CHOMBEZO

Ep 04: Play Boy

SIMULIZI Play Boy
Play Boy Sehemu ya Nne

 IMEANDIKWA NA: ANDREW CARLOS

*********************************************************************************

Chombezo: Play Boy

Sehemu ya Nne (4)

“..well done..!! well done jeff..!!!”

ilikuwa ni sauti ya dada mmoja aliyekuwa pembeni yangu akinisikiliza nilivyokuwa naongea na simu kisha akanipigia makofi, nadhani alikuwa akimjua vizuri helleiner..

“..jeff acha kuteseka kisa mapenzi jamani..?”

“..unasemaje..? kwani wewe nani..? na unamjua helleiner..?”

“..ahhaa haaaa haaaaa.., hapa mtaani kote wanajua mimi na helleiner tukoje.. she iz my best friend na mimi naitwa violet vivah ukipenda niitei vio na wewe nilikuwa nakusikiaga tu kumbe ndio jeff wewe..?”

Songa nayo sasa…

“..so pliz vio helpme..!! yupo wapi helleiner..?”

“..nikwambie kitu wewe mkaka sijui ndo jeff….!”

“..nifuate kwa nyuma nikakuoneshe alipo..”

Moyo wa matumaini ulianza kunijia ingawa lengo langu kubwa lilikuwa nikumpata jacky wangu, tuliongozana naye mpaka kwenye nyumba niliokuwa siifahamu kisha tukaingia mpaka ndani japo kulikuwa hakuna mtu hata mmoja..

“..subiri hapa hapa sebuleni nikakuitie..”

akaingia muleda akatoka na simu yake..

“..haya ongea naye kwenye simu..”

“..hallow helleiner, uko wapi na jacky wangu..?”

“..jeff mpenzi nipo huku bagamoyo na jacky wako niko naye anatibiwa na mganga wa kienyeji usihofu atapona tu..”

“..what…? unasemaaa…..???”

hasira kali zilinijaa mpakakufikia yule yule dada akanipora simu yake nakuikata..

“..umeshajua ukweli sasa..? haya unataka kupelekwa..?”

“..pliz Vio nipeleke nikawaone..”

“..so, unataka upelekwe sio..?”

“..ndio nipeleke..”

nikamshuhudia akiingia tena chumbani nakutoka na baunsa lenye bonge la mwili huku akiwa amevalia miwani meusi kisha akaniambia..

“..twende chumbani ukamuone huyo helleiner wako..”

nguvu ziliniishia,sikuwa na jinsi ikanibidi nijikokote hivyo hivyo mpaka huko chumbani huku nikiwa bado sijielewi elewi kama kweli helleiner yupo chumbani,ile naingia tu..

“..jamani helleiner nimekukosea nini..? jacky amekukosea nini..?”

nilijiona kama mikosi inaendelea kuniandama mpaka nikatamani kama ingekuwa ni ndoto tu, kwani jacky alikuwa ameningi`inizwa na kamba mithili ya mtu aliyejinyonga huku helleiner na michelle sura mbaya wakimpulizia moshi wa sigara kwa zamu..

“..ooohh karibu jeff…”

“…jeff pliz tusamehe..”

“..awasamehe nani wapumbavu wakubwa nyie..”

nilianza kwa kumfuata kwanza michelle sura mbaya huku mkononi nikiwa na kile kisu bila kupoteza muda nikamchoma nacho michelle.,

“…jeff pliz usiue bado nakupenda jeff wangu..”

ilikuwa ni sauti ya chinichini ikitokea kwa mchumba wangu jacky aliyekuwa amening’inizwa kwa juu nakunifanya nisitishe lile zoezi huku mwili wote ukinisisimka na pembeni yangu helleiner na vio wakitoa machozi nakunitazama,

“..jacky mpenzi mzima wewe..?”

nikaanza kumfungua zile kamba alizofungwa haraka haraka kisha nikamuweka begani nakutoka naye mpaka nje nakuwaacha helleiner na vio wakimlilia michelle..

“..niwaishe ubungo fasta..”

nilichukuwa tax nakuondoka tena kwa kasi ya ajabu huku nikimwacha helleiner mule chumbani akiwa na zile maiti..

“..atajijua kwanza shauri yake kwani mi ndio niliowatuma wamtese jacky wangu..”

nilijikuta naongea peke yangu kwa sauti ya chini chini huku nikimtolea macho ya huruma mpenzi wangu jaky.


Ndani ya dakika kama 15 tayari nilikuwa ndani ya Ubungo tena katika zile stendi za mabasi yaendayo morogoro..

“…mpaka moro nauli sh. Ngapi..?”

“..elfu 6 na mia 5 tu bro.., unataka tiketi ngapi..?”

“..chukuwa hii elfu 12 bhana tufanyie tiketi 2…”

“..pouwa usijari mwana..”

tulifanikiwa kupata basi la Hood lakwenda mpaka moro, nilimpakiza mchumba wangu Jacky kisha safari ya kuelekea morogoro ikaanza..

Njia nzima jacky alikuwa ni mtu wakulala tu na kila akishtuka nilikuwa nikimsogezea mfuko karibu hivyo alikuwa ni mtu wakutapika tu tena kama nyongo kwani matapishi yake yalikuwa ni yale ya njanoo..

“..pole jacky mpenzi, usijari utapona, utapona beiby..”

“..noo jeff siwezi kupona.. siweeezi..!!”

jacky alionesha kukata tamaa kabisa ya kuishi, kwa sauti ya kukauka tena ile ya kwa mbaali aliyokuwa akiitoa dhahiri utasema haponi, kidume siku zote hachoki kumpa mwanamke pole tena ukiwa unampenda kwa dhati.

Jacky alipata tena usingizi, hivyo nikabaki nimezubaa tu peke yangu huku safari ikiendelea, nilichungulia kwa nje nikagundua kuwa hapa moja kwa moja tupo maeneo ya chalinze kwani basi lilisimama kidogo,

“..samahani kaka..?”

ilikuwa ni sauti ya mdada aliyekuwa amekaa siti ya nyuma yangu nikageuza macho yangu kumuangalia anataka nini.., akatoa noti ya sh. Elfu 1..

“..naomba uninunulie vocha ya tigo hapo nje,mi dirisha langu halifunguki hapa..”

nilimchukulia nakumkabidhi, kisha akaniangalia mara mbili mbili huku akinilegezea macho ya uchokozi na mdomo akiulamba lamba kisha akaniangalia usoni mwangu nikamshuhudia akivuta pumzi juu juu, akaamisha macho yake nakumuangalia jacky wangu..

“..mpe pole mgonjwa namuona kalala..”

“..hapana wala si mgonjwa.. Nani kakwambia ni mgonjwa..?”

nikamkazia macho.

“..nimekusikia njia nzima ukimbembeleza nakumwambia atapona tu..”

“..aah okey ahsante kwa niaba yake..”

nikashangaa yule dada yani kama alikuwa anatafuta njia ya kuniongelesha sijui,

“..mnaelekea moro enh..?”

“..ndio.”

mara gari ikaendelea na safari yake hivyo yule dada akakaa kwenye siti yake vizuri..

Nilijikuta napitiwa na usingizi mkali na nilipokuja kushtuka nilikutana na kijikaratasi mikononi mwangu na sijui kilikuwa kimetokea wapi kilikuwa kimeandikwa hivi..

“..my number 0713214656 call me Esther.. Luv u Boy..!”

nilibaki kama nimepigwa na butwaa huku nisielewe kimetokea wapi? Nikamwangalia jacky wangu bado alikuwa usingizini, mara yule dada niliyomnunulia vocha kule chalinze akageuka na kuniangalia,kisha akanikonyeza nakunipa busu la kwa mbali lile la chini chini nakunitamkia maneno,

“..N a k u p e n d a a a a a h h…”

nikamnyoshea kidole cha kumkalipia lakini tayari jaky wangu kwa muda huu alikuwa ameshaamka na amekichukuwa kile kikaratasi nayeye akikisoma kisha akanitizama mimi na yule dada.. .

“.. Jeff kwanini unataka kunisaliti tena jamani..?”

“..Noo Jacky kwani vipi mpenzi wangu…”

“..Hiki kikaratasi kimetokea wapi sasa..”

“..Mmmh, ammh, mmh… Kitakuwa kimedondoka tu hapa bahat…”

Kabla sijamaliza kujitetea nikamshuhudia Jacky akijipinda pinda huku akiikunja sura yake kana kwamba kunakitu cha uchungu kimempata..

“..Jeff nakufa., Nakufa Jeff wangu ona..”

Sehemu ya begani kwake kulikuwa kumebadilika rangi nakuwa nyeusi sana huku damu yake ikivilia.,

“..Kwani vipi umefanyaje tena hapa..?”

“..Kule uliponitoa, wale kinadada walinitesa sana Jeff., wamenisababishia maumivu ya ndani kwa ndani hivyo naumia sana Jeff.. naumia mimi…”

Nilimshikashika kama namkanda kanda hivi mpaka usingizi ukampitia.

Haraka haraka nikachukuwa simu yangu mfukoni nakuingiza namba ya simu kutoka kwenye kile kijikaratasi alichonitupia yule mdada wa siti ya karibu yangu..

Nilipomaliza kuifadhi ile namba pale pale nikamtumia ujumbe mfupi..

“…NAKUOMBA UNIACHE NA MCHUMBA WANGU PLIZ USINIHARIBIE..”

kisha nikamtumia kupitia ile namba ya kwenye kijikaratasi.

Haikuchukuwa muda akawa amesharudisha majibu,

“..KWA BOY KAMA WEWE SIWEZI KUKUACHA.. WAJUA NAKUPENDA..! TENA NIPO SERIOUZ..?”

Ilinibidi kukaa kimya bila ya hata kumjibu kitu chochote, niliona anataka kuniletea mambo yaleyale yakina helleiner niliyoaçha kulee..

Nilichokifanya nikaizima simu yangu nakuirudisha mfukoni..


Ilituchukuwa kama lisaa 1 na nusu kufika katika huu mkoa wa morogoro, Ilikuwa ni mida ya jioni sana kwenye saa 12 hivi kwani kale kaubaridi kwa mbali ndicho kalichomfanya hata na Jacky wangu kushtuka kutoka usingizini..

“..Jeff naskia baridi.. Na kichomi kimenianza..”

“..Jikaze mpenzi wangu, tumeshafika sawa..?”

“..Saaawa..”

Tulishuka kwenye basi kisha nikamchukua Jacky wangu ile nataka kuondoka tu nilishangaa naguswa begani..

“..Samahani we mkaka..”

Alikuwa ni yule yule mdada aliyekuwa akinisumbua ndani ya basi., Nilijawa na hasira ghafla..

“..Unasemaje..?

“..Utakuja nikumbuka tu na lazima unitafute..”

“..Unasikia..? Kukumbuka haitakuja kutokea hata siku moja, na siwezi kukutafuta mpumbavu kama wewe..”

Nilimwangalia kwa jicho la dharau huku jacky wangu naye akimtolea macho.

Akachukua taksi nakutuacha pale tukisubiri usafiri wa kwenda mjini japo tukakodi gesti yeyote..

Kwakuwa hatukuwa na mizigo yoyote tukapanda daladala na ulipofika muda wa konda kudai nauli ndipo..

“..shiit..!! Jacky mpenzi nimeshapoteza pochi yangu..”

“..Kwani umeipotezea wapi tena..?”

“..Kwenye basi.. Kwenye basi Jacky hakuna kwingineko, tema atakuwa yule yule dada ameiokota..!”

“..Dada..? Dada yupi tena.?”

“…Si unakumbuka tuliposhuka tu. Kunadada alinishika bega..?”

“..nimekumbuka..”

“..enhee huyo huyo.. Lazima atakuwa kaikokota pochi yangu kwenye basi.. Ni yeye tu..”

Ilikuwa ni mshikemshike ndani ya daladala kwani kondakta hakutaka kutuelewa kabisa kuwa eti hatuna nauli, tulitukanwa sana na kudharauliwa ndani ya daladala na yule konda mpaka mmoja wa abiria akasimama na kuongea na kondakta..

“..Konda kuwa muelewa, hawa watu wameshakuambia kuwa wamedondosha pochi, kwanini hutaki kuwaelewa..?”

“..Skia nikwambie mzee, we hujui tu, hapa mjini kuna matapeli wengi tu., hawa wezi tu..!”

“..basi mi nawalipia nauli hao unaowaita matapeli., konda gani we usio na ubinadamu..?”

yule mzee alitoa noti ya shilingi elfu 1 nakutulipia nauli mimi na Jacky wangu..

“..Ahsante sana mzee wangu..”

Nilimshukuru huku aibu kubwa ikinishika lakini haikuwa na jinsi kwa kilichotokea..


Haikuchukuwa mwendo sana kwani ndani ya dakika kama 15 tayari tulikuwa morogoro mjini tukitokea Msamvu.. Giza lilikuwa limeshatanda, halmashauri yangu ya kichwa ikafanyakazi fasta kuwa nikiendelea kukaa hapa stendi bila yakuwa na pesa yeyote nitadharirika na kuaibika hivyo nikanyanyua ile simu yangu nakumpigia yule mdada tuliepanda naye basi..

“..hallow..”

“..yas naongea na nani..?”

“..Jeff Ryder, yule kaka uliepanda naye basi moja kutoka Dar leo..”

“..Anhaa naongea na yule boy aliekuwa ati na galfriend wake..?”

“..ndio, nahtaji kukuona sasa hivi..?”

“..right now..? (sasa hivi..?) ok njoo mpaka Boma Road karibu na magorofa ya Canvas, ukifika nipigie simu..”

Sikutaka kuchelewa kabisa fasta fasta nikaulizia boma road nakumbe hakukuwa ni mbali hivyo nilijikongoja na Jacky wangu hivyo hivyo japo alikuwa akijikongoja kutokana na kuumwa kwake..

Ndani ya dakika 20 tulikuwa maghorofa ya Canvas hivyo nikanyanyua simu yangu nakumpigia huyo dada..

“..Tumeshafika..”

“..Mko kwa wapi..?”

“..Hapahapa getini kama unataka kuingia humu ndani maghorofani..”

Haraka haraka akaja mpaka pale tulipo, hasira kali zilinishika huku nikiendelea kuamini kuwa ni yeye tu atakuwa aliichukuwa pochi yangu kwani alionesha kuwa karibu sana na mi kwenye basi na hata pale niliposinzia alinitupia kikaratasi nakuniandikia namba yake ya simu,

“..ole wake aniambie tofauti nazaa naye hapahapa na ndo atamjua Jeff Ryder ni nani..?”

Nilijikuta nikiongea mwenyewe kimoyomoyo huku nikiendelea kumtizama yule dada ambaye kwa muda huu alikuwa ameshafika mbele ya macho yetu pale getini..

“..Karibuni..!”

“..Hatuna haja ya kuingia wala kupajua kwako..”

kwa hasira nilizokuwanazo nilimshikilia nguo zake kwa nguvu zote huku nikimtikisa..

“..where is my wallet..? (pochi yangu iko wapi..)”

“..wallet..? What kind of wallet..?(pochi.? Pochi ya aina gani..?)”

“..Nimepoteza pochi kwenye basi tuliopanda na am sure 100% utakuwa wew umechukuwa tu..!!”

“..How sure you are..?(una uhakika gani..?) ati nskize kwa makini we mkaka, kama umetumwa hapa kwangu hupati kitu, nikuibie pochi boy kama wewe ninadhiki gani mie..?”

Yule dada alianza kuongea kwa jazba nakufanya hadi nianze kuamini huenda namsingizia, alilalamika sana mpaka Jacky wangu akaingilia kati..

“..Tumekuja hapa kujua tu kama uliichukuwa kwa bahati mbaya turudishie.. Embu tuonee huruma hiyo pochi ndio inakila kitu hata kadi yangu yake ya benki na pesa zakuniuguza, embu tuangalie hatuna hata nauli na hata hela ya gesti hatuna..”

Maneno makali aliokuwa akiyatoa Jacky kwenda kwa yule dada yalimfanya yule dada kukaa kimya kwa muda mrefu kisha..

“..Naomba nieleweke jamani, sijaichukuwa pochi yenu, na niko tayari kuwapa hifadhi kwangu kwani naishi alone..”

Ilinibidi kumuachia Mungu tu kwa yote huku akili yangu yote nikiielekeza nijinsi gani nitaishi na Jacky wangu katika huu mkoa tena bila yakuwa na hata senti tano., Tuliingia kwa yule dada alikuwa akikaa ghorofa ya chini tena peke yake huku akiwa amekamilika kwa kilakitu mule ndani, Tulifikia sebuleni huku akielekea jikoni na baada ya muda alituletea juisi kisha..

“..Jamani karibuni., kuweni wavumilivu nipo napika huku jikoni..”

“..poa usijari..”

Jacky alitaka kwenda kumsaidia lakini nilimzuia kutokana na hali yake kiafya kwani hakuwa akiendelea vizuri..

Ndani ya dakika kama 20 tayari alituletea hotpot lilokuwa limejaa mapocho pocho kama kuku rosti na wali tena ule wali maua, kwa njaa niliokuwa nayo nilijihisi kama minyoo ya tumboni kwangu imesimama, nilifakamia chakula kama pleti mbili nikamalizia na ile juisi kisha nikanywa na maji..

Tulipomaliza kupata chakula wote, alikuwa na vyumba viwili tu na jiko na bafu,choo..

Tulipiga sana stori za maisha, nilimficha asielewe chanzo cha mimi na Jacky kuwa pamoja, na akatuambia kuwa yeye ni mfanyabiashara tu hapa Moro tena anaishi peke yake na ni raia wa kenya.

Ulipofika muda kulala…

Alituonesha chumba ambacho nitalala mimi na Jacky wangu kisha nayeye akaenda kulala chumbani kwake..

Mawazo mengi bado yaliendelea kutawala ndani ya kichwa changu ukizingatia nilikuwa sijui hata nitaishije na jacky wangu bila ya kuwa na pesa yeyote..

Hatimaye nikapitiwa na usingizi..


Ulikuwa ni usiku sana na kilichonishtua ni baridi kali lililosababisha mkojo kunibana, sikutaka kuwasha taa, nikajikongoja mpaka chooni kujisaidia,wakati narudi chumbani kwangu ndipo nikapishana na yule dada naye alikuwa akielekea chooni akaniongelesha kwa sauti ya chini chini,

“…mmh Jeff mambo vipi..?”

“..salama tu..”

Nikamjibu huku nikielekea chumbani kabla sijaingia alinivuta mkono kisha..

“..usiku mwema tena Jeff..”

Halafu akaniachia.

Niliingia chumbani nakuwasha taa, kisha nikamshika Jacky wangu tena kwa maeneo ya usoni taratibu..

“..nakupenda Jacky wangu na sintokuja kukusaliti mpenzi..”

Nilijisemea kimoyomoyo huku nikiendelea kumtizama Jacky wangu akiwa usingizini., nikiwa bado naongea peke yangu mara mlango ukafunguliwa..

“..Shhh.. Natumai umeshajua kilichonileta Jeff..”

“..whaaat.? (niiini..?) hapana please go back to your room.. (samahani rudi chumbani kwako..)”

“..wajua saa ile vile nimekushika mkono, nilipaka dawa ya usingizi kwa mkono wangu..”

“..mbona sikuelewi..?”

“..najua tu umeshamshika gal wako.., so hapo alipo anausingizi balaa, wala hawezi jua lolote..!”

Sikutaka kuamini mpaka nikamtikisa kwa nia yakumuamsha Jacky wangu ili aamke lakini aliendelea kulala fofofo huku akikoroma bila hata kushtuka..

“…please just stand up Jeff..(samahani nyanyuka basi Jeff..)”

“..no no no.. I can’t..(hapana, sitaki..)”

Nilimkazia macho lakini bado yule dada aliendelea kuning’ang’aniza kwenda chumbani kwake., ilifika muda yule dada akaanza kuvua nguo zake zote mpaka akabaki mtupu kabisa huku akitoa machozi..

“..nahitaji jibu moja tu Jeff, sex or no sex..”

“..please nionee huruma nina mchumba wangu huyu hapa tena bado mgonjwa embu muone mwenyewe..”

“..nadhani ati hujanielewa vizuri Jeff., sex or no sex.?”

“…sijakuzoea, ndo kwanza tumejuana jana tu jamani na pia siwezi kumsaliti mpenzi wangu..”

“..Jeff i had almost 2 yearz without any boy.. So please help me just for sex.. Please.., Jeff please.. (..Jeff nina kama miaka 2 bila ya mwanaume., kwahiyo nisaidie japo nifanye mapenzi nawe jamani.. Nielewe.., nielewe Jeff..)

Safari hii alilegeza sauti yake kabisa nakuwa ya kimahaba nakunifanya hata

Kale kaubaridi nilikokuwa nakasikia kaishe ghafla nakufanya nijihisi joto si joto hapo hapo

kidume mie uzalendo ukaanza kunishinda..,

“..Play boy., alwayz ni play boy tu.. Wacha nikampagawishe hanijui ati..”

nilijisemea kimoyomoyo huku nikitikisa kichwa changu kuonesha ishara ya kumkubalia.., kisha akafurahi nakuchukuwa nguo zake na tukaongoza mpaka chumbani kwake huku nikimwacha Jacky wangu kalala fofofo pale kitandani..

Harufu ya ‘air freshner’ ndio ilikuwa ikinivutia sana tulipoingia tu chumbani kwa huyu mdada, hakuwa amewasha taa zaidi ya mishumaa midogo midogo ambayo nayo ilikuwa ikitoa harufu nzuri sana.. Nikiwa bado nashangaa shangaa umaridadi wakile chumba.., yule dada akanivuta taratibu nakuniweka kitandani kwake..

“..Jeff..? Unajiskiaje kuwa humu kwangu..”

“..dah.. so unbelievable.. (yaani nashindwa kuamini..) umesema unaishi peke yako..?”

“…yeah., sure Jeff.. (ni kweli Jeff..)”

Kisha akavuta pumzi juu juu nakunisogelea mpaka usoni mwangu nakuanza kuingiza ulimi wake kwenye maskio yangu huku akilalamika..

Alipomaliza maskioni aliutelezesha ulimi wake mpaka ukakutana na mdomo wangu nakilichofuata nikushindana kunyonyana ndimi zetu kila kona huku tukipokezana kupeana ndimi zetu zilizochanganyika na mate..

“…Jeff..!! Jeff..”

“..yeah.. yeah.. ni a a a mbiee uhhff..!!”

“…do you know how to suck Jeff..?(..Jeff unajua jinsi ya kunyonya..?)”

“..yeah why not..” (..ndio kwanini nisijue..)”

Akakaa vizuri huku kanitanulia mapaja, utundu ukaanzia kwenye maziwa yake taaratibu mpaka kitovuni huku nikimkwarua kwa makucha kwa mbaali huku nikikaribia yale maeneo yetu mara nikaskia mlio wa simu yangu ukiita chumbani kwangu nilipomuacha Jacky..,

“..Sorry.. Naweza kwenda kupokea simu yangu..?”

“..nöo nöo Jeff..! Huwezi.. Sitaki endelea bwana..”

Nikaendelea kumshika shika mapajani mwake huku nikijiweka sawa kumnyonya lakini ile simu ilizidi kuita tu..

“..please nakuja sa hivi, ngoja nikapokee hiyo simu labda ya muhimu sana..”

“..Jeff we hurudi bwana., kama unataka tusex kabisa angalau hata kimoja ndio uende ukapokee hiyo simu yako..”

Alivyoongea hivyo nikama amechochea hisia zangu upya kwani nilivua boxer yangu naye akaniwahi kunishika kifua changu huku akipapasa ‘garden love’ (kifua kilichojaa nywele) kisha akakilaza kichwa chake kifuani mwangu na mkono wake mmoja akaupitisha hadi kunako kisha…

“…Jeff nimeamini we mzuri., umekamilika tena kila sehemu.. Ila nataka nihakikishe kwenye kitu kimoja tu..”

“..kitu gani hicho..”

“..Sex Jeff hakuna cha zaidi.., nahitaji kukuona ukini…”

Kabla hajamalizia kuongea tukahisi mlango kama umefunguliwa, tukabaki tukishangaa tusielewe kuna kitu gani, yule dada akanyanyuka nakuchukua kanga yake..

“..usitoke Jeff nisubiri humu humu chumbani kwangu..”

Kidume cha mbegu ujasiri ukaanza kama kidizaini kunipungua vile, kwani nilikuwa sielewi elewi huku akili ikinituma huenda Jacky wangu kaamka nakanikuta sipo naye hivyo ananitafuta.,

Ndani yadakika kadhaa nikasikia tena simu yangu ikiita na kwa muda huu aliniletea yule mdada..

“..chukuwa pokea., pokea..”

aliniambia kwa sauti ya chinichini., niliangalia ile namba lakini sikuwa naifahamu hivyo nikapokea tu hivyo hivyo..

“…hallow., nani mwenzangu..?”

“…Mie Vio vivah rafiki yake na helleiner..”

“..enhe nikusaidie nini..?”

“..unajifanya hujui ulichokifanya Dar enh..?”

Kabla hajamalizia kuongea nikamkatia simu nakuiweka pembeni..

“..Jeff ati kwani ni manzi gani huyo aliokupigia phone..?”

Aliniongelesha huyu mdada.,

“..ni long story (..hadithi ndefu).,achana nayo.., vipi mpenzi wangu hujamkuta ameamka..?”

“..kwa ile dawa..? From now onwards.., it takes 8 up to 10 hours..(..kutokea muda huu.., inachukuwa masaa 8 hadi 10)., tuendelee tu Jeff..”

Tukaanza zoezi upya kabisa la kumtengeneza huyu mtoto wa Ki Kenya kwani kiukweli alikuwa nakamwili kauchokozi fulani kuanzia kifua mpaka miguu na maeneo ya nyuma kidoogo., safari hii sikumshika shika sana..

“…where is Condom..? (..kondomu ziko wapi..?)”

“..Jeff si nilishakwambia ninamda mrefu sijasex..? Sasa hizo kondomu nizitolee wapi..?”

“..kwahiyo hamna..?”

“…yeah, hamna lakini tunaweza kufanya hivi hivi bila kutumia kinga..”

“..Niskize.! Sijawahi na wala haitatokea hata siku 1 kufanya mapenzi bila kinga..”

Nilimdanganya tena huku nikimkazia macho kana kwamba mie sio play boy na wala siendagi kavu kavu wakati siyo..

“..whaat…! (..niini..!) kwa jinsi nilivyokuwa ‘hot’ lazima ni sex nawewe Jeff ‘by any means..'(..kwa njia yeyote..)”

Nilimfanyia vituko mpaka akabadilika kabisa huku akihema juu..

“..let us make it tommorow..(..tufanye kesho tu..)”

Maneno hayo yalimuuzi sana nakumfanya anikumbatie kwa nguvu zote huku akivuta nanii yangu kwa nguvu..

“..Jeff.. Tufanye pliz..! Embu ingiza huko jamani..”

“..huelewi tu..? Kondomu hamna, tufanye kesho..!”

“..aaku.. mi sitaki bwana.. Sitaki..nataka sa hivi.. Nifanye Jeff..”

Mafua ya ghafla yalianza kumtoka huku akionesha sauti kama ya kulia lia hivi kwani nilikuwa nimeshamlegeza haswaa, nikamkubalia nakumkalia juu yakifua chake kisha nikaanza mautundu zaidi nakumfanya alalamike tena kwa sauti ya juu sana., nilipomaliza cha kwanza tu nilishangaa nafinywa namakucha yake akitaka tena kingine. Mara meseji ikaingia kwenye simu yangu

“…NIPO HAPA MLANGONI MAGHOROFANI NIFUNGULIE..

“…Jeff vipi mbona umebadilika ghafla..”

“..am mh mh kuna meseji imeingia nashindwa kuielewa elewa…”

“…achana nayo kwanza zima tu hiyo phone yako tuendelee bwana..”

Niliona kama ananizingua tu kwani mwili wangu wote ulikuwa umebadilika nakusinyaa huku nikisitisha zoezi la kuendelea kusex., nikavaa boxer yangu tayari kwa kuondoka kwenda huko nje..

“…sasa atakuwa ni nani jamani., mbona nimekwisha tena nimepatikana haswaa Jeff mimi..”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikijitwisha nguvu na uwezo wa kijasiri tayari kwa kukutana na yeyote hapo nje., ile nataka kutoka tu mule chumbani..

“..Jeff unataka kurudi chumbani kwako mara hii jamani..? No tuendelee bwana pleaseee..!”

“..funguo za nje kabisa unaziwekaga wapi..?”

“..Jeff huko nje unaenda kufanyaje tena..?”

Uzalendo ukanishinda ikabidi nimshirikishe naye ajue natoka nje kufanyaje..

“..kuna meseji nimetumiwa na mtu nisiyemjua wakati tukisex na ameniambia eti yupo nje nimfungulie..”

Nilipomwelezea tu nilishangaa yule mdada akiangua kicheko tena cha dharau nakunifanya hasira zinizidi nakuamini huenda anajua kila kitu..

“..mbona unacheka..? Yani nipo seriouz nakwambia unanicheka si ndiyo..?”

“..hapana Jeff kumbe nikitu hicho tu., embu rudi bwana tulale..”

“…kwahiyo unamjua aliyonitumia hiyo meseji..?”

“…yeah., si mimi..! Embu angalia vizuri hiyo namba..?”

Nilijihisi kama mazingaombwe kwani nilipoiangalia ile namba vizuri ni kweli ilikuwa namba ya huyu mdada..

“…kwanini umeamua kunitumia hivyo na umeituma sa ngapi..?”

“..Jeff meseji niliituma wakati upo chumbani kwako na gal wako.., na ilikuwa njia tu ili utoke huko chumbani… Kumbe bado ilikuwa ‘pending’ (hewani) na ndio imeingia ‘right now..?(sasa hivi..?)”

Nilishusha pumzi huku nikimwangalia huyu dada mara mbili mbili bila ya kumpatia jibu lolote..

“…Siku nyingine utakuja kuniua kwa presha we mwanamke..”

Nilisema kiutani huku nikirudi kitandani kwake kwa fujo zote nakuvua tena boxer yangu..nilianza tena kwa kumpapasa huku nikijiandaa kumpatia bao la pili..

“..Jeff wajua we ni mtamu..?”

“…Sure..? (..kweli..?)”

“…unajua jinsi ya kumwandaa gal..”

Akiwa bado ananisifia hapo hapo nikaupeleka mdomo wangu mpaka kwenye kitovu chake nakutoa ulimi wangu tayari kwa nakuanza kumnyonya.., alilalamika sana huku akijikunja kunja mithili ya nyoka hapo hapo nikaanza zoezi zima la kummaliza mpaka akaning’ata eneo la shingoni mwangu kwa mapenzi niliyompa..

Nilipomaliza tu kusex usingizi ukaanza kuninyemelea huku nikijihisi mwili kuchoka kwani nikamuda kidogo sikusex…


Ubaridi uliokuwa ukiingia ndani ya mwili wangu ndio uliofanya nishtuke usingizini .. Nilijigundua bado nipo chumba ambacho si changu hivyo nikamwacha yule dada akiwa mtupu tena yupo bado usingizini nakuelekea chumbani kwangu alipo mchumba wangu Jacky..

Nilipofika sikuiwasha hata taa nikanyata taratibu mpaka kwenye kitanda nakufunua shuka taaratibu tayari kwa kulala..,

~ Asubuhi ~

Nilikuwa bado kitandani huku nikijiona mvivu mvivu wakuamka, nilimwangalia Jacky wangu pembeni yangu bado alikuwa kapitiwa na usingizi mzito..,

“…Jacky mpenzi amka, amka mpenzi..”

safari hii nilimwamsha akaamka nakunitazama.,

“…mambo Jeff wangu..? Umeamkaje..?”

“..safi tu., enh niambie unajiskiaje..? Bado unaumwa..?”

“..Jeff nahisi nimeshapona, kwani sijiskii kuumwa kabisa..”

Nikiwa bado naongea na Jacky mara nikamshangaa ananitolea macho sana sana maeneo ya shingoni mwangu kisha akanishika vizuri nakuniangalia..

“..Jeff umefanyaje tena hapa shingoni..?”

“..mbona unanitisha hivi..? Kwani kunanini..?”

“..Jeff usijifanye hujui, si alama za meno hizi..? Nani amekufanyia hivi na lini mbona jana hukuwa nayo..?”

“..kweli Jacky nina alama..?”

Nikamuuliza tena kwa kumtolea mijicho kana kwamba sijui chochote kilichonisibu..

“..Kweli Jeff hizi ni alama za meno kabisaaa tena sijui aliyekung’ata ni mwanamke..?”

“…Jacky..? Jacky..? Umeshaanza kuniudhi mpenzi wangu, yani badala unionee huruma kwa kilichonitokea we unaanza kuhisi mambo ya ajabu ajabu.. Haya basi tufanye wew ndio ulioning’ata usiku maana si nimelala na wewe..?”

Niliweka ukali mpaka Jacky akawa kama mchozi unamlenga lenga.,

“..basi Jeff mpenzi wangu nisamehe nimekukosea..”

“..Ujue Jacky yani we kila siku nikunihisi tofauti tu.., kwanza unajua jinsi gani nakupenda..? Wanawake wangapi wananitaka lakini siwataki kwa ajili yako..?”

Hayo maneno yalimuingia sana Jacky nakuanza kulia tena kwa sauti ya juu nakunifanya nitoke zangu mule chumbani nakuelekea sebuleni huku nikimwacha Jacky akiendelea kulia peke yake..

Nilipofika sebuleni nilimkuta yule dada keshahamka …

“..Jeff niambie..”

“..safi tu zakuamka..?”

Kabla sijamjibu mlango ule wa chumbani kwangu ukafunguliwa kisha Jacky akatoka huku macho yake yakionekana mekundu sana kutokana na kulia, tena alionesha sura ya huruma sana akaja mpaka pale subuleni nakukaa kochi moja na mimi..

“..Jacky mambo, umeamkaje..?”

Yule dada alimuongelesha Jacky..

“..nimeamka salama na nimepona kabisa.. sijui wewe..”

“..niko pouwa., tena bora umeamka nahitaji unisindikize twende sokoni tukanunue mahitaji kwani yameniishia kabisaa..”

“..usijari niko tayari kukusindikiza kwani ni muda gani…?”

“…saa hivi ngoja nijiandae na wewe jiandae tuondoke.., Jeff wewe tutakuacha kwa muda..”

“..Pouwa mtanikuta msijari..”


Ndani ya dakika kama 5 tayari Jacky na yule mdada walikuwa wameshamaliza kujiandaa wakatoka nje nakuelekea huko sokoni nakuniacha kidume peke yangu..

Kama kawaida yangu huwa napenda sana kusikiliza nyimbo laini na kwa bahati nzuri kulikuwa na cd ya ‘kenny Rogers’ nikaiweka huku nikivuta hisia kwa mbaali kwani nyimbo ya ‘Lady’ ilikuwa ikinikosha sana., Nikiwa bado katika dimbwi la burudani mara nikasikia mtu anapiga hodi, mwanzoni nilijua huenda ni nyumba ya jirani lakini ile sauti iliendelea zaidi nakunifanya nichungulie kwa dirishani ndipo nikagundua kuwa hodi inapigwa nyumba hii nilipo nikafungua mlango kisha..

“..karibu..! Karibu dada..”

“…ahsante., mwenyewe nimemkuta..?”

Alikuwa binti mmoja hivi mdogo mdogo mweupee..

“…unamuhitaji nani..? Dada mwenye nyumba..?”

“…ndio Irene nimemkuta..? Kwani aliniambia atarudi jana kutoka dar..”

“..Yeah nikweli amerudi jana kutoka Dar.., na kwasasa ameelekea sokoni., Kwani umempigia simu leo..?”

“…Nah simu yangu imeisha chaji kabisa..”

Nikachukuwa simu yangu nakumpigia lakini namba yake ikawa haipatikani, na Jacky wangu hana simu, hivyo nikamkaribisha tu ndani

“..Ok karibu ndani umsubiri atarudi muda si mrefu kwani ameenda na rafiki yangu..”

Sikutaka kumwambia kuwa yupo na mchumba wangu kwani kiukweli ninakaugonjwa na hawa mabinti weupe..

Nilijikuta nikijiuma uma mwenyewe huku nikiishiwa pozi kabisa kila nikitaka kumuangalia yule binti nageuza sura nakuangalia pengine..

“…mh.. mh.. mh.. umesema unaitwa nani vile…?”

“…me…? Naitwa Sammy…”

“…Ooh, jina zuri sana bila kukosea we ni mpare hee…?”

“…nat…, mi mnyaturu..”

“…dah basi ndio maana.., nilijua tu kwa huo weupe wako lazima utakuwa kati ya hayo makabila..”

Nikawa namuongelesha huku naelekea kwenye kabati la vyombo nakutoa grasi kisha nikafungua friji nakutoa juisi nakuimimina nakumpatia,

“..karibu juicy Sammy…”

“..mh, mara hii jina langu umeshalikariri..? Lakini hujaniambia we waitwa nani..?”

Aliongea kiutani nakufanya moyo wangu kuingiwa na furaha ya ajabu kwani kwangu ni kosa kubwa sana kama ukitaka kunifahamu au kunijua tena kwa binti kama huyu..

“…Niite Jeff Ryder…”

“..Kwani we ni mwenyeji wa wapi..?”

“..am.. mh.. mh.. mie ni mchaga…”

“..kweli..?”

“..ndio..”

Nilishangaa Sammy kunizoea ghafla huku tukiendelea kupiga stori kana kwamba tunajuana..

Alipenda sana nyimbo nilizokuwa nasikiliza,

“…Jeff pliz, embu rudisha hiyo nyimbo ya ‘Lady’ tena naipenda kweli..”

Nilimrudishia akaisikiliza huku anaimba kwa sauti tamu na nyororo..

Sikutaka kufanya makosa kabisa nikachukuwa namba yake ya simu nakumuahidi nitamtumia meseji kama ataiwasha simu yake ataikuta..

Ndani ya kama Lisaa 1 na nusu tayari Jacky wangu na yule mdada (Irene) walikuwa wanagonga mlango.. Nikainuka pale kwenye kochi nakwenda kuwafungulia mlango..

“…Waooh jamani Sammy.. Upo..?”

“..niiipo shosti za masiku..?”

Ilikuwa ni sauti ya Irene na Sammy wakikumbatiana na kuzungumza..

Niliwapokea vitu nakupeleka mpaka jikoni kisha nikarudi sebuleni nakuwakuta ndo kwanza Sammy na Irene wamenogewa kwa stori huku Jacky wangu akiwatolea macho..

“..basi nikwambie shosti kule Dar kuna kimbembe huko..?”

“..kitu gani tena Sammy..? Embu nipe michapo Irene mie..!”

“Michelle kauliwa…

Moyo ukanilipuka ghafla na nisielewe ni Michelle yupi huyo aliyeuliwa.., nikajiweka vizuri kwenye lile kochi kwa kusikiliza,

“…michelle shosti.., yule wa kwa Mama Grace..”

“..usiniambie..? Enhe ilikuwaje kuwaje akauliwa..?”

Akili ikazidi kunichemka huku nikibaki nisielewe,

“..Mama Grace..? Mama Grace ndio nani tena..? Au ndio Mama yake na Helleiner..?”

Nilijikuta nikijisemea kimoyo moyo huku nisielewe ni Michelle yupi kwani kama ndio yule niliyemuua kule Dar nitakuwa nimekwisha tena Jeff mimi..

“…baasi.., unaambiwa majambazi kama 3 hivi wakawavamia.., wakawakata kata mapanga kuanzia Michelle mpaka wazazi wake na mfanyakazi wao…”

Niliposikia hivyo tu nikashusha pumzi nakuelekea kwenye friji kisha nikatoa maji nakunywa, sikutaka tena kusikiliza ile stori kwani nilikuwa na uhakika kuwa siyo michelle niliomuua mimi..

“..Jamani niko hapa nje nashangaa shangaa kidogo..”

Niliwaacha wakiendelea na stori huku mie nikitoka nje na baada ya dakika chache Jacky wangu naye akanifuata,

“..wewe nawe..? Yani kunifuata fuata nyuma tu kama nyuki..?”

Nilimwambia Jacky kiutani huku akirudishia vizuri ule mlango wakutokea nje..

“…Jeff mpenzi wangu inakuwaje sasa mstakabali wetu..?”

“..wa kuhusu.?”

“..kwahiyo umesharidhika kabisa tukae hapa.?”

“..Jamani Jacky..? Leo ndio kwanza siku ya kwanza na hilo suala nalitambua tuvumilie kwa siku chache ntajua cha kufanya..”

Nilimjibu Jacky huku moyoni mwangu nikiwa na uhakika wa kuishi hapa hapa kwani Irene ni kama tayari mtu wangu kwa jinsi alivyojileta mwenyewe..

“..wacha niende ndani nikatengeneze chakula cha mchana..”

“..poa.”

Jacky alirudi ndani nakuniacha pale nje na haikupita muda nikasikia kama naitwa huko ndani..

“..Jeff..? Jeff..?”

Nikaingia sebuleni..

“..yap..”

Alikuwa ni Irene akiniita,

“..Mgeni anataka kukuaga anaondoka..”

“..okey jamani Sammy karibu tena..”

Nilimshika mkono ili nimuage nikajikuta nasisimka karibu mwili wote huku nikimtolea macho eneo lakifuani mwake ambapo alikuwa kayapiga ‘Jeki’ matiti yake na hivi yalikuwa meupe dah kidume mie nikaishia kuyaangalia huku nikijisahau na kuendelea kumshika mkono, mpaka nilipojishtukia kuwa Irene ananiona ndipo nikamwachia,

“..karibu., karibu tena..!”

“..Jeff si umeshamuaga jamani mbona mara mbili mbili tena..?”

Alihoji Irene kiutani huku akifungua mlango wa nje, fasta fasta nikamwangalia Jacky pembeni yangu hakuniona na Irene pia ndipo ukawa mwanya wa kumkonyeza mtoto Sammy kisha nikamwambia maneno kwa vitendo kuwa nitampigia simu, alinielewa akaondoka zake huku Irene akiendelea kumsindikiza..


Siku nzima niliiona kama mbaya kwangu kwani kila nikijaribu kumpigia simu Sammy ilikuwa bado haipatikani,

“..au atakuwa kanidanganya nini kanipa namba za gari..? Yani muda wote hajafika kwake tu.? Au kasahau kuiweka simu yake kwenye chaji.?”

Nilijikuta nikijiuliza maswali mengi bila ya kuyapatia majibu huku nikiwa nimeshakula na nipo chumbani kwangu huku Jacky na Irene wakiwa sebuleni wanacheki tv..

Nikaamua kutuma meseji nzuri ya uchokozi kwa Sammy..

‘..MH, HATA KUNIAMBIA KAMA UMEFIKA SALAMA..? Its Me Jeff mchaga wa maghorofani kwa Irene Moro..’

Kisha nikaituma haraka haraka kabla Jacky wangu hajatokea.

Nilikaa kama dakika 10 nzima bila majibu yeyote wala simu yangu kuonesha kama kuna meseji imeshatumwa(delivery), Ndipo baadaye sana nikasikia mlio wa meseji katika simu yangu, furaha ya ajabu ikanijia huku nikiamini kwa asilimia 100 atakuwa ni mtoto Sammy na tena atakuwa ametuma majibu mazuri, Nikaichukuwa simu huku mdomo wangu na macho na vidole vikionesha kufurahi,

“..mie ndio Jeff Ryder bwana na hapa Moro nitahakikisha nafagia wote..”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikitaka kuifungua ile meseji ndipo nikashtuka baada ya kuona meseji inatoka kwa Helleiner, mwili wote ukawa kama umepigwa ganzi huku nikijihisi kizungu zungu, nikajikaza ili japo niweze kuisoma ile meseji,

“…SMS YAKO NIMEIPATA DEAR, KESHO ASUBUHI NA MAPEMA NITAKUWA HAPO..”

Nilirudia kuisoma mara mbili mbili bado jibu lilikuwa ni lile lile kuwa inatoka kwa Helleiner,

“..aha ha.. Ah ahaa haiwezekani..”

Nikajikuta nina Jazba huku nikiingia sehemu ya kuangalia meseji nilizotuma nikagundua kuwa nikweli nilituma meseji kwa Helleiner..

“..Nimekwisha Jeff mimi, ona sasa, aiyaa iyaa.., iyaaa.., iyaaaa..”

Nilijikuta sauti ya juu ilioambatana

na mchozi huku mafua ya ghafla yakininyemelea huku nikiendelea kuitolea macho ile simu.. Mara ikaanza kuita, haraka haraka nikapangusa mchozi huku naichukuwa simu nakuiangalia anayepiga,

“..yale, yale..”

Nilizidi kuumia moyo, kwani simu ilionesha jina la Helleiner na ndio aliokuwa akipiga simu, niliiacha ikaita wee mpaka ikakata yenyewe, akapiga tena mara ya pili ikaita sana tu nayo ikakata, ile anapiga mara ya tatu nikajipa moyo wakijasiri nakuona litalo na liwe nikaipokea huku nikiikaza sauti yangu haswaa tena kwa kukoroma na kwa hasira kali..

“..Hallow, Unasemaje..?”

“..Hee, samahani naongea na Jeff..?”

“..ndio mimi sema shida yako..?”

Nilimkazia sauti haswa mpaka akakata simu mwenyewe, haikupita tena muda akapiga, kwa safari hii ule woga ulikuwa umeshanipotea hivyo nikaipokea bila kuwa na wasiwasi wowote,

“..Hivi we dada..? Unachotaka kwangu ni nini..?

Sikutaki enh..? Sasa na umesema utakuja hiyo kesho, nakusubiri malaya mkubwa wee na ntahakikisha na wewe nakuua tu..”

Nilimtukana nakumkatia simu huku nikifurahi kimoyomoyo nakuona kwa mikwara niliompa kama atapiga tena simu basi atakuwa mwanamke sugu tena lile nunda haswa.

Hata ile hamu ya kulala ikapotea ikiwa na mawazo yakumuwazia Sammy nayo yakapotea, nilichukuwa kioo nakujiangalia usoni, macho yangu yalikuwa mekundu sana yalioambatana na mishipa iliokuwa imenitoka pembezoni mwa paji la uso. Nikiwa bado najishangaa pale kwenye kioo, nikasikia tena mlio wa meseji katika simu yangu pale kitandani nikaiwahi nakufungua ile meseji cha kwanza kuangalia ilikuwa jina kujua inatoka kwa nani..,

“..dah huyu Helleiner kweli mbishi, na asipoangalia nitamteketeza kweli..? We muache tu hajui kama Jeff sometimes ni Mafia na sometimes ni Play boy..”

Nilijisemea kimya kimya huku nikiendelea kuifungua ile meseji nakuisoma,

‘JEFF NIMEKUKOSEA NINI GHAFLA UNANICHUKIA HIVYO..? Au KUJA KWENU LEO NA NILIVYOKUPA NAMBA YANGU NI KOSA..?”

Nikashtuka nakujiweka vizuri huku nikiirudia kuisoma ile meseji mara mbili mbili, nilipomaliza kuisoma nikaangalia imetumwa na nani napo jina ni lile lile la Helleiner,

“..Hapana.. Hapana hapa kuna mchezo nafanyiwa sijijui tu..”

Ikanibidi nianze kuichambua simu yangu, na nikalipitia jina moja mpaka jingine katika simu yangu na nilipomaliza nikagundua kuwa hakuna jina la Sammy katika simu yangu,

“..embu ngoja namba ya Helleiner naijua yote ni 0713133633..”

Nilijikuta naongea peke yangu huku nikitafuta jina la Helleiner kwenye simu yangu, nikalipata na nilipoangalia namba zilikuwa tofauti na ninazozijua., akili ikaanza kunichemka,

“..Ooh Shit, maskini nilikosea badala ya kusevu jina la Sammy niliandika Helleiner dah..”

Bado nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa ghafla kwa kile kilichonitokea huku nikiendelea kuongea mwenyewe na kijasho chembamba kikinitoka. Nikachukuwa simu nakufuta lile jina la Helleiner nakuliandika la Sammy kisha nikampigia simu Sammy ili nimuombe msamaha kwa kilichotokea mpaka nikamtukana.

Simu yake iliita tu bila kupokelewa, nilijaribu kama mara mbili tatu bado haikupokelewa, nilichokifanya nikaenda mpaka sebuleni ambapo alikuwepo Jacky wangu na Irene wakiangalia tv, bila woga wowote,

“..Samahani Irene simu yako ina pesa kidogo..? Kunamtu nahtaji kuongea naye..”

Nilimdanganya Irene akanipa simu nikarudi mpaka chumbani kumpigia simu Sammy na nilijua kwa njia hii lazima atapokea tu simu nikapiga.

“..niambie shosti..”

Alipokea kwa mbwebwe nikabaki kimya kwa muda kisha nikamjibu,

“..unaongea na Jeff na siyo Irene..”

“..Jeff..? Hivi ulivyonitukana na ukatishia kuniua kama ulivyoua sijui huko dar., bado unanifuata fuata..”

“..zile zilikuwa ni hasira tu si unajua namba yako nilikuwa sijaisevu jamani..?”

“..Jeff we utakuwa muuaji kweli, nakuogopa ahaa haa na nitamwambia tu shosti Irene..”

Simu ikazima chaji, nikaenda mpaka sebuleni tena kuchukuwa chaji na nilipoiweka tu nikampigia tena lakini akawa hapatikani tena..

Nguvu ziliniisha kidume mimi, sikuwa tena na jinsi zaidi ya kufuta namba ya Sammy na kisha kumrudishia Irene simu yake sebuleni…

“..ahsante Irene, simu yako hii hapa..”

“…poa..”

Aliichukuwa huku akiendelea kuangalia tv, sikuwa nahamu hata yakuiangalia hiyo tv,

Kitendo cha kugeuka tu pale nakuelekea chumbani, nikasikia mlio wa simu ya Irene ukiita, nilibaki njia panda huku nisielewe anayempigia ni nani, nilitamani nikampore huku nikijipa asilimia 100 atakuwa ni Sammy tu,

“..huyu ni Sammy tu atakuwa anataka kuharibu kila kitu, we unafikiri nitaishi wapi tena..?”

Nilijisemea kimoyo moyo huku nikiyatega masikio yangu vizuri,

“…hee niambie shost za tangu jana..?”

Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi huku hasira zikianza kunipanda..

“..yupo.. Nipo naye hapa sebuleni, nikupe uongee naye..?”

Nikavuta pumzi juu juu huku macho nimemkazia Irene akinyanyuka pale kwenye sofa.

Lakini ikawa kama kinyume kwani nilishuhudia simu akimpa Jacky wangu,

“..mambo, zatoka jana..? Lini utakuja kututembelea..?”

Nikawa kama mtu aliyeshikwa na butwaa huku nisielewe chochote kinachoendelea,

“..sasa, kama hawaongei na Sammy, watakuwa wanaongea na nani..?”

Nikati ya swali lililokuwa linanisumbua akili. Nilisubiri mpaka Jacky akamaliza kuongea na simu kisha..

“..Jacky pliz nakuomba mara moja..”

Nilimwita nakuongozana naye mpaka chumbani tulipofika,

“..Jacky pliz embu niambie ukweli..”

“..ukweli..? Kuhusu nini tena Jeff..?”

“..Ulikuwa unaongea na nani kwenye simu pale sebuleni..?”

“..Jeff nawe kwa wivu..? Yule ni rafiki yake Irene..”

“..nani..? Sammy..?”

“..wala hata siyo Sammy, anaitwa Happy..”

“..Happy..? We umemjuaje sasa..?”

“..Jeff na we kwa udadisi..? Mara hii umeshasahau hata kama jana nilienda sokoni na Irene..! Na ndipo tulipokutana na huyo rafiki yake Happy na nikamjua hapohapo..”

“..ahaaa, kumbee..”

“..unachoshangaa nini sasa..?”

“..mh.. mh.. hamna kitu..”

Moyo wangu sasa ukawa umeshatulia,

“..Jacky..? Nakupenda mpenzi wangu..”

Nikambusu shavuni kisha tukarudi sebuleni, na tulipofika hatukumkuta Irene nadhani alikuwa kaelekea chumbani kwake.

Kama kawaida yangu niliweka nyimbo laini, lakini haikupita muda simu yangu ikaingia meseji kucheki inapotoka alikuwa ni Irene nikaifungua nakuisoma,

“..UNANITAMANISHA NA HIZO NYIMBO..? NA LEO USIKU SI UTANIPA TENA JAMANI…”

Sikuwa na pesa kwenye simu hivyo sikumjibu..

Ndani ya dakika chache nikatumiwa tena meseji kuangalia alikuwa huyo huyo Irene,

“…MBONA HUNIJIBU JEFF MPENZI..? HAMU HAIJAISHA MWENZAKO..”

Ikanibidi nikope tiGo kisha nikamrudishia majibu…

“…Leo zamu ya mchumba wangu Jacky..”

Kisha nikamtumia..


* Jeff kaingia majaribuni kwa Irene, Je unavyodhani Jacky atavumilia akijua ukweli..??

**** Hii ndio Play Boy na Simulizi hii inaelekea kuisha.. Je unavyodhani mwisho wa Play Boy utakuwaje..?? Shusha utabiri wako hapa..

ITAENDELEA

Play Boy Sehemu ya Tano

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment