CHOMBEZO

Ep 02: Mrembo Mcharuko

SIMULIZI Mrembo Mcharuko
Mrembo Mcharuko Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: LATIFA

*********************************************************************************

Chombezo: Mrembo Mcharuko

Sehemu ya Pili (2)

Yule msichana akasogea adi mbele uku akionekana muoga sana.

“Uishi miaka mingi ewe Mfalme wetu”

Alitoa heshima kwa Mfalme ambae alikuwa amekunja sura.

“Kazimta njoo umchukue uyu binti”

Aliongea Mfalme mara akaja mwanaume mwenye mwili mkubwa nakumbeba yule msichana

“Nisamehe Mfalme nimekosa”

Alilia akiomba msamaha nilipigwa mshangao sikujua kosa lake ni lipi.

Mfalme akaanza kuongea

“Mnaonyesha tabia mbovu kwa mgeni uyu binti hana heshima inawezekanaje Mfalme afike wa kwanza alafu yeye achelewe anakuja kwa maringo kama bata maji vile shenzi kabisa”

Alionyesha kweli amechukia sana.

“Tumepata mgeni uyu binti anaitwa Lisa”

Alisema Mfalme nakuniomba nisimame watu wanione utambulisho ukafanyika kila mtu akanijua sasa baada ya apo watu wakatawanyika yule msichana ambae nilisikia anaitwa Shamima alisamehewa akaambiwa asiludie tena kuchelewa.

Maisha yangu mapya yakaanza apo nikiishi kwa Mfalme nikiwa kama mmoja wa familia yao.

Baada ya siku chache kupita mtoto wao wa kike alirudi ambae anaitwa Nuhri alitamburishwa kwangu alifurahi kuniona umri wetu ulilingana tukazoeana nakuwa marafiki, nilipenda kujua madhari mengi ya iko kijiji ambapo Nuhri akaomba ruhusa kwa wazazi wake tukawa tunatoka nakunitembeza sehemu mbalimbali nione kulivyo.

Siku moja vijakazi walikuwa wanaenda mtoni kuchota maji nikaongozana nao namimi nikabeba chungu kimoja kikubwa maana hakuna ndoo ni vyungu na maji mengine yanahifadhiwa kwenye mitungi yanakuwa ya baridi sana.

Basi tulifika tukakuta ugomvi msichana mmoja na Shamima

Ikabidi nisogee niulize kunanini

“Mimi nimewahi kufika nachota maji uyu Shamima amwkuja nakunipokonya kata alafu anachota yeye”

Alisema uyo msichana sikujua jina lake nani na uyo Shamima nilimjua sababu ya kumuona siku ile aliyochelewa kwenye kikao.

Nikatizama uyo Shamima kwanza

“Wewe kwanini usingoje mwenzio amalize kuchota maji ndo ufate we zamu yako?”

Nilimuuliza msichana ananyodo sana alinitazama kwa dharau juu adi chini akatoa msonyo nakutema mate iliniuma sana.

“Naisi unijui kama mie naitwa mrembo mcharuko ngoja nikufundishe adabu ukasimulie wenzio”

Nilimwambia nikamvaa mwilini tukadondoka chini nikaanza kumshushia makofi alikuwa ata nguvu hana analia kuomba msaada wale wengine walipoona nampiga walishangiria sana.

“Mpigee uyooo amezidi kujiona mzuri apa kijijini mkomeshe”

Nikasema kumbe ndo alivyo leo atanitambua tena alikuwa mwembamba mie bonge nilimkalia juu nilimpiga alilia sana nilipotosheka nikainuka.

“Haya omba msamaha”

Nilimwambia alikuwa analia tu

“Inuka muombe msamaha moze”

Yule msichana mwengine jina lake moze nikamwambia amuombe msamaha akainuka nakumuomba baada ya apo vijakazi wakachota maji tukaondoka nakurudi nyumbani.

Yule msichana alienda kwao akamshtakia mamayake ambae alichukia sana wakabebana adi kwa Mfalme wao kuja kushtaki.

“Mfalme tumeishi miaka mingi kwa amani kijijini kwetu hakujawahi kutokea ugomvi uyo binti mgeni ni mkorofi kampiga mwanangu kwanini?”

Mama aliongea kwa hasira uyo akimwambia Mfalme, mimi nilikuwa chumbani na Nuhri tukipiga story nikamsimulia yaliyotokea alicheka sana, Mara akaja Somoiye kuniambia naitwa na Mfalme tukatoka wote na Nuhri tukaenda nilishtuka kumuona Shamima yupo na mwanamke mtu mzima nikajua ni mzazi wake.

Basi kesi ikaanza apo nikasemwa kwanini nimepiga.

“Uyu binti anadharau sana alafu anajiona mzuri mwenyewe ivi mimi na uyo nani mzuri ebu niangalieni mbele na nyuma ananifikia uyo”

Yani akili zangu nazijua mwenyewe niliulizwa lingine nikanibu lingine nakusimama nikijigeuza wanitizame kwanza.

“Wewe mtoto sijafata shepu yako apa kwanini umempiga mwanangu?”

Alipandwa hasira yule mama,

“Nimemfundisha adabu sababu hawezi kunidharau mimi”

Niliongea adi Mfalme akaingilia nayeye nakuomba tuyamalize tuombane msamaha

“Looh nani amuombe msamaha uyu”

Nilikataa na yule nae akakataa mwisho wakafukuzwa waondoke

“Nitakukomesha wewe”

Alisema Shamimu

“Hehe halooo ingia anga zangu nikutoe manundu”

Nilimjibu nikikunja ngumi wakaondoka uku nyuma Nuhri aliangua kicheko kikubwa

“Nakupenda bure Lisa yani umejua kunichekesha leo”

Alisema tukaingia ndani nakuendelea kupiga story Mfalme yeye alikuwa ananiangalia jibu lakunipa hana tangu siku iyo habari ikaenea kijijini nimepiga Mrembo wa kijiji Shamimu ni msichana ambae alikuwa anajisikia nakujiona mzuri sana anadharau hana heshima kabisa sasa alinipata kiboko wake nilimnyima raha sana sababu kijiji kizima alikuwa anatingisha yeye kuja kwangu kulimfanya asiwe na amani alinichukia sana alafu nilimzidi kilakitu basi alibaki anaumia tu.

Basi siku moja Asubuh nikaona wanaume wengi wamekuja nakumchukua Muthan yule mtoto wa Mfalme wakiume wakaondoka nae siku mbili hakurudishwa ikabidi nimuulize Nuhri

“Muthan kapelekwa wapi?”

“Ooh sikukwambia kumbe anataka kuoa yule ameenda mizimuni kutambika”

“Wee kumbe anataka kuoa sasa uyo mwanamke wake mbona sijawahi kumuona apa?”

Nilizidi kumuuliza

“Sio ivyo yani mila zetu mwanaume akifikisha miaka ishirini na tano anatakiwa aowe na mwanamke pia miaka ishirini anatakiwa aolewe na mila zetu hairuhusiwi kuzini wala kuwa na uhusiano na mume au mke ujutafutii bali tunaweka ngoma wasichana vigoli wanacheza na mwanaume anachagua alafu ndoa inapita”

Alinielezea Nuhri nikamuelewa.

“Kwaiyo Muthan pia ataweka ngoma kutafuta mke?”

Nilimuuliza

“Ndio tena leo anarudi naisi kesho ngoma inawekwa”

Alinambia nikamuelewa sasa nilibaki kwa hamu nione harusi zao inakuwaje.

Maandalizi yakaanza watu wakaweka ngoma zao uwanjani moja ikapigwa wakakusanyika wanakijiji nakupewa habari wale wasichana vigoli wanaotaka kuolewa wakaambiwa wajiandae.

Maandalizi yakafanyika Usiku Muthan akarudi nakuwekwa ndani akipokea baraka za wazazi wake.

Hatimae kesho yake ikafika siku yakumtafuta mke wa mtoto wa Mfalme.

Wanakijiji wote walikusanyika kwenye uwanja mkubwa ambao ni maalumu kwaajiri ya ngoma, kulikuwa na sehemu pembeni wamezungusha makuti hao vigoli wanaotaka kuolewa wanakaa humo alafu mmoja mmoja anatoka nakuja uwanjani kucheza adi wote waishe alafu wanajipanga mstari anapita mtoto wa Mfalme nakumchagua mmoja aliempenda.

Basi mambo yakaanza uwanjani apo ngoma zikaanzwa kupigwa uku watu wakijiweka tayari kumpokea Mfalme na familia yake ambapo alitoka nyumbani kwake nakuelekea kwenye ngoma sasa akiwa na mkewe pamoja na watoto wake wawili na mimi nikiwepo pia walinzi wengi walitulinda adi tulipofika nakwenda kukaa sehemu iliyotengwa maalumu kwa Mfalme viti kikubwa vya ngozi viiliwekwa apo.

Baada yakukaa wakatoa salamu zao kwa Mfalme nakumtakia maisha marefu, Mara akaja mwanaume mmoja mbele akiwa ameshika karatasi nakuanza kuongea.

“Jamani wanakijiji tumekusanyika apa kwenye tukio kubwa linalomuhusu mtoto wa Mfalme Muthan anaetaka kuchagua mke leo hii, naamini wote tumefurahia ili jambo pia mabinti au vigoli wetu warembo wameshajiandaa vizuri kwaajiri yakuonyesha uwezo wao wakucheza ngoma vigeregere jamani kinamama”

Alisema nakufanya watu walipukwe kwa shangwe kubwa, alafu akaendelea kusema.

“Kuna mabinti kumi waliojitokeza ngoja niwaite majina yao waje apa mbele muwaone Shamima, Maua, Somoe, Halima, Mwaija, Sara, Shani, Moze, karima, na Zawadi ni wasichana wanaojiamini sana sasa nawakaribisha wa kwanza ni Moze aje mbele”

Aliita majina yao wote wakatoka mbele kila mtu akawaona nilishtuka kumuona Shamima kumbe nae alikuwepo nikajisemea kimoyomoyo ngoja nione nani atashinda.

Basi ngoma ikapigwa akaanza Moze kucheza alijitaidi mwenyewe akacheza nusu saa nakutoka akaja mwengine pia ivyo ivyo adi ilipofika zamu ya Shamima alikuwa anajikakamua uyo kama mfyatua matofari nilibaki namtizama nikitamani nikamtie ata makofi atoke pale mbele basi alipomaliza akaingia msichana wa mwisho Zawadi nae akacheza apo alipotoka tu nikasema sikubali naingia kati maana ngoma ilinisisimua balaa nikaisi mwili wote unanisisimka, nilitoka mbio kule mbele nilipokaa adi watu wakashangaa kunanini walinzi wakataka kunikamata nikawastopisha wasiniguse apo wazimu ushanipanda sasa, niliingia kati nikazungusha kiuno kama sina akili nzuri

“Watu wanacheza kama wamebemendwa vile ngoja niwaonyeshe ngoma zinachezwaje”

Nilijisemea kimoyomoyo apo watu wote kimya macho yapo kwangu nilizungusha kiuno nimesimama adi nikachuchumaa ufundi wote nilimaliza apo nikaona nikae staili ya chura sasa na zigo langu snura akasome basi nilianza kucheza kuchurachura apo mara nitishinge tako moja moja burudani ya nguvu nikaitoa nilikata mauno watu hawakuamini wakaanza kushangiria namimi ndo mizuka ikazidi nilicheza uwiii adi nikaja kunyanyuliwa juu juu

“Lisaaa Lisaaaa Lisaaa oyooooo piga keleleeeee”

Basi nakwambia nilibeba juu juu uku wakizidi kushangiria, walinikera kunikata stimu yangu.

Mara ghafla namuona Muthan amekuja nakuwaambia wanishushe chini baada ya apo akasogea kunikumbatia

“Nakupenda Lisa jamani uyu ndo mkewangu”

Aliongea watu wakazidi kushangiria mara akaja Nuhri

“Waoo wifi yangu”

Alinikumbatia nakunishika mikono adi kwa Mfalme nikapewa baraka apo apo wakaja wamama wawili na kanga nikafunikwa kama mwali nakutolewa uwanjani nikapelekwa ndani kwenye chumba kimoja kwaajiri ya maandalizi ya ndoa.

“Jamani mimi sipo tayari kuolewa nilicheza kujifurahisha sio kutaka kuchaguliwa”

Yan mambo yalipelekwa haraka ata sikuelewa kwanini imekuwa ivyo nilijuta kwenda kucheza ngoma imeniponza nikiolewa nitarudije nyumbani nilijikuta nashindwa kujizuia nikaanza kulia.

