Mwajuma Utamu Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA: JUMA HIZA
*********************************************************************************
Chombezo: Mwajuma Utamu
Sehemu ya Kwanza (1)
Nakumbuka ulikuwa ni mwaka 2010, nilipata bahati ya kufanya kazi za ndani katika nyumba moja iliyokuwepo maeneo ya Kijitonyama. Ilikuwa ni familia ya Mzee Gidion pamoja na mke wake ambapo katika maisha yao walifanikiwa kupata watoto wawili, mtoto wa kwanza alikuwa ni wa kiume aliyejulikana kwa jina la Daniel na mwingine wa mwisho alikuwa ni wa kike aliyejulikana kwa jina la Naomi.
Mzee Gidion alikuwa akimiliki kampuni moja hapa mjini iliyomuingizia kiasi kikubwa cha pesa, aliishi maisha mazuri yeye pamoja na familia yake.
Baada ya kupita miezi mitatu tangu nilipoanza kufanya kazi za ndani katika nyumba hiyo Mzee Gidion alianza kunitamani, alichokuwa akikihitaji ni penzi langu tu, aliahidi kunifanyia mambo mengi sana katika maisha yangu endapo kama ningekubali ombi lake la kulala naye kitanda kimoja.
Kiukweli lilikuwa ni jambo gumu mno hasa ukizingatia mke wake ndiye aliyenileta katika nyumba hiyo kwa lengo la kufanya kazi, sikuwa tayari kumkubalia ombi lake lakini kutokana na tamaa za pesa zilizoniingia nikajikuta nikimkubalia na kuanzisha mahusiano naye ya kimapenzi.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kushiriki mapenzi tangu nizaliwe, Mzee Gidion ndiye alikuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu, alionekana kufurahishwa sana na kitendo hicho, kwanza hakutegemea kama angeweza kunikuta na usichana wangu mpaka kufikia umri wa miaka ishirini niliyokuwa nayo, hilo lilizidi kumfurahisha mno.
Niliendelea kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Mzee huyo ambaye aliniambia nilitakiwa kufanya siri, hakutaka mke wake afahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alinitahadharisha niwe makini kwani kama mke wake angeweza kufahamu mahusiano yetu ningejiingiza katika matatizo makubwa.
Hilo halikuwa tatizo, niliendelea kuwa katika mahusiano na Mzee Gidion huku penzi lake likizidi kuniteka. Ukumbuke kuwa Mzee Gidion ndiye alikuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu, alikuwa amenifungulia dunia mpya ya mapenzi, hapo kabla nilikuwa ni mtu wa kuyasikia mapenzi jinsi ambavyo watu walivyokuwa wakiyasifia pamoja na utamu wake, sikuwa nikifahamu lolote kuhusu mhemko na raha ambazo mtu alikuwa akizipata wakati akifanya mapenzi.
Tangu nilipofanikiwa kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza na Mzee Gidion nilijihisi kuwa kiumbe kipya, nilijiona kukamilika kuwa msichana.
Kipindi hicho Mzee Gidion alianza kunijali, alikuwa akinipa kiasi cha pesa chochote nilichokuwa nikikihitaji.
“Msichana mrembo kama wewe unatakiwa uwe na simu kali, upendeze yaani ubadilike, uishi kimjinimjini, nitahakikisha nayabadilisha maisha yako Mwajuma,” aliniambia Mzee Gidion.
“Nitashukuru Baba,” nilimwambia.
“Usiniite Baba, sifananii kuwa Baba yako mzazi hata wa kuchorwa, niite mpenzi au Gidion tu inatosha,” aliniambia.
Kwa kumtazama Mzee Gidion alionekana kuwa Baba yangu kabisa, alikuwa ni Mzee wa makamo ambaye alifanikiwa kuwa na watoto wawili. Kipindi hicho Daniel ambaye ndiye mtoto wake wa kwanza alikuwa akisoma chuo kikuu cha Daresalaam, alikuwa akisomea sheria, ulikuwa ni mwaka wake wa pili.
Kwa upande wa Naomi alikuwa kidato cha tatu, alikuwa akisoma Morogoro katika shule moja ya bweni, maisha yake yote yalihamia huko mpaka wakati wa likizo ulipofika ndipo ambapo aliweza kurudi nyumbani.
Unaweza ukaona jinsi ambavyo maisha yalivyokuwa katika nyumba hiyo, kila mtu alionekana kuwa bize na mambo yake, kuanzia Mama, Baba na watoto, muda mwingi nilibaki peke yangu nyumbani.
Mzee Gidion aliitumia nafasi hiyo kuwa fursa ya kuwa karibu na mimi. Aliamua kuninunulia simu kwa lengo la mawasiliano, alihitaji kuwasiliana na mimi zaidi na zaidi.
Siku ziliendelea kukatika huku penzi kati yangu na Mzee Gidion likizidi kupamba moto. Alipanga kuninunulia nyumba pamoja na gari la kifahari kwa dhumuni la kunihamisha nyumbani hapo, hakutaka kuona mapenzi yetu yakiendelea kuwa siri, alinogewa na utamu wa penzi langu.
Nilijisikia furaha sana kusikia hivyo, niliamini huo ndiyo ulikuwa mwanzo wangu wa kusahau umasikini niliyotoka nao nyumbani kwetu Mtwara.
Kila kitu kilichokuwa kikiendelea kiliniweka katika wakati wa furaha sana, nilizidi kumpenda Mzee Gidion, nilisahau kama alikuwa ni mume wa mwanamke aliyenitoa kijijini na kunileta mjini kwa lengo la kufanya kazi, ahadi nilizowaahidi wazazi wangu pamoja na kiapo nilichokiapa mbele yao kwa wakati huo nilikuwa nipo kinyume kabisa.
Katika kipindi hicho ambapo nilikuwa katika mapenzi na Mzee Gidion, Daniel mtoto wa Mzee huyo na yeye alianza kunitamani, sijui nilimvutia na nini ila nilishangaa akinitongoza, alionekana kunihitaji kupita maelezo.
“Daniel embu acha kunitania bhana,” nilimwambia huku nikionekana kutomuamini kabisa.
“Sikutanii Mwajuma kweli nakupenda, nahitaji kuwa na wewe,” aliniambia Daniel.
“Umenipendea nini sasa?” nilimuuliza.
“Vingi tu vingine siwezi kukuambia,” alinijibu.
Unajua kwanini sikuweza kumuamini Daniel? Kwanza alikuwa ni mtoto aliyetokea katika familia ya kitajiri, alikuwa ni msomi ukiachana na mimi ambaye nilifeli kidato cha nne, pili alikuwa ni handsome, alivutia mno, kwa kumtazama ilikuwa ni vigumu kuamini mvulana kama yeye kukosa msichana.
Alinisumbua sana, kila siku ombi lake lilikuwa ni moja, kuna kipindi nilimuonea huruma alipoingia chumbani kwangu kisha akawa ananibembeleza nimkubalie. Haikuwa rahisi kumkubalia kwani tayari nilikuwa katika mapenzi mazito na Baba yake na tulikuwa kwenye mipango mingi, nilikuwa nikisubiria itimie.
“Hapana Daniel siwezi kukubali hilo litokee wewe ni kama kaka yangu,” nilimwambia Daniel.
“Mwajuma nakupenda, macho yangu yamekutazama wewe, una kila sababu za kuwa na mimi, umeuteka moyo wangu wa mapenzi tafadhali naomba usiuumize nitakufa,” aliniambia Daniel huku machozi yakimlengalenga.
Nilishindwa kuvumilia kumuona Daniel akiendelea kuteseka kwa ajili yangu, nilimuonea huruma sana, mwisho wa siku nikajikuta nikishawishika na kumkubalia tukawa wapenzi.
Daniel alifurahi sana, hakuamini kama alifanikiwa kunipata huku nyuma ya pazia hakujua nini kilichokuwa kikiendelea kati yangu na Baba yake.
Kitendo cha kumchanganya Baba na mtoto kimapenzi hakika kilikuwa ni hatarishi sana, sikutaka kumwambia lolote Daniel, nilihofia mambo mengi mabaya ambayo yangeweza kunitokea.
Nilizidi kufaidi utamu wa penzi la Baba na mtoto huku kila mmoja kwa nafasi yake akikiri kunipenda kupita kawaida.
Siku ziliendelea kukatika, Mzee Gidion alianza kuingiwa na wasiwasi juu yangu, alihisi kuna mchezo mchafu ambao nilikuwa nikimchezea, hakutaka kuamini jambo hilo hata mara moja, alianza kufanya uchunguzi wake na mwisho wa siku akafanikiwa kugundua kuwa nilikuwa nikitembea na mtoto wake. Hilo lilimuumiza sana, alinilaumu mno. Naweza kusema siku hiyo ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kumuona mwanaume mtu mzima kama Mzee Gidion akilia mbele yangu huku sababu ikiwa ni mapenzi, hakutaka kuamini kama yeye pamoja na mtoto wake walishiriki mapenzi na mimi.
Mzee Gidion alipagawa, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, moyo wake ulimuuma mno, aliponitazama alionekana kuwa mwenye hasira, machozi yalikuwa yakimdondoka kwa wakati huo.
Nilishindwa kuamua la kufanya kwani mpaka kufikia muda huo nilikuwa tayari nimeshafanya makosa. Kwanza nilikuwa nikitembea na mume wa mtu kwa kujua, pili niliwachanganya kimapenzi baba na mtoto. Haya yalikuwa ni makosa ambayo kiukweli sikuwahi kukaa na kuwaza kwamba kuna siku yangeweza kunigharimu maisha yangu.
Nilishindwa kuvumilia kumuona Mzee Gidion akiendelea kulia mbele yangu kama mtoto mdogo, ilibidi nimsimulie kila kitu kilichotokea kwa Daniel mpaka nikajikuta nikimkubalia na kuwa wapenzi, sikuacha kumuomba msamaha kwa kosa nililokuwa nimelifanya, nilikiri kukosea na kumuahidi kutorudia tena makosa.
Baada ya kumueleza hayo pamoja na kumuomba samahani Mzee Gidion hakutaka kunielewa kabisa, alinichukia, alinifananisha na kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima.
Hilo lilizidi kuniumiza mno, kitendo cha kuniita kahaba ambaye nilikuja kwenye familia yake kwa lengo la kutembea na ukoo mzima hakika kiliniumiza sana, moyo wangu ulikuwa kwenye maumivu makali mno.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuishi maisha ya visasi kila siku, Mzee Gidion alikuwa ni mtu wa kunitishia maisha, alinikosesha amani ya moyo niliyoishi nayo kwa muda mrefu, sikuwa huru tena, muda wote nilikuwa nikimfikiria pamoja na vitisho alivyokuwa akinipa.
Kuna kipindi nilitamani kumueleza mke wake ukweli wote wa kile kilichokuwa kikiendelea kati yangu na mume wake lakini unafikiri ningeanzia wapi? Ningeupatia wapi ujasiri huo wa kumueleza kila kitu na wakati hapohapo tayari nilishamkosea kwa kitendo cha kutembea na mume wake.
Hiyo iliendelea kubaki siri ya moyo wangu, siri iliyokuwa ikinitesa mno. Mzee Gidion hakuacha kushiriki kufanya mapenzi na mimi, aliendelea kunitumia kimwili lakini safari hii haikuwa kama hapo awali, alibadilika na alikuwa akifanya mapenzi na mimi kama sehemu moja wapo ya starehe, yaani alinifanya kuwa kama kahaba ambaye alinitumia wakati alipohitaji kufanya mapenzi tu. Hilo liliniumiza sana, siwezi kusema ni maumivu kiasi gani niliyokuwa nayo katika moyo wangu lakini naweza kusema tamaa zangu za pesa ndizo zilizonipelekea nipitie katika wakati huu mgumu.
Daniel alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuigundua tofauti yangu japo Mama yake alianza kuniuliza kuhusu mabadiliko yangu lakini nilimficha, sikutaka kumueleza ukweli.
“Niambie nini kinachokusumbua mpenzi, malaika, mke, malkia wa maisha yangu,” aliniuliza Daniel.
“Hakuna kitu,” nilimjibu.
“Usiniambie hakuna kitu wakati nikikuangalia nakuona kabisa kuna kitu unanificha,” aliniambia.
“Kweli hakuna kitu.”
“Usinifiche tafadhali.”
“Naogopa kukuambia Daniel.”
“Unaogopa nini wewe niambie au mimba imengia?”
“Hapana bora ingekuwa mimba ningejua baba yake yupo.”
“Ni nini sasa?”
“Ni kuhusu baba yako.”
“Amefanyaje?” aliniuliza Daniel kisha nikaanza kumsimulia kila kitu. Nilipomaliza kumsimulia nikamuona akivuta pumzi ndefu na kuziachia kwa pupa, kama ilivyokuwa kwa Baba yake na yeye pia hakutaka kuamini, kitendo cha kuwachanganya kimapenzi na Baba yake kilimuumiza mno.
Nilishangazwa na maamuzi aliyoyachukua Daniel, hakutaka kuendelea kuushuhudia uchafu kama huo ukiendelea mbele yake, alichoamua kukifanya ni kuniambia kuwa siku hiyo ndiyo ulikuwa mwanzo na mwisho wa mapenzi yetu, hakutaka kusikia nikimuita mpenzi tena.
Niliumia sana baada ya Daniel kuchukua maamuzi hayo, mtu ambaye niliamini ndiye angeweza kuwa msaada wangu kwa wakati huo hakutaka kunisikia hata mara moja.
Maisha yalibadilika ndani ya nyumba, kila siku nilikuwa ni mtu wa kumuomba Mungu aninusuru na mabaya ambayo yangeweza kunitokea. Nilifahamu hapakuwa na amani tena, kuanzia Baba na Mtoto wote walikuwa na visasi juu yangu, hawakunitazama kwa macho ya wema tena, nilionekana kuwa mbaya tena adui mkubwa ambaye walitakiwa kuniepuka.
Vitisho havikuishia hapo, Mzee Gidion aliendelea kunitishia kuniua kila kukicha, wakati mwingine alikuwa akiniambia ni lazima niondoke katika nyumba yake nikiwa maiti ndani ya jeneza.
Wakati yote haya yakiendelea mke wake alikuwa hafahamu lolote, iliendelea kubaki siri katika moyo wangu mpaka pale nilipoanza kukosa uvumilivu, nilitishiwa sana, sikuwa na amani tena katika moyo wangu, uhuru wangu wote ulipotea, nilikuwa nikiishi maisha kama ya mfungwa aliyetoroka gerezani.
Wazo la kutoroka likanijia kichwani, nilichokuwa nikikiwaza kwa wakati huo ni kutoroka na kwenda mbali. Sikuwa mwenyeji wa jiji la Daresalaam, tangu nilipoweza kufika kwa mara ya kwanza maisha yangu yote yalikuwa ni ya kukaa ndani, labda siku moja moja za wikiendi niliweza kupata bahati ya kupelekwa katika fukwe za Coco ambapo hata njia ya kufikia huko nilikuwa siifahamu.
Nadhani unaweza ukaona ni kwa jinsi gani nilivyokuwa mgeni katika jiji hili. Wakati ambapo nilikuwa sifahamu mtaa hata mmoja tayari nilikuwa nimejiwa na wazo la kutoroka. Unafikiri nilifanikiwa katika mpango huu? Jibu ni hapana, niliendelea kujiuliza maswali ambayo yalizidi kuniumiza kichwa.
Ni katika kipindi hicho ambapo kumbukumbu za nyumbani kwetu zikaanza kunijia, nilipakumbuka mno, nilitamani kuambiwa kuwa nilitakiwa kurudi nyumbani kwetu lakini jambo hilo halikuweza kutokea hata mara moja.
Nitaishi maisha ya vitisho mpaka lini? Hili lilikuwa ni swali lililoniumiza usiku na mchana, nilikosa wa kumsimulia maisha niliyokuwa nikiyapitia kwa wakati huo.
Baada ya kupita mwezi mmoja huku nikiendelea kuishi maisha ya vitisho, siku moja majira ya usiku Mama Daniel aliniita na kuniambia kuwa alifahamu kila kitu kilichokuwa kikiendelea, aligundua kuwa nilikuwa nikitembea na mume wake jambo ambalo lilimuumiza mno.
“Mwajuma msaada wangu wote niliyokusaidia katika maisha yako leo umeamua kunilipa kwa kutembea na mume wangu kweli?” aliniuliza, wakati huo machozi yalikuwa yakimbubujika mashavuni mwake.
“Hapana Mama nili….” kabla sijamaliza kuzungumza alinikata kauli, nilishtukia nikipigwa kofi moja zito lililoniyumbisha, wakati nikiendelea kuugulia maumivu ya kofi, hakuishia hapo, alianza kunipiga kila sehemu ya mwili wangu huku akinilaani kwa kitendo nilichomfanyia. Nilipata maumivu makali mno, siwezi kuyaelezea maumivu niliyokuwa nikiyapa, nililia sana, nilimuomba kila aina ya msamaha lakini sikuweza kuambulia jibu lolote zaidi ya kipigo kikali kama cha mbwa koko na mwisho wa siku aliweza kunifukuza.
Nilifukuzwa kama mbwa usiku huo, nilitupiwa begi langu la nguo na kupewa kila kilichokuwa changu. Nililipwa pesa yangu ya mshahara wa mwezi uliyopita niliyokuwa nikidai pamoja na mwezi huo ambao niliweza kulipwa nusu yake.
Hakukuwa na mtu ambaye alinisaidia siku hiyo, nilionekana kuwa mbaya kupita kawaida, niligeuka kuwa adui. Kuna muda nikatamani nimwambie kila kitu kuhusu mume wake lakini nilikosa muda huo, tayari nilishafukuzwa na sikuhitajika tena kuwemo katika familia hiyo.
Sikujua nilitakiwa kwenda wapi usiku huo, nilipolifikiria hilo nikazidi kuchanganyikiwa.
Nilijutia mambo mengi mno lakini kubwa nililolijutia ni hili la kutembea na mume wa mtu, tamaa yangu ya pesa iliniponza na kuniweka katika wakati mgumu ambao sikutegemea kuupitia.
Machozi yalikuwa yakinidondoka muda wote, kila hatua niliyokuwa nikiipiga njiani nilipishana na watu wengi, baadhi yao walinishangaa kutokana na muonekano niliyokuwa nao, ulitosha kabisa kunielezea kuwa nilifukuzwa na muda huo nilikuwa katika safari nisiyoifahamu mwisho wake.
Nilitembea umbali mrefu sana mwisho nilichoka, sikuwa nikifahamu sehemu hiyo au mtaa huo niliyokuwepo uliitwaje.
Niliwaona wanaume wawili wakinifuata nyuma yangu, mwanzo sikutaka kuogopa kitu kwani kulikuwepo na watu wengi niliyopishana nao hivyo niliamini kuwa salama lakini nilipofika eneo hilo nilishangaa nikiwa peke yangu, hakukuwa na mtu niliyepishana naye zaidi yangu na hao wanaume wawili waliyokuwa wakinifuata.
Nilianza kuingiwa na wasiwasi baada ya kuwaona wakizidi kukazana kunifikia, moyo wangu ukalipuka paaa!! hofu ikanitawala, mapigo ya moyo wangu yakaanza kunienda kasi.
“Habari yako binti,” alinisalimia mwanaume mmoja huku yule mwingine nikimuona akiangalia huku na kule, nilifahamu hawakuwa na nia nzuri na mimi. Hofu ikazidi kunitawala.
“Nzuri,” nilijibu huku nikitetemeka.
“Mbona unaogopa usiogope sisi ni watu wazuri unaitwa nani?” aliniuliza yule mwanaume mwingine.
“Naitwa Mwajuma,”nilimjibu.
Walitazamana kisha wakapeana ishara fulani, sikujua walimaanisha nini ila nikashangaa wakinisogelea, ghafla! yule mwanaume wa kwanza akanirukia na kunikaba, nilishtukia nikipigwa na ubapa wa panga kwenye paja na kuambiwa nisipige kelele na endapo kama ningekiuka agizo hilo ningeweza kuuliwa, niliogopa mno, nilibaki nikiugulia maumivu ya ubapa wa panga pamoja na kabali niliyokuwa nimepigwa.
Yule mwanaume mwingine alianza kunisachi, akachukua simu, pesa pamoja na lile begi la nguo. Alipojiridhisha kuwa alifanikiwa kuchukua kila kitu changu alimpa ishara mwenzake na ndipo hapo alipoweza kuniachia.
“Sasa sikia wewe fala ukipiga kelele tunakuua, kaa kimya hivyohivyo,” aliniambia kisha akanitukana tusi la nguoni.
Nikabaki kimya huku nikiendelea kuugulia maumivu niliyoyapata. Wale wanaume wakakimbia eneo hilo.
Wakati nikiendelea kuugulia maumivu huku nikiwa sijui nini nifanye mara akatokea mwanaume mmoja ambapo aliponiona alinifuata na kuniuliza nilikuwa na tatizo gani?
“Nimeibiwa kaka yangu, wameniibia,” nilimwambia huku nikionekana kuchanganyikiwa.
“Embu subiri kwanza akina nani hao wamekuibia?” aliniuliza.
“Siwajui, siwajui kaka angu” nilimjibu huku nikianza kulia.
“Usilie sasa taratibu niambie kwanza unatokea wapi na unaitwa nani?”
“Naitwa Mwajuma nimetokea huko nilipokuwa nafanya kazi za ndani.”
“Wapi?”
“Kijitonyama.”
“Sasa huku umekuja kufanyaje?”
“Wapi?”
“Kwani unajua hapa upo wapi?”
“Hapana sijui kaka angu kwani hapa ni wapi?
” Tandale,” alinijibu kisha akaanza kunionea huruma,
“Umesema umetokea Kijitonyama?’
” Ndiyo.”
“Kwanini sasa wamekuruhusu kuja sehemu kama hii usiku?”
“Hapana nimefukuzwa,” nilimjibu kisha akaonekana kunihurumia zaidi.
Mpaka kufikia muda huo nilikuwa bado sijalifahamu jina lake, alinitazama kama niliumia sana lakini hakukuwa na majeraha niliyoyapata zaidi ya kuugulia maumivu ya ndani kwa ndani. Hakutaka kuona nikiendelea kubaki eneo hilo kwani aliniambia mtaa huo palikuwa na vibaka wengi sana, hakuishia hapo alizidi kunipa sofa mbaya za mtaa huo hivyo kitendo cha mimi kuendelea kuwepo mahali hapo kingeweza kunihatarishia maisha yangu.
Baada ya kusikia kuwa nilifukuzwa na sikuwa na mahali pa kwenda usiku huo, alihitaji kunisaidia. Aliniambia alikuwa akiishi peke yake hivyo kama nisinge jali anichuke na kwenda naye kwake usiku huo.
ITAENDELEA
Mwajuma Utamu Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;