Cosa Nostra Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA: THE BOLD
*********************************************************************************
Simulizi: Cosa Nostra
Sehemu ya Tatu (3)
Baada ya kuvamiwa na vuruga za vita kukolea magereza mengi yaliharibika na wafungwa wote wakiwemo mafia kutoroka.
Baada ya majeshi ya kifashisti yakiongozwa na Mussolini kushindwa, na Mussolini mwenyewe kuuwawa, majeshi ya magharibi yakaanza kuchagua uongozi wa muda kwenye miji mbali mbali nchini Italian.
Wanasiasa wengi wanao fungamana na Mafia walichangamkia fursa hii na kuteuliwa kuwa viongozi katika jimbo la Sicily.
Jambo kubwa lililowasaidia ilikuwa ni vile toka awali (kabla ya vita) walikuwa hawaungi mkono sera za kifashisti na ukomunisti ulioanzishwa na Benito Mussolini.
Baada ya Mafia waliofungwa kutoka magerezani na viongozi wao kuchukua tena madaraka, taratibu mitandao yao ya kihalifu na shughuli zao zikaanza kurudi tena katika jimbo la Sicily na Italia kwa ujumla.
SEHEMU YA II
VITA KUU YA KWANZA YA WENYEWE KWA WENYEWE.
Baada ya vita kuisha na Italia na Dunia yote kurudi katika halia ya kawaida, shughuli za kihalifu za Mafia ziliendelea.
Mwaka 1962 Moja ya mabosi wa mafia aliyeitwa Don Cesare Manzella aliandaa mpango wa kusafirisha mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Italia ili kuuingiza mchini marekani.
Mzigo huu ulisafirishwa kwa meli.
Kama ilivyo ada kwenye shughuli za mafia mtu akiwa na “dili” alipaswa pia kuhusisha familia nyingine za Mafia katika kulitekeleza, hivyo basi Don Manzella akawapa jukumu familia ya Grecos na La Barberas kusimamia usafilishaji wa mzigo huo.
Wakiufikisha marekani walitakiwa kuuwasilisha mzigo kwa Bosi mwingine aliyeitwa Don Calcedonio Di Pisa.
Mzigo ulipofika marekani na kupokelewa na Don Di Pisa na kisha kuupeleka kwa wanunizi wa jumla, akalipwa hela ndogo na kuwaambia waliouleta (familia ya Grecos na La Bearbaras) kuwa wanunuzi wamemtapeli wakidai mzigo ni Mdogo.
Familia ya La Berbaras hawakuamuamini wakamshutumu kwa ameiba sehemu ya mzigo na kuuficha kabla ya kupeleka kwa wanunuzi wa jumla.
Suala hili ikabidi lipelekwe kwenye tume ya Mafia (nitaeleza baadae kuhusu Tume za mafia).
Kwa mshangao mkubwa Tume ikafikia hukumu kuwa ni kweli wanunuzi wa jumla wamemtapeli Don Di Pisa na kumpa hela ndogo..
Suala hili likawatia hasira familia ya La Berbaras na kuamua kuwawimnda na kuwauwa kuanzia aliyewatuma kupeleka mzigo marekani (Don Manzella) na waliyemkabidhi mzigo Don Di Pisa.
Kitendo cha kuuwawa kwa mabosi hawa kikaanzisha mtafaruku mkubwa baina ya familia tofauti tofauti ndani ya Mafia huku kila familia ikiegemea upande fulani.
Mtafaruku ukawa mkubwa kiasi kwamba ukatengeneza uhasimu wa familia tofauti ndani ya mafia na punde tu wakaanza kuwindana na kuuwana mchana kweupe.
Jambo baya zaidi hawakuishia kuuwana wenyewe kwa wenyewe tu bali pia hata wasiohusika walikumbwa na madhira haya.
Kwa mfano polisi waliokuwa wanahisiwa kuunga mkono familia fulani waliwindwa na kuuwawa na familia nyingine.
Pia marafiki wa familia hii waliwindwa na kuuwawa na familia nyingine.
Ndani ya miezi 6 ( May 1962 hadi January 1963) kulikuwa na vifo zaidi ya 700 vilivyosababishwa na ugomvi wa familia za Mafia.
ITAENDELEA
Cosa Nostra Sehemu ya Nne
Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;