Akaitwa Mfalme nakuambiwa sitaki kuolewa ikabidi aje na mkewe wakanibembeleza nakunisii nikubali watanipeleka nyumbani kwetu apo kidogo moyo wangu ukaridhika.

Ninakubali sasa Malkia Tamara alifurahi sana.


Hatimae nikaanza kusingwa mwali nakufundwa kuishi na mume, maandalizi yalipamba moto uko nje vyakula vikaanza kupikwa watu wakaalikwa adi kutoka falme nyingine waje kuhudhuria sherehe.

Nilisingwa kiasili nikapendeza sana walinipaka hina wifi yangu Nuhri alinichora mwilini jamani nilikuwa kama malaika ikaletwa nguo ya kimalkia nikavishwa gauni kubwa zuri limenakishiwa na vito vyakumeremeta ni mamamkwe wangu uyo ndo alienipa iyo nguo Muthan nae alipendeza alivaa joho kubwa lakifalme.

Basi maandalizi yalikamilika na ndoa ikafungwa uku watu wote wakishiriki kwenye harusi yetu walikunywa na kula adi wakasaza.

Kulikuwa na kijana ni mtoto wa Mfalme ambae babayake aliarikwa kwenye sherehe yetu wakahudhuria wote aliponiona alinipenda sana nakutamani iyo ndoa angekuwa ananioa yeye, moyo wake uliuma sana bahati nzuri akamuona Shamima ambae alikuwa mnyonge sana sababu tangu mwanzo alikuwa anajitapa yeye ndie ataolewa lakini imekuwa tofauti ilimuuma ata kwenye harusi watu wote walikuwa na furaha kasoro yeye alikuwa mnyonge sana.

Yule mtoto wa Mfalme aliitwa Millar akamfuata Shamima nakujenga ukaribu nae ambapo aliwatuma walinzi wake wamuitie Shamima nakuanza kuongea nae

“Kunakitu nataka unisaidie”

Alimwambia nakumfanya Shamima ashtuke.

Sherehe yetu iliendelea kunoga waliohudhuria waliburudika sana, watu walicheza ngoma za asili walikunywa pombe za kienyeji na vitu vingine vingi ambavyo ndo ilikuwa mara ya kwanza naona.

Hatimae ikafika tamati tukaondoshwa bwana na bibi harusi nakupelekwa ndani uku nje waliendelea kuburudika adi walipochoka kila mtu alielekea nyumbani kwake.

Maisha ya ndoa yakaanza kwangu nilitamani wazazi wangu wangeudhuria ila ndo hawakuwepo.

“Mbona unamawazo mke wangu?”

Aliniuliza Muthan

“Nimewakumbuka wazazi wangu natamani wangekuwepo”

Nikamjibu kiunyonge

“Usijali nitajitahidi kupate njia yakufika uko kwenu tutaenda kuwaona”

Alisema nikafurahi sana.

Basi tuliongea mengi mwisho tukalala ilikuwa usiku.

Nilitokea kupendwa sana kwenye iyo familia ya kifalme hawakunitenga sababu mimi si mzaliwa wa apo walinichukulia kama nimeishi nakulelewa apo.

Siku zikazidi kusonga nikiendelea kuishi adi nilipofikisha miezi sita ya ndoa yangu mumewangu akabadirika nakusema alikosea kunichagua mimi anamtaka Shamima kila mtu alishangaa.

“Wewe Muthan umepatwa na kitu gani kwani?”

Aliuliza Babayake

“Baba namtaka Shamima nampenda sana”

“Wewe mtoto unawazimu eeh usiniletee ujinga apa na uyu Lisa ni nani si mkeo uyu unamtaka Shamima iweje?”

Malkia Tamara alipandwa na hasira nakumuuliza mtoto wake ambae hakujali alishikilia lazima amuoe Shamima.

Mzozo ulikuwa mkubwa sana mi ata sikujali kwani kuolewa kwenyewe ilitokea bahati mbaya sikupenda nikaona bora aolewe uyo Shamima mie niweze kuondoka, lakini Mfalme na Malkia waligoma akuna kumleta Shamima kwenye familia yao ikawa balaa sasa maneno mengi yakazuka apo tafrani tupu.

Muthan akahama chumbani nakwenda kuhamia nyumba nyingine hakutaka kabisa kuwa karibu na mimi.

Sababu wazazi wake waligoma asimuoe Shamima alichokifanya ni kilasiku anamleta apo nyumbani analala nae adi asubuhi anaondoka alikuwa anamficha akuna aliekuwa anaona adi siku moja akafumwa na wazazi wake ambao walichukia sana nakutaka kuwapa adhabu wote.

“Nina mimba ya Muthan mimi msiniazibu”

Alinitetea Shamima akilia ikabidi Mfalme apunguze hasira kilichofanyika ni kupanga ndoa sababu kuzaa nje ya ndoa ni haramu kwao.

Basi mipango ikafanyika apo ndoa ikapita na wakaanza kuishi mume na mke namimi ata sikuwafatilia Shamima alikuwa anajiona yeye ndo mwanamke wa nguvu mie tena nilikuwa kama kinyago mbele yake lakini sikutaka kujali wazo la nyumbani likanijia nakutamani niondoke, wanakijiji wengi walinionea huruma kisa nimeachwa nakuolewa mwengine ila sikuwafatilia niliona kawaida tu.

Baada ya miezi michache kupita nikajiandaa nakuwaita Mfalme na mkewe nakuwaaga mie naondoka narudi kwetu.

Walihudhunika sana kuondoka kwangu basi nikapewa walinzi watakao nisindikiza safari yangu!

Nikaagana nao kwa hudhuni nakuondoka, tukiwa njiani tukakutana na msafara wa mtoto wa Mfalme mwengine Millar ambae ni yule aliekuwa ananipenda.

Alishuka kwenye farasi aliepanda nakuwaomba hao walinzi waniache yeye atanipeleka basi walikubali nikaagana nao

“Panda farasi twende”

Alinambia nikapanda baada ya apo safari ikaanza, tulipita maporini adi tukatokea sehemu moja inajumba kubwa zuri limenakishiwa kwa dhahabu tupu uku nje wamejaa walinzi wengi wenye mikuki na mishale nikaogopa uku tena wapi nimeletwa.

“Millar umenileta wapi?”

Nilimuuliza

“Karibu kwenye ufalme wa dhahabu”

Alinambia akitabasamu apo ndo nikamuona vizuri uyu mwanaume alikuwa anamwonekano wa pesa yani alikuwa smart sana, nikakaribishwa nakuingia ndani adi niliogopa kukanyaga utasema wanaishi malaika humo ndani ni peponi kuzuri ajabu kote kumejaa dhahabu kilakitu viti meza sijui nini dhahabu tupu niliisi kupagawa.

Basi nikakaribishwa nakukaa kwenye kiti uku natetemeka,

“Nakuja mama nisubiri”

Alisema Millar akandoka nakuingia ndani ambapo baada ya muda mfupi alitoka nakuja akiwa ameongozana na mwanamke mtu mzima kiasi aliekuwa anameremeta na nguo yake aliyovaa gauni kubwa lefu linaburuzika chini, nilibaki nimeganda namshangaa uyo mama alivyopendeza ata sikujua salamu zao zipoje nilishindwa kusalimia.

“Ujambo binti?”

Alinianza yeye

“Sijambo mama shikamoo”

Alijibu uku ananitazama kama ananithaminisha vile nafaa au sifai.

“Lisa uyu ni mamayangu Malkia Rawani”

Alinitambulisha Millar akanionyesha jinsi yakumsalimia basi nikamsogelea nakumbusu mikono yake nayeye akanibusu kwenye paji ya uso.

“Millar nimempenda sana uyu binti ebu ngoja niite vijakazi wambadirishe kwanza”

Alisema malkia, japokuwa ni mcharuko ila nilikuwa na bahati yakupendwa sana.

Basi wakaitwa hao vijakazi wakanichukua nakunipeleka chumba cha mavazi magauni mengi yamejaa humo yakila aina, nikachagua moja nililolipenda nakuvalishwa nikatengenezwa nywele zangu nilipendeza ajabu nikatolewa sasa nakurudishwa alipokuwa Malkia waliponiona hawakuamini.

“Waoo umependeza”

Alisema Millar

“Uko Mrembo sana najivunia kuwa na mkwe mzuri ivyo”

Alisema Malkia nakunifanya nishangae nimekuwa mkwe tena.

“Millar sitaki ndoa yenu ichelewe wasiliana na babayako mdogo aje afanye mipango ya ndoa pia muite Maulid akatangie watu wakusanyike”

Alitoa maagizo Malkia Rawani niliisi nguvu zinaniisha uku pia naolewa kwetu nitarudije sasa ata sikuelewa.

Basi wakaanza kufanya utaratibu apo lakin nilichogundua huu ufamle wanaishi tofauti kule nilipotoka ni kijinini na uku kama mjini japo sijaona gari zaidi ya farasi lakini nyumba zao akuna ya nyasi zote dhahabu tu yani unaitwa ufalme wa Dhahabu ni kuzuri sana.

Nikapelekwa chundani nakupewa chakula kizuri sana baada ya kula nikaanza kuandaliwa kwaajiri ya ndoa uku nje watu walipata habari wakajaa nakuanza maandalizi ya ndoa.

Siku iyo ikapita kesho yake ikafika nikatolewa nje nakufungishwa iyo ndoa yani ilikuwa haraka sana naisi Millar aliogopa kuniacha muda mrefu labda nitamkimbia sijui basi hatimae nikaolewa mara ya pili tofauti na kule nilikataa apa nilijikuta nakubali maana nikiangalia mazingira yake mazuri ajabu na izo Dhahabu roho yangu inaridhika sana.

Basi ndoa ikafungwa apo sherehe kubwa ikafanyika mwisho tukaingizwa chumbani na watu wakiendelea kuburudika uko.

“Mke wangu kwanza samahani nimekuoa bila kuongea nawewe ila yote ni kutokana na upendo wa kweli kwako na pia kuna jambo nataka nikiri kwako nimefanya nahitaji msamaha wako”

Alisema Millar tukiwa chumbani nilishtuka moyo ulienda mbio nikamuomba aniambie ni jambo gani ilo.

“Siku ya harusi yako na Muthan nilikuwepo kiukweli nilitokea kukupenda sana, nilitamani uwe mkewangu na mtu nilieona ananifaa kunisaidia ni Shamima..

Kabla ajaendelea alipotaja ilo jina moyo ulipiga paa

“Nilimfata Shamima nakumueleza shida yangu ni kuwa nawewe ajabu atayeye pia akasema anatamani kuolewa na Muthan nilifurahi kusikia ivyo nilichokifanya ni kumpa dawa ili Muthan ampende na akukatae wewe”

Alisema Millar nakuendelea

“Yote yaliyokuwa yanatokea Shamima alinieleza adi pale ulipoondoka na walinzi nilijua ndo maana nikaja kukufuata Lisa usichukie kwa aya nikuambiayo yote ni mapenzi ya dhati niliyonayo kwako”

Aliongea nakumaliza kuniomba msamaha sikuona haja yakukataa sababu tayari tumefunga ndoa nikamkubalia alifurahi sana.

“Vipi kihusu kurudi nyumbani kwetu?”

Nilimuuliza

“Kwani nyumbani kwenu ni wapi na unajua apa ulipo ni wapi?”

Nilishtuka nikatamani nijue nipo wapi

“Kwetu ni Dar es salaam kwani apa ni wapi?

“Apa ni misri”

Hee nilishtuka ndo maana niliona watu wengi kama waarabu

“Sasa nitarudije kwetu?”

“Utarudi mkewangu usijal”

Alisema akanikumbatia.

Siku zikazidi kusonga hatimae nikapata ujauzito, mumewangu alinipenda nakunijali sana Mfalme pia na Malkia walinipenda niliishi kwa amani na furaha.


Kule kwa Muthan mkewe alishika ujauzito ajabu wazazi wake walishangaa sana kumbe Muthan hana uwezo wakumpa mimba mwanamke.

Basi walichokifanya ni kumuweka chini Shamima aeleze iyo mimba ni ya nani.

“Ujauzito wa mumewangu”

Alijitetea Shamima

“Si kweli Muthan hana uwezo wakumpa mimba mwanamke ila kushiriki tendo anaweza mimi ndio babayake nalijua ilo tueleze mimba ya nani?

Mfalme alichukia nakutaka kuambiwa ukweli.

“Baba labda uwezo nimekuwa nao jaman ebu muacheni mkewangu”

Muthan aliingilia kusema

“Sawa kesho tutaenda mizimuni kuona iyo mimba ni ya nani na huo uwezo unao au huna tutajua kesho”

Alisema Mfalme nakuondoka kuwaacha wenyewe

“Familia yako hainipendi”

Shamima aliongea akilia

“Usijal mkewangu mimi nakupenda sana”

Muthan alimfariji mkewe baada ya apo wakaingia ndani kulala, ilikuwa usiku Shamima alipoona mumewake amelala alinyata akafungua mlango nakutoka adi nje walinzi walikuwepo lakini alipita kwa nyuma hawakumuona akazidi kutembea ndani ndani bila kuonekana adi alipofika kwenye nyumba anaishi kijana mmoja aitwae Mahdi akagonga mlango nakuingia ndani.

Tofauti na mawazo yake akuna aliemuona kumbe Mfalme alimuweka mlinzi mmoja amchunguze Shamima. Alipotoka alionekana nakufatiliwa adi alipofika kwenye iyo nyumba ya mwanaume mwengine.

Kijijini apo akuna kufuri wala funguo ila kulikuwa na kamba za mgomba unafunga mlango wako kwa nje na mtu akiwa ndani awezi kutoka ndio alivyofanya uyo mlinzi wa Mfalme alipohakikisha Shamima kaingia alifunga mlango kwa nje nakuondoka kupeleka habari kwa Mfalme ambae alisema kesho ndo mwisho wake Shamima.

Muthan aliamka nakujikuta yuko pekeyake mkewe hamuoni akaisi labda amenda chooni alikaa muda mrefu hamuoni kurudi adi akapata wasiwasi akaamua kutoka nje nakumuangalia hakumuona akarudi ndani nakulala adi kulipokucha akasikia ngoma inapigwa nje alishtuka kunanini alitoka nakukutana na babayake

“Kuna nini mbona ngoma Asubuhi?”

Aliuliza

“Mkeo yupo wapi?

“Sijui tangu usiku sijamuona”

“Sawa leo utajua kilakitu kuhusu uyo mwanamke wako unaemuona bora adi ukamkataa Lisa”

Alisema Malkia nakumfanya Muthan asielewe kitu.

Watu walijazana wote apo uwanjani na Mfalme akatoa akasema waelekee kule alipokuwepo Shamima.

“Kunanini baba inamaana unajua mkewangu alipo?”

Muthan aliuliza

“Eeh tulia utaona uko uko”

Malkia Tamara nae akamjibu basi msafara ukaanza kuelekea nyumbani kwa Mahdi.

**

Shamima alienda kwa Mahdi kumueleza kuhusu mimba aliyokuwa nayo ni yake ikiwezekana watoroke kumbe uyo Mahdi ni mpenzi wake kabla ya Muthan aliumia kuona mwanamke wake kaolewa na mtoto wa Mfalme lakini hawakutaka kuvunja mapenzi yao kwaiyo wakawa wanaendelea kukutana adi ilipopelekea kushika mimba.

“Mfalme kajua nina mimba kibaya zaidi Muthan hana uwezo wakumpa mimba mwanamke Mahdi tutoroke tutauliwa ndio maana nimekufata usiku huu”

Alisema Shamima ambapo wakakubaliana nakuchukua vitu baadhi ambavyo wataondoka navyo, baada ya apo wakasogea mlangoni nakufungua watoke ajabu mlango haukufunguka

“Imekuwaje huu mlango?”

Aliuliza Mahdi

“Ata sijui mbona”

Basi wakajitahidi mlango haukufunguka adi wakakata tamaa nakukaa chini Asubuh ilifika wakasikia ngoma Italia

“Mungu wangu tumekwisha”

Shamima alisema kabla hawajakaa sawa wakasikia mlango unafunguliwa na walinzi wakaingia ndani kuwatoa wakakutana na wanakijiji wengi pamoja na Mfalme wao wapo nje wanawatizama.

“Wakamateni wote”

Mfalme Odinga alitoa tamko, walinzi wakawashika kwa pamoja nakuwapeleka adi uwanjani ambapo watu wote walikuwa kimya wakisikiliza nini kimetokea na imekuwaje Shamima akutwe kwa Mahdi.

Waliwekwa mbele ya wanakijiji nakusubiria adhabu yao Shamima alikuwa analia sana nakujuta.

“Baba sielewi nataka nijue nini kinaendelea?”

Muthan alisema

“Shamima ebu eleza ukweli wako apa huyu kijana ni nani yako?”

Alisema Mfalme Odinga ambae hakuwa na chembe ya masihara.

“Ukweli Mahdi alikuwa mpenzi wangu kabla sijaolewa na Muthan”

Alisema apo minongono ikaanza kwa wanakijiji kwani hairuhusiwi kushiriki mapenzi kabla ya ndoa na lazima msichana Aolewe akiwa kigoli yani bikira tayari Shamima alipatikana na kosa moja kaolewa na Mtoto Wa Mfalme akiwa si bikira.

“Endelea tunakusikiliza”

Alisema Malkia Tamara

“Nilipenda sana kuolewa na Muthan ata siku ya ndoa nilijua nitashinda mimi bahati haikuwa kwangu akachaguliwa Lisa iliniuma sana nikawa sina raha bahati nzuri nilikutana na mtoto wa Mfalme wa Dhahabu Millar nayeye alimpenda Lisa akaniomba nimsaidie kumpata nikamueleza namimi nampenda Muthan akanipa dawa nijipake nikikutana na Muthan atanipenda na kumfukuza mkewake ivyo ndio ilivyokuwa lakini nilitaka Muthan anipende sana asiniache nikaamua nibebe mimba ya Mahdi nakusema ni ya Muthan, naomba nisamehe mumewangu”

Alimaliza kusema uku macho yamevimba machozi yamemjaa wanakijiji wote walibaki wameshika midomo hakuna alieamini yaliyotokea.

“Haiwezekani Lisa mke wangu yupo wapi Lisaaaaa”

Muthan alikuwa kama amezinduka sasa akili yake iiyoka kwenye ufungwa wa dawa aliyopewa na Shamima

“Namtaka mkewangu mama mkewangu babaa mkewangu yupo wapi nampenda bado”

Muthan alilia sana hakuamini hasira zilimpanda akatoka mbio kwenda ndani aliporud alikuwa na pamba akitaka kumkata nalo Shamima bahati nzuri watu wakamzuia nakumtorosha Shamima na mwanaume wake

“Ondokeni mshaikosea mizimu hamfai kuishi apa na sitak kumwaga damu yenu”

Alisema Mfalme Odinga, adhabu yao ilikuwa ni kifo lakini hakutaka kuona ilo linatokea akaamua hawafukuze kwenye milki yake.

Muthan alibaki mnyonge hakuwa na raha kabisa alimlaumu sana Millar kumchukua mke wake hakuwa na jinsi kuukubali ukweli akaanza maisha mapya hakutamani tena kuwa na mwanamke.


Siku zilizidi kusonga mimba yangu ikiwa kubwa, nilishazoea maisha ya kifalme sikutaka tena kurudi nyumbani kwetu.

Siku zilizidi kusonga adi nilipofikisha miezi tisa yakujifungua, uchungu ulinishika sana wakaitwa wakunga waje kunizarisha mara chupa ya uzazi ikapasuka

“Mama weee mwanangu amekufa”

Nilipiga kelele

“Sio mwanao iyo ni chupa ya uzazi aya lala chali”

Alisema mwanamke mmoja sababu walikuwa watatu.

Basi nikaelekezwa jinsi yakukaa hatimae nikafanikiwa kuzaa mtoto mzuri wa kiume.

“Wee Lisaaa amka uko ujiandae saa mbili hii umelala tu”

Mara nikasikia sauti ya mama inanisemesha

“Uyu mama nae kaletwa na nani uku kwenye ufalme?”

Nikajiuliza mara nikashtuka nipo kitandani kwangu kwetu ubungo sipo ufalmeni wala sina mtoto

“Haaa inamaana nilikuwa naota au?”

Nilijiuliza nilipojiangalia kitandani nimejikojolea kumbe ile chupa ya uzazi iliyopasuka ndo mikojo loh nilitoka mbio adi bafuni nikaoga nakubadirisha mashuka fasta nikajindaa nakutoka na begi langu mkononi.

“Shikamooni”

Niliwasalimia wote walikuwa wamekaa mezani wanakunywa chai nikajiunga namimi tulipomaliza tukapanda gari wote baba,mama, na kaka Gedion safari ikaanza yakwenda Songea kwa bibi nyumbani tulimuacha Leah yule mfanyakazi.

“Ile ndoto jaman adi raha eeh mungu ifanye iwe kweli”

Niliongea nikiwa nimekaa kwenye siti ninamawazo yangu apo kumbe Gedion alinisikia sababu tulikaa nyuma baba na mama wapo mbele dereva ndo baba.

“Wewe Mrembo mcharuko unasemaje?

Akaniuliza

“We acha shogayangu nimeota ndoto nzuri iyo”

Nilijisahau kakayangu nikamuita shogayangu wee alinitandika kofi ilo adi nikapiga kelele

“Mnaanza ujinga wenu nyie watoto?”

Mama akasema

“Si uyu Lisa ananiita mie shogayake”

Gedion akanisemea

“Uyo Lisa ni chizi ngoja tukamuache uku kijijini leo nimeshamchoka”

Baba alisema nilichukia

“Bora ile ndoto iwe kweli tu nikakae kwa wafalme”

Nikajisemea kimoyomoyo uku gari linazidi kwenda.

Gari zikazidi kwenda adi tukafika maeneo ya kitonga kabla yakupandisha ule mlima kuna Restaurant tukashuka apo, nakwenda kupata chakula kulikuwa na nyama nyingi za kuchoma mishikaki kibao niliisi kupagawa nilivyoona basi baba akasema tuagize nikachukua mishikaki ishirini na ndizi tano zakuchoma.

“Heee mishikaki yote iyo?”

Gedion akaanza umbea wake

“Yangu haikuhusu”

Nilimjibu nikaachana nae nakukaa pembeni kula baba na mama waliniangalia bila kunisemesha.

Basi kaka Gedion nae akajifanya sharobaro akachukua mishikaki miwili na ndizi moja akaja nilipo tukakaa wote

“Dah Lisa niongeze mshikaki”

Alisema nilitamani kucheka

“Nyoo si umejifanya sharo wewe sikupi mishikaki yangu”

Nilimwambia mwenyewe alipendeza lakin kakangu handsome wa nguvu mama alijua kuzaa mbona.

Basi nikampa mitatu na ndizi mbili tukala apo nakumaliza tukaingia kwa gari safari ikaanza tena.

“Eeh mungu tenda miujiza ndoto itimie”

Nikasema tulipokuwa tunapanda huo mlima kitonga.

“Yani kama gari lipinduke tudondoke kule chini alafu watokee walinzi wanichukue nipelekwe kwa Mfalme”

Nilisema kwa sauti wote wakasikia.

“Wewe mtoto maneno gani ayo ya ajabu unasema?”

Mama akauliza

“Lisa Lisa wewe jini makata usiejielewa nitakukata kichwa chako”

Baba akaanza maneno yake anafoka balaa

“Basi mumewangu yaishe kuwa makini tusijekupinduka kweli”

Mama nae akanitetea nakumpandisha hasira baba zaidi

“Unamtetea uyu mwanao maneno gani ayo anasema ivi Mama Lisa uyu mtoto ulimzaa wewe au hospital walikubadirishia maana sielewi naisi mwanangu alikufa ukaiba uyu mtoto”

Baba alizidi kufoka ugomvi ukaibuka kwao

“Maneno gani ayo mumewangu unasema jamani mbona unanikosea mimi?”

Waliendelea kulumbana sikutaka ata kuwasikiliza nikampokonya headphone Gedion alizovaa nikaweka kwangu nakusikiliza nyimbo adi nilipopitiwa na usingizi.

Safari ilikuwa ndefu sana adi jioni giza limeingia ndio tukafika kwa bibi ilikuwa mara yangu ya pili kwenda mwanzo nilikuja nikiwa mdogo miaka nane sijui.

Basi tulipokelewa kwa furaha na bibi yangu

“Waoo mke mwenza uyo umekuwa mama jaman”

Bibi alisema tukakaribishwa ndani

“Umeona bibi eeh nimekuwa mkubwa eti adi sasa baba ananipiga”

Nikamwambia nakumfanya bibi ashangae

“Haya kisa nini kunipigia mjukuu wangu?”

Akamuuliza baba wee nilifurahi nikatamani nimbebe juu bibi yangu.

“Mama uyo mtoto ni mtukutu, jeuri hana adabu ata kidogo”

Baba nae akasema

“Atakama sio umpige unamkomaza bure mwambie tu kwa maneno”

Bibi aliendelea kunitetea basi wakaongea apo mwisho tukakaribishwa ndani tena maana tulikuwa nje bado

Bahati nzuri nyumba kubwa kila mtu akapewa chumba chake.

Baada ya apo tukakaa sebuleni nakula chakula tulikuta ameshatuandalia mimi nilipomaliza kula tu nikaenda chumbani kwangu kulala nikawaacha apo baba anatoa mashtaka yangu sikutaka ata kusikiliza nilishamchoka tena nikajifungia mlango kabisa wasije kuingia ndani.

Basi nililala adi Asubuh kulipokucha nikaamka saa tatu nakuta nyumba kimya nikashangaa imekuwaje,

“Bibiiii we bibiii weeee”

Nilianza kumuita nikamuona anatoka jikoni

“Hee ndo unaamka jana ulichoka sana? Wazazi wako wameshaondoka”

“Afadhali wameenda”

Nilisema nakukaa chini bibi akacheka

“Aya ujambo lakin?”

“Sijambo shikamoo”

“Marahaba kaoge basi uje kunywa chai”

Alinambia nikainuka nakwenda kuoga kisha nikatoka nimevaa kanga apo ndani nina chupi tu.

“Bibi kweli wameondoka hao watu?”

Nilimuuliza

“Watu gani tena?”

“Si baba Gedion na mkewe na mtoto wao?”

“Hee makubwa kwaiyo we sio babayako?

“Bibi acha tu simpendi baba kilasiku ananipiga tu bila kosa ananipiga ata naisi sio babayangu yule hanipendi kabisa”

Niliongea kwa uchungu mwenyewe adi machozi yalinitoka.

“Basi mjukuu wangu usiseme ivyo yule babayako mzazi mzoee tu”

“Sawa ila mi nyumbani sirudi nakaa uku uku”

“Sawa hamna tatizo tutaishi wote”

Basi tuliongea na bibi yangu apo tukapatana wenyewe, nikanywa chai adi nilipomaliza nikainuka kupeleka vyombo jikoni

“Wee Lisa iyo kanga ndani umevaa nini?”

Bibi aliniuliza

“Bibi naniliu bwana si unaona joto?”

“Ujue wazazi wako wametoka kuangalia mashamba yao uko Mpitimbi muda wowote wanarudi pia kakayako yupo ndani sasa aje kukuona na iyo kanga moja jamani itakuwaje?”

“Bibi uyo Gedion anamademu kabisa kwaiyo kuniona mie ata si ajabu”

Basi nikamwambia nakwenda jikoni nimamkuta msichana anapika

“We mambo”

Nilimsalimia nikimshangaa maana sio ndugu yetu

“Poa ujambo mdogo angu?”

Loh eti mie mdogo wake alinichefua katika kitu sipendi mtu anidharau eti mie mdogo

“Mfyuuuuu mdogo wako nani yani nimekustahi tu kukupa salamu ukajiona bonge la mjanja mie ukaniona boya eeh eti mdogo wangu loh huna haya wala ujui vibaya mja mtoka pabaya na bichwa lako kama tikiti maji”

Nilimporomoshea kichambo mdada wa watu adi akaangua kilio kilichomshtua bibi akaja jikoni, Mara nasikia honi inalia wazazi wangu wanarudi nao

“Kunanini uku jikoni we Suzy unalia nini?”

Bibi akauliza

“Amna bibi amejikata na kisu”

Nikamjibu mie apo

“Ooh pole basi ngoja niangalie hao waliokuja”

Alisema nakutoka nje nikamsogelea Suzy sasa

“Nisamehe dadangu usiseme nimekuchamba babangu mkorofi uyo kama kazaliwa porini usiseme nitakupa pesa ila unizoee mimi ndio nilivyoumbwa”

Nilimwambia nikimbembeleza akanielewa mwenyewe basi tukaanza kupiga story apo uku nikijishaua kumsaidia kazi eti

Mara mama nae akaja jikoni nakunishangaa

“Hee Mrembo mcharuko leo unasaidia kazi makubwa”

Alisema akicheka

“Mama nawe sasa umefata nini uku?”

“We mtoto koma nisiingie jikoni kisa nini?”

Alienda kwenye friji akachukua matunda nakutoka zake, basi Suzy akapika apo adi alipomaliza nikamsaidi kutenga mezani wakaanza kula.

Siku iyo walishinda apo apo adi usiku nikaitwa na baba kikao niliwekewa.

“Lisa kesho tunaondoka nakuomba ukae vizuri na bibi yako umapepe wako uache ole wako nisikie umemsumbua nitakuja kukukata maskio ayo”

Baba akaanza mikwala yake,

“Mwanangu utulie usimsumbue bibi yako”

Mama nae akasema mara Gedion akadakia

“Ndio Lisa umsikilize bibi”

Nilimkata jicho baya ilo maana anajifanya mwema mbele ya wazazi kumbe ovyo adi wanawake anao.

Basi wakaongea apo adi walipotosheka wenyewe mimi nikawaaga nakuingia chumbani kulala.

“Yani mimi ilikuwa nizaliwe marekani uku bongo bahati mbaya tu uyu baba kama apate ajari afe sijui lipoje kwanza naisi alizaliwa vita kuu ya dunia ananikera ningejua anapoishi Izraeli mtoa roho ningempelekea pesa aje achukue roho yake”

Nilikuwa naisi naonewa sana nilimchukia baba kuliko shetani.

Basi nililala adi asubuhi niliposhtuka mlango unagongwa nikaamka kufungua ni mama

“Mwanangu sisi ndio tunaondoka ubaki salama shika hii pesa utakusaidia”

Alinipa elfu hamsini nikamshukuru mamangu mara baba nae akaja

“Kwaheri ndo tunaondoka ivyo”

“Sawa safari njema”

“Aya”

Akasema nakuondoka

“Hee baba ndo unipi pesa?”

“Wewe oesa yanini kilakitu kipo apa?”

“Kwaiyo nikiwa na tatizo nitoe wapi pesa?”

“Tatizo gani mtoto mdogo wewe?”

“Nikiwa kwa siku zangu je chu..

Kabla sijaendelea mama akaniziba mdomo.

“Aibu mwanangu kumwambia babayako ivyo loh jaman Lisa utakuwa mkubwa lini mungu wangu mie”

Mama nae akaanza kulalamika

“Ameyataka mwenyewe mi namuomba pesa ataki adi ajue nataka za nini sindo nimemwambia”

Baba alijua kosa lake hakusema kitu akaingia mfukoni nakutoa wallet yake akanipa elfu therathini, basi tukaagana apo kisha wakapanda gari nakuondoka.

Nilishukuru walivyoenda nipumzike kipigo sasa, ilikuwa bado mapema saa kumi na mbili asubuhi nikarudi tena kulala adi saa tatu ndo niliamka.

“Shikamo bibi”

“Marahaba ujambo?”

“Sijambo mbona umependeza asubuhi yote hii safari ya wapi?”

Nilimkuta anakunywa chai kapendeza na gauni lake la kitenge alafu bibi yangu nae kajaaliwa anamshepu wa nguvu adi raha.

“Kanisani kwani ujui leo jumapili?”

Aliposema ivyo nikazusha ugonjwa apo apo

“Mama weeee kiuno kinauma uuuuhh bibiiii”

Nikaanza kulia nakumshtua

“Wewe lisa nini tatizo?”

Bibi akanikokota adi chumbani nikafikia kulala nikijifanya kweli naumwa.

Akatoka nakwenda kumuita Suzy

“Baki umuangalie Lisa mie naenda kanisani”

Alimwambia nakuondoka nililaa kama nusu saa nikaamka

“Unaenda wapi?”

Akaniuliza Suzy

“Naenda kunywa chai njaa inaniuma”

“We si mngonjwa lakini?”

“Kwaiyo kama mgonjwa nisile nife eeh ata kuuguza ujui baada uniletee chakula umekaa tu apo”

Nilimjibu nikatoka nakwenda jikoni kuchukua chai nikanywa.

“Suzy ivi wapi wanakodisha cd za movie?”

Nilipomaliza kula nikamuuliza

“Kule juu barabarani”

“Sawa ngoja nichukue pesa twende tukakodi tuje kuangalia”

Basi niliinuka nakuingia chumbani nikachukua elfu tano tukatoka nakuelekea uko wanapokodisha izo cd.

Nilikuwa naangalia mazingira ya iyo mitaa sijui kunaitwaje mi bado mgeni sikujua bado.

Basi tukafika kwenye fremu moja tukaingia apo tulikuta wakaka watatu wamekaa wanacheki movie kwenye Laptop

“Mambo zenu”

Suzy aliwasalimia mi ndo ata muda wakusalimia nilikuwa sina.

“Aah poa warembo karibuni”

“Asante”

Alijibu, basi nikawa bize kuchagua zangu cd nilipenda sana zakiindi

“We mkaka ile cd aliyoekti Sonil sheti ipo wapi?”

“Inaitwaje iyo?”

“Bwana sijui jina we tafuta nipe”

Basi akainuka mmoja nakunisaidia kutafuta

“Mmmh we mdada umebarikiwa jamani”

Alisema uyo mkaka sikumjibu na wenzake pia wakaniangalia vizuri kumbe mwanzo hawakuniona walikuwa bize kucheki movie

“Ee bwana dah mtoto mbona kajazia sana kama mlima kitonga duh”

Basi wakaanza kunisifia apo wote wakainuka kanisadia kutafuta izo cd

Suzy alibaki anawatizama tu hao wakaka walivyopagawa na umbo langu tena kama kawaida nina kanga moja tu na juu nilivaa kitop kilinibana.

“Naomba namba yako ya simu”

Mmoja akasema

“Sina ata simu mie”

“Dah basi poa badae jioni njoo nina zawadi yako oya nyie shemeji yenu huyu sitaki shobo”

Aliwapiga mkwara wenzake nikamjua uyo ndo mwenye iyo library sijui yakukodisha izo cd basi nikamuitikia.

“Yani nimekupenda ata pesa sikudai”

Alisema nilifurahi nikashukuru pesa yangu imepona nikachagua movie karibu cd kumi bure kabisa baada ya apo tukaondoka zetu nakuacha gumzo uku nyuma wakiniongelea.

“Twende dukani tukanunue soda”

Nilimwambia Suzy

“Mmmh ila Lisa wewe noma cd zote bure ningekuwa mimi ningeogopa”

“Kwani nimeiba si mwenyewe amenipa atanibaka au si adi nikubali kulala nae”

Nilimjibu tukizidi kutembea, njiani wanaume wakware hawakuacha kuniangalia maana iyo vibration nyuma si mchezo.

Basi tulifika tukanunua soda nakurudi nyumbani tukaweka cd nakuangalia adi jioni tulikesha tunaangalia cd tu Suzy akaingia kupika mie habari sina aliivisha tukala nakuzidi kutizama adi bibi aliporudi.

“Hee makubwa aya izo cd mmezipata wapi?”

“Nilikuja nazo bibi”

“Ooh sawa”

Akaingia ndani Suzy wacha acheke

“Yani Lisa wewe”

Basi siku iyo ikapita kesho yake ikafika bibi akasema babangu mdogo aliekuwa chuo mbeya anarudi tujiandae tukampokee na uyo baba atasikuwahi kumuona mie.

Basi ilipofika muda tukaenda stand nakumpokea nilijua mkubwa kumbe mkaka tu miaka ishirini na tano sijui, basi tukarudi nyumbani.

Siku zikazidi kusonga nilipata mashoga mitaani nikawa naenda kuzurura uko adi jioni narudi.

Basi ikafika December sikukuu ya Christmas nikatoka na marafiki zangu Nora na Maureen tukaenda club kwa mara ya kwanza nikaingia club wezangu wakaagiza pombe wakanishawishi namimi ninywe marafiki wabaya jamani wanapotosha.

Basi nikanywa adi nililewa wenzangu wakapata mabwana nakunikimbia nikabaki pekeyangu ata sijielewi nimelewa hatari akatokea mwanaume mmoja akanichukua nakunipandisha kwenye gari tukaondoka adi lodge alipochukua chumba tukalala humo yote yalitokea sijielewi nimelewa vibaya ndo mara ya kwanza kunywa pombe.

Asubuhi sasa kulipokucha nikaamka pombe apo zimeisha nikajishangaa nipo wapi mara sijakaa vizuri namuona mwanaume kajifunga taulo anatoka chooni nilishtuka kumuangalia usoni ni babayangu mdogo Dominic

“Haaaaa baba”

ITAENDELEA

Mrembo Mcharuko Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment