Mikono ya Jasusi Sehemu ya Tatu
IMEANDIKWA NA: AHMED JIRIWA
*********************************************************************************
Simulizi: Mikono ya Jasusi
Sehemu ya Tatu (3)
“Kwa ajili yako hakuna shaka nitajitahidi kukupigia ifikapo saa saba mchana sijui tunakutana wapi?”
“Usijali ni hapahapa hotelini na tutakutana kwenye ukumbiwa wa chakula wa Hoteli hii.”
“Asante nitafika bila kukosa.” Alishukuru Maisara kisha akaongeza tabasamu na kumuangalia Alan akishuka tokea garini na kuzirusha hatua zake taratibu akipotelea kwenye mlango wa kutokea mapokezi. Jicho lake liliridhika mara baada ya Alan kupotelea ndani kabisa ya Hoteli ile. Alan alipofika mapekezi alipokelewa na wanadada wawili ambao walikuwa kwenye mavazi nadhifu ya sare za kazi za rangi nyeusi ya sketi zao fupi zilizopita kidogo magoti na mashati meupe ya kupendeza. Aliwasabahi akilipamba tabasamu lake la kichokozi kisha baada ya salamu aliomba huduma ambayo alipewa pasi na shaka yoyote hakutaka kupoteza muda hivyo aliondoka na binti mmoja kati ya wale wawili ambaye alikwenda kumuelekeza chumba chake kilipo. Ilikuwa ni ghorofa ya pili chumba namba 16. Baada ya yule msichana kuondoka aliitazama ile korido ya mahali chumba chake kilipo kisha akaenda hadi mwisho wa korido ile ambako alikutana na kona ambayo ilikuwa inaelekea mahali akaifuata hadi alipokutana na ngazi zilizokuwa zikishuka chini. Hakutaka kuzifuata hadi chini na badala yake alichungulia kupitia kioo kilichokua na uwezo wa kumuonesha mtu kwa upande wa nje. Akajua moja kwa moja ngazi hizo zilikuwa na uwezo wa kumtoa hadi upande wa nyuma wa Hoteli hiyo. Alitabasamu na kufurahishwa na muundo wa Hoteli hiyo, alirudi hadi kilipo chumba chake akafungua na kuingia ndani. Kilikuwa ni chumba kikubwa chenye kitanda kikubwa cha futi tano kwa sita, kulikuwa na kabati dogo la kuhifadhia nguo na zulia safi laini ambalo lilikipendezesha sana chumba hicho. Kulikuwa na meza ya kioo katikati ya kile chumba na meza moja ya kusomea ikiwa na viti viwili pembeni kidogo mwa dirisha ambapo juu yake kulikuwa na majarida mawili. Alan alikichunguza chumba kile kwa udadisi mkubwa hadi alipojiridhisha kuwa kilikuwa salama, alisogea hadi dirishani na kuchungulia nje ambako kulikuwa katika utulivu mkubwa. Alirudisha pazia la chumba kile na kurudi kitandani ambako alipanga vifaa vyake vya kazi katika mpangilio mzuri vile vya kuficha alivificha kiasi kwamba isingekuwa rahisi kuonekana na vile ambavyo havikuhitaji kufichwa aliviweka katika hali nzuri na kufungua begi lake jingine la nguo akatoa fulana moja nyeusi na suruali ya jeansi ya rangi nyeusi pia sambamba na raba za rangi hiyo zenye kuhimili kashikashi. Akaitoa suti yake mwilini na kuvaa mavazi yale ambayo yalimuweka katika muonekano mwingine kabisa na wa kikazi. Alikamata begi lake la kushika mkononi na kunyanyua saa yake. Ilikuwa tayari ni saa sita na dakika zake nyingi tu. Alihakikisha kuwa zana zake za kazi zipo imara na mahali ambapo panafikika kirahisi pasipo kusahau bastola yake anayoipenda aina ya Auto Mag uliyobuniwa huko U.S.A mwaka wa 1969. Ambayo aliifutika kuinoni ukiachia mbali zana nyingine ndogondogo huku bastola aliyopewa na mkuu wake wa kazi ikiwa kama ziada tu ya silaha zake nyingine. Huu ulikuwa ni usiku wa kazi na kazi hiyo inayomtoa ndicho hasa kilichopelekea yeye kutumwa na mkuu wake wa kazi ndani ya jiji hili la ‘Waja leo kuondoka majaaliwa.’ Akasogea tena pale dirishani na kuchungulia upande wa nje, bado utulivu ulikuwa ni mkubwa sana na anga lilikuwa jeusi lenye nyota chache kama vile linalotangaza kunyesha kwa mvua wakati wowote hali ile ikiendelea vile hivyo alilirudisha pazia na kutoka mule chumbani akiwa ana hakika kabisa hakuna mtu yeyote hadi muda huo ambaye aliweza kuutambua uwepo wake jijini hapo kutokana na kuingia muda ule kama yupo basi alikuwa ni Maisara dereva teksi aliyelitumia gari lake kumfikisha hotelini hapo na wahudumu wa Hoteli hiyo. Alishuka ngazi taratibu hadi akafika mapokezi ambako aliwakuta wale wahudumu wakiwa katika mazungumzo yao akawaaga na kuwaambia kuwa asingechelewa kurudi. Nje ya Hoteli Maua Inn alipokelewa na anga lililotanda kiza utulivu ukihanikiza baadhi ya maeneo ya chochoro mbalimbali hata hivyo hivi vilikuwa ni sehemu ya vitu anavyovipenda sana kwani kitu kinachoitwa giza kwake kilikuwa ni burudani hasa anapokuwa kwenye harakati zake za kijasusi. Kwa majira haya, alitakiwa kuwa kwenye Hoteli ya Mtendele au Mtendele Hotel Limited ambako ndipo kifo kilipomkuta Luteni Jenerali Leous Mipango.
FUNUA FUNUA IMEANZA.
Nje ya Hoteli Maua Inn alipokelewa na anga lililotanda kiza utulivu ukihanikiza baadhi ya maeneo ya chochoro mbalimbali hata hivyo hivi vilikuwa ni sehemu ya vitu anavyovipenda sana kwani kitu kinachoitwa giza kwake kilikuwa ni burudani hasa anapokuwa kwenye harakati zake za kijasusi. Kwa majira haya, alitakiwa kuwa kwenye Hoteli ya Mtendele au Mtendele Hotel Limited ambako ndipo kifo kilipomkuta Luteni Jenerali Leous Mipango.
SONGA NAYO….
Wakati akiwa anapiga hatua zake za taratibu alikuwa akiyafikiria maneno ya mkuu wake yaliyomtaka kwanza afike Hospitali ya mkoa Bombo ili kupata majibu ya kiuchunguzi kabla ya kufanya jambo lolote hata hivyo yeye mwenyewe amekuwa na aina yake ya uchunguzi ambao huupenda sana na ndiwo hupenda zaidi kuutumia. Aina hiyo ya ujasusi wa kupenda kulichimbua tatizo kwanza kabla ya yote, aliuona au alipa kuusoma kupitia vitabu na hitoria mbalimbali na ujasusi huo ulikuwa ukitumiwa na jasusi mmoja hatari sana duniani. Jasusi aliyekuwa akitambulika kwa jina la Richard Sorge.
Richard Sorge alikuwa akitambulika kama jasusi mfukuzi na mwerevu kuliko wote katika karne ya 20. Jasusi huyo raia wa ki-Rusi na mwalimu wa hujuma aliwahi kufanya kazi duniani kote kabla na wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia. Katika shughuli zote hizo alijifanya kama mwandishi wa habari za kimataifa akitembelea sehemu mbalimbali za ulaya na katika harakati zake hizo alikuwa hasahasa akiangalia uwezekano wa wakomunisti kuleta vurugu.
Wakati wa vita ya pili ya Dunia inaanza alienda nchini Japani akijifanya mwandishi wa habari kutokea nchini Ujerumani ndipo akaanza kupeleka Urusi habari kuhusu silaha na wanajeshi wa nchi ya Ujerumani na Japani. Pia akaonya kuhusu shambulio la Japani katika bandari ya Pearl (Marekani), mipango ya nchi ya Ujermani kutaka kuivamia Urusi na mengine mengi hata hivyo taarifa zote hizo zilikataliwa na Stalin ambaye ndiye aliyekuwa kiongozi wa nchi ya Urusi enzi hizo. Hata hivyo Sorge alikamatwa na wajapani mwaka 1944, ingawa hakuwahi kukiri kama alikuwa jasusi kutokea nchini Urusi na akanyongwa muda mfupi baadae.
Alan alivutiwa na utendaji wa jasusi huyu ambaye aliwahi kuwa tishio ingawa alisoma historia nyingi za majasusi tishio duniani kama mwanadada Margaretha Geertruida Zelle au kwa majina yake ya kificho akijulikana kama Mata Hari au 2-H 21. Jasusi wa Ujerumani aliyejifanya mcheza dansi maarufu na muuza mwili mkubwa jijini Paris; Ufaransa kumbe alikuwa ni mtoa taarifa mzuri wa Ujerumani. Pia alipata kuzisoma habari za Julius na Ethel ambao walikuwa ni majasusi wa Marekani wanaotoa siri za silaha za nyuklia za Urusi ambao waliishi kama wanandoa, Aldrich Ames ambaye alikuja kuwa jasusi wa Urusi baada ya kuisaliti Marekani ambayo ndiyo iliyompa mafunzo ya kijasusi toka kwenye shirika la kijasusi la CIA. Pia kuna Giacomo Casanova ambaye alikuwa jasusi wa Venetia, Klaus Fluch ambaye alikuja kuwa jasusi wa Urusi pia, Shi Pei Pu; jasusi wa China, Sidney Reilly ambaye alifahamika kama Ace of Spies; jasusi wa Marekani, Kim Philby; jasusi wa Uingereza, Frederick Joubert Duquesne p.a.k Black Panther; jasusi wa Ujerumani, Virginia Hall p.a.k Artemis; jasusi wa Marekani na jasusi pekee mwenye asili ya ki-Afrika nchini Marekani aliyefahamika kwa jina la James Armistead Lafayette. Habari za majasusi aliwahi kuzifukunyua kupitia mitandao mbalimbali ya kijasusi zilikuwa zikimsisimua sana mwili wake na kuzidi kuipenda kazi yake ha kijasusi ingawa alikuwa akifahamu namna anavyocheza na hatari ya wazi kabisa hata hivyo bado alikuwa na mapenzi makubwa sana na kazi hiyo kiasi kwamba alikuwa radhi kufanya lolote lile kwa ajili ya taifa lake.
Kwa majira hayo ya saa sita na dakika arobaini na kitu kimya kilikuwa kimetawala sehemu kubwa ya barabara aliyokuwa akipita akielekea Chuda. Hakukuwa na usafiri wowote kwa majira hayo hivyo alitumia mwendo wa miguu huku akiwa makini kutazama kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akizifuatilia nyendo zake. Hadi hapo utulivu ulikuwa ni mkubwa. Alilipita soko la Tangamano na kituo cha Televisheni cha Tanga Tv upande wake wa kuli na Hospitali ya Ngamiani kwa upande wake wa kushoto akiwa katika mwendo wa kasi kido, akiwa anakaribia kuipita Hospitali ya Ngamiani, akaona kivuli cha mtu kikiwa kimepiga hatua kama kilichokuwa kikitaka kuingia barabarani kisha kikarudi nyuma kwa hatua moja kubwa na kutoonekana tena. Damu zikamtembea Alan na nywele kumsimama hali ya hatari ikijichora akilini mwake. Alijaribu kusimama kuona kama kivuli kile kingeweza kujitokeza tena hata hivyo hakikujitokeza na kumfanya Alan azidi kupata wasiwasi huku jasho jembamba likianza kuvitekenya vinyweleo vyake ngozini. Hakuwa na namna nyingine zaidi ya kusonga mbele kwani hatari ilikuwa ni moja ya majukumu yake. Alitembea kwa tahadhari kubwa huku akijishika kiunoni mahali ilipo silaha yake ili kuwa tayari kufanya lolote endapo kungeweza kutokea jambo la kuhatarisha uhai wake. Alizidi kuzirusha hatua zake hadi alipoanza kusikia sauti ya mkoromo. Hapa akapata hofu zaidi na ule utayari wa kuikamata bastola yake vema ukamuingia mwilini mwake akazidi kusonga huku akijitahadharisha. Alipokuwa akiikaribia ile kona ya njia iliyokuwa ikielekea shule ya msingi Chuma na Masiwani akaona kifurushi kilichojidhihirisha kuwa alikuwa ni mtu kikiwa kinajikurupusha pale chini pasipo mafanikio yoyote huku kikitoa mikoromo mingi. Wazo la kuwa ni kiumbe kimeviringitwa na nyoka mkubwa pale chini likamjia hata hivyo akalipuuza na kuona isingekuwa rahisi kwa eneo la katikati ya mji kama vile halafu eti kuwe na nyoka mkubwa kiasi kile, wazo la kuwa ni mtu alikuwa amekabwa na kibaka labda liliweza kuzirahisi hisia zake ziamini. Akajisogeza zaidi huku mkono wake ukiwa kiunoni na mara akatukana tusi zito la nguoni kukiendea kile kifurushi mtu mara baada ya kugundua alikuwa ni mlevi aliyezidiwa na pombe za kienyeji mara baada ya kifurushi mtu kile kuanza kuimba nyimbo za kilevi kwa taabu kubwa huku kikijizoazoa bila mafanikio. Ndiyo maana mnaliwa na wanaume wenzenu kwa ulevi usio na maana. Unalewaje kwa kiasi hicho mwanaume mzima…subiri mateja waje wakuzoe wakakutafune pumbavu wewe. Alizungumza na mawazo yake Alan huku akijiweka sawa na kuzidi kuyoyoma na barababara ile. Alikuja kulipita karakana la mabasi ya Rahaleo Chuda kisha baa ya Kilimanjaro na punde akawa anatazamana na Mtendele Hotel Limited. Hapa alipunguza mwendo na kutazama mandhari ya eneo hilo la Hoteli alipojihakikishia usalama alizivuta hatua zake hadi ndani ya Hoteli ile ambapo aliingia hadi kwenye ukumbi wa vinywaji na chakula wa hotelini hapo kisha pasipo kupoteza wakati aliingia kwa upande wa ndani ambako alikuta kukiwa hakuna mtu maeneo hayo zaidi ya sauti ya runinga iliyokuwa ikisikika kwa taratibu. Aliyasoma mandhari ya hapo kwa haraka na kuona makochi mazuri ya kisasa yakiwa yamepangiliwa kwa upande wa mbele mara tu ukiingia mapokezi hapo pia kulikuwa na kochi jingine moja la kisasa kwa upande wa kushoto huku kwa upande wa kulia kwake kukiwa na ngazi ambazo zilikuwa zikielekea ghorofa za juu. Akiwa hapo akisubiri, alitokea msichana mmoja mwembamba mweusi akiwa katika sare za kazi. Alimsabahi kisha kumtaka utulivu kidogo akaondoka na punde alitokea msichana mwingine mwenye umbo la saizi akiwa mweupe na aliyezitengeza nywele zake katika muonekanao wa kuvutia.
“Karibu kaka na samahani sana kwa kukuweka…?” Alisabahi yule dada akiwa katika tabasamu la kibiashara huku akijiweka nyuma ya meza yake ya kufanyia kazi.
“Asante na usijali, huduma tafadhali…?” Akasabahi Alan akiwa katika tabasamu pia la kukirimu tabasamu alilopewa na mrembo yule.
“Ipo karibu?”
“Ok, asante ningependa kupata chumba namba 24…!” Akasema hitaji lake Alan huku akimtazama mwanadada huyo kwa umakini kuona kama kungekuwa na aina yoyote ya wasiwasi. Mwanadada yule hakujibu kwa haraka kwanza alimtazama mteja wake kwa kitambo kifupi na cha haraka kisha akainamia daftari lake na kunyanyua tena macho na kumtazama mteja wake ambaye alikuwa kwenye tabasamu la kichokozi sana ikambidi naye kulipokea tabasamu hilo kwa tabasamu pia.
“Samahani chumba ulichohitaji kipo katika matengenezo hivyo hakiwezi kutumika kwa sasa. Tunavyo vyumba vingi na vizuri kiasi kwamba utafurahia hadi pale utakapoondoka. Unaweza kufanya uchaguzi mwingine tafadhali…?” Alitoa maelezo yule dada wa mapokezi huku akitabasamu zaidi kumchokoza mteja wake. Maelezo aliyopewa Alan alikuwa akiyategemea sana kwani alijua fika kuwa chumba hicho hakitumiki na pengine bado kipo kwenye uchunguzi wa kipolisi. Alichotaka yeye ni kujihakikishia kama kweli chumba hicho bado hakijaanza kutumika.
“Hakuna shaka dada nipatie chumba namba 22 nadhani kitanifaa sana.” Alisema Alan. Akafanya taratibu zote za huduma ile aliyokuwa akiihitaji kisha akaelekezwa mahali kilipo chumba chake. Alizipanda zile ngazi hadi kwenye ghorofa husika, akatembea kwenye korido iliyobeba vyumba vingi kwa kila upande hadi alipokutana na chumba namba 22. Akatazama kwenye ile korido na kuona namna utulivu ulivyokuwa mkubwa akafungua chumba chake hadi ndani na kupokelewa na chumba kizuri chenye kitanda kilichokuwa kimetandikwa shuka safi jeupe huku juu ya kitanda hicho kukiwa na mito miwili yenye foronya laini na safi. Akakikagua chumba kile kama ilivyo ada yake hadi pale alipojiridhisha ndipo alipopata wasaa wa kuweza kukaa kitandani na kutafakari namna ambavyo angeweza kuifanya kazi ile iliyomfikisha kwenye Hoteli hiyo. Usiku huo kwake ulikuwa ni usiku muhimu sana na hakutakiwa kuipoteza nafasi hiyo hata kwa sekunde moja. Alisimama na kusogea katikati ya chumba na kulisukumia begi lake uvunguni kisha akaufuata mlango na kuufungua taratibu akachungulia nje kwenye ile korido, hakukuwa na kitu cha aina yoyote chenye kutilia shaka na bado ukimya ulimpokea, akatoka na kuifuta ile korido kuanzia pale akizifuata namba kwa kwenda juu. Alikipita chumba namba 23 na kukifikia chumba namba 24 ambacho ndicho chumba alichoambiwa na yule dada wa mapokezi kuwa kiko kwenye matengezo. Chumba hiki alikifahamu tofauti na ambavyo aliambiwa na yule dada, yeye anakijua chumba hicho kwa namna ya pekee sana na hitaji lake kubwa ni kuhakikisha anaingia ndani ya chumba hicho na kuangalia mazingira yaliyofanikisha kuitoa roho ya marehemu Luteni Jenerali Leous Mipango. Alitumbukiza mkono mfukoni na kutoa lundo la funguo zake malaya na kufungua kile chumba akaingia ndani taratibu na kuurudisha kwa nyuma yake. Hakuwasha taa na badala yake alitumia kurunzi yenye mwanga mwembamba na mkali sana ya kijasusi (penlight). Alimulika kila kona ya chumba kile. Kilikuwa ni chumba kilichopekuliwa kwa kiasi kikubwa, kitanda kilikuwa wanguwangu mashuka ya kitanda hicho yalikuwa yamekusanywa mahali pamoja na kila mahali kulikuwa shaghalabaghala. Hakika chumba kile kilikuwa kimefanyiwa upekuzi usio wa kawaida hakutia shaka juu ya hilo akili yake ilimwambia kuwa moja kwa moja waliyofanya mambo yale walikuwa ni askari polisi au wapelelezi waliokabidhiwa upelelezi wa kifo hicho. Mashuka yalikuwa na damu na yalitapaa damu nyingi kiasi kwamba ilimshangaza. Haikuwa siku nyingi tangu kutokea kwa mauaji hayo hadi muda ambao yeye alifika hapo ni siku mbili zimetimia. Alipekuwa hiki na kile katika uangalifu mkubwa huku ile kurunzi yake ya kijasusi ikiwa inampa msaada mkubwa. Hakuna alichoambua hata hivyo alijiridhisha kwa macho yake kuwa kweli afisa yule wa jeshi aliuawa, kitu pekee kilichokuwa kikipita kichwani mwake ni kuhusiana na sababu iliyomfikisha Luteni Jenerali Leous Mipango mahali hapo wakati hakukuwa na sababu zilizomfikisha mahali hapo. Nini kimepelekea kufika hapo na kwanini kifo kimkutie hapo na si mahali pengine. Alan aliona kabisa kuwa kulihitajika uchunguzi mkubwa ili kuweza kuijua sababu husika na asingeweza kupata mwanzo wa uchunguzi wake huo kama hajapajua nyumbani kwa marehemu. Alitakiwa aijue hata familia yake ili kuweza kujua sababu ya yeye kukutwa akiwa mfu kwenye chumba cha Hoteli. Hiyo ilikuwa na maana gani…? Hiyo ilikuwa na maana ya kuwa ni lazima ajue utaratibu mzima wa maisha ya kawaida ya afisa huyo wa jeshi.
Alan aliinyanyua saa yake ya mkononi na kugundua kuwa muda ulikuwa umekwenda sana na hakukuwa na sababu ya kuendelea kumuweka mahali pale na pia hakuona umuhimu wa kuendelea kulala kwenye Hoteli hiyo ambayo watu wengi wamekuwa wakiinyooshea vidole hata hivyo kila kukicha imekuwa ikipokea wageni wa aina tofauti ambao wamekuwa wakija kwa mambo mengi. Alicho kifanya Alan baada ya hapo ni kurejea chumbani kwake kisha akachukua vitu vyake na kupotea kwa njia ambayo hakuna mtu yeyote ambaye angegundua. Alirudi moja kwa moja kwenye Hoteli ya Maua Inn na kuingia chumbani kwake kisha akaelekea maliwatoni na aliporudi alilikurubia koti la suti yake na kutoa pakiti ya sigara akachomoa moja na kujiwashia akaanza kuvuta huku akiitafakari kazi ile kwa mapana zaidi. Alipomaliza kuivuta ile sigara akawa tayari amepata wazo la kuwa ifikapo asubuhi ni lazima akaonane na madaktari aliotakiwa kuonana nao hapo ndipo alipotegemea kuianza kazi yake ya kuchunguza kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango. Alijitupa kitandani akazima taa na kulivuta shuka akauruhusu usingizi umchukue.
Alipomaliza kuivuta ile sigara akawa tayari amepata wazo la kuwa ifikapo asubuhi ni lazima akaonane na madaktari aliotakiwa kuonana nao hapo ndipo alipotegemea kuianza kazi yake ya kuchunguza kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango. Alijitupa kitandani akazima taa na kulivuta shuka akauruhusu usingizi umchukue.
SONGA NAYO…..
Gari moja ya rangi nyeusi ilikuwa ikiegesha nje ya jengo moja tulivu huko Raskazone ambalo liko pembezoni mwa bahari ya hindi. Baada ya gari ile aina ya Toyota Harrier kuegeshwa kwenye maegesho ya jengo hilo, ukimya ukachukua nafasi pasipo kuonekana mtu wa aina yeyote kuteremka garini. Ulipita muda wa dakika tatu nzima ndipo watu wawili walipofungua milango ya gari ile kwa upande wa mbele kila mtu kwa upande wake; ule wa dereva na upande wa abiria. Alikuwa ni mwanamke mrembo sana mwenye mwili wa wastani aliyekwenda hewani akiwa amevaa sketi fupi iliyoyaanika mapaja yake hadharani kwa kiasi kikubwa huku juu aliwa amevaa koti dogo la suti ambalo lilikuwa na vishikizo viwili kwa upande wa chini kiasi kwamba pamoja na kwamba vilifungwa hata hivyo havikufanikiwa kuyaziba matiti yake makubwa na mazuri yaliyokuwa yamefichwa nusu tu kwa sidiria ya rangi ya kibuluu. Alikuwa ni mwanamke mweupe wa ngozi mwafrika aliyejaaliwa urembo, nywele zake alikuwa amezimwaga na kuziachia kiasi kutaka kuuficha uso wake mpana kiasi uliobeba macho makubwa ya kurembua ambayo yaliongezewa na wanja wa kuuwa nguvu za kidume yeyote kuhimili kuikwepa ngono. Alivaa viatu vyenye visigino virefu ambavyo viliongeza urefu wake mara dufu. Mwendo wake wa maringo uliokuwa ukizitikisa nyama zake kubwa za makalio kiasi kwamba mwanaume yeyote rijali asingeacha kumtazama, ulikuja kumkutanisha na mwanaume aliyevaa suti ya bei mbaya kwa upande wa mbele wa ile gari ambaye naye aliteremkia upande wa pili wa ile gari. Bwana huyu ambaye kwa muonekano wa kawaida ni kwamba aliwahi kuonekana jijini Nairobi; Kenya akiwa na jopo la watu watatu ndani ya chumba kimoja cha Hoteli wakiwa wanajadili jambo fulani. Bwana huyu alikuwa ni yule ambaye alipenda kuzikata ndevu zake kwa mtindo wa ‘O’. Bwana yule alikwenda kukikamatia kiuno cha mwanamke yule na kumuongoza kuingia kwenye jengo lile mara baada ya mlango ule kufunguliwa punde tu waliposhusha miguu yao chini kutokea garini.
Huyu bwana ni nani? Na ni kwa namna gani leo hii ameweza kuonekana hapa nchini? Na ikumbukwe kuwa walipokuwa kule jijiji Nairobi na jopo lake walikuwa wakijadili kuhusiana na tukio lile la utekaji na mauaji ya maafisa wale wa jeshi ambao walikwenda kule kama wajumbe wa mpango ule wa kijeshi. Mauaji yalifanyika na wao wakaongea mafumbo ikiwa ni kama lugha waliyoichagua ili kuleta uelewano baina yao na ikiwa ni mara tu yule njorinjori alipowaletea taarifa ya kuwafurahisha ambayo mimi na wewe pengine hatukuielewa kwa vile ilivyokuwa imesheheni mafumbo kisha kila mmoja akachukua hamsini zake, leo hii anaonekana akiwa na mwanamke mrembo tena akimshika kiuno kabisa kudhihirisha kuwa alikuwa na mahusiano naye ya kimapenzi. Hili si la kushangaza sana kwa kuwa inawezekana na ni jambo la kawaida kutokea kwa watu wenye jinsia mbili tofafauti, Kitu kinachoanzisha maswali mengi na yenye shida kujibika ni yeye kuonekana huku tena kukiwa kumetokea kifo cha afisa mwingine wa ngazi za juu za jeshi nchini siku mbili nyuma tena ikisemekana kuwa kifo hicho kikiwa kimefanana na kile kilichowakuta wajumbe wale. Hii ni hatari tena hatari kubwa.
Balaa hili!
Waliongozana watu wale wakipita kwenye chumba hiki na kile na kufungua mlango huu na ule wa jumba lile kubwa lenye maskani yake huko mafichoni Raskazone kisha wakatokea kwenye korido ndefu na nyembamba ya kuvitia iliyopandwa taa zenye mwanga hafifu zilizokuwa zikimulika kwenye kuta safi zenye rangi ya kahawia. Sakafu yake inayonyurutika kwa usafi na kuifanya ionekane kama kioo, iliwafanya wazisikie hatua zao za madaha walizokuwa wakizirusha juu ya sakafu hiyo hata hivyo waliifuata kwa kitambo kifupi, kabla hawajafika mwisho wa ile korido wakaingia upande wa kushoto ambako kulikuwa na korido nyingine fupi ambayo hawakuifuata sana wakasimama mbele ya mlango wa kioo. Mlango ule ukajifungua wenyewe na wao wakapita huku wakiwa bado wamekumbatiana viuno, walikuja kulakiwa na chumba kipana cha kisasa ambacho kilionekana hakikutumika kwa ajili ya kulalia bali mikutano ama kupumzikia. Kilikuwa na meza pana ya mbao ngumu na viti vingi vilivyoizunguka meza ile. Hawakukaa kwenye vile viti pale mezani na badala yake yule bwana akamgeukia yule mwanamke na kumshika mgongoni akamvutia kwake. Hakuwa amevaa nguo nyingine ndani zaidi ya sidiria pekee baada ya lile koti la suti lililoshikizwa kidogo kwa chini kiasi ambacho tumbo lake zuri lote kuonekana hadi maeneo yale ambayo vishikizo vya kile kijambakoti viliposhikilia.
“Nategemea kupata burudani safi sana leo kutoka kwako mrembo wewe.” Alizungumza maneno hayo huku akiyaminyaminya makalio malaini na makubwa ya yule mwanamke. Mwanamke yule pamoja na kukashifiwa kwa kutomaswa namna ile hakuonekana kuchukizwa bali alitabasamu kwa kuchombeza kabisa kana kwamba aliimbiwa wimbo mzuri, alionekana akiifurahia ile hali ya kutomaswa makalio yake kwani alikuwa akijiramba kingo za midomo yake kwa ulimi wake huku akiwa ameyalegeza macho yake makubwa ya urembo yaliyomfanya yule bwana azidi kukoleza mchezo wake. Yule bwana alimvuta zaidi na kumpa mdomo naye yule mwanamke akausogeza wa kwake na kupena mate. Kitendo kile cha kuwafurahisha kiliongezwa na miguno yao ya kimahaba huku bwana yule akiendelea kumpapasa yule mwanamke kwa kiwango kikubwa kwani sasa alikuwa akiipandisha ile sketi fupi kiasi kutaka kuonesha hadi makalio yake.
Sauti ya hatua za viatu vilivyokuwa vikiiadhibu sakafu ya mule ndani ikaenda kutoa onyo la kuachiana kwa wawili wale. Wote waligeuka wakiwa na nyuso za furaha wakitazama mahali hatua zile zilipotokea. Bwana yule wa kutengeneza ndevu kwa mtindo wa ‘O’ aliyapiga kofi la wastani makalio ya mwanamke yule na kumuelekeza chumba cha kuelekea mara baada ya kuikutanisha sura yake na mzee mmoja aliyehifadhi nywele nyeupe na nyingi kichwani mwake akiwa na bakora ya rangi ya udongo mwekundu mkononi mwake huku moshi mwingi wa sigara ukitawanyika kutokea kinywani mwake na kuhanikiza chumbani mule. Bwana yule alipiga hatua za maringo huku yule mzee naye akipiga hatua za maringo wakisogeleana wote wakiwa wamebeba sura zenye furaha.
“Mohammed Saloom…asalam aleykum…?” Alisalimia yule mzee kwa furaha kubwa huku akimpa mkono yule bwana mwenye kuweka ndevu zake kwa mtindo wa ‘O’. Mohammed Saloom aliupokea kwa furaha ileile akiijibu ile salamu.
“Waaleykum salaam bwana mkubwa Zayd Aboushