Julai Saba Sehemu ya Tano
KIJASUSI

Ep 05: Julai Saba

SIMULIZI Julai Saba
Julai Saba Sehemu ya Tano

IMEANDIKWA NA: RICHARD MWAMBE

*********************************************************************************

Simulizi: Julai Saba

Sehemu ya Tano (5)

Baada ya kikao cha Scolleti na watu wake kukamilika, Scolleti alibaki peke yake katika ofisi hizo za FK Security Group, alipohakikisha kila kitu kipo sawa na hakuna mtu mwingine mle ndani, akabonya kitufe Fulani kilichofichwa ukutani nyuma ya kalenda, mara mlango mkubwa ukafunguka kwa chini na ngazi ndefu zikaonekana zikishuka, akateremka taratibu na ule mlango ukajifunga nyuma yake. Akalegeza tai yake na kuvuta suitcase yake iliyokuwa kitandani, akapekuwa ndani na kukuta kila anachokihitaji kipo sawa, akapekua hapa na pale na kuweka sawa hati mbalimbali ikiwemo ya kusafiria, tiketi ya ndege iliyokuwa iondoke saa mbili asubuhi ya julai saba kuelekea Nairobi kwa kikao kingine na hao watu wake wa Freedom Fighters. Akafunga mkoba huo na kuingia maliwato, akajiswafi na kutoka nusu saa baadae. Alipohakikisha yuko kamili akaburuza hiulo sanduku lake na kutoka njea kwa mlango mwingine. Kelele za majogoo zilikuwa tayari zikipasua anga kuashiria kuwa kumekucha.

Saa kumi na moja alfajiri, Scolleti alishika kitasa cha mlangowa gari yake aina ya Land Cruiser VX, akapakia sanduku lake na kisha yeye mwenyewe kuingia mlango wa dereva. Akaketi tayari kwa kuondoka, mara akahisi kitu baridi kikimgusa nyuma ya shingo yake.

“Tulia, fuata maelekezo ninayokwambia, washa gari na utoke nje ya eneo hili,” ilikuwa sauti nya kike iliyopenya masikio ya Scolleti, haikuwa sauti ngeni. Akawasha gari na kutoka getini akifunguliwa na walinzi kisha akafuata barabara hiyo mpaka katika barabara kubwa ya Bagamoyo karibu kabisa na mataa ya Morocco. Yule mwanamke akamuamuru kufuata barabara ya kwenda Mwenge naye akafanya hivyo, alipoingia tu barabara kubwa kuelekea Mwenge na muda huohuo Kamanda Amata alikuwa akiwasili eneo hilo, akapiga kona kali na pikipiki lake na kuanza kuifuata ile VX kwa maana alikuwa anaifahamu sana. Aliifuata taratibu mpaka maeneo ya Tangi bovu ile VX ikasimama pembeni. Akateremka akiwa mikono yake iko kichwani.

ShaSha nae akateremka chini akiwa kamnyoshea bastola Scolleti.

“Kila kona watu wanalalamika juu yako, nimetumwa kwa jambo moja tu, serikali yako ya India imekuchoka, imechoka kulalamikiwa na nchi rafiki hata kupelekea kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kwa ajili yako haya yote,” ShaSha aliongea kwa lugha ya Kihindi, Kamanda Amata na Gina walisimama kwa tahadhari nyuma kidogo ya nguzo kubwa ya chuma iliyobeba tangazo kubwa la Safari Lagera, alikuwa akisikia wanachokiongea alikuwa akielewa kidogo lugha hiyo.

“Siko tayari kurudi India,” Scolleti alijibu.

“Swala sio kurudi India, kwanza hakuna anayekutaka kule, hata mimi nimetumwa kuchukua nafasi ya Israel ambaye anachelewa kuja kwako kutimiza kazi yake, nimetumwa kukuua,” ShaSha aliongea kwa uchungu. Scolleti aliposikia swala la kuuawa akashusha mikono yake na kugeuka mzima mzima na kutazamana na domo la bunduki ya mwanamke huyo.

“We msichana, wenzako hawakuwa wajinga kukutuma, ni kwa sababu ya kimbelekimbele chako tu, nani hapa duniani mwenye uwezo wa kupambana au kumkamata au kumuua Scolleti? Kwa taarifa yako ni Mungu tu, na hata huyo Mungu mpaka leo anajishauri anianzie wapi,” Scolleti aliongea kwa kujiamini huku mikono yake kajishika kiunoni.

“Unajiamini sio?” ShaSha akauliza.

“Sio najiamini, ila nataka nikwambie kitu ambacho wewe hukijui, sikiliza, wewe na serikali ya Tanzania nani mwenye uwezo wa kunikamata? Kama wao wamenipokea na kila mwezi nawapa pesa nzuri iliyotakata viongozi nao wananihifadhi ujue wazi utafia hapa. Kila mtu atakushangaa kusikia umeniua, Watanzania watakushangaa sana na kukupiga mawe,” akasonya, “Toa kibunduki chako hapa,” akaipiga kwa kofi ile bunduki ya ShaSha nayo ikatoka mkononi na kuanguka chini, alipotaka kuiokota tu Scolleti akawa tayari na bastola mkononi.

“No no no no, usijaribu hilo kabisa,” Scoleti alimwambia ShaSha huku akimuelekezea bastola kubwa lenye nguvu, revolver, kichwani mwake, “Kama unataka utajiri we sema, nitakupa pesa na si kunifatafata mimi, mi sifuatwifuatwi namna hii, unanidhalilisha, sasa kwa taarifa yako mimi sikamatiki, na kila anayeifuata harufu yangu lazima nimmalize kama nitakavyokufanya wewe, polisi wengi na wapelelezi wan chi hii na nyinginezo wametajirikakwa pesa zangu, mimi ndio Scolleti Shang’harandha, nakuua halafu ukawaambie kuzimu kuwa chini yaofisi yangu kuna ghala kubwa la silaha za kisasa, sawa?” Scolleti alipomaliza kusema hayo. Aliondoa usalama wa bastola yake, kidole kwenye kifyatulio akakikunja huku akibana meno, ShaSha akajishika kichwani kwa mikono yote miwili akijua kuwa sasa nay eye siku yake imekwisha.

“Aaaaaaaiiiiggghhhh!!!!” Scolleti alitoa ukelele wa uchungu huku ile bunduki yake ikimtoka mkononi, na mkono wa kushoto akijishika kiganja cha ule mkono ulioshika bunduki, damu zikitiririka. ShaSha aliiwahi ile bunduki yake pale chini na kuiweka tayari kutekeleza lile alilotumwa.

“Nani alikwambia kuwa serikali hii inakuogopa?” Ilikuwa ni sauti ya Kamanda Amata akisogea taratibu pale aliposimama Scolleti, “Unajifanya unatoa misaada ya kibinadamu kumbe nyuma yake unafanya maovu makubwa ya kumuangamiza binadamu huyohuyo, sasa leo ndiyo mwisho wa yote haya.”

Kabla Amata hajamalizia kauli yake, ShaSha aliyekuwa sasa hataki kupoteza nukta, alifumua kifua cha Scolleti kwa risasi tatu, bwanyenye huyo akajibwaga chini kwenye vumbi.

“Go Bastard !” (nenda mwanaharamu ), ShaSha aliishusha bunduki yake huku akihema kwa hasira, kisha akageuka na kumtazama Kamanda Amata.

“Sorry Kamanda, najua, labda ulimtaka akiwa hai, lakini nimetimiza nililotumwa, na wakuu wangu wa kazi watapenda kuona picha za mwili huu leo hii ukiwa hauna uhai, lakini asante sana kwa kuniokoa”. ShaSha alimwambia Kamanda huku akimwendea na kumkumbatia kwa nguvu, akampa busu la ulimi. Gina kutoka pale alipo alisonya na kuita “Kamanda!”. ShaSha na Kamanda wakageuka, na kuachana.

“Gina, huyu ni ShaSha, detective kutoka India,” kisha akamgeukia Gina na kumtambulisha kwa ShaSha.

Baada ya kupiga picha kadhaa kwa kamera yake ndogo wakasaidiana na kuupakia ule mwili katika buti la ile VX kisha Kamanda Amata akapiga namba ya dharula, 112, na kuwataarifu polisi juu ya mauaji hayo akijitambulisha kama raia mwema.

Juu ya pikipiki moja wote watatu walitosha na kuondoka eneo hilo. Tayari muda huo watu walianza kutoka majumbani mwao na kuanza shughuli mbalimbali, saa kumi na mbili asubuhi.

§§§§§

9

Pambazuko la

Julai 7

MADAM S alitulia kando ya dirisha lake la ofisini, ilikuwa ni saa moja imepita tangu aingie ofisini asubuhi hiyo, hakujisikia kufanya lolote siku hiyo, mawazo na akili yake yote vilisimama, kwa ujumla alikuwa ni mtu wa mawazo mengi sana. Aliitazama saa yake na kuona bado dakika tisini Yule gaidi aachiwe huru kutoka gerezani. Akainua simu yake na kumpigia kijana wake.

“Chiba, naomba uwe unanipa taarifa yoyote ya kinachoendelea hapo Ukonga mi sijisikii kuja huko kisha tuonane hapa mchana wa leo,” akakata simu. Akabonya namba nyingine na kuweka sikioni.

“Kamanda Amata, saa nne kamili Jegan Grashan anaachiwa huru..” kabla hajamaliza kusema sauti ya Amata iliikata ile ya Madam S.

“Sikiliza Madam! Kwanini tunakuwa waoga hivi, kazi ya kukimaliza kikundi chao inawezekana kabla ya hiyo saa nne, kwa nini mnamuachia mtu ambaye amedhulumu maisha ya binadamu wengi duniani, sikubaliani na ninyi, mkimuachia najua nitachofanya lakini Grasha hawezi kuiacha hii ardhi ya Tanzania akiwa hai,” Kamanda akakata simu.

Madam S alishusha pumzi ndefu na kurudi katika kiti chake akajitupa na kuchukua kitambaa cha kufutia jasho akajifuta uso wake.

Kwa ujumla Madam S alikuwa amechanganyikiwa, hajuila kufanya, mara simuyake ikaita tena, ilikuwa nisimu ya Kamanda Amata, akaitazama na kisha akaipokea mara moja.

“Madam, hao jamaa mnaotaka kumuachia ndugu yao, wametega bomu kama si mabomu katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere pale Sabasaba, taarifa hiyo nimeipata kutoka katika tafutishizangu zausiku wa leo. Naomba kwa amri yako ulishughulikie hilo haraka sana kabla Watanzania wengine hawajapoteza maisha,” kamanda Amata alimwambia Madam S kisha akakata simu na kuizima kabisa.

Madam S, alikiona kiti cha moto, kila alipopiga simu kwa Kamanda Amata haikupatikana, mara alijishika kichwa mara akaijisjika kiuno, aliliendea dirisha kubwa lililo katika ofisi yake linaloangalia barabara kubwa, akatfakari, na kuitaza kalenda yake ya ukutani, Julai 7 iliipamba kurasa ya mbele, siku hiyo ambayo ni mapumziko ya kitaifa Tanzania ilikuwa ni siku ya ufunguzi rasmi wa maonesho ya saba saba, maonesho ya kimataifa ya biashara ambayo hujumuisha makampuni makubwa kutoka mataifa mbalimbali, aliwasha luninga yake na kukuta matangazo ya moja kwa moja kutoka katika uwanja huo wa Mwl Nyerere. Mamia kama si maelfu ya Watanzania walikuwa wakizidi kumiminika ndani ya uwanja huo.

Madam S akakurupuka kutoka katika mawazo ambayo yalimchelewesha kutoa maamuzi, akainua simu na kupiga moja kwa moja kambi ya jeshi la Mgulani na kuwapa hiyo taarifa na kuwaomba wasiipuze.

UWANJA WA MAONESHO SABASABA

Saa 2:57 asubuhi

MUDA HUO kila aliye nyumbani alikuwa akitoka kama sin a familia yake basin a marafiki kwenda kujionea bidhaa mbalimbali zinazooneshwa huko katika viwanja vya sabasaba. Tarehe saba mwezi wa saba daima ni siku ya mapumziko kwa wafanyakazi wa kila aina hapa nchini isipokuwa tu wale wenye idara nyeti.

Mambo mengi sana yalikuwa huko kama vinywaji, vitafunwa, bendi mbalimbali za muziki zikitumbuiza katika mabanda mbalimbali ya biashara, michezo ya watoto kama mabembea, treni ndogo ambayo inakuzungusha kuona mandhari ya uwanja huo na kadhalika. Mistari mirefu ya Watanzania ilikuwa ikisubiri kuingia ndani ya uwanja huo asubuhi hiyo, kila mtu alitaka kuwahi kuingia ili akaitumie pesa yake vizuri, ilikuwa ni kawaida kwa kila mwaka kuwapo na tukio hilo. Polisi wenye farasi na mbwa walizagaa tayari kwa lolote maana penye wengi pana mengi.

Siku hii ikuwa mheshimiwa waziri mkuu wan chi aje kutembelea maonesho hayo, hivyo ulinzi uliimarishwa kila kona.

Katika moja ya mabanda yaliyomo humo ndani hili lilionekana kuvutia wengi sana, watu walikuwa wakijazana kuangalia umahiri wa vijana aliokuwa wakionesha katika kukabiliana na majanga ya moto na mambo ya uokoaji. Wakiwa wamevaa maguo yao ya kiung’aa ambayo hayashiki moto, kila mtu alipenda kwenda hapo kujifunza juu ya kujikinga na kuukabili moto, moto na athari zake, aina za moto na jinsi gani ya kumsaidia mtu aliyepatwa ajali ya moto. Kutokana na hilo kila mtu alisogelea banda hilo hilo kuangalia na kujifunza.

§§§§§

Ngrrrrrrrrrrrrrrrr ngrrrrrrrrrrrrrrr, simu iliita kwa fujo katika moja ya ofisi za jeshi Mgulani. Huyu bwana aliyekuwa katika chumba cha mawasiliano alikuwa amesinzia hata hakusikia kelele zote hizo za simu hiyo ya kizamani ambayo ikiunguruma lazima uzibe masikio kwa kelel zake. Akakurupuka kama aliyetoka kufumaniwa, akainyakuwa na kuiweka sikioni.

“Hallo, hapa ni kikosi cha jeshi Mgulani, nikusaidie nini?” aliongea askari Yule.

“Unaongea na idara ya usalama wa taifa, naweza kuongea na mkuu wa kambi?” sauti ya madam S iliunguruma katika chombo hicho. Yule askari akatulia kwa pozi na taharuki, kisha akajibu, “Subiri na usikate simu tafadhali,” alijibu.

Baada ya sekunde chache Madam S aliunganishwa na mkuu wa kambi hiyo, kambi ya Generali Twalipo, taarifa ya tetesi za bomu ilimfikia mkuu huyo, Meja Jenerali Kisanga, naye akapeleka taarifa panapohusika, muda huohuo wakapewa taarifa wataalamu wa milipuko wa jeshi, wakajiandaa na kila kitu kinachohitajika wakaingia kwenye jeep takribani tatu za kijeshi, safari fupi ya kufika eneo hilo ikawadia.

Kila mtu alishangaa katika ule uwanja wa maonesho, wanajeshi kama thelethini wakiwa na vifaa vya ajabu waliteremka na kusimamaisha zoezi la watu kuingia ndani ya uwanja huo, kisha kutoa taarifa kwa wanausalama waliopo humo ndani kuanza kutoa watu wote waliomo ndani ili uwanja huo ubaki mweupe yaani bila watu. Kiongozi wa oparesheni hiyo alitoa amri mara moja watu wote kutolewa nje, msafara wa waziri mkuu ukasitishwa kutoka nyumbani kwake kwenda katika viwanja hivyo, hali ikawa tete, milango ya kuingilia uwanja huo haikuwa ikitosha kutokea, kila mtu alifikiri kuokoa maisha yake.

Wanajeshi waliokuwa na vifaa mikononi vya kuweza kutambua milipuko waliingia ndani ya uwanja huo na kutembea kila mahali kutafuta uwezekano wa kuwepo aina yoyite ya mlipuko.

Counter-IED kifaa maalumu kwa kazi hiyo kinachofanya kazi peke yake bila kushikwa na mtu kilitumwa kuingia katioka uwanja huo, kilikuwa kikitembea barabarani taratibu kikisimama hapa na pale, huku wanajeshi wengine wakitapakaa sehemu mbalimbali. Bado watu walikuwa wakiendelea kutoka katika uwanja huo, ilikuwa ni patashika kweliweli.

GEREZA LA UKONGA

Saa 09:00 asubuhi

GARI za ofisi ya ubalozi wa nchi ya Jegan Grashan ziliingia katika geti la Magereza lililoko upande wa kaskazini mwa ngome hiyo, zikajivuta taratibu kuelekea lango kuu la gereza mpaka kwenye maegesho. Waandishi wa habari kama kawaida walikuwa hapo wakitaka kushuhudia na kupiga picha za gaidi huyo ambaye siku hiyo alikuwa akiachiwa huru. Askari wa KM wa Magereza walikuwepo kulinda usalama kama kuna hatari yoyote itakayotokea.

Kamishna wa magereza, mkuu wa magereza mkoa wa Dar es salaam na wahusika wengine walikutana kwenye chumba maalumu kwa ajili ya kukabidhiana mfungwa huyo. Maofisa wa ubalozi walikuwa pale tayari kumchukua raia wao. Ilikuwa utata mtupu. Jegan Grashan aliletwa ndani ya chumba hicho akiwa na pingu pamoja na minyororo miguuni mwake akasimamishwa sehemu ndani ya chumba hicho hicho.

Saa 09:15 asubuhi

Kamanda Amata, alikuwa juu ya pikipiki lake akielekea Ukonga kushuhudia zoezi hilo, Madam S alikuwa akifunga ofisi na hajui aende wapi, ama sabasaba au Ukonga, alikuwa akijishika kichwa kila mara kujiuliza la kufanya, hali ilikuwa sio nzuri kichwani mwake, mama huyu alijiona kwa siku hiyo moja kazeeka ghafla.

Wakati huohuo, freedom fighters walikuwa tayari kwenye sehemu waliopangiana kukutana, lakini walishangaa wawili kati yao walikuwa bado kufika, wakajaribu kupigiana simu ili kujua kulikoni majibu waliyoyapata yalikuwa tata. Maafa, maafa ni hali iliyowakata matumaini ya kumpata mwenzao, mara kidogo wakapata taarifa ya kuuawa kwa Scolleti hapo wakachanganyikiwa, hawakujua wafanye nini. Shailan aliamua kuwapanga vijana wake upya, akawaita hao wote walio katika yadi zile waende haraka katika point ya kukutania ambapo wenzao wote tayari walikuwa kwenye boti maalumu wakisubiri kufuinguliwa kwa ndugu yao, waondoke naye.

Saa 09:30 asubuhi

Madam S anazinduka, anawasha gari kuelekea Ukonga, ilikuwa ni mapumziko hivyo hakukuwa na foleni barabarani, aliendesha kwa kasi gari yake aina ya BMW, ili awahi tukio hilo, alipuuzia simu zote zilizokuwa zikiita, wakati huo. Akili na mawazo yote yalikuwa kuwahi Ukonga.

Kamanda Amata alikuwa tayari kawasili eneo la tukio, akaegesha pikipiki lake nje ya wigo na kutulia usawa kabisa wa lango kuu, akitenganishwa na barabara ya Pugu na seng’enge iliyolinda gereza hilo, alimuona Madam Salipokuwa akiingia getini na gari yake, Kamanda akatikisa kichwa kuashiria, ‘kazi imeamka’.

Kichwani mwake Kamanda alikuwa na mambo mengi lakini alishindwa afanye nini, Sabasaba aliamini kabisa kuwa JW watakamilisha hiyo kazi ya kuutafuta huo mlipuko, lakini magaidi wengine walikuwa wametoroka na mpaka hapo hakujua wamekwenda wapi, alikuwa akisubiri milipuko aliypitengeneza katika yadi zile ifanye kazi, lakini zaidi alikuwa akitaka kumuona huyo Jegan Grashan akiachiwa huru, akabaki juu ya pikipiki lake huku akili ikiwa imesawajika, haijui jema wala baya.

§§§§§

SHAILAN aliinua mkono wake kutaza saa yake aina ya casio, tayari muda ulikuwa ukiyoyoma, alikuwa akisubiri taarifa ya kutoka kwa Tashrini aliyekuwa pale gerezani, ili awaambie tu kuwa ndugu yao kaachiwa nao waanze sherehe kwa kufungua champagne.

Yote yalikuwa sambamba, vijana wa JW wakati huo kijasho kikiwatoka kusaka huo mlipuko walioambiwa lakini bado walikuwa hawajang’amua chochote, walianza kukata tama, wakisema hakuna mlipuko wowote kwani kila mahali ni salama kabisa, walitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya usalama. Na wao kujipanga kuondoka kurudi kambini.

Chiba na Gina walikuwa wakielekea uwanja wa maonesho ya sabasaba kushuhudia hali ilivyo, wakapata taarifa hiyo ya kuwa kila kitu kiko salama.

“Hapana Chiba, kuna mlipuko kule umewekwa, naamini kabisa, kwa maana walipokuwa wanautengeneza nilisiki amazungumzo yao!” Gina aliongea kwa jazba huku akipigapiga dashboard ya gari ya Chiba.

“Basi mama utavunja gari yangu wakati hata mkopo benki sijamaliza,” Chaba akajibu kwa utani.

Mara Chiba akaitoa gari yake baranbarani na kuiweka pembeni alipokuwa maeneo ya polisi ufundi.

“Vipi?” Gina aliuliza.

“Kuna mawimbi ya kielektroniki ya kigeni kabisa yamepita kwenya kompyuta yangu,” akafungua dashboard ya gari kwa kubonyeza mahali Fulani, kulikuwa na kijikompyuta kidogo, akaingiza nywila zake nayo ikaanza kufanya kazi, akabonya hapa na pale, akaanza kusikia mawimbi mbalimbali ya sauti, huku yakiwa yanajichora kwa mistari ya kuyumbayumba lakini pia yalikuwa yakifanya sauti Fulani. Chiba alijaribu kuiweka sawa sauti hiyo ili aweze kupata tafsiri ya mionzi hiyo, akajaribu na kujaribu lakini ilikuwa ngumu kuigundua kirahisi, akapima umbali inapotoka na inapokwenda kwa kutumia namba maalumu anazojua mwenyewe.

“Gina, kuna hapa kuna kitu hakiendi sawa, nikizungusha antenna yangu, inaniambia kuna mawimbi mapya na mageni yanatokea mashariki kuelekea, range yake sio mbali sana,” Chiba alikuwa akituamia chombo maalumu kilichofungwa katika gari yake, chombo kinachojulikana kwa jina ‘MiniGRAIL’ kinachoweza kunasa mawimbi yoyote ya kielektroniki yanayopita hewani. Chiba akachuku laptop yake yenye nguvu, akapachika vifaa maalumu vya kusikilizia, kisha akamwambia Gina aendeshe gari kuelekea uwanja wa sabasaba.

Saa 09:45 asubuhi

“Jegan Grashan, uliyefungwa kwa tuhuma za ugaidi katika ofisi za balozi ya Marekani, unaachiwa huru na serikali ya Tanzania kwa tamko la Rais wan chi, kuanzia saa nne kamili leo hii utakuwa raia huru. Pamoja nahayo, serikali inakutaka kuondoka nchini ndani ya masaa 12 kwa njia yoyote, na hutakiwi kukanyaga tena ardhi ya Tanzania, iwe wewe, mkeo au watoto wako, imesainiwa jana tarehe 6 Julai na kugongwa mhuri wa Ikulu.” Hati hiyo ‘removal’ ilisomwa na kamishna wa MagerezaTanzania huku akitetemeka, alipomaliza, alimtaka Jegan kusaini mahali Fulani, akafanya hivyo kisha nay eye akasaini pale panapomstahili, wakapeana mikono na zoezi hilo likakamilika, Jegana akatakiwa kuketi chini kusubiri saa nne kamili ili atoke nje ya gereza.

Madam S aliyefika kwa kuchelewa kidogo, alikuta ndiyo wakisoma hiyo hati kutoka Ikulu, akatulia na kushuhudia huyo jamaa akimwaga wino wa kuondoka kama raia huru. Ijapokuwa ilimuuma lakini hakuwa na jinsi, ikishaandikwa na Rais basi haiwezi kubadilika labda abadili yeye mwenyewe.

Japokuwa siku hiyo ilikuwa ni mapumziko lakini pia ilikuwa siku ya maombolezo ya watu waliopoteza maisha kwenye pantone eneo la Kivukoni siku iliyotangulia.

§§§§§

Gina aliegesha gari nje ya uwanja wa maonesho ya biashara ‘sabasaba’ Chiba akashuka na kompyuta yake akawa akieelekea ndani ya uwanja huo. Moja kwa moja akiongozana na Gina walifika kwenye banda kubwa la maonesho, banda la zimamoto, liliandikwa kwa nakshi nzuri, FK SECURITY and FIRE BRIGADE, banda hilo lilijawa na watu kama mwanzo wakiangalia hayo maonesho ya uokoaji. Chiba alipofika eneo hilo, akaingia ndani ya ofisi kubwa iliwekwa vitu mbalimbali, sasa akagundua kuwa yale mawimbi aliyoyanasa yanaishia hapo kati banda hilo. Akavua makorokoro yake na kuyaweka mezani akachukua simu yake na kubofya namba flani.

“Chiba anaongea,” alizungumza mara tu baada ya simu ile kupokelewa na Madam S,

“Ndio Chiba niambie,” Madam S alimwambia.

“Kuna mawimbi ya kielektroniki nimeyagundua katika mtambo wangu, na nimeyafuatilia sasa nipo hapa uwanja wa sabasaba, nina wasiwasi na banda hili la FK Security maana signal zinaonesha kuwa hapa niliposimama ndio point ziro, nipe mamlaka nifanye kazi inaonekana kuna hatari kubwa sana eneo hili,” Chiba alimaliza. Kila mtu aliyekuwa ndani ya banda hilo alimshangaa Chiba, hakumuelewa ni nini alikuwa akisema.

Madam S, alijikuta akidondokwa na simu mikononi, akiwa kapigwa na bumbuwazi, akili ikamchanganyika, akamtazama Jegan pale kwenye kiti, kisha akaiokota simu yake.

“Fanya lolote kuzuia hali hiyo,” Madam S alijibu, kisha akapiga namba ya Kamanda Amata na kumpa taarifa hiyo, akatoa tena taarifa Jeshini kwa mara nyingine.

§§§§§

Shailan, Shakrum wakiwa ndani ya boti wakimsubiri Jegan, muda wao ulikuwa umefika wa kile wanachokiita ‘kutoa shukrani kwa Watanzania’, Shakrum alifungua briefcase yake kubwa na kuanza kubofya hapa na pale akipanga renji na kila kitu, kisha akawasha kuitafuta sakiti aliyoitengeneza ndani ya tanki la mafuta lakini lililojazwa gesi aina ya methane upande mmoja na mwingine liquefied petroleum gas (LPG), vyote vilikuwa vimeshindiliwa kwa mkandamizo mkubwa sana kiasi kwamba zikidaka moto basi ilo tanki lote lazima ligeuke kombora baya kuliko kombora lenyewe.

Shakrum alipofanikiwa kupata uelekeo wa sakiti hiyo na kuanza kuhesabu muda wa kuiwasha ili itengeneze moto ndani ya tanki hilo, tayari Chiba alikuwa ameyanasa mawimbi hayo, hivyo alichokifanya hapo sasa ilikuwa ni jinsi gani ya kuyakata, ili kusiwe na mawasiliano kati ya vitu hivyo viwili. Chiba akaendele kucheza na kompyuta yake, ilikuwa ngumu kuelewa ni nini anakifanya kwa ni ni namba tu zilizokuwa zikonekana kupishana na katika kioo cheusi cha kompyuta. Kwa kutumia program maalum kwa kazi hiyo ambayo Chiba aliipata wakati akiwa katika mafunzo huko NASA alifanikiwa kuyakamata mawimbi yale na kuyafanya yasitende lililokusudiwa, kisha akaanza kufanya ukaguzi sehemu mbalimbali za jengo lile.

“Oooh shiiit!” Shakrum alionekana wazi kuchanganyikiwa kwa hilo, aligundua kuwa kuna muingiliano wa mawimbi umetokea, kila alipojaribu bado alijikuta anakwama, nywele zikamsimama.

“Washenzi wameyaingilia mawimbi yangu,” akamwambia Shailan.

“Inawezekanaje?” Shailan akauliza.

“Itakuwa kuna mtaalam wa mambo haya ndiye kafanya hili” Shakrum akajibu.

“Sasa tutafanyaje?” Shailana akauliza.

“Hatuna jinsi kama inawezekana hapa ni kufika eneo husika na kutumia mbinu nyingine, mbinu mbadala ya kulipua lile tank bila ya sisi kudhurika,” Shakrum alieleza huku akiisogeza kompyuta byake pembeni, akakizungusha kiti na kugeuka walipo wenzake. Mara simu ya Shailana ikaita, alipoitazama ilikuwa namba ya Tashrini, akajua mambo yameiva, kwa vyovyote vile.

“Ndiyo Tashirini, nipe taarifa,” Shailan alizungumza kwenye simu.

“Jegan yuko huru na sasa anatoka gerezani, nasikia kelele nyingi za wafungwa wengine, zikimsindikiza nje,” Tashrin akajibu.

“Mungu mkubwa, kamwe hamtupi mja wake, hii ndiyo njia pekee ya kuwashinikiza hawa wanaojipendekeza kwa mataifa ya Maghalibi,” Shailan alijibu huku wengine wote wakishangilia.

Saa 04:00 asubuhi – Gereza la Ukonga

JEGAN Grashan aliachiwa huru, hakuwa na pingu za mikono wala za miguuni. Alitembea kwa hatua zake mwenyewe ijapokuwa alikuwa na uchovu kidogo. Madam S na wakuu wengine waliokuwa pale, walimshuhudia gaidi huyo akiondoka taratibu katika gereza hilo, akipita katika mlango mkubwa na kuelekea katika gari la ubalozi lililoandaliwa huku akisindikizwa na maofisa usalama wa ubalozi wa nchi yake, akaingia na kufunga mkanda sawia, akashusha kioo na kumuonesha Madam S alama hya mkono akiashiria kuwa amemtukana tusi baya kabisa, ile gari ikaondoka. Msafara wa gari nne zenye namba za njano kwenye kibao cha kijani zililiacha geti la gereza na kushika barabara ya Nyerere kuelekea mjini.

Kamanda Amata akawasha pikipiki lake na kuvaa kofia yake ya usalama iliyomficha uso wake, moyo wake ulijawa na gadhabu ya kuachiwa huru Jegan, hakupenda hata kidogo. ‘Liwalo na liwe,’ akajisemea na kuaca kati yake na wao magari kama sita hivi kisha akaingia barabara ni na kuondoka.

Uwanja wa maonesho sabasaba

Gina alisikia mlio wa beep kutoka eneo Fulani lililokuwa na matanki makubwa kwa ajili ya maonesho ya kampuni hiyo.

“Chibaaaa!” akamwita kwa ukelele, Chiba akaacha kompyuta yake na kukimbilia kwa Gina, akausikia mlio wa beep hiyo, haraka sana akapanda juu ya tanki moja na kulifungua kwa shida mfuniko wake, ule mlio ulikuwa ukiongezeka. Wakati hayo yakitukia, polisi waliokuwemo uwanjani wakisaidiana na vijana wa skauti kutoa watu nje ya uwanja, na kuwaweka mbali na eneo hilo, vijana wa jeshi walirudishwa tena kuhakikisha usalama huo.

Chiba alikuwa akifungua ule mfuniko kwa tabu maana aulifungwa kwa kifungo maalum, haikuwezekana kukata kwa gesi maana unaweza ukasababisha mlipuko usio wa lazima.

§§§§§

Kamanda Amata akiwa tayari kwenye pikipiki yake aliingia barabara ni, nyuma ya msafara wa gari zilizombeba Jegan, kichwa chake kilishatawaliwa na gadhabu mbaya juu ya mtu huyo, hakuamini kabisa kuwa anakuwa huru na kuacha uovu wake, hapana, bali aliamini wazi kuwa bado maadamu yupo hai basi ataendelea kufanya yale anayokusudia kwa raia wengine wasio na hasira, alivuta mafuta na kutafuta sehemu nzuri ambayo angeweza kufanya yake, kufanya lile alilokusudia. Kama unavyojua kasi ya gari za ubalozi haikuwa ya kawaida, yakiwa yamewasha vimulivimuli na kupishwa yalikuwa yakienda kasi kwelikweli. Mara saa ya Kamanda ikaanza kutoa kamlio hafifu, akauinua mkono na kuisikiliza inasemaje.

“Kamanda Amata, Chiba hapa,” alikuwa ni Chiba aliyekuwa akimpigia Kamanda wakati huo.

“Nimekusoma chiba endelea,” kamanda aliirusu simu hiyo.

“Nipo, uwanja wa maonesho wa sabasaba hapa Mtoni Mtongani,” akaendelea kusema.

“Endelea,” Kamanda akamruhusu aendelee kuzungumza.

“Kuna aina ya mlipuko ambayo imetegwa hapa, sasa najaribu kutafuta chanzo lakini naona kidogo utaalam unaniishia, pamepekuliwa kwa mitambo ya kisasa lakini hakujaonekana bomu wala kitu kinachofanana na hicho, nipe aidia mpya tafadhali,” Chiba alieleza lile linalomsibu.

“Ok, jaribu kutazama mitungi ya gesi kama ipo maana nayo inaweza kufanya milipuko mibaya kuliko bomu lenyewe, hakikisha kwa amri yako umeclear eneo lote ili kama itabidi kufa basi ufe peke yhako kama kiapo chetu kinavyosema, niko njiani kuja huko huko, Jegan Grashan amekwishaachiwa huru,” Kamanda Amata alimjibu na kukata simu ile kisha akarudisha mkono kwenye usukani wa pikipiki na kuongeza kasi zaidi na zaidi, alikuwa akipita gari kwa overtake za hatari mpaka madereva wa magari walikuwa wakitukana kila mtu kwa lugha yake. Dakika mbili baadae aliziona zile gari za ubalozi zikiwa kasi katika eneo la Karakana karibu na Tazara, sekunde chacahe akawa ameufikia msafara huo.

‘Mtu wenu anaachiwa ninyi bado mnataka mtulipue, sasa leo ama zangui ama zenu,’ Kamanda alijisemea huku akiupita ule msafara kwa kasi na kuwa mbele yake. Kisha kama mtu aliyepagawa alikunja kona kali na kuwa mbele yao, zile gari nazo zikafunga breki kali mbele ya pikipiki hiyo zikisota na kufanya ukelele mkali kwa msuguano wa tairi za barabara, gari mbili za nyuma ziligongana zenyewe kwa zenyewe na ile ya mbele almanusura imgonge Kamanda ambaye tayari alikuwa na bastola mkononi, alikwishaiondoa usalama na alikuwa akiitafuta shabaha yake anayoitaka. Kidole cha shahada kikaitekenya ile bastola, risasi tatu zilipasua kioo na kufumua kifua cha Jegana Grashan.

Muda na saa hiyohiyo

Milipuko mikubwa ilitokea katika maeneo mawili tofauti, mmoja katika yadi ya Bunju ya kuhifadhia mafuta iliyokuwa ikimilikiwa na Scolleti nay a pili yadi ya Mabibo, kwa nukta na sekunde ileile mabomu yaliyotegwa na Kamanda Amata yalifanya mambo yaliyokusudiwa.

Mji wa Dar es salaama ulipatwa na hekaheka siku hiyo kwani barabara ya Ally Hassan Mwinyi ilifunikwa na gari za zima moto na ile ya Mandela nayo vivyo hivyo. Moshi mkubwa ulitanda anga ya Dar es salaam.

‘Kama walijifan ya wao magaidi basi hawakujua kama na mimi ni gaidi zaidi yao,’ Kamanda alijisemea huku akipita vitongojo vya katikati vya wilaya ya Temeke, akafika mahali kulikuwa na nyumba nyingi zilizobanana, Kamanda Amata alipinda kona na kuingia katika ua wa nyumba hiyo, moja kwa moja akaiegesha pikipiki yake kwenye stoo ndogo ya mkaa, akaizima, akina mama waliokuwa wakifua na kuosha vyombo walipiga kelele na kuwanyakua watoto wao.

Kamanda Amata akashuka na kuvua ile kofia ngumu akaipachika juu ya kioo cha kutazamia nyuma, akavua yale mavazi ya kuendeshea pikipiki na kuyaweka pale juu, akabaki na suti safi nyeusi iliyopambwa na tai ya buluu, hakuongea na mtu alitoka haraka na alipofika nje alipanda tax aliyoikuta barabarani.

“Sabasaba tafadhali,” alimwamuru dereva.

§§§§§

Watu wa usalama wa ubalozi walijitahidi kumsaidia Jegan Grashan lakini walichelewa, ilikuwa ni mvurugano eneo lote, wamachinga walikimbia huku na huku , wakiijaribu kunusuru maisha yao.

Wanausalama wa ubalozi hawakuwahi kumkamata Kamanda Amata kwani tayari Alishakwisha waacha mbali. Wakabaki wakitizamana hawana la kufanya.

Muda si mrefu, Land Cruiser moja nyeusi ilipunguza mwendo katika eneo hilo la ajali ambapo polisi wa usalama barabarani alikuwa tyari yuko kazini na wale maofisa wa ubalozi wakiwa wamezagaa nje na bastola zao mikononi. Kioo cha gari ile kikateremka taratibu, Madam S, akatzama lile tukio, akatikisa kichwa chake na kupandisha kioo kisha gari ikaongeza mwendo na kupotelea mjini.

§§§§§

Habari mbaya zilimfikia Shailan na Shakrum waliokuwa katika boti wakisubiri wenzi wao ili watoroke na kuwaachia Watanzania vilio vikuu ndani ya siku wanayoipenda, siku ya Julai saba. Shailana alihisi kuchanganyikiwa, kwanza kwa habari ya kifo cha Scolleti, pili milipuko ya yadi zote mbili, haikumuuma sana kwani si mali yao, ila hili la kifo cha Jegan Grashan, Shailan na Shakrum walilia machozi huku wakiwa wamekumbatiana, na walikuwa hawajui hatima ya wenzao waliokuwa katika yadi hizo ambao walikuwa wakiwasubiri pamoja na Tashirni aliyeleta taarifa hiyo. Shakrum akaiendea televisheni na kuiwasha, hakukosea, kioo kilikuwa kimepamba kwa maua ya moshi mzito na wakati mwingine kwa tukio la Kalakana pale Tazara, hasira akazima Tv na kurudi kwenye kompyuta yake, akaketi lakini alipojaribu kuichezea akakuta imefungwa kwa codes maalum ambazo hakujua ni nani aliyefunga, “Shiiiiiittttt!” akapiga ukelele nan kuipiga ngumi ile kompyuta.

Shakrum na Shailan hawakuwa na la kufanya, walitamani waondoke peke yao lakini hawakuona vema, akaendelea kusubiri wenzao mpaka muda waliopanga.

Saa 4:30 asubuhi

Simu ya Kamanda Amata ikaita tena wakatyi akiwa maeneo ya Tandika kuelekea sabasaba, akaitazama, Madam S, akatabasamu, ‘Lazima kapata salamu zangu pale barabarani’ akajiwazia.

“Kamanda, upo wapi?” akauliza kwa ukali.

“Nipo Sabasaba Madam vipi?” Kamanda akajibu.

“Hivi we una akili kweli?” Madam akafoka kwenye simu.

“Kwanini Madam? Nina akili timamu kabisa,” Kamanda akajibu.

“Unajua unachokifanya wewe? Sasa umeshaharibu na we mwenyewe unalijua hilo,” Madam akaendelea kufoka kwenye simu.

“Madam tutaongea ofisini mi nipo kazini kwa sasa,” Kamanda akajibu na kukata simu.

Madam S alikasirishwa sana na kitendo alichokifanya Kamanda Amata, alipopita katika eneo lile la tukio na kuona hali halisi alijua wazi ni Amata kwa sababu alikwishasema mbele yake na alishakula yamini juu ya hilo. Alijua nini kinakuja kumkuta Amata, Madam alilia machozi kwa hilo, alisikitika na kuumia sana, lakini lilikuwa limekwishatokea, hakukuwa na jinsi. Aliendesha gari yake taratibu kuelekea uwanja wa maonesho ya sabasaba.

§§§§§

Chiba alifanikiwa kuufungua mfuniko wa tanki kubwa la gesi, kosa moja alilolifanya ni kuwa hakujiandaa kwa hali hiyo, ijapokuwa aliipata sakiti iliyofungwa chini tu ya mfuniko huo lakini yeye mwenyewe aliathirika sana na ile gesi mbaya. Gina alimshuhudia Chiba akianguka kutoka katika lile tanki kwa msukumo mkubwa sana, akajishika mdomo kwa kiganja cha mkono wake, akili ikaja haraka, akageuka huku na kule, na kuona kabati lenye gas mask, akalivunja na kuchukua, akaivaa haraka kisha akakimbilia kule aliko Chiba akiwa na mask nyingine iliyojazwa hewa ya oksijeni na kumvika Chiba.

“Msaada!” alipiga kelele ndipo vijana wa jeshi walipoona jambo lile, nao haraka wakawahi mask na kwenda kufungaa mfuniko wa tanki lile kwa tabu sana kwani mkandamizo wa gesi ulikuwa ni mkubwa hivyo mvujo wake nao ulikuwa wa nguvu sana. Bkutokana na ujasiri na ukakamavu wa vijana hao walifanikiwa kuufunga na kupunguza athari ya gesi hiyo.

Hali ya Chiba ilikuwa mbaya, Gina akamkokota na kutoka nae katika eneo leneye hewa, kwa bahati nzurti katika banda hilo kulikuwa na gari ya wagonjwa iliyowekwa kwa ajili ya maonesho, kmpakia Chiaba nay eye akaketi katika usukani, na kuitoa gari hiyo kwa kasi eneo lile huku akiwa amewasha ving’ora vyote. Akainua simu na kumpigia dokta Jasmine. Dr Jasmine akamwelekeza moja kwa moja ampeleke hospitali ya taifa Muhimbili, Gina alitoka katika geti la uwanja huo kwa kasi na kuingia barabara ya Kilwa kurudi mjini.

Kamanda Amata alipishana na ile gari ya wagonjwa lakini hakujua kuna nini ijapokuwa dereva wa gari ile aliweza kumfananisha. Alikimbia haraka mpaka kwenye banda husika na kukuta vijana wa jeshi wakihaha huku na huku kujarib u kudhibiti hali iliyokuwepo hapo. Kamanda Amata alipofika alizuiwa kupita eneo hilo lakini kwa kitambulisho chake alairuhusiwa huku akipewa mask na kuivaa, akaingia ndani ya banda hilo na kukuta baadhi ya wanajeshi wakijaribu kutoa huduma ya kwanza kwa wafanyakazi ambao walikuwamo ndani ya banda hilo lakini gesi ile iliwaathiri. Kamanda Amata akaiwahi kompyuta ya Chiba iliyokuwa juu ya meza Fulani, ilikuwa inaendeleaa na kazi ambayo Chiba alikuwa anaifanya.

Akatazama kwenye kioo cha kompyuta hiyo, akaelewa kilichokuwa kinafanyika mara ya mwisho. Chiba kabla hajaenda kutafuta sehemu ya mlipuko alikuwa akijaribu kutafuta uelekeo wa wapi mawimbi yale ya kielektroniki yalikuwa yakitokea, mpaka yeye anaiacha kompyuta hiyo bado ilikuwa ikiendelea, Kamanda Amata akasoma nyuzi (degrees) zilizojiandika, akaelewa, kilikuwa kipimo cha ardhi katika longitude na latitude, na eneo husika lililolengwa kadiri ya nyuzi hizo aligundua ni maeneo ya Kigamboni, akaendelea kuperuzi na kwa chini kidogo, akasoma kwa makini sana namba zile zilizokuwa zikibadsilishana hapa na pale ili kupata uelekeo sahihi.

“Kigamboni Kaskazini,” akajisemea na kisha akiinua ile kompyuta na kutoka nayo mpaka nje, akatzama huku na kule na kuiona gari ya chiba akaiendea, akaingi na kujifungi ndani yake, kama anavyofanya Chiba, akaunganisha ile kompyuta na kijimtambo maalum kilichofungwa ndani ya gari hiyo, sasa akaweza kusoma eneo halisi kwa kutumia screen ndogo iliyopo ndani ya gari hiyo, akaiwasha na kutoka katika uwanja huo, akachukua simu ya upepo iliyo ndani ya gari hiyo na kubofya kitufe Fulani.

“Madam S, Madam S,” akaita kwa mtindo huo.

“Nakupata Chiba,” madam S akajibu.

“Hapana sio Chiba, hapa ni Kamanda Amata,” akamrekebisha.

“Nimekusoma nipe ripoti,” akaendelea Madam.

“Natoka uwanja wa maonesho wa sabasaba, hali sio mbaya sana lakini Chiba inaonekana ana hali mbaya ameondolewa na Gina kuelekea hospitalini, la pili inaonekana kuna jambo maeneo ya Kigamboni kadiri ya tafutishi nilizozikuta katika kioo cha Chiba, niko mbioni kuelekea huko, haraka iwezekanavyo.” Kamanda akabofya kitufe kingine katika redio hiyo.

“Umesomeka Kamanda, mama anabadili uelekeo, tukutane Kigamboni,” madam S akamaliza na kukata ile simu.

Simanzi na majonzi viliwajaa Shakrum, Shailan na wengine waliokuwa ndani ya boti, ukimya ulitawala wakati injini ya boti hiyo ikiwa inaunguruma kwani muda ulikuwa tayari umewadia wa kung’oa nanga. Kutoka mbali Shailani aliona kitu kama boti ndogo inayokuja kwa kasi, akachukua darubini na kutazama hakuamini macho yake kwa kile anachokiona, Tashrini na wengine wawili walikuwa katika boti hiyo wakija kwa ajili ya safari. Ingawa wao walisalimika lakini maumivu makaubwa yalibaki kwa ndugu yao Jegan Grashan. Dakika tatu tu ile boti ilifika ukingoni kabisa mwa ile boti kubwa ya akini Shakrum, wakashuka na kuhamia katika boti hiyo kisha milango ikafungwa tayari kwa kuondoka.

“Maafa yaliyotokea ni makubwa sana,” Tajan alimweleza Shailan.

“Nini?” aliuliza Shakrum.

“Akiba yote ya mafuta kamanda Amata kalipua yadi zote mbili hivi tunavyoongea zinateketea kwa moto. Scolleti amekwishauawa na Yule mwanamke wa Kihindi, Jegan nae kapigwa risasi na mtu asiyejulikana,” Tajan alitoa ripoti. Shakrum alikuwa amesimama akimsikiliza, mara hiyo akajiegemeza katika moja ya nguzo zilizo katikati ya boti hiyo akiwatazama wenzake hao.

“Na mlipuko wetu umetenguliwa kule sabasaba, wametuweza, kiukweli sikufikiri kama hawa jamaa watakubali Jegan aondoke hivihivi,” Shakrum alieleza.

“Jamani, hapa tumeshacheza pata potea, washa mashine tuondoke, si ajabu na sisi wakatukamata hapahapa au wakatushushia kombola moja tu tukapotea wote,” Shaiilan aliwaeleza wenzake, injini ikawashwa, milango ikafungwa, kiyoyozi kikaanza kuyoyoza, taratibu chombo kikaanza kuondoka eneo hilo kikichanganya polepole na kugeuka kuelekea upande mwingine, kila mmoja ndani ya chombo hicho alikuwa tayari ameketi mahala pake aliyekuwa anafungua kinywaji sawa, aliyesoma gazeti sawa, tayari walikuwa wamekwishaamua kuondoka.

§§§§§

OFISI ZA UBALOZI WA KHAZAKISTAN

Gari za ubalozi ziliingia katika kiwanja cha ofisi hizo, maofisa wa usalama wakashuka na kuiendea gari iliyokuwa haina kioo, ndani yake alikuwamoi Jegan Grashan.

“Nilijua hawawezi kukuacha hivihivi,” alisema mmoja wa maofisa hao alipokuwa anamvua bullet proof Jegan.

“Dah! Mungu mkubwa, nashukuru mlijiandaa Yule jamaa alikuwa ananimaliza kabisa,” Jegan alijibu huku akimkabizi Yule mwanausalama lile koti. Jegan Grashan akateremka garini na kukanyaga ardhi ya uraiani, kwa hatua za polepole huku akiwa ameshikwa mkono na mmoja wa wanausalama ambaye mkononi mwake alikuwa amekamata short gun alisindikizwa kuingia ndani ya jengo hilo.

“Ni saa nne sasa karibu na dakika arobaini na tano, boti itakuwa inang’oa nanga, kwa vyovyote vile wao wanajua wewe umekwishakufa,” ofisa mwingine wa ubalozi alimweleza Jegan.

“Haina shaka, naweza ungana nao sasa na kuondoka, asanteni sana,” Jegan aliwashukuru na kuwakumbatia mmoja mmoja, kisha akakiendea chombo cha mawasiliano na kuwasiliana na ndugu zake hao walioko ndani ya boti.

Jegan aliingizwa kwenye chombo maalum na kufungiwa ndani yake kisha ikabonyezwa swichi Fulani na chombo kile kikawasha injini zake ndani ya chumba maalumu kilichojazwa maji ambacho moja kwa moja kinatokea kwenye mkondo wa bahari. Dakika moja baadaye kile chombo kikasukumwa kwa nguvu na kutoka ndani ya jengo kwa kupitia kidirisha Fulani, kikapaa na kujibwaga baharini kisha kwa mwendo wa kasi kikapotelea baharini.

Ndani ya boti saa 4:45 asubuhi

Furaha na shangwe ziliijaza boti hiyo baada ya kusikia sauti ya mpendwa wao Jegan ikawahakikishia kuwa yuko hai, hajafa. Furaha ilikuwa mara mbili ya ile ya kwanza pale walipokipokea chombo maalumu kilichomhifadhi Jegan, na walipofungua ndani walimtoa ndugu yao huyo na sherehe ikawa sherehe, shampein, risasi za hewani vyote vililindima katika boti hiyo, nyimbo zikaimbwa na kuchezwa, kati yao wote hakuna aliyepotea, wote walikutana tena kama ndoto yao ilivyokuwa.

“Nimeachiwa huru, asanteni sana kwa juhudi zenu za kuishinikiza serikali ya Tanzania, mmefanya lililo jema hata sasa niko nanyi. Lakini huu sio mwisho wa mapambano, huu ni mwanzo, lazima tuikomboe nchi takatifu kutoka katika mikono ya watu wa Maghalibi na vibaraka vyao. Nisingeelewa kanchi kama haka ka Afrika mashariki kajifanye kana sauti ya kupambana na sisi, dunia yenyewe inapiga magoti mbele yetu, wao ni nani? Hawakujiuliza kuwa kwa nini Amerika na washirika wake kama Uingereza, Ufaransa na wengineo wako kimya? Wote hao wanajua kuwa freedom fighters tunajua tunachokifanya wanajua hilo ndo maana walibaki kimya,” Jegan Grashan alitoa hotuba ya nyodo katika boti na kufuatiwa na nderemo za wafuasi wake. Hakukuwa na linguine zaidi ya kuondoka, safari ikaanza taratibu, boti ile ilikuwa ikiambaa na maji ya bahari ya Indi ikichana mawimbi kuelekea Mombasa ambako wenzi wao walikuwa wakiwasubiri.

§§§§§

Kamanda Amata alijirusha majini na kupiga mbizi, akipita chini kwa chini kuielekea ile boti ambayo ilionekana kwa mitambo maalumu ya kijeshi pale kigamboni. Msoma rada alieleza wazi kuwa walikuwa wakiichunguza boti hiyo karibu masaa kumi tangu imefika eneo hilo, hawakuitilia nashaka kwa kuwa ilikuwa ikipepeza bendera ya ya Tanzania. Siku hii ndipo walipogundua kuwa haikuwa boti ya kawaida bali imeingia hapo kwa shughuli maalumu.

Madam S alimtazama Amata akipotelea majini, nay eye alirudi upande mwingine ambako kulikuwa na wanajeshi wanamaji waliojiandaa tayari kwa lolote lile. Kamanda Amata alipewa maagizo ya kuhakikisha kuwa waliopo wanakamatika wakiwa hai na uhai wao. Aliifikia ile boti kwa muda mfupi tu, bahati nzuri alipoifikia na chombo kilichombeba Jegan Grashan kilikuwa kikiwasili, aliona pale kilipoingilia ma yeye akajipenyeza hapohapo.

Wakiwa ndani ya boti wanashangilia ushindi huo, ndipo Kamanda Amata alipomshuhudia Jegan Grashan ambaye alijua wazi kuwa amemuua kule Tazara akiwa hai mbele ya macho ya wengine. Jambo hili lilimtia hasira na uchungu, akabadili mpango wake haraka na kujitokeza mzima mzima. Wakati wao wanapiga shampeini na risasi za hewani kushangilia ushindi, Kamanda Amata alikuwa kazimama mbela yao kama mzuka.

“Jegan Grashan, nani aliyekwambia kuwa utaondoka ndani ya nchi hii ukiwa na pumzi yako? Kama ulijuwa kuwa umepona sasa ndio mwisho wa maisha yako, nafikiri hukutaka kufa peke yako ulikuwa na akili sana na sasa mtakufa wote pamoja kwa mkono wangu huu, wasalimie kuzimu, mwanaharamu, mwanadamu ambaye hukustahili hata kuzaliwa,” Kamanda Amata alishikwa na hasira kali, akisema maneno hayo hakuna aliyeamini kama mbele yao yupo kiumbe huyo anayeogopwa kila kona ya sayari yetu, kabla hawajajiweka sawa wakiwa bado kwenye butwaa, kichwa cha Jegan Grashan kilifumuliwa kwa risasi mbili kutoka katika bastola ya Amata, mara hii alihakikisha anakufa.

Kamanda Amata alijirusha upande wa pili na risasi yab tatu ikamfumua Yule aliyeshika shotgun aliyekuwa akimlenga Kamnda, hola! Alifanikiwa kupiga viti na vyupa vya pombe wakati Kamanda akijiviringa kuelekea upande mwingine. Ilikuwa ni hali ya taharuki kwa freedom fighters.

“Muueni shetani mweusi!” Shakrum alipiga kelele huku akitafuta pa kujificha. Tayari watu watatu walikuwa chini bila uhai.

“Jegannnnnn!!!!!!” Ilikuwa sauti ya Shailan aliyekuwa akilia kwa uchungu aliposhuhudia mwana mapinduzi wao akifumuka kichwa. Dakika moja baadae wote walikuwa chali sakafuni, Shakrum alibaki hai kwa kuwa aliwahi kujificha. Kamanda Amata akatazamana na Shailan.

Jicho la hasira la Kamanda Amata lilikuwa likimwangalia Shailan aliyekuwa amemshika Jegan mfu akilia kwa uchungu.

“Kama kuna aliyewaambia kuwa mtaondoka nchi hii mkiwa hai amewadanganya kabisa, hamkustahili kuishi wala kuzaliwa,” Kamanda Amata aliongea hayo na kufyatua risasi moja iliyopiga kifua cha Shailan na kumtupa nyuma. Alipotaka kufyatua risasi ya pili akajikuta ameishiwa risasi. Mara akajikuta akidakwa kwa nyuma, kabla hajakaa sawa, alikabwa shingo. Amata akafikiri la kufanya kwa haraka, akainama na kumyanyua huyo mtu na kumbwaga mbele, Shakrum. Hasira za Amata zikawaka maradufu, Shakrum akanyanyuka na kumkabili Kamanda Amata.

“Nilikuwa nakutamani sana wewe kiumbe! Na sasa umeingia mkononi mwangu, sitakupa hata nukta ya kuomba sala ya mwisho,” Shakrum alimwambia Kamanda Amata, alipomaliza sentensi yake alimvamia Kamanda kwa jinsi ya ajabu, akampiga ngwara moja maridadi, Kamanda alijirusha hewani akaichanua miguu yake na kuipata shingo ya Shakrum, alimpiga teke kwa mguu wake wa kulia nyuma ya shingo, Shakrum aliyumba na kujipigiza ukutani. Akaruka sarakasi na kusimama wima, akaweka mikono katika mtindo wa kuvutia wa mapigo ya karate, Kamnda Amata naye akajipanga kivingine. Shakrum alitoa mapigo ya kasi mfululizo kumuelekea Kamnda Amata lakini hakuna hata pigo moja lililomfikia Amata, mapigo yote yalipanguliwa kiufundi sana, mwisho wa yote Kamanda Amata akajirusha sarakasi na kumpa Shakrum nafasi ya mita kama tano kutoka kwake. Kwa sekunde chache alizozipata Amata alijipanga na kupeleka mapigo ya kazi ambayo yote yalimuioshia Shakrum na kumtupa chini akiwa hoi.

“Mi nilifikiri unajua kupigana kumbe ni mwanafunzi namna hiyo!” Amata alimwambia shakrum aliyekuwa akitambaa chini huku yeye akimfuata kwa nyuma.

“Ulipigania Jegan kuachiwa huru, sasa wewe utakaa jela badala yake,” Amata alimwambia Shakrum na kumkamata ukosi wa fulana yake na kumvuta kwa nguvu mpaka kijana huyo akakohoa, akamuinua kwa nguvu na kumbamiza ukutani. Shakrum hakuwa na la kufanya, Kamanda Amata akatoa pingu tayari kumfunga Shakrum lakini lo, bomu aina ya grunet lililoondolewa pini ya usalama likaanguka kutoka mkononi mwa Shakrum na kutua chini liokadunda mara ya kwanza na likaelekea kugoinga sakafu mara ya pili.

Shakrum alimshika kamanda kwa nguvu zake zote.

“Hatoki mtu hapa, kama wewe umeua ndugu zangu, lazima nawe ufe na sisi,” Shakrum alimwambia Amata.

“Kamwe haiwezekani!” Kamanda Amata akajibu na kumpiga kichwa cha nguvu kilichomfanya Shakruma amwachie. Kamanda Amata hakupoteza sekunde, alikimbia kwa kasi yake yote, hakukuwa na mlango ila dirisha kubwa la kioo mbele yake, alichumpa na kutanguliza kichwa akakipiga kioo nay eye mwenyewe kutoka nje kupitia hapo. Nyuma yake ulitokea mlipuko mkubwa, ile boti yote ikateketea kwa moto.

§§§§§

Madam S alijishika kichwa baada ya kuushuhudia mlipuko ule kupitian chomb o maalumu katka kambi ya jeshi la wanamaji Kigamboni.

“Oooh! My son! (Oooh Kijana wangu!)” alipiga kelele.

Moyo ulimwenda mbio hakujua afanye nini. Akikumbuka Chiba kaumizwa na gesi, sasa Kamanda ndani ya mlipuko, Madam S alijikuta anabaki peke yake, machozi ya uzee yalimdondoka huku mikono yake ikifunika kinywa chake kwa uchungu.

Chumba kizima walichokuwa maofisa wa Jeshi pamoja na Madam S wakishuhudia tukio lile kilikuwa kimya, hakuna hata aliyekohoa. Madam S alihisi akishikwa bega. Akageuka na kumtazama aliyemshika, alikuwa waziri wa ulinzi aliyefika muda huo katika kambi hiyo ya wanamaji.

“Pole Madam, lakini vijana wetu wamekufa kishujaa!” alimwambia Madam S.

“Nani aliyekwambia vijana wangu wamekufa?” madam S alijikuta akipiga kelele kupingana na kauli hiyo. Mara kelele zikaibuka katika chumba kile, Madam alipogeuka alimuona Kamanda Amata akiogelea majini baada ya kuibuka.

“Mpe msaada haraka!” illikuwa ni sauti ya waziri wa ulinzi, na mara hiyo hiyo boti iendayo kazi ikaanza safari yake na kumfuata Kamanda Amata.

Madam S alijikuta akifurahi kwa tukio hilo, hakuamini kab isa anachokiona mbela yake.

“Mungu mkubwa!” alishukuru.

MADAM S aliinua simu yake baada ya kushusha pumzi ndefu, katika sakata hilo ni yeye tu aliyekuwa upande wa peke yake tangu mwanzoni baada ya kusikiliza kile ambacho Kamanda Amata alimwambia tangu mwanzo kuwa hakubaliani na kuachiwa huru Jegan. Ijapokuwa Madam S aliwasikiliza wajumbe wengine katika jopo lile la baraza la usalama la taifa chini ya waziri wa ulinzi, aligeuka baadae kwa kuungana na kijana wake, TSA 1 lakini swala moja walikuwa wakitofautiana. Kamanda Amata aliapa wazi kuwa laiti Jegan akiachiwa huru yeye atamrudisha kwa risasi, uamuzi huu ungekuwa kinyume na maadili ya kazi kama kungetolewa hati ya jambo hilo. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, Kamanda Amata alimpiga risasi Jegan Grashan katika msafara wa gari za ubalozi. Ijapokuwa Jegan alikuwa amevikwa nguo zisizoingia risasi na kusalimika katika tukio hilo. Aligadhibika sana alipomuona Jegan akiwa hai ndani ya boti ile, akipongezana na wenzake na kutoa maneno ya kashfa, Kamanda Amata hakushindwa kutumia bastola ile ile iliyofanya kazi katika tukio la kwanza, na sasa alifumua kichwa kabisa maana labda angekuwa na nguo nyingine isiyopitisha risasi. Alijua alilolifanya.

‘Liwalo na liwe!’ alijisemea moyoni huku akiitazama boti ile iliyokuwa ikiteketea kwa moto, hakuna hata mtu aliyetoka, hakikusalia hata chuma juu ya chuma kingine. Kazi ilikuwa imekwisha namna hiyo. Akajigeuza na kuendelea kuogelea kuelekea pwani ambako palikuwa na umbali kidogo lakini alipoanza kuogelea tu, aliona helkopta kubwa ya jeshi ikija eneo lile, akaipungia mkono na chombo kile kikasogea hadi pale alipo na kumteremshia kamba iliyofuingwa kwa mafundo mafundo, akaikamata na dude lile likaondoka nae kutoka pale kwenda nae nchi kavu.

KIGAMBONI – KAMBI YA JESHI LA WANAMAJI

saa 7:14 mchana

MADAM S alisimama kwenye uwanja wa kushukia helkopta, pembeni yake kulikuwa na waziri wa ulinzi, walikuwa wakimwangalia Kamanda Amata alipokuwa akija upande wao akiwa chapachapa, ametota maji.

Madam S alimkumbatia Kamanda Amata kwa nguvu zote bila kujali kama kalowa maji, alimbusu mashavuni.

“Kazi nzuri kijana wangu, nimefurahi sana kwa ulilofanya, nina uhakika hakuna aliyetoka mle ndani,” Madam S alimwambia Amata.

“Hakuna anyeweza kutoka kwenye mikono ya Kamanda aamuapo jambo, si Jegan, si Shailan wala Shakrum, wote leo nyama zao zinaliwa na watoto wa samaki, lazima ulimwengu ujue kuwa kuna wana usalama makini katika kazi, Mungu ibariki Tanzania, nahitaji kumuona kaka yangu Chiba,” Kamanda alimwambia Madam S, akamtazama waziri wa ulinzi kisha akapita b ila kumsalimia na kuingia kwenye gari ya usalama, akaketi katika siti ya nyuma na Madam akaingia siti ya mbele nyuma ya usukani wakaiacha kambi hiyo na kuelekea mjini.

MUHIMBILI saa 7:54

CHIBA alitolewa kwenye chumba cha daktari na kupelekwa sehemu maalumu ambayo ni yeye peke yake alikuwa amehifadhiwa humo, chumba maalum chenye mitambo tiba ya kila aina ambayo ina uwezo wa kukushikia roho yako wakati wewe ukifanya mambo mengine. Alilazwa kitandani na kuwekewa hewa ya oksijeni ili imsaidie kupumua huku mitambo mbalimbali ikishirikiana kuonesha mwenendo mzima wa maisha ya mtaalamu huyo. Ijapokuwa ni yeye alikuwa mtaalamu wa kompyuta lakini mara hii kompyuta zilikuwa zikimuongoza yeye. Hakuweza kufungua macho ndani ya ubongo wake alikuwa akipitiwa na mapito mengi mabaya nay a kutisha, aliota Kamanda Amata anakufa kifo cha moto, na mara akaota Kamanda Amata anafukuzwa kazi. Ndoto mbaya zaidi ilikuja baada ya muda mfupi, alipoota wapelelezi wawili maarufu sana wa Tanzania wakiuawa vibaya katika sehemu moja ya Afrika wakiwa wanataimiza majukumu yao ya kiserikali. Mara vile vyombo vikaanza kupiga kelele na kuonesha kuwa mapigo yake ya moyo yanashuka kwa kasi. Muuguzi aliyekuwa hapo akamwita dakatari haraka. Dr Jasmin, alikuwa akitokwa na jasho akijaribu kuokoa maisha ya Chiba, Chiba alikuwa akipigania maisha yake ya mwisho, ulikuwa mpambano mkali na shetani. Katia maono yake alikuwa akipambana na joka kubwa lenye vichwa saba, haukuwa mpambano wa kitoto, lakini Chiba alijitahidi kutumia nguvu na ujuzi wake wote ili kulishinda joka hilo, lakini haikuwa hivyo. Joka lilimdhibiti Chiba likamkaba mwilia wake na kumnyonga.

Mitambo tiba iliyokuwa ikipima mwenendo wa moyo wa Chiba ilionesha mstari ulionyooka kuashiria kuwa Chiba hana uhai tena. Dr Jasmine alishindwa kuvumilia hali hiyo alijikuta akilia kama mtoto. Nukta hiyohiyo Madam S na Kamanda Amata waliingia ndani ya wodi hiyo wakiwa haihai walipofika pale walikuta vurugu ya madaktari wakisaidiana na wauguzi, wakati huo Gina alikuwa hana hali kwa kilioo cha vikwifuvikwifu.

“Nini Gina?” Kamanda aliuliza.

“Man down Kamanda,” Gina alimwambia huku akilia. Kamanda Amata alielewa haraka maana ya neno hilo likimaanisha Chiba amekufa, Kamanda Amata hakusubiri linguine, haraka alikimbilia walipo madaktari ambapo tayari Madam S alikuwa amekumbatiana na Dr Jasmine wakilia kwa uchungu.

“Noooooooooo!!!!!!!” kamnda Amata alipiga kelele na kuwatawanya madaktari waliokuwa pale, wengine wakaanguka na wengine wakayumba na kusimama wima. Kamanda Amata alimtazama Chiba ambaye alikuwa ametulia kimya macho yake yakiwa meupe, mboni zake hazikuonekana, “No my brother, don’t leave me!!!!!!” (Hapana ndugu yangu, usiniache peke yangu,) Kamanda Amata kama kawaida yake huwa hakubali kushindwa jambo, wakati madaktari wakimshika amuache Chiba hakukubaliana nao, alitazama huku na huku, akaona waya wa umeme wa 6.0mm uliokuwa ukipitisha umeme kuelekea kwenye mitambo ya oksijen, Kamanda kutoka aliposimama alikanyaga kimeza cha dawa za mgonnjwa na kuukamata ule waya akaning’inia nao mpaka ule waya ukachomoka katika joint box, akashika jirani na miisho yake ambayo ilikuwa ni nyaya mbili, nyekundu na nyeusi, bila huruma wala kuchelewa akampiga shoti Chiba akiwa kitandani, akarudia mara ya pili.

Jambo lisiloaminika likajitokeza, mashine iliyokuwa ikipima mapigo ya moyo ikaanza kusoma mapigo ya juu sana na baada ya sekunde kumi ikatulia na kuonesha mapigo yaliyo sawa. Chiba akafumbua macho, akamtazama Kamanda, Madam S, Madaktari na wauguzi waliopo katika wodi ile. Chiba akaondoa mwenyewe kwa mikono yake ile barakoa ya oksijeni, akainuka na kuketi kitandani.

“Kamanda Amata, umepona?” akauliza Chiba.

“Nimepona kaka,” Kamanda akajibu.

“Jegan najua amekufa na wenzake je?” Chiba akauliza tena.

“Wote wamekufa, hakuna aliyesalia,” Kamanda akajibu, Chiba akampa ishara Kamanda Amata ya kuwa asogee jirani, akamkumbatia kwa nguvu. Kamanda akautupa ule waya chini, na wakati huo fundi umeme alikuwa keshafika baada ya kuitwa haraka.

“Asante Kamanda Amata,” Chiba akashukuru.

“Asante na wewe kwa kuokoa maisha ya Watanzania wengi,” Kamanda akamshukuru Chiba. Wale madaktari wakamchomoa vifaa vyote vilivyokuwa mwilini mwake. Chiba akatoka kitandani na kuongozana na Madam S, Kamanda Amata, Gina na Dr Jasmine wakatoka na kuingia kwenye gari kisha wakaliacha eneo la Muhimbili na kutokomea zao.

§§§§§

BAADA YA SIKU MBILI

OFISI NYETI

KAMANDA Amata akiwa amesimama mbele ya meza kubwa, safi ambayo unaweza kujiona mwenyewe, alikuwa akitazamana na Madam S ambaye naye alikuwa amesimama wima, wote wakiwa katika vazi la kufanana, suti nyeusi, shati jeupe na tai ndefu nyeusi kasoro Madam S. Chiba alikuwa pembeni na watui wengine wawili akiwamo Dr Jasmine.

“Tukisimama hivi unaelkewa kabisa kuwa tunahitaji nkuongea kiofisi zaidi,” Madam S alimwambia Kamanda Amata ambaye alikuwa kimya bila kujibu lolote, akatoa kitambaa chake cheupe na kufuta machozi yaliyokuwa yanayajaza macho yake angavu, kisha akaendelea, “Baada ya kikao cha jopo lilelile lililokuwa likikaa tangu mwanzo wa sakata hili mpaka jana limekaa tena. Na agenda kubwa ilikuwa ni juu yako Kamanda wangu, kwanza unapongezwa sana kwa kazi nzuri uliyoifanya kwa kushirikiana na wenzako wote, mmeudhihirishia ulimwengu kuwa usalama wan chi hii upo mikononi mwetu wenyewe, lakini pamoja na pongezi hizo Kamanda, kuna habari mbaya nay a kusikitisha juu yako na juu ya ofisi yetu pia,” akakohoa kidogo na kuendelea tena, “Siku zote kwenye kitambaa cheupe kinachoonekana ni doa jeusi tu, watu hawaangalii wema ila mabaya yako na kukupatiliza kwayo, ndani ya kazi yako nzuri ambayo sisi kama wanausalama tumeiweka kwene kablasha linalojulikana kama JULAI 7, Kamanda umeonekana kufanya kazi kijeuri bila utii kwa maamuzi yako mwenyewe na kupinga maagizo ya jopo la usalama na kwa sababu hiyo baraza la usalama limekupa barua ya kusimamisha kazi katika kitengo cha ujasusi cha TSA, utakivua cheo chako cha TSA1 na kukabidhiwa mtu mwingine kuanzia nimalizapo kusema haya, haijatolewa kama ombi bali ni amri na itekelezwe mara moja, imesainiwa na waziri wa Ulinzi kwa niaba ya baraza zima la usalama wa taifa.” Madam S alimaliza na kufuta machozi.

Kamanda Amata alitulia kama dakika moja, kimya kilitawala, hakuna aliyeongea isipokuwa kufuta machozi na makamasi yaliyokuwa yakiwatoka waliopo kwa uchungu. Aliyekuwa ngangari ni katibu wa wizara ya ulinzi tu, akasogea na bahasha ya khaki, akatoa karatasi tatu nyeupe zilizochapwa kwa mashine ya kisasa, upande mmoja ilisainiwa na waziri wa ulinzi na upande wa pili zilibaki saini mbili moja ya Kamanda na nyingine ya Madam S kama mkuu wa kitengi maalumu, kitengo cha kijasusi kisicho na mipaka. Akaipokea ile barua na kusaini kisha akampa Madam S nae akazisaini kisha, wakagawana moja kwa ofisi ya baraza la usalama wa Taifa, nyingine kwa ofisi ya TSS nay a mwisho akapewa Kamanda Amata, naye akamkabidhi Gina.

Baada ya hapo, Kamanda Amata akavua beji maalumu ya usalama wa taifa na kumkabidhi Madam S, beji ya dhahabu, kimkoba kidogo cha bastola ambacho ndani yake kilikuwa na vifaa kadhaa vya kijasusi ambavyo alikabidhiwa pindi alipopewa kazi hiyo maalumu. Mwisho akapeana mikono na wote waliopo ndani ya ofisi hiyo nyeti.

Ilikuwa ngumu kuzuia machozi ya kila mmoja lakini hali halisi ilikuwa hiyo.

“Nakuhitaji nyumbani Kamanda ndani ya masaa matatu, wewe na wenzi wako kwa chakula,” Madam S alimpa ujumbe Amata.

NYUMBANI KWA MADAM S

“Sikuweza kukutetea tana Kamanda, ijapokuwa wapo nwaliojaribu lakini wengine walikazia ufukuzwe kazi” Madam S alimwambia Kamanda Amata walipokuwa wameketi katika bustani kubwa ya nyumba hiyo, Gina, Chiba na Dr Jasmine walikuwa ndani wakiendele kupata vinywaji.

“Usijali Madam, yote maisha, mimi nimetoka TSS atakuja mwingine naye kutimiza wajibu wake,” Kamanda alimwambia Madam S.

“Najua, lakini kwa sasa kumpata mtu shupavu, mwelevu, mwepesi, mwenye mbinu na ujuzi wa mipango ya kumsaka adui au kummaliza, mbabe kama wewe itachukua miaka mingi sana, usijali Kamanda naamini kuwa muda mfupi tu mataifa makubwa yatakuchukua, mi nakutakia maisha mema sana Kamanda, kwa lolote tuwasiliane mimi ni mama yako na wewe ni mwanangu,” Madam S akamaliza, wakakumbatiana kwa nguvu kila mmoja akimwaga machozi ya uchungu kisha wakaachana na kurudi ndani.

§§§§§

Gina na Kamanda Amata waliondoka kwa Madam S na kupitia vijiwe kadhaa kabla hawajafika nyumbani.

“Nikupeleke kwako au?” Kamanda akauliza.

“Sitaki, leo nataka kulala kwako,” Gina akamwambia Kamanda Amata kisha wakaendelea na safari mpaka nyumbani kwa Kamanda Amata. Walikuwa wamelewa, Gina alifika na kuingia chumbani akifuatiwa na Kamanda.

“Kamanda Amata, uliyekuwa TSA1 wenye roho mbaya wamekufukuza kazi, usijali mimi leo nataka nikupe kazi njione kama kweli we mwanaume,” Gina aliongea kwa sauti ya kilevilevi.

“Gina ulale sasa,” Kamanda alisititiza na kutoka kwenda sebuleni. Gina akachukua nafasi hiyo kwenda maliwato, akaoga na kurudi kisha akaingia ndani ya kitanda kikubwa na kujifunika kwa shuka safi yenye maua ya kuvutia, akazima taa kali na kuwasha ile ya buluu.

Dakika chache baadae Amata aliingia chumbani, naye vivyo hivyo, akaenda kuoga na kurudi, Gina kwa hila zake akajifunua shuka na kulitupa pembeni akabaki kama alivyozaliwa.

“Njoo Kamanda, najua una mambo mengi leo, njoo nikufariji,” Gina alimwambia Kamnda huku akiwa anjipindapinda pale kitandani.

Kamanda Amata akamtazama mrembo huyu ambaye siku zote walikuwa wakiheshimiana sana lakini leo hii heshima ilikuwa inataka kubadili uelekeo.

Gina alikuwa akimtazama Kamanda, Kamanda alikuwa akimtazama Gina aliyekuwa kajilaza pale kitandani, mwanga wa taa buluu ulifanya umbo la Gina lionekane kama madini ya Tanzanite, lilimvtia Kamanda, akapatwa na wakati mgumu, kabla hajaamua la kufanya. Gina aliinuka na kumtoa taulo Kamanda kisha akaizungusha mikono yake na kuiokutanisha nyuma ya shingo ya Kamanda Amata.

“Nakupenda sana Kamanda Amata”.

MWISHO

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment