanjani ambapo ni mbele ya nyumba ya Mfalme basi tulipomaliza kula tukatoka wote pamoja nakuelekea uko kwenye uwanja ambapo kulikuwa na mikeka imetandikwa mingi watu wamekaa apo kwa mbele kulikuwa na viti anavyokaa Mfalme na familia yake.

Ilikuwa sehemu maalumu kwa mikutano hakikuwa na jua walijenga kama ukumbi ivi ambapo likitokea tatizo wote wanakusanyika apo.

Watu walikuwa wengi zaidi wamevaa nguo za kitamaduni walipendeza machoni mwangu.

Wakubwa kwa watoto walijaa apo,

“Mdumu miaka mingi Mfalme na Malkia”

Walisema wote nakuinama kwa heshima.

Mfalme alisogea akaka kwenye kiti chake cha ngozi sijui ya mdudu gani yule na malia pia akakaa kwake na mtoto wao akakaa pamoja na mie uku pembeni walikuja walinzi kama sita na mikuki yao wakasimama pembeni yetu kutulinda.

Mfalme akakooa nakuanza kuongea na wananchi wake

Kabla ajaanza akatokea msichana mmoja kavaa nguo zake fupi sana anatembea kwa maringo uyo akasogea sehemu nakukaa uku akijipepea kama anasikia joto.

“Uyo binti aliefika sasa aje uku mbele”

Aliongea Mfalme akiwa amechukia

ITAENDELEA

Mrembo Mcharuko Sehemu ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment