Cosa Nostra Sehemu ya Nne
KIJASUSI

Ep 04: Cosa Nostra

SIMULIZI Cosa Nostra
Cosa Nostra Sehemu ya Nne

IMEANDIKWA NA: THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi: Cosa Nostra

Sehemu ya Nne (4)

Ndipo hapa serikali ikabidi kuingilia kati na kuanza kuusambaratisha mtandao wa Mafia.

Zikaendeshwa oparesheni maalumu za kijeshi kuwatambua na kuwakamata wanachama wa familia za mtandao wa Mafia.

Ndani ya miezi miwili pekee wanachama 177 wa familia za mafia walikamatwa.

Hii ikasababisha wanachama wengine wa familia zote kusitisha shughuli zao na kujificha.

Zaidi ya miaka mitano (1963 – 1968) hakukuwa na shughuli zozote za kihalifu za mtandao wa Mafia.

VITA KUU YA PILI YA FAMILIA ZA MAFIA

Kwa miaka mitano hakukuwa na shughuli za mtandao wa Mafia, lakini ilipofika mwishoni mwa mwaka 1969 taratibu sana mtandao wa mafia ukaanza kurejea tena katika shughuli zake.

Ilipofika mwaka 1970 nchini ufaransa serikali iliendesha oparesheni kali ya kufunga maabara za kihalifu zilizokuwa vinatengeneza madawa ya kulevya aina ya Heroin.

Pia walipiga marufuku uvutaji na uingizaji wa sigara nchini Ufaransa.

Hivyo basi uhitaji wa madawa aina ya heroin na sigara ukakua kwa kasi kubwa nchini ufaransa.

Mabosi wa mtandao wa Mafia wakaona fursa adhimu ya kibiashara. Hivyo basi wakaitisha mkutano na kusuluhisha migogoro yote iliyotokea huko nyuma.

Wakaweka lengo moja tu kuwa, mtandao wa Mafia uteke soko heroin na sigara nchini ufaransa na marekani.

Wakafungua maabara za kutengeneza heroin na kutengeneza mitandao ya kihalifu ya usambazaji mizigo.

Baada ya mwaka mmoja wakawa wameteka soko la heroin nchini Ufaransa.

Baada ya hapo wakaingia marekani hasa majimbo ya kaskazini na kuanza kutengeneza mitandao ya uuzaji na usambazaji wa heroin.

Hili walilifanikisha kwa ustadi mkubwa kwani, migahawa mingi ya kuuza Pizza (Pizzaria) nchini marekani ilimilikiwa na waitaliano.

Kwahiyo waliingia makubaliano na wenye migahawa ambapo mzigo wa heroin ulifikishwa kwao na wao walitumia kivuli cha kuuza pizza kuwapa wauzaji wa mtaani (street dealers).

Ndani ya miaka miwili tu Mafia wakawa wanamiliki 80% ya soko la heroin kwa majimbo ya kaskazini mwa Mareni.

Ndipo hapa wanasema “palipo ridhiki hapakosi fitna”.

Mwaka 1975 kipindi ambacho mapato yatokanayo na shughuli za Mafia yako juu sana, kiongozi wa familia ya Carleone aliyeitwa Don Luciano Leggio ambaye pia alikuwa ni mjumbe wa tume ya Mafia (Mafia Commission) akaanzisha kampeni ya siri ya kuunganisha familia za Mtandao wa Mafia na akaziita Corleonesi yeye mwenyewe akiwa kama kiongozi Mkuu.

Lengo kuu lilikuwa ni kutawala kuatawala biashara na shughuli za Mafia huku wakiwatenga familia nyingine ambazo zilikataa kujiunga katika umoja huo wa Carleonesi.

Katikati ya mwaka 1975 Don Leggio akapata Bahati mbaya kukamatwa na serikali akishutumiwa kwa kosa la uuaji na akatupwa gerezani.

Hii ilimlazimu kumuachia madaraka msaidizi wake aliyeitwa Don Salvatore Riina.

Baada ya Don Riina kuchukua madaraka akaanzisha mipango ya kuwaondoa katika Tume Mabosi wa familia ambazo walikataa kujiunga na umoja wao wa Carleonesi.

Nieleze kwa ufupi kuhusu Tume ya Mafia (Mafia Commision)

Hiki ni kakao maalumu au baraza ambalo linaundwa na mabosi wa familia zote za Mafia.

Kazi kubwa ya Tume hii ni kusuluhisha migogoro, kugawa maeneo ya biashara na kuweka mikakati ya kibiashara.

Kwa hiyo Don Riina akatamani Tume hii itawaliwe na mabosi wanaounga mkono umoja wao wa Carleonesi pekee.

Hivyo akaanza kuzusha tuhuma za uongo dhidi ya mabosi wenzake ambapo tuhuma hizo zilisababisha mabosi hao kukosa sifa ya kuendelea kuwa wajumbe wa Tume ya Mafia.

ITAENDELEA

Cosa Nostra Sehemu ya Tano

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment