Mauaji ya Kasisi Sehemu ya Tano
IMEANDIKWA NA : RICHARD MWAMBE
Simulizi : Mauaji Ya Kasisi
Sehemu ya Tano (5)
Mara mlango ulifunguliwa na wale jamaa wakaingia ndani wakashangaa kukuta kiti wazi, hayupo Fr Frank. Mmoja wao akainua redio yake na kutoa taarifa kwa waliowatuma kuwa mtu wao katoroka, akiwa tayari kamaliza kuongea na simu hiyo, aliirudisha mahala pake na kwaamuru wake wenzake kumfuata, lakini kabla hajafika mbaliki lilikuwa ni t eke zito lililotua nyuma ya sjingo yake, kisha akajiviringa na kusimama upande wa pili, wale wawili nao wakaja kwa pamoja Fr Frank akaruka juu nakuitawanya miguu yake na kumpiga kila mmoja kwa mguu wake, mmoja alijibamiza vibaya katika nguzo iliyokuwa katika banda hilo na kupasuka sehemu ya nyuma ya kichwa chake. Akajibwaga chini akiwa tayari hana uhai, wakati mmoja akiwa tayari katoka nje mwingine aliendelea kumkabili Fr Frank, alirusha ngumi ikakwepwa, akarusha nyingine ikakwepwa tena kwa mtindo uleule, kabla hajakaa sawa Yule jamaa akapigwa teke hafifi katika kanyagio la mguu wake, aliposhusha sura kuangali chini, alijikuta anachezea makonde yasiyo na idadi ambayo yalimpeleka chini sakafuni akiwa hajiwezi, akiwa anatambaa alipigwa teke moja la nguvu mbavuni na akalala chini bila kipingamizi.
Fr Frank alimwangalia Yule jamaa akigalagala pale chini, mara akakumbuka kuwa kuna aliyetoka nje, akaichomoa bastola katika mfuko wake na kuvuta hatua chache kuuelekea mlango, mara akasikia nyuma yake mlio wa kiondoa usalama cha bastola, kwa kazi ya ajabu aligeuka na tayari kidole kilikuwa kwenye trigger, aligeuka huku akiwa anaenda chini kupiga goti moja akachezesha kidole na risasi mbili zikamtwanga Yule jamaa kifuani, akatoa yowe la maumivu nay eye akajiunga na wenzake pale sakafuni.
“Mwambe Bill, sina shida nae, na hsinifuate fuate,” alimwambia Yule aliyekuwa hai bado lakini hali yake ilikuwa mbaya kwani alimvunja mbavu mbili.
Akatoka nje ya ile nyumba na kuingia katika gari yake iliyotumika kumleta pale akapotelea mjini kama kawaida, akarudi mpaka misheni, akaegesha gari palepale, na kuingia ndani.
§§§§§
KAMANDA Amata hakuamini anachokiona katika darubini yake, mmoja wa wahudumu wa misheni, aliyempokea siku alipofika alikuwa akiongea na watu Fulani katika jumba la Don Andreas, Kamanda Amata akagundua hapo kuwa kumbe siri zingine za yeye kufika pale ijapokuwa ilikuwa kwa njia ya siri ni yeye aliyeipeleka kwa watu hao, akatoka na kuelekea jikoni, pale aliwakuta wafanyakazi wengine wakiandaa chakula cha jioni, hakuongea na mtu, akakiendea kibao kinachoonesha zamu za wafanyakazi, kweli siku hiyo Yule mfanyakazi alikuwa off, akaondoka akarudi ndani kila mtu mle jikoni alikuwa akimwangalia mtu huyu mweusi, walimdharau kwa rangi yake lakini yeye hakujali. Alirudi tena chumbani kwake mara hii hakumuona Yule mtumishi pale alipokuwa mwanzo. Akatembeza tena darubini yake na kunasa dirisha linguine lakini hakuwaona wale watu waliokuwa wakiongea na Yule mhudumu.
‘Msaliti’ alijisemea, na mara mlango wake ukagongwa, akauendea na kuufungua taratibu, alikuwa Fr Frank, akaingia na moja kwa moja akasimama mbele ya Kamanda, “Bill ameshajua kama tuko hapa?” Frank alisema, Kamanda Amata akatulia kumwangalia, hakuielewa kauli yake, “Uko hapa na nani?” akauliza. Fr Frank akagundua kuwa ametereza katika maongezi yake, akamtazama Amata, akakutana na sura ilijikunja kuwa sasa haina utani hata kama na askofu, Kamanda Amata akatoa bastola yake na kumnyooshea Fr Frank, “Niko na nani?” akauliza tena, “Mmeamua kunicheza shere sio? Mpishi wenu anatoa siri za mimi kuwapo kwa Bill sivyo, kumbe mnajua kila kitu, niambie niko na nani?” akazidi kuuliza. Fr Frank hakuwa na la kujibu, “Usihofu Kamanda, mimi si mbaya kwako,” akasema huku akitetemeka.
“Ninyi wote ni wasaliti humu ndani,” Kamanda Amata bhakuonesha kabisa masihara katika hilo, uso wake uliloa jasho la hasira. Fr Frank akamtazama tena Kamanda, “Mimi niko upande wako Kamanda,” akamwambia.
“Naitwa Frank Edson, kutoka FBI, idara ya upelelezi ya Marekani, nipo hapa kwa kazi maalumu lakini hakuna anayejua,” akajieleza.
“Lete kitambulisho,” kamanda akaomba, Fr Frank aktoa kitambulisho katika mfuko wake wa ndani na kumpa Amata akakisoma, ni sahihi kabisa.
Frank Edson, mpelelezi kutoka shirika la kipelelezi la Marekani FBI, alikuwa amepewa kazi maalum na ofisi yake, kazi ya kumfuatili Bill ili amtie mkononi na kumpeleka Marekani akajibu mashitaka yake. Frank kama alivyo alikuwa kasisi katika kanisa la Katoliki huko Texas Marekani, ijapokuwa alikuwa akifanya kazi hiyo kwa siri kubwa sana lakini viongozi wake wa juu walilifahamu hilo.
Katika harakati za kumsaka Bill kama jasusi linaloendesha shughuli zake kwa kukodiwa kwa nia mbaya na matajiri mbalimbali duniani, Marekani ilianza kumsaka tangu pale alipotekeleza mauaji ya balozi wao kule Iraq miaka kadhaa nyuma. Walimsaka kila kona bila mafanikio. Bill akaibuka tena katika sakata hilo la Nairobi, kwa kuwa wale waliokuwa wametumwa Kenya walishindwa kumnasa Bill, Frank alitumwa muda mrefu huko Ujerumani kabla Bill hajaenda Nairobi, hivyo akapewa kazi ya kuhakikisha anamtia mkononi hukohuko.
Frank alifika Aachen kama kasisi aliyekuja kwa kazi maalum na kufikia katika kanisa kuu la Aachen. Hivyo alijua kila kitu kinachoendelea juu ya Bill, hata Kamanda ASmata alipokuwa anakuja, Frank alikuwa akimfuatilia tangu akiwa Nairobi hivyo alijuwa wazi kuwa lazima atafika kwa kazi hiyo. Ili asilete Madhara, kwa kuwa yeye alitakiwa ampfikishe Bill akiwa hai huko Marekani, alijua kuwa Kamanda Amata kaja kwa mawili kummaliza. Hivyo alimpokea Amata kwa maelekzo toka ubalozi wa Tanzania, wakijifanya kuwa kanisa linataka kushirikiana na Tanzania katika sakata hilo hasa kwa kuwa walikuwa wanaitaka monstrance yao kumbe sivyo.
Bill alimjua vyema Frank Edson, na alipewa taarifa kuwa yuko hapo kitambo na mmoja wa mashushushu wake ambaye ni mfanyakazi wa misheni hiyo. Frank Edson, siku zote hakugundua kuwa ndani ya misheni hiyo kuna mamluki mpaka alipokuja kupewa siri hiyo na Kamanda Amata.
§§§§§
Fr Frank akamuonesha Kamanda Amata beji yake maalum ya FBI iliyobanwa vizuri katika loop ya suruali yake. Kamanda Amata akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni. “Samahani, si unajua hizi kazi zetu hakuna kuaminiana,” akamwambia Frank, “Hamna shida hata ningekuwa mimi ingekuwa hivyohivyo,” akajibu Frank, kisha wote wakasogea pale dirishani.
“Sikiliza, unamjua huyu?” kamanda akamuuliza na kumuonesha baadhi ya picha zilizopigwa na ile camera yake aliyoiunganisha na ile darubini pale dirishani, Frank alipigwa na bumbuwazi akabaki midomo ikimchezacheza, “Kaka ungeshakufa muda mrefu sema tu huo ukasisi wako umekulinda, la tayrai mauaji ya kasisi yangeshafanyika hapa Aachen,” Kamanda alimwambia Frank huku akimpigapiga kifuani kwa ngumi yake.
“Sasa Kamanda, hapa mambo yameshaharibika inaonekana huyu mpishi anajua na ameshawapa kila habari zetu, ndo maana walikufuata kule makaburini. Bill huwa hatoki ovyo lakini alinifuata leo hapa,” Frank akmwambia Kamanda. Habari hiyo ilimfanya Kamanda kushtuka, “Unasema Bill alikuja hapa?!” kamanda akauliza.
“Ndiyo, Bill kaja akaniteka hapa leo asubuhi na kunipeleka huko kwenye maficho yao,” Frank akaeleza. “Sasa nani kakuokoa?” lilikuwa swali la Kamanda.
“Si nimekwambia mi ni FBI yaani Federal Beureau of Investigation, sishindwi kujiokoa kwa watu dhaifu kama hawa,” Frank alitamba, sasa akiwa amevua ile kanzu ya kikasisi. “Laiti ningepata hiyo nafasi ningemmaliza huyo mtu palepale, maana sihitaji mahojiano naye, nimetumwa kuirudisha roho yake kwa muumba wake, bas,” Kamanda akamwambia Frank. “No Kamanda, sikiliza, unatakiwa unisaidie tumpate Bill akiwa hai, serikali ya Washington inamtaka akiwa hai ili akaungane na wenzake kule Guantanamo bay,” Frank akamwambia Amata.
“Hamna shida, mimi serikali ya Dodoma imenituma niitenganishe roho na mwili wake, so tutagawana, wewe utamchukua akiwa hai na mi nitamtoa roho yake,” Kamanda Amata alimwambia Frank, kisha wakatazamana si kirafiki tena sasa kiadui zaidi. “Na hapa siwezi kuishi, hapanifai, kwa heri ya kuonana,” Amata akamalizia, kisha akamuacha Frank bado amesimama akitweta kwa hasira wakati yeye anaifungua ile darubini yake pale dirishani.
Saa moja baadae, Kamanda Amata alikuwa nje ya uwanja wa misheni hiyo, hakuna aliyejua kuondoka kwake, akiwa kava kofia kubwa aina ya pama na miwani myeusi akasimamisha tax iliyokuwa ikipita mbele yake, “Novotel tafadhali,” Kamanda alimwambia Yule dereva, naye bila kushangaa alipiga gia na kusonga mbele, dakika chache walikuwa mbele ya hotel hiyo, “Deutsche Mark 75 tafadhali,” Yule dereva alimwambia Amata, “Bado unatumia hiyo pesa ya kizamani? Hapa nina Euro na Dollar,” Kamanda akmwambia yule dereva, “Ok, US Dolar 65” akabadilisha, Kamanda Amata akampatia pesa yake kisha akaiendea kaunta ya bhotel ile.
“Nikusaidie boss,” mmoja wa wahudumu alichukua suitcase ya Amata na kutangulia Kaunta kisha akasubiri pembeni.
“Jina tafadhali,” sauti ya mhudumu mrembo kama Malaika ikamuuliza Kamanda Amata. Kama unavyojua ugonjwa wa kamanda Amata, warembo, akatabasamu, “Fransisco Kintu,” akajitambulisha kwa jina bandia. Yule mhudumu akaandika kwenye kompyuta yake, “Passport yako au kitambulisho tafadhali,” Yule mhudumu akaomba vitu hivyo kimojawapo.
Kwa kuwa Kamanda daima alikuwa habahatishi, alivuta wallet yake na kuchomoa moja ya kitambulisho akampa, ‘Fransisco C. Kintu – Utaifa: Uganda – Kazi: Muandishi wa habari UBC.’ Maelezo hayo yalionekana juu ya kitambulisho. Baada ya kuingiza maelezo hayo katika kompyuta yake, akamrudishia kile kitambulisho. Kamanda Amata akauliza bei kwa siku, akatajiwa akahesabu fedha ya siku mbili akampa Yule dada, “Oh samahani bwana Fransisco, tuhitaji Maestro card au Visa card kama hauna basi kadi yoyote ya malipo,” Yule mhudumu alimwambia Amata, akili ya Kamanda ikafanya kazi haraka, “Samahani situmii hivyo vitu, ninalipa cash, kama haiwezekani basi.”
“Ok, nitakusaidia kwa leo, lakini mara nyingine ukija Ulaya hatulipi kwa cash, sawa bwana?” Yule mhudumu akamwambia Kamanda kwa lugha safi ya kiingereza.
“Ich danke Ihnen” (nakushukuru) Kamanda Amata alishukuru kwa Kijerumani msaada huo.
“Danke, gleichfalls!” (nakushukuru pia) Yule mhudumu naye akajibu, huku akisimama na kelekea sehemu Fulani, akaja na kadi mkononi akampatia, Kamanda Amata akaitazama, kisha akatoa kadi yake ya kibiashara na kumuwekea mezani, akaondoka pale kaunta na kuelekea ghorofa ya juu kwa kutumia lift.
175 ilikuwa ni namba iliyosomeka mlangoni mwa chumba hicho, Kamanda Amata kama kawaida yake aliingia ndani na kukikagua chumba hicho kwa staili ileile aliyoizoea kuona kama kuna chochote cha kufanya ajulikane uwepo wake.
9
CHAKULA cha jioni kilikuwa tayari, simu ikapigwa chumbani kwa Amata kutoka pale kwenye chumba cha chakula ambapo Fr Frank na wageni wengine walitumia. Simu iliita kwa muda mrefu haikujibiwa, ikarudiwa na kurudiwa lakini wapi. Ikabidi Fr Frank aende chumbani kwa Kamanda Amata akamwangalie, alipogonga mlango hakuna jibu lililotoka ndani, akanyonga kitasa na mlango ukafunguka, alipoingia ndani hakukuta mtu, chumba kilikuwa tupu, kitanda kilitandikwa vizuri kana kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa akikitumia chumba hicho.
Akili ikamzunguka Fr Frank, akaona sasa kazi yake inakuwa ngumu ya kumpata Bill akiwa hai kutokana na kutoweka kwa Kamanda Amata.
Fr Frank alirudi mezani akiwa na hasira, “Mgeni wetu hayupo, kaondoka bila kuaga,” wale wahudumu wakashangaa kapitia wapi kwa kuwa hawakumuona kupita hata katika mlango wa kutokea nje. Fr Frank ndipo alipoelewa maneno aliyoambiwa tangu mwanzo na wakuu wake wa kazi, ‘Mtazame sana Kamanda Amata, ni mjanja zaidi ya CIA, huyo ni TSA no 1 ana uwezo wa kujigeuza hewa,’ Fr Frank alipokumbuka maneno hayo akaanza kucheka mwenyewe, kisha akaketi na kuendelea kula huku akifikiri zaidi juu ya Amata, kama alitaka kufanya kazi aliyopewa kwa muda mrefu basi sasa ilimlazimu kubadili utaratibu huo kwani Kamanda Amata alitaka kuifanya kwa muda mfupi zaidi, kasheshe.
§§§§§
NOVOTEL AACHEN – CASINO
KAMA ILIKUWA ni siku ya bahati kwa Kamanda Amata basi hiyo ilikuwa mojawapo kati ya chache katika maisha yake. Alipotoka kaunta alipewa kijikaratasi kama brosure ndogo, hakuwa na muda wa kuifungua ndani, baada ya kujiweka sawa, alipomaliza kuoga na kuchagua suti safi kati ya zile alizozikuta ndani ya kabati hilo, akaijonge meza yake na kukinyanyua kile kijikaratasi kilichopambwa kwa rangi za dhahabu za kuvutia, akakifungua na kukisoma, kilikuwa ni juu ya shindano la kamali ambalo lingefanyika siku hiyo saa 3:30 usiku katika casino iliyopo katika hotel hiyo, matajiri wengi walialikwa, hakuamini kabisa kama katika walioalikwa alikuwemo Don Andreas.
Akajua hapo kuwa Don Andreas ni mcheza kamali maarufu sana kwa jinsi alivyoelezewa pale katika hiyo karatasi, pia matajiri wengine wengi walialikwa, hivyo hata yeye alipewa nafasi kama angependa kushiriki, ama kwa kutazama shindano hilo au kwa kushindana kama ana uwezo. Tabasamu pana likaupamba uso wa kijana shababi, Amata. Katika ile karatasi ya mualiko kulikuwa na namba za kupiga kama utahitaji kushiriki kucheza, akavuta simu ya mezani na kupiga hizo namba kisha akaongea na mchezweshaji wa huo mchezo na kusajiliwa. Kamanda Amata akasubiri muda ufike ili aweze kushiriki mchezo huo na pia kuonana na Don Andreas ana kwa ana.
SAA 3:00 USIKU
POKER POINT
WAGENI walianza kuingia katika ukumbi huo mkubwa wenye kila aina ya starehe, huku kukiwa na muziki wa jukwaani ukipigwa na mwanamama mkongwe aliyealikwa siku hiyo Tina Turner kutoka Marekani. Watu walikuwa wengi na kila mmoja alionekana akiwa ametingwa na shughuli zake ama kunywa pombe na wapenzi wao au wakicheza michezo kama roulette, slots machine, lucky wheel na mingineyo mingi.
Ni meza moja kubwa sana ilibaki wazi hakuna mtu aliyeketi kwenye viti vilivyozunguka meza hiyo, viti kumi na nne, saba kwenye mstari wa mbele uliopakana na meza hiyo yan kijani yenye michoro kadhaa na saba vingine vilikuwa nyuma yake, lundo la karata maalum zisizochoka lilikuwa limewekwa hapo juu, taa angavu kabisa isiyokusumbua macho ilikuwa ikiwaka na kumulika eneo lile nyeti kwa watu nyeti. Mmoja baada ya mwingine waliingia eneo lile wakisindikizwa na akina dada warembo kabisa na kuwapanga vitini kwa namba. Baada ya kutimia vilibaki viti viwili, kimoja cha mbele na cha nyuma cha mpambe.
Wote walishangaa kumuona mtu anayeletwa na mwanadada mrembo, kijana mweusi, aliyependeza kwenye suti nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe na tai ndogo ya kubana shingo (neck tie), akakribishwa na kuketi katika kile kiti kimoja, akawatazama mmoja baada ya mwingine kisha mchezo ukafunguliwa na mchezeshaji akiwataka wachezaji kujitambulisha mmoja baada ya mwingine. Kila mmoja alijitambulisha na Kamanda Amata alijitambulisha kwa jina lile la bandia akijisema kuwa yeye ni mwanahabari lakini ni mcheza kamali mzuri sana katika macasino ya Afrika Mashariki.
Akakribishwa kwa kupigiwa makofi. Kamanda Amata alijikuta akiwa amekaa uso kwa uso na Don Andreas. Mtu mmoja mnene, mwenye sura ya tabasamu muda wote, alikuwa akimtazama kijana huyu bila kummaliza. Mchezo ulianzishwa na kila mmoja alitakiwa kuweka dau la kuanzia lisilopungua $ 2500, matajiri hao wakaanza kuweka na kuweka pesa zao kwa kutumia chungu maalumu kilichopitishwa mezani na mmoja wa wachezeshaji. Kila mtu aliweka kiwango anachojua kuwa anaweza kumudu. Zamu ya Kamanda Amata, kila mmoja alimtazama usoni, akaingiza mkono ndani ya koti na kutoa $ 5000 na kuweka katika chungu hicho. Mcehezo ukaanza taratibu kila mtu akiwa na karata zake. Mchezo ulikuwa mgumu kidogo kwa maana kila mmoja alikuwa anatumia akili sana katika kuzifananisha karata hizo na zile zilizofichwa, kila aliyeshindwa alitoka, hivyo wakazidi kupungua, Kamanda Amata alikuwa wa nne kutoka na kuwaacha watatu, Don Andreas, na tajiri kutoka Venezuela pamoja na mwanamama tajiri kutoka Berlini. Mchezo ukaendelea na mwisho wa mchezo Don Andreas akatoka mshindi na kukusanya maelfu ya dola za Kimarekani.
Makofi ya pongezi yakatawala katika meza ile. Mchezo ule ukaisha, ukatakiwa kuanza mwingine kwa wale wanaohitaji kuendelea. Wote walirudi tena mezani na ‘betting’ zikaanza kwa mara nyingine, chungu kikapita na kila mmoja akatia mkono kuweka chochote lakini wenzako sharti waone kile uwekacho, zamu ya Kamanda Amata, kama kawaida wote walimtolea macho, akaingiza mkono wake tena katika koti na kutoa kitita kama kilekile, $ 5000 zingine akaweka, wengine katika katika mchezo ule wakaguna, kwa jinsi walivyomtazama hakuwa na muonekano wa kuwa na pesa kiasi hicho anachotoa katika kila bett moja. Yeye mwenyewe hakuwajali, kwa kuwa hakuna aliyejua mpaka hapo kuwa ni nini anachokitafuta, hivyo hakuona tatizo kutumia pesa hizo anazopewa maalum kwa ajili hiyo ili kupata kile anachotaka. Mchezeshaji aliendelea kuchezesha mchezo ule kwa makini na mbwembe za hali ya juu. Mchezo ukaendele, poker, mchezo wa karata ambaon unatakiwa ucheze kwa kupanga kareta zako zifanane na ile iliyofichwa ambayo hakuna anayeijua, mchezo wa matajiri unaochezwa kwa kuwekeza pesa nyingi, wengine huweka magari au majumba.
Kamanda Amata mchezo huu aliupanda sana na sehemu yake kubwa ya kucheza ilikuwa pale New Africa casino, Dar es salaam. Wachezaji walianza kupungua katika mchezo kwa kuwa hawakufaulu, walizidiwa maarifa na wengine, mara hii Kamanda Amata alidumu katika mchezo, japokuwa hakushinda lakini alitoka wa pili na mchezo wa mwisho alicheza na Don Andreas, ambapo alizidiwa kwa ujanja mdogo sana.
“Mr Fransisco, unaweza kucheza tena kwa kuwa umeikaribia bahati, umekaribia utajiri, weka dau lingine na ucheze tena. Kamanda Amata alijikuta hana pesa zaidi, alikuwa na kiasi kidogo ambacho hakingefaa sana kununua token. Mchezeshaji akawapa breki ya kujiweka sawa. Kamanda Amata akainuka na kuelekea kaunta ambako aliagiza glass moja ya pombe kali, akinywa taratibu huku akiandika ujumbe kwa kupitia saa yake kwenda kwa Madam S, dakika moja baadae, alipata majibu na akayafanyia kazi. Mara moja akafanya mchakato palepale hotelini kuweza kubadilisha pesa aliyotumiwa na Madam S, $ 1500 si haba kwa mchezo huo wa mwisho kwa mujibu wa Yule mchezeshaji.
Meza ilijaa tena wadau, kabla hawajaanza mchezeshaji akatoa rai yake kama ilivyo sheria ya mchezo.
“Sasa tunaingia raundi ya mwisho, tumeona wote waliofanya vizuri katika raundi zilizopita, tumeona pia uchezaji wa mgeni wetu kutoka Uganda si mbaya sana, sasa angalisho, kila mtu aweke dau ambalo hatoathirika katika akiba yake baada ya kushindwa mchezo huu,” akamaliza kusema kisha akzungusha chungu, wote wakaweka mapesa kibao, mmoja wao, Yule tajiri wa Venezuela alikuwa ameishiwa na kubaki na kiasi kidogo, akaweka dau gari yake ya thamani, Marcedes Benz CLA45 AMG 4MATIC 355-hp. Ilikuwa ni gari mpya kabisa, toleo jipya ambalo thamani yake si ya kitoto. Kamanda Amata akatupia katika chungu kile $ 1500 kama zilivyo, kila mtu akaguna tena, lakini hawakuguna kwa Yule aliyeweka gari kwa sababu walijua kuwa ana uwezo wa kununua nyingine.
Mchezo ulianza na kila mtu alikuwa makini sana mara hii, hakuna aliyetaka kupoteza mchezo huwo wa thamani kwa maana atakayeshinda atakuwa ni milionea wa kutupwa kwa pesa atakazokusanya. Lakini kamali ni kamali tu, mmoja baada ya mwingine walianza kupanguka.
Mwisho wa mchezo wakakutana Don Andreas na Kamanda Amata. Ilikuwa ni nafasi nzuri sana kwa Kamanda Amata kutazamana uso kwa uso na tajiri huyo ambaye siri ya safari yake pale Ujerumani iko ndani ya kifua chake. Don Andreas alikuwa haelewi afanye nini, mara ajishike nywele, mara shavu, mara ajikune ilimradi kutaka kushinda mchezo huo wa dhahabu, wakati Kamanda Amata alikuwa katulia kitini akimtazama kwa makini tajiri huyo anavyochachawa. Wakati mchezo huo ukiendelea, kijana mmoja aliyevalia suti safi nyeupe aliingia pale mezani na kuzunguka nyuma ya Don Andreas akamnong’oneza kitu, Don Andreas alipata mshtuko wa mbali kidogo ambao mpaka uwe mzoefu wa mambo ya kiintelijensia ndio waweza kugundua. Kamanda Amata aliisoma hali hiyo, akapata hisia ya kitu Fulani. Mchezeshaji alimuhamasisha Andreas kucheza. Mwisho wa mchezo, Kamanda Amata akaibuka mshindi, makofi mengi yalitawala wakatia akikusanya kete zote kuwa ni ushindi wake, pamoja na funguo ya gari ile ya kisasa, aliegemea kiti chake na kumtazama Don Andreas aliyeonekana kuchoka ghafla kitini mwake. Wale wengine walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine kwa maana mchezo ulikuwa umefikia mwisho. Kamanda Amata aliiegemea tena meza na kumtazama Andreas.
“Sasa tucheze mimi na wewe, wawili tu,” Kamanda alimwambia Andreas. Don Andreas alimtazama Kamanda Amata.
“Sina dau kwa sasa la kupoteza, wewe tumia utajiri uliopata,” Don Andreas akamwambia Amata huku akijiandaa kuondoka, wapambe wake tayari walikuwa wamekwishafika. Kamanda Amata akamzuia Don Andreas kwa kumgusa kiganja cha mkono alichokisahau mezani, akastuka na kumtazama Kamanda, “Dau unalo, tena la gharama sana,” kamanda Akamwambia Don. Tabasamu la uongo likatoka katika sura ya Andreas.
“Mostrance, weka dau Mostrance,” kamanda Amata alimwambia Don. Neon hilo lilimfanya Don Andreas kukunja sura ghafla na kurudi sawia kwenye kiti chake kama awali, “Unasemaje Mr…” kabla Andreas hajamaliza kutaja jina, Kamanda Amata akajitambulisha rasmi, “…Kamanda Amata,” akamalizia. Ilikuwa ni kama tetemeko la ardhi ka Don Andreas kujua kuwa yupo na nani mbele yake. “Hutoliona jua la kesho kijana,” Andreas akamwambia Kamanda Amata.
“Kama wewe ndiwe umeweka jua liangaze mchana, sawa, ila kama si wewe nitaliona, ila wewe na Bill sijui nani ataliona kati yenu,” Kamanda Amata alinyanyuka kitini na kuanza kuondoka huku yule mchezeshaji akikusanya zile kete tayari kuzibadili kuwa pesa ili apatiwe Kamanda Amata. Kamanda Amata alipoanza kuondoka akakutana na binti mmoja mzuri wa sura, mavazi yake yalionesha asilimia 80 ya mwili wake usiokuwa na nguo, wakasimama na kutazamana nyuso zao, Yule binti akatabasamu, tabasamu la
wizi, kamanda Amata akamshika kiunoni na kuondoka naye mpaka kaunta ambako aliagiza kinywaji na kuanza kukimiminia kinywani mwake huku cheers nyingi na Yule binti, Kamanda alikuwa millionea ghafla, lakini alijua wazi hatari inayomkabili muda huo.
“Unahitaji cash au tukuwekee katika akaunti yako?” sauti ilitokea kaunta ikimuuliza Kamanda juu ya pesa zake, “Weka kwenye akaunti kisha nipe namba ya muamala wangu kwa ajili ya kuhakikisha,” alimjibu yule mhudumu wa kaunta.
“Beibi, nimekupenda ghafla,” Yule mwanamke alimwambia Amata. “Usijali leo ni mimi na wewe mpaka majogoo yawike,” kamanda Amata aliongea kwa Kijerumani cha kubabaisha, “Mmmm aliyekwambia huku kuna majogoo ni nani?” Yule binti alizidi maneno ya mtego, “Aaaaa jamani majogoo huyajui,” Kamanda Amata akawuliza Yule binti. Alipokabidhiwa kadi maalumu yenye namba za muamala wake, akamshika mkono Yule binti na kutoka nae pale kaunta, hatua mbili, mkono mmoja ukazungushwa kiunoni, wakapotelea nje ya hotel hiyo.
§§§§§
BILL VAN GETGAND alishusha mtemba wake kutoka kinywani, akapuliza moshi mwingi hewani na kusababisha mchafuo wa mazingira kutokana na huo moshi taka, akashusha kioo cha gari iliyombeba mpaka chini kabisa, kisha akatupa kipisi kilichobaki kwa kulenga katika kasha maalum la takataka liliwekwa hapo jirani na maegesho.
Alimtazama Kamanda Amata akitoka na Yule binti wa kizungu, wakiwa wamekumbatian viunoni, walipolifikia lile gari, wakakumbatiana kwa kutazamana, wakapeana mabusu ya kuinyonyana ndimi zao. Kengele za hatari zikagonga katika kichwa cha Amata, akatoa miwani yake na kuivaa, alipotazama kwenye maegesho akashuhudia kioo cha Vogue kikimalizia kupanda juu, akajua kuna kitu.
“Uko peke yako?” Kamanda Amata akamuuliza.
“Yeah, peke yangu,” Yule binti akajibu.
“Huwa unakuja kufanya nini hapa?” swali lingine kutoka kwa Kamanda.
“Mmmmm huwa nakuja kutafuta wanaume wazuri kama wewe,” akajibu Yule binti. Kamanda Amata akaminya kitufe kwenye funguo ya gari aliyopewa na Benz moja nyekundu ikawaka taa zake kuashiria kuwa ndiyo yenyewe, akaiendea na kufungua milango akajitoma nyuma ya usukani, na Yule binti akakaa pembeni.
“Unanipeleka wapi?” akauliza Yule binti.
“Beach,” kamanda akajibu huku akiondoa gari ile katika maegesho. Nyuma yake ile Vogue nayo ikaondoka, lakini haikuwafuata njia waliochukua wao. Kamanda Amata aliendesha gari hiyo taratibu sana akiizunguka mitaa ya mji huo mkongwe kabisa huko Ujerumani, huku akiwa macho yake yakitazama nyuma, mbele kwa umakini mkubwa sana kujua kama kuna anyemfuata au vipi.
Kamanda Amata aliendelea kuzunguka katika mitaa ya mji huo bila kuegesha gari popote huku akiwa hana maongezi yoyote na Yule mwanamke katika gari hiyo.
“Hey beibi, mbona huongei, na wala huniambii unanipeleka wapi? Mi nataka twende kwangu,” Yule mwanamke alimuuliza na kumwambia Amata ambaye alikuwa ametingwa na usukani wa gari hiyo.
“Najaribisha gari yangu mpya, usijali, nikichoka tutakwenda kwako,” Kamanda Amata alimjibu Yule bibie huku akiendelea kuchapa mwendo, akipita barabara hii na kutokea barabara ile. Mara nyuma yake akasikia ving’ora vya polisi vikija upande wake, akaangali kwenye kioo cha kuendeshea gari akaona gari mbili za polisi zikija kwake, akaongeza mwendo na zile gari zikawa zinakuja kwa kasi. “Polisi,”Yule mwanmke akamwambia Kamanda.
“Usiogope, hao sio polisi, kwa jinsi wanavyoendesha gari,” Kamanda Amata akajibu.
“AA 768 G weka gari pembeni!!” ilikuwa sauti kutoka katika kipaza sauti ambacho polisi wale walitumia kumsimamisha Kamanda Amata, lakini badala ya kusimama aliendelea kutimua mbio na gari lile, sasa alitembea mwendo wa hatari zaidi. Kamanda Amata kwa ujumla alikuwa akijua kuwa Andreas, Bill na vibaraka wao lazima watakuwa wakimnyemelea katika mitaa hiyo hivyo hakutaka kuuacha mji ule mapema wala hakutaka kurudi hotelini mapema ili aone nini mwisho wake, alishajua kuwa kurudi hotelini ni kujiweka kwenye hatari zaidi.
“Unaitwa nani?” ndio kwanza Kamanda Amata anagundua kuwa hakuwa amemjua kwa jina yuel mwanamke.
“Naitwa Hellen,” akajibu huku akijinyoosha kwa kujipindapinda mwili wake klitu ambacho kilimsisimua Kamanda Amata hasa alipokuwa akikiona kile kifua kilichopambwa na matiti mawili mazuri yakiyotuna kwenye kigauni hicho chepesi sana.
“Hellen, unamfahamu Don Andreas?” Kamanda Amata akauliza.
“Ndio, namfahamu sana, kwani kuna mtu ambaye hamfahamu tajiri huyo matata hapa mjini? Kibosile mpenda vimwana, vipi una shida naye?” Hellen akajibu na kurusha swali.
“Hapana siwezi kuwa na shida na mtu masikini kama Yule,” kamanda Amata akajibu huku akimtazama Hellen, wakati huo ile Mercedes Benz ilikuwa inasoma 158 km/h, mwendo mkali kwelikweli. “Mr Francisco, unajua wewe ni mgeni sana hapa Aachen,” akaanza dodoso zake za kike.
“Hapana, huwa nakuja mara nyingi sana hapa ila wewe hujawahi kuniona, kwa nini unauliza?” kamanda Amata aliendeleza mazungumzo kwa kuwa alijua nini kitafuata. “Usimwite Andreas masikini, ana masikio zaidi ya million hapa Aachen,” Hellen aliongea kwa mapozi.
“Oooh, sikujua huyo atakuwa shetani basi, maana binadamu kawaida ana masikio mawili tu,” Amata akajibu kwa utani, lakini alipomwangalia Hellen akaona hata kutabasamu hakupo usoni mwake, akajuwa kuwa sasa kaanza kumfika moyoni kwa maneno yale. Hellen alimtazama Kamanda Amata hakummaliza, akaingia za mkono wake mkobani na kutoa kitu kama kikebe cha wino wa mhuri, akakifungua, ndani yake mlikuwamo na sigara tano na kiberiti cha gesi, vyote viliweza kutosha ndani ya kikebe kile. Akachomoa sigara moja na kuiweka mdomoni, akamtazama Kamanda Amata, kabla hajafanya lolote Kamanda Amata aliitambua ile sigara, haikuwa sigara bali ni mfano wa sigara ambayo ukiiweka mdomoni na kusukuma pumzi kwa nje, sio kwa ndani kama kawaida ya kuvuta sigara, hutoa vumbi jepesi sana ambalo litakupa usingizi ndani ya sekunde kumi tu.
Kamanda Amata alimnyang’anya ile sigara na kuitupa pembeni, Hellen alipiga kelele, na kitendo hicho kilimfanya Kamanda Amata kukanyaga breki za ghafla akiwa katika mwendo mkali. Hellen alikuwa hajafunga mkanda hivyo alichomoka kwenye kioo cha mbele na kutoka mpaka nje akadondokea barabarani. “Bull shit!” aling’aka Amata, akakanyaga klachi ya gari hiyo na kuweka gia ya kurudi nyuma na gari ile ikatii amei pale alipoachia klachi na kutimba pedeli ya kusukuma mafuta, kona moja kali ikamgeuza kutazama alipotoka na kutupia namba moja, kisha mbili, mara tatu, akawa amemuacha Hellen pale barabarani akiwa hoi na yeye kurudi kwa kasi alikotoka. ‘Mwanamke mpumbavu sana huyu,’ alijisemea moyoni huku akiongeza kasi ya gari lile ambalo injini yake bado ilikuwa ikidai gia ya sita wakati tayari zilikuwa zimekwisha zile zilizopo. Akiwa katikati ya mawazo yale na kumsonya Yule mwanamke huku akimtukana kimoyomoyo, aliona taa kali zikimmulika usoni akashindwa kupambanua njia halisi iko wapi na hicho pele ni kitu gani.
Puuuuuuuu!!!!! Kishindo kikubwa kikasikika, gari aliyokuwa akiendesha Kamanda Amata ilikutana uso kwa uso na katapila la kutengeneza barabara, ilijipiga kwenye jembe la chuma cha pua, ikapinda boneti yote kuelekea kwenye kioo cha mbele, kisha lile katapila likainamisha jembe lake na kuiangusha ile gari na kuibonda vibaya, ikaibeba tena na kukokota mpaka kwenye jalala la kutupa magari mabovu. Yule operetta wa lile katapila aina CAT aliinua simu yake ya upepo na kuongea na watu walio upande mwingine, “Kazi tayari boss (…) hawezi kutoka mpaka Yesu arudi amtoe kimiujiza,” kisha akakata ile simu na kuegesha katapila lake pembeni. Range Rover Vogue, lilifika katika jalala lile ambalo halikuwa mbali sana na pale ilipotokea ajali ile ya kutengenezwa, ikasimama na watu wanne wakashuka, Bill akiwa mmoja wao mkononi akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea.
“Mali hiyo hapo boss,” Yule operetta akamwambia Bill huku akimuonesha kwa mkono ile Marcedes ilivyopondwa na kuwa chuma chakavu kwa ghafla namna hiyo.
“Vizuri sana, alikuwa ananiumiza kichwa sana huyu jamaa, akapumzike kwa amani, jivu kwa jivu. Vumbi kwa vumbi,” Bill alipomaliza kusema hayo, akampa Yule jamaa kitita cha noti kama shukrani kwa kazi hiyo ndogo aliyoifanya. Kisha wao wakarudi garini na kuondoka usiku ule, akaigeuza taratibu Yule drva na kuchukua uelekeo ule waliojia, Bill akainua fimbo yake na kuigemeza dirishani, ncha ya kutembelea ikwa imetazama kule aliko Yule operetta, akakifyatua kijichuma kidogo kilichoupande wa mshikio na kukivuta kwake, lo, Yule jamaa alikuwa akishangaa kuiangalia ile Vogue huku akiwa haamini kupata kile kitita cha noti, alijikuta akipenywa na kitu kama msumari kifuani mwake, mara akadondoka na kuanza kuona macho yake yanakuwa mazito kama yaliyojawa na ukungu, tayari kulikuwa ni giza muda huo lakini giza linguine zito lilimfunika, roho yake ikaacha mwili. Bill alikuwa amemuua operetta Yule kwa risasi kutoka katika hiyo anayoifanya ni fimbo ya kutembelea. Kijana mmoja kati ya wale waliokuwa garini pamoja na Bill akashuka na kwenda mpaka pale kwa Yule operetta marehemu, akachukua ile pesa na kurudi garini, akamkabidhi Bill. “Kazi ngumu lakini imekwisha bila jasho, alale pema peponi Kamanda,” Bill alizungumza na ile gari ikaondoka eneo lile.
§§§§§
DON ANDREAS hakuamini anachoambiwa na Bill kuwa Kamanda Amata hayupo duniani. Akiwa katika sebule yake kubwa pamoja na mgeni wake kutoka Vatican, Fr Gustav Maker wakijivinjari kwa vinywaji vikali, wote waliifurahia taarifa hiyo kutoka kwa Bill. Dakika chache baadae Bill aliungana nao hapo sebuleni na tafrija isiyo rasmi ikaendelea.
“Kazi haikuwa rahisi mjomba,” Andreas alikuwa akimsimulia Fr Gustav juu ya mkakati mzima mpaka kuipata ile Monstrance.
“Pole sana mjomba lakini maadam umeipata basi utajiri wako utakuwa wa milele,” Gustav alimwambia Andreas, akinua glass yake iliyojaa kinywaji na kujimiminia kinywani mwake, kisha akamwangalia Andreas na Bill, “Iko wapi hiyo Monstrance?” akauliza.
“Ipo katika chumba cha siri,” Andreas akajibu, “Unataka kuhakikisha kuwa ipo au la?” akamtupia na swali.
“Yeah, hilo ni la msingi, nipeleke nikaione,” akaomba. Andreas aliinuka pamoja na Bill kisha wakafuatwa na Fr Gustav. Wote watatu wakaingia chumba cha siri ambacho ni mtu mmoja tu mwenye dhamana ya kukifungua, Andreas mwenyewe kwa kuwa mlango wake unahitaji, namba maalumu ya kubonyeza, alama ya kidole gumba na alama za macho, vyote hivyo ni vya Andreas, walipofika pale alifanya hayo yote, kisha wqakafunga kwa ndani na kuingia huko ilikohifadhiwa hiyo monstrance.
Fr Gustav, akaitazama ile monstrance kwa makini sana ikiwa imelazwa juu ya kijisanduku kidogo ambamo ilitosha kabisa, akainyanyua na kuigeuzageuza, ilikuwa iking’aa sana kutokana na taa iliyokuwa ikiwaka ndani ya chumba kile, ilikuwa ni dhahabu safi ambayo haijachakachuliwa bado. “Niliambiwa kuwa monstrance hii ina siri kubwa sana ndani yake, lakini mpaka sasa sijaijua,” Andreas alimwambia Fr Gustav.
“Ni kweli, na nimekuja hapa kwa sababu hiyo tu, hii Monstrance lazima irudi Vatican,” Kwa kauli hiyo, Andreas na Bill walibaki wakitazamana kabla ya wote kumgeukia Fr Gustav. “We una kichaa ee!” Andreas alimwambia Gustav.
“Hata kama nina kichaa, lakini monstrance hii lazima irudi Vatican, siri iliyomo nitakwambia lakini hiki chombo lazima kirudi”
Gustav akaishika katikati ile monstrance mkono mmoja upande wa kitako na mkono mwingine upande wa juu akainyoga katikati kama anaivunja au anaifungua, ikafunguka, kisha akaweka kitako chini, akabaki na kipande cha juu. Don Andreas alikuwa bado akishangaa hakujua kuna nini kinafanyika. “Na hii ndiyo siri iliyomo katika chombo hiki,” Gustav akawaambia huku akiinamisha na kikaratasi kirefu kikatoka ndani ya kile kibomba kidogo ambacho hushika kitako na sehemu ya juu ya chombo kile.
Gustav akaiweka chini ile monstrance na kuchukua ile karatasi, akaifunjua kunjua kwa uangalifu, ilikuwa ni ramani kubwa sana inayoonesha njia za kupita mpaka kwenye hazina kubwa ya madini ya dhahabu iliyojificha huko kwenye milima ya Peramiho, kusini mwa Tanzania, mawe makubwa amabayo chini yake kulikuwa na kama mapango yenye madini ya thamani. Andreas ilikuwa nusu azimie kwa kkile anachokiona, alikuwa akisoma maandishi yale ya kijerumani huku akiwa na tabasamu pana kuliko sura yake. Alipomaliza kuitazama ile ramani na kuyasoma kwa ufasaha yale maandishi yaliyoandikwa karne kwa karne lakini hayakuwa yamefutika, bado yalionekana kwa upya wake. Andreas alitingisha kichwa chake kuashiria kweli amekubali maneno ya babu yake. “Gustav, tumekuwa matajiri wa maisha,” Andreas alimwambia Gustav. “Ni kweli, lakini unajua hazina hiyo hiko wapi?” akauliza.
“Tanganyika kwa maelezo haya, ambayo ni Tanzania ya sasa,” Andreas alijibu.
“Na utaendaje huko kufanya hiyo kazi?” lilikuwa swali la Gustav.
“Aaah Gustav, hiyo sio shida, ni kwenda pale na kununua eneo lote lile, pesa ninayo, watanikubalia tu wale masikini kisha tunachimba. Siri ni uwekezaji tu, tukishawapa kishika mkono basi viongozi wataachia njia,” Andreas alisema kwa kujiamini.
“Haya nakutakia kila la kheri, lakini mmefanya kosa kubwa moja ambalo mimi sikulifurahia,” Gustav akaikatisha furaha ya Andreas.
“Kosa gani?” akauliza.
“Kosa ni watu uliowatumia, kumuua Fr Gichuru ni kosa kubwa sana ambalo usipoangalia litakugharimu,” Gustav akamwambia Andreas.
“Kama amekufa amekufa tu,” Bill akashindilia msumari wa mwisho katika hilo. Andreas akaiweka ile ramani juu ya kijimeza kidogo kwa minajiri ya kuja kuisoma vyema baadae, kisha wote watatu wakatoka nje ya chumba hicho na kikafungwa tena kama klilivyokuwa mwanzoni.
§§§§§
10
KAMANDA AMATA alijikunguta vumbi, alijitazama hapa na pale alikuwa na michubuko michache lakini alisikia maumivu makali sana katika mkono wake wa kulia, akajaribu kuunyoosha na kuufanyisha mazoezi. Kidogo ukakaa sawa. Akajiangalia zile silaha zake nyeti ambazo huzificha ndani ya nguo zake, bastola yake ilikuwepo, camera na vitu vingine vyote vilikuwa vimetimia, kwa hatua za taratibu alijivuta kurudi barabarani.
Ulikuwa ni usilku mnene sana ambapo hakukuwa na magari mengi katika barabara hii ya kutokea nje ya mji wa Aachen, zaidi yalipita malori. Alitembea hatua za taratibu akipandisha kilima kidogo kilichokuwa hapo, alipofika juu, alikuta kuna Motel, taa zilikuwa bado zikiwaka na magari machache yalikuwa yamepaki nje yake. Akaiendea motel hiyo na kuingia ndani, kulikuwa na watu wachache ambao walionekana washari washari hivi, wakiwa wamevaa kiuni, wengine wakilewa [pombe na wengine wakiwa wanacheza kamali.
“Nahitaji msaada,” alimwambia Yule mwanadada wa kaunta.
“Tukusaidie nini?” Yule dada alijibu kwa Kijerumani safi. “Mna box la huduma ya kwanza?” akauliza Amata. “Ndiyo; bila shaka,” Yule mhudumu wa kaunta akajibu na kuingia nyuma ya kaunta akatoka na kikasha chenye alama ya msalaba mwekundu akampatia, Kamanda Amata akafungua ndani yake, akatazama akakuta kuna dawa aina ya Iodine akaichuku, bomba moja la sindano na kijichupa kidogo cha dawa aina ya Diclofenac, akavua shati, akaliweka pembeni, katika mkono wake palikuwa na jeraha kubwa kiasi kutokana na mburuzo alioupata alipokuwa akiruka kutoka ndani ya ile gari kabla haijagongana na katapila, akajipaka ile iodine huku akikunja sura kutokana na maumivu ya dawa hiyo, akaijiwekea na pamba kisha akamuomba Yule mhudumu wa kaunta amfunge bandeji naye akatekeleza hilo. Kamanda Amata alipoona kuwa hapo amekamilisha akajidunga sindano ya Diclofenac kutuliza maumivu.
Akaismama na kutoa shukrani kwa Yule dada, akavaa shati lake jeupe ambalo sasa lilikuwa halitamaniki kwa vumbi. Alipokuwa akitoka, mlangoni alikuta kuna majaketi yametundikwa, akajichagulia moja la rangi nyeusi akajitupia juu yake na kutoka nje, hakuwa na usafiri. Akatazama magari yaliyoegeshwa hapo, akaona moja inayomfaa. Ford Cortiner ya rangi ya buluu ilikuwa imeegeshwa pembeni kidogo mwa jengo hilo na mwenyewe alikuwa ameliacha likiunguruma yeye akiwa ndani kunywa kahawa, bila shaka lilikuwa linatoka safari ya mbali, Kamanda Amata aliingia na kukanyaga mafuta akarudi barabarani, muziki mzuri wa You are not alone uliopigwa na Michael Jackson alikuwa ukitumbuiza. Saa katika dashboard ya gari hiyo ilionesha ni saa nane za usiku ikielekea saa tisa.
Mwendo haukuwa wa kawaida barabarani, Kamanda Amata akili yote ilikuwa imehamia kwa Bill, sasa alikuwa anataka kumaliza biashara yake na Bill. Alikata mitaa michache na kushika barabara inayopita mbele ya kanisa kuu, akalitazama kwa mbali na kupitiliza, akalikaribia hekalu la Don Andreas, kwa kujifanya kuwa hana kazi nalo alipitiliza na kwenda kusimama mbali kidogo, akaegesha gari karibu na kituo cha mafuta, akaliacha linanguruma kama alivyolikuta, alipokuwa anatoka akawasha taa ya ndani kuangalia hiki na kile, hakuamini macho yake alipoiona AK 47 double barrel, akaitoa na kuvunja katikati kama kawaida, haikuwa na risasi, akapekua hapa na pale akakutana na kikebe chenye risasi kama kumi hivi akakichukua, akajaza risasi zote katika mashine hiyo na kujivuta kwa mguu kulielekea jumba hilo lenye ulinzi mkali. Haikumchukua muda kuifikia himaya hiyo yenye utulivu wa pekee, kwa nje ya jumba hilo alifanikiwa kuona gari mbili zimeegeshwa, moja ikiwa ni ile Vogue, ‘Hisia zangu zimesema kweli, Bill yupo hapa na atafia hapa, leo sina huruma na kiumbe cha mtu,’ kamanda Amata alijisemea moyoni, hasira ikiwa inamtawala kila baada ya nukta. Alitazama ulinzi ulivyojipanga akaona kuwa juu kuna walinzi lakini hakujua atafanyaje wasimuone.
Akachomoa bastola yake yenye kiwambo cha sauti, akamlenga mmoja na kumpata sawia kichwani, bajati nzuri aliangukia juu kulekule. Akaona sawa, mmoja tayari, alipokaribia ule wigo wa wavu maalum, akasita, kitu kikamwambia geula kulia, alipogeuka akakutana na taa kubwa inayoongozwa na sense, ukiingia umbali Fulani kutoka ule wigo, taa ile inakumulika kwa mwanga mkali na vingola vinaasha walinzi, hakuwa na mda wa kuhangaika na taa ya mtu, akaifumua kwa risasi moja, kisha akarudi nyuma na kutimua mbio kuuelekea ule wigo akapiga samasoti maridadi kabisa akapita juu ya wigo ule bila hata ya kuugusa, alipotua tu tayari AK 47 ilikohoa na kumteremsha mlinzi mwingine mpaka chini, alipogeuka kushoto kuna mwingine, kwa kutumia bastola yake akamfyatulia moja makini sana iliyochana bega upande wa moyo, Kamanda Amata akahama pale alipokuwa kwa maana alijua ataonekana, akapenya katika ya maua na kuifikia maiti ya mlinzi mmoja akaivua shot gun semi automatic, akaibeba mgongoni. Kamanda Amata akaendelea kusafisha nje kote, alihakikisha si mbwa si binadamu habakishi kitu.
Milio ya risasi ilifikisha taarifa ndani kuwa huko nje hakufai, Bill akanyanyuka na kuwaambia vijana wake wawe tayari. “Bila Shaka, tumevamiwa,” akmwambia Don Andreas ambaye alionekana wazi presha ikipanda. “Nani atuvamie wakati Kamanda amekwishakufa?” Bill akatoka nje ya nyumba hiyo, hakuna mtu, akiwa amefyumu kwa hasira, akiwagombeza vijana wake kwa uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi. Akarudi ndani, hakumkuta Don Andreas, kaenda wapi, bahati nzuri vyumba vyake vya siri Bill anavijua, akaingia cha kwanza, cha pili akamkuta, “Hapa si pakukaa Andreas, tuondoke,” Bill alimwambia Andreas.
“Ramani ile pamoja na monstrance lazima tuondoke nazo,” Andreas alimsisitizia Bill, “Don, hatuna muda huyu jamaa ni kichaa,” Bill aliendelea kumnong’oneza. Wakatoka pamoja pale mafichoni na kuukimbilia mlango mkubwa lakini Andreas akarudi tena akiuendea ule mlango ambao una zile hazina zake zote. Bill alimtazama Andreas akiwa anahangaika kuufungua ule mlango. Bill akapotelea upande mwingine wa jumba hilo, sasa akiwa na bastola yake mkononi, akimuwinda huyo aliyevamia.
Kamanda Amata alikuwa akinyata kuuelekea mlango wa siri uliokuwa ukitokea upande wanyuma, aliutazama mlango ule ulikuwa wa chuma imara, sio shida, akaizungusha saa yake nayo ikaanza kuzunguka kwa kasi na kutoa mionzi iliyoweza kukata eneo la kitasa la mlango ule, aliporidhika akaizikma ile saa, akaujaribu mlango ukafunguka bila kipingamizi, akajitoma ndani. Akiwa katika kutembea taratibu, akahisi kitu kama kitu chenye ncha kali kikipenya eneo Fulani la shingoakaanguka chini na kupoteza nguvu, alijaribu kupambana na hali hiyo ikawa ngumua sana, akakumbuka vidonge alivyopewa na Madam S, akapenyeza mkono wake kwenye mfuko wa ndani wa suruali akachukua kimoja na kutumia nguvu yake ya mwisho kukimeza, mara akalegea na kujilaza.
“Ha ha ha ha ha ha ndege mjanja hunasa katika tundu bovu,” Kamanda Amata alisikia sauti hiyo kwa mbali sana, akafumba macho. Mara akasikia kitu kama kiatu kikimkanyaga kwa nguvu kichwani mwake. Akaamka l;akinin hakuonesha kukurukakara yoyote, bado alikuwa palepale chini, “Utafia ughaibuni, Mbwa mweusi wewe, wewe unaweza nkujifanya polisi wa dunia wewe? Wenzako FBI wamefeli, we una nguvu bgani na hiko kishirika chenu cha upelelezi kuvuka mipaka kuja huku, sasa leo ndio mwisho wako, nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,” Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
§§§§§
FR FRANK Edson, alipojuwa kuwa Kamanda Amata ameingia katika mtanange hivyo anaweza kumuwahi kumpoteza Bill ilhali yeye anatakiwa ampeleke akiwa hai, aliamua kuyavulia maji nguo na kujikita katikati ya hatari hiyo, alilivamia jumba la Don mapema sana hata kabla Bill hajarudi akajificha katika moja ya stoo zilizokuwa ndani ya jumba hilo. Kwa bahati mbaya au nzuri alipoikuwa katika harakati za kutafuata pazuri pa kujificha kamera ndogo sana ya usalama ilimuona na kupeleka taarifa panapohusika ndipo shughuli ilipoibuka humo ndani, kipigo alichokipata kwa mkono wa Iron Man The Killing Machine alibaki hoi hajiwezi na kutupwa huko shimoni ambako hakuna hewa hakuna chochote ni mateso mpaka unakufa.
Fr Frank alishindwa kujitetea kwa jitu hilo la miraba mine baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi. Alikuwa nusu mfu katika chumba kile.
Kamanda Amata alijilegeza huku akiburuzwa mpaka katika lango la chumba hicho ambamo kinachofanyika ni kukutumbukiza, utakaa umo ufe kisha inamwagwa dawa maalum ambayo inakusagasaga na kuwa katika vipande vidogovidogo kisha wanaflash kama chooni na taka hizo zote hupelekwa baharini kupitia mfumo wa maji taka. Walipofika mlangoni, tayari kumtupa mle shimoni, Kamanda Amata alijitikisa kidogo, wale jamaa wakashtuka, mmoja akainama kumwangalia kama ni mzima au la, Amata akamtemea mate, kwa uzembe wa Yule mlinzi akauchia mkono wa Kamanda ili ajifute mate usoni, kosa. Konde moja zito lilitua tumboni kwa jamaa Yule akatema damu, huyu mwingine hajakaa sawa akachezea kipepsi kimoja kilichjomfanya ajisjike tumbo, sasa Kamanda Amata alikuwa huru na nguvu zake zilezile, alijurusha kiufundi na kuwapiga mateke ya migongoni kisha wale wawili wakaingia shimoni.
Kamanda akasonya na kurudi kwa njia ileile. Akapenya hapa na pale na kutokea eneo lenye veranda kubwa, akawa kizungukazunguka ajui nini cha kufanya, akiwa katika hali hiyo alihisi mkono wenye nguvu umekamata bega alipogeuka akakutana uso na jitu la miraba minne, mara akasikia vicheko kutoka sehemu asiyoijua. Lile jitu likamnyanyua na kumbwaga chini, Amata alijitonesha tena katika majeraha yake, akabaki kugugumia maumivu tu. Aliinua kichwa na kumwangalia huyo aliyemfanyia kitendo hicho, lilikuwa ni jitu lenye pande la mwili, lililojaa misuli mikubwa, kamanda Amata akaona wazi kuwa Frank Edson hakuwa na budi kuwa katika hali ile kama alipambana na dubwana hili, akajikokota kunyanyuka ajaribu bahati yake, konde la pili lilimrusha nyuma na kujibamiza vibaya ukutani, Kamanda Amata akatema damu, alipokuwa akijaribu kuinuka akapigwa teke la mbavu, nguvu ya teke lile ilimsukuma mpaka ukuta wa pili, Kamanda alijikuta akiwa na hali mbaya, alijitahidi kuinuka lakini ilikuwa ngumu, alibaki kutambaa.
Mara sauti ikasikika kwenye chombo maalumu kilichofungwa darini, ilianza na kicheko; “Ha ha ha ha ha ha, Kamanda Amata, wewe unajua sana kufuatilia nyendo za watu sio za miungu kama sisi, sasa leo pambana huyo Israel mtoia roho, kama wewe unaweza kukishinda kifo basi leo tutaona ujanja wako uko wapi, ha ha ha ha ha ha hapo ulipo ndio kuzimu ulipokuwa ukikusikia kwenye vitabu vya dini zenu, pambana na mashine ya kifo hiyo, ukiishinda nitakupa utajiri wangu wote,” Maneno yale yaliyokuwa yakisemwa na mtu asiyemuona yalimtia hasira sana Amata, “Utajiri wako baki nao mwenyewe, kwa kuwa sikutaka kukutoa roho sasa umeniladhimisha kufanya hivyo,” ilikuwa sauti ya uchovu kutoka kwa Kamanda Amata. Vicheko vikaanza tena kwenye kile chombo, sasa vikiwa kwa fujo zaidi, Kamanda Amata alihisi kitu kama upepo kimepita sikioni mwake pindi alipokuwa akigeuka, kumbe guu la lile jitu lilipita akiwa na lengo la kumpiga teke la kichwani pale chini alipojiinamia, Kamanda Amata kwa kasi akaona amepata nafasi nzuri ya kufanya mambo, alipiga ngumi moja iliyotua kwenye korodani za jitu hilo, likaguna kwa maumivu.
Akajiinua kwa ustadi na kujisahaulisha maumivu yake, akawa wima, alikusanya nguvu zake zote na kuruka hewani alikoichanua miguu yake na mateke yote mawili yakatua shavuni mwa lile jitu, lakini halikutikisika hata kidogo. Kabla mguu wa Amata haujatua chini, ulidakwa, Kamanda akautumia kama nguzo na kujivuta kuelekea usoni mwa lile jitu, akalipiga kichwa cha jichoni kwa maana alijua kwa vyovyote atalipoteza maboya, kama aliota. Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye nguzo ya chuma, akaiwahi na kuichukua akaivunja taa yake nayo ikabaki bila taa, akaiinua na kumpiga nayo mgongoni, lilipoguka kamanda Amata akatumia ule mnara wa taa akamchoma tumboni, lakini hakufanikiwa hata kumtoboa kutokana na ulaini wa chuma kile lakini alimpiga shoti moja mbaya ya umeme kutokana na kwamba alikuwa hajaichomoa kwenye soketi pale ukutani, Amata akatabasamu kwa hilo.
Lile jitu, lilipigwa shoti iliyolisukuma na likajibwaga zimazima pale chini. Vicheko katika kile chombo vikasimama ghafla. Kamanda Amata aligundua kuwa jinsi ya kulishinda lile jitu sio nguvu bali akili, alipi mguu chini na mara kitu chenye ncha kali kikachomoka kwenye sehemu ya mbele ya solo ya kiatu chake, na mguu mwingine vivyo hivyo, Kamanda Amata sasa akaanza kutumia miguu kuilishmbulia lile jitu, mateke ya usoni, mbavuni yalilifanya jitu lile lipoteze nguvu maana kila alipopigwa kwa teke aliachiwa jeraha kubwa kutokana na vile vyuma kenye viatu vya Amata. Zilikuwa dakika tatu za shughuli kubwa ya kulikalisha chini lile dubwana. Kamanda akasimama tayari kwa pambano akiliangalia lile jitu likigalagala sakafuni huku damu zikitapaka kila mahali.
Upande wa pili, Bill na Andreas walikuwa kimya wakitazama pambano hilo kupitia luninga ndogo ndani ya chumba nyeti cha Andreas, hawakuamini kile wanachokiona, kile kinachofanywa na Kamanda Amata, jinsi anavyotumia akili kuliadhibu jabali lile, mashine ya kifo kama wanavyoiita.
Tangu Andreas amnunue binadamu huyo wa ajabu huko Honduras na kumsafirisha kwa siri mpaka Ujerumani na kumuhifadhi katika nyumba yake, alishamtumia kwa kuua watu wengi sana wakiwezmo maafisa wa polisi, wanajeshi na wote wanaofuatilia nyendo zake kwa ukaribu, hakuna aliyewahi kufurukuta, wengi walikata roho kwa pigo moja tu, kisha miili yao aliitupi ‘kuzinu’ katika chumba alichokiandaa kwa kazi hiyo,. Akishakutupa humo hufungulia hewa yenye chemical kali amabayo hukukausha na kukumeng’enya kuanzia nyama yako mpaka mifupa vyote vinakuwa unga, kisha maji mengi huingia katika chumba hicho na kuondoka na mmeng’enyo huo kupitia mabomba yha maji taka, watu wako watakutafuta miaka nenda rudi na hawatakuona, umefutwa katika orodha ya binadamu duniani.
Leo ilikuwa tofauti, alimshuhudia Kamanda Amata akitoa dozi mbaya kwa jitu lake hilo analolitegemea kwa kazi hiyo. Kijasho kilipita kutoka kwapani na kufika mpaka kwenye kiuno kabla hakijaishia katika nguo alizovaa.
Kamanda Amata alipohakikisha dude hilo limezimika alitzama huku na kule ili kuona cha kufanya, sasa akili yake ilirudi kwa Bill na mwenzake Andreas, akiwa katika kutazamatazama mara akasiki kama nyayo za binadamu zikimfuata kwa nyuma, akatazama kwenye kioo kikubwa kilicho mbele yake na kuliona lile dude limesimama likielekea kwake kwa nguvu zote, Kamanda Amata hakuwa na silaha yoyote ya maana, akajua sasa kuwa amekwisha, kabla hajaona la kufanya, lile jitu likamfikia, likiwa na hasira mbaya, lilimpiga kikumbo Amata akapitiliza mpaka kwenye kioo cha mbele yake, alijibamiza na kile kioo kikamwagika pakabaki wazi, Kamanda Amata akadondokea upande wa ndani wa kile chumba kilichotenganishwa na kile kioo. Ilikuwa ni ofisi ndogoi lakini iliyojaa kila aina ya nakshi na samani za gharama, Kamanda Amata akanyanyuka na kuchukua chungu kilichokuwa na ua ndani yake na kukirusha sawia kichwani mwa jitu lile, likapepesuka kidogo, kabala halijatuliya, Amata akajirusha doule kick na kutu kifuani mwa lile jitu, kutyokana na kupoteza nguvu liliyumba na kujibamiza ukutani, ule mtikisiko wa ukuta ulifanya pambo la juu ambalo lilikuwa ni bichwa la Nyati lililotengenezwa kwa chuma.
Lilianguka na kumpiga kichwani, kisha lile bichwa la nyati liakadondoka sakafuni. Lile jitu likajitahidi kusimama lakini ilikuwa ngumu kutokana na kugongwa vibaya na lile bichwa la nyati bandia, ilikuwa ni nafasi ya Amata ya kumaliza mopja kwa moja akaanguka juu ya lile sanamu la kichwa cha Nyati, akachomwa na pembe za nyati zilizojinyomnga vizuri zikitanguliwa na ncha kali, likatoa kelele za uchungu huku macho yakiwa yamemtoka pima, likakata roho. Kamanda Amata akakung’uta mikono yake kwa kuashiria kazi imeisha, hakuamini kiama kalimaliza hayawani hilo.
Bill aliinuka na bastola mkononi, akiuelekea mlango ili atoke nje, mkono mmoja akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea.
“Bill, hapa pameshakuwa pabaya, mi nafunga vyangu najificha dhidi ya huyo mtu wako,” Andreas alimwambia Bill, wote wawili walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, wakivujwa na jasho jingi. Andreas alichukua begi tupu, akainyanyua ile monstrance na kuiti begini kisha ile ramani, akaenda ukutani na kushusha picha moja, nyuma yake nkulikuwa na vibonyezo au vitufe kumi na mbili vikiwa na nmba pamoja na alama chache, akaanza kuvibonyeza ili mlango wa siri ulio kwenye sakafu ya chumba hicho ufunguke, nukawa unagoma kufunguka, alipojaribu mara ya pili nay a tatu mlango ule ukakubali, taratibu ukawa unapanda juu ili kuwezesha mtu kuingia.
Bill aliona taanyekundu ikiwaka juu ya dari la chumba hicho, ikiashiri kuna hatari, mara alishuhudia ule mlango mnene wenye ulinzi mkali ambao huwezi kuingi bila kuthibitisha vitu vitatu, namba ya siri, alama za vidole na alama za macho, na hivyo vyote vilikuwa ni Andreas peke yake aliyeunganishwa. Mlango ule ulionekana kwa ndani ukikatwa duara kutoka nje, Bill akajua sasa hapa Kamanada anaingia, akaiweka sawa bastola yake, hakuwa tayari kufa wakati anayemlinda anatoroka, akainyosha bastola kwa Andreas, Andreas akasikia mlio wa bastola hiyo ikiwekwa sawa kulipua, “Bill vipi tena?” Andreas akamuuliza Bill. Sikia bwege wewe, yaani huna shukrani, kazi yote niliyokufanyia, sasa hivi unaona mambo yameharibika unakusanya vyako unataka kutoroka na kuniacha mimi hata kunipa chochote sio, sitaki maelezo, nakumaliza mwenyewe,” Bill alimwambia Andreas kwa ukali.
“Sikia Bill, mi naokoa hii mali ya thamani, wewe ukishamuua huyo Kamanda Amata tuonane nitakupa donge nono,” Andreas alijitetea. “Siki, mi si motto, Kamanda Amata keshakufa mara mbili na kafufuka sasa unafikiri hapa atakufa tena?” Bill alimuuliza Andreas, Mara lile pande la chuma linalokatwa kwa saa ya Kamanda Amata, lilikuwa tayari kutoka mahala pake na kuruhusu mtu wa nje kuingia ndani, Bill alipiga risasi moja na kufumua kifua cha Andreas, Andreas akaanguka chini na kutoa yowe la maumivu, Bill akanyanyua tena mkono wake ulioshika ile bastola na kulenga lile tundu ili ampate Kamanda Amata, alipofyataua, viligongana vyuma tupu, hakuna risasi, akaitupa chini bastola na kunyanyua lile begi alilochukua Andreas na kuingia kwenye ule mlango na kuzama ardhini huku mlango ule ukijifunga nyuma yake.
§§§§§
Kama alitegemea kupona basi ilikuwa kwa asilimia ndogo sana, Frank Edson, aliona kile alichofanya Kamanda Amata pale mlangoni alipokuwa ameletwa na wale watu ili kutupwa ndani ya shimo hilo kusubiri kifo chake. Aliona kitu kidogo ambacho Kamanda Amata alikiangusha kwa makusudi wakati alipowaadhibu vikali wale jamaa wawili na kuwatumbukiza mle shimoni.
Ilikuwa ni kitu kama kidonge kidogo, kwa tabu sana Fr Frank Edson alijivuta kwa kutambaa mpaka akakipata kile kidonge alipokitazama alikijua vyema, kidonge kinachotumika kurudisha nguvu kwa haraka kwa mtu aliyekuwa na uchovu mwingi wa kupigwa au wa shuruba yoyote, pia kinaondoa maumivu kwa muda mrefu. Fr Frank Edson alimuona Amata kama Malaika wake, alikiokota na kukitia mdomoni, akakimung’unya, muda kumi na tano tu alipata nguvu taratibu mpaka akawa sawa na maumivu yake yakapotea, akajinyanyua kutoka pale alipo, akasimama wima, akatazama wale jamaa waliolala pale, waliotupwa na kwa kipigo kikali na Kamanda Amata. Akawapekua katika nguo zao na kupata bastola moja iliyobakiwa na risasi mbili tu, ‘Sio mbaya’ akajisemea.
Sasa kazi ilikuwa atatokaje kwenye chumba kile kisicho hata na dirisha, aliuangalia mlango ulikuwa juu umbali wa mita kumi na ukuta wote ulikuwa umewekwa kitu kama niru ambayo kamwe huwezi kuzikwea kwa jinsi zinavyoteleza, ulikuwa mtihani mgumu kwake, akakizunguka kile chumba akigusa hapa na pale, baada ya kuchunguza sana ndipo alipogundua ile sehemu ya kuingizi maji ndfani ya chumba kile, haikuwa na bomba bali ni uwazi mwembamba wa futi mbili kwa upana na uwazi wake ulikuwa ni kama milimita tano, palitengenezwa hivyo ili maji yakitoka yatoke kwa mbinyo na kasi kubwa kutokana na msukumo wa pampu. Akapaangalia na kuona kama anaweza kupita katika upenyo huo, lilikuwa ni wazo finyu sana hata kama angekuwa motto mdogo, sehemu ambayo asingeweza kupenya hata mjusi, lakini yeye alidhamiria kupenya hapo, akiwa kama aliyechanganyikiwa ndipo akagundua kuwa haiwezekani kufanya hilo analotaka kufanya, akajicheke mwenyewe hasa alipojua kuwa yale maji kuna yanapokwenda, akaenda kwenye moja ya kona za chumba hicho, alipotazama kwa makini sana akaona kuna kitu kama kimebandikwa katika ukuta huo, lakini kilikuwa kimefanana sana na ule ukuta, akajua kwa vyovyote hapo pana kitu, akaanza kugongagonga ukuta kwa ile bastola aliofika eneo hilo akasiki ule mlio unabadilika na kuwa mkubwa kiasi akagundua kuwa nyuma yake lazima kuna uwazi, hakuwa na budi, kwa kutumia bastola hiyo hiyo alifyatua risasi moja na ikatengeneza tundu zuri ambalo lilimuwezesha kuona mpaka upande wa pili.
Kweli kulikuwa na uwazi mkubwa, Frank alisikia sauti ya maji yanayotembea, lakini alipochungulia kwa jicho lake aliona mwanga hafifu sana, akaanza kubomoa lile eneo kwa kupiga na ile bastola kama nyundo mpaka akafanikiwa kutengeneza tundu la kutosha, akajipenyeza na kudondokea kwa ndani. Lilikuwa ni bomba kubwa la maji taka, aliweza kutembea kwa kuinama kidogo huku akipita kwenye maji hayo na asijue ni wapi anaelekea, harufu iliyokuwa humo haikuwa tatizo kwake, alitembea mwendo mrefu kidogo, kwa mbele akaona kuna pacha ya bomba hilo ikiungana na bomba linguine ambalo nalo lilikuwa likileta maji kuunga na hili nkisha kuelekea yanakokwenda, Frank alipoifikia ile pacha akasikia kelele ya mtu anayekimbia katika maji, akatul.ia kusibri aone mtu huyo ni nani.
§§§§§
KAMANDA Amata alipoona kuwa lile lango la kwenda chini alikoingia Bill limejifunga, akachoka ghafla, akatazama huku na kule, alichokiona akajua tu ni switchi ya mlango huo, akaelekea pale ukutani hakuwa na akaminya namba ya siri ambayo kuna jinsi unavyoipanga inaweza kufungua kila aina ya mlango, akaingiza tarakimu hizo kumi na mbili na alama Fulani kwa mpangilio maalumu, akabonyeza ok, akadaiwa kuweka alama ya kidole gumba, akajua tu lazima ni kidole cha Andreas kinachohatajika, alimtazama akiwa pale chini amelala hana uhai.
“Ndiyo shida ya dhukuma, ukidhulumu utadhulumiwa” akaongea mwenyewe huku akiuendea ule mwili, akachukua kipande cha kioo kizito kilichovunjika hapo, akakata kidole gumba cha Andreas na kwenda kukipachika pale kwenye ile sense, taa ya kijani ikawaka, ule mlango ukafunguka, haraka akauendea, alipotazama mezani akagundua kuwa Bill ameisahau ile fimbo yake Amata akaitazama na kuichukua, alipoigeuza geuza akagundua kuwa haikuwa fimbo ya kawaida, akaingia nnayo na ule mlango ukajifunga, alimweza kumuona Bill kwa mbali akiendelea kwenda, “Billlllllll…..” aliita, lakini Bill hakusimama. Baada ya kumfuata kama dakika moja na nusu hivi, akamuona Bill akisimama na kugeuka alikotoka, akiwa na begi lake mkononi. Bill hakuwa na ujanja, alikuwa katikati, huku Frank Edson FBI huku Kamanda Amata TSA.
“Bill, huna ujanja, mwisho wako umefika,” ilikuwa sauti ya Fr Frank. Amata aliiskia akajua kuwa ni Frank anaye ongea lakini bado alikuwa hajamuona kutokezea. Bill alibaki pale katikati akihema. Mara Frank akatokezea na kugongana macho na Kamanda Amata. “Kamanda Amata, niachie Bill niondoke naye, asante sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kunirahisishia kumpata Bill Van Getgand, asante sana, huyu inabidi afike hai pale Washington,” Fr Frank alimwambia Kamanda Amata.
“Sikia Frank, unajua kuwa ulikwishakufa wewe? Kwa nini husemi asante kwa kukurudishia uhai wako? Sasa sikiliza Bill utamchukua akiwa hai wala usijali cha muhimu ni kutafuta njia nya kutoka humu ndani, na njia hiyo lazima yeye Bill atuoneshe,” Kamanda Amata akamwambia Frank, Frank akamsogelea Bill na kumnyang’anya lile begi, Bill hakuwa na ubishi, Frank akamrushia begi Amata, nae akalidaka. “Haya, njia ya kutoka humu ndani iko wapi?” akamuuliza Bill, alipoona ukimya wake unazidi, akaamua kutumia nguvu, alimshika Bill kwenye ukosei wa shati na kumbamiza kwenye kingo za bomba hilo mara kadhaa, Bill alikuwa akitokwa na damu nyingi katika paji lake la uso.
“Frank! Mbona huna huruma wakati wewe ni mchungaji wa kanisa?” Kamanda aliuliza, “Kwa taarifa yako, ukimfanya hivyo hatofika hai Washington, nifuate njia ipo huku,” akaongeza, kisha akatangulia na Frank akamfuata na Bill akiwa katikati mikono akiwa ameshika kichwani. Walikwenda mpaka kwenye ule mlango, akaufungua na wakatoka wote, wakaingia kwenye chumba kile cha siri, kisha wakaelekea katika lile sebule kubwa, Frank alishangaa kulikuta lile jitu lililomtia adabu likiwa marehemu, Frank moyoni mwake alikiri kuwa Kamanda ni kiboko kama amelizimisha jitu hatari kama lile. Jumba la Andreas lilikuwa kimya ni polisi tu waliokuja kutoka mjini walikuwa huku na kule wakifanya upekuzi wa hapa na pale.
“Weka mikono juu!” ilikuwa sauti ya polisi mmoja wa kike akimuamuru kamanda Amata. Amata akanyanyua mikono juu ile fimbo aliyoichukua pale mezani ikaanguka chini, na Yule poilisi akamuamuru mwenza aichukue. Mara Bill akatokea na nyuma akiwamo Fr Frank Edson.
“Frank Edson FBI,” akaonesha na kitambulisho, wale polisi wakaja kumchukua Bill na kumtia pingu. “Na huyu?” waliuliza juu ya Kamanda Amata, “Muacheni aende zake, ni mwenzetu kutoka shirika la upelelezi Tanzania,” Yule askari akamwita na kumuongoza kuelekea kwenye gari ya polisi. Nje ya jumba la Andreas kulitanda gari za polisi zikiwaka vimulimuli vilivyong’aza eneo lote hilo, Kamanda Amata akatazama saa yake, ilikuwa ni saa kumi na mbili alfajiri. Polisi walikuwa wakikusanya miili na kufanya upekuzi wa hali ya juu katika jumba hilo ambalo siku na miaka yote waliliona ni jumba la mtu mwema.
Mlio wa Helkopta ulisikika ukikaribia eneo hilo, Frank akamtazama Amata, “Kamanda, Bill anaondoka moja kwa moja USA, uje muagane tafadhali,” Fran alimwambia Amata kwa nyodo. Kamanda Amata akavuta hatua na kufika pale aliposimama Bill huku nyuma yake akiwa ameshikwa na polisi wawili wa kijerumani na Frank alikuwa alikuwa nyuma yao.
Bill na Amata wakawa uso kwa uso, “Bill nilikwambia siku yetu inakuja, na ndiyo leo, nitautwaa uhai wako kwan kisasi cha Fr Gichuru, Kahaba Rose na wengine wote uliowapotezea maisha yao pa sin a hatia. Nakuapia, hautakanyaga gereza la Guantanamo wala wapi sijui,” kamanda Amata aliongea kwa sauti ya chini ni Bill aliyekuwa akisikia na wale polisi wawili, Frank alikuwa akiongea na redio aliyopewa na mmoja makamanda waliokuja na kikosi hicho.
Bill alimtazama Kamanda Amata, akamtemea mate usoni, Kamanda Amata akamkazia macho Bill, “Sintoyafuta mate haya mpaka nihakikishe umekufa na haupo katika dunia hii, kifo chako ulikinunua mwenyewe kwa gharama kubwa sana,” Bill aliposikia maneno hayo aliikumbuka ile fimbo yake na akaitazama ikiwa nikononi mwa Amata, kisha Kamanda akageuka na kuondoka kueleka upande ambao gari za polisi zilegeshwa, waandishi wa habari kama kawaida yao, walichukua picha huku na huku na kutafuta majibu ya maswali yao. Dakika chache helkopta kubwa likakanyaga ardhi yenye nyasi safi na kutulia tuli, wanajeshi wane waliovalia sare ya jeshi yenye nembo ya bendera ya Marekani walishuka na kumchukua Bill tayari kuondoka nae, itifaki za kuondoka na mtuhumiwa huyo zilifanywa haraka sana na pande mbili za mataifa hayo rafiki. Kamanda Amata alikuwa kasimama upande wa pili wa gari moja ya bpolisi akiwa kaegemeza tumbo lake kwenye ubavu wa gari hiyo, begi lake kalitupia ndani ya gari na ile fimbo ya Bill kaiweka juu ya gari, akiangalia kila kinachoendelea.
Aliishika ile fimbo na kuwa kama mtu anayeichunguza pale juu ya gari, bahati ilioje alipogundua kuwa ile haikuwa fimbo bali ni silaha mbaya sana yenye risasi za mtindo wa msumari, silaha ya Kirusi iliyotumiwa sana na wanazi wa KGB ambamo Bill alikuwa mmoja wao nyakati hizo, aliitazama haraka na kuikuta bado nina risasi tatu, akaiweka vizuri juu ya gari na kulenga shabaha, hakuna aliyemwangalia wala kugundua hila yake. Mguu wa Bill ulikuwa ukikanyaga ngazi ya helkopta hiyo huku akisukumiwa ndani na wale wanajeshi, Fr Frank alikuwa akifuata nyuma, lo, mara walishuhudia Bill akijishika kifua, mara kichwa, akalegea na kuanguka chini, tafrani ikazuka, walipomwangalia tayari alikuwa marehemu, lakini hakuonekana tundu lolote la risasi.
Kamanda Amata aliingia kwenye gari mara tu baada ya kumaliza azma yake, alikuwa akisubiri Bill akanyage japo ngazi ya helkopta hiyo, naye palepale akafyatua bunduki hiyo ya siri, bunduki ya kijasusi, akamtoa uhai Bill Van Getgand.
Fr Frank Edson akawaacha wale wanajeshi wakimhudumia Bill ambaye alikuwa tayari marehemu, akamjia Kamanda pale aliposimama, na kamanda akatoka pale alipo kumuendea Frank, akampa mkono, lakini Frank hakuupokea mkono huo.
“Kamanda Amata, umefanya nini sasa?” Frank aliuliza.
“tatizo nini, wewe ulimtaka akiwa hai sivyo, si umemshika akiwa hai, na mimi nilishakwambia serikali ya Dodoma inataka roho yake tu basi. Asante sana Frank, umeifanya kazi yangu kuimaliza kwa wepesi kuliko nilivyofikiria,” kisha Kamanda Amata akageuka na kuingia kwenye gari iliyokuwa imekwishawashwa tayari, Frank alibaki kumtazama hakuwa na la kufanya, aliitazama ile gari ikitoka getini na kutokomea mjini huku na zingine zikiendelea kutoka moja baada ya nyingine.
DAR ES SALAAM
Saa 09:30 usiku
SIMU YA kitandani mwa Madam S iliunguruma kwa fujo usiku huo, alishtuka na kukunja sura kama kawaida yake kwani alikuwa hapendi sana kukatishwa usingizi. Aliinyakua simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Madam S!” ilikuwa suti ya Chiba.
“Ee Chiba, niambie, mbona usiku sana,” Madam S aliuliza.
“Fungua, televisheni yako, Deustche Welle,” akamwambia na ile simu ikakatika. Madam S akaiwahi rimoti haraka na kuwasha luninga yake kubwa iliyofungwa ukutani katika chumba chake cha kulala. Habari ya dharula aliyoikuta kwenye kioo hicho ilimfurahisha kuliko habari zote alizowahi kuzisikia. Ilikuwa ni habari ya moja kwa moja iliyobebwa na maadishi ‘Breaking News’ ilikuwa ikieleza juu ya kukamatwa kwa jasusi lililoisumbua dunia, lakini hata hivyo ikasemekana limejiua kabla halijapakiwa katika helkopta tayari kupelekwa Marekani. Habari hiyo ilikuwa ikisifia shirika la nkipelelezi la Marekani kwa kufanikiwa kulinasa jasusi hilo. Akiwa katika kutazama habari hiyo, fax yake ya mezani karibu na kitanda ikaanza kutoa mlio kama wa mdudu, kijikaratsi chepesi kilikuwa kikitoka na maadishi. Akaiendea na kuisoma fax hiyo.
“…kazi uliyonituma nimeimaliza, Bill Van Getgand amekshaisalimisha roho yake… TSA 1” Madam S alijua kuwa ujumbe huo umetoka kwa Kamanda Amata, akatabasamu, akazima luninga yake na kurudi kitandani.
HATIMA
KAMANDA Amata alikuwa kwenye kititanda cha wagonjwa katika kliniki binafsi ndani ya mji huo wa Aachen, akigangwa majeraha na maumivu mengine. Huku akijisomea magazeti nya siku hiyo akipata habari za tukio lililotukia usiku wa siku hiyo na kusoma habari nyingi za kweli na za uongo.
“Kamanda, Sindano!” alishtuliwa na sauti laini ya kike, kamanda Amata akamwangalia Yule muuguzi wa kizungu aliyekuwa na chano yake yenye kila kitu kwa ajili ya tiba hiyo. Kiukweli pamoja na ujasiri wote, kamanda Amata kwenye swala la sindano alisalimu amri, aliogopa sana kitu hicho tangu utoto. Alitamani kulia alivumilia mpaka shughuli hiyo ilipokamilika.
“Asante dada mzuri, hata sikujua kama umenichoma sindano,”Amata alimchokoza muuguzi. “Kwa nini?” Yule muuguzi akauliza. “Kwa jinsi ulivyo na mikono laini, na upendo unaomfanya mgonjwa asihisi hata kama anapasuliwa nini kuchomwa sindano!” Amata aliongea kwa lugha ya uchokozi, “Hallo,” Kamanda aliita tena wakati Yule muuguzi alipokuwa akitoka mle chumbani, “Nini? Unahitaji sindano nyingine?” akauliza huku akirudishia mlango na kurudi kwa Amata, Kamanda Amata akampa ishara ya kuwa asogee amwambie kitu, Yule muuguzi akasoge kumsikiliza, Kamanda akamshika kwa mikono yake kichwani pande za masikio, akamvutia kwake, hakukuwa na ubishi, akambusu na ndimi zao zikabadilishana mawazo.
Baada ya dakika kama mbili za mchezo huo ambao uliwafanya wote wasahau majukumu na magonjwa yao, akamtoa na kumtazama usoni. Yule mwanadada alikuwa akihema kwa nguvu, pepo limechukua nafasi, akajichomoa kutoka kwenye mikono ya Kamanda, akavua viatu na kumpandia kitandani, shughuli mpya ikaamka, Kamanda Amata alipogundua kuwa pazia la dirisha liko wazi, akshika kimnyororo kidogo cha kazi hiyo na kukivuta, pazia likarudi mahala pake na kuwaficha wawili hao kati ulimwengu wa peke yao.
ææææ MWISHO ææææ
Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;