Mzee wa Dodo Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA: ALLY MBETU “DR AMBE”
*********************************************************************************
Chombezo: Mzee Wa Dodo
Sehemu ya Tatu (3)
Walijikuta wamesahau kama walikuwa wakila na kujikuta wapo katikati ya bahari. Snura kujituma kukumbushia enzi walipoanza mapenzi, japokuwa kulikuwa na tofauti ya mwili. Zamani alikuwa na mwili mdogo na mwepesi kwenye nyonga lakini baada ya kunenepa alijitahidi lakini nyonga ilikuwa nzito.
Mchakamchaka haukuwa wa kitoto kila mpira ulipotua Snura alifika, faulo ulipiga yeye kona yeye golikiki yeye kutupa yeye. Mpaka wanakwenda mapumziko palikuwa pamechimbika bila jembe.
SASA ENDELEA…
Waliposhtuka walikuta kitanda kimetapakaa tambina mchuzi zingine zikiwa zimewaganda mwilini.
“Mmh! Kazi kwelikweli kumbe unaweza,” Tumu alimtania mkewe.
“Mume wangu kazi zinanikosesha raha ya mapenzi.”
“Sasa tutafanyaje?”
“Hakuna cha kufanyaje, nimerudi rasmi sitaki tena mchezo.”
“Hakuna tatizo mke wangu.”
“Mume una mwanamke wa nje,” Snura alianza kulia wivu.
“Kwa nini mke wangu?”
“Mbona siku hizi una hamu na mimi?”
“Mke wangu mapenzi gani ya upande mmoja, hivi penzi tamu kama hili hata kila siku sitalichoka.”
“Basi mume wangu nitajitahi kurudisha furaha yako, nakupenda mume wangu.”
“Hata mimi nakupenda mke wangu.”
Walikumbatiana bila kujali kama wamelala kwenye mchuzi na tambi. Penzi lilikuwa shatashata kama ndiyo siku yake ya kwanza kukutana kimapenzi. Tumu alishangazwa na mkewe kumpa kitu ambacho kilikuwa kigeni katika medani ya mapenzi. Hata vilio vilikuwa vipya kama mtoto wa mbwa mwenye njaa alivyokuwa akinung’unika.
Tokea siku ile mambo yote muhimu ya ndani aliyafanya mwenyewe Snura na kuifanya nyumba yake kurudisha furaha iliyopotea. Chakula chote cha usiku alipika mwenyewe na kula na mumewe ambaye naye alibadili ratiba ya kuwahi nyumbani ili asimuudhi mkewe.
Kazini nako alijipanga kuhakikisha haaribu sehemu yoyote, kazi ilikwenda vizuri na mumewe alipata penzi kamili lililomfanya ayafurahie maisha ya ndoa.
Wakati Snura akifurahi penzi lake, hali ilikuwa mbaya kwa Teddy aliyekuwa amezoea kujilia kwa upole kwenye shamba lililokosa mwenyewe.
Kutokana na tajiri yake kuliacha shamba bila mlinzi na ngedere kama Teddy kujilia kwa upole. Baada ya Snura kugundua udhaifu wake na kuamua kurudi kwenye shamba lake. Kwa upande wa Teddy iligeuka kuwa mateso mazito.
Kila usiku kwake ulikuwa mrefu usingizi ulimkimbia kabisa kwa kutamani angalau apate hata mguu wa jini ili apate angalau kulala, lakini Snura alikuwa akikaba mpaka penati.
Kila alipozidiwa alitumia maji ya moto kupunguza mateso ya wadudu wadogowadogo waliokuwa wakinyemvua vibaya. Lakini alijikuta akiyazoea na kufanya kila aalipoyatumia hayakupunguza kitu chochote.
Siku moja alishtuka usiku wa manane baada ya kuota yupo katika ya mnazi wa Tumu akikaribia kuyafikia madafu. Haja ndogo iliyoharibu ndoto yake.
Baada ya kutoka kujisaidia alijikuta kwenye wakati mgumu sana. Kwa bibi kulikuwa na hali mbaya kama kachambia pilipili na mkunaji hakuwepo. Alinyanyuka hadi sebuleni na kukaa kwenye kochi akiwa na upande wa kanga bila kitu kingine mwilini ili kuvizia labda Tumu angetoka.
Kila dakika hali ilizidi kuwa mbaya, alijikuta akiamua liwalo na liwe. Alisogea hadi kwenye mlango wa chumba cha tajiri zake. Wazo la kugonga lilikuja lakini alijiuliza akitoka Snura atamwambia nini.
Alijua kama atatoka Tumu hatakuwa na tatizo kwani atamueleza tatizo lake. Kila alipotaka kugonga moyo ulisita. Alijikuta alia mwenyewe baada ya wadudu kuzidi kunyemvua. Alijikuta akirusha miguu kama anakanyaga moto.
Alipata wazo la kurudi kwenye kochi kuvulimia huenda Mungu akabariki Tumu akatoka. Lakini alijikuta akipitiwa usingizi bila kujua.
Tumu alikuwa wa kwanza kuamka na kuelekea sebuleni kuangalia magazetini kwenye tivii. Alipotoka sebuleni alishtuka kumkuta Teddy akiwa amejilaza akiwa ametanua miguu, mguu mmoja ulikuwa juu kwenye mkono wa kochi. Kidole gumba cha mkono wa kulia kilikuwa mdomoni na kukinyonya kama mtoto mdogo ananyonya chupa ya maziwa na kidole cha kati cha mkono kushoto kilikuwa kwenye kisiwa cha burudani.
Alishtuka sana kwa kujua kama mkewe angewahi kuamka ingekuwa picha mbaya ambayo lazima ingetoa picha ya madhambi aliyofanya na Teddy.
Alitembea haraka mpaka alipokuwa amelala na kumtikisa ili aamke aende chumbani kwake.
Alipofika alipokuwa amejilaza Teddy huku akinyonya dole gumba na kidole cha kati kikitafuta kitu kilichojificha ndani. Alijikuta akisisikwa na kutamani kumsaidia kwa analojia badala ya kujipa raha kwa dijitali, lakini bahati mbaya mkewe alikuwepo.
Kingine kibaya mkewe kujirudi hakutaka kumwacha mumewe wakati wa kwenda kazini kama zamani ambapo Tumu alimaliza haja zake asubuhi.
Kila alipotoka alifuatana na mumewe kwenye gari moja na jioni Snura alikuwa akiwahi kurudi kabla mumewe hajarudi.
Kitu kile kilimnyima nafasi Teddy ya kujivunia shamba lisilo na mwenyewe.
“Teddy…Teddy,” alimwita kwa sauti ya chini.
Lakini Teddy hakumsikia aliendelea kula raha aliyojipa mwenyewe na kuthibitisha usemi wa raha jipe mwenyewe. Tumu aliendelea kumwita kwa sauti ya chini bila mafanikio.
Alipoona hasikii alimtikisa kwa mkono huku akiendelea kumwita. Teddy alifumbua macho taratibu na kukutana na Tumu. Kama nyani alimrukia huku akilia.
“Shemeji ndo unanifanya nini?”
“Te..Teddy niachie.”
“Sikiachii mpaka unipe haki yangu.”
“Subiri basi kwanza.”
“Nisubiri nini, leo siku ya ngapi unanipita kama daladala lililojaa mbele ya trafiki.”
“Teddy hebu niachie dada yako akiamka itakuwa soo.”
“Ili isiwe soo nipe hata mguu wa jini.”
“Sasa hapa nitakupaje, basi tangulia chumbani kwako.”
“Sitangulii hapa mguu kwa mguu.”
“Mmh! Haya.”
Tumu hakuwa na ujanja aliongozana Teddy hadi chumbani kwake. Walipofika Teddy hakusubiri, alimfanya Tumu kama mhindi wa kuchemsha kwa kumtoa maganda kisha kumsukumia kitandani.
Akiwa kama teja aliyekuwa akibembea kwa hamu aliudandia mnazi na kuanza kuukwea mwenyewe bila msaada wa mwenye mnazi. Alipoanza kujivuta kama funza mzee kuelekea juu ili afikie nazi, sauti ya Snura kumtafuta mumewe. Iliwashtua na kumfanya Tumu amsukume Teddy aliyeanguka chini ya kitanda.
Sauti ilizidi kuita huku ikielekea upande wa chumba cha Teddy, kitu kilichowaweka wote kwenye hali ngumu. Tumu alimlaumu Teddy kimoyomoyo na kujua hata kama nyumba yake itavunjika au kuingia katika migogoro atakuwa yeye.
Lakini baada ya muda sauti ilionekana kuondoka eneo lile kuonesha baada ya kumkosa amekwenda kumtafuta kwingine. Tumu akiwa amevaa nguo zake wasiwasi ulimjaa, alitoka taratibu huku akiomba Mungu asikutane na mkewe.
Alipofika sebuleni paliwa patupu, kwa haraka alikwenda kufungua mlango wa kutokea nje. Lakini kabla hajamalizia mkewe alitokea.
“Mume wangu unatoka wapi?”
“Nje.”
“Nje! Kufanya nini?”
“Wakati natazama magazeti kwenye tivii jirani aliniita.”
“Alikuwa na shida gani?”
“Gari la lilikuwa haliwaki,” Tumu alitengeneza uongo.
“Mume wangu ufundi wa magari umejifunzia wapi?” Snura alimshangaa mumewe.
“Mke wangu ukiisha kuwa na gari lazima ujue matatizo madogomadogo na jinsi ya kuyatatua.”
“Mi ndo maana nilikueleza tuweke tivii ndani kwa tabia yako ya kuniacha kitandani peke yangu.”
“Lakini wewe ndiye uliyekataa kuweka tivii chumbani kuwa inakupigia kelele.”
“Ni wakati ule.”
“Lakini hii kubwa hatuwezi kuiweka hii ndani kwa vile inatumika kwa watu wote.”
“Basi leo nikirudi jioni narudi na tivii ndogo ya chumbani.”
“Hakuna tatizo.”
“Yaani mume wangu niliposhtuka usingizini nilikuwa na hamu na la asubuhi. Nimetoka nikajue upo sebuleni lakini hola, nilijikuta nakwenda kukutafuta msalani kwa jinsi nilivyoshikika.”
“Pole mpenzi wangu.”
“Sijapoa, twende ndani ukanipe haki yangu.”
Tumu aliongozana na mkewe chumbani la kumpa la asubuhi kisha walioga pamoja kujiandaa kwenda kazini. Wakati wao wakila raha zao Teddy chumbani alikuwa akiteseka na kujilaumu kuwachokoza nyuki wakati hana mbio matokeo yake wamemuuma chini.
Kwa jinsi alivyokuwa ameshikika, hata nguvu za kunyanyuka kitandani hakuwa nazo. Alijikuta akiichukia ile nyumba na kuwa tayari kuondoka siku ileile kwa vile hali aliyokuwa nayo shetani wake ndiye aliyekuwa akijua. Hakutaka kujisindikiza kwa vidole kama kinanda kwa kuamini muwasho anaokuwa akisikia kwa kujipapasa kama kinanda aliona sawa na kujikuna na vidole butu visivyo na kucha ambavyo haviondoi muwasho.
Aliapa moyoni siku ile hata iwe vipi atamtafuta hata mtu wa nje na kumpa fedha ili tu ammalize muwasho wake, kwani aliamini siku ile ingepita bila kupata angeweza kupoteza uhai.
Kama wangekuwa vidudu vya maralia vingepimwa basi vingekutwa milioni moja vinavyoweza kumuua mgonjwa mara moja, ndivyo hali aliyokuwa nayo Teddy baada ya kuupanda mnazi nusu na kusukumwa na tajiri yake baada ya kusikia sauti ya mkewe akimtafuta.
Wadudu wadogowadogo walikuwa wakinyemvua kama wanataka kutoka nje. Bwawa lilijaa maji na kuanza kuchafua shuka. Mateso yalipozidi alianza kulia na kusahau asubuhi ile alitakiwa kuandaa chakula cha bosi wake na cha mtoto.
Aliendelea kujilaza kitandani huku akipiga miguu kwa nyuma kama yupo ndani ya maji. Aliamini njia ya kumtafuta mtu wa nje ingeweza kumbakisha kazini. Bila hivyo hakuwa na budi ya kuondoka.
Akiwa bado amejilaza kitandani bila kitu chochote mwilini. Snura baada ya kujiandaa alikwenda mezani kupata kifungua kinywa. Alipofika alishangaa kukuta hakuna kilichoandaliwa mezani. Alishtuka na kujikuta akielekea chumbani kwa Teddy akiwa na hasira.
Mlango wa chumbani kwa Teddy ulikuwa kazi, aliingia bila hodi. Alishangaa kumkuta Teddy alilala kifudifudi mikono kailalia kwa ndani huku miguu akipiga kwa nyuma kama anaogelea.
“Teddy!” alimwita kwa sauti.
Teddy hakujibu aliendelea kupiga miguu kwa nyuma kitu kilichomshtua Snura. Alisogea hadi kitandani na kumtikisa.
“Teddy una nini?”
Teddy hakujibu aliendelea kulala, Snura alishtuka na kumtikisa.
“Teddy mdogo wangu una nini?”
“Tumbo dada,” alijibu kwa sauti ya chini.
“Limefanya nini?”
“Linakata.”
“Tokea saa ngapi?”
“Usiku.”
“Mbona hujatuamsha?”
“Nilijua litapoa.”
“Mmh! Sasa itakuwaje?”
“Acha tu dada litapoa tu.”
“Haiwezekani, itabidi shemeji yako akupeleka hospitali mi nawahi kazini.”
“Hapana dada nyie nendeni tu litapoa.”
“Wee Teddy lisipoe toka usiku lipoe asubuhi, hapana mi naenda kazini lakini shemeji yako atakupeleka hospitali, kitakachoendelea atanijuza.”
“Sawa dada,” kauli ile Snura aliiona ndiyo tiba sahihi ya maradhi yake.
“Baba Gift,” Snura alimwita mumewe kwa sauti ya juu.
“Naam.”
“Mkeo anaumwa.”
“Nini?”
”Tumbo.”
“Limemuanza lini?”
“Usiku.”
“Mbona hakusema?”
“Alijua litapoa.”
”Sasa.”
“Itabidi ubaki ili umpeleke mkeo hospitali.”
“Hakuna tatizo.”
Kauli ile ya kubakia Tumu kidogo imfanye Teddy apige vigelele kwa kuona mtego asio utegemea umenasa.
“Sasa mdogo wangu hebu amka ukaoge ili shemeji yako akupeleke hospitali.”
Teddy alinyanyuka na kujifunga upande wa kanga na kutembea kisanii kwa kuinama kuonesha tumbo linamuuma. Alikwenda kuoga na kupewa huduma ya kwanza ya kunywa glasi ya maji moto na kujifanya limeanza kupoa.
“Teddy lazima upate tiba kamili.”
“Sawa dada.”
“Basi mi niwahi kazini, kama tumbo limepoa kidogo basi mtayarishie Gift chakula kisha muelekee hospitali.”
“Hakuna tatizo dada.”
Snura aliondoka kuwahi kazini na kumwacha Teddy akielekea jikoni kuandaa chakula cha mtoto. Tumu alijua nini kinaendelea kwa kuamini kabisa Teddy alikuwa haumwi chochote, ili kupata uhakika baada ya mkewe kuondoka alimfuata jikoni na kumuuliza.
“Teddy kweli unaumwa?”
“Ndiyo.”
“Nini?”
“Subiri nikifika kwa daktari utajua.”
“Sawa malizia basi ili nikupeleke hospitali kisha niende kwenye kazi zangu.”
“Sawa.”
Teddy aliandaa chakula cha mtoto, baada ya kumlisha na kumuosha alimbembeleza na kulala. Alimlaza sebuleni kitu kilichomshangaza Tumu.
“Teddy mbona umemlaza mtoto wakati tunataka kwenda hospitali?”
“Kwani tatizo nini, si kwenda hospitali tutakwenda tu hofu ondoa.”
“Mmh! Haya,”Tumu alijibu huku akipeleka macho kwenye runinga.
Teddy baada ya kukamilisha kila kitu cha muhimu. Aliamini muda muafaka wa kupata tiba imewadia. Aliingia chumbani na kuvua nguo zote na kubakia kama alivyo zaliwa.
Baada ya zoezi lake kukamilika alimwita Tumu.
“Shemeji.”
“Naam.”
“Njoo.”
Tumu bila kujua anachoitiwa alikwenda na kuingia chumbani. Alishtuka kumkuta Teddy hana nguo.
“Vipi Teddy?”
“Safi, mbona unashangaa?”
“Ndiyo, mbona upo hivyo?”
“Kipi cha ajabu?”
“Hakuna cha ajabu, kwa nini umevua nguo?”
“Ili unitibu maradhi yangu.”
“Teddy si unaumwa tumbo?”
“Walaa, ila upupu ulionipaka uliponiacha chumbani ndiyo unaonisumbua hebu nikune uwahi kwenye kazi zako.”
“Na hospital?”
“Nikafanye nini?”
“Si unaumwa tumbo?”
“Mimi siumwi tumbo.”
“Mbona ulimwambia dada yako unaumwa tumbo?”
“Sasa ulitaka nimwambie nanuka shombo ulilonipaka wakati anakutafuta?”
“Ha..ha..pana.”
“Sasa, bila kusingizia ugonjwa angekubakiza leo? Kila siku kakuganda anajua mwenye kuwashwa ni yeye wengine hatuwashwi na kukunwa.”
“Lakini Teddy, si..si..si.”
“Shemu usiniudhi hebu nipe haki yangu ili uwahi kazini.”
“Akiuliza umetibiwa wapi?”
“Mwambie hospitali yoyote.”
“Akitaka cheti?”
“Shida yake cheti au kupona kwangu, baada ya tiba yako atanikuta nimechangamka kama nimetiwa ndimu.”
“Mmh! Sawa,” Tumu naye alikuwa sitaki na taka kwani alilimisi penzi live la Teddy binti mchanga.
Naye mashetani yalianza kumpanda kila jicho lake lilipotua kwenye mwili mchanga wa Teddy hasa ‘dodo’ waswahili wanaita embe nyonyo almaarufu mkoa wa Morogoro maeneo ya Mzinga, ambazo hutakiwi kutumia kisu zaidi ya mdomo kunyonya ndipo utafaidi utamu wake.
Mahanjamu yalimpanda Tumu na kujikuta yupo katikati ya mnazi huku Teddy akitoa kilio cha mtoto wa mbwa aliyekuwa akifurahia nyonyo ya mama yake aliyoikosa toka asubuhi. Mchana uliingia bila kujijua kwani kila wapomaliza na kupumzika kidogo na kuendelea kutokana na kila mmoja kuwa na hamu na mwenzake baada ya kukosana kwa muda mrefu.
Snura kazini baada ya kumaliza kazi zake majira ya saa tano alimpigia simu mumewe kutaka kuja hali na Teddy, lakini simu iliita bila kupokelewa, alirudia zaidi ya mara kumi bila kupokelewa.
Alijaribu namba ya Teddy nayo iliita bila kupokelewa. Hali ile ilimtia wasiwasi na kuamini huenda Teddy amezidiwa. Wazo la haraka lilikuwa kuomba ruhusa ili arudi nyumbani kwenda kuangalia kinachoendelea kwani kazi ilimshinda.
Alikwenda kwa bosi wake kuomba ruhusa ili akaangalie hali ya msichana wake wa kazi aliyewacha mgonjwa na kuruhusiwa. Aliingia kwenye gari na kurudi nyumbani.
Snura aliendesha huku akiwa na mawazo mengi kuhusu msichana wake wa kazi na hali aliyomwacha nayo asubuhi. Wasiwasi wake mkubwa labda amezidiwa sana. Alijikuta akimlaumu mumewe kushindwa kumtaarifu kwa njia ya simu kipi kinaendelea.
Kibaya zaidi kilichozidi kumchanganya simu zote alizopiga kwa mumewe na msichana wa kazi ziliita kwa muda mrefu bila kupokelewa zilidizi kumchanganya.
Wakati akikaribia nyumbani Teddy na Tumu walikuwa wanatoka kuoga kama mtu na mkewe. Sauti ya gari nje ilimshtua Tumu alipochungulia nje alishtuka kuona gari la mkewe.
“Mungu wangu! Mama Gift,” alisema macho yamemtoka pima.
“Nani?” Teddy aliyekuwa amesimama ameshikilia kanga bila kuifunga alishtuka na kuuliza kama hakusikia.
“Mke wangu?”
“Mkeo wako nani?” Teddy naye alichanganyikiwa.
“Snura.”
“Yupo wapi?”
“Teddy najificha chumbani kwako akija mwambie nimekurudisha muda si mrefu unatoka kuoga na hujambo umekutwa huna ugonjwa wowote na sasa hivi hujambo huumwi tena na mimi nimekwenda kazini na Gift amekula ameshiba na amelala,” Tumu alipagawa.
“Jamani shemu nitaweza kujibu yote hayo mengine naweza kusahau.”
Sauti ya geti kufunguliwa ilizi kuwaweka kwenye hali mbaya, Tumu kumshika mkono Teddy na kukimbilia naye hadi chumbani kwake.
“Teddy mi naingia uvunguni, mjibu nilivyo kwambia sawa?”
“Sawa, sijui kama nitaweza yaani natetemeka mpaka utumbo.”
Snura alipofika mlangoni alisukuma mlango na kukuta umefungwa. Alibonyeza kengele iliyoashilia yupo mlangoni. Teddy kabla ya kwenda kufungua mlango alijipa ujasiri kwa kuvuta hewa ndani na kuitoa kisha alifuta mikono usoni na kusema.
“Mmh! Sina jinsi, liwalo na liwe.”
Alikwenda mpaka mlangoni na kufungua, alijenga tabasamu la uongo huku akisema:
“Karibu dada, mbona umerudi mapema?”
“Tuachane na hayo yote, unaendeleaje?”
“Sijambo.”
“Umekwenda hospitali?”
“Ndiyo.”
“Vipi, umepata tiba?”
“Ndiyo.”
“Unajisikiaje kwa sasa?”
“Mmh! Sijambo, huwezi kuamini yaana nina nguvu kama kifaru.”
“Wamesema tatizo nini?”
“Wamesema sina ugonjwa wowote ni mshtuko wa mwili wamenipa dawa za maumivu.”
“Mmh! Pole sana, shemeji yako ameondoka saa ngapi?”
“Kama saa moja iliyopita.”
“Sasa kwa nini hajanijulisha afya yako wala nisingekuja huku.”
“Aliponifikisha tu aliondoka sijui alipigiwa simu na nani?”
“Na wewe mbona hupokei simu?”
“Ooh! Yaani jinsi nilivyokuwa hata simu niliisahau nyumbani. Na niliporudi nilifikia kujilaza kidogo na muda huu niliamka na kuoga ili niandae chakula cha mtoto na changu.”
“Kama hujisikii vizuri ungepumzika nitakupa hela ya chakula cha mchana na jioni.”
“Hapana dada nipo sawa,” Teddy kwa msisitizo alirukaruka kuonesha yupo sawa.
“Basi nimekubali, sasa huyu mwanaume atakuwa wapi?” alisema huku akitoa simu kwenye pochi na kumpigia mumewe.
Ajabu baada ya kuweka sikioni simu ya mumewe iliita kwenye kochi palepale sebuleni. Teddy alishtuka na kuona ameumbuka mpaka tumbo lilimpundika na kuhisi tumbo la kuhara, lakini Snura hakuwa na wazo hilo.
“He! Na hii simu vipi?” alisema huku akiichukua na kukuta Missed calls zaidi ya ishirini kuonesha haijaguswa muda mrefu.
“Hata najua, labda amesahau,” Teddy alijitahidi kujibu japokuwa angebanwa sana angechemka.
“Basi haraka zake hizo, sijui alikuwa anawahi nini mpaka kusahau simu. Sasa mdogo wangu kwa vile nimekuta hujambo, wacha mi nirudi kazini.”
“Hakuna tatizo, usiwe na wasiwasi nipo fiti kama chuma,” Teddy alizidi kumtoa hofu Snura.
“Hata mi naona kama asubuhi ulikuwa vile sasa hivi upo hivi. Ila simu sitaichukua najua lazima atarudi tu muda si mrefu. Shemeji yako toka nimjue hajawahi kuacha simu zaidi ya dakika tano. Leo nashangaa inawezekana ugonjwa wako na haraka ya huko anakokwenda kumfanya asahau simu.”
“Inawezekana.”
“Haya wacha niwahi maana sikuwa na amani moyoni, Gift amelala.”
“Akila akashiba hana tatizo ndo maana nafanya kazi zangu kwa nafasi.”
“Haya kwa heri.”
Snura aligeuza na kuwahi kazini, Teddy alimsindikiza kwa macho mpaka gari lilipopotea machoni mwake ndipo aliposhusha pumzi ndefu na kupiga alama ya msalaba huku akisema:
“Asante Mungu.”
Kweli wanadamu tunamgeuza Mungu babu yetu, yaani atoke kwenye kumchukiza halafu amshukuru kwa lipi, unamwambia asante badala ya kusema.
“Asante shetani,” kwa vile yeye ndiye mhamasishaji mkubwa wa maovu.
Alikwenda hadi chumbani na kumueleza Tumu mkewe ameondoka.
“Bwana eeh! Hebu toka mkewe amekwisha ondoka.”
“Mmh! Leo nilikuwa naumbuka mzee mzima.”
“Mmh! Halafu kwa nini ulitaka kuchoma picha.”
“Kivipi?”
“Simu si uliisahau juu ya kochi.”
“Mungu wangu! Amesemaje?”
“Amejua umesahau wala akuhoji kitu na kuamini utarudi muda wowote kwa vile hujawahi kutembea bila simu.”
“Alikwenda chumbani?”
“Walaa, aliposimama wakati ananikuliza ndipo alipogeuza na kurudi kazini.”
“Mmh! Kwa vile hana wasiwasi na wewe ndipo maana hakutilia mashaka.”
“Basi ondoka uwahi kwenye mihangaiko yako unipe uhuru wa moyo.”
“Nimechoka lakini sina jinsi lazima niondoke mmejua kunitesa leo kama mliambiana. Lakini lazima niondoke ili nipate la kunitetea.”
“Kuanzia leo kumbuka una wake wawili ndani ya nyumba wote tunahitaji haki sawa.”
“Nitajitahidi nitakupangia siku zako.”
“Sawa, siyo kila siku hata mara mbili kwa wiki inatosha, ukishikwa sana na mamaa, hata mara moja kwa wiki, basi isipite wiki bila kuyashusha mashetani yangu.”
“Sawa mama.”
Snura alirudi hadi ofisini mapema tofauti na jinsi alivyoondoka mpaka shoga yake Edna alimuuliza.
“Vipi mbona mapema?”
“Nimemkuta hajambo.”
“Lakini si ulipata ruhusa kwa nini usirudi kesho?”
“Kukaa nyumbani peke yangu mpaka jioni nitaboweka, bora ingemkuta mzee najua siku ingekuwa nzuri.”
“Tena siku hizi husinzii au ushaanza kumtengea mzee ajipakulie na kuondoa vyombo?”
“Walaaa, shoga nimejipanga, huwezi kuamini leo muadhini ndiye aliye tutenganisha na asubuhi nilipoamka nikawa sawa,” Snura alijitapa kwa kujisikia.
“Unatumia nini ili kutochoka sana?”
“Walaa, nimejipanga, nilijiachia sana lakini mwanamke nafanya kazi zote za jioni na mume wangu anapata haki yake mpaka anasema basi.”
“Basi shoga nami nimeliazisha kwangu, juzi shemeji yako alipodondosha dafu moja kama kawaida akataka kuteremka kwenye mnazi nikamwambia anakwenda wapi usiteremke juu ya mnazi mpaka uangeshe nazi tatu.”
“Mmhu, ikawaje?”
“Jamani mbona nilimuonea huruma baba yule, kumbe naye alijizoesha akiangusha dafu moja anateremka, la pili aliweza kudondosha lakini la tatu mwanaume kachemka mpaka nikamuonea huruma.
“Na asubuhi nilipoamka nilimwacha amelala, lakini leo kaniapia lazima atalipa kisasi kwa hiyo shoga kesho kazi zikinishinda ujue mwenzio nimepigika.”
“Wala usihofu, ulinibeba nitakubeba.”
Mashoga walicheka na kugongeana mikono huku wakiendelea na kazi.
Tumu ilibadili utaratibu angalau mara moja kwa wiki alimpa haki yake Teddy ambaye kidogo ilimpunguzia mateso na kufanya mambo yaende vizuri ndani.
Teddy alianza kupendeza na kunenepeana na kuonekana mwanamke aliyepevuka kama embe bivu huku Tumu akizidi kuchanganyikiwa na binti mchanga.
Alianza kujishangaa kuchukia baadhi ya vyakula vya ndani na kichefuchefu cha kila mara kitu kilichomfanya aende kumuuliza shoga yake aliyekuwa akifanya kazi nyumba ya pili.
Wakiwa wanatoka sokoni alimweleza shoga yake hali iliyokuwa ikimtokea muda ule.
“Koleta kuna hali imenitokea kama siku nne hivi siielewi.”
“Hali gani Teddy?”
“Sasa hivi baadhi ya vyakula vinanishinda, pia kichefuchefu hakiniishi bila kulamba ndimu natamani kutapika.”
“Mmh!” Koleta aliguna.
”Mbona unaguna?”
“Wee, isiwe mimba.”
“Mimbaaa?” Teddy alishtuka.
“Ndiyo, hizo dalili huwa za mimba.”
“Mungu wangu kama mimba nimekwisha mtoto wa kike nitamwambia nini dada,” Teddy aliingia woga.
“Kwani una mpenzi?”
“Ndi..ndi..ha..hapana,” Teddy alibabaika.
“Teddy mbona sikuelewi?”
“Hapana sina.”
“Sasa kama huna mwanaume inaweza kuwa maralia japo dalili zako ni za mtu mwenye mimba.”
“Mmh! Sijui itakuwaje?”
“Kwani vipi?”
“Mwenzangu huu utata kama kweli ni mimba, kwa usalama wangu lazima nitoloke bila kuaga.”
“Wewee, vipi mzee alikuwa akila raha?”
“Ndi..ndi.. ha..ha…pana.”
“Teddy mbona una jichanganya, hebu kuwa mkweli, kama unakula kipi cha ajabu?”
“Koleta naomba leo uniache tutazungumza baadaye.”
“Hebu sikiliza ndugu yangu, kama ulikuwa ukila raha na bosi wako hakuna kigeni kwani mtu akijipendekeza we kula tena na mshahara unapanda.”
“Lakini dada akijua nina ujauzito wa mumewe anaweza kuniua.”
“Kwani mama Gift anajua?”
“Hajui.”
“Sasa wasiwasi wako nini, mbona hata mimi najilia kitoga bila woga kwa bosi wangu.”
“Sasa nitafanyaje kama nina mimba?”
“Mweleze aliyeiweka ili mjue mtafanya nini?”
“Na dada akiniuliza?”
“Mwambie mwenye mimba ulikutana naye kwa bahati mbaya hujui anapokaa.”
“Mmh! Nitajitahidi.”
“Lakini kwanza ukapime maralia ujue tatizo.”
“Nitafanya hivyo shoga yangu.”
Teddy aliagana na Koleta na kuwahi kupika, alipofika nyumbani aliandaa chakula huku kipande cha ndimu kipo pembeni.
Jioni aliporudi bosi wake alikificha kipande cha ndimu na kukila kwa kujificha. Baada ya kukosa kulamba ndimu kwa muda mrefu uzalendo ulimshinda na kujikuta akikimbilia nje kutapika.
Hali ya kutoka mbio ilimshtua sana Snura na kuamua kumfuatilia nje. Alipofika nje alimkuta Teddy amechutama akitapika. Alipofika alisimama nyuma yake na kumwacha atapike kwanza.
Baada ya kutapika alifukia matapishi na kutaka kurudi ndani, alipatwa na mshtuko baada ya kumuona dada yake kasimama nyuma yake.
“Ha! Dada?”
“Vipi mdogo wangu unaumwa?”
“Ndiyo dada sijisikii vizuri toka mchana.”
“Mbona hujasema?”
“Nilijua hali ninayoisikia labda itakata.”
“Mdogo wangu mbona sikuelewi unasumbuliwa na nini?”
“Dada hata sijui, nimekuwa nachukia baadhi ya chakula na kusikia kichefuchefu.”
“Mmh! Mdogo wangu isiwe mimba!”
“Mimbaaa? Ha..ha..pana!” Teddy alijifanya kushtuka sana.
“Eeeh mbona umeshituka?”
“Haa..a.pana haiwezekani!” Teddy bado alizidi kutengeneza usanii japokuwa hofu ilizidi kumjaa moyoni na kuamini kama kweli ni ujauzito angejitetea vipi.
“Lakini usiogope labda ni maralia..twende tukaangalie hospital.”
Kwa vile muda ulikuwa bado, Snura alimpigia simu mumewe kumjulisha kuwa anakwenda hospitali kumpeleka Teddy aliyekuwa hajisikii vizuri.
Walitoka na gari hadi kwenye hosptali ya Huruma iliyokuwa karibu na wanapoishi. Walipofika walikwenda moja kwa moja kwa daktari aliyewapokea.
”Karibu mama Gift.”
“Asante, Sakina leo upo usiku?”
“Ndo’ nataka kutoka.”
“Vipi shoga mbona usiku bi shost?”
“Msichana wangu hajisikii vizuri.”
“Anasumbuliwa na nini?”
“Teddy hebu mwelezee daktari tatizo lako,” Snura alimgeukia msichana wake wa kazi.
“Nasumbuliwa kichefuchefu mwili kuchoka pia hata baadhi ya vyakula vimekuwa sivipendi.”
“Mmh! Hebu akapime damu na haja ndogo.”
“Sawa daktari.”
Aliandikiwa cheti cha kwenda maabara, waliongozana hadi maabara na kuchukua vipimo na kurudi kusubiri majibu. Baada ya muda waliitwa kwa daktari. Waliingia na kukaa kwenye kiti, baada ya kutulia daktari aliwasomea majibu.
“Majibu yanaonesha kwenye damu ana maralia kidogo, lakini kwenye haja ndogo anaonesha ana ujauzito.”
Majibu yale yalimfanya Teddy abubujikwe na machozi huku akisema kwa sauti ya chini akiwa ameshikilia mikono kifuani.
“Eeh! Mungu wangu balaa gani hili!” kitu kilichomfanya Snura ahoji:
“Mdogo wangu kushika ujauzito ni balaa? Wakati kuna watu wanapoteza mamilioni ya fedha kutafuta watoto?”
“Si kwa njia hii.”
“Kwani umempata kwa njia gani, umebakwa?”
“Hapana sijabakwa.”
“Sasa tatizo nini?”
“Huwezi kuamini baba ya mtoto huyu hayupo.”
“Amekwenda wapi?”
“Sijui.”
“Basi mdogo wangu wewe sasa hivi si mfanyakazi bali ndugu nitailea hiyo mimba, nitamweleza shemeji yako nina imani atanielewa. Usihofu jione mtu uliye na haki ya kupata mtoto tena una haki ya kuitwa mama.”
“Na..a..a..shukuru dada,” Teddy alijibu huku akifuta machozi na michirizi ya kamasi nyembamba. Snura alijua msichana wake wa kasi kuna siku alionja na kuruka na ujauzito na bwana mwenyewe kaingia mitini.
Lakini alikuwa tayari kumwacha lazima nimuoneshe na yeye shukrani zake kwa yote aliyomfanyia ya kumlindia nyumba na mwanaye kipenzi Gift. Alipanga kutafuta mfanyakazi mwingine wa kumsaidia Teddy kutokana na hali ile.
Waliporudi nyumbani Snura alimtoa hofu Teddy kwa kumuhakikishia kuilea ile mimba mpaka atakapojifungua na kisha kumtafutia kazi.
“Teddy mdogo wangu usiwe na wasi kama baba wa mtoto hataonekana basi mimi nitamtunza na akikua nitakutafutia kazi.”
“Asante dada nashukuru.”
Baada ya kuandaa chakula cha usiku Tumu alirejea nyumbani akiwa hajui lolote. Snura alipomuona mumewe akirudi alimweka Gift kwenye kochi na kwenda kumpokea mumewe.
“Waaawoo mai bebiii,” alimkumbatia kabla kumpokea mizigo. Baada ya kukaa kwenye kochi alipewa maji na kunywa na kuulizwa habari za kazi.
“Pole na kazi mume wangu.”
“Asante, Pole na wewe.”
“Asante mpenzi wangu.”
Snura alichukua mizigo aliyompokea na kuipeleka chumbani, akiwa amejilaza kwenye kochi alimuona Teddy amekaa ameshika tama akionekana mtu mwenye mawazo mengi. Walipokutanisha macho Teddy aliangalia pembeni kitu kilichomfanya amuulize mkewe aliyekuwa akirudi toka chumbani alipopeleka mizigo ya mumewe.
“Mamito.”
“Abee Papito.”
“Vipi mama Gift alikuwa na tatizo gani?”
“Mmh! Sasa mkeo mama kijacho,” alijibu huku akitabasamu.
“Una maana gani?”
“Kumbe matatizo yote mkeo ni mjamzito!”
“Etiii?” Tumu alishtuka mpaka glasi aliyokuwa ameshikilia mkononi ikamponyoka na maji kidogo kumwagikia.
“Mume wanguuu kipi cha ajabu mpaka ujimwagie hivyo maji?”
“Si ajabu, lakini namuona Teddy mdogo.”
“Mume wangu siku hizi wanaume wanapima mguu ukitosha kwenye kiatu watu wanatembea bila wasiwasi.”
“Mmh! Haya.”
“Ila mume wangu pamoja na mtu aliyempa ujauzito hajulikani muda wote Teddy atakuwa hapa mpaka atakapo jifungua.”
“Na kazi?”
“Nitamtafutia msichana wa kazi, sasa hivi Teddy si msichana wa kazi bali ndugu wa kuzaliwa tumbo moja. Kanitunzia Gift wangu kama mwanaye wa kumzaa.”
Kauli ile iliuchoma moyo wa Teddy na kumfanya ajutie kufanya mapenzi na mume wa tajiri wake na kushindwa kujizuia na kuangua kilio kwa sauti kubwa. Kitu kilichowashtua wote pale.
“Teddy nini mdogo wangu?” Snura alimfuata Teddy na kumkumbatia.
“Dada inauma, ningeyajua haya nisingekubali.”
Kauli ile ilimtisha Tumu na kumfanya mapigo ya moyo yamwende mbio na kujua kila kitu kingekuwa wazi kama vazi la kahaba. Ili kuikwepesha aibu alimfinya jicho Teddy aliyekuwa amekumbatiana na mkewe na macho yake kumtazama yeye.
Alisema kwa uti ya kibubu.
“Usimwambie kama ni mimi,” Tumu alisema huku amekusanya mikono kama anaungama.
Maneno yalimfanya Teddy azidi kulia kwa uchungu na kumfanya Snura aingie kazi ya kumbembeleza.
“Mdogo wangu si nimesema nitakulea wewe na mwanao?”
“Sawa dada lakini inaniuma sana, ningeyajua yote haya nisinge kubali.”
“Pole mdogo wanangu najua hukutegemea, yote maisha tu mdogo wangu.”
Muda wote huo Tumu alimbembeleza bila sauti ili asimtaje mwenye mimba.
“Dada nashukuru kwa yote uyaseamayo..lakini..laki..,” hakuendelea kuongea alianza kulia kitu kilichonifanya Snura ajiulize kuna siri gani ya ujauzito ule. Mmh, au ame..ha.aapana, aliyapinga mawazo yake kwa nguvu zote.
Tumu hali iliyokuwa pale sebuleni mapigo ya moyo yalimfanya ajisikie vibaya na kuamua kuondoka kwenda chumbani kusubiri bomu lilipuke. Moyoni aliapa kupinga kwa nguvu zote na kumfukuza kama mbwa Teddy kama atawanga mtama ule.
Baada ya kuelekea chumbani Snura aliendelea kumbembeleza msichana wake wa kazi aliyeonekana ameshtushwa sana na ujauzito ule.
“Teddy una siri gani moyoni mwako mdogo wangu?..au shemeji yako ame..aah…,” Teddy alimkata kauli Snura huku akiwa amemtumbulia macho yaliyoonekana vizuri ukubwa wake kwa kusema:
“Shemeji amekwambia nini?”
“Hajaniambia lolote ila nilikuwa na wasiwasi labda kuna siku alikueleza neno baya kama ukibeba ujauzito na kukufanyia ukose amani ya moyo wako,” Snura alimuuliza kwa sauti ya upole.
“Walaa basi tu, sijui kwa nini umeshika ujauzito huu?”
“Aah! Teddy mdogo wangu wewe si wa kwanza kushika ujauzito, kibaya ungekuwa unasoma,” Snura alijikuta akiingia katika kazi ya kumtuliza Teddy aliyepaga baada ya kujijua mjamzito.
“Unafikiri mtoto asiye na baba na mimi sijui hatma ya maisha yangu hasa nikizingatia familia yangu ilivyo maskini wa kutupa lazima mtoto wangu atapata tabu.”
“Apate tabu ya nini na sisi tupo na hatujaonyesha kukutenga zaidi ya kukujali na kukuona zaidi ya ndugu zangu. Teddy wema ulioupanda hauta oza milele,” Mmh! Makubwa kauli yangu ile ilimfanya Teddy alie kwa sauti na kumfanya Snura achanganyikiwe na kujiuliza kwa nini analia vile.
“Dada inatosha maneno yako yanauchoma moyo wangu…inatosha dada,” Teddy alisema huku akijilaza kifuani kwa Snura.
ITAENDELEA
Mzee wa Dodo Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;