Isabel Ndani ya Mpango Hasi ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Isabel Ndani ya Mpango Hasi

SIMULIZI Isabel Ndani ya Mpango Hasi
Isabel Ndani ya Mpango Hasi ya Pili

IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE


Simulizi : Isabel Ndani Ya Mpango Hasi

Sehemu ya Pili (2)

Joseph Msengiyunva akiwa katika mazoezi yake ya karate ndani ya ua wa nyumba yake, kijasho kikimtoka kutokana na nguvu alizotumia katika mchezo huu anaoupenda tangu akiwa mtoto. Hata alipokuwa jeshini katika jeshi la serikali palae Burundi kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwafundisha mchezo huu askari wenzake ambaye walikuwa hodari sana. Lakini nyuma yake alijihusisha na watu wenye kazi za kijasusi kuwasaidia hapa na pale katika kazi ngumu walizohitaji zifanyike haraka na kwa makini.

Baada ya kumaliza mazoezi yake aliingia ndani kuelekea maliwatoni kwa ajili ya kupata maji kabla hajaanza ratiba nyingine. Alipofika sebuleni kwanza kabisa alifungua compyuta yake ndogo na alipoingia mtandaoni alikuta kuna email mpya imeingia

‘JOB’ ndivyo ilivyoandikwa na hakukuwa na neno lingine. Jomse aliitazama email ile na kuvuta kiti kisha akakaa vyema nae akaijibu vile vile

‘JOB’ alipoenda kuoga na kurudi akiwa mezani anapata chai email nyingine iliingia ‘Job 7:15’ , baada ya kusoma hiyo naye akatuma jibu

‘Holy bible’, muda si mrefu alipata email iliyosema

‘Fellowship’ akasoma na kusubiri kidogo email nyingine ikaingia ‘Bujumbura Cathedral Library’ .

Saa moja na robo asubuhi Jomse alipandisha taratibu ngazi za kuingia kanisa kuu la Bujumbura, baada ya kumaliza ngazi hizo alipita kushoto na kuelekea iliko maktaba ya kanisa hilo, aliingia na kutazama huku na huku hakuna aliyemjua, alielekea kati shelf la vitabu vya dini na akachagua Biblia Takatifu moja kwa moja alifungua agano la kale kitabu cha Job, alipofungua tu akakuta kijikaratasi kimepachikwa hapo, ‘utamkuta Gitega Stadium mbele ya mlango mkubwa, muombe atakupa moto’ . Jomse alitoka katika maktaba ile na kukodi tax

“Uwanja wa mpira wa Gitega tafadhali” alimueleza dreva. Na dreva aliijua kazi yake sawasawa. Dakika chache alikuwa mbele ya mlango wa uwanja huo, kijana mmoja alikuwa ameketi kwenye jiwe akisoma gazeti, Jomse akamsogelea na kumgongea kidole kama ishara ya kuomba kitu, kijana yule akatoa kiberiti cha gas na kukiwasha.

Gari nyeusi ilisimama mbele yao na wote wakaingia ndani na kuelekea kusikojulikana. “Jomse, kutana na Mandi” kijana yule akamtambulisha Jomse kwa Mandi ambaye alikuwa analiendesha gari hiyo

“Na mimi naitwa Ton au Tonton kutokana na mwili wangu mdogo.” Naye alijitambulisha na wote wakacheka sana. Gari ile ilisimama katika nyumba Fulani na wote wakashuka na kuingia humo.

Mzee kasimu alikuwa chini amelala kimya hakujua hata kinachoendelea duniani, damu zikimtoka kifuani bila kujali. Mandi alishampiga risasi mzee huyu baada ya purukushani katika chumba kile cha injini. Sasa Mandi hakujua hata afanyeje kupunguza mwendo wa treni lile ambalo muda huo lilikuwa kwenye kasi ya ajabu. Mandi alijificha kuangalia kinachoendelea, mara akasikia sauti za watu wakiongea na kutahamaki aliwaona koplo Kibona na afande Benso wakiingia na bunduki zao. Wote walipigwa bumbuwazi baada ya kuona mwili wa mzee Kasimu ukiwa bila uhai.

“Ni nini hiki kinachotokea?” afande Benso aliuliza kwa mshangao

“Phhhh!!!!” Koplo Kibona alishusha pumzi ndefu na kujishika kiuno kisha akasema “Nikimkamata huyu au hawa, kama ni embe dodo ntawala na maganda”

Waliuweka vizuri mwili ule na kuuhifadhi, kisha wakapiga redio kwenye behewa lao la usalama kutoa taarifa.

“Sasa hili dude nani ataliongoza!? Maana opereta ndiyo huyu kauawa, nani anayefanya unyama huu?” Koplo Kibona alichuki akaongea huku akirusharusha mikono yake. Alimuacha pale afande Benso aikmuomba awasiliane na steshen masta ili amuelekeze anagalau cha kufanya ili kusimamisha kabisa treni ile. Koplo Kibona alitoka kwenye injini na kuelekea mabehewa ya nyuma ambayo yote yalitawaliwa na habari ya mauaji hayo, lakini hakuna aliyejua kama treni hilo lilikuwa likienda bila opereta.

Ton na Jomse walikuwa bado kwenye maficho yao kila mmoja akikwepa polisi lakini walishangaa kwa nini Mandi hajafanikiwa kumfanya operetta yule apunguze mwendo. Jomse alitulia na kila alipoitafuta simu ya Mandi haikuita kabisa, Ton nae vivyo hivyo. Koplo Kibona na askari wengine walii\kutana kwenye behewa lao la mwisho wakitafakari la kufanya huku hali ya afande Kirama ikiwa si yakuridhisha.

Isabel alikaa sana katika maficho yake, alijaribu kufikiria cha kufanya na aliumia sana alipojua kuwa yule askari kijana aliyekuwa naye mle ndani kapoteza maisha kwa ajili yake, Isabel akaanza

kulia, na liposikia Koplo Kibona akiongea na wenzake kuwa operetta ameuawa ilimchanganya zaidi ‘yote haya kwa ajili yangu’ alijisemea moyoni, aliumia sana alipojua kuwa muda wowote treni ile inaweza pata ajali na mamia ya watu kufa alijiona kuwa yeye ndiye chanzo cha kila kitu. Alisali na kuomba Mungu ampe njia au wazo la kufanya lakini hakuamini kabisa kama polisi wale akiwashirikisha watamsaidia au watamuweka ndani tu. Isabel akapata wazo, akaichukua ile memory card na kuitazama ukubwa wake akatoa simu yake nyingine ambayo ina uwezo wa kusoma card za mtindo huu akaipachika na kuiwasha simu akaona kuna faili Fulani lakinihaikuweza kufungua faili lile kutokana na format iliyotumika. Isabel alikuna kichwa, afanye nini akapata wazo akashusha begi lake la mgongoni kwa hadhari kubwa na kuchukua waya maalumu wa simu hiyo ambao unaweza kuunganisha ili kufanya kazi fulanifulani, akaupachika na kuunga katika laptop yake. Aliiwasha laptop kwa kufunika na likitambaa aliloliokota hapo ili mwanga usionekane na atakayepita njia. Akafungua Memory card ile nakukuta kuna faili moja tu lenye kichwa cha habari ‘Mpango Hasi’ , Isabel alisoma taratibu faili lile huku akitetemeka na kulia, kila mara machozi yalidondoka kwe keyboard ya laptop ile, aliendelea kusoma mpango mzima Isabel alijikuta akiacha kusoma mara kwa mara faili hilo. Mpango hasi, mpango uliyoandaliwa na kikundi Fulani ambacho leno lake ni kuja kufanya mapinduzi nchini Tanzania kama ilivyofanyika huko Rwanda na Burundi mwaka 1994, mpango huo ulionesha utaratibu wote wakutimiza azma hiyo kwa hapa Tanzania lakini kuna watu ambao lazima wauawe kabla mpango huo haujaanza rasmi kwa kuwa watu hao watakuwa vikwazo katika mpango huo. Isabel alisoma majina yale yapatayo kama kumi na tano hivi. Isabel alibaki mdomo wazi, sasa alijua kwa nini watu wale wanaitafuta memory card ile. Isabel alifikiri afanye nini kuliokoa taifa lake alipendalo kutoka katika mpango huu ulioitwa mpango hasi ‘sasa taifa liko mikononi mwangu’ alijiwazia lakini hakuwa na la kufanya. Kila wazo la kuwapatia polisi taarifa ile lilipomjia alilifuta mara moja. Akarudisha akili tena katika majina yale ambayo yaliandikwa katika orodha ile, majina yale yaliandikwa na mbele yake kuliandikwa sehemu mtu huyo anafanya kazi na ni kazi gain, Isabel alisoma majna moja baada ya jingine, majina mengine alishawahi kuyasikia lakini mengine ni mage sana kwake.

Macho ya Isabel yakavutiwa na jina moja tu kwa jinsi lilivyo ‘Amata Ga Imba TSA namba 1’ , Isabel alilisoma mara kwa mara lakini aliona labda huyu anaweza kutatua kitendawili hiki baada ya kusoma kirefu cha ile TSA (Tanzania Secret Agency) shauku ilimjaa Isabel lakini atampataje mbona hata simu haijui. Kwa kuwa msichana huyu alikuwa mtundu sana alipata wazo haraka, akachukua moderm yake na kuiunganisha kisha akawasha mtandao na kuiita kurasa maarufu duniani ‘facebook’, alipoingiza nywila zake kurasa ikafunguka na moja kwa moja alikwenda kwebye search bar, akaclick find friend akaingiza jina Amata Ga .. kabla hajamaliza yenyewe ikamalizia Ga Imba, akabofya add friend na hapo hapo akaingia kwenya meseji na kumuandikia

‘Amata Ga Imba,

mimi naitwa Isabel, hivi sasa nipo katika treni ya kutoka Kigoma kuelekea Dar es salaam. Kuna watu wanataka kuniua naomba msaada wako haraka. Si mimi tu tupo watanzania zaidi ya elfu kumi ambao muda si mrefu tutakufa kwa ajali mbaya ya treni. Polisi mmoja na muendesha treni wameuawa,majambazi tunao humu ndani’

Alipomaliza kuandika hiyo meseji akatazama kuna notification moja alipoicheki akakuta Amata Ga Imba ameconfirm urafiki, Isabel alijikuta anataka kuruka kwa furaha. Meseji yake ikajibiwa haraka

‘Isabel,

Hunijui na wala sikujui hayo matatizo waeleze polisi ndiyo kazi yao na si mimi’

Isabel aliumia sana akajua kuwa labda alikuwa anawasiliana na mtu mwingine, hakusita akaandika tena.

‘kuna mpango kabambe, mpango wa mapinduzi katika nchi yetu, mpango huu unaitwa mpanho hasi. Lakini kabla haujaanza plan A ni kuwauwa watu watakaokuwa vikwazo na wewe ni mmoja

wao. Mimi nimeokota memory card ndimo nimesoma na kujaribu kila jina na lako ndiyo nimelipata katika mtandao’

Isabel aliweka mikono yake mashavuni akiomba meseji ile ijibiwe haraka. Kwa upande wa Amata aliona swala kama hili si la kuletea mchezo, maana michezo kama hii ya dhihaka ameizoea ila hapendi kuipuuzia.

‘Attach file, tuma kwangu’

Isabel akasita lakini afanyeje, akaanza kufanya haraka kutuma faili lile, lakini kabla halijawa tayari alijikuta kashikwa bega alipogeuka alipokea kofi moja kali, Isabel laptop ilimtoka mikononi na kudondoka chini, akatoka pale alipokuokota ile laptop kabla hajaifikia Ton alimpiga teke la mbavu liliomfanya aanguke jirani kabisa na ile laptop bila kuchelewa alibonyeza tarakimu Fulani kabla hajamaliza Jomse alimkanyaga mkono, Isabel alilia kwa uchungu akanyanyua mkono mwingine na kubofya fasta na meseji ile ikaenda, lakini bahati mbaya faili lile halikuweza kwenda. Ton aliichukua laptop ile na kuivunja vipande viwili walijaribu kupekua begi lake lote lakini hawakupata walichokitaka, Isabel akaona hapa mambo yameharibika alijivuta kutoka alipo huku akilia akaidaka ile simu akaifungua haraka na kuto ile memory card, kabla Ton na Jomse hawajamuona Isabel aliimeza ile memory card. Mara simu yake iliita akaitoa mfukoni na kuipoipokea kicha akaitupia karibu na mizigo ikiwa imepokelewa.

“Iko wapi?” Ton alipga makelele huku akimpiga mateke Isabel, Isabel alilia kwa uchungu akiwa pale chini anagalagla

“Utasema husemi, unafikiri kuna mtu wa kukutetea hapa? Nakuua”Jomse alimtishia na bastola yake. Polisi walifika eneo lile

“Freeze!” akiwa kamnyoshea SMG Ton, Jomse alifyatua bastola yake Koplo Kibona alipaishwa na kujigonga juu kabla ya kudondoka chini akiwa mfu… kimenuka.

Hali ya hewa ika wa mbaya, polisi walirusha risasi kuwashambulia Jomse na Ton lakini kazi haikuwa rahisi kwani vijana hawa walikuwa wana mafunzo maalum ya kijeshi, walitoweka eneo hilo na kukimbilia kwenye mabehewa ya watu wengine, polisi nao wakaliunga uko huko.

Amata Ga Imba, Tanzania Secret Agency namba 1, alisikia kila kitu kilichoendelea kwenye treni ile kupitia simu ya Isabel. Alitamani muda huo ajikute ndani ya treni hiyo baada ya kusikia kilio cha uchungu cha Isabel kupitia simu ile, afanyeje? Alinyanyu simu yake haraka na kumpigia nkuu wake wa kazi

“Hello” Amata aliita

“Hello mbona usiku sana kuna nini wakati mimi nimekwambia upumzike, Kamanda Amata” Madam Suzan au kama wenyewe wanavyomwita ‘S’ aliinuka nakuketi kujibu simu hiyo “Dharula, miss S, kuna habari nimepata sasa, kwenye treni ya Kigoma Dar kuna mauaji

yanaendelea na huyu mtu kawasiliana na mimi moja kwa moja, msaada wako” Amata alisubiri jibu lakini akaona ukimya umetawala. Simu ikakatika, Amata alikunja uso wa lawama kwa mkuu wake wa kazi. Simu ya Amata iliita tena

“Kamanda Amata samahani nilimpigia RPC wa Tabora na IGP kuhusu hilo nimepata taarifa, kutokana na uzito wa shughuli yenyewe nakuteua uende sasa hivi, helkopta ya polisi inakusubiri

airport.” Amata hakusubiri simu ya S iendelee. Alikurupuka kitandani na kufungua kabati lake akachukua bastola yake moja na vikasha vya risasi kadhaa akatupia kenye kibegi chake, akavaa jeans lake jeusi, fulana nyeusi, boot ya kazi akapachika kisu chake kiunoni … kamili! Alivaa kofia lake la puendeshea pikipiki.

Muda mchache alikuwa barabara ya Kawawa akielekea Magomeni, usiku huo hakukuwa na magari, ilimchukua muda wa dakika kumi tu kuwasili uwanja wa ndege terminal one, alikuta tayari rubani na msaidizi wamewasha injini tayari kuondoka.

“Kamanda… twende!” rubani wa Helkopta alimwita Amata na bila kuchelewa Amata alijirusha ndani safari ikaanza.

Wakiwa hewani Kamanda Amata alijilaza kwenye kijitanda cha kamba akitafakari hili na lile akijiuliza imekuwa Isabel atumbukie katika tatizo kama hilo alijipa moyo kuwa akifika atajua kila kitu, moyoni alimsifu sana Isabel kwa kutumia akili siyo tu ya kuzaliwa lakini naya shule pia.

Lakini mara nyingine alijiona mjinga sana akaona ingekuwaje kama amewekewa mtego kwa mtindo huo na ye kanasa kijinga namna hiyo, alijicheka na kujiona kweli yeye mjinga, lakini bado alijiuliza kwa nini usiku ule aliendelea kubaki akicheza na mtandao labda Mungu ana alikuwa na mpango wake katika hili.

“Kamanda, tukushushe Tabora stesheni au kituo cha polisi kati Tabora, maana tumeambiwa tukusikilize wewe” rubani wa helkopta alimweleza Amata

“Itafute treni yenyewe, nataka kushuka kwenye treni” Amata aliwajibu

Helkopta la polisi lilikata anga, kwa kuwa rubani alikuwa analiongoza kuelekea katika makao makuu ya polisi ya mkoa Tabora, ilibaidi abadili uelekeo na kuitafuta treni ile ilipo kwa wakati huo. “Kpteni Scopa, Chopper namba PLS 12 H ova” rubani yule aliongea kwenye chombo maalumu cha kuongelea alichokivaa masikioni mwake

“Tunalipata Kepteni, tupe habari ova” sauti kutoka makao makuu ilimjibu “Tunabadili uelekeo, kadiri ya maelekezo ya Kamanda ova”

“Uelekeo wapi Kepteni?”

“Ameomba tuelekee mahali treni ilipo ili kazi ianze mara moja ova” “Read and clear ova”

“Work in progress” mabadilishano ya taarifa hiyo yalikamilika na kepteni Scopa alimpa ishara msaidizi wake Baba Lao ageuze uelekeo. Chopper lilibinuka upande upande kuelekea magharibi mwa mji wa Tabora ilikuwa yapa saa saba kasoro usiku giza nene lilikuwa limefunika anga.

Kamanda Amata alitoa bastola yake ndogo na kuijaza risasi na magazine iliyobaki aliihifadi vizuri, aliweka vizuri kisu chake na kuvaa soksi zake za mikono tayari kwa kazi, aliicheki saa yake na kuibonyeza kuweka kitu Fulani vizuri, alivaa kofia yake aina ya nyeusi aina ya mzula akatia big G yake mdomoni.

Kepteni Scopa na msaidizi wake walikuwa bize kuliongoza dude hilohuku wakisikiliza muziki wa Les Wanyika walionekana wakiipenda sana kazi yao. Kwa mbali walianza kuiona treni ile ikiendelea kuikata reli kwa kasi ya ajabu ambayo ilimfanya kepteni Scoba kuhofu,

“Kamanda” aliita

“Hii treni ya umeme au?mbona inakimbia namna hii?” aliuliza “Kuma itilafu kwenye Injini naenda kurekebisha” Amata alijibu

“All the Best” Scopa alipokea jibu hilo na kutoa saluti kwa Kamanda Amata Tayari Chopper ya polisi ilikuwa ikienda sambamba na treni hiyo

“Weka Chopper juu ya treni” Amata alitoa amri huku tayari akiwa mlangoni, upepo mkali ulimsumbua macho. Scopa aliipeleka Chopper ile juu, na Kamanda Amata alivizia kuona kasi ile ya treni kama inawiana na Chopper ili aweze kurukia juu yake.

Hekaheka zilendelea katika stesheni ya treni ya Tabora, polisi tayari walikuwa pale usiku ule wakiwa na hasira dhidi ya majambazi hao kwa kuwaumiza wenzao

“Ama zao ama zetu” walisikika wakitamka neno hilo mara kwa mara. Stesheni masta alikaa tu ofisini kwake haelewi kinachoendelea ni jinsi gain ataikoa treni hiyo ambayo sasa ilikuwa inakwenda kwa kasi isiyo ya kawaida tena bila operetta, mara kwa mara alisimama na kukaa chini, aliweka mikono kichwani na kuitoa kisha kuiweka mfukoni, mara alikwenda haja ndogo na kurudi, alishika hiki akashika kile ili mradi tu hali ilikuwa ni mkanganyiko hasa alipofikiria kuwa endapo treni hiyo itapata ajali katika mwendo kama huo ni wangapi watabaki Yatima, wangapi watabaki Wajane na walemavu ndiyo usipime, aliteseka sana moyoni na kila alipopiga simu katika treni hiyo simu haikujibiwa kabisa.

Alitoka nje ya ofisi na kuangalia hekaheka zilizopo hapo nje, waandishi wa habari walishafika, vijana wa msalaba mwekundu walikuwa pale tayari kwa lolote, polisi walitanda kila kona ya stesheni ile wenye mbwa, farasi, acha wale wenye bunduki za aina mbalimbali.

Stesheni masta Bw Nimrod Msigwa alivuta hatua ndogondogo kushuka ngazi za jingo lile la stesheni huku akionekana wazi hajui ni wapi anaenda.

Punde tu RPC wa mkoa wa Tabora aliingia eneo hilo naye kushuhudia kinachotokea baada ya kupata simu toka makao makuu ya Polisi huko Dar es salaam. Alikutana na stesheni masta Bw Nimrod na kusabahiana lakini wote walionekana wakiwa na mawazo mengi walisimama pamoja kimya wakiangalia hekaheka za hapa na pale hakuna aliyemsemesha mwenzie. Mafundi nao walijaribu kurekebisha reli huku wakiimba nyimbo zao.

“Samahani, Bw Nimrod, kwa uzoefu wako unafikiri treni hii itafika hapa saa ngapi?” kamanda wa Polisi wa mkoa Tabora Bw. Sylvester Matinde alimtupia swali Bw Nimrod ili kuvunja ukimya ule “Kawaida ingeingia hapa saa kumi na moja alfajiri ndiyo ratiba ykae lakini kwa jinsi ya hali ilivyo itafika mapema zaidi ila siwezi kujua ni saa ngapi” alijibu

“Sasa kama watu wa reli mnachukua hatua gain kuokoa vifo vitarajiwa?”

“Kama unavyoona mafundi wapo kazini, wanatengeneza njia moja tu ya reli ili kama ikifika hapa basi inyooshe njia na wao watafanya utaratibu wa kuipunguza kasi, wenyewe wanajua kazi yao, usiwaguse” Stesheni masta alimalizia jibu lake.

Kamanda wa polisi aliendele kuongea machache na watu wake na kuwapanga hapa na pale mara nyingi aliwasiliana na vijana wake walioko ndani ya treni hiyo japo kwa taabu kidogo lakini waliendelea kuwasiliana.

Kigali Rwanda

Simu ya mezani iliita usiku huo chumbani kwa Madam Rose, kabla ya kupokea simu hiyo aliangalia saa yake ya ukutani na kugundua kuwa ilikuwa tayari ni saa saba za usiku, alikunja sura kwa kuwa hakupenda kupokea simu mida hiyo…

“Hello!” aliita kwa mapozi kama kawaida yake

“Madam, we are in trouble!” sauti ya upande wa pili iliongea kwa kutweta kama mtu aliyekimbizwa na mbwa wakali.

“What?” Madam Rose aliuliza kwa hasira huku akitoka kitandani kwake na kusimama dirishani akiangalia nje

“Vijana tuliyowapa kazi wameharibu kwa uzembe wao” sauti ile iliendelea “Khaaaa!” alinguruma Madam Rose na kuendelea

“Imekuwaje?” aliuliza

“Amenipigia simu Mandi kuwa wapo kwenye treni ya kwenda Dar, lakini ile memory card imepotea na wanamuhisi msichana mmoja kuwa kaichukua, sasa wameshaingia matatizoni na Polisi. Tutapona?” sauti ile iliongea kwa kukata tama

“Come on!!! Ni wajinga sana, nimewapa tiketi za ndege wawahi Dar, sasa wanapoteza muda, mbona tutaonekana wote hopeless” Madam aling’aka kwa hasira. Sauti ya upande wa pili ilitulia bila kusema kitu

“Frank! Frank!” Madam Rose aliita kwa hasira

“Yes Madam, nakusikia” sauti ile ilijibu

“Unashauri nini katika hili?” Madam aliomba ushauri kwa Frank maana alihisi wazi kuwa endapo watakamatwa basi halihaitakuwa shwari hata kidogo maana wanaijua serekali ya Tanzania jinsi isivyotaka mzaha katika dulu za usalama.

“Madam hakuna jinsi, inabidi tuwaokoe wenzetu ili tuuokoe mpango wetu” Frank alijibu sasa kwa kujiamini

“Ok Frank fanya hivyo halafu tuwasiliane, lakini hawa jamaa ni wapumbavu kabisa. Na ukiwaokoa uwalete hapa moja kwa moja” Madam Rose aliendelea kufoka kwenye simu, alipomaliza aliitupa simu hiyo na yeye mwenyewe kujitupa kitandani kwa hasira.

Frank, alipiga simu kwa vijana wake walioko huko msitu wa Nyakanazi ambao wao wapo tayari kwa lolote na muda wowote, vijana waliochoka maisha ambao kwao kuua haikuwa shida ilikuwa kama chai ya asubuhi tu. Maisha yao waliyajenga huko Biharamuro katika mapori ya Nyakanazi kikubwa ni kuteka mabasi na kupora mali za wasafiri, kila kukicha walipambana na polisi katika shughuli zao hizo lakini hawakukoma kabisa. Katika kimbizanakimbizana hiyo wengine walikimbilia mbali huko sehemu za Nguruk, Kazolamimba mpaka Uvinza, kote wakijifanya wababe kupora mali za wananchi, wengine waliishia jela, wengine waliuawa kwa risasi za polisi au wananchi wenye hasira, lakini wengine walisalimika nakufanya makazi yao katika mapori hayo, hakuna mtu aliyejua wanasubiri nini siku zote hiko, hata wao hawakujua wanachokisubiri ni kipi na kitatokea lini.

Simu ya mmoja wao ilinguruma katika mfuko wa koti lake

“Nani tena usiku huu anapiga au ndiyo wanga wenyewe” aliongea maneno hayo kwa sauti ya kilevi, huku akijipapasa kuitoa mfukoni

“Eee lete maneno mdosi” alimwambia mtu wa upande wa pili

“Ee nakupata mdosi”(…)“Vijana wapo gado kaka, hawana kwere”(…)“Niambie kiongozi”(…) “ok nimekupata, kuwaokoa tu, tunajua kazi yetu vizuri, hii ndiyo rescue mission… tega sikio utapata habari” yule kijana alikata simu na kuwaamsha wenzake.

“Oya Masela, inabidi tufanye rescue, mabradha wametaitiwa kwenye gogo, sasa tuhakikishe tunawatoa hai mwana” aliwaeleza wenzake ambao tayari muda huo walikuwa wameshaanza kukoroma.

“Donge lipo? Sio tunafanya kazi ya kanisa” mmoja wao alimuuliza “Donge lipo we twende kazini” akampajibu.

Vijana wale walinyanyuka na kupotelea msituni, mara walitoka na jeep ya kijeshi wakiwa na zana mbali mbali tayari kutekeleza waliloagizwa, bangi zilikuwa zikifanya kazi muda huo.

Kilometa mia moja na hamsini kabla ya stesheni ya Tabora vijana wale walianza kufungua vyuma vya reli ili kuipoteza njia, wao hawakujali kama wangapi watapoteza maisha ila walichojali wao ni kuwaokoa watu wao watatu tu waliotumwa. Kazi iliendelea kwa nguvu zote kulfungua mataruma hayo.

“Madogo fasta madogo, kaza kaza” kiongozi wao aliwaelekeza vijana wake. Kisha akachukua simu yake na kupiga namba ileile

“Ee mdosi, sasa waambie walengwa wasogee behewa moja kutoka kwenye injini, kwa maana kwenye ajali yoyote ya treni behewa la pili hua halianguki, hapo tutawapata na kutokomea nao” yule kijana alionghea kwenye simu na kutoa hayo maelekezo. Kazi ilikamilika trauma mbili moja ya kushoto na nyingine ya kulia zilishaondolewa, vijana wale walijificha porini umbali kama wa mita mia tano wakiangalia na kusubiri kuona kitachotokea.

Gurudumu mia mbili za chuma ziliendelea kusumbuana na vyuma vigumu vya reli ya Mjerumani usiku ule, kasi ya treni ile haikuwa ya kawaida, watu wote walitulia kimya wakiwa hawajui watafanya nini kila mtu aliomba kwa Mungu wake aepushe balaa hilo, wakati wengine wakiwa katika maombi lakini wengine walikuwa hoi bin taabani, afande Kirama alikuwa ameshapoteza fahamu muda mrefu, Koplo Kibona nae alikuwa tayari tayari ameshaitwa jina lingine ‘Marehemu’, Mzee kasimu nae alikwisha iaga dunia baada ya kupigwa vibaya na Mandi pale alipojifanya kuleta ubishi, na mwili wake wakati alipokuwa akianguka alikigonga kinobu cha kuongezea mwendo kasi wa treni hiyo hivyo treni iliendelea kuongeza kasi bila mpangilio. Kengele za hatari zilianza kugonga ndani chumba cha operetta wa treni hiyo, hakuna la kufanya, Polisi aliyeachwa hapo hakujua chochote cha kufanya alibaki aking’aa macho tu.

Mandi aliendelea kujibanza palepale katika moja ya vijichumba vidogo vilivyopo katika injini hiyo, aliendelea kuangalia nyendo zote za askari yule hakuna alichokitaka zaidi ya bunduki yake aina ya SMG. Askari yule alikuwa akitembea hukuna huku na mara nyingi alikuwa akikaa kwenye kile kiti kirefu cha operetta akitazama huko treni hiyo iendako. Mandi alitoka katika maficho yake na polepole alianza kunyata kumfuata askari yule pale alipoketi, kwa kuwa viatu vyake vilikuwa na soli ya mpira hakuweza kusikika katika sakafu ile ya chuma. Yule askari aliketi vile vile kwa utulivu akiwa ameshika bunduki yake lakini alishamuona Mandi kupitia katika kioo cha mbele kilichokuwa kikiangazwa na mwanga hafifu kutoka katika moja ya balbu ndogo iliyopo katika kijichumba fulania katika injini hiyo. Yule askari slijifanya kama anainzia hivi lakini alokuwa akimwangalia Mandi kwa kificho, Mandi alipojiandaa kumvamia akiwa karibu kabisa alijikuta akipigwa kwa kitako cha bunduki, maumivu yalimfanya mandi kuyumba na kujishika paji lake la uso ambalo mpaka hapo lilishavimba kutokana na pigo lile, yule askari alitoka pale katika kile kiti na kurukia chini, kabla Mandi hajatulia alipigwa mateke mawili ya kuzunguka na alipotaka kujiweka sawa alijikuta akipata ngumi za mfurulizo zilizompelekea kwenda chini, damu zilimtoka mdomoni na puani, kwa kasi ya umeme mandi alijinyanyua kisarakasi na kupiga mapigo ya judo yaliyompata yule askari kifuani na kumfanya akohoe kidogo na kutema damu, Mandi alijirusha kwa ufundi na kuzamilia kuuwa lakini askari yule aliepa na migugu ya Mandi ikatua katika dash board ya treni ile mguu mmoja uliinasa kamba ya bunduki nayo ikaanguka chini, mandi alipotaka kuichukua yule askari aliipiga teke ikasogea mbali kidogo, Mandi akatua pale ilipokuwa ile bunduki, alipofika chini tu yule askari bila kuchelewa alimpiga teke lililotua usoni na kumgeuza Mandi kuwa chali, mguu wa pili wa yule askari haukufanya ajizi ulitua kwenye koromeo kwa mtindo ‘kutimba’ Ma ndi aliushika mguu ule na kujaribu kuutoa kutoka katika koromeo lake, kutokana na misuli yenye nguvu ya mikono ya Mandi aliweza kuuondoa mguu ule na

kuuzungusha , maumivu makali yalimpata askari yule akapiga yowe la uchungu na kudondokea upande wa pili. Mandi alijinyanyu na kuifuata ile bunduki kabla hajafika alihisi kupigwa na kitu kama chuma kisogoni, yule askari pale alipodondokea kulikuwa na kasha la vifaa vya ufundi ‘tool box’ alichukua spana na kumrushia Mandi, Mandi aliyumba na kujigonga katika bomba la chumba lililopo ndani ya cabin hiyo.

“Shusha zaidi! Tena, tena, tena. Apo hapo haya ongeza kasi” Kamanda Amata alikuwa akitoa maelekezo kwa kepteni Scoba aliyekuwa akiliongoza chopper lile la kipolisi

“Kisha hakikisha unakuwa mbele ya treni,mbele sana ili kuangalia usalama wa reli kisha nipe taarifa” Kamanda Amata alimuelekeza kepteni Scoba huku akimpa kidude Fulani cha kuongelea ‘walk talk’ na kumpatia nay eye moja akaibana katika mkanda wake wa begi. Amata alitua vizuri kabisa juu ya paa la moja ya mabehewa ya treni hiyo ambayo ilikuwa ikienda kasi sana, alitulia

kidogo kuliacha chopper lile liende, na baada ya hapo alianza kutembea kwa mtindo wa ‘jogging’ kuelekea kati ya behewa na behewa ili apate nafasi ya kuingia ndani.

“Tutoke kwa nje tupande juu ya paa ili kama jamaa wameshahujumu sisi tutapona kwa kurushwa pembeni” Ton alimwambia Jomse ambaye alionekana kutokubaliana na hilo.

“Hatuwezi kuondoka mpaka tuhakikishe tumeipa ile memory card” Jomse alisisitiza “Tutapata hata hatujui ilipo?” Ton aliuliza

“Anayo yule msichana, tumeshamzimisha twende tukaubebe mwili tumpekue kwa utulivu” Jomse alimwambia Ton, lakini Ton alionekana kutoafiki wazo hilo.

“Mandi, hatuna information yoyote toka kwake” Ton alimwambia Jomse

“yule nae bwege, achana nae kama kakamatwa atajua yeye” Jomse alijibu kwa mkato

“Sio hivo Jomse we unafikiri akikamatwa na sisi tutapona? Sote tupo kwenye mission moja lazima tumtafute, atatoa siri akibanwa na polisi.” Ton alimueleza Jomse. Jomse aliona kweli amekosea kutoa jibu lile, akakubaliana na Ton. Mara simu ya Jomse ilipokea meseji ‘Rescue mission imekamilika, nendeni behewa la pili kutoka katika injin haraka’

“Twende” Jomse alimvuta Ton, na wote kwa mwendo wa kunyata walitoka katika maficho yao na kuelekea huko walikoagizwa kwa tahadhari kubwa. Jomse alipendekeza wapite kwa nje, Ton mara hii akaafiki, kwa kutumia dirisha moja walifanikiwa kutoka na kupanda juu ya paa wakiwa na nia ya kutembea juu ya paa mpaka behewa la pili lakini pia ikiwa ni moja ya kuwakwepa Polisi ambao bado walikuwa wakipekua behewa moja baada ya jingine.

Amata ga Imba kwa kutumia upenyo kati ya behewa la usalama na la abiria aliteremka taratibu katika maungio hayo na kukanyaga sawia panapotakiwa, moja kwa moja aliingia behewa la polisi kwanza

“Simama apo hapo ulipo” Polisi mmoja mwenye short gun mkononi alimuamuru Amata, bila kupinga Amata alinyanyua mikono yake juu. Kutokana na hali iliyogubika katika treni hiyo Amata alijua wazi akileta mchezo atafyatuliwa maana polisi walishaona kila mtu sasa ni adui kwao. “Samahani nimekuvamia” huku akitoa kitambulisho ambacho mara nyingihuwa akioneshi ovyo. “Samahani Kamanda!” askari yule aliomba msamaha na kutoa salute ya kiukakamavu. Amata aliuangalia mwili wa afande Kibona uliokuwa umelazwa kwenye machela na kufunikwa kwa shuka maalum kwa kazi hiyo, kisha akamwangali afande Kirama ambaye alionekana kupoteza fahamu.

Amata alitoa bastola yake na kuiweka vizuri tayari kwa kazi. Alianza kupita behewa moja na jingine akiwa na bastola yake mkononi, mabehewa mawili ya mwanzo yalikuwa tupu akafika behewa la mizigo ambalo lilikuwa na giza, amata alitembea kwa hadhari kubwa sana, taratibu akitazama huku na huko aliweza kuona vizuri kutokana na mawani yake aliyovaa ambayo inamuwezesha kuona gizani. Aliona mtu kalala chini, alipomwangalia vizuri ni msichana, damu nyingi zikimtoka mdomoni na puani, uvimbe ulikuwa katika uso wake, Amata alirudisha bastola yake katika kikoba chake na kuufikia ule mwili kwa haraka, pembeni aliona laptop iliyovunjika vipande, simu iliyokosa betri na mfuniko.

“Isabel…” alijikuta akiita hata kama hakuwa na uhakika kuwa ni yeye, alichukua begi alilolikuta hapo na kutia vile vipande vya laptop na ile simu kisha akjaribu kuangalia hapa na pale katika begi hilo akakuta kitambulisho alipokisoma ndipo alipohakikisha kuwa ni yeye. Akamyanyua kutoka pale chini, haikuwa rahisi kwa maana Isabel alikuwa kibonge kwelikweli, alipomuweka vizuri katika mikono yake alitembea mpaka behewa la usalama na kumuhifadhi vizuri, lile begi nao aliliweka pazuri, akatoa walk talk yake

“Scoba, Scoba!” aliita

“Yes kamanda, tupo mbele sana hali ni shari kamanda”

“Geuza chopper uje haraka behewa la usalama” Amata alimuamuru Scoba

“Nimekusoma Kamanda”. Scoba aligeuza chopper na kurudi, haikuchukua muda walikuwa tayari wameifikia treni hiyo. Kupitia dirishani alimuelekeza Scoba kushusha chopper ile mpaka mlangoni, kwa kushirikiana na yule askari mmoja walihamisha mwili wa koplo Kibona kuuweka katika chopper, kisha afande Kirama na Isabel, kazi haikuwa rahisi sana kwa kuwa vyombo vyote

vilikuwa katika kasi kubwa lakini kwa kusaidiana walikamilisha zoezi hilo. Amata alipiga salute kwa Scoba kuonesha shukrani na Scoba aliondoa chopper kuwawahisha hospitalini Tabora.

Amata pamoja na askari aliyebaki walianza safari ya kwenda behewa na behewa, behewa nne za mwanzo zilikuwa tupu, kwa sababu Koplo Kibona marehemu aliwaamuru abiria kukaa sehemu moja ili kuweza kufanya ukaguzi kuwapata wauwaji.

Zoezi lilikamilika lakini hakuna aliyeshukiwa kuwa na hatia hiyo, hata wale waliohisiwa nao waliachiwa kutokana na kuwa hakukuwa na ushahidi uliokamilika. Abiri waliruyhusiwa kurudi mabehewa ya nyuma ili kutoa na nafasi kwa operesheni hiyo kwenda mabehewa ya mbele.

Jomse na Ton walilala juu ya paa la behewa la kwanza wakisubiri kitachotokea kama walivyoamuriwa, walimtumia meseji Mandi ili kama yupo hai afanye mchakato kama huo. Mandi alikuwa hoi baada ya kupambana na polisi yule ambaye sasa aliwekwa chini ya ulinzi wake. “Simama juu!” yule askari alimuamuru Mandi kisha akaendelea

“Ongoza njia twende”

Mandi akiwa mikono kichwani aliongoza njia kuelekea kwenye mabehewa mengine huku nyuma yake akifuatiwa na yule askari baada ya behewa moja kulipita walipofika behewa la pili mbele yao kulikuwa na askari wawili wakija upande huo. Mandi aliona sasa amekwisha hana jinsi iliyobaki ni kujitetea awezavyo, alishusha mikono na kugeuka kwa kasi, kwa pigo moja tu alilompa yule askari alifanikiwa kuipata bunduki ile na kuiweka sawa kwa mashambulizi, kabla hajafanya lolote aliona kitu kama jinamizi likipita juu kwa kukanyaga mabega ya askari wale, pigo moja la usoni lilimpepesua Mandi na bunduki ikamtoka mikononi, Mandi alijiinua kwa ustadi na kusimama wima kumkabili Amata ambaye alikuja hapo kama mzimu, Mandi alipiga kareti ambazo Amata alizipangua kwa ufundi sana, Mandi akaona hapa anapambana na mjuzi. Alipiga pigo lilingine na Anata alimkata vizuri na kumtwanga kichwa ambacho kilimtonesha ile nundu yake Mandi alijitoa katika mikono ya Amata akarusha ngumi ambayo Amata aliiona na kuikwepa kisha kutumi viganja vya mikono yake alimsukuma nyuma na kumrukia teke la kichwani lililompepesua na kumpeleka chini, alijigonga vibaya kwenye meza iliyopo hapo

“Mkamate tia pingu” Amata aliamuru

Kabla hawajamfikia Mandi alijinyanyua na kujirusha nje kupitia dirishani, Amata alitikisa kichwa na wote wakakimbilia dirishani kuangalia. Mandi alinasa kidogo mguu na hivyo kupoteza uwelekeo, alijipiga katika ubavu wa behewa na alipochomoka tayari gurudumu za chuma zilishadaka mikono kilichofuatia ni kifo kibaya cha kukanyagwa na treni, mwili wake ulisambaratika huku na huko.

“Amejichagulia kifo chake, muache aende” Amata aliwaambia wale polisi.

Amata na wale polisi walifika kwenye injini lakini hawakuweza kuona cha kufanya, Amata alipojaribu kuchezea ile nobu ya kupunguza kasi alikuta imejam haifanya kazi tena.

“Oya, mchuma umekufa huo hauwezi kusimama wala kupungua kasi, cha kufanya tuokoe ndugu zetu” Amata aliwaeleza wale polisi,

“Kivipi kamanda?” mmoja wa wale askari aliuliza

“Tutenganishe mabehewa kutoka katika injini” Amata aliwapa mbinu

Kwa kuwa wao walikuwa behewa la pili kutoka injini na behewa la kwanza halikuwa na mtu hivyo wakaanza kusaidiana kutenganisha behewa la pili kutoka injini, kazi haikuwa rahisi maana wote hawakujua mabehewa hayo yaliunganishwa vipi, walijitahidi kufyatua hiki na kile wakianza na mipira ya upepo na nyanya za umeme.

“Jamani hivi humu hakuna Tiitii?” Amata aliuliza

“Maana wao wangeweza kutusaidia” Amata aliongeza kusema. Kazi iliendelea kutenganisha kiungio kile, jasho liliwatoka wanaume wale lakini walishindwa, wakiwa wamekaa upande wa behewa la tatu, Amata alishikwa na hasira na kukanyaga kwa nguvu chuma kimoja kilichokua hapo katika maungio, mara aliona behewa lile likijiachia, cheche za moto kidogo zikatawanyika huku na huko lakini walishuhudia injini na behewa moja vikienda peke yake, na mabehewa yaliyobaki yalifuata kwa kasi ileile, Amata na wa le polisi walibaki kuangalia nini kitachotokea.

Kikao cha dharula kiliitishwa katika ofisi ya waziri wa ulinzi eneo la Msasani makao makuu ya JKT. Kikao hicho kiliwakutanisha watu wachache usiku ule, waziri wa ulinzi mwenyewe, madam S akiwa ndiyo top wa idara ya TSA, na IGP.

“Unajua tatizo lenyewe jinsi alivyoeleza Kamanda Amata bado halijawa wazi, anasema aliyumiwa ujumbe wa facebook na mwanamke usiku ule na katika mabishano yao alifanikiwa kupata namba ya simu na kumpigia ndipo aliposikia kilio cha msichana na sauti iliyomlazimisha kutoa kitu Fulani, kasha mirindimo ya risasi ikasikika.” Madam S aliueleza mkutano huo

“Mi nilipiga simu kwa kamanda wa polisi Tabora na akathibitisha kuwa kapokea simu toka kwenye treni kuwa kuna mauaji yanaendelea na kijana wetu mmoja ana hali mbaya baada ya kupigwa risasi na hao majambazi.” IGP aliongeza

“Sasa hao majambazi wanataka nini kwa huyo mwanamke? Mi nafikiri hili swala tuwaachie polisi washughulike kabla hatujaamua kuingiza nguvu kubwa japokuwa tumeshaanza kufanya hivyo”

Waziri alitoa rai

“Hebu ngoja tupate mrejesho kutoka Tabora baada ya Amata kukamilisha uchunguzi wake halafu tutawasiliana” Madam S alishauri.

Mazungumzo mawili matatu yaliendelea juu ya usalama wa nchi lakini bado walikuwa na kitendawili cha ni nini kilichotoke katika treni hiyo hata mawasiliano yaende kwa Amata moja kwa moja, lilikuwa ni kama wingu zito kati yao ambalo hakuna hata upepo wa kuliondoa. Waziri wa ulinzi mara ashike hiki mara kile hakujua afanye nini

“Sasa ni nini kinaendelea? Kwa nini treni hiyo isizuiwe?” Waziri aliuliza

“Mheshimiwa, kwa taarifa tulizo nazo operetta wa treni hiyo ameuawa kwa hiyo hakuna anayeweza kulimudu, hivyo linakwenda tu” IGP alimjibu Mh waziri.

“Ha! Endapo litapata ajali si mamia watakufa… mama yangu!” Mh waziri alishtushwa na taarifa hiyo na alionekana wazi kabisa kuchanganyikiwa bila kuficha. Kimya kilitawala katika mkutano huo na kila mmoja alikuwa anawaza lake na hakujua nini mwenzake anachofikiria. Madam S alikuwa wa kwanza kuvunja ukimya huo kwa kujikohoza kidogo

“Kwa nini tusiwasiliane na mkuu wa polisi Tabora kujua kinachoendelea?”

“Kwa ujumla amesema yupo pale stesheni Tabora pamoja na stesheni masta hawana la kufanya kwa sasa ila tu kuna wale mafundi wa reli ndiyo wanatengeneza njia ili kama ikifika hapo isilete maafa zaidi” IGP alitoa jibu

“Hiki ni kitendawili kikubwa, wananchi watakufa mamia kwa mamia, Yesu wangu!” Mh waziri alisikitikia hali hiyo na kutoa maagizo

“Hebu mwambie mkuu wa polisi Tabora ahakikishe anafanya lolote kuokoa maisha ya watu” Waziri alitoa ombi. Madam S katika kiti chake cha kuzungukazunguka alikuwa hana shaka sana

“Tusubiri kitachotokea, naamini Kamanda Amata atafanya kazi, na roho za watu zitapona tu”

Madam S aliyasema hayo huku akichezea kalamu yake kwa mikono yake miwili “Madam S, una uhakika Kamanda atafanya kitu?” Waziri aliliza

“Naamini kwa asilimia tisini na tisa mheshimiwa, ndiyo maana sina wasiwasi na hilo” Madam S alijibu kwa kujiamini kabisa.

“Ok basi fuatilieni tukio hilo hatua kwa hatua mnijulishe, na asubuhi tuondoke wote kwenda Tabora” Waziri alimaliza na kufunga kikao hiko cha dharula.

ITAENDELEA

Isabel Ndani ya Mpango Hasi Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment