CHOMBEZO

Ep 03: Mzoa Takatakata

Mzoa Takatakata Sehemu ya Tatu

IMEANDIKWA NA : HAFIDHI J IKRAM

*********************************************************************************

Chombezo : Mzoa Takataka

Sehemu Ya Tatu (3)

“Salumu usilie swala la kunisaidia mie ushachelewa nakufaa!!!

baada Mwanaidi kutamka vile akaanza kutapa tapa mwisho akatulia kimyaa

nikabaki kumtikisa huku nikimwita

kwa nguvu “Mwanaidiiiiiiiiiii….

mama yake huku nae akiwa analia akaja mbio akiwa na majilani vilio vikaongezeka basi tukaenda kumzika kipenzi changu aliye niingiza kwenye ulimwengu wa

mapenzi

yani kama bikra tulitoana wote tukamuombea alazwe mahala pema peponi katika makaburi ya keko mwanga

ndio tulipo mlaza baada kutimia kama wiki moja hivi kidume nipo mzigoni na Benz langu jipya nazoa takataka

nikiwa sina hili wala lile gafla bin vuu nikajikuta nalowana mwili mzima baada gari moja hivi kupita kwa kasi eneo lile kulikuwa na dimbwi la maji machafu ya

vua yaliyo chanyika na yachooni dereva hakuwa muungwana hata kidogo nilizani atasimamisha gari kuniomba samahani lakini hakufanya hivyo

baazi ya watu wakakilaani kitendo

kile nikatoka

na mkokoteni

wangu kwa ajili ya kusonga

mbele zaidi siku hiyo nilipiga

kazi yani najaza rumbesa nikienda

dampo nazimwaga kisha nakuja kujaza tena ilikuwa siku ya neema kwa sababu wazoa takataka manispaa ya temeke wameweka mgomo kisa mshahara mdogo

mie nalipwa na yule nitakaye beba takataka zake iwe mia tano au zaidi basi nashukuru tu nikajisemea waweke mgomo daima kwa hali hii sitokufa njaa kamwe

nikiwa bado katika kuchakalika si nikamuona yule boya

aliye kuwa anatembea na marehemu

Mwanaidi akiwa kaongozana na kisichana flani hivi kikiwa ndani ya sale za shule kwa jinsi walivyo shikana bila shaka ni wapenzi nikasikitika sana ila nikaitaji

kwenda kumuokoa

yule binti ila nikajiuliza inawezekana washafanya ngono si zaidi ya mara moja hata nikienda kumtonya nitakuwa nishachelewa

basi nikapiga moyo konde itakavyo kuwa wacha iwe “oyaa mangi babu,

“yeah niambie mzoa takataka,

“naomba uniangalizie mkokoteni wangu huu kuna sehemu naenda mara moja, “poa hamna shida,

basi nikatoka zangu kuwafatilia nyuma nyuma mpaka nikawaona kwenye kichochoro kimoja wapo hivi wamesimama yule binti akatoa kanga kwenye begi lake

na kujitanda yani aonekane kama mmama flani hivi ila nikawafata pale pale yule jamaa baada kuniona akastuka ila alijikaza tu nikamuuliza “hivi wewe ni zaidi

ya gaidi ehee!!! mpaka sasa ushauwa wangapi umeambukiza wangapi yani

mpaka kabinti haka kadogo unataka

kwenda kukauwa duhuu”……

“wee boya tu sema shida yako usepe kama takataka hapa hakuna, ndivyo alivyo nijibu yule jamaa si akanyanyua mkono wake kunipiga kofi kwa kitendo cha

haraka nikamdaka na kuubamiza ule mkono ukutani akapiga yowe la uchungu tu nikamgeukia yule binti na kumwambia “mapenzi….na….shule haviendaniiii

ukiwa shuleni!! tulia darasani…embu msikilize mwalimu anafundisha nini kuwa makini ukitoka shuleni usipite vichochoroni nenda moja kwa moja mpaka

nyumbaniii

wakati namwambia hivyo binti yule mchozi ukamtoka baada kugundua kumbe basha wake ni muasilika kwa sauti ya kilio akaniambia “sijui nikushukuru vipi

kaka yangu kwa kuniokoa na janga hili maana ndio nilikuwa naenda nae guest

ndio maana nilipo mwambia anunue condom alikataa kwa kisingizio utamu wa pipi ule bila ganda,

nikamwambia binti

“siku zote tamaa ni hatal!!! kwa kupenda vitu vizuliii ndio maana mnafer

sikutaka kuongea sana nikaseba kuwai Benz langu mie kama msaada

nishatoa,!

Binafsi nilijisikia faraja sana kwa kuweza kumuokoa yule binti katika mdomo wa mamba. Nikarudi moja kwa moja nilipoupaki mkokoteni wangu.

“oyaa mangi mi ndio nawasha mchuma huu!!! ni maneno niliyo mwambia mangi baada kufika pale

dukani kwake, nae akanijibu kwa kusema

“sawa kaka hamna shida!”

basi nikau sukumiza mkokoteni wangu mpaka ninapo ishi

lakini hofu ikanishika ghafla baada kumuona mzee mmoja hivi akifoka kwa maneno ya ajabu ajabu.

“habari za kusema kesho au mwakani sitaki ninacho taka ni pesa yangu tu pumbavu zenu hii nyumba sio ya baba zenu!!! hakuna cha bure hapa”….

Nikawa natetemeka huku nikijiuliza iwapo mkataba wa Madebe ukiwa umeisha itakuwaje na ndani

nina shillingi elfu kumi na tano tu!

basi nikampita bila kumpa salamu maana nilimuhofia nikiwa najiandaa kufungua mlango ghafla nikaguswa begani kwa kupigwa pigwa.

“wee kijana!!!

alikuwa yule mzee huku macho yakiwa mekundu akanikazia na kuniulia “hivi ulivyo pita pale uliona gogo au?”

nikashindwa cha kumjibu akaniuliza tena kwa sauti ya ukali zaidi

“nakuuliza wewe ulivyo pita pale uliniona gogo au jiwe!!!

huku nikibabaika nikamjibu.

“nisamehe mzee wangu unajuwa tena muda mwingine kazi zetu hizi zinatupa mawazo chungu nzima”

Akaniambia

“haya tuyaache hayo hiki chumba mpaka sasa kina miezi sita hakijalipiwa kodi kwa hiyo ninacho taka ni pesa yangu lasivyo uhame!!!

nikamjibu “kwa leo mzee wangu sina kitu nivumilie mpaka wiki ijayo nitakupatia pesa yako,

Akawaka kwa hasira

“wee!!! kijana yani nimetoka kijijini huko kibada kuja hapa kufata pesa yangu alafu nirudi mikono mitupu hapa nilipo sina hata sentano ya nauli. Nitarudi kwa

miguu au utanipakiza kwenye mkokoteni wako?”

nikamjibu “kuhusu nauli nitakupa baba!

“haya nipe hiyo nauli ukumbuke na ya soda njiani maana kibada nimbali basi nikaingia chumbani na kutoka na ile pesa shilling…elfu kumi na tano

nikampa ila nikashangaa alivyo zipokea haraka na kuondoka zake ila sikutaka kujali sana zaidi ya kuingia zangu ndani nifanye mambo mengine

zikiwa zimepita siku kama mbili hivi

siku hiyo nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe nikastushwa na sauti ya makelele “yeyooo!!!

kucheki ni Madebe akiwa na mabegi yani kwa jinsi alivyo kuwa kama vile katoka America basi nikaenda mbio kumpokea tuka kumbatiana kwa furaha nikabeba

mabegi na

kuingia nayo ndani “vipi kaka mbona ulinikimbia?”

“hapana ndugu sijakukimbia ila kuna zali lilitokea ghafla. Yani hata muda wa kuja kukutonya haukuwepo basi nikakwea pipa na kwenda kwa madibaa!!!

“kwa madiba, ndio wapi kaka?”

“kumbe kwa madiba hupajui ndugu?”

“ndio sipajui ila nasikia sikia tu vijana wakipataja,

“ni South africa hiyo!

“ahaa kumbe South,

nafikaga ndotoni tu, “ha!ha!ha! unafikaga ndotoni tena ila usijali utafika live yani itakuwa sio ndoto tena vipi yule binti wa siku ilee ulitusua au akazingua?”

“mimi tena nilitusua mpaka mtoto akazimika mwenyewe kila day anakuja ning’ate kitumbua, “ha!ha!ha! wee noma kwa hiyo siku ile sikupata dhambi?”

“dhambi za nini tena

Madebe?”

“si nilivyo enda kumkamata kinguvu yule demu nikamtishia kukikata kitumbua chake nikinyofoe chote iwapo tu atakataa kulala na wewe,

“duhuu kumbe ulimtisha hivyo ila usikonde kaka wewe mwenyewe utamuona akija hapa na kutupikia msosi, basi

Madebe akacheeka na kusema

“basi kama hivyo itabidi hili ghetto nikuachie wewe afu mimi nichukuwe chumba cha pale karibu na chooni,

“ehee ume nikumbusha kitu kaka!!!

“kitu gani hiko tena?”

“juzi kati kuna mzee flani kaja hapa akaanza kufoka mbaya akitaka pesa ya kodi bila shaka atakuwa baba mwenye nyumba tu!

Madebe akaniuliza “yukoje huyo mzee?”

nikamuelezea jinsi alivyo akasema

“ahaa yule boya sio nyoko zake yani kitendo cha kumwambia niko South tu kaja hapa kudai kodi ya nyumba sio

vipi wewe hajakusumbua?”

“wee asinisumbue tena mchezo kaniwakia mbaya kama sina pesa nihame kwakuwa ndani nilikuwa nina pesa kidogo nikamtoa ndio akasepa,

“duhuu ulimpa pesa shilling ngapi?”

“nilimpa elfu kumi na tano tu baada kusema vile

Madebe akacheka sana na kusema

“kudadeki yule mzee mwanga sana ila

Salumu kaka nisamehe mie kwa kutokwambia mapema hata ningetokea kufa ghafla sijui ingekuwaje

binafsi hii nyumba ni yangu na washkaji wote kitaa wana fahamu hilo ila some time sipendi kujionyesha tu

kuhusu nilipo zipata pesa mpaka nikanunua nyumba hii ni hizi hizi kazi zetu namiliki hadi daladala kama tatu hivi maduka ya nguo ninayo mawili huko k/koo.

Kusema kweli napiga pesa sana”…..

“lakini kaka kwa nini usingeniajili niwe hata konda kwenye daladala hata moja kuliko kuwa mzoa takataka?”

“sikia nikwambie kitu Salumu sio kama nakuacha uwe mzoa takataka ukajuwa mi napenda uwe hivyo hapana ndugu nakuandalia mazingira kwanza yani siku ya

siku ukija kutoka basi utoke kweli,!

basi nikaweza kulizishwa na maelezo yake

Madebe huku akisema “yule mzee hiyo pesa atainya tu kumbe ni Ankor wake

nakumbuka zikapita siku kama nne hivi siku hiyo nikiwa natoka zangu dukani kwa Rahma kupiga story mbili tatu nakaribia nyumbani nikaweza kuona kama

chumba ninacho kaa mimi kuna watu wanabishana hivi. Basi sikuwa na wasiwasi nikajuwa labda washikaji tu wamekuja kama kawaida yao

kupiga story mbili tatu lakini nafsi ikaniambia Salumu

kuna hatari ipo karibu yako maana mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda mbio baada kusikia sauti nzito ya mwanadada ikitokea chumbani mule. Kwa kusema

“sikia

Madebe usijifanye mjanja hata kidogo mie jana tu nimepiga simu South kuulizia huo mzigo nikajibiwa ya kwamba mzigo wote umekabidhiwa wewe!!!

nikamsikia

Madebe akimjibu yule Dada “mzigo mimi sijauchukuwa ila Jacko anaongopa tu”….

“wewe Madebe acha mambo ya kifara hapa usitufanye sisi watoto wadogo ukazani ukitupa pipi tutalainika

ukweli wote ninao kwenye simu yangu wakati unakabidhiwa mzigo kuna video walishuti jamaa amenitumia. Sasa embu cheki hii huyu si wewe ukiwapa tano

jamaa,

sasa chaguwa moja tu kati ya mambo mawili je umlete yule kijana unayeishi nae tumbebeshe mzigo tumboni au ufe!!!

baada kusema vile nikasikia sauti za wale watu wakijiandaa kutoka mule ndani nikatoka mbio na kwenda kujificha nyuma ya choo ila nikaweza kuwaona ni

mipandikizi ya mibaba yani kama wale wacheza miereka kina John Cena au Batister hata yule mwana Dada nae zinga la jitu basi wakaingia kwenye magari

waliyokuja nayo na kuondoka zao.

Nikabaki kujiuliza ni mzigo gani huo”…. alio uchukuwa

Madebe mpaka anadaiwa vile na kijana yupi anaye itajika kubebeshwa huo mzigo tumboni. Bila shaka ni mimi tu je ni mzigo gani, nijuwavyo mimi mzigo unao

bebwa tumboni ni mimba tu tena kwa Wanawake basi sasa mimi nibebeshwe mzigo why?”

nilijiuliza maswali mengi pasipo kupata jibu. Basi nikajinyanyua na kwenda chumbani nilipo ingia

Madebe sikumkuta nikajiuliza labda katoka kwenda chooni au dukani tu nikawa nina hofu balaa hata hamu ya kula sikuwa nayo mawazo yakanisonga

usingizi nao ukanichukuwa nikaja kustuka usiku wa manane kucheki pembeni ya kitanda hakuna mtu “hivi

Madebe atakuwa kaenda wapi?” usiku huo kitanda nilikiona kama kina miba basi nikaichukuwa cm yangu na kumpigia Rahma

ikawa inaita tu bila kupokelewa nikamcheki

Madebe yeye hapatikani dahaa,

hofu juu ya hofu ikanitanda zaidi nisijuwe nini kitatokea juu yangu

Usiku ulikuwa mrefu sana kwangu mie nikatamani kukuche haraka niweze kujuwa mustakabari mzima wa maisha yangu. Nikaitizama saa ndio kwanza saa tisa

kasorobo kidume nilikuwa natetemeka kama vile kifaranga cha kuku kilicho nyeshewa vua,

Taratibu nikajinyanyua na kutoka zangu nnje, Kitendo cha kutoka tu nikashitukia kama vishindo vya watu wakija eneo lile, Sikuweza kujuwa wala kufahamu ni

watu gani hao ila nikajihami mapema kwa kukimbia na kwenda kujificha sehemu ambayo nilihisi kabisa hawatoweza kuniona. Iwapo wamekuja kwa rengo la

kunifata Mimi, au Madebe nikiwa nimejificha nikaweza kushuhudia kikundi cha watu kama sita hivi wakiwa wameficha sura zao kwa vitambaa usoni mkononi

kila mmoja akiwa na dhana yani,

Nyundo panga chupa nikajikuta natumbua macho tu ghafla nikashitukia nakabwa kwa nyuma huku nikizibwa mdomo nisiweze kupiga kelele nikajikaza kujitoa

wapi nikaisikia sauti ikinisihi nitulie “Salumu kaka ni miee tulia basi, Kumbe alikuwa Madebe akaniachia na kunipa.

“pole sana kaka!”

nikamjibu

“usijali nishapoa,

Akaniambia

“sasa hapa naitaji tucheze mchezo wa kicommando!”

Nikauliza

kwa sauti ya chini

“tuucheze vipi huo mchezo?”

“si umewaona wale maboya wamekuja kwenye kumi na nane zangu, sasa ninacho kihitaji ni kuwafunza adabu maana nishaandaa kikosi cha Maafande watafika

hapa muda si mrefu!”

Nikamuuliza kwa shahuku kubwa ni kweli au?”

“ndio ni kweli ndugu naitaji niwachomeshe tu kisha nitubu dhambi zangu nianze kuswali swala tano zote yani niwe mtu safi kabisa!”

baada Madebe kusema vile akaniambia twenzetu,’ tukawa tukinyata kuwanyatia wale vijana wawili waliobaki nnje wengine wameingia chumbani kupiga search

baada kuwafikia tu wote kwa pamoja kila mmoja akamrukia wa kwake na kwenda nae mpaka chini nilijitahidi kwa nguvu zote kumkaba yule jamaa huku

nikivutia hisia jinsi ninavyo sukuma, Mkokoteni wangu pindi ninapo pandishaga kirima jamaa akafurukuta mwisho akawa kimyaa tulicho kifanya baada ya hapo

ni kuvaa magwanda yao na vile vitambaa tukakaa nnje

Tukiwa na sura za ukauzu balaa. Ghafla mlango ukafunguliwa na kutoka wale jamaa wengine na kusema, “Oyaa hawa watoto wa Malaya hawapo humu ndani

sijui wameenda wapi kama vipi tutawatimbia kesho!” baada kusema vile wakatupita ikiwa ishara ya kwamba twenzetuni hawakujuwa kama wanafanya kosa

kubwa sana kitendo cha kutupa migongo tu kila mmoja akaandaa Rungu lake kwa nguvu ya ajabu tukaenda kukita kwenye vichwa vyao, Kila mmoja akayumba

na kwenda chini haraka haraka tukavua yale magwanda punde tu maafande hao.

“kazi nzuri vijana tena ongera sana kwa kuweza kutusaidia kazi ya kuwakamata hawa Nguchiro, ilikuwa kauli ya pongezi kutoka kwa Afande Mark basi, kwanza

wakawapima pumzi isije ikawa tumeuwa nikashusha pumzi baada kuonekana kumbe wazima ila wamezimia tu,

Kesho yake Asubuhi nikiwa dukani kwa mpenzi wangu Rahma kuna jamaa mmoja hivi akaja na kuanza kumsumbua sumbua Rahma kwa kumtongoza wakati

kidume ninae miliki mzigo niko hapohapo.

“sikia binti mi binafsi nimetokea kukupenda nipo tayari kukupa chochote ukitakacho katika maisha yako!”

Rahma akamjibu

“sikia kaka naomba unikome kama ulivyo likoma ziwa la Mama yako kama pesa ninazo mpaka nashindwa kujuwa wapi pa kuziweka!”

“Nenda zako huko Malaya mkubwa tu wewe unazani nani asiyekufahamu ulikuwa unajiuza kule Temeke mwisho,’ siku zote mwanaume akitongoza na

kukataliwa utamkuta lazima aponde nikashikwa na hasira kwa kitendo cha mpenzi wangu kuitwa Malaya hata kama ni kweli,

Nikaenda kumkunja yule jamaa nikamtandika kichwa kilicho mfanya abimbilike kwenye ngazi maana tulikuwa juu kidogo nikamshukia chini na kuanza

kumshambulia kwa mateke nikaja kushikwa na Madebe na kunisihi niache binafsi nikabaki kushangaa kwa jinsi Madebe alivyo vaa yani katinga kanzu kubwa

nyeupe na barakashia nzuri mkononi kashika tasbihi na Msahafu, akaniambia

“Salumu kaka huu sio muda wa kufanya matendo ya ajabu ajabu kama haya siku zote Allah (s.w.t) anasema katika Qur’an ya kwamba Na penye chukizo pasi

jiepushe,

Ikiwa na maana kufanya hivyo itakuwa ni bora zaidi kwako kuliko ukaingia kwenye maasi wakati Madebe ananihusia hivyo kumbe yule jamaa akaingia ndani ya

gari yake na kutoka na bastora bila kuuliza akafyatua risasi iliyokuwa ikiitaji kunipata mimi, Madebe akaja kukinga ikampata moja kwa moja kwenye tumbo.

Yule jamaa akawasha gari na kukimbia eneo lile nikabaki kuita “Kakaa!”

Kakaa!!! kwa sauti ya chini iliyo ambatana na maumivu Madebe akasema “Salumu mdogo wangu huna haja ya kulia binafsi nakufa kifo cha kishujaa sana angali

nishatubu mazambi yangu Salumu naomba upiganie kuhusu ile Nyumba maana hati niliandika jina lako nilitambua sitoweza kuishi muda mrefu nitakufa tu,

Usijaribu kutaka kulipa kisasi”….

ghafla Madebe akatoa macho na kutulia kimya sikuweza kuamini kama nampoteza kamanda wangu,

Mkombozi wangu wa maisha yangu nililia sana na kuita “Kaka!!!kaka!!!

hakuweza kuamka tena police walifika na kufanya uchunguzi wakaondoka na mwili wa marehemu mkononi mwangu nikabaki na Tasbihi pamoja na Msahafu tu

nikajiapia kama sheria itashindwa kumnasa yule jamaa na kumchukulia hatua nitamnasa mimi nikajivika roho ya kishetani nikakodi boda boda kwenda kituo cha

police niweze kujuwa kinacho endelea taarifa za kifo cha Madebe zilisambaa kama umeme uliokatika ghafra Temeke nzima walistushwa kwa kifo cha mmbabe

huyo sio Temeke tu Tandika Buguruni hadi Mbagara na vitongoji vyake. Watu wakazidi kujazana kuja nyumbani kwenye msiba ule hapo nikaweza kuwaona

ndugu zake feki wakilia kwa uchungu machozi ya kinafiki tu,

Hatimae tukaenda kumzika Madebe kwa heshima zote za dini yetu ya Kiislamu kwenye makaburi ya mtoni mtongani, tokea Madebe azikwe ni siku ya nne sasa

eti ndugu wanajadili mari za marehemu.

“wewe tena usiongee kabisa wakati marehemu yupo hai si ulimfukuza nyumbani kwako kama mmbwa afu leo hii unaitaji ugaiwe gari upati kitu hapa!”

“nani amekwambia sipati nisipopata patachimbika tu!

“kwanza tambueni ya kwamba sisi tunajadili mari tu ila tukae tukitambua ya kwamba marehemu enzi za uhai wake kuna kijana alikuwa anaishi nae kama ndugu

yake ambaye ni yule pale!”

“bwana ee huyo Kijana sisi atatusaidia nini kama aliye mfadhili kuishi keshaondoka kama vipi amfate kaburini”

sio siri maneno aliyokuwa akiyatamka Dada yule yakazidi kuuchoma moyo wangu ila nikapiga moyo konde tu nisije kutenda kitu cha ajabu, wakaulizana “sasa

naona tunapanga tu kugawana mali je Hati miriki nani anazo?” kila mmoja akanigeukia mimi yule Dada mwenye maneno ya Nyodo akaniuliza “wewe mbwa

tunaomba utupatie Hati miriki zote!”

Nikainuka pale nilipokuwa nimekaa nikiitaji kwenda kumfumua zinga la teke yule Dada nikakumbuka aya aliyo nisomea Marehemu kabla hajafa nikashusha

hasira na kuwaambia hivi “binafsi hakuna hata mmoja wenu ninae mtambua hapa sasa basi Hati zote ziko katika mikono yangu na mimi ndio mrithi halali wa

mali hizi.

Nyie toeni mimacho tu binafsi alicho kizungumza huyu Mama ni ukweli mtupu ya kwamba lazima mnishilikishe mimi!”

Yule Dada akasema

“nadhani wewe kijana unijui sio sasa nakupa masaa 24 tu uwe tayali ushatoa Hati zote vinginevyo utakufa siku si zako!”

kwa nnje nikamuona yule Bibi muokota machupa ya maji akiniita nikatoka kwenda kumfata,

“Shikamoo Bibi!”

“marhabaa Baba yangu kwanza pole sana kwa kufiwa na ndugu yako!”

Hasante Bibi nishapoa ukizingatia wote njia yetu ni moja tu mbele yake nyuma yetu!”

“Ni kweli kijana ila jiandae na vita vilivyoko mbele yako ni vizito sana, “Bibi unasema!?

“ni ukweli mtupu ninao kwambia yule binti mwenye kidomo domo ni Mchawi mwanga mkubwa tu usipokuwa makini atakupoteza ila kwakuwa mi nipo

nitakusaidia usijali!” baada Bibi yule kusema maneno yale akaondoka zake huku akiokota makopo tu nikarudi na kukuta mzozo tu,

Zile vurugu hazikuweza kunitisha kwa chochote kile. Nikabaki kuwatizama tu jinsi wanavyo tukanana.

Kisa mali za marehemu dahaa,

“Ndio nishasema vyovyote itakavyo kuwa na iwe tu zile gari tatu ni za kwangu mimi!”

“wee tena ishia hapohapo yani uchukuwe gari zote tatu peke yako alafu sie wengine tugawane nini?”

“hilo mtajuwa nyie wenyewe nikiwa kama mtoto wa kiume na Kaka wa marehemu nastahiri kuchukuwa kila kitu!”

“endelea kujidanganya hivyo hivyo eti mtoto wakiume kama kidume kweli uliye kamilika utachukua ila nikiwa kama Mwanamke ninaye jielewa tena

nasimamisha kama unavyo simamisha wewe Yale magari tunagawana!”

Wakazidi kuzozana tu mpaka kufikia hatua ya kurushiana makonde dahaa aibu hii jamani ndio kwaanza. Marehemu kazikwa siku si nyingi kidonda kwenye moyo

wangu kikiwa bado kibichi nawaona ndugu zake sijui feki au original wana dundana.

Nilicho kifanya ni kuingia chumbani na kuchukua panga nikatoka nalo kwa kasi ya ajabu na kupangusa ukutani huku nikipandisha sauti

“kila mmoja atoke apotee ndani ya nyumba hii.

Wakataharuki na kuanza kukimbizana yule aliyekuwa anataka magari matatu akawa mbishi kutoka akasema “wee boya acha kunitishia panga Niko hapa kudai

haki yangu siogopi kitu!”

Ahaa kumbe aogopi ehee kwa kasi ya ajabu nikamtandika panga la mgongo ila nilitumia ubapa akapiga yowe la. Uchungu.

“jamani nakufaa akatoka mbio mpaka nnje nikawa namkimbiza wale ndugu wengine wakajuwa kumbe jamaa hatanii kila mmoja akatokomea zake na kuahidi

kunionyesha si najifanya mjanja nitaona tu.

Baada kupita siku kama tatu hivi tokea tukio la kuwatimua wale ndugu nikaanza kuotaota ndoto za ajabu usiku some time nakula mavi au nyama mbichi za

binaadamu nikiamka Asubuhi nakuwa nimechoka vibaya mno naweza nikawa nimelala upande huu wa kitanda nikija kushituka Niko chini ya kitanda au

uvunguni kabisa.

Nikaitaji kumtafuta Bibi baada kufahamu vita ndio vimeanza hivyo.

Hakika nilianza kuwa mnyonge sana, furaha sikuwa nayo

kabisa, Rahma akajitahidi kuniuliza nini tatizo sikuwa na jibu la kumpa.

“Salumu kipenzi changu mbona umeanza kukonda ghafla,

Au ndio kumuwaza ndugu yako

Madebe?”

Nilimtizama Rahma huku nikiwa nimeshika tama”……

akaniuliza tena,

“Sasa baby ukikaa kimya utakuwa unitendei haki niambie nini tatizo

Ehee!”

akakishika kichwa changu kwa mikono yake miwili, mikono

rainii kisha akakiegemeza kichwa changu kifuani kwake.

Utasema mtoto ambaye anataka kunyonya”……

Nikajikunyata maana Rahma

ndio mwenye kunipa faraja kwa matatizo haya yanayo nisibu,

Washikaji nao hawakuacha

kunipa moyo na kuahidi watakuwa bega kwa bega pamoja nami katika vita hivi,

Siku hiyo nikiwa nafua nguo zangu nikiwa sina hili wala lile nikahisi kama mlango wa chumbani umefunguliwa na mtu kuingia ndani nikaacha kufua na kuingia

ndani kwa kunyata ajabu sikuweza kuona mtu. Nikasonya na kutoka zangu nnje ajabu nikamkuta Bibi kakaa kwenye kisturi nilipo muona nikafurahi sana.

Shikamoo Bibi!”

“marhabaa mjukuu wangu kijana wangu mwenzako wiki hii yote nilikuwa naumwa kutwa kucha nipo ndani nikashindwa hata kujinyanyua niweze kutoka nnje!”

“Dahaa pole sana Bibi yangu unaumwa nini?”

“Maralia ndio inayo nisumbua unionapo sijala chochote tokea juzi naishia kunywa maji tu!”

“Duhuu pole sana lakini hospital si umeenda au umemeza dawa tu?”

“mmh! uwezo tu wakununua chakula sina nitawezaje kwenda hospital au kununua dawa nilikata mualuvera nikaukamua nikanywa!”

Binafsi ni kweli Bibi hakuwa katika hali nzuri kihafya nikaingia ndani na kuandaa chai baada kuandaa kila kitu nikamkaribisha aweze kunywa chai akaingia ila

nikamsikia kama ameguna hivi kisha akasonya.

Nikataka kumuuliza ila nikanyamaza nisije kuzua mambo yasio nihusu.

Nikaenda nnje kuendelea kufua dakika kama tano hivi nikasikia ananiita.

“Wee Salumu”

Nikaenda kumsikiliza anasemaje baada kufika akaniambia kitu ambacho kilinistua sana

ITAENDELEA

Mzoa Takatakata Sehemu ya Nne

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment