La Ultima Letra Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA: THE BOLD
*********************************************************************************
Simulizi: La Ultima Letra
Sehemu ya Pili (2)
Baada ya kuwasiliana naye na kufanikiwa kufanya naye kikao maalumu akamueleza juu ya azma yake na kumuomba kumsaidia kutengeneza kutengo maalumu cha kijeshi ndani ya genge lake la Gulf Cartel, kwa ajili ya ulinzi na kusambaratisha wapinzani wake kibiashara.
Luteni Salinas akakubaliana na ombi la Boss Cardenas wa Gulf Cartel na akamuahidi kuunda kikosi cha kijeshi chenye weledi na ufanisi kuliko kikosi chochote cha uhalifu dunia ilichowahi kukiona.
Luteni Salinas akatumia uzoefu wake wa kijeshi kushawishi wanajeshi wengine 30 kutoka vitengo vya kijeshi vya weledi na oparesheni maalumu katika jeshi la Mexico, wakajiunga naye kuunda kikosi maalumu cha kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa viongozi wa Gulf Cartel na kusambaratisha washindani wote wa Gulf Cartel.
Huo ndio ukawa mwanzo wa kikundi ambacho kilikuja kuwa tishio kwa ukanda mzima wa Amerika ya kusini, kutawala biashara nzima ya mihadarati nchini Mexico na kuingiza hofu isiyomithirika katika jamii Mexico kiasi kwamba hata muandishi wa habari au mtu mtaani aliogopa kutamka jina lao.
Wenyewe walijiita “Los Zetas”
Masalia ya viungo vya Wanachama wa Sinaloa Cartel walio katwa katwa viande kama wanyama.
La Ultima Letra
Ndani ya miezi miwili luteni Salinas alikuwa amefanikiwa kuwasiliana na wanajesh 30 ambao walikubali kujiunga naye na kutengeneza kitengo cha kijeshi ndani ya genge la Gulf Cartel.
Wanajeshi hawa ambao luteni Salinas aliwachagua walikuwa ni wale pekee ambao walikuwa wamepatiwa mafunzo ya weledi wa hali ya juu katika jeshi la Mexico.
Kwa mfano, kulikuwa na wanajeshi ambao walikuwa wamepata mafunzo yao kutoka katika kikosi maalumu cha kijeshi cha nchi ya Israel (Israel Special Forces Units) na wengine mafunzo yao waliyapata kutoka katika vikosi maalumu vya jeshi la Marekani (American Special Forces).
Baada ya kukutana na kujadiliana kuhusu namna watakavyo endesha shughuli zao ndani ya genge la Gulf Cartel, moja ya washiriki aliyeitwa Arturo Decena akapendekeza kwa wenzake kwamba, kwa kuwa watakuwa wanaendesha shughuli zao katika mtindo wa kijeshi basi ni vyema hata kikosi chao wajiite jina la kijeshi na akapendekeza waitwe ‘Los Zetas’ (The Z’s).
Ni kwamba, Katika mfumo wa mawimbi ya simu ya kijeshi (military radio airwaves) nchini mexico, kamanda mwenye ngazi ya juu kabisa kwenye eneo husika huwa anatambuliwa kama ‘Z’ katika mawasiliano ya simu za jeshi.
Ndio kusema kwa mfano kamanda wa ngazi ya juu kabisa ataitwa ‘Z 1’ anayemfuatia kwa cheo atakuwa ‘Z 2’ anayefuatia ‘Z 3’ vivyo hivyo na kuendelea.
Hii ndio ilikuwa maana halisi ya wao kujiita ‘Los Zetas’ (The Z’s) wakimaanisha kuwa kikosi chao wanakifananisha na mkusanyiko wa wanajeshi makamanda wa ngazi za juu kabisa wenye weledi wa kutosha.
Pia wao wenyewe ndani kwa ndani walipenda kuitana jina la utani ‘la ultima letra’ (herufi ya mwisho).
Angelitos (Malaika Wadogo)
Baada ya kikosi cha Los Zetas kuwa kimezinduliwa rasmi baada ya kikao hicho, Arturo Decena ambaye alipewa jina la fumbo (code name) Z 1, alipewa wadhifa wa kuwa kamanda Mkuu wa Los Zetas.
Kisha kila mwanachama kati ya wanachama wote 31 akaamuriwa kutafuta vijana wasiopungua 8 wenye uzoefu au waliowahi kupitia jeshi au polisi.
Kila mmoja kati ya wanachama hao 31 akaleta vijana hao wasiopungua 8 hivyo wakapata vijana waliokaribia 300.
Gulf Cartel ikatengeneza kituo kijeshi maeneo ya mpakani na Guatamala kinachofanana kabisa na kituo cha kijeshi cha serikali. Kituo kilikuwa na kila kitu kinachohitajika kukidhi matakwa ya kuwa kituo cha kijeshi.
Kisha vijana hawa wapatao 300 wakapelekwa kwa ajili ya kupatiwa mafunzo.
Kumbuka vijana hawa karibia wote walikuwa na uzoefu wa polisi au jeshi lakini katika kituo hiki walipatiwa mafunzo maalumu ili kuwapatia weledi ju kazi watayoenda kufanya kwa “mwajiri” wao mpya, Gulf Cartel.
Mafunzo hayo yalihusisha ushushu (intelligence gathering),utekaji (kidnaping), ulinzi maalumu, utesaji (torturing) na namna ya kudhibiti serikali za mitaa (local authorities).
Baada ya vijana kuwiva katika mafunzo waligawanywa tena kwa makamanda wakuu 31 ambao waliwatafuta na kuwaingiza Gulf Cartel. Kila kamanda alipatiwa vijana wasiopungua 8 na yeye kamanda pamoja na vijana wake wakapangiwa sehemu ndani ya mexico ambayo wataenda “kufanya kazi”.
Makamanda hawa 31 waliwaita vijana wao waliopewa ‘Angelitos’ (little angels (malaika wadogo)).
Baada ya Makamanda na ‘malaika’ wao kugawanywa kwenye maeneo waliyopangiwa kwenye miji tofauti tofauti ndani ya mexico, kazi ikaanza.
Mmoja wa Angelitos. Kijana mdogo mpiganaji chini ya makamanda wa Los Zetas.
ITAENDELEA
La Ultima Letra Sehemu ya Tatu
Also, read other stories from SIMULIZI;