Kitanzi cha Mwisho Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE
*********************************************************************************
Sehemu ya Pili (2)
BUGURUNI kwa Mwinyi Amani, au kwa mnyamani kama walivyozoea kupaita wakaazi wengi wa Dar es salaam, barabara zake zilijaa tope hasa ile ya kutokea Kiembe Mbuzi, watu walikuwa wakijaribu kuruka matope hapa na pale huku wenye magari nao wakipita kwa fujo na kusababisha adha kubwa kwa watembea kwa miguu, wengine wakiwatukana kwa kukosa ustaarabu na wengine wakiishia kukasirika tu. Jioni hiyo tayari na wauza samaki walikuwa wamekwishaanza kazi yao, mioto ya vibatari iliangaza hapa na pale kiasi kwamba usipokuwa makini kwenye dimbwi la maji utakanyaga sponge ukijua tofali kumbe watoto wa mtaani wamekutegeshea ili ukitumbukia majini kwao burudani.
Miongoni mwa wote hao, mwanadada mmoja mwenye mwili wenye nyama kidogo alikuwa akitembea kwa kuchechemea akijitahidi kuvuka yale maji na matope huku macho yake yakiangaza angaza huku na kule kuangali kinachoendelea, hakuna mtu aliyemtzama mwanamke huyo kwa maana jiji hilo kubwa kila mtu kivyake. Kwa hatua zilezile za kuchechemea alivuka reli na mbele kidogo akasimama, alipoona watu hawamwangalii aliingiza mkono ndani ya nguo yake kwenye maeneo nyeti na kutoa kijikaratasi kidogo na kukisoma, sekunde kadhaa alimaliza zoezi hilo dogo na kuendelea na safari yake.
Yaumi alisimama mbele ya nyumba moja iliyoonekana kuukuu na kupanda ngazi zake taratibu hadi mbele ya mlango uliyomkaribisha kwa maandishi BGN/MNI 612 B zikiashiria namba ya nyumba na kiwanja, kabla hajafanya lolote akatokea motto mdogo wa kiume mkononi akiwa na andazi, akamwamkia Yaumi na Yaumi hakuona haja ya kumuacha bila kumuuliza, “Ujambo motto mzuri? Eti unamjua mama Naksadi?” yule mtoto badalaya kujibu alikimbilia ndani na punde tu alitoka mwanamke mrefu aliyevalia baibui kuanzia usoni mpaka miguuni, Yaumi alimtazama yule mwanamke na kumtambua mara moja akatumia lugha ya alama kuongea nae naye badala ya kujibu alishuka ngazi mbili na kumshika mkono Yaumi kisha kuingia nae ndani, moja kwa moja mpaka chumba cha wageni na kumketisha humo, kisha akatoa lile baibui lake na kubaki na jeans na tshrt nyekundu maridadi mwilini mwake, kifua chake kilichobeba matiti madogo kilimfanya aonekane mwanamke mrembo wa kuweza hata kugombea umiss, wote walibaki wakitazamana.
KIKAO cha maafande wachache kilichukua nafasi katika kituo kidogo cha polisi Tabata Kimanga, taarifa za uchunguzi wa awali juu ya mauaji ya mtu mwingine katika nyumba ya marehemu Kajiba zilikuwa zikiwasilishwa. Utata uligubika juu ya kifo hicho lakini swali lilibaki kuwa je mtu huyo alifuata nini katika nyumba ya marehemu, nyumba ambayo kwa wakati huo haikuwa imekaliwa na mtu baada ya mke wa marehemu, Yaumi, kuwekwa rumande.
“Hivi tukiliongea hili jambo kitaalamu, inaingia akilini kweli mtu asiye na uhusiano wowote na nyumba hiyo aingie na kujificha ndani? Anatafuta nini? Anamngoja nani? Wakati mwenye nyumba amekufa na mkewe yuko rumande” ilikuwa ni sauti ya ACP Chonde, aliyeonekana mara kwa mara akitikisa kichwa kana kwamba kuna mdudu ndani ya ubongo wake. Akawatazama wale vijana aliowapa kazi ile na kuwauliza, “Ok, sasa ninyi mnamhofia Yaumi ndiye muuaji?”
“Ndio afande,” mmoja lijibu
“Nipe uthibitisho wako kama askari,” ACP Chonde alisema huku akijiweka sawa kitini.
“Afande, ulipotutuma kufanya uchunguzi wa ule mwili wa marehemu, pia tulijaribu kuona jeraha lake litakuwa limesababishwa na risasi aina gani, japo ilikuwa ni vigumu kwetu kutambua lakini mtaalamu kutoka makao makuu alihisi kuwa marehemu ameuawa kwa risasi ya Colt 45, na katika kumbukumbu za usalama, marehemu Kajiba alikuwa anamiliki silaha ya aina hiyo ambayo mpaka sasa haijawasilishwa kwetu, ni hayo tu afande,” alijibu yule askari.
ACP Chonde alishusha pumzi na kuizungushazungusha kalamu yake mkononi kisha akavuta kijidaftari kidogo na kuandikaandika vitu Fulani. Bado swala moja lilikuwa gumu kichwani mwa ACP Chonde, kama ni kweli aliyeua ni Yaumi, je aliwezaje kutoka rumande na kutekeleza uhalifu huo, nani alimruhusu kufanya hivyo, akili ya ACP Chonde ilivurugika na moja kwa moja akaona wazi kuwa hapo kuna jambo kama si mambo, alitaka kuwapa kazi hiyo wale vijana kukamilisha uchunguzi kule magereza lakini akaona si vyema ni bora swala hilo akalifanya mwenyewe. Aliwashukuru wale vijana na kuwaruhusu kwenda zao. Ofisini alibaki peke yake, alijaribu kupitia lile jalada upya na kuandika maswali Fulani juu ya kila kurasa aliyoona ina shida ya kueleweka na mwisho akaandika mambo ya msingi ya kufanya ili kupata utatuzi wa hilo.
˜˜˜
Kijua kikali kililitawala anga la Dar es salaam, ACP Chonde aliketi katika moja ya viti vilivyopo katika bar maarufu iitwayo Mangumi katika eneo la Segerea akijipatia kinywaji baridi kupoza kiu iliyobana koo lake kwa fujo huku akiangalia wahudumu warembo waliovalia sare maridadi wakitoa huduma safi katika bar hiyo. Akiwa mkononi na gazeti fulani alilolinunua hapo muda si mrefu aliendelea kunywa taratibu bia yake ya safari lager ladha kamili inayoridhisha zaidi, alilifungua gazeti hilo na kusoma habari mojawapo iliyopamba gazeti hilo, ‘Mauaji ndani ya nyumba ya marehemu yaitatanisha polisi,’ aliisoma habari ile kwa kina na kutikisa kichwa kuonesha kuwa umbea wa wanahabari tayari ulichukua nafasi wakati hata polisi wenyewe hajaliweka wazi jambo hili.
Aliporidhika na kinywaji hiko alinyanyuka na kulipia kinywaji chake, “Karibu tena kaka,” mhudumu mmoja alimkaribisha huku akiipokea noti ile ya elfu tano, “Keep change,” Chonde alitoa ofa hiyo bila kujitegemea, kwa kudanganywa tu na macho ya mwanadada huyo wa Kimburu.
Geti la gereza la Segerea lilikuwa limefungwa kama kawaida ya magereza yote, ACP Chonde alisukuma kijibati kidogo kilichopo kwa ndani ya lango kuu na mara mlango ukafunguliwa, akajitambulisha na kuonesha kitambulisho chake, alipoeleza shida yake moja kwa moja akapelekwa katika ofisi maalum ya ‘admission’.
Mbele yake aliketi askari mmoja mkakamavu aliyeonekana kuwa na macho mekundu kama anavuta bangi lakini ndivyo alivyozaliwa. ACP Chonde akaeleza shida yake na askari yule aliielewa vyema.
“Sasa hilo swala afande, nikupeleke kule upande wa wanawake ili wakusaidie, ila kwa uzoefu wangu sijasikia tukio kama hilo kwani hapa pana ulinzi mkali kama unavyojua magereza,” yule askari alimjibu na kisha kunyanyuka kumpeleka upande wa wafungwa wanawake, pale akakutana na staff sajini mmoja ambaye alimsikiliza lakini nay eye alionekana kupigwa na butwaa.
“Unasema ameua? Atauaje na wakati yeye tulikuwa nae hapa siku hiyo?” akamtupia swali ACP Chonde.
“Si kwamba ameua ila tunataka kujua wakati wa tukio hilo kule nyumbani kuna mahusiano yoyote? Inawezekana labda alitoroka je; yote yanawezekana afande,” Chonde alimueleza yule mwanamama sajini.
“Siwezi kukupinga, na wala tusiandikie mate,” yule mwanamama akavuta likitabu likubwa na kulipekuapekua vyema kisha akatulia kwenye kurasa fula akitembeza kidole chake kutoka juu kwenda chini, kisha akavuta simu ya mezani na kubofya namba Fulani na kumngoja mtu wa upande wa pili. Alipomaliza kuongea na simu hiyo haikupita muda mrefu akaja afande mwingine wa kike, mwembaba, mrefu na kujibu maswali kadhaa aliyoulizwa na ACP Chonde.
“Usiku wa siku hiyo zamu nilikuwa mimi, sauda na afande Marina, na nakumbuka siku hiyo Yaumi alikuwa anaumwa na alilazwa hapo katika hospitali yetu, na nilifunga mimi pingu pale kitandani,” alijibu yule dada. Kichwa cha ACP Chonde kilionekana kupata shida kidogo katika hili, akioanisha taarifa za askari wake, zinaleta ukweli kidogo na hizi huku zinamaliza kabisa, kipi ni kipi, jibu halikupatikana, akashusha pumzi nzito na kutoa kitambaa chake kujifuta jasho, akaandika vitu Fulani katika kijitabu chake, akaaga na kuondoka zake akiwa nusu kachanganyikiwa nusu mzima.
Baada ya lisaa limoja alikuwa ofisini kwa mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni akitaka kuoanisha matukio kadhaa anayohusishwa Yaumi.
“Yeah tumefanya uchunguzi wa kina sana, inasemekana kwenye ile gari kulikuwa na mwanamke pia, ila sasa hajulikani alipo, ila bado tunamsaka kwa udi na uvumba, afande unafikiri matukio haya mawili yana uhusiano?” aliuliza yule mkuu wa upelelezi.
“Aaa hatuwezi kusema yana uhusiano au hayana, lakini kitu kimoja, yule dada alipewa dhamana, na akachukulia kwenye gari aina ya vitz iliyokuwa na watu wengine wawili ndani, na hiyo iliyoungua umesema ni vitz huoni kuna uhusiano hapo?” Chonde aliuliza. Yule afisa upelelezi akatikisa kivhwa juu chini kuashiria kuwa hapo kuna kitu anaking’amua kwa wakati huo.
“Sasa na mtu wa tatu yuko wapi?” lilikuwa swali lililowatoka wote kwa pamoja kisha wakacheka na kugonganisha viganja vya mikono yao mikakamavu. Baada ya mazungumzo mawili matatu walinyanyuka na kutoka pamoja nje ya kitu hicho.
˜˜˜
Meseji moja kwenye simu ya marehemu jambazi ilifurahisha sana Yaumi alipokuwa akizisoma meseji zile, ilikuwa ni ya mapenzi, yaumi aliiangalia sana ile meseji na kubaini yule msichana ni wapi anapatikana baada ya kufuatilia mtiririko wa mazungumzo hayo, hiyo kwake ilikuwa ni jambo zuri kwani alijua akimtia dada huyo jambajamba lazima atasema tu kazi nay ale yote aliyokuwa akijishighulisha nayo huyo bwana wake. Hakuona haja ya kupoteza muda, aliitazama saa yake na kugundua tayari ilikuwa saa mbili usiku ikienda saa tatu, alijiweka tayari na kuipachika bastola yake kiunoni, tshirt ndefu iliyofuniko makalio vizuri ilimsitiri kwa hilo, akajitazama kiooni akaona yuko poa, akatumbukiza vikorokoro vyake vyote mkobani, aliamua kuhama gesti hiyo ili sasa akajipange kwa shoga yake Fasendy na siku inayofuata arudi kwenye nyumba yake aliyojenga na mumewe. Alijiweka begi lake mgongoni na kutoka ndani ya chumba chake, wakati akifunga mlango wake aligeuka upande wa pili akasimama kama aliyepigwa na shoti ya umeme na kukodoa macaho yake kuelekea upande ule.
MACHO ya afande Marina yalikutana na yale ya Yaumi, hakuna aliyeingea na mwenzake, Yaumi alianza kutweta akimwangalia Marina, mara akatoka jamaa aliyekuna Marina nakuuzungusha mkono wake kiunoni mwa Marina kisha wakatoka kuelekea nje Yule bwana akiwa hajui kilichotokea. Yaumi alikuja nyuma yake taratibu mpaka nje, akawatazama mpaka walipoingia kwenye gari moja na kuondoka. Sonyo refu likamtoka Yaumi, akaita bodaboda na kuondoka zake.
Yaumi alitembea polepole kuuelekea mlango wa nyumba hiyo iliyoonekana kuchokachoka sana kwa kuwa na umri mrefu. Aligonga mlango, binti mmoja akaja kuufungua, yaumi akaulizi kama Yule dada anayemhitaji yupo ndani, akajibiwa kuwa hayupo kaenda msibani Kimara. Akajua mara moja kuwa utakuwa ule msiba wa Yule jambazi. Akaiacha nyuma hiyo na kukodi tax kuelekea kwa Buguruni kwa Mnyamani moja kwa moja kwa Fasendy, akaingia ndani ya chumba kilekile.
“Niambie shoga,” alianza Fasendy
“Ah majanga, kule gesti nimekutana na Marina Yule askari magereza,”
“Hajakuletea noma? Simpendi mwanamke Yule!” Fasendy alilalama
“Ipo siku yake, nitamtia mkononi,” yaumi alijibu na kusonya.
“Ok, sasa ile kazi yako nimeifanya sawasawa,” Fasendy akaanza kutoa mrejesho, “Ile namba ulonipa ni namba za posta huko Kampala, Uganda.”
Yaumi alisikiliza kwa makini sana habari yote aliyokuwa akiambiwa na Fasendy, ‘Kampala’ alijiwazia, alikumbuka siku moja katika uhai wake akiwa na mumewe marehemu Kajiba waliwahi kutembelea jiji hilo, akakumbuka sehemu mbalimbali walizotembelea ikiwemo ofisi moja kubwa ya posta, akatikisa kichwa kuashiria kuwa ameelewa, ‘Kuna nini kampala?’ alijiuliza, ‘Niende?’ hakupata jibu la moja kwa moja, lakini pia hakumwambia Fasendy juu ya hilo, akalimezea moyoni na kujipanga kimawazo kwa safari hiyo.
˜˜˜
ACP Chonde aliingia ofisini kwake, moja kwa moja macho yake yakatua mezani na kukutana na bahasha ya kaki iliyofungwa vizuri, akainyanyua na kuitazama vizuri, ‘ACP Chonde’ iliandikwa kwa mashine juu yake, akaigeuza geuza na kuichana, ndani kulikuwa na karatasi dogo tu la ukubwa wa A5 limeandikwa maneno machache,
‘…najua ni jinsi gani unaipenda kazi yako na unaifanya kwa akili zako zote,lakini nakupa onyo acha kufatilia lolote linalomhusu Yaumi, ubishi wako utakuingiza matatizoni…’
ACP Chonde, akashusha pumzi ndefu na kuiweka barua ile mezani, haikua na jina la muandishi wala anwani ya ilikotoka. ACP Chonde alijikuta akitiririkwa na kijasho chembamba, na pumzi zikienda mbio kidogo kugombana kutoka katika matundu madogo ya pua za askari huyo, akaiweka bahasha ile mfukoni na ikuketi kwenye kiti chake cha chuma kilichowekwa nyuma ya meza chakavu iliyojaa majalada yaliyozagaa bila mpangilio.
Tafakari iliyoambatana na mawazo viliuteka moyo wa Chonde, alijaribu kufikiri barua hiyo ni wapi itakuwa imetoka, lakini hakupata jibu, labda angetazama muandiko ili ajue umefanana na nani lakini haiukuwezekana kwani barua hiyo iliandikwa kwa mashine, haikuwa na tarehe wala saini, ilikuwepokuwepo tu, alipouliza wenzake ni nani kaileta barua hiyo jibu alilopata ni kuwa imekutwa juu ya kaunta ya kituo, ilikuwa ni barua iliyoharibu siku ya Chonde, aliahidi moyoni mwake kuivalia njuga kesi hiyo na lolote liwalo liwe, alituliza mawazo kabla ya kuanza kufanya maamuzi juu ya hilo, ‘najua jinsi ya kumpata muandishi wa barua hii lazima niendeleepa na uchunguzi wa hii kesi,’ aliwaza peke yake huku akilivuta faili Fulani lililopo hapo juu ya meza na kuandika mambo kadhaa ambayo yeye aliona wazi kuwa yatamfaa katika kazi zake.
ACP Chonde, alikuwa askari mahili sana katika katika kazi yake, aliipenda na hata kuifanya kwa umakini wa hali ya juu, hakuogopa mtu wala kitu, daima alipenda kufanya kazi ambazo huatarisha maisha yake au hata kazi yake kama hii, alijikuta akiingia kwenye uchunguzi wa ksi hii kwa sababu tu ilikuwa katika eneo lake la kazi, Tabata Kimanga, kutokana na utata ulioigubika kesi hiyo ndipo alipoona umuhimu wa kujua zaidi nini kimejificha ndani yake.
Habari za uchunguzi huo zilimfikia bwana Matinya kupitia Marina, askari magereza wa kike, mwenye mahusiano ya kimapenzi naq bwana huyo, mtu mzito, alitwanga barua hiyo haraka na kuiingiza kituoni hapo pa si mtu kujua, na ikakutwa asubuhi ikiwa hapo, aliyeiokota ndiye aliyeiingiza ofisini kwa Chonde.
˜˜˜
YAUMI aliamua kupanga safari kwenda Kampala, Uganda. Alichokumbuka mara moja ni safari ya mwisho aliyoifanya na mumewe bwana Kajiba miaka mine iliyopita, zaidi ya hapo ni mwenyewe Kajiba tu alikuwa akienda kwa biashara zake. Yaumi hakujua jinsi ya kufika pale Kampala kwa maana ilikuwa ni mara moja na ya mwisho kwenda huko, kutokana na ujanja aliozaliwa nao aliamua kwenda kwa kupitia njia zilezile alizotumia na mumewe mwaka ule. Siku hiyo alijidamka mapema sana kama saa tisa hivi alfajiri, na breki ya kwanza ilikuwa ni CRDB tawi la Ubungo, akacheza na ATM na kutoa kitita kama cha shilingi laki mbili hivi, akihakikisha anapata nauli na hela ya matumizi njiani, alipekua kwenye kibegi chake chenye tafutishi zile alizochukua kwenye kabrasha za mumewe, akaikuta tiketi aliyosafiria miaka mingi nyuma, kama alijua kuwa itamsaidia alikuwa ameihifadhi vizuri sana. Akamba Bus Service, ilikuwa imeandikwa juu yake na jina lake lilikuwa pale chini likiwa limeandikwa kwa wino. Yaumi aliifananisha ile ya zamani na ile mpya aliyoikata alfajiri hiyo pale Ubungo zilitofautiana kidogo, hii ya sasa ilikuwa nzuri zaidi, ‘mambo hubadilika,’ alijiwazia. Saa kumi na mbili asubuhi, Yaumi alikuwa katika moja ya viti sitini vya basi hilo la Kenya, akiwa katika safari ya kuelekea Kampala Uganda, lakini kila alipojiwazia anaenda kufanya nini alikosa jibu, lakini alijipa moyo kuwa kitaeleweka uko huko akifika.
Yaumi hakupenda kumshirikisha mtu yeyote juu ya safari yake, alimuaga shoga yake Fasendy kuwa anakwenda kwao Monerumango kwa mapumziko mafupi na angerudi baada ya siku chache.
˜˜˜
Taarifa za safari ya yaumi zilimfikia Matinya, taarifa zilizotoka kwa wapelelezi wake waliokuwa wakifuatilia nyendo za Yaumi kila aendako tangu muda ule alipotoka pale nyumba ya wageni ya Mshangano, mara tua baada ya kukutana na Marina, bila kuchelewa Marina alimpa taarifa Matinya akijifanya alikuwa akimfuatilia kumbe alikuwa na mwanaume mwingine, amejikosha.
Yaumi akiwa hajui kama anafutailiwa na watu wa Matinya, aliendelea kufanya shughuli zake kama kawaida ikiwa ni pamoja na kwenda nyumbani kwake ambako sasa alikuwa haishi kwa kipindi hiki, alikuwa akitaka kuhakikisha kuwa anakamilisha kazi yake ili hata akihukumiwa kifo basi awe amejiridhisha katika hilo.
Vibaraka wa Matinya waliendelea kumfuatili na wakagundua mara moja kuwa alikuwa amehifadhiwa na shoga yake Fasendy, siku hiyo usiku huo walipopanga kumvamia Fasendy ili wampate Yaumi, lakini walikosea, walipofika kwa Fasendy hawakumkuta Yaumi tayari alikuwa amekwishaondoka kuelekea Ubungo, baada ya kumpa kibano cha maana Fasendy hakuna walichoambulia zaidi ya kuelekezwa Monerumango. Lakini kwa akili za ziada waligawana kazi, wengine Ubungo na wengine Buguruni kufuatilia gari za kwenda huko Kisarawe mpaka Monerumango. Bingo ilikuwa kwa wale wa Ubungo ndiyo waliomuona Yaumi akichukua usafiri huo wa Akamba bus, baada ya taarifa hiyo kumfikia Matinya akaona wazi kuwa lazima kuna jambo haraka kabisa akatuma watu wawili akiwemo Scogon kwa ndege ya KQ ili kufika Kampala kabla yake na kuendelea kumfuatilia ili kujua nini anakifuata huko…
KAMPALA
SAA 5:15 ASUBUHI
BASI la Akamba lililokuwa likifanya safari zake kutoka Dar es salaam mpaka Kampala kupitia Nairobi liliingia katika stendi kuu ya mabasi ya kampala, Yaumi akiwa ndani ya jeans nyeusi, fulana nyekundu iliyobeba maandishi ‘Mbongo Halisi’ alijivuta taratibu kuingia mjini, kutokana na jua kua kali, aliipachika miwani yake na kuvuka barabara mpaka upande wa pili, akaingia katika moja ya mgahawa uliopo hapo na kuketi, akaagiza kinywaji, juice ya maparachichi iliyochanganywa na maembe kwa mbali, akawa anakunywa taratibu. Alijaribu kuvuta kumbukumbu ya jiji hilo tangu alipofika miaka kadhaa nyuma, alikumbuka tu kuwa yeye na mumewe walifikia kwa rafiki yake lakini hakukumbuka mtaa gani wala uelekeo wake, baada ya kuumiza kichwa sana kwa hilo, hakuona sababu kwa kuwa alichokitaka yeye kilikuwa ni kufika ofisi za posta tu na si kingine, hakujua kuna nini hadi afike huko lakini alitaka kuhakikisha anafika siku hiyohiyo. Akanywa juice yake haraka haraka na kunyanyuka, akatoka nje na kutafuta usafiri wa kwenda huko posta, kwa kuwa alikuwa hapajui ilimbidi kuchukua tax ambayo ingemfikisha moja kwa moja mahali anapopataka.
Dakika kama kumi na tano hivi, ile tax iliegeshwa karibu na office ya posta pembezoni mwa barabara ya Kampala, Yaumi akashuka na kumlipa Yule dereva kasha akatembea taratibu kuelekea geti la kuingia katika ofisi hizo, kitu kikubwa kilichokuwa kikimpa tabu ni lugha, watu wa Uganda walikuwa wakizungumza Kiganda na kiingereza tu, alisukuma mlango na kuingia ndani, mbele yake kulikuwa na mwanadada mweusi aliyesuka nywele zake katika mtindo wa kuvutia, Yaumi aliketi kiti cha mbele yake na kumtazama dada huyu,
“Habari!” alimsalimu, Yule dada akabaki kumtazama Yaumi.
“Are you a Tanzanian?” (Wewe ni Mtanzania?) alimuuliza. Kwa kuwa Yaumi hakuelewa anachoambiwa, alifungua kibeki chake na kutoa kikaratasi kidogo akampatia Yule dada, Yule dada akakiangalia na kuingiza zile namba katika kompyuta yake, kasha akamtazama Yaumi. Yule mwanadada akamuoonesha Yaumi ishara ya ufunguo kama anao, Yaumi akatikisa kichwa kuwa anayo funguo. Wote wawili wakaongozana mpaka upande wa pili wa jengo hilo, walipofika, Yaumi aliona zile namba zikiwa zimeandikwa katika moja ya vijisanduku vidogo vidogo. Akaichukua ile funguo na kuitumbukiza katika tundu husika, ndipo alipogundua nkuwa hakuwa peke yake, mkono wenye nguvu ulimkamata kiganja chake na kuzungusha ufunguo katika kile kisanduku. Yaumi aligeuka nyuma na kukutana na mwanaume mrefu kidogo mwenye tambo la haja, kidevu chake kilichafuka kwa ndevu zilizokaa kitambo bila kunyolewa, lakini zilizokolea mafuta kwa jinsi zilivyong’aa.
“Mbio za Sakafuni, huishia ukingoni, leo huna ujanja fungua chukua kilichomo turudi Tanzania kwa ndege ya usiku wa leo,” Yule bwana akamwambia Yaumi ambaye alikosa ujanja katika hilo, akafungua kile kisanduku huku moyo wake ukienda mbio kwani hakujua ni nini atakachokikuta ndani yake, akaingiza mkono lakini hamna kitu isipokuwa kadi ndogo iliyolala ndani yake, kwa bahati mbaya alipokuwa anataka kukichukua alikisukumia ndani kikadondoka kwa ndani, akautoa mkono wake, na kumtazama Yule bwana.
“Hakuna kitu, “ alimwambia. Yule bwana akajisahau akamvuta nyuma na na kutazama ndani ya kile kijisanduku, hamna kitu! Alipogeuka nyuma kumtazama Yaumi, hamna mtu. Akasimama akaanza kuangaza huku na huku kumtafuta mwanamke huyo. Akatoka pale aliposimama na kuwaendea vijana waliokuwa wakipiga soga mitaa hiyo na kuwauliza, wakamuonesha upande ule alioelekea, Yule jamaa akavuka barabara na kujaribu kutazama, akmuona Yaumi akiishia ndani ya jengo Fulani, akamuendea mpaka katika lile jengo, hakumuona, akaingia ndani, ilikuwa ni supermarket kubwa sana, watu wengi walikuwa wakifanya manunuzi yao wakiwa hawana hili wala lile. Yaumi alikuwa bado akimtazama Yule mtu kila hatua aliyokuwa akipiga nay eye akijificha nyuma ya mashelf ya bidhaa. Yule jamaa bado alikuwa akimtafuta Yaumi kila kona hakumuona. Yaumi aliwaendea askari wanaolinda mlango katika jengo hilo, na kuwaambia kuwa kiuna jambazi linalomfuata humo ndani linataka kumuibia, wale askari wakawaita wenzao ambao walikuwa maha;lip engine kwa kutumia redio zao za upepo, wakafika na kuwapa taarifa hiyo, Yaumi akawaonesha wale askari waliokuwa na virungu mikononi mwao, wakaingia kumfuata Yule jamaa. Wakati yote hayo yakifanyika Yule jamaa alikuwa akiwaona wanavyoongea na Yaumi pale mlangoni, akaona sasa hapa mambo yataharibika, hakujali alienda palepale mlangoni na kukutana na wale askari ambao walimzuia wakitaka kumkamata, purukushani zikatokea pale mlangoni, Yule bwana aliwakamata wale askari kila mmoja kwa mkono wake na kuwagongesha vichwa kasha akapita katikati yao na kutoka nje akiangaza macho huku na huku, Yaumi hayupo.
¤¤¤¤¤
ACP Chonde alikuwa ameketi na afande Magreth, wakibadilishana mawazo juu ya kazi yao, ugumu na wepesi wake.Chonde alimshirikisha Magreth juu ya ile barua na mwenendo mzima wa kesi ile ya Yaumi jinsi inavyokanganya.
“Sasa Yaumi yupo nje kwa dhamana,nani alimuwekea hiyo dhamana?” Magreth aliuliza
“Unajua hapo ndipo penye utata, nimefanya upelelezi wangu nimegundua kuwa hii kesi ina utata ndiyo maana nimekuita uniambie siku ile ya kwanza mliyoenda na kumkamata Yaumi ni nini mlikigundua?” ACP Chonde alimuuliza Magreth. ASfande Magreth akatulia kimya kidogo na kukumbuka tukio la siku ile, simu iliyoita pale kituoni, ikisikika maneno machache “…mke wangu, mke wangu, ananiua…”, alikumbuka walipofika pale na kumkuta Yaumi akiwa ameshika kisu na bastola pembeni mwa mwili wa marehemu akiwa amechafuka kwa damu kutokana na majeraha ya marehemu. Alama za vidole zilizochukuliwa katika kitasa cha mlango na sehemu zilizotakikana zilikuwa za Yaumi. ACP Chonde akatikisa kichwa kwa taarifa hiyo, na ni kweli upelelezi uliokamilika ndiyo huo.
“Nimepata hii barua asubuhi ya jana,” Chonde akaitoa ile barua na kumpa Magreth, akaisoma, na kumrudishia.
“Kuna mkono wa mtu,” Magreth alisema, “Nasema hivyo kwa sababu hata m I nimeona vikwazo vingi sana katika upelelezi wetu, unajua ile gari iliyoungua kule Salasala na mtu mmoja kufa ni Yaumi aliyeua baada ya kuichunguza kwa kina ile gari iliypungua, ndiyo ileile iliyomchukua pale mahakamani, kifo cha Yule mtu mmoja pale nyumbani kwake ni yeye aliyeua kutokana na kwamba hakuna mtu anayejua wapi funguo ya pili ilipo au inapofichwa, hatukuaokota ganda la risasi lakini mtaalamu wa majeraha ya risasi amesema lile jeraha la marehemu ni Colt 45, na hiyo ndo silaha ambayo alikuwa anamiliki Marehemu kajiba, mpaka sasa haijapatikana na haijulikani ilipo,” Magreth aliongea kwa kirefu sana.
ACP Chonde alitikisa kichwa kukubaliana na hilo, sasa alikuwa amefunguka kimawazo katika tukio hilo, “Kwa kuwa hawataki niendelee kuchunguza, basi sasa nitachunguza nani yupo nyuma ya hili,” Chonde alimwambia Magreth.
“lakini angalia kama kuna wazee nyuma yake wasije kukukatiza maisha” Magreth alimuasa Chonde. “Ah potelea mbali tutaogopa mpaka lini?!” Chonde aling’aka.
“Kesi itasomwa tena siku mbili zijazo, unajua mtuhumiwa hayupo hapa,” Magreth alisema.
“Umejuaje?” Chonde akauliza.
“Tulikuwa tunafuatilia tujue kinachoendelea, hayupo kila kona,” magreth alijibu.
Magreth na Chonbde waliongea mengi sana siku hiyo mwisho wakaamua waunganishe nguvu kufuatilia sakata hilo iwe kwa shari au kwa heri.
¤¤¤¤¤
Ilikuwa ni katika kijia kimoja ambako Yaumi alikuwa katika harakati za kujiokoa jioni ya siku hiyo, mara ghafla mbele yake vijana watatu walisimama kumzuia njia alipotaka kugeuza arudi alikotoka Yule mtu anayemfuata naye alikuwa anakuja. Yaumi alisimama, mara wale vijana ambao mmoja wao anamfahamu fika walikuwa wakimjia pale alipo, Yaumi alichomoa bastola yake na bila kukosea maana al;ijua hapa ni ama zao ama zangu, risasi ya kwanza ilimpiga kijana mmoja kifuani ikamtupa huko, watu wakaanza kupiga makelele kuwa majambazi wamevamia eneo hilo, kizaazaa, wale waliobaki walijikuta wanashindwa kumdhibiti Yaumi, alipojaribu kufyatua risasi nyingine, lol, bastola imeishiwa, haina risasi, kumbe ilibaki moja tu na alisahau kujaza nyingine.
Kabla lolote halijafanyika, gari ya polisi ilifika eneo hilo wakashuka na kuanza kumkimbiza Yaumi ambaye alikuwa na bastola mkononi, kila walipompigia kelele asimame, yaumi hakutii, alikimbia na nyuma akifuatiwa na polisi, polisi walipoona hatii amri, mmoja wao akaamua kutumia risasi, akafyatua ya kwanza ikapiga kiatu na kumparaza kidogo wayo wa mguu wake, yaumi akaanguka chini, wakamfikia na kumtia pingu. Mtaa mzima uligubikwa na kelele za wapiti njia waliokuwa wakishuhudia tukio lile.
Polisi wa kampala walimchukua Yaumi na kumytia kwenye gari, pembeni alikuwa akiwaona wale watu waliokuwa wakimfukuza, aliwaangalia kwa jicho baya lililowaambia kuwa ‘dawa yenu ipo jikoni’.
Gari ya polisi iliondoka taratibu huku kelele za watu bado zikiwa zikipaa hewani. Yaumi alifikishwa katika kituo cha polisi kikuu pale Kampala na kutupwa ndani. Polisi waliomchukua Yule aliyepigwa risasi walitoa ripoti kuwa Yule bwana alifia palepale kwani risasi ile ilipita kwenye moyo. Mkuu wa kituo kikuu cha polisi alitulia kimya kwa muda, akaiangalia kile bastola aliyotumia Yaumi ambayo ilikuwa kwenye mfuko wa plastic, kasha akachukua hati za kusafiria za Yaumi ndipo alipogundua kuwa mwanamke huyo ni Mtanzania. “Tangu lini Watanzania wakawa na tab ia ya kuchezea silaha ovyo namna hii? Kwa jinsi walivyo waoga,” aling’aka Yule bwana mkuu wa kituo. “Nileteeni huyo mwanamke hapa,” aliamuru na Yaumi akaletwa mbele yake, wakatazamana. Yule mkuu wa kituo aliishuhudia sura ya kisasi ya Yaumi, iliyojaa hasira na uchungu, “Wewe ni nani?” akamuuliza.
“Yaumi, kutoka Tanzania,” Yaumi alijibu baada ya kuona mkuu huyo anajua Kiswahili japo cha kuombea maji.
“Kwa nini unafanya ,mauaji ya holela kwenye mitaa ya mjini wewe, wewe ni jambazi?” Yule mkuu alimuuliza Yaumi.
“Mimi sio jambazi, wala sipendi kutumia silaha, lakini nilikuwa najilinda dhidi ya watu waliokuwa wakinifuata kutokea stendi kuu ya mabasi,” akajibu.
“Ina m,aana wewe umefika leo hapa? Umefuata nini?” Yule mkuu aliuliza
Yaumi alitaka kujibu lakini akasita, akanyamaza kimya, akamtazama Yule mkuu wa kituo.
“Kwa kuwa umefanbya mauaji ndani ya nchi hii, sheria ya Uganda itakuhukumu na ikibidi utafungwa hapahapa” Yule mkuu alisema hayo na kunyanyuka akaamuru Yaumi arudishwe mahabusu….
YAUMI alirudishwa mahabusu, uso wake wote ulisawajika kwa matatizo yanayomkabili, ‘Heri ningekuwa Tanzania, ningepata wa kunisaidia, huku ananijua nani?’ alijiuliza na kuanza kulia kwa vikwifukwifu, kumbukumbu za mume wake zilirudi kichwani mwake upya kabisa akimkumbuka kwa mema yote aliyokuwa akimtendea kwa upendo mkuu. Alikumbuka alipokuja mara ya kwanza na mumewe Kajiba katika jiji hilo la Kampala, majengo marefu na mazuri yalimlaki kama mgeni mashuhuri, maisha ya raha katika mahoteli makubwa yalimfanya ajisikie peponi lakini leo hii ule ubaya wa mji huo uliojificha nyuma ya majengo yake mazuri ulimtokea waziwazi mbele yake, Yaumi alishindwa kuamini kile kinachotokea kwake kwa wakati huo, afanyeje? Hakuna la kufanya alijikunyata hapo alipo pamoja na wanawake kadhaa waliorundikwa katika chumba hicho cha mahabusu.
˜˜˜˜
TAARIFA za kukamatwa Yaumi zilifika siku ya pili katika makao makuu ya polisi Tanzania, mkuu wa kitengo maalumu cha kushughulika na Watanzania wanaokamatwa nje ya nchi kwa makosa mbalimbali aliipokea fax ya kukamatwa Yaumi baada ya kufanya mauaji hadharani katika nchi ya kigeni, kumiliki bastola ambayo hakuwa na vibali nayo kinyume cha sheria, taarifa ilisema kuwa mwanamke huyo atapandishwa kizimbani katika mahakama kuu ya Kampala kusomewa mashitaka yake baada ya masaa 24 kupita, zaidi ya hapo taarifa hiyo iliomba msaada wa polisi wa Tanzania kufikisha taarifa zozote kama mtu huyo ana makosa mengine au la.
‘Yaumi,’ Yule bwana alilifikiria hilo jina, akawasha kompyuta yake na kuingiza jina hilo kisha kuita kama kuna maelezo yoyote juu yake katika idara za usalama. Hakutegemea lolote lakini alishangazwa na faili lililofunguka mbele yake, lenye jina na picha ileile iuliyotumwa kutoka Kampala, hakuamini, aliitazama kwa makini, ‘Du, kumbe kuna wanawake Tanzania ni maninja!’ alijisemea peke yake ndani ya ofisi hiyo, akanyanyua simu yake na kuwasiliana na mwanasheria mkuu wa jeshi la polisi nchini na kumuomba kuonana nae, akakubaliwa. Yule bwana akakusanya ile fax na kuitia bahashani kisha akaelekea ofisi iliyopo kama mlango wan ne hivi kutoka yake katika jengo hilohilo la makao makuu ya polisi.
Meza moja ilikuwa katikati yao walipokuwa wakizungumzia swala hilo, “Huyu dada ana kesi pale mahakama kuu, na yupo nje kwa dhamana, hakutakiwa kutoka nje ya Dar es salaam,” alizungumza Yule mwanasheria mkuu wa jeshi la polisi, akajivuta kwa mbele kidogo na kumuinamia Yule bwana, “Hilo tayari ni kosa linguine, kesho anatakiwa asomewe shitaka lake tena pale Kisutu, wape hiyo taarifa halafu tutaona wanasemaje ili tuweke mambo sawa,” alimwambia, kisha wakaagana na kila mmoja kubaki na shughulio zake
Bwana Matinya aliketi ofisini mwake akiwa na mawazo mengi sana juu ya habari aliyoipokea, hakuamini alichoambiwa na Scogon kilichotokea huko Kampala, unyama alioufanya Yaumi, jambo lililomchanganya zaidi ni Yaumi kukamatwa, ‘Harakati zetu zitaishia wapi?’ alijiuliza huku akikunakuna tumbo lake kubwa na kubembeabembea kwenye kile kiti chake. Kwa ujumla hakuwa na raha siku hiyo, kila mlango ulipogongwa yeye moyo ulimwenda mbio, akiwaza labda watu wa usalama au sijui nani, kwa kuwa alijua dhambi inayomtafuna. Akanyanyua simu yake na kupiga namba Fulani, “Hey, Scogon, achana na huyo Malaya, panda ndege na mwenzio mrudi mara moja huku tupange plan B maana naona hiyo A imefeli, ila kitu kimoja kabla hujaondoka hakikisha unamulika ofisi ya posta ambayo huyo mwanamama alikwenda, fanya hima nasubiri habari,” kisha akaizima simu bila kusubiri jibu na kuitia mfukoni. Akanyanyuka kitini lakini kabla hajaondoka akakumbuka kitu, akaiwasha tena ile simu na kumpigia afande Marina na kumuomba wakutane chumba chao cha siri kwani alikuwa na mazungumzo ya falagha.
˜˜˜
Jioni ya siku hiyo ilimkuta ACP Chonde katika zahanati ndogo ya jeshi la Magereza pale Segerea, akitazamana uso kwa uso na Dr Omongwe, sura zilionesha wazi kama kuna kitu ambacho hakiendi sawa mahala hapo.
“Lakini wewe si nilishakupa jibu, unataka maelezo gani tena kutoka kwangu?” Omongwe alimwambia Chonde.
“Sikatai, lakini dada yangu nataka nikwambie kitu, kitu ambacho hakuna anayekijua ila mimi nakihisi nah ii itamsaidia Yule mwanamke mwenzako,” Chonde alimlainisha Omongwe kwa namna ya pekee.
“Kitu gani?” Omongwe aliuliza lakini kabla hajasema lolote, mara mlango ukafunguliwa afande Marina akaingia ndani ya ofisi ile bila hata kukaribishwa.
“Eh, jamani hugongi hodi!?” Dr Omongwe akauliza.
“Nigonge hodi hapa chumbani au chooni, nomba ule mzigo wangu maana naona huko na shem nisiwapotezee muda mie…” Marina alisema hayo huku macho yake yakitazamana na Chonde na kila mmoja kumsoma mwenzake kwa kina, alipopewa anachotaka akaondoka zake.
“Wambea wenyewe ndio hawa,” Dr Omongwe alimwambia Chonde. “Ok, unatoka kazini saa ngapi nataka tuonane mahali maana hapa hapana usalama kwa mazungumzo yetu,” Chonde alimwambia Omongwe. “Bado kama lisaa limoja hivi,” Omongwe akajibu. “Sawa, wapi tunaweza kuonana nikakusubiri?” Chonde akauliza. Dr Omongwe alishusha pumzi na kumtazama Chonde usoni, “Sikia, mi ni mke wa mtu, siwezi kukaa ovyo na mwanaume mahali popote pale zaidi ya nyumbani kwangu, kwa hiyo kwa hilo itakuwa ngumu kaka, we zungumza hapahapa” Omongwe alimwambia Chonde.
“Yaumi amekamatwa Kampala, anashikiliwa na polisi wa huko na kesho anapanda kizimbani kwa kosa la kuua,” Chonde alimwambia kwa sauti ya chini, Omongwe alishtuka na kujishika kifua kwa uchungu, “Masikini Yaumi,” alisikitika. “Yaumi una nasaba nae?” Chonde akamuuliza, badala ya kujibu Omongwe alianza kuangusha machozi, “Masikini Yaumi,” aliendelea kusikitika kwa hilo, “Ni rafiki yangu sana, nilikuwa naye jeshini JKT,” alimueleza Chonde. “Basi ndio hivyo, sasa unafikiri shoga yako utamsaidiaje kwa hilo?” akauliza tena Chonde. “Chonde, naomba nitafute kesho mchana tulizungumze hilo sasa hivi siwezi kufanya maamuzi,” alijibu Omongwe na kumuomba Chonde aondoke.
Akiwa katika pikipiki yake aina ya Kawasaki, Chonde alikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu, alitafuta ukweli hasa wa kujua ni nini kinamfanya Yaumi kufanya mauaji hayo katika mtindo huo, ilikuwa haingii akilini. Akiwa bado na mawazo hayo, hakuangalia vizuri barabara ile ya Baracuda, gari moja aina ya Spacio ilifunga breki kali sana na kumfaya Chonde kuyumba vibaya na kuingia mtaroni, watu wakajaa eneo lile lakini kwa kuwa pikipiki ile ilikuwa na maandishi ‘POLISI’ wakamsaidia kumuinua na kumtoa eneo lile.
Daktari Omongwe alitoka kazini majira ya saa kumi na mbili za jioni na kumuachia mwenzake Kinyerezi, kichwa chake kilikuwa kikifanya kazi ya ziada, kwanza kwa nini Chonde arudi tena kumuuliza maswali yale au kutaka kujua nini zaidi kwake juu ya Yaumi, hakujielewa afanye nini, alijitupa kitandani na kupitiwa na kausingizi katamu.
˜˜˜
AFANDE Marina alifika maeneo ya Mbagala kuu mida kama ya saa mbili usiku hivi, akaegesha gari yake katika kituo kimoja cha mafuta katika eneo hilo kisha akavuka barabara na kusubiri kidogo, haikuchukua muda ilikuja gari ndogo nyeupe, hakuwa na haja ya kuuliza, alifungua mlango wa nyuma na kuingia, ile gari ikaondoka.
Baada ya kukatisha mitaa miwili mitatu, ile gari ikasimama mbele ya nyumba moja nzuri iliyojengwa kwa na kuwekwa naksi za kisasa, “Asante kijana,” Marina alishukuru na kushuka garini kisha akaingia katika nyumba hiyo, moja kwa moja katika mlango alioukusudia, akajifungia. Haukupita muda mlango mwingine ukafunguliwa nao ulikuwa ukiendea chumba hicho, bwana Matinya akajaa ndani akiwa hoi kwa uchovu, alivua mkanda wa suruali yake na kuutupia pembeni, viatu akabwaga huko, akafungua jokofu ndogo na kutoa pombe kali GIN akanywa karibu nusu chupa bila kuzimua, mambo yote hayo Marina alikuwa akimtazama tu, alijua wazi mzee huyo siku hiyo hakuwa sawa kama alivyomzoea, lakini alisubiri muda muafaka wa kumuuliza.
Alipomaliza kugida mchupa huo, akaukita chini kwenye meza, akamtazama Marina na kufungua kinywa chake, “Tukileta mchezo tumekwisha!” akamwambia. Marina akamtazama tena na kumtupia swali, “Kuna nini mpaka useme hivyo?”
“Yaumi, amekamatwa Kampala, ameua mmoja wa jamaa tuliemkodi kule ili amfuatilie, sasa endapo polisi wa kule wakisema walivalie njuga ili swala siri itafichuka,” Matinya alimjibu. “Mh, ina maana hizo Kabrasha ziko Kampala?” Marina akauliza. “Nafikiri, kwa nini Yaumi aende Kampala? Na moja kwa moja aende posta? Napata mashaka, kama zipo humo posta na akisema hilo wakazikuta, Marina, sijui tutajificha wapi” Matinya alionge kwa uchungu uliochanganyika na hasira, akanyanyua tena ile chupa yake na kujimiminia kinywaji kile kikali bila kuzimua, akaishusha kwa mtindo uleule.
“Sweetie, nina habari mpya hapa!” Marina alianza kuingiza umbea wake. Sentensi hiyo ilimgutusha matinya kutoka kwenye mawazo yake, “Unasemaje, habari gani hiyo?” akauliza. “ACP Chonde, alikuwa magereza leo akiongea sana na Dr Omongwe, nahisi kuna kitu,” Marina alizungumza. “Aaaa Chonde, ina maana ile barua hajaipata au ni mkaidi wa moyo? Namhitaji haraka sana niongee nae, hawezi kuingilia maswala nyeti kama haya wakati yeye ni kisisimizi kidogo tu,” akanyanyuka na kuchukua simu yake akapiga namba fulani kisha akaweka sikioni, “Chumba cha siri tafadhali,” akakata simu, kisha akajiegemeza katika sofa lile akipiga mluzi, akiwa katika hali hiyo, simu yake ilipata uhai, meseji ya maandishi ikaingia, akaichukua na kuisoma,
“… JNIA…” akasisoma kisha nay eye akajibu, “Chumbani haraka,” akaitupia pembeni ile simu. Marina alikuwa ametulia tuli akitazama kila kinachoendele, bado mpaka dakika hiyo Marina hakujua hasa ugomvi wa Yaumi na huyu hawara yake, Matinya, alikuwa akishobokea tu bila kujua lililopo. Siku hii akaamua kuyavulia maji mnguo akamuuliza Matinya, “Hivi bebi wangu, mi mpaka leo sijajua kwa nini mna bifu na Yaumi wakati Yule ni muuaji tu?”
Matinya alimwangalia kwa jicho kali sana Marina, akaigeuzageuza sura yake tayari pombe zilikuwa kichwani, “Wewe unachotakiwa ni kufuata ninalokwambia, kuniburudisha kitandani, na kufanya ninachotaka, swala la Yaumi na mimi liache, utalijua siku ya mwisho nitakapokununulia ghorofa na helikopta au utakapokuwa jela ukisubiri kitanzi cha mwisho,” akanyanyua tena lile chupa na kugida kwa mtindo ule ule, alipolitua tena mezani akamwuliza Marina, “Au una tatizo? Sema, kama kuna tatizo utapatiwa ufumbuzi haraka,” akabaki akimtazama. “Hapana mpenzi sina,” Marina akajibu. “Ok vizuri kama huna, hebu njoo hapa nilipokaa uichezeechezee na kuinyonyanyonya hii ndungula nahitaji burudani ya kusahau matatizo yangu, asubuhi inafika hiyo.” Marina akanyanyuka kwenye kochi lake na kuhamia kwa Matinya, taratibu akamfungua zipu ya suruali na kulichoropoa lile lililopo ndani. Mara simu ya Matinya ikaita…..
“Aaaaah, nani tena watu tupo kwenye starehe zetu,” Matinya alisema huku akiinua simu yake iliyokuwa mezani na kumsogeza pembeni Maria. “Yeah kijana (…) Ok umefika? Sawa nisubiri hapo dakika 2 tu,” Matinya akanyanyuka na kumuacha Marina pale kwenye kochi kisha yeye akapotelea kwenye mlango Fulani ambao kwa jinsi ulivyojengwa, hupita chini ka chini kama handaki na kutoke nyuma ya tatu mtaa wa nyuma, huko utokea mlango ambao waishio humo siku zote hujua ni chumba chake cha kulala, kwa kuwa hakuna hata mmoja ambaye aliwahi kuingia ndani humo zaidi ya mfanya usafi ambaye pia huingia kwa nadra sana. Akatoka nje na kuiendea gari moja ndogo iliyoegeswhwa karibu kabisa na duka kubwa la vinywaji, alipofika alifungua mlango wa gari hiyo na kujitoma ndani katika kiti cha mbele.
“Sikia kijana, kuna kazi ndogo sana ya kufanya, katika kituo cha polisi cha Tabata Kimanga kuna mtu anaitwa ACP Chonde, chukua vijana, peleleza anapopatikana, kisha…” akamuonesha ishara ya kukata kuua kwa kutumia kidole gumba chake cha mkono wa kulia kukikatisha shingoni mwake, “Pesa?” Yule kijana akauliza. “Kama hauna swali basi husingeuliza,”Matinya akamtupia bahasha moja ya khaki na yeye akaondoka zake.
Alipofika katika kile chumba chake alichomuacha Marina peke yake sasa alikuta na wengine wawili wanaume, Scogon na Simbila walikwishajumuika pamoja nao. “Marina tupishe kidogo,” Matinya alimuamuru Marina ambaye aliingia chumbani. “Nipeni habari,” Matinya aliendelea.
“Habari si nzuri kama tulivyokwambia, jamaa tuliekodi kwa pesa nyingi lakini amezidiwa na Yaumi, sasa hatuna kazi nae kwa kuwa Yaumi yuko mikononi mwa polisi,” Scogon aliongea.
“Na aliyeuawa ni nani?” matinya akauliza
“Aliyeuawa ni mtu mwingine katia wale tuliowapanga kufanikisha zoezi hilo,” Scogon akaeleza. “Ok, na ile kazi nyingine je mmetekeleza?” Matinya akaendelea kuuliza kwa shauku. “Bila shaka mzee tumeweka kitu cha masaa hivi nyuma yetu kitanuka tu, we kodoa jicho luningani,” Scogon aliendelea kutoa ripoti ya kazi, “Mmetumia njia gani ambayo mna uhakika haitaweza kugundulika Simbila?”
“Mzee, tumetumia mbinu nzuri tu, kwa Yule mwanamke aliiacha funguo katika sanduku lake la posta, kwetu ilikuwa ni nafasi nzuri sana, baada ya kuhakikishwa amewekwa nguvuni na kama ulivyotupa maagizo tulimuweka mtoto ndani ya sanduku lilelile tukamuacha humo tukiwa tumeshampa maelekezo ya muda gani wa kuamka,” Simbila alieleza hayo kwa Boss Matinya. “Sawa, sasa kuna mtu anaingia anga zetu anaitwa SCP Chonde,” wakati Matinya anasema hayo Scogon akamkatisha, “Chonde wa Kimanga?”, “Ndiyo, uyo huyo, nimemtuma kijana akammalize haraka iwezekanavyo, ninyi mnajua hii ishu ilivyo nyeti, sasa hapa kila anayeonekana kujua ni kumpoteza tu, sawa jamani? Mimi kesho nina kikao nyeti na wazee kisha nitawapa taarifa”
Baada ya kikao hicho kifupi, Scogon na Simbila waliondoka zao, Matinya alibaki juu ya kochi lile lenye raha zote za dunia, akafungua vishikizo vya shati lake na kuruhusu tumbo lake lote lionekane ukubwa wake, alihisi kama kijasho kikimtoka, mawazo yalikusanyika, akaona wazi kuwa sasa kama ni arobaini basi zinakaribia kutimia, wakati mwingine alijipa faraja lakini kila alipokumbuka kuwa ni vipi likibumbuluka alikosa raha na alihisi tumbo lake likisinyaa ghafla. Gabriel Matinya, kigogo wa idara nyeti ambayo hata ukiambiwa huwezi kuamini, aliigeuka kazi aliyokabidhiwa na mheshimiwa Rais na kufanya yale anayoyajua yeye akishirikiana na vigogo wengine wenye dhamana. Alijiinua pale kochini na kuingia mlango wa chumbani, huko alimkuta Marina keshapitiwa na usingizi muda mrefu, ‘Wanawake wengine bwana, wavivu, ona sasa keshalala,” alijisemea moyoni kisha akjitupa na yeye kitandani, ukizingatia tayari alikuwa na pombe za kutosha kichwani haikuwa kazi kuukusanya usingizi.
KITUO CHA POLISI KATI – KAMPALA
“Tuambie kulikuwa na nini katika sanduku lako la posta hapa Kampala?” askari mmoja aliuliza huku akizungukazunguka kiti ambacho Yaumi alikuwa ameketishwa, kiti cha chuma. Yaumi alikuwa amegeuzwa na kufungwa katika kiegemeo chake, fulana aliyovaa iliondolewa akabaki wazi sehemu yote ya juu. Askari Yule wa kike aliyevalia sare nadhifu ya kipolisi alikuwa akizunguka huku na huko wakati Yaumi akiwa hoi katika kile kiti, damu ambazo hazikujificha zilichirizika kutoka majeraha ya waya ule aliokuwa akiutumia Yule askari kumchapa ili aseme. “Sijui, Sijui, nilikuja kuona kuna nini lakini sikukuta kitu,” Yaumi aliongea kwa tabu sana, maana hata kichwa tu alishindwa kunyanyua, “Wewe ni Mtanzania gaidi siyo?” Yule askari akauliza tena na wakati huo waya ulitua mgongoni mwake, Yaumi alijikunja mgongo kwa maumivu lakini haikumsaidia kwani hakuweza kufikisha mkono wake mgongoni japo kuyafariji majeraha yake.
Pamoja na mateso yote aliyoyapata kwa masaa zaidi ya mawili katika chumba hicho, Yaumi hakuweza kusema lolote kwa kuwa kiukweli alikuwa hajui nini kilikuwa katika box la posta la mumewe. Yaumi alitolewa katika kile chumba akiwa hoi kwa kipigo, hakuweza kujimudu kutembea, wale askari wengine wa kike waliokuwa katika chumba kile walimfungua kitini na kumburuta mpaka katika selo ile aliyowekwa mwanzo wakamtupia huko na fulana yake wakamtupia pia, Yaumi alijilaza kama mfu.
Katika kituo hichohicho cha polisi kati jijini Kampala kulikuwa na kikao kikiendelea katika moja ya ofisi zilizopo ghorofa ya juu yake, wazee wawili na mwanamama mmoja alieonekana ndiyo mkubwa wao walikuwa na mazungumzo mazito. “Hivi mnavyoona huyu mwanamke anajua juu ya hili kweli?” Yule mama aliuliza, “Kwa kweli kwa mateso aliyoyapata hata angekuwa gaidi angesema, nahisi hana hatia, ila yamemkuta,” mzee mwingine alijibu, “Lakini hata hivyo haitaeleweka kwa kuwa lile bomu kadiri ya uchunguzi wa awali limelipukia katika box lake la posta, nani atakuelewa kuwa yeye ahusiki?” kweli ulikuwa mjadala mzito sana kati ya wazito hao, mjadala uliokuwa ukiendelea katika ofisi hiyo usiku wa manane. Mkutano huo na mateso makali ya Yaumi vilikuja baada ya mlipuko uliotokea katika ofisi hizo za posta katikati ya mji, hakuna kifo kilichopatikana kwa kuwa wafanyakazi wote hawakuwapo muda huo, lakini mali na nyaraka nyingi ziliungua na kuteketea kabisa. Ilikuwa ni hali ambayo kiukweli iliwachanganya viongozi wa usalama wa Uganda usiku huo, ilikuwa hakuna kulala. “Hujuma, hii ni hujuma,” Yule mwanamama alikuwa akiwaambia wenzake, “lakini hujuma itakujaje kufanywa na Mtanzania? Hapana huu ni ugaidi,” kila mmoja katika kikao hicho alikuwa akitoa maoni yake kadiri ya upeo wake wa kazi.
Kazi ya uokoaji na uzimaji wa moto ilikamilika alfajiri ya ya siku iliyofuatani baadhi tu ya vitu ambavyo viliokolewa, mara moja uchunguzi wa kina juu ya moto huo na wahusika wa tukio hilo vilichukua kasi.
KULIPOKUCHA – SAA 2:00 ASUBUHI
Jiji la Kampala lilikuwa katika pilikapilika zake kama kawaida, waliokuwa wakiwahi kwenda kazini walifanya hivyo na wale wa biashara nao walifungua maduka yao, kilichoshangaza siku hiyo ni zile sehemu za kuuzia magazeti, ama ukute hazina gazeti la habari na kubaki yale ya michezo au ukute kundi la watu wakiwa wanaongelea tukio la jana yake usiku, tukio la moto katika ofisi za posta.
Ilikuwa ni asubuhi hiyo ambapo bwana mmoja katika mitaa ya ya nje kidogo ya jiji la Kampala alipoamka kwa kuchelewa sana, akiwa bado hajatoka kitandani mkewe bi Eliza alikuja chumbani kwa kasi kidogo na kuingia bila hodi, “We nini?” Yule mwanaume aliuliza. “Yaliyojiri huko mjini mume wangu, mi naogopa,” aliongea Yule bi Eliza sasa akiwa kamrushia gazeti mumewe. Bwana Godfrey Kyomukama hakuamini kile anachokiona, picha ya juu katika gazeti ilikuwa ni yaule moto wa usiku wake wakati habari yenyewe ilibebwa hujuma. Alipofngua kurasa ya ndani ndipo akakutana na picha Yaumi, aliisoma habari ile kwa makini sana, akamkumbuka shemeji huyo na akayakumbuka maneno ya rafiki yake bwana Kajiba
“…hifadhi huo mzigo, mpaka nitakapouhitaji, laity mimi nikifa basi mke wangua anaweza kuuhitaji…”
Ulikuwa ni ujumbe ambao aliuambatanisha na briefcase hiyo ndogo. Iliyotumwa kwa njia ya posta kwa jina na anuani ya Godfrey Kyomukama, lakini hakuweza kuifungua briefcase kwani alikuwa hajui code namba zake, aliuchukua na kuuhifadhi vizuri sana katika chemba yake ya kuhifadhi vitu vya thamani. Alinyanyuka kitandani na kuvuta hatua mpaka kwenye picha kubwa sana iliyopambwa ukutani, akaisukuma kidogo na kubofya namba Fulani katika ukuta huo kijimlango cha chuma kikafyatuka, akaufungua vizuri na kutazama ndani, briefcase ndogo nyekundu ilikuwa ndani ya chemba hiyo juu yake ikizibeba noti nyingi za kizungu. ‘Wakati umefika!’ alijiwazia bwana Kyomukama na kurudi kitandani, sasa akawasha televisheni na kutazama kile kinachooneshwa asubuhi hiyo, alishindwa kuvumilia alioga haraka haraka na kumuaga mkewe hata hakujali kunywa chai, aliingia kwenye gari yake na kutokomea mjini. Breki ya gari ya bwana Kyomukama ilikanyagwa sawia katika maegesho ya jengo la mahakama ambako umati wa watu ulikuwa umekusanyika kushuhudia huyo gaidi wa kike kutoka Tanzania aliyesemakana kutega bomu katika ofisi za posta. Aliteremka na kujaribu kupenyapenya kati ya vijana wengi waliojazana mahali hapo. Hatimaye alifika mahali ambapo angeweza kumuaona kama si kumshuhudia shemeji yake, Yaumi, akiletwa hapo, haja kubwa ni kuhakikisha kama ni kweli ni yeye au la. Haikuchukua muda, king’ora cha gari ya polisi kilisikika na kupewa heshima zake kwa kupisha njia, ile gari aina ya Toyota Land Cruise ilisisimama karibu kabisa na mlango wa jengo hilo, vurugu kubwa ikiatokea watu wakitaka kushuhudia hilo.
Bwana Kyomukama alikuwa ni mtu tajiri sana katika Kampala, alikuwa akimiliki maduka makubwa ya nguo na spea katika miji mbalimbali ya Uganda, alifahamiana na bwana Kajiba miaka karibu kumi nyuma walipokutana katika mambo yao ya kibiashara huko Kisumu nchini Kenya, wakatokea kuelewana sana hata kuwa kama ndugu, familia hizi zilikwishakutembeleana japo mara moja, hata watoto wao walikuwa wakisoma shule moja huko USA.
Ilikuwa ni wakati wa maumivu sana ya moyo kwa Bwana Kyomukama alipomuona shemejiye akiteremshwa garini na polisi watatu wa kike, hali aliyokuwa nayo ndiyo ilikuwa ya kushangaza, hakuweza kutembea kwa nguvu zake, akajuaa lazima mateso makali yamempata kwa maana aliwajua fika polisi wa Uganda. Akatoka katika lile kundi la watu, waliomjua walimpa heshima yake na wasiomjua walimkatalia hata pa kupita. Sliingis kwenye gari yake na kuketi kimya huku kiyoyozi kikimpa faraja, alichukua simu yake na kupoga namba ya Kajiba, haikujibiwa, haikuwa mara ya kwanza, karibu wiki kadhaa sasa, lakini hakujua bwana Yule ni nini kimempata, akatulia akavuta subira….
KYOMUKAMA alifikiri kumtafuta mkuu wa jeshi la polisi pale Uganda ajaribu kuongea nae, lakini akili yake ilikataa kabisa kwa kuwa alijua kama atafanya hivyo basin a yeye ni rahisi kuingia katika wimbi hilo akaonekana ni moja kati washiriki. Ijapokuwa aliumia sana moyoni, alitamani kumsaidia shemejiye lakini alikuwa hana jinsi, hana la kufanya, machozi yalimlenga, akawasha gari na kuondoka kwa kasi kurudi nyumbani.
Alipofika alimkuta mkewe ameketi kwenye kochi akiangali matangazo ya luninga na habari iliyotawala ilikuwa ni ile ya mlipuko wa ofisi ya posta, “Karibu mume wangu,” alimkaribisha mumewe huku akimshika mkono na kumuongoza chumbani akamkumbati mara baada ya kuufunga mlango nyuma yake. “Niambie mume wangu, ni yeye?” akauliza mkewe.
“Ndiyo ni shemeji Yaumi, lakini nashindwa nimsaidieje?” Kyomukama akajibu.
“Kwa nini? Mbona mkuu wa polisi ni rafiki yako sana na pia Yule jaji, wale ukiongea nao nafikiri watamsaidia,” mke wa Kyomukama alishauri. “Mke wangu unayoyasema ni sahihi, lakini kumbuka kuwa kesi yenyewe imeshaitwa ya kigaidi sasa tukijiingiza na sisi tutawekwa chini ya uchunguzi halafu balaa linguine litazuka, hapa cha kufanya tusijihushe, ila tufanye maombi,” Kyomukama akashauri na punde si punde maombi yalianza kuifunikiza nyumba ya Kyomukama, kumuomba Mungua avunje minyororo ya shetani.
§§§§§
Kama kuna kesi iliyovuta maelfu ya watu ni siku hiyo katika jiji la Kampala ni hiyo ya Yaumi, kila mmoja alitaka kumuona huyo mwanamama anayesadikiwa kufanya uhalifu huo. Waandishi wa habari wa magazeti, redio na televisheni walikuwa pale, mashirika kwa mashirika, kila mmoja alitaka habari ambayo gazeti lake au kituo chake cha redio kingevuta macho ya wananchi. Kila kona Yaumi alijaa katika midomo ya watu.
Akasomewa mashitaka matatu, la kwanza ni kumiliki silaha kinyume cha sheria za Uganda, la pili kutekeleza mauaji kwa silaha hiyo na la tatu kutega bomu ndani ya ofisi ya posta. Yaumi hakuna alichoongea zaidi ya kulia muda wote akiwa hajiwezi kwa njaa na kiu. Baada ya kesi hiyo kughairishwa Yaumi alipelekwa katika gereza la Luzira kusubiri mwezi unaofuata ili asomewe tena kesi hiyo kwa mara ya pili. Yaumi alikuwa mpole kama kondoo anayepelekwa machinjioni, akaswekwa ndani ya moja ya selo za mahabusu katika gereza hilo, akiwa peke yake kwani alitenganishwa na wenzake kwa sababu maalumu.
Akiwa amejibanza katika kona moja ya kijichumba hicho, Yaumi alitulia tuli kama maji ya mtungini akitafakari hili na lile, akiwa katika tafakari, mbele yake aliiona taswira ya mumewe aliyekuwa akiongea nae, alimwambia maneno mengi sana ya faraja. Yaumi alibaki akilia nguo yake ilijazwa na machozi, alipoinua sura yake hakumuona tena Yule mtu isipokuwa kipepeo kidogo chenye rangi nyrusi na madoa ya njano kikirukaruka huku na huko, alikiangali kile kipepeo na kutabasamu, kile kipepeo kikaja na kutua katika mikono yake aliyoikutanisha mbele ya magoti, yaumi alikitazama kwa makini sana mpaka kilipoondoka na kutokomea nje ya vyuma vya milango hiyo. Yaumi alijikuta anabaki na tabasamu pana, sauti ikimwambia ndani yake ‘Kila kitu kitapita, usikate tamaa,’ akaendelea kubaki palepale alipo akimezwa na tafakari, mara ghafla moyo wake ulienda mbio, alipokuwa katika tafakari hiyo aliona neon REVENGE lililoandikwa kwa damu, ambalo ni yeye mwenyewe aliliandika, likampa mshtukop, akajishika kifuani, akitweta kama mbwa aliyekimbizwa huku akipigwa mawe.
§§§§§
DAR ES SALAAM- TANZANIA saa 4:30 asubuhi
‘MLIPUKO mkubwa waiteketeza ofisi ya posta Kampala, Gaidi wa kike kutoka Tanzania ahusishwa,’
Kilikuwa ni kichwa cha habari katika gazeti moja la kila siku linalotoka hapa nchini, kichwa hicho habari kilivutia macho ya walio wengi waliojazana katika mbao za wauza magazeti katika kona mbalimbali za jiji la Dar es salaam. Ndani ya ofisi moja binafsi katika jengo kubwa na zuri ambalo limepambawa kwa maandishi mazuri ya kumetameta yenye rangi nyekundu yanayosomeka JM MALL, kijana mmoja alitulia kwenye kiti chake cha kuzunguka akizunguka huku na huku akiisoma habari hiyo iliyoonesha wazi kuwa ilimvutia kwa kiwango kikubwa sana, hakutaka hata kusemeshwa na mtu alizama kabisa katika habari hiyo iliyounasa moyo wake, baada e alifunga gazeti hilo na kulitupia mezani, kisha akafungua kompyuta yake kubwa iliyokaa juu ya meza hiyo ya kisasa, akatulia kidogo kuisubiri iwe tayari kwa kazi. Mkono ukiwa katika upande wa kiti hicho ambao ulistarehe na kidole chake cha shahada kikilibonyeza shavu la kulia.
“Vipi? Tayari damu inachemka? Maana we nakujua vizuri kama ninavyokijua kidole change cha mguuni,” ilikuwa ni sauti tamu ya kike iliyomgutua kutoka katika lindi la mawazo, akamtazama mwanadada huyo aliyekuwa akisogea mezani kwake akiwa na chupa ya chai kwenye chano iliyoambatana navikombe viwili, akaitua mezani na kumtazama kijana huyo.
“Unanichokoza wewe!” Kamanda Amata alimwambia Gina kwa utani kama kawaida yao wawapo pamoja, “Tena wewe ndio ulitakiwa upate uchungu juu ya hili lakini aaaaa umetulia tu,” akaendelea kusema.
“Uchungu katika lipi?” Gina akauliza. “Mwanamke mwenzio huyu, Gaidi, amekamatwa huko Uganda, tena isitoshe Mtanzania,” Kamanada amata alimueleza Gina huku akipokea kikombe cha kahawa kutoka kwake. “Kama ye gaidi muache sheria imnyooshe,” Gina alijibu, huku akivuta kiti na kuketi sambamba na kumwangali Kamanda Amata aliyekuwa akiichezea kompyuta yake. “Aliyekupa hizo nyota za upolisi kakupendelea, maana inaonekana wajibu wako hauujui,” Amata alizidi kutania. “Hebu nambie kwanza juu ya hiyo habari maana wewe huchelewi kuharibu mipango ya watu,” Gina alimwambia Kamanda Amata. Aliweka kompyuta yake vizuri na kuanza kuchambua habari mbalimbali alizoziscan kutoka katika vipande vya magazeti tangu alipoanza kuifatilia kesi ya Yaumi, kilichomvutia zaidi ni pale aliposoma habari ya Yaumi kupewa dhamana na kisha kusadikiwa kumuuwa huyo mdhamini wake, habari hii ilimpa kiulizo Kamanda Amata, na mswali lukuki yakafuatana na hilo, ‘Kwa nini amuue mumewe? Kwa nini aue mdamini wake?” kamanda Amata alijiuliza maswali mengi ambayo hakika yalimuacha njia panda, sasa anakutana na habari ya mtu huyo akihusishwa na mlipuko wa Kampala, Kamanda Amata kutokana na uzoefu wa kazi za kiintelijensia aligundua kuwa hapo kuna ulakini, akaanza taratibu kuzifuatilia habari zote za mwanamke huyo kupitia magazeti, na vipande vyake alikuwa akiviscan na kuvihifadhi katika kompyuta yake wakati yale magazeti akiwapa wauza maandazi huko mitaani.
“Gina, huyu mwanamke kwa jinsi habari yake ilivyo, naanza kupata wasiwasi hapa kuna mchezo ama unachezwa nay eye mwenyewe kupoteza ushahidi wa kitu Fulani au anafanya hivyo kwa kujenga defence kati yake na watu Fulani, nini kinajificha, mi na wewe hatujui, sasa leo lazima niwe mgeni wake, hata kama hayupo nyumbani,” Kamanda Amata alimueleza Gina. Gina hakuwa na la kusema alibaki kimya akiisikiliza habari ile. “Kwa nini uende nyumbani kwake? Si ukaanzie kazi yako katika kituo cha polisi alichoshtakiwa, pale ungepata habari ya kwanza kabisa pindi tu alipokamatwa na nina uhakika hata aliyeshika kesi yake utampata kiurahisi,” Gina alitoa mawazo. “Yeah, sasa umeongea kama WP kabisa aliyepewa cheo chake kihalali, nitafanya hivyo mrembo wangu na nitakujulisha, mi nina uhakika kabisa hapa kuna kitu na ni lazima nikijue ni kitu gani kipo ama mbele au nyuma ya pazia hili,” akamtazama Gina, “Washa gari twende Tabata Kimanga tukaanze taratibu kujua kinachoendelea,” Gina na Amata walitoka ofisini na kuondoka kwa kutumia gari yao, wakiwa wawili tu mazungumzo yaliendelea, huku wakiendelea kukata mitaa kuelekea Tabata. Walifika katika kituo hicho majira ya saa sita mchana, walteremka garini na moja kwa moja waliiendea kaunta ya kituo hicho na kupokelewa na askari mmoja aliyekuwa katika kaunta hiyo, “Sijui niwasaidie nini wapendwa?” akawauliza. Kamanda Amata hakuwa na haja ya kuzunguka, “Mimi ni ACP Jafarry Macholo kutoka makao makuu ya polisi, niko hapa kikazi nimekuja kujua zaidi juu ya kesi ya Yaumi Mwangemi” Yule askari akakunja sura, “Ok, kwa kuwa umevaa kiraia ningependa kuona kitambulisho chako tafadhali,” Yule askari akaomba, Kamanda Amata akatoa kitambulisho na kumpatia, akakisoma na kumrudishia kisha akampa saluti yake ya ukakamavu, “Afande kesi ya Yaumi Mwangemi, ilishatoka hapa kituoni na kwa sasa ipo chini ya mahakama,” akajibu kwa nidamu ya hali ya juu. “Sawa najua, lakini shida yangu kutoka makao makuu ni kuonana na aliyeishika kesi hiyo hapa kituoni kuna mambo ya kuweka sawa ili Yule mtuhumiwa arudishwe nchini,” Yule askari akamsikiliza Kamanda kwa makini, na kwa kuwa alikwishasikia kuwa Yaumi yuko Uganda mikononi mwa polisi haikuwa shida yeye kujua kuwa hakika ACP Jafarry kaja kwa kazi hiyo. “Ok, sasa kesi hii ina watu wawili, mara ya kwanza kabisa ilishikwa na afande Margreth kwa kuwa siku ya tukio yeye ndiye alikuwa kituoni na alifanya upelelezi wa awali, baada ya kwenda mahakamani, kukatokea tukio linguine ka mauaji ndani ya nyumba yake hapo sasa uchunguzi ukashikwa na ACP Chonde mwenyewe ambaye ndiye anashika kituo hiki kwa sasa, lakini bahati mbaya hajafika mpaka sasa na si kawaida yake,” Yule askari aliendelea kuzungumza kwa utulivu. Kamanda Amata alishusha pumzi na kumwangalia Gina, “Na huyo afande Margreth yuko wapi?” Gina akauliza. “Amekwenda kufanya uchunguzi wa tukio Fulani la ubakaji huko Kisukulu,” Yule askari akajibu. Baada ya mazungumzo mawili matatu katia ya Gina na Kamanda Amata, wakarudi tena kwa Yule askari, “Ok, sasa kwa kuwa tuna shida ya haraka, tunaomba tuonane na afande Margreth, popote alipo mwambie aje mara moja,” Yule askari akanyanyua simu ya upepo na kumuamuru afande huyo arudi mara moja, bahati nzuri alikuwa tayari yuko njiani kurudi hivyo haikuchukua muda mrefu akawa tayari kituoni hapo. Yule askari wa kaunta akawatambulisha na Magreth akatoa heshima ya kijeshi kwa Kamanda Amata. Kisha wakaingia ndani ya chumba Fulani na kufanya mazungumzo yao huko.
“Kwa hiyo yaumi kamuua mumewe?” Amata aliuliza,
“Ndiyo, na uchunguzi wote unaonesha kuwa ndiye muuaji hamna la kupinga, lakini kwa kuwa mimi baada ya hapo sikuifuatilia hii kesi, ila ACP Chonde anajua mengine zaidi, kwa sababu nay eye juzi amepata barua ya kuachana na uchunguzi wa kesi hiyo na hakujua ni wapi imetoka,” habari hiyo ya barua ikamshtua Amata, kengele za hatari zikagonga kichwani mwake. Wakati Magreth anataka kuendelea na mazungumzo hayo Kamanda Amata akamkatisha kwa kumshika mkono wake pale mezani, “Chonde ana tabia ya kufika kazini saa ngapi?” Kamanda akauliza, “Huwa hana tabia ya kuchelewa, lakini leo mpaka sasa na hatuna taarifa yoyote,” Magreth akajibu, “hamuoni kama kuna hatari yoyote ambayo imemkuta labda ukizingatia na alipata barua ya vitisho,” Kamanda Amata akamfungua masikio Magreth, ukimya ukatawala. “twende nyumbani kwake kama unapajua labda anaumwa au ana shida nyingine, afande lazima ujue mkuu wako hali ya mkuu wako kila wakati,” kamanda Amata akasema hayo huku akinyanuka kitini na kufuatiwa na Gina, kisha Magreth akafuata, wakaaga kaunta kuwa wanakwenda kumuona Chonde nyumbani kwake.
Haikuwachukua muda kufika katika nyumba ya ACP Chonde pale Vingunguti Kiembe mbuzi, walimkuta kijana wa kiume walipomuuliza yuko wapi mke wa Chonde walijib iwa kuwa kaenda kazini kwa mumewe kuulizia juu ya mume wake kwani hajarudi tangu jana yake. Kamanda Amata akamgeukia Magreth, kisha akamtazama Gina, halafua akarudi kwa Yule kijana. “Jana aliondoka saa ngapi?” Magreth alimtupia swali Yule kijana, “Alitoka asubuhi kama kama kawaida akaja kazini baada ya hapo hatukumuona tena, mapaka sasa shemeji amekwenda Kimanaga kuulizia, kwa si kawaida yake,” Yule kijana akajibu. “Ok, asante sana, tutarudi baadae,” Kamanda Amata alikata mazungumzo kisha wakarudi ndani ya gari. Kamanda alimgeukia Magreth aliyekuwa ameketi kiti cha nyuma, “Afande, hapa kuna jambo na si dogo, mi nimeshapata wasiwasi, ok, kwa kuwa tulikuwa tunataka kujua juu ya kesi ya Yaumi ili kufanya mpango wa kurudishwa nchini, basi we fanya uchunguzi kisha taarifa yote umtumie huyu dada,” Kamanda Amata akamwambia Magreth kisha wakarudi hadi Kimanga wakiwa njiani, Magreth alionesha nyumba ya Yaumi kwa mbali kutoka barabarani, wakafika na kumuacha Magreth kisha wao wakaondoka zao.
“Gina, umeona hii habari inavyochanganya?” Kamanda akauliza. “Hapo nimejua kwa nini ulikuwa unaifuatilia kupitia magazeti, sasa utafanyaje, hata hivyo hili swala liko polisi na mahakamani,” Gina alijibu. “Ndiyo, ila lazima nijue kwa nini mambo yanajipanga hivi? Chonde atakuwa kapotea katika mazingira ya kutatanisha, haya je na hiyo barua aliipokea kutoka wapi na kwa nani?”
TAARIFA ya habari ya saa kumi jioni ilitangaza juu ya kuokotwa mwili wa mwanaume unaoonekana kuuawa na kutupwa kandokando ya bonde la mto Msimbazi maeneo ya Mongolandege. Kamanda Amata alikuwa akiisikiliza taarifa hiyo kwa makini sana akiwa katika gari yake akielekea nyumbani kwa mapumziko ya jioni, alivutiwa na habari hiyo kiasa kwamba aliitoa gari yake pembeni na kusimamisha kisha akaisikiliza vizuri taarifa ile iliyoishia kwa kusema kwamba mwili huo umeifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Amana. Akili ya Amata ilizunguka ikifikiri kama atakuwa ni Chonde au la. Kwa kuwa taarifa ile ilisema tu kuwa mtu huyo hakujulikana jina lake, ilikuwa ni utata juu ya utata. Kamanda Amata akasukuti kama dakika mbili hivi, kisha akainua simu yake na kubofya namba Fulani, “Hallo, unaongea na ACP Jaffary, Magreth kuna mwili wa marehemu umeokotwa kule Mongolandege, fanya hima tukutane Amana hospitali tuutambue kama ni wa Chonde au la,” Magreth akakubaliana na Amata, kisha baada ya hapo akawasiliana na Gina na kumpitia nyumbani kwake, wote wawili wakaelekea Amana.
HOSPITALI YA AMANA – saa 11:30 jioni
KAMANDA AMATA aliegesha gari panapohusika na kuteremka akifuatiwa na Gina, hatua za harakaharaka ziliwafikisha katika korido ndefu inayoelekea mapokezi. Magreth alikuwa amekwishafika hospitalini hapo, alipowaona akawaendea moja kwa moja na kuanza kufanya kazi iliyowapeleka. Kwanza walionana na daktari aliyekuwa zamu wakati huo na kumueleza shida yao, Yule daktari alikiri kupokea mwili huo lakini aliwaeleza kuwa bado haujafanyiwa uchunguzi hivyo hawezi kutoa majibu yoyote ya kifo hicho. Baada ya hapo wakiwa na mhudumu wa chumba hicho walienda pamoja kuutambua mwili huo.
Mwanaume wa haja, wliyekuwa na siha hasa ya kibabe na upiganaji, alikuwa amelazwa ndani ya mfuko wa plastiki katika kitanda cha chuma katika chumba hicho chenye hewa nzito na baridi inayoshidwa kupambana na hewa hiyo. Kamanda Amata alikisogelea kitanda hicho akiwa na Yule daktari, wakafungua ule mfuko kisha Amta akamwita Amgreth kuutambua mwili huo kwa kuwa yeye alimfahamu vizuri mkuu wake wa kazi. Afande Magreth alipoutazama mwili ule, alipatwa na mshtuko mkubwa na kukosa nguvu, kama asingekuwa Gina karibu basi yangekuwa mengine kwa jinsi ambavyo angeanguka vibaya.
“Dokta, asante, nafikiri jibu limepatikana, huyu dada hasingepoteza fahamu kama marehemu tunayemtafuta si huyu, lakini jambo moja huu mwili uhamishiwe Muhimbili ili daktari wetu kutoka wizara ya mambo ya ndani ili afanye uchunguzi wa kifo hiki,” Kamanda Amata alimweleza Yule daktari naye bila kipingamizi aliwasiliana na mkuu wake wa kazi kisha kibali kikatolewa. Jioni ile kwa kutumia gari ya wagonjwa ya hospitali ya Amana ule mwili ulihamishwa mpaka Muhimbili ambako Dr Jasmine aliupokea.
Taarifa za umauti wa ACP Chonde zikafika kila panapohusika na mwisho kabisa nyumbani kwake Vinguguti Kiembe Mbuzi.
§§§§§
HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI
DR JASMINE, Kamanda Amata na Gina walikuwa katika chumba maalum cha kufanyia uchunguzi wa maiti, huku Dr Jasmine akiendelea na kazi yake hiyo Kamanda Amata alikuwa akifuatilia hatua moja baada ya nyingine katika zoezi hilo.
“Kamanda, watu waliofanya mauaji haya ni wataalamu wa kazi hii,” Dr Jasmine alisema.
“Kwa nini unasema hivyo?” Kamanda Amata akauliza. “Kwa sababu uchunguzi wa kwanza wa kawaida, huyu mtu inaoneshwa hakunyongwa, hakukabwa, hakupigwa kwa kitu chochote kile,” Dr Jasmine alijibu. Kamanda Amata akatikisa kichwa. “Ok, sasa inakuwaje hapo?”
“Naingia hatua ya pili, hii lazima itatupa jibu tu,” Dr Jasmine alitoa matumaini kwa Amata. Uchunguzi ukaendelea sasa, mwili ule ukapasuliwa na kutazamwa kwa ndani, “Kamanda njoo hapa kama una uvumilivu,” Dr Jasmine alimwita, Kamanda Amata akasogea karibu na ule mwili na kutupia jicho sehemu hiyo iliyofunuliwa, lo, ni damu iliyoganda kwenye maeneo mbalimbali ya ndani ya mwili ule. “Mh!” Kamanda akaguna, akatikisa kichwa, akarudi nyuma hatua kadhaa na kugeukia sinki la kunawia mikono lililokuwa hapo, akajitazama kwenye kioo, akatikisa kichwa. “Wamefanyaje?” akauliza kutokea kulekule alikosimama, “Wamemuua kwa kumtikisa, kwa hiyo baadhi ya viungo muimu kwa mtyikisiko ule vimenyofoka kutoka sehemu yake ndio maana damu nyingi imemwagika kwa ndani,” Dr Jasmin alimueleza Kamanda.
Kazi ilikamilika, Dr Jasmine na Kamanda Amata waliagana. “Vipi mpenzi?” Gina aliuliza wakati akiliacha geti la Muhimbili na kuchukua barabara ya Mindu. “Watu wabaya sana, wamemuua kwa njia mbaya sana. Lakini uovu haulipwi na mshahara wa dhambi mauti.
SIKU ILIYOFUATA ASUBUHI SAA 3:20
GABRIEL MATINYA alikuwa ofini kwake alipopata taarifa ya kifo cha ACP Chonde, alijifanya kusikitika ili aonekane hivyo na wasaidizi wake, lakini moyoni mwake alikuwa akifurahi kwa kuwa kikwazo kimoja amekiondoa duniani hivyo alijuwa kuwa mambo yake yataenda vizuri, alinyanyuka kitini na kuaga kuwa atarudi baada ya masaa matatu kwani ana mkutano muhimu sana. Alitoka ofini na gari ya ofisini kwa kutembea na kupita nyuma ya jengo hilo mpaka jengo linguine zuri sana lililokuwa hapo, akaingia na kukutana na Yule anayemhitaji.
“Karibu Matinya, bila shaka una habari nzuri,” mtu mkubwa alieketi kwenye kiti hicho ambacho kilionekana wazi kuonewa kwa uzito alimkaribisha Matinya kitini.
“Asante sana, bila kuchelewa, ile kazi tayari, Yule kijana ameshaondolewa kiufundi kabisa,” Matinya alifikisha ujumbe. “Ok, sasa, kama nilivyokwambia, leo tunakutana saa sita mchana kwa kikao na wale wadau, hivyo lazima uwepo tujue sasa tunalimaliza vipi hili swala kabla halijaingia katika mikono isiyostahili, itakuwa ni aibu Matinya, mtu kama mimi au wewe ambao tuna dhamana na taifa hili,” Yule bwana aliongea kwa sauti ya wastani ili katibu wake asisikie. Baada ya mazungumzo machache, walitoka ofisini pamoja na kuingia kwenye gari ya bwana huyo na safari yao ikaanza, moja kwa moja mpaka posta bandari ya Zanzibar, wakateremka ngazi na kuingia kwenye boti moja ya kifahari, ndani yake walikuta watu wengine wawili. Watu wale waliketi katika mtindo wa mduara, mmoja alikuwa ana asili ya kiarabu na hawa watatu ni weusi yaani wabantu. Ile boti iliondolewa eneo lile na lusogea katikati ya maji ili kuwapa nafasi watu hao kuzungumza yao.
“Nafikiri katika hilo, tufanye tuwezalo Yule mwanamke afe kabla hajaleta madhala makubwa,” Yule mwarabu alizungumza kuliambia lile jopo. “Hapana, tukimuua Yule, itakuwaje kwa zile kabrasha zetu? Maana mpaka sasa ni yeye anajua zilipo,” matinya alijibu.
“Hapo Matinya unaeleweka, lakini kumbuka kama ni zile kabrasha zilikuwa posat kampala zimeteketea kwa moto, hivyo tuna uwezo wa kutengeneza zingine,” Yule mwarabu alijibu, lakini mjumbe mwingine akadakia hapohapo, “Kutengeneza mpya sawa inawezekana lakini bwana Salim, tuna uhakika gani kama zile za mwanzo zimeungua?” aliuliza mjumbe Yule aliyekuja na Matinya. Hapo ukimya ukatawala, kila mmoja akiwaza lake. Kati yao mjumbe mmoja aliyeonekana kusinzia muda wote wa kikao hicho alikurupuka ghafla, “Kwa hiyo tunauza hatuuzi?” kila mtu aliduwaa, hakuelewa bwana huyo anaongelea kuuza nini, “ Mbona mnashangaa, si tumegiza mzigo nje, uje na ndio huu mnasema documents sijui zingali nini sijui, ndio nauliza tuitauuza hatuuzi?” kila mtu akaangua kicheko kati kikao hicho, hakuna aliyekuwa na jibu kwa hilo walibaki kutazamana. Yule mwarabu akaktisha ukimya huo na kuwarudisha tena katika mstari, “Sasa tufanye kinachoeleweka, kontena la ule mzigo lnafika keshokutwa hapa dare s salaam, na inabidi litolewe mara moja bila kuchelewa, sasa ninyi hapo ndio wadau, mi sina sauti,” bwana Salim alimaliza kuongea na ujirudisha katika kiti chake huku akikiruhusu kinesenese kumpoa raha. “Mheshimiwa, fanya unaloweza, Yule mwanamke arudi hapa nchini, na anaporudi atekwe kabla hajafika Mahabusu,” Yule bwana mkubwa akamwambia Matinya. “Sawa nitaandaa mazingira kwa jinsi ninavyoweza na Yule mtuhumkiwa atafika kabla ya kontena kufika,” Matinya akawapa uhakika wa hilo kisha wakavunja kikao, wakakubaliana kukutana siku inayofuata. Kila mtu alirudi kuendelea na majukumu katika ofisi yake, hilo linguine lilikuwa tu jukumu la ziada. Wajumbe waliokuwa kati kikao kile wote baada ya kupata taarifa ya kuuawa kwa Chonde iliyotolewa na bwana Matinya walionekana wazi kufurahishwa kwa hilo.
§§§§§
GABRIEL MATINYA alikuwa amekutana na vijana wake mchana wa siku hiyo, pombe zikiwa zimetawala vichwa vyao huku Afande Marina akiwa ndiyo mhudumu wa siku hiyo.
“Sasa vijana mmefanya kazi nzuri tangu tulipoanza, ijapokuwa bado Yule mwanamke anatusumbua lakini kikwazo kingine ni hiki mmekiondosha, safi sana. Sasa sikilizeni, mpango upo tayari, Yule mwanamke anarudi kesho chini ya ulinzi mkali, lakini lazima atekwe, na tukishamteka ni kesho hiyohiyo auawe mchezo uishe, tuanze plan B, tumeshachelewa sana mpaka hapa tulipo,” Matinya aliwaambia vijana wake huku sherehe isiyo rasmi ikiendelea, wakati mke wa Chonde, ndugu na watoto wakilia kwa uchungu, hawa wengine wakisherehekea kwa furaha zote, kweli dunia tambara bovu.
Marina alianza kuelewa kinachoendelea kwa mbali, alisikia mazungumzo ya watu hao na akaelewa wazi kuwa kuna mtu keshanyofolewa maisha, lakini afanye nini, hakuna jinsi, ilibidi tu aendelee kuwa mpole labda atajengewa ghorofa kama alivyoahidiwa na Matinya lakini vipi akikabiliwa na kitanzi? Kwa nini? Jambo hilo lilimpa wakati mgumu sana, alitamani kuachana na Matinya kimapenzi lakini kila alipokumbuka fadhila na utajiri alionao, wote ulitoka kwa mwanaume huyo mkubwa kiwadhifa serikalini, mwenye ofisi nyeti sana yenye dhamana kubwa na taifa hili. Marina alikuwa tayari kwa lolote hata alipoambiwa kunyonya dhakari, alifanya hivyo na vingine vyote alikuwa radhi kuvifanya ilimradi apate kitu kwa Matinya, mimba kadhaa alizitoa ili aendelee kuonekana bado kigoli mbele ya macho mawili ya bwanyenye huyo.
“Sasa boss, huyo mwanamke anakuja na usafiri gani?” Scogon aliuliza
“Anatua na na Rwandair, kesho saa sita kamili mchana, inabidi hujuma ifanyike, kama si kumteka basi auawe palepale.” Matinya alijibu.
“Na vipi ulinzi aliopewa? maana ameshapanda cheo amekuwa gaidi,” Scogon aliuliza tena kisha wote wakaangua kicheko. “Usiogope, askari wawili tu wa kike watakuja naye kutoka Uganda, ila hapa atapokelekwa kwenye gari maalumu ambalo hata ulipige risasi halidhuriki, tairi zake hazitumii upepo, haina dirisha nyuma isipokuwa kwa dereva na kuna tundu moja tu ambalo hutumika na mtu wa ndani kupenyeza mtutu wa bunduki kama inabidi kufanya hivyo,” Matinya alieleza. Scogon aliwatazama wenzi wake na kuwaona kila mmoja akiwa kimya akitafakari jambo, jambo ambalo hakulijua akilini mwake.
“Kwa hiyo mafunzo kule yanaanza rasmi lini? Maana mafunzo ya kawaida tayari vijana wamefuzu,”
“Kule, Kontena linaingia kesho jioni, hivyo siku tatu baadae mambo yatakuwa sawa,” Matinya aliwaeleza mkakati mzima ulivyo na kuwaahidi pesa nyingi kama watafanikiwa kuituliza hali hiyo iliyotawala harakati zao. Baada ya kumaliza mazungumzo yao wakatawanyika, kila mtu kuchukua njia yake wakiwa wamekubaliana siku inayofuata kuingia kazini, kazi ambayo ilihitaji taaluma ya hali ya juu kuifanikisha, Scogon hakuwa na hofu kupanga kikosi chake japokuwa alikuwa na pigo la kuondokewa na vijana wake mahiri.
§§§§
YAUMI akiwa na pingu mikononi na mnyororo miguuni aljivuta kwa hatua za polepole huku akiwa katikati ya askari polisi wawili kutoka Tanzania, waliokuwa wakimlinda kwa ukaribu mkubwa. Gari ya polisi iliyoandaliwa kumbeba mpaka uwanja wa ndege ilikuwa tayari ikimsubiri. Yaumi alionekana wazi akiwa amechoka kimwili na kiroho, hata uvutaji wa hatua zake zilikuwa za taratibu sana, macho yake yalijawa machozi yasiyokwisha, huku vimulimuli vya camera za waandishi wa habari vikiwa vinamsumbua macho asubuhi hiyo, alikuwa bado akitembea polepole kuielekea gari hiyo, akafika na kupakiwa garini kisha wale polisi wawili nao wakapanda mlango ukafungwa kwa nje na kwa ndani pia. Safari ya kuelekea uwanja wa ndege wa Kampala ikaanza. Gari ya Kyomukama ilikuwa kama ya nne hivi kutoka gari ile iliyombeba Yaumi, hakuweza kufanya lolote lakini alifurahi tu alipojuwa kuwa Yaumi anarudishwa nyumbani na mambo yote yatakuwa huko. Katika gari ya kyomukama aliyokuwa akiiendesah mkewe nay eye mwenyewe akiwa ameketi upande wa kushoto, hakuna aliyeongea na mwenzake, ilikuwa ni kama kumsindikiza tu Yaumi. Macho ya Kyomukama yalikuwa yakitoa machozi daima, alimhurumia shemeji yake huyo, lakini alijua wazi kwa nini yaumi alikuwa Kampala, ila kwa wakati huo hakuwa na lolote la kumsaidia.
Ule msafara uliiacha barabara kuu na kuingia katika uwanja wa ndege wa Kampala, uliojengwa katika maeneo ya vilima vya Kololo.
Yaumi alishushwa katika gari na kusindikizwa na polisi kadhaa wa Kampala, huku bado waandishi wa habari wakimwandama kwa picha. Aliingizwa ndani ya jengo na moja kwa moja alipelekwa chumba maalum kwa ukaguzi na kuruhusiwa kwa safari. Abiria wote walikuwa tayari wameketi ndegeni wakisubiri kuondoka, Yaumi alipakiwa na kuwekwa kiti cha nyuma kabisa katikati ya wale WP wawili waliovaa kiraia lakini walionekana kuimudu vema kazi yao. Majira ya saa nne asubuhi waliondoka kuelekea Dar es salaam, Yaumi alikua akilia muda wote, akijua kuwa sasa mwisho wake ulikuwa umefika bila kipingamizi, kitanzi kilikuwa kikimsubiri nyumbani Tanzania…
DAR ES SALAAM – 4:10 asubuhi
KIKOSI KAZI kilikuwa tayari kwa kile kinachowakabili siku hiyo mchana, Scogon alikuwa akipanga vijana wake tayari kwa kazi hiyo nzito na ngumu inayohitaji umakini wa hali ya juu.
“Eneo la tukio litakuwa Vingunguti mbele kidogo ya yadi ya Tata, kwa taarifa ambayo mzee ametupa gari itakayotumika, haipenyi risasi na wala tairi zake hazitumii upepo, kwa hiyo ile mbinu yetu ya kushambulia kwa risasi ili kumpata mateka wetu haiwezekani, inabidi tupange plan B,” Scogon aliwaeleza vijana wake. “Sasa ni mbinu gani tutatumia kukamilisha zoezi? Maana inabidi tulimalize ndani ya dakika tatu tu,” Mdumi aliuliza. “Usijali Mdumi, mpango upo hivi, sisi tutatega pale boza la maji, mmoja wetu atakuwa kama anatengeneza boza hilo, wao watakapofika pale itabidi kusababisha ajali amabyo itapelekea lile gari ama kuanguka au kupoteza uelekeo kisha tunafanya kazi yetu, gari yetu ya uokoaji itakuwa jirani.” Baada ya maelezo hayo Scogoni aliwapa mikono vijana wake na kuwatakia kazi njema kwani yeye alikuwa anahitaji kuonana na mzee kujua itakuwaje kwa mzigo unaoingia bandarini jioni hiyo.
“Ndiyo Scogon!” Gabriel Matinya alijiegemeza kwenye kiti chake na kutoa kauli hiyo tata ambayo msikilizaji hujui kama ni swali au hoja. Scogon alimwangali boss wake huyo aliyeonekana kukonda kwa siku chache tu. Akiwa amekalia kiti cha wageni alijiweka vizuri na kuegemeza mikono yake mezani, “Plan B tayari kiongozi,” akatamka Scogon. Matinya ambaye alionekana kuwa na mawazo sasa lionekana kidogo kupata uhai baada ya kusikia hilo. “Una uhakikia kilam kitu kitaenda sawa?” akauliza, “Ndiyo boss!” akajibu. “Ok maana kutakuwa na ulinzi mkali wa polisi, hivyo mjipange vyema na mfanye kazi yenu kiakili,” Matinya alitoa rai ya mwisho. Baada ya hayo machache Scogon na Matinya waliongea yao mengine juu ya kontena linaloingia jioni hiyo ambalo halitakiwi kulala zaidi ya siku moja bandarini, hivyo ilipangwa mwanamke huyo akipatikana tu lazima aeleze kila document ilipo ndani ya muda mchache na ili kumaliza mchezo akibisha basi auawe maana kumuacha nje kutasababisha hatari nyingine.
Matinya na Scogon walitoka na kuelekea ofisi nyingine lakini ndani ya jengo hilohilo, wakaenda kumuona mtu mwingine naye alikuwa ni mtu mwenye dhamana kubwa kwa wananchi, wakaingia bila ya hodi na kumkuta mtu huyo akiwa ametingwa na shughuli kadhaa mezani mwake, “Karibu mkuu,” alisimama na kumkaribisha huku akimpa salamu ya kijeshi iliyomstahili. Kiaha wote wakaketi na mazungumzo yakaanza, “Sasa ule mpango umekamilika,” Matinya alimwambia Yule bwana. “Sawa ulinzi uliopo sio mkali sana hivyo wajitahidi tu kufanya kazi kwa umakini, kama watashindwa kukata lile bati la ile gari basi nitawapa funguo za akiba za ule mlango,” Yule bwana alitoa maelekezo. “Hapana usitoe funguo ila tutatengeneza zingine ambazo watatumia, ili kama ikionekana hujuma basi funguo zikutwe ofisini” Matinya alieleza. Kisha Yule bwana akachukua zile funguo na kuzichora katika karatasi nyeupe kwa kuwa hakuwa na sabuni ya kuikandamizia, akampa Scogon ile karatasi na kuagana naye.
Scogon hakupata shida kwa hilo, moja kwa moja alifika Gerezani Kariakoo ambako kila kitu hupatikana na kila kitu hutengenezwa kasoro roho tu. Alifika katika kibanda kimojawapo ambacho kilikuwa na mtu anayefanya kazi hiyo.
“Kijana, una dakika ishirini na tano tu kuhakikisha funguo hii imepatikana, nakunywa bia pale ukimaliza uje nayo,” Scogon alimpa maelekezo Yule kijana. “Sasa kaka si unajua hii itakuwa ni express hivyo malipo yako juu,” Yule kijana lillalama, “Unapoteza muda tengeneza, pesa kitu gani,” Scogon alijibu.
Dakika zilezile alizopewa na Scogon ile funguo ilikuwa tayari imekamilika, Scogon aliitazama hakuamini, ilikuwa ni ileile kama aliyopewa kule ofisini akiwa na Matinya. Scogon alimpatia pesa yake ya ujira Yule kijana, hakuwa na muda wa kupoteza, aliondoka zake na kuelekea walipo vijana wake.
Kama walivyoagizwa, Mdumi na wenza walifika na gari bovu eneo la Vingunguti, kisha wakajifanya limeharibika na kuanza kulibomoa bomoa ilimradi lionekane kuwa liko matengenezoni, baada ya muda kidogo ilikuja gari ndogo aina ya McLaren GTI HP 450 ikaegeshwa kwa mbele kidogo na wakati huo huo landrovar moja mbovumbovu iliegeshwa katika moja ya vivuli vya miti iliyojirani hapo, ndani yake kukiwamo na mtu mmoja aliyeonekana kusinzia. Kikosi kilijipanga tayari kwa kazi, kilikuwa kikisubiri tu muda kufika.
§§§§§
MAKABURI YA SEGEREA
VILIO VYA WAOMBOLEZAJI vilikuwa vikisikika huku na kule, akina mama waliokuwa wakijitupa tupa kwa kilio kikali cha kumuomboleza ACP Chonde aliyekuwa akizikwa katika makaburi hayo.
Kamanda Amata akiwa amesimama kwa utulivu pembeni yake kukiwapo na Gina. Ibada ya mazishi iliendelea huku jua kali la mchana likiwaka, nyimbo za maombolezo zilizokuwa zikiwakumbusha waombolezaji kutenda mema duniani zilizikika.
Kutoka mbali Kamanda Amata alimuona afande Magreth akiongea na mtu mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni sana.
“Gina, Yule anayeongea na Magrteth ni nani?” kamanda akamuuliza Gina. Gina akatazama kwa wizi kisha akarudisha macho yake mbele na kumjibu Amata, “OCD Kambale, namfahamu sana Yule mzee,” kamanda Amata akatikisa kichwa kuwa ameelewa alichoambiwa na Gina.
Saa 6:45 mwili wa ACP Chonde ulikuwa ukishushwa kaburini, kila mtu alikuwa akifuatilia tukio hilo kwa huzuni kubwa sana, vijana walikuwa wakiongea yao katika vikundivikundi, Kamanda Amata alijichanganya na vijana wengine kuona labda atapata lolote katika hayo mazungumzo. Katika kundi moja alivutiwa sana na kile walichokuwa wakiongea kwani alisikia wakitaja jina moja na kulisifia sana kuwa ni mtu hatari na anyeogopwa, Kamanda ASmata alitaka kujua zaidi juu ya mtu huyo ‘Chilungu’, akamkariri Yule kijana aliyekuwa akizungumza na wenzake, ili asimpoteze kwenye macho yake kwani baada ya maziko alijua atakuwa na kazi naye.
Miongoni mwa waombolezaji waliokuwa hapo, dokta Omongwe alikuwa miongoni mwao, mara baada ya zoezi la kufukia lilipoanza, kutokana na vumbi lililokuwa linatimka, Omongwe alichomoka na kurudi kwa nyuma, katika harakati hizo akakutana Magreth, wawili hawa walikuwa wanafahamiana hasa kutokana na sakata la Yaumi ambalo liliwafanya wakutane si zaidi ya mara mbili kila mmoja akiwa katika majukumu yake. Walisabahiana na kisha wote wawili kusimama kando wakisubiri zoezi hilo liendelee.
“Hivi afande ile kesi ya Yaumi inaendeleaje?” Omongwe alimuuliza Magreth.
“Si unajua aliyoyafanya Uganda?” Magreth akmuuliaza na Omongwe akajibu kwa kutikisa kichwa.
“Kuna kazi kubwa maana ni visa juu ya visa, mchana huu anarudishwa nchini kuendelea na kesi yake, lakini sasa imeongezeka upana kutokana na yale ya Kampala, keshokutwa ndiyo kesi yake,” Magreth alijibu kimbea si unajua akinamama wakikutana tena.
Wakati wa kuweka mashada ya maua ulifika, ukiacha mke, ndugu wa karibu, pia OCD Kambale wa kituo cha Tabata alipewa nafasi hiyo kuwakilisha askari wa kanda hiyo, Magreth kama mfanyakazi mwenzake wa karibu nae alipata fursa hiyo ya kuweka shada la maua.
Mara baada ya shughuli nzima kumalizika, Kamanda Amata alikuwa jirani sana na kile kikundi cha wale vijana kilichoonekana kujua mengi, wakiwa katika kutoka makaburini pale alikuwa akiwatazama kama watapanda magari yaliyopo au wana ajenda nyingine. Kamanda Amata akasogea chini ya mkorosho huku mkono mmoja amemshika Gina. Pembeni kulikuwa na grosary ndogo yenye vinywaji, akaingia na kuketi karibu na mlango wa kuingilia wateja, mara aliona lile kundi la vijana kama watano hivi wakiendelea na stori, sasa zilikuwa za Simba na Yanga, walipokaribia pale akawashtua.
00
“Oya, karibuni tujumuike, maana tumeanzia mbali kwa nini tumalize tofauti?” akawauliza, wale vijana wakacaheka huku wakitazamana, “Aah Braza we endelea tu si tunaenda mbele hapo,” wakamjibu, lakini Kamanda alikuwa akiwabembeleza mpaka wakakubali, wakajumuika nae, vinywaji vikaanza kupopolewa kutoka kaunta, kwa mwenye grosari ilikuwa neema kubwa, ama kweli kufa kufaana.
Baada ya lisaa limoja walikuwa tayari wamechangamka na kila mmoja akiongea cha kwake, ndipo hapo Amata alipoanza utundu wake wa kukusanya habari, muda wote Gina alikuwa akiongea kwa chati tu lakini alishajua kile ambacho Kamanda alikuwa akikitafuta. Mazungumzo yao ya kilevi yakaenda mpaka kwenye tukio la kuuawa Chonde, vijana wale wakafunguka kwa kile wanachokijua, jina la Chilungu likarudi tena mezani, wakimsifi kuwa ni jamaa asiyefaa, wakihofu kwa vyovyote itakuwa ni kazi yake. Kamanda Amata akapeleleza maeneo anayoishi, akaambiwa kuwa huyo jamaa ni nyoka hana sehemu maalumu ya kuishi, lakini alitajiwa kuwa anapatikana sana maeneo Baracuda Bar kwani hapo ndipo kijiwe chake kilipo. Baada ya hayo, kamanda Amata aliagana na wale vijana akawaacha hela ya bia tano kila mmoja kisha ye na Gina wakapanda gari yao na kuelekea mjini, “Unajua Kamanda, tupite barabara ya Nyerere, hii ya Mandela kuja buguruni sasa hivi ipo tight sana” Gina alieleza. Kamanda akapinda kulia na kuchukua barabara ielekeayo Kinyerezi kisha akaiacha ile ya Mbezi na kukunja kushoto kuja Majumba sita. Dakika tano zilwafikisha njia panda Segerea ambako walipinda kushoto na kukamata barabara ya Nyerere kuelekea mjini.
ITAENDELEA
Kitanzi cha Mwisho Sehemu ya Tatu
Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;