Tinginya la Ba’mdogo Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA: BABU LAO WA UKWELI
*********************************************************************************
Chombezo: Tinginya La Ba’mdogo
LILIAN alishtuka na kukumbuka kuwa alistahili kuketi na kuagiza chochote. Akakifuata kiti na kuketi. Mhudumu yule wa kiume akamsogelea na kumuuliza, “Tukusaidie nini, shangazi?”
“Kwani kuna nini?”
“Kuna supu, chapati na mtori.”
“Supu ya nini?”
“Ipo ya kuku, samaki na ng’ombe.”
“Leta supu ya kuku na chapati mbili.”
Mhudumu alipotoka Lilian alitwaa simu yake na kuanza kubofyabofya akilisaka jina fulani. Alipolipata alibonyeza sehemu ya kuita na kutega sikioni na aliposikia ikiita upande wa pili akakata. Alijua kuwa huyo aliyepigiwa atajua ni nani ‘aliyem-beep.’
SAMMY alikuwa ni kijana aliyeishi kikapera. Alikuwa amepanga chumba kimoja katika mtaa huohuo wa Rufiji. Nyumba ya tatu tu kutoka pale alipoishi Lilian ndipo Sammy alipoishi.
Sammy alikuwa ni mtoto wa Mzee Kibutu. Mzee Kibutu alikuwa akifahamiana na Tonny kwa kuwa walikuwa wakifanya kazi pamoja kabla mzee Kibutu hajastaafu.
Ukaribu uliokuwapo kati ya Sammy na Tonny uliwafanya baadhi ya watu wawafikirie kuwa ni wa ukoo mmoja. Ndipo kijana Sammy ambaye wakati huo alikuwa akimalizia masomo katika Chuo cha Biashara alipojikuta akimwita ‘ba’mdogo.’ Hakuwa baba yake mdogo kiukoo bali tu ni sababu ya uhusiano mkubwa uliokuwapo kati ya Tonny na Mzee Kibutu.
Ni baba yake Sammy ndiye pia alimshawishi Tonny aachane na ukapera.
“Oa…oa uheshimike, Tonny,” mzee Kibutu alimwambia Tonny.
Mwaka mmoja baadaye Tonny alikuwa na mke. Na hakuoa, mradi anaoa, alichukua muda kuchagua mwanamke ambaye hata watu wakimwangalia mitaani wakiri kuwa ni mwanamke anayestahili kuitwa mwanamke mzuri.
Ugonjwa wa Tonny ulikuwa ni macho yaliyolegea, midomo iliyonona na makalio makubwa. Kwa mwanamke wa aina hiyo, Tonny hakusikia wala kuambiwa kitu. Ndipo siku moja akakutana na mwanadada huyu mrembo, Lilian, akamwaga sera. Urafiki ukazaliwa. Hatimaye urafiki huo ukazaa uchumba kisha ndoa.
Lilian akawa mke wa mtu, Tonny mume wa mtu. Wakaanza maisha mapya.
Mwaka mmoja baadaye mtoto Sambe akazaliwa, Mama Sambe akazidi kunawiri. Alinenepa, akawa gumzo mitaani.
“Cheki tinginya hilo….dah…limetimia…” vijana wa vijiweni walikuwa wakinong’onezana kila walipomwona akipita mtaani.
“Linakaa wapi tinginya hilo?” msela mmoja alimuuliza mwenzie.
“Nani anajua?” alijibiwa kwa swali.
“Dah…hapo mpaka uwe na umate-umate mwanangu…kama huna kitu jiengue mapema…hayo maji marefu,” mwingine alisema.
Miongoni mwa ambao macho yao yalitua kwa Lilian na kujikuta wakishindwa kustahimili ni huyu Sammy. Yeye alitambua fika kuwa alipaswa kumheshimu kwa asilimia mia moja huyu mke wa Tonny.
Lakini kwani ni mama yake mdogo wa ukweli? Ni hilo lililompa kiburi. Kujuana na kufahamiana kwa muda mrefu kati ya mzee Kibutu na Tonny ndiyo iwe sababu kwake kumheshimu na hata ikibidi kumwogopa? Hapana, hakuwa tayari kutii hilo.
Lilian siyo mama yake mdogo! Alijiaminisha hivyo na sasa ndipo alipoamua kumvalia njuga…
Siku moja alidiriki kumwambia rafikiye waliyekuwa pamoja kazini. “Kuna tinginya hilo mshkaji wangu….linaniumiza kichwa…”
“La wapi?”
“Siyo mbali, ni jirani tu na ninapoishi kama nyumba ya tatu hivi…ni tinginya la ba’mdogo wangu lakini dah…linanitia wazimu baba’ake.”
“Liko fresh sana?”
“Acha kabisa, mwana. Huwezi kuliangalia mara moja. Tinginya lina macho, macho kweli, mwanangu! Likikuangalia utadhani mko chimbo mnaduu…lazima ishtuke ndani ya suruali kudadeki… Huko nyuma nd’o acha kabisa…dah… zigo ni zigo kweli! Hapafai…likitembea mifurushi inamwagika pwata…pwata…pwata…tako, ni tako kweli!”
Jamaa yake aliguna. Akamuuliza,“Lakini si unasema ni tinginya la baba’ako mdogo?”
“Nd’o maana’ake…mkewe kabisa…ba’ mdogo anajilia kiulainiiii mpaka kishamtotolesha dogo mmoja.”
“Duh…sasa mbona unalimezea mate msh’kaji wangu?!”
“Labda hujaliona nd’o maana unashangaa…”
“Pamoja na hayo, lakini si mke wa baba’ako mdogo?!”
Ndipo Sammy alipoamua kupasua. Akamweleza ukweli kuhusu uhusiano uliopo kati ya Mzee Kibutu na Tonny.
“Haa!” jamaa yake akashangaa baada ya kuisikia simulizi hiyo. “Kumbe poa tu…kula mzigo mwanangu…vipi, u’shamtokea au nd’o bado unambwela-mbwela tu na kulialia ka’bwege? Kama ni mimi siku nyingi ningekwishampindua…ningembiduabidua mpaka akaomba poo!”
Sammy alicheka kisha akasema, “Sijamtokea mwana…lakini nd’o sasa nimeamua…inanibidi niwe makini maana’ake wanawake wengine kama hawategemei kuwa unaweza kumwambia mambo hayo duh…demu kama amejaliwa mdomo mchafu, anaweza kukuwakia mpaka ukaona giza. Kuna mademu ni mbili kasorobo kichaa wangu. Demu domo lake litakumwagia matapishi utadhani hakuuona mswaki asubuhi…anakupiga makavu tena hadharani ‘live’ baba’ake.”
“Yeah. Lakini si mna ukaribu? Mmezoeana?”
“Kwa sana tu.”
“Poa, cheza nae, mwana.”
SAMMY aliuanza mkakati. Akamfuatilia Lilian taratibu kwa siku tofauti. Ndipo ikaja siku. Ilikuwa ni jioni moja, Sammy alikuwa akitoka ndani ya duka moja lililokuwa ndani ya Soko Kuu la Kariakoo kuchukua mahitaji yake, akakutana na Lilian.
Lilian alikuwa amebeba fuko la plastiki lililosheheni matunda mbalimbali. Wakatazamana. Sammy akawa mwepesi wa kuachia tabasamu la kirafiki, tabasamu lililomshangaza Lilian kiasi cha yeye pia kujikuta akalijibu tabasamu hilo kwa kuachia tabasamu la mbali.
“Vipi ma’mdogo, naona umetoka kurekebisha mambo ya msosi,” ni neno la awali lililomtoka Sammy huku akimsogelea na kumnyooshea mkono.
Lilian naye alinyoosha mkono. Viganja vyao vikakutana. Sammy akahisi vitu vikimtambaa mwilini kwa msisimko. Hakukumbuka ni lini aliwahi kushika kiganja laini na chenye joto kama hiki. Kiganja cha mwanamke ampendaye! Alihisi mabadiliko fulani mwilini kiasi cha kujikuta akiikosa sauti yake kwa muda.
Lilian na Sammy hawakuwa na mazoea sana. Lilian alimtambua vizuri Sammy kuwa ni mtoto wa mzee Kibutu, ambaye ni rafiki mkubwa wa Tonny. Hivyo mara chache ambazo iliwahi kutokea Sammy alifika kwa Tonny akiwa ametumwa na baba yake, au kwa sababu yoyote nyingine ya kawaida, walizungumza kidogo tu na zaidi ni kusalimiana na kusema kilichompeleka.
Hata hivyo, Lilian aliwahi kumfumania Sammy akimtazama kwa namna izungumzayo mengi siku walipopishana na baada ya hatua chache Lilian akageuka.
Ndiyo, ni siku hiyo alipohisi kuwa yale macho ya Sammy yalikuwa na kitu kingine kilichojificha moyoni. Kwa ujumla Sammy alimtazama kwa matamanio, jambo ambalo halikuwa la ajabu kwa Lilian kwani mara kadhaa alishawahi kuwaona watu wakimkodolea macho na hasa inapotokea akawa amevaa suruali zilizomshika vilivyo mwilini.
“Ndiyo, ma’mdogo,” hatimaye Lilian alijibu huku akiuachia mkono wa Sammy taratibu. “Za saa hizi?”
“Nzuri tu. Za kwako?”
“Shwari tu,” Sammy alijibu na kuongeza papohapo: “Vipi nd’o unakwenda home?”
“Ndiyo.”
“Hata mimi. Nadhani tufuatane.”
Walifuatana. Njiani wakawa na mazungumzo ya kawaida lakini wakati huohuo Sammy akipanga namna ya kumwingia Lilian. Alijali kutumia ustaarabu katika kujieleza, asije akamkwaza na kujikuta ameharibu kila kitu.
Ni wakati walipokuwa wakiuvuka Mtaa wa Msimbazi ndipo Sammy alipoamua kukata mzizi wa fitina. Akajitahidi kujieleza kwa kifupi lakini kwa ufasaha, akimfikishia ujumbe maalum wa dukuduku lake.
Hakutarajia jibu la kukubaliwa haraka, lakini pia aliamini kuwa kujieleza kwake kulijitosheleza hivyo hakuwa akitegemea kukataliwa bali ‘kupigwa kalenda.’
Lilian alimtazama Sammy, akishindwa kuamini kama hayo aliyosema Sammy yalimtoka kwa dhati au ulikuwa ni mzaha fulani. Na kama ni mzaha, anaweza kufikia hatua ya kumfanyia mzaha wa aina hiyo?
Hakukasirika, alishangaa tu kisha akacheka kidogo na kumuuliza, “We Sammy mbona huna adabu?”
“Kwa nini ma’mdogo?”
“Mbona unaleta utani huo?’
“Niko serious, ma’mdogo,” sauti ya Sammy ilikuwa kama aombolezaye. “Sijawahi kukwambia hivi, na hata hatujawahi kutaniana. Mpaka hapo huoni kwamba siwezi kuleta masikhara kwa ishu hii?”
Wakati huo walikuwa wamefika kando ya duka moja na Sammy akapendekeza waketi wanywe soda. Lilian hakukaidi. Wakaketi na kuagiza vinywaji.
NI wakati walipokuwa wakiuvuka Mtaa wa Msimbazi ndipo Sammy alipoamua kukata mzizi wa fitina. Akajitahidi kujieleza kwa kifupi lakini kwa ufasaha, akimfikishia ujumbe maalum wa dukuduku lake.
Hakutarajia jibu la kukubaliwa haraka, lakini pia aliamini kuwa kujieleza kwake kulijitosheleza hivyo hakuwa akitegemea kukataliwa bali ‘kupigwa kalenda.’
Lilian alimtazama Sammy, akishindwa kuamini kama hayo aliyosema Sammy yalimtoka kwa dhati au ulikuwa ni mzaha fulani. Na kama ni mzaha, anaweza kufikia hatua ya kumfanyia mzaha wa aina hiyo?
Hakukasirika, alishangaa tu kisha akacheka kidogo na kumuuliza, “We Sammy mbona huna adabu?”
“Kwa nini ma’mdogo?”
“Mbona unaleta utani huo?’
“Niko serious, ma’mdogo,” sauti ya Sammy ilikuwa kama aombolezaye. “Sijawahi kukwambia hivi, na hata hatujawahi kutaniana. Mpaka hapo huoni kwamba siwezi kuleta masikhara kwa ishu hii?”
Wakati huo walikuwa wamefika kando ya duka moja na Sammy akapendekeza waketi wanywe soda. Lilian hakukaidi. Wakaketi na kuagiza vinywaji.
Kwa kuwa walikuwa peke yao hapo nje ya duka, Sammy aliendelea kumshushia mistari Lilian.
Hatimaye: “Itakuwa ngumu, Sammy,” ilikuwa ni kauli ya awali ya Lilian, akithibitisha kuwa sasa ameelewa kila alichokuwa akikihitaji Sammy.
“Kwa nini ma’mdogo?”
“Sijui, lakini kwa kweli sijazoea mchezo huo. Nina mume, halafu tena nifanye mchezo huo!Yaani hata hainiingii akilini. Baba yako na Baba Sambe ni marafiki wakubwa kama ndugu vile, halafu….mmmh…hapana haiwezekani!”
“Unachohofia ni nini, ma’mdogo?” Sammy alikuwa king’ang’anizi. “Au una wasiwasi kuwa huenda ishu ikabumburuka? Basi ondoa hofu. Nakuhakikishia itakuwa ni siri yetu, siri isiyovuja.”
Walizungumza kwa kirefu, na walipoachana bado hakukuwa na mwafaka halisi uliopatikana. Na Sammy alijiwa na wazo la kuomba namba ya simu lakini akasita. Akahisi kuwa atajisikia vibaya endapo Lilian atamtolea nje. Akauchuna japo moyo ulimuuma.
Alitambua fika kuwa kwa dunia ya leo mawasiliano ya simu ni muhimu, lakini hata hivyo alitambua pia kuwa watu wengi hususan wanawake walioolewa sio wepesi wa kutoa namba zao za simu waombwapo na mwanamume mwingine ambasye hawana nasaba yoyote.
Hata hivyo, Sammy hakukata tamaa. Alijua kuwa ipo siku watakutana tena, na watazungumza tena, na huenda siku hiyo ndipo atajua kama ‘maharage ni mbegu au mboga.’
Ujirani wao ulikuwa ni nafuu zaidi kwa Sammy. Aliutumia mwanya huo kumvizia Lilian mara kwa mara ili apate nafasi ya kukutana naye tena. Wakakutana tena, kwa mara ya pili, safari hii ikiwa ni eneo la kituo cha daladala cha Fire. Wakazungumza kwa kifupi na baada ya Sammy kuiomba namba ya simu ya Lilian kwa kusihi sana, hatimaye alipewa, naye Lilian akachukua namba ya Sammy.
“Lakini usiwe na pupa ya kunipigia,” Lilian alimwambia, kauli ambayo Sammy aliichukulia kuwa ni hatua moja nzuri ya kwenda kwenye mafanikio.
“Muda gani ni mzuri kwa kukupigia?”
“Usipate taabu. Usipige, mimi nikiwa na nafasi nitaku-beep.”
Zilipita siku tatu bila ya chochote kutokea. Kila wakati Sammy alitarajia Mama Sambe angempigia, lakini haikuwa hivyo. Hata hivyo, alijitahidi kulinda makubaliano yao, kuwa asipige simu hadi Lilian mwenyewe ‘atakapom-beep’ pale atakapokuwa na nafasi nzuri ya kuongea.
Hisia kuwa huenda Lilian alimwambia hivyo kwa kukusudia kutokuwa na mawasiliano naye zikamjia. Ilishafika wiki nzima bila ya Lilian ‘kum-beep.’ Kuna lolote hapo? Kuna matumaini tena? alijiuliza kwa kukata tamaa.
Alianza kukata tamaa, lakini labda angekata tamaa kabisa kama siku moja, asubuhi, kitu kama saa mbili hivi, asingeona neno JIRANI kwenye ‘screen’ ya simu yake wakati ilipoita. Ndiyo kwanza alikuwa yuko kwenye daladala eneo la Makumbusho akielekea Mwenge ambako alikuwa akifanya kazi kwenye kiwanda cha uchapishaji vitabu.
Alishtuka na kubaki akiitazama tu simu hiyo bila kuminya kitufe cha kupokelea. Simu iliendelea kuita. Hatimaye akashtuka na kuminya kitufe hicho huku akiisogeza simu sikioni. Kwa mbali alihisi mapigo ya moyo yakimwenda kasi.
“Haloo,” alisema kwa sauti nzito na ya chini.
“Hellow,” sauti nyembamba na ya unyonge ikapenya sikioni mwake. “Ni Sammy?”
“Yeah. Ma’mdogo?”
“Ndiyo. Uko wapi?”
”Nd’o naelekea kazini. Niko maeneo ya Makumbusho.”
“N’na shida na wewe. Tunaweza kuonana mida hii?”
Sammy alifikiri kidogo na kisha akajibu, “Inawezekana. We’ uko wapi?”
“Niko Kariakoo.”
“Kariakoo?! Na unataka tuonane hukohuko Kariakoo?”
Ukimya mfupi ukapita. Kisha: “Sio lazima tuonane huku. Sema wewe.”
Sammy alishusha pumzi ndefu akiwaza. Hakutarajia kupigiwa simu na Lilian leo, na siyo leo tu bali hakutarajia kupigiwa simu asubuhi kiasi hicho. Kuna nini? Kuna tatizo? Japo alimpenda na kumhitaji sana Lilian, lakini pia hakutarajia kama ingekuwa ghafla kiasi hicho.
Hata hivyo, hakuwa tayari kuipoteza nafasi hiyo. Hivyo, baada ya kufikiri harakaharaka, akasema, “Fanya hivi, njoo Kinondoni.”
“Kinondoni?”
“Ndiyo. Njoo Kinondoni. Shukia kituo cha Studio. Ukifika hapo unijulishe.”
“Ok.”
Sammy akalazimika kukiumiza kichwa chake kwa kufikiria la kufanya. Hakutaka kuipoteza nafasi hii pekee ambayo hakujua ni lini ataipata tena. Na sasa yeye anakwenda kazini. Atumie hila gani za kuwahadaa wakuu wake wa kazi ili apate mwanya wa kukutana na Lilian?
Msiba.
Naam, aliona kuwa taarifa inayoweza kukubalika kwa wakuu wake wa kazi ni inayohusu kupatwa na msiba. Hivyo, wakati alipoteremka kituoni ndipo alipoamua kupiga simu kazini kwake. Huko akaongea na bosi wake moja kwa moja akimdanganya kuwa mpangaji mwenzake kafariki.
Bosi wake hakuwa na kipingamizi chochote, akamruhusu ‘kushinda msibani.’ Ruhusa hiyo ilimpagawisha Sammy. Akakimbilia daladala jingine lililokuwa likielekea Kariakoo. Muda mfupi baadaye akawa njiani kwenda Kinondoni.
Akiwa ametulia kitini, daladala likipita eneo la kituo cha ITV, alitwaa simu yake na kuandika ujumbe: UMESHAONDOKA? Akautuma ujumbe huo kwa Lilian. Dakika chache baadaye, jibu likarudi: NITAKUJA BAADA YA NUSU SAA.
Sammy akasonya. Akilini mwake aliamini kuwa tangu walipowasiliana, tayari Lilian alishapanda daladala na hivyo huenda alikuwa maeneo ya Magomeni. Kumbe hata mtu mwenyewe hajatoka huko Kariakoo!
Hata hivyo hakuona kuwa kuna kilichoharibika. Subira yavuta heri. Kwa kuwa hakukuwa na foleni, aliwahi kufika kituo cha Studio na kuteremka. Na ndipo alipokumbuka kuwa alikuwa hajatia kitu tumboni tangu alipotoka kitandani.
“Usela huu!” alinong’ona huku akicheka kimoyomoyo. Alijua kuwa kama angekuwa na mke, basi asubuhi angeondoka huku akiwa amepata stafutahi nzito na hivyo labda asingehitaji kutia kitu tena tumboni mchana.
Hata hivyo, kwa kuwa hakujua kuwa lengo la Lilian ni nini, na huenda pia siku hiyo ikawa ndiyo bahati yake ya ‘kula kuku’, akaenda kwenye baa moja iliyokuwa jirani na kituo hicho. Hapo aliagiza supu na chapati tatu na kuvishusha tumboni kwa usongo. Kisha akashushia maji baridi lita moja.
Alipotoka hapo alikwenda kwenye kibanda cha kituo cha daladala na kuketi akijisomea gazeti.
KITU fulani kilimwambia Lilian kuwa ‘Akuanzae mmalize.’ Na akaamua kuufanyia kazi usemi huo. Hivyo asubuhi hiyo, baada ya kumpigia simu Sammy, alipata kifungua kinywa cha nguvu katika mgahawa huo na alipohakikisha kuwa tumbo limetosheka alitulia kidogo, akimwazia Tonny na tabia zake mpya alizozianzisha.
“Ni kama vile karogwa!” alinong’ona kwa sauti ambayo haikuweza kuyafikia masikio ya mteja mwingine aliyeketi jirani yake
ITAENDELEA
Tinginya la Ba’mdogo Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;