Sharobaro wa Tandale Sehemu ya Tatu
CHOMBEZO

Ep 03: Sharobaro wa Tandale

SIMULIZI Sharobaro wa Tandale
Sharobaro wa Tandale Sehemu ya Tatu

IMEANDIKWA NA: ZULFA HUSSEIN

*********************************************************************************

Chombezo: Sharobaro Wa Tandale

Sehemu ya Tatu (3)

“Jamaaa yangu kwa sasa hayupo nchini kaenda kusoma Marekani, sina mtu ndiyo maana nakuomba kama hutajali uchukue nafasi yake,” Atu alimwambia Dullah .

Dullah alifurahi sana kupata habari hiyo njema alimkubalia Atu na kumwambia aonde shaka watakuwa pamoja lakini moyoni alijiuliza itakuwaje dada huyo aliyeelewa Dullah alikuwa mambo safi atakapobaini kumbe alikuwa kibarua aliyekuwa akimsaidia fundi ujenzi kubeba zege.

“Hili si litakuwa soo hili?” Dullah alijisemea moyoni.

Hata hivyo, alipanga kutumia ujanja wa hali ya juu ili Atu asigundue kama hakuwa na kazi na baada ya maongezi ya kusifiana walivyopeana raha yalipoisha walikwernda kuoga.

Baada ya kumalizika kwa zoezi hilo, walitoka mle gesti wakiwa wepesi ambapo Atu alitangulia nje na kumuacha Dullah akimalizana na mhudumu wa ile gesti.

Wawili hao waliondoka pale gesti kila mmoja akiwa amefurahia walichokuwa wamekifanya bila kujali kama walikuwa na maradhi kwa sababu hawakutumia kinga jambo ambalo lilikuwa hatari.

Kwa kuwa Dullah alikuwa akielekea Tandale, walipofika kituo cha daladala, kijana huyo kabla ya kuagana na Atu aliyekuwa akielekea karibu alitaka kumpatia shilingi elfu tano lakini msichana huyo alikataa.

Hata hivyo, kabla ya Dullah kupanda gari walipanga kukutana tena siku ya Ijumaa jioni kisha kijana huyo alipanda kwenye daladala la Tandale akiwa mwenye furaha kufuatia kujiburudisha na Atu baada ya kumkosakosa Doreen.

Alipofika Tandale breki ya kwanza ilikuwa nyumbani kwa fundi Yassin kwa nia ya kumpa mchapo wa kilichojiri akiwa na Atu na kumshukuru kwa sapoti ya hela alizomtumia.

Bahati nzuri alipofika kwa fundi huyo alimkuta akiwa amesimama kibarazani, Dullah aliyekuwa na furaha alimshukuru fundi wake kwa kampani nzuri aliyompa na kumweleza kila kitu kilichojiri na Atu.

“Mi nilijua tu yule mtoto asingechomoa maana wewe ni mtaalam wa vimwana wakali,” fundi Yassin alimwambia Dullah wakaishia kucheka.

“Kaka siyo siri, mtoto nimemkubali na yeye kanikubali vilevile yaani kanifagilia kinona kwamba hakuwahi kukutana na mtu kama mimi, hata hivyo kwa mambo niliyomfanyia ana haki ya kutoa ufagio,” Dullah alimwambia fundi Yassin, wakacheka.

Fundi Yassin alipogundua mkewe angesikia maongezi yao ya kipuuzi alimwambia Dullah kwamba siku iliyofuata wataongea kwa kirefu ili ampe mchapo wote ndipo kijana huyo ambaye alikuwa kalewa kwa mbali alimuaga lakini akakumbuka harufu ya pombe ingemuumbua kwa wazazi wake.

Baada ya kubaini hivyo, alikwenda kwenye genge la kijana mmoja wa Kimakonde aliyezoeleka kuitwa Chinga aliyekuwa akichelewa kufunga biashara yake akamwambia ammenyee tango.

Kwa kuwa Chinga huyo alikuwa akifahamu kwamba tango linakata kilevi pamoja na harufu akamtania kwamba alikuwa akiogopa so kwa washua wake nini, Dullah akacheka na kumwuliza alijuaje!

“Jamani niuze matango nisijue pia kama yanakata kilevi?” Chinga alimwambia Dullah , wakacheka.

“Tena kula na ndizi hii mbivu hakuna atakayekushtukia kabisa,” Chinga alimwambia Dullah na kumpa ofa ya ndizi moja mbivu.

“Na ndizi zinakata kilevi?” Dullah alimwuliza.

“Tena fasta,” Chinga alijibu kisha kumkabidhi Dullah tango alilokuwa amelimenya na kumwambia akipenda anaweza kula huku akitoweza kwenye chumvi.

Wawili hao waliendelea kupiga stori za hapa na pale na Dullah alipomaliza kula tango alimlipa Chinga shilingi mia mbili kisha akamuaga na kwenda kwao, ambapo aliwakuta wazazi wake wakiangalia runinga.

Baada ya salamu, baba yake alimuuliza habari za kazi aliyokwenda kuifanya akawaambia ilikuwa nzuri na kuwaelezea jinsi watu walivyokuwa wakijenga majumba ya kifahari pande za Madale.

“Kwa hiyo mwanangu na wewe leo umefanya kazi anazofanya baba Hadija?” mama yake Dullah alimwuliza kijana wake.

“Tena hapa nilipo hadi mgongo unaniuma kwa ajili ya kuchota mchanga, yaani tulipofika walinipangia kazi ya kuhamisha mchanga kwa kuuzoa na chepe,” Dullah aliwaambia wazazi wake ambao walicheka kwani hawakutegemea kama kijana wao sharobaro angeweza kufanya kazi hiyo.

“Lakini umeifurahia hiyo kazi?” baba yake Dullah mzee Reli ya Uhuru alimwuliza kijana wake.

“Sana tu, kwani nimeweza kufika eneo ambalo sikuwahi kufika, nimefahamina na vijana wawili mmoja anaitwa Zakayo na mwenzake anaitwa Haruni wanaomsaidia baba Hadija kazi, hata kesho nitaenda,” Dullah aliwaambia wazazi wake.

Baada ya kuzungumza na wazazi wake ambao hawakugundua kama kijana wao alikuwa ametoka kufanya mambo yasiyofaa na Atu na alikuwa amekunywa pombe, Dullah alikwenda chumbani kwake.

“Mama Dullah umemsikia mwanao mpenda usmati alivyosema kafanya kazi ya kuhamisha mchanga kwa chepe, kweli hiyo ni habari njema na huko ndiko kujifunza maisha,” baba Dullah alimwambia mkewe.

“Nami kaniacha hoi, nahisi leo alipewa kazi nyepesi, tusubiri siku atakayotuambia kabeba zege akituambia ataendelea hapo nitaamini kweli kaamua kujishughulisha,” mama Dullah alimwambia mumewe.

Kule chumbani Dullah aliendelea kumuwaza Atu hasa alivyokuwa akiyazungusha macho yake mazuri na alivyokuwa akihema, akajikuta akisema peke yake kwamba watakapokutana Ijumaa waliyokubaliana atampa mambo matamu zaidi.

Hata hivyo, kutokana na ulevi aliokuwanao kichwani hakuchukua muda mrefu alipitiwa na usingizi hata mama yake alipokwenda kumuamsha ili akale hakumsikia.

“Baba Dullah , kweli mwanao leo kachoka, nimemwita mpaka nikapata wasiwasi, nilipoingia kumwangalia yaani kalala fofofo,” mama huyo alimwambia mumewe.

“Ndivyo inavyotokea kwa mtu ambaye hajazoea kufanya kazi ngumu, muache akiamka atakula,” mzee Reli ya Uhuru alimwambia mkewe bila kujua Dullah licha ya kuchoshwa na kazi lakini zaidi ni kwa vile alitoka kumdungua kiumbe na pombe aliyokunywa.

Mpaka wazazi wake wanakwenda kulala, Dullah hakuamka hadi kulipokucha akawa wa kwanza kuamka kujiandaa kwenda site na fundi Yassin, akiwa anaoga mama yake naye aliamka.

Alipomaliza kuoga na kutoka bafuni alimkuta mama yake akiwa anaweka mkaa jikoni kwa ajili ya kumwandalia chai baba yake, wakasalimiana ndipo mama mtu akamwuliza jana yake alikuwa kachoka sana?

“Yaani mama nilichoka sana, lakini ndiyo kazi na maisha hayana njia ya mkato,” Dullah alimwambia mama yake.

“Nilijua tu ulichoka maana nilikuandalia chakula nikaja kukuamsha lakini hukunisikia kabisa, vipi nikupashie moto utakula alfajiri kwa chai?”

Baada ya mama mtu kumwambia hivyo mwanaye, Dullah aliwambia asiwe na wasiwasi atakunywa site mama hakuwa na la zaidi akamwambia sawa ndipo kijana huyo akaingia chumbani kwake kujiandaa kisha amfuate fundi Yassin.

Baada ya kujiandaa wakati anataka kutoka alikutana na baba yake wakasalimiana kisha alimuaga ndipo mzazi wake akamtakia kazi njema, Dullah akatoka na kuelekea kwa fundi Yassin.

Alipofika alimkuta fundi huyo akimsubiri na baada ya salamu wakaondoka bila kuwa na mzigo wowote kuelekea kupanda daladala la Mwenge, kwa bahati walikuta ma DCM matatu yakiwa yanasubiri abiria, wakapanda na kukaa siti ya pamoja.

Gari lilipojaa wakaanza safari ndipo fundi Yassin aliyekuwa na shauku ya kujua kilichojiri kati ya Atu na Dullah akaomba ampe mchapo huo, Dullah akaanza kumsimulia kwa sauti ya chini ili abiria wengine wasisikie.

“Wewe dogo sikuwezi, unatisha kuliko hata moto wa gesi,” fundi Yassin alimwambia Dullah baada ya kijana huyo kumpa mchapo wote na wakati huo walikuwa wamefika Magomeni.

“Kiasi tu bro, unajua wakati mwingine tunajenga heshima tu kwani huwezi kumuona mtoto mzuri kama yule halafu umuache tu, hivi unajua unaweza kulaumiwa hata huko mbinguni?” Dullah alimwambia fundi Yassin, wakacheka.

Hata hivyo, Fundi Yassin alimwambia Dullah aache utani wa kuhusisha mambo maovu na mbinguni, Dullah akagundua kosa lake na kutengua kauli yake, ambapo fundi Yassin akasema hapo sawa kabisa.

Kwa kuwa wakati walipokuwa wakipeana michapo walikuwa bize na jambo hilo, Dullah akuwaona mabinti wawili wakali waliokuwa wamepandia Kigogo ambao walikosa siti hivyo kusimama pembeni yake.

Kufuatia kuwaona mademu hao, moyo ukapiga pa akambonyeza pajani fundi Yassin, fundi alipogeuka akamnong’oneza kama aliwaona watoto wale wakali.

“Wewe ndiyo unawaona muda huu, mbona wamepandia Sinza Vartican” fundi Yassin alimwambia Dullah .

“Sikuwaona mkuu, da watoto wakali sana hawa hasa huyu aliyevaa suruali ya jinzi, ana kifua kama ninavyovipenda,” Dullah alimwambia fundi Yassin kwa kumnong’oneza.

Wakati akifanya hivyo, yule dada mwenye suruali ya jinzi alimuona na kubaini Dullah alikuwa kadatishwa na uzuri wake kwa makusudi mazima akajigeuza ili kumuonesha Dullah kiwowowo chake tata.

Baada ya msichana huyo aliyesimama pembeni ya kiti cha Dullah kujigeuza, Dullah akajikuta damu zikimwenda mbio kwani kihisia alimvua viwalo dada huyo na kupata picha kama vile walikuwa chimbo, akapagawa kabisa.

Hata hivyo, Dullah alizidi kuumia kwani alishindwa hata kumsemesha mrembo huyo hadi walipoteremka kituoni, jambo lililomuweka Dullah katika wakati mgumu kwani alipanga kama wangefika mwisho wa safari pamoja lazima angeomba namba yake ya simu.

“Kaka leo imekula kwako, watoto wameshuka hata salamu hujawapa,” fundi Yassin alimtania Dullah .

“We acha tu mkubwa wangu, ila tungefika mwisho ungeona ambavyo ningepewa namba yake kirahisi si unanijua lakini mi mdogo wako?” Dullah alimwambia fundi Yassin wakacheka.

Wawili hao waliendelea na stori hadi walipofika Mwenge wakapanda gari la Tegeta, wakiwa kwenye gari hilo Dullah akiwa anamuwaza Doreen ghafla fundi Yassin akamkatisha kwa kumuuliza alijisikiaje kufanya kazi za kifundi.

“Bro bwana! Kazi ni kazi tu na mtoto wa kiume hapaswi kuchagua kazi!” Dullah alimjibu fundi Yassin.

“Kama ni hivyo, poa sana tena kadiri tutakavyokuwa pamoja nitakufundisha kazi kibao,” fundi Yassin alimwambia Dullah .

Kwa kuwa gari lilikuwa likienda kwa kasi, kufumba na kufumba walifika Tegeta ambapo walipanda basi la kuelekea Kisauke na hawakuchukua muda mrefu wakawasili site.

Kama kawaida, fundi alipofika getini alibonyeza kitufe cha kingele na baada ya dakika kama moja geti likafunguliwa, ingawa ilikuwa kawaida kufunguliwa na Anne siku hiyo likafunguliwa na Doreen.

Sharobaro Dullah na Doreen walipokutanisha macho kila mmoja akaachia tabasamu lakini fundi Yassin kwa umahiri mkubwa alijifanya anaangalia nyuma ili wasibaini kama aliona jinsi walivyotabasamu.

“Shikamoo fundi?” Doreen alimwamkia fundi Yassin.

“Maraba, hujambo Doreen?” fundi Yassin alimsalimia Doreen.

“Nzuri fundi!” Doreen aliitikia.

“Mambo yako?” Doreen alimsalimia Dullah na kuachia tabasamu pana lililoonwa na fundi Yassin lakini alijifanya hakuliona.

“Nzuri, za hapa?” Dullah alitikia salamu ya mtoto huyo wa kigogo.

“Poa!” Doreen aliitikia ndipo fundi Yassin akamwuliza kama akina Zakayo na Haruni walikwishafika.

“Wamefika lakini siyo zamani sana wako kule ndani nahisi watakuwa wameanza kazi,” Doreen aliyekuwa kafurahi sana kumuona sharobaro Dullah aliwaambia.

Baada ya salamu msichana huyo ambaye mpaka muda huo alikuwa hajafunga geti alilifunga kasha akaanza kutembea kuelekea nyumba kubwa lakini kabla hajaingia aliangalia nyuma na kugongana macho nay a Dullah wote wakatabasamu.

“Yaani huyu kijana kanivutia sana nitafanya kila liwezekanalo lazima nifurahi naye tena leo sijui kama itapita na nilivyo na hamu we acha tu!” Doreen aliwaza akiwa amejibwaga sofani.

Wakati Doreen anawaza hivyo, kama vile waliaambiana na Dullah naye alikuwa amepanga kufanya ukomandoo wake kuhakikisha anamchinja mtoto huyo palepale kwake ili kujenga heshima.

“Kumuacha mtoto kama huyo aliyeonesha dalili zote na za kunikubali ni kosa kubwa kuliko hata walilofanya mafisadi waliokwepa kulipa kodi bandarini, huyu namhesabia kama siyo dakika saa lazima niwe nimempa mambo,” Dullah aliwaza.

Dullah aliyekuwa akiwaza mambo ya kuduu tu alishtuka baada ya kumsikia fundi Yassin akisalimiana na Haruni na Zakayo, kasha Zakayo ambaye alikuwa mkubwa kuliko akina Dullah alimsalimia Dullah kwa kusema;

“Vipi dogo za tangu jana?”

“Poa bro vipi hali yako?”

“Mi nipo fiti, nilidhani leo hautakuja kwa jinsi alivyochoka maana naona hizi kazi hujazizoea?” Zakayo alimtania Dullah .

Dullah alimwambia atazioea kadiri siku zinavyokwenda, kwa kuwa walikuwa bado hawajasalimiana na Haruni walipeana hi kasha fundi Yassin alimwambia Dullah akaendelee na kazi aliyokuwa akiifanya jana yake.

Dullah aliyefikiria siku hiyo angepangiwa kazi nyingine alipoiambiwa hivyo alifurahi sana kwani alijua ingekuwa rahisi kupiga stori na Doreen na hata kuingia ndani kwao.

Baada ya kupangiana majukumu, Dullah alibadili nguo na kwenda kuendelea na kazi huku fundi Yassin na akina Zakayo wakiendelea na kazi ya kuweka marumaru ndani.

Kwa kuwa akili yake ilikuwa kwa mtoto mkali Doreen, kabla hata ya kuanza kazi aligeuza shingo na kuangalia dirishani si akamuona Doreen akiwa anamtazama kwa jicho linalosema ‘jamani wewe kaka na uzuri wote huo unafanya kazi ya ujenzi!’

Kitendo cha wawili hao kutazamana, walitabasamu kwa pamoja ndipo Doreen alimuuliza Dullah kama alifungua kinywa, kwa kuwa hakunywa hata maji alimwambia bado.

Msichana huyo alipojibiwa hivyo alimwambia Dullah aingie ndani kwa kupitia mlango wa uani ili amwandalie chai, Dullah bila woga akafuata maelezo na kwenda moja kwa moja kukaa kwenye sebule ya kishua.

“Vipi Yule dada mwingine sujui Anne hayupo?” Dullah alimwuliza Doreen.

“Unajua Yule licha ya kwamba ni dada wa kazi baba anamsomesha chuo cha kompyuta kishaenda chuoni kwao mapema sana, hapa nimebaki peke yangu,” Doreen alimwambia Dullah .

“Da! Kumbe baba yako ana roho nzuri sana, anamsomesha hata hausigeli?” Dullah aliyekuwa kafurahi kusikia Anne hayupo alimwambia Doreen.

“Yeah! Hapendi akitoka hapa kwetu akaendelee kufanya kazi za ndani ndiyo maana kaamua kumsomesha,” Doreen alimwambia.

Baada ya mazungumzo hayo, Doreen akiwa anachekacheka alikwenda kuchukua chupa iliyojaa maziwa, mkate wa bofro, jam na kumuandalia chai Dullah , Dullah alifungua kinywa kama vile alikuwa mtoto wa tajiri.

Alipomaliza kunywa, Dullah alimtazama na kumrembulia macho na kumwambia jana yake alimuweka katika wakati mgumu sana, Dullah akamwuliza kivipi!

“Muone kwanza vimacho, eti unaniuliza kivipi si vile ulivyonifanyia yaani usiku sijalala mwenzako da!” Doreen alimwambia Dullah kwa sauti f’lani ya kuhamasisha malovee.

Dullah aliposikia mtoto wa kike wa ushuani akilalamika, akajisemea moyoni kwamba pale alikwenda kazini lakini kufanya kazi na dawa halikuwa kosa, akamuuliza Doreen alitakaje?

“Jamani eti ninatakaje, wewe sijui ukoje?” Doreen alimwambia Dullah na kumpiga kibao cha uchokozi shavuni Dullah akaachia tabasamu lakini tayari mwili wake ulishapata moto.

Dullah alipokitazama kipensi cha kubana hipsi alichokivaa Doreen na kitopo kilichoonesha michomoko ya viembe sindano vya mtoto huyo akaona ni halali kabisa inzi kufia juu ya kidonda yaani alikuwa tayari fundi Yassin amtimue site lakini siyo kuidhulumu nafsi yake.

Kijana huyo aliyekuwa na hamu ya kumchinjia baharini Doreen alikivamia kifua chake na kuanza kumfanyia vurugu zilizokwenda sambamba na denda ambalo a.k.a yake kula mua mpaka mtoto wa watu macho yakamuiva mithili ya tunda damu.

Wakati mtoto huyo wa kishua akijibu mashambulizi ya kumshika Dullah maeneo mbalimbali ya mwili wake hususan makazi ya rais mpenda raha, Dullah akadata kabisa.

Alichokifanya kijana huyo ni kumuuliza Doreen eneo ambalo lingekuwa salama kwao kuzitafuna tende kama siyo harua, Doreen akamshika maungoni na kumkokota kwenda naye chumbani kwake.

Kwa kuhofia fundi Yassin au Zakayo angetoka na kukuta hayupo, wawili hao walipofika ndani Dullah hakuona sababu ya kuremba kwa sababu Doreen hakuwa dada yake, akampunyua kila kitu kisha akajipunyua haikupita hata dakika moja uwanja waliokuwa wapo juu yake ulichimbika balaa.

Sharobaro Dullah , hakuwa na huruma na mtoto wa watu, alimvuruga kweli Doreen ambaye alikuwa amemisi kuvurugwa kwa muda mrefu na kwa utaalaam wa kuchimbua visiki wa kijana huyo wote walijikuta wanagota mwisho wa safari pamoja.

Baada ya kumaliza kazi nzito iliyokuwa mbele yake, Dullah hakutaka kuendelea kukaa mle chumbani, aliingia bafuni akajimwagia maji na kutoka haraka lakini ile anatokeza sehemu aliyotakiwa kuhamisha mchanga akamuona Zakayo akiwa amesimama.

Dullah ambaye wakati huo hakujali chochote kufuatia kumkwangua mtoto mzuri Doreen ambaye aliumbika hasa na kumhamasisha mwanaume yeyote rijali, akawa anacheka.

Zakayo ambaye alifahamu kwamba Dullah hakuwa mfanyakazi zaidi ya usharobaro alimkata jicho na kuingia ndani ambako fundi Yassin alikuwa akiendelea na kazi.

“Kaka mkubwa, kama ambavyo nilikuwa nakuambia huko nje hakuna kazi inayofanyika sikukosea hata kidogo, nilipokwenda kumuangalia huyo dogo uliyetuletea nimemkuta akitokea jikoni kwa bosi,” Zakayo alimwambia fundi Yassin.

“Acha masihara bwana! Yaani bado hajaanza hata kazi?” fundi Yassin alimwuliza Zakayo.

“Ndo maana yake, yaani chepe kalichomeka juu ya mchanga nahisi tayari kisha kuwa mwenyeji kutupita wenyeji, kweli hawa vijana masharobaro wana mambo,” Zakayo alimwambia fundi wake.

Kufuatia kauli ya Zakayo, fundi Yassin anayemuelewa vizuri Dullah akaishia kucheka ndipo Haruni akamwuliza Zakayo kwa nini alisema Dullah kishakuwa mwenyeji kuliko wao.

“Hivi sisi tangu tulipoanza kazi hapa miezi miwili sasa na ushee tumewahi kuingia hata jikoni kwa bosi?” Haruni alimwuliza Zakayo.

Zakayo alimwambia hawakuwahi kisha alimfahamisha

kwa jinsi alivyomuona Dullah alikuwa ametoka ndani kabisa kwa bosi wao na ilivyoonesha hata chai alikuwa kanywa.

Alipowaeleza hivyo, fundi Yassin na Haruni waliishia kucheka kisha fundi akasema ndiyo mambo ya mjini yalivyo, ukiwa shapu mambo yatakunyokea na ukizubaa itakula kwako.

“Unamaanisha nini kaka mkubwa?” Zakayo akamwuliza fundi Yassin.

“Si nyie tangu mfike hapa mmejaa uoga sasa dogo kaja kishamzoea mtoto wa bosi na chai tena nzito kaanza kunywa,” fundi Yassin aliwaambia akina Zakayo walioshia kucheka.

Baada ya maongezi mafupi kuhusiana na Dullah , wakasikia mchanga ukilia tii wakajua dogo kisha anza kazi, kweli fundi Yassin alipokwenda kuangalia akamkuta Dullah akichota mchanga na kuusogeza sehemu aliyomwelekeza.

Kwa kuwa alitokea kwa nyuma, Dullah hakuweza kumuona akamwita, Dullah alipogeuka akacheka sana na kumwambia fundi wake kwamba pale ilikuwa kazi tu, fundi akaangua kicheko pia.

“Poa kaka, hapo kazi tu! Wewe endelea na kazi na sisi tunaendelea na kazi huku ndani,” fundi Yassin hakutaka kumweleza chochote alichoambiwa na Zakayo.

Fundi Yassin na vijana wake wakiwa wanaendelea na kazi, Zakayo aliyekuwa kama ameamka ghafla akamwambia Yassin kwamba siku si nyingi Dullah angewaletea balaa pale site.

“Kwa nini unasema hivyo?” fundi Yassin alihoji.

“Kaka mkubwa huyu dogo hajatulia, siku bosi akirudi na kubaini anaingia ndani kwake na kunywa chai si atajua ana uhusiano na binti yake, wewe unafikiri tutapona kweli kama siyo kufukuzwa hapa?” Zakayo akamwambia.

Maneno ya kijana huyo yalimwingia vilivyo fundi Yassin aliyetegemea kupewa kazi kibao na bosi wake aliyekuwa kasafiri, lakini hakutaka kujibu chochote.

“Kwanza huyo dogo siyo mfanyakazi kabisa, tangu alipokuja hapa jana hakuna kazi aliyofanya, sasa ni hivi mkubwa, kama ataendelea kuja hapa site mimi naona ni bora niache kazi tu, yaani naiona hatari mbele yetu,” Zakayo alipiga mkwara.

“Poa Zakayo nimekuelewa sana, naomba kazi hiyo niachie mimi niliyemleta,” fundi Yassin alimwambia Zakayo.

“Lakini kaka mkubwa, nami naungana na mawazo ya Zakayo, mwenendo wa huyu dogo utatuponza, yeye kaja jana tu nyumba yote ya bosi kishaizoea na chai nzito ya kishua anakunywa!” Haruni naye akachombeza.

Kule chumbani, Doreen alikuwa kajilaza chali kitandani kwake kufuatia vionjo vya uhakika vya asubuhi alivyopewa na Dullah akapanga siku hiyo kumpa zawadi kama asante yake.

“Huyu kaka siyo siri anajua mapenzi, kama kwa muda mfupi tu niliokuwanaye kanipa raha namna hii, je tungekaa zaidi ya saa nne si ingekuwa balaa, huyu lazima nimpe zawadi,” Doreen aliyekuwa kavaa nguo ya mwisho pekee alijisemea moyoni.

Msichana huyo ambaye kwenye droo yake alikuwa na shilingi 230,000 alijiuliza ampatie laki moja au kwa kuwa Dullah hakuwa na simu ampatie simu yake ambayo alikuwa haitumii.

“Pesa hapana, kwa ninavyomuona anaweza asinunue simu ya maana ili zingine afanyie kazi nyingine, nampa simu,” Doreen aliwaza kisha aliinuka pale kitandani.

Kwa kuwa mbele yake palikuwa na kabati kubwa la kujipambia lililokuwa na kioo, wakati anajongea kwenye kabati hilo akacheka sana baada ya kuangalia kufuli alilokuwa amevaa na jinsi macho yalivyokuwa yamemlegea baada ya kulishwa tende na Dullah .

“Da! Huyu kaka kajua kunilegeza mtoto wa kike, zawadi inayomfaa ni simu tu ya kisasa,” Doreen akajisemea moyoni na kufungua droo ya kabati na kuchukua boksi la simu na kuliweka juu ya kitanda.

“Hii ndiyo zawadi pekee inayomfaa, kijana mzuri namna hii ataishije bila kuwa na simu, tena itarahisisha sana kuwasiliana naye kwani nitakapotaka kukutana naye hata huko nje ya hapa ni suala la kumpigia na kumwambia sehemu ya kumiti,” Doreen alijisemea moyoni.

Baada ya kuwaza hivyo, alijifunga kanga na kwenda kwenye chumba ambacho dirisha lake lilikuwa sehemu ambayo Dullah alikuwa akihamisha mchanga, lengo lake ni kutaka kumtazama tu kijana huyo aliyempenda ghafla.

“Kweli hii dunia saa ingine haina usawa, huyu kijana alifaa awe anafanya kazi kwenye ofisi kubwa akicheza na kompyuta muda wote kama siyo laptop a.k.a kompyuta mpakato, sasa anafanya kazi ya kusomba mchanga, sikubali,” Doreen aliwaza kwa huzuni.

Wakati msichana huyo akiwaza hivyo, Dullah aliendelea kuchota mchanga na kila aliporusha chepe kadhaa alipozi na kujishika kiuno na kujinyoosha kuashiria kwamba ile kazi hakuizoea.

Doreen aliyekuwa akimtazama alimuonea huruma akajikohoza ndipo sharobaro Dullah akageuka kumtazama, walipogangana macho Dullah aliachia tabasamu.

“Pole mpenzi wangu kwa hiyo kazi ngumu!” Doreen alimwambia Dullah .

Kitendo cha Dullah kuitwa mpenzi, kilimfurahisha sana na kichwa kumvimba kama puto, akamwambia asante ndipo mtoto huyo wa kishua akamwambia kabla ya kuondoka alihitaji kuzungumza naye jambo f’lani.

“Mbona unanipa kimuemue jamani, si niambie hilo jambo sasa hivi my d?” Dullah alimwambia Doreen.

Doreen alipoambiwa hivyo na kuitwa my d na Dullah , alijisikia raha na kutamani kama ingewezekana warejee tena kugaragara kwenye uwanja wa fundi seremala na kijana huyo aliyeyajua mapenzi utafikiri aliletwa duniani kwa kazi hiyo.

“Kama hakutakuwa na soo kwa fundi toroka uje huku ndani mara moja itakuwa poa sana,” Doreen alimwambia Dullah .

Kitendo cha kijana huyo kuambiwa hivyo, Dullah ambaye mwili ulikuwa ukitiririka jasho hakuremba akaamua kuzama ndani kwa akina Doreen kwa kupitia mlango uleule wa jikoni.

Ile kuingia tu jikoni wakakutana na Doreen aliyekuwa kavaa kanga nyepesi iliyoonesha kufuli jeupe aina ya bikini alilovaa, Dullah akasisimkwa sana kama siyo aliyezila tende tamu za binti huyo muda mfupi uliopita.

Wakati Dullah akiwa katika hali hiyo, Doreen naye kitendo cha kumuona kijana huyo aliyemwingia moyoni kwa muda mfupi akajikuta akilihitaji tena penzi lake tamu si akamkumbatia bila kujali jasho lililomtiririka!

Kufuatia Dullah kukumbatiwa, naye akaizungusha mikono yake maungoni mwa binti wa kishua Doreen kisha wakaanza kula mua ambalo wengine huliita denda kwa dakika moja na vipointi hivi.

Walipoachiana kila mmoja macho yake yalikuwa mekundu na malegevu kuashiria kwamba kilichotakiwa kufanywa na vijana hao ambao damu zao bado zilikuwa zinakimbia ni kugaragazana tu hili kuzitendea haki nafsi zao.

Alichokifanya Doreen ambaye muda huo embe zake bolibo zilikuwa zimepata moto hadi kumsimama ni kumkokota Dullah hadi chumbani kwake, huko alimpunyua viwaro vyake kisha kuifungua kanga aliyovaa na kumalizia kiwalo cha mwisho wakawa kama walivyokuja katika ulimwengu huu wenye raha na karaha.

Mtoto wa kike alipokiona chombo cha Dullah jinsi kilivyokuwa kimechangamka akatabasamu, kwa kuwa walikuwa wamejibwaga kwenye uwanja wa fundi seremala na alivyokuwa kapagawa, akaamua kujisevia chakula hicho kisicho na muda maalum wa kukila.

Dullah aliyekuwa kawa kichaa kwa alivyopagawishwa na Doreen, hakukumbuka kabisa kwamba alikuwa eneo lile kikazi badala yake kazi ikawa ni kumpa mambo mazito mtoto wa kishua aliyeishia kulia kwa midadi maana Dullah alijua kumbana kiume.

Kitendo cha Doreen kutoa kilio hicho cha ushirikiano, kilimfanya sharobaro Dullah kuwa kichaa zaidi na vile alipenda sana kusifiwa alimvuruga kisawasawa mtoto wa watu ambaye alijikuta akipasua madafu mfululizo na kunywa maji yake.

Sharobaro Dullah alipobaini mtoto wa kishua alipasua karibu madafu matatu ndipo naye akapasua lake moja lenye ujazo mziri kwa ufundi wa hali ya juu na kumnywesha maji matamu Doreen.

Baada ya shaborobaro Dullah kumnywesha maji matamu, Doreen alianza kujilamba huku akiwa kayalegeza macho yake mazuri kisha alivuta pumzi na kuzishusha kuashiria alikuwa amekatwa kiu yake.

“Mh! Umejua kuniweza kwa kweli, wewe ni balaa!” Doreen alimwambia Dullah aliyeishia kutabasamu.

“Jamani kukuwezaje, hujapenda?” Dullah alimwuliza.

Kufuatia kuulizwa hivyo, Doreen alimwambia siku hiyo alikuwa kamfurahisha sana kwani hakutegemea kama alivyokuwa akimuona angeweza kumfanyia mambo mazuri kama yale.

Dullah akiwa kavimba kichwa huku akitabasamu baada ya kuona mtoto wa kishua kamkubali, naye alimsifisia kwamba alikuwa yupo vizuri kila idara.

“Nipo vizuri kama vipi, niambie kila kilichokufurahisha,” Doreen alimwambia Dullah .

“Shepu yako nzuri unashikika, embe zako nzuri sana na tamu, macho yako nashindwa hata namna ya kuyaelezea, midomo yako ndiyo sisemi, vibastola vyako mwisho wa matatizo,” Dullah alimsifia Doreen aliyefurahi sana.

“Kweli my love?” Doreen alimwuliza.

“Tena hivyo ni vichache, nikwambie vingine?” Dullah alimwuliza.

“Niambie mpenzi wangu,” Doreen alimruhusu.

Kufuatia kuambiwa hivyo, Dullah akawa anacheka na kusahau kabisa kama pale alikwenda kwa ajili ya kufanya kazi.

“Usijali mpenzi wangu, vilivyobaki nitakuambia kesho ila wewe elewa kwamba umeumbwa na kuumbika, mi naona nitakuoa kabisa,” Dullah alimwambia Doreen aliyecheka sana.

Kama unavyojua masuala ya mapenzi, wawili hao wakiwa wamelaliana, Doreen akamwambia Dullah kwamba kama hatajali afumbe macho yake kwa sekunde kadhaa.

“Kufumba tu macho d, hilo usiliwaze kabisa,” Dullah akamwambia Doreen na kufumba macho huku akiwa kalala chali.

Dullah akiwa katika hali hiyo, mtoto wa kishua Doreen alifunua taulo alilokuwa amefunikia boksi la simu na kuliweka juu ya kifua cha Dullah kisha akamwambia afumbue macho.

Dullah alipofanya hivyo akakutana na boksi lililokuwa na simu ndipo Doreen akamwambia ilikuwa zawadi yake kwani alifurahi penzi shatashata alililompa, Dullah akabaki ameduwaa.

Alipofungua boksi hilo alikutana na simu kali ya kisasa akashindwa kuvumilia, akamkumbatia Doreen na kuanza kumvurumushia mabusu motomoto huku akimshukuru.

“Usijali mpenzi wangu, tena hii ni sapraizi ya mwanzo kuna mambo mengine nitakufanyia ila utanichukia na kuniona mbaya siku nitakayogundua una msichana mwingine,” Doreen alipiga mkwara.

“Ondoa shaka mpenzi wangu, kwa sasa sina msichana niliyekuwa naye niliamuacha kitambo sababu hakuwa mwaminifu,” Dullah mpenda mademu wakali alimdanganya Doreen.

Wawili hao wakiwa mle chumba, fundi Yassin alitoka lakini hakumuona Dullah akaanza kumwita; “Dullah , Dullah , Dullah !”

Kufuatia kuitwa, Dullah alikurupuka na kutaka kuchukua nguo zake lakini Doreen alimzuia na kumweleza asubiri maana kama angetoka na fundi Yassin kumuona akitokea ndani kwao ingeleta picha mbaya.

Baada ya kushauriwa hivyo, Dullah alitulia ndipo fundi Yassin akaendelea kumwita bila mafanikio akarudi katika chumba alichokuwa akifanya kazi na akina Zakayo.

“Hivi mnajua dogo kaacha kazi na sijui kaenda wapi?” fundi Yassin aliwaambia.

“Kaka mkubwa, mimi nimekwambia yule dogo majanga sasa umeamini maneno yangu?” Zakayo akamwambia fundi Yassin.

Wakati mafundi hao wakijadiliana kuhusu Dullah , kule ndani kijana huyo mpenda mademu alikuwa katulia tuli katika kitanda kipana cha mtoto Doreen akipulizwa na AC.

“Sasa sikia, leo pia utafanya kama siku ile nitakutoa nje kwa kupitia mlango wa uani chukua hii hela ukanunue maji au soda kisha gonga geti kubwa huku ukiwaita watakufungulia, sawa mpenzi wangu?” Doreen alimwambia.

“Yaani wewe una akili sana, sasa hii simu itakuwaje?” Dullah alimwuliza.

“Hebu ilete nikuoneshe cha kufanya,” Doreen alimwambia.

Dullah alipomkabidhi mtoto huyo wa kishua, Doreen aliitoa kwenye boksi pamoja na chaji yake, kwa kuwa suruali ya Dullah ilikuwa na mifuko akaingia simu pamoja na chaji kwenye mifuko ya nyuma.

“Ukishusha na hiyo fulana yako hakuna atakayejua una simu, sawa mpenzi wangu?” Doreen akamwambia.

Dullah alicheka baada ya kuvaa fulana yake iliyofunika kabisa mifuko ya nyuma hivyo kutokuwa rahisi mtu kuona kama alikuwa ameweka kitu, akamshukuru Doreen kwa utundu wake.

Msichana huyo wa kishua ambaye moyo wake ulikuwa kwatu kwa kupewa raha na Dullah , alifungua mlango wa uani ambao ulikuwa haufunguliwa mara kwa mara, Dullah akatoka.

Kama alivyopewa ujanja, alipotoka alikwenda kwenye duka moja la jirani akanunua soda tatu na maji chupa moja na kurejea getini, akaanza kugonga huku akimwita Zakayo amfungulie.

Kufuatia geti kugongwa na kuitwa jina lake, Zakayo aligundua aliyekuwa akimuita alikuwa Dullah , akamwambia fundi Yassin kwamba mtu aliyewapelekea ndiye aliyekuwa akigonga geti.

“Unasema kweli?” fundi Yassin alimwuliza.

“Kaka mkubwa bwana na huyo dogo wako unachekesha, ila ni kama nilivyokwambia bila ya kumuondoa mimi naacha kazi tusije wote tukaonekana tunashabikia vitendo vyake maana kwa ninavyomfahamu bosi akibaini ujinga wake atatutimua,” Zakayo alimwambia.

Fundi Yassin alipoelezwa hivyo, alipata hasira akaamua kwenda kufungua geti na kweli alipofanya hivyo akamkuta Dullah kasimama huku akitabasamu na mkononi akiwa na mfuko.

“Dullah naona umeshindwa kazi, ingia ndani uchukue vitu vyako urudi nyumbani mambo mengine tutazungumza huko,” fundi Yassin alimwambia Dullah kwa hasira.

“Kwani bro nimefanya kosa gani, wakati naendelea na kazi nilibanwa na kiu nikaamua kwenda kununua maji, hata nyinyi nimewaletea soda hizi hapa,” Dullah alimwambia huku akimuonesha zile soda.

Kitendo cha dogo huyo mpenda mademu kuongea kwa upole na kumuonesha zile soda, fundi Yassin akajikuta akicheka na kumwambia alikuwa na bahati kwani alitaka kumtimua.

“Bro bwana, sasa unitimue kwa kosa gani, kwenda kununua soda?”” Dullah alimwambia.

Kabla fundi Yassin hajajibu, Dullah alitoa soda moja ya kopo akampatia kisha afunga geti na kuongozana kwenda ndani walikokuwa akina Haruni na Zakayo.

Walipofika fundi Yassin aliwafahamisha kwamba Dullah hakutegea kazi ila alikwenda kununua soda, sharobaro huyo akatoa soda zilizobakia akawapatia akina Zakayo.

“Ila wewe dogo una mambo mengi kama unga wa ngano, hii kazi haikufai wewe ulifaa uwe mwanamuziki wa Bongo Fleva,” Haruni ambaye hakuwa akipenda kuongea alimwambia Dullah , wote wakacheka.

Wakati wakizungumza, hakuna kati yao aliyejua dogo huyo kwenye mfuko wake wa nyuma kulikuwa na simu ya kisasa aliyopewa na mpenzi wake Doreen.

“Ulichokiongea Haruni nakiunga mkono kwa asilimia mia moja, huyu alifaa awe msanii wa Bongo Fleva, huku kaja kwa bahati mbaya,” Zakayo naye alidakia.

Mafundi hao walifanya kazi hadi jioni ambapo hata hivyo Dullah hakuweza kumaliza kuhamisha mchanga, kama ilivyokuwa kawaida ya fundi Yassin kumuona Doreen kwa ajili ya malipo alimwita msichana huyo.

“Vipi fundi mnataka kuondoka,” Doreen alimwuliza fundi Yassin.

“Ndiyo, nafikiri tukija kesho tutamalizia kuweka marumaru kule vyumbani kisha tuhamie subuleni,” fundi Yassin alimwambia.

Alipoambiwa hivyo, Doreen aliyekuwa akimtupia jicho kijanja Dullah aliwapa pole ya kazi kisha alimkabidhi fundi Yassin bahasha ya khaki iliyokuwa imetuna, kwa vile alijua ulikuwa ‘mpunga’ fundi Yassin alitabasamu na kumshukuru.

Baada ya kuagana na Doreen, fundi na vijana wake waliondoka lakini kabla ya kufika kituo cha daladala alifungua ile bahasha na kukuta ilikuwa na shilingi 250,000.

Alimpatia Haruni shilingi 50,000, Zakayo 50,000 na Dullah shilingi 30,000 kisha vijana hao wakiwa na furaha walielekea kituo cha basi walikopanda gari, wa kwanza kuteremka alikuwa Haruni na walipofika Tegeta Kibaoni Zakayo kabla ya kumuaga fundi Yassin alisema:

“Kaka mkubwa kama nilivyokwambia, usipoufanyia kazi ushauri wangu kesho nikija itakuwa mara yangu ya mwisho kufanya kazi.”

Maneno ya Zakayo yalimwingia barabara fundi Yassin ambaye hakuwa tayari kumpoteza dogo huyo mchapakazi aliyekuwa akiijua kazi yake na wakati mwingine alipokuwa na dharura alikuwa akifanya kazi zake bila tatizo.

“Sawa kaka mkubwa nimekuelewa,” fundi Yassin alimwambia Zakayo bila Dullah kujua kama jambo hilo lilimhusu yeye.

“Kaka mkubwa, kwani Zakayo kakupa ushauri gani ambao anasema usipoufanyia kazi kesho ndiyo itakuwa mara yake ya mwisho kufanya kazi?” Dullah alimwuliza fundi Yassin.

“Ni mambo tu ya kawaida, nitakuambia,” fundi Yassin alimwambia Dullah .

Walipofika Kituo cha Kwa Ndevu, Dullah na fundi Yassin walipanda daladala la kwenda Ubungo ili pale waunganishe la tandale, kwa kuwa walipandia mwanzo walikaa katika siti moja.

Safari yao ilikuwa nzuri sana kwani haikuwa na foleni hadi Ubungo walikopanda gari la Tandika, njiani walikuwa wakizungumza mambo mchanganyiko yakiwemo ya mademu lakini fundi Yassin hakupenda kumuweka wazi kuhusu jambo alilokuwanalo moyoni.

Walipoteremka Tandale, fundi Yassin alimpeleka sharobaro Dullah kwenye baa moja ambapo alimwambia aagize kinywaji chochote alichohitaji pamoja na chakula.

Dullah aliagiza kilevi alichokuwa akitumia pamoja na chipsi na mishkaki mitatu, fundi Yassin aliangiza soda na kongoro pamoja ndizi mbili wakaanza kujiburudisha.

“Dogo, samahani kuna jambo nataka kuzungumza na wewe lakini lichukulie kawaida kwani ndiyo changamoto za maisha,” fundi Yassin alimwambia Dullah .

Dullah alipoambiwa hivyo, alishtuka na kumwuliza fundi Yassin ni jambo gani hilo ndipo akamwambia anashukuru kwa kuwa pamoja naye kule site kwa siku mbili lakini siku ile ilikuwa ya mwisho kuendelea kufanya kazi kule.

Dullah alipoambiwa hivyo alimwuliza kwa sababu gani ndipo fundi huyo akamwambia kila kitu kuhusu uwezo wake kikazi na jinsi alivyomzoea haraka Doreen na nyumba bosi wake jambo ambalo lilikuwa hatari kwake.

“Kama ulivyomsikia Zakayo akisema kama sitaufanyia kazi ushauri wake ataacha kazi, jambo lenyewe ndiyo hili ninalokueleza ndiyo maana nimeona nikwambie ukweli mdogo wangu,” fundi Yassin alimwambia Dullah .

“Yaani aliyependekeza unifukuze kazi ni Zakayo si ndiyo?” Dullah alimwuliza fundi wake.

“Siyo kapendekeza, tumeona hatari iliyopo mbele yetu kwa bosi, wewe kuwa mpole kama hela za matumizi nitakuwa nakupa wakati ukiangalia nini cha kufanya,” fundi Yassin alimwambia Dullah .

Pamoja na kauli ya fundi Yassin, Dullah alimmaindi sana Zakayo kwani alijua yeye ndiye aliyemchongea na kujisemea moyoni kwamba ‘watu wengine bwana wana roho mbaya, yaani mimi kuzoeana na mtoto wa bosi kuna ubaya gani?’

“Oke bro kwa kuwa umeamua hivyo poa tu!” Dullah alimwambia fundi Yassin.

“Siyo nimeamua, wewe kuwa mpole kama nilivyokwambia wala usimmaindi mtu yeyote,” fundi Yassin alimwambia.

Kufuatia alichoelezwa na fundi wake, Dullah alikosa raha hata bia aliyokuwa akinywa aliiona chungu, akawa anamfikiria Doreen huku ajisemea moyoni kwamba ndiyo atamkosa.

Kwa vile jambo hilo lilimchanganya akasahau kabisa kama alikuwa amepewa simu na binti huyo wa kishua hadi aliposhtuliwa na fundi Yassin aliyemwita.

“Dogo naona uko mbali kabisa,” fundi Yassin alimwuliza.

“Bro we acha tu, unajua tayari nilishaanza kuizoea kazi na kuifurahia sasa umenikatili sana wewe hujui tu!” Dullah alimwambia fundi Yassin huku moyoni akiwa na lake jambo.

“Usiwaze sana mdogo wangu, nitakapoanza kazi katika site nyingine tutaenda wote,” fundi alimwambia.

ITAENDELEA

Sharobaro wa Tandale Sehemu ya Nne

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment