La Ultima Letra Sehemu ya Tano
IMEANDIKWA NA: THE BOLD
*********************************************************************************
Simulizi: La Ultima Letra
Sehemu ya Tan (5)
Special Forces wa Mexico wakiwa na Cardenas Guillen, boss wa Gulf Cartel siku alipokuwa anahamishwa kutoka katika magereza ya Mexico na kupelekwa nchini Marejani.
Hii ilimaanisha kwamba uongozi wake ndani ya genge la Gulf Cartel ulikuwa umeishia hapo.
Hapa ndipo mtafaruku ulipoanzia kati ya ‘muajiri’ Gulf Cartel na ‘muajiriwa’ Los Zetas.
Baada ya Cardenas kuhamishiwa nchini marekani mwaka 2010 uongozi wa juu ndani ya Gulf Cartel ukapendekeza kuwa Mdogo wake Cardenas aliyeitwa Antonio arithi nafasi ya kaka yake kama kiongozi wa genge.
Suala hili halikukubaliwa na Los Zetas kwani wao walitaka kamanda wao mkuu Lazcano ndiye achukue mikoba ya Cardenas. Mabishano hayo yaliendelea kwa miezi kadhaa na kufanya uhusiano wao udorore kiasi.
Wakiwa katika kipindi hiki cha sintofahamu, Kuna siku ilitokea moja kiongozi wa ‘kamati’ za juu ndani ya Gulf Cartel aliyeitwa Flores Borrego walikuwa wanabishana na moja ya maluteni wa Los Zetas aliyeitwa Pena Mendoza. Baada ya mabishano makali, Borrego alishikwa na hasira na kutoa bastola akamtandika risasi Mendoza.
Taarifa hii ilipowafikia makamanda wa Los Zetas wakaamuru viongozi wa Gulf Cartel wamkabidhi muuaji wa Mendoza kwao ili walipe kisasi.
Viongozi wa Gulf Cartel wakakataa.
Siku hii ilikuwa ni mwezi September mwaka 2010 na ndiyo siku rasmi ambayo Los Zetas walijitenga na Gulf Cartel na kuanzisha genge lao linalojitegemea.
Vita kuu II
Mara tu baada ya kujitenga, kwakuwa Gulf Cartel walikuwa wanafahamu uwezo wa kijeshi wa Los Zetas ikabidi wajihami mapema ili wasije kumalizwa na Los Zetas.
Hivyo basi wakawasiliana na adui yao mkuu wa siku nyingi El Chapo kiongozi wa Sinaloa Cartel na kumuomba waunganishe nguvu kwadhibiti Los Zetas.
Sinaloa Cartel wakakubaliana na ombi la Gulf Cartel kwa sababu mbili kuu.
Moja, walikuwa na kinyongo na Los Zetas kwani toka kikundi hicho kimeanzishwa walikuwa wameua wanachama wao wengi.
Pili, walikubali kwasababu Gulf Cartel walikuwa tayari kukabidhi baadhi ya miji iliyoko chini ya himaya yao ya kibiashara wanaitoa iwe chini ya Sinaloa Cartel.
Suala hili lilikuwa ni jema machoni kwa El Chapo. Akakubali washirikiane kuwatokomeza Los Zetas.
Wakati wao wanapanga mipango hiyo, Los Zetas wakaweka makao yao makuu katika mji wa Nuevo Laredo mji uliopo mpakani kati ya Mexico na Marekani. Kisha wakaanzisha kampeni ya kusajili wanachama wapya na kuwapeleka katika kambi zao za mafunzo ya kijeshi.
Mwishoni mwa mwaka 2010 vita ikaanza rasmi ambapo Los Zetas walivamia mji wa Tamaulipas ambao ndio makao makuu ya Gulf Cartel mchana kweupe na kuendesha oparesheni ya kuwasaka wanachama wa Gulf Cartel nyumba kwa nyumba.
Ndani ya siku kadhaa mji wa Tamalipas ukageka uwanja wa vita risasi zikirushwa nje nje baina ya wanachama wa magenge hayo. Nyumba zilichomwa moto. Biashara ziliharibiwa. Mji wa Tamaulipas ukageka kama magofu yaliyoachwa miaka ya kale.
Mpiganaji wa LOs Zetas akiwa anamchinja mwanachama wa genge pinzani. Pembeni yake mkono wa kulia unaonekana mwili wa mtu ambaye amekwisha kuchinjwa tayari.
Ultima.
Vita hii Kali iliendelea kwa zaidi ya miaka miwili katika miji mbali mbali ndani ya Mexico na imegharimu maisha ya zaidi ya watu 35,000 na mpaka sasa vita hii bado inaendelea.
Mpaka sasa ni dhahiri kuwa Los Zetas ndio mshindi wa hii vita kwani kwasasa wao ndio wenye miji mingi chini ya himaya yao. Takwimu za ofisi za DEA ya nchini Marekani zinaonyesha kuwa Los zetas wana miji 26 ukilinganisha na miji 11 ya Gulf Cartel.
Los Zetas haikuishia hapo tu kwani wamevuka mipaka ya nchi, na kwasasa wao ndio wanaotawala biashara haramu ya mihadarati nchini Guatemala na pia wamefungua matawa nchini marekani katika jimbo la Texas ambapo wanashirikiana na genge la MS-13 pia wana tawi nchini Italia ambako wanashirikiana na genge la Ndraghetta.
Ushawishi wa genge la Los Zetas umekuwa mkubwa kiasi kwamba katika miji mingi nchini Mexico hauwezi kuwa kiongozi wa serikali (hasa nafasi ya Gavana) pasipo kuwa kibaraka wao.
Weledi wao wa kijeshi wa hali ya juu unawafanya waendelee kuitawala biashara ya mihadarati. Ukatili wao unawafanya waogopwe hata na watawala wa serikali.
Hata waandishi wa habari nchini Mexico abadani hawawezi kuripoti habari inayoweza kuwaudhi Los Zetas na waandishi wengi wameamua kuto wazungumzia kabisa, kwa heri au ubaya.
Wenyewe wanajitetea kuwa hawafanyi ukatili kwa mtu asiye na hatia bali kila anayekumbwa na madhira yao basi alijiingiza kwenye mambo ambayo hakupaswa kujiingiza.
Huko Mexico vijana wenye kupenda maisha ya anasa na fedha za haraka wanajiunga kila uchwao na kikundi hiki cha kikatili.
Hakika, ulimwengu umeshuhudia magenge mengi ya kiharifu. Lakini linapofikia suala la weledi, ufanisi, na ukatili, wao wanasimama katika viwango vyao tofauti kama heruzi Z ilivyojitenga mwishoni mwa alfabeti na hakika inaakisi jina lao.
Herufi ya mwisho. La ultima letra. Los Zetas. The Zs.
Jiunge na Group langu la WhatsApp kusoma simulizi mpya kila siku. Kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi. Wasiliana nami 0759 181 457
Mwisho.
Also, read other stories from SIMULIZI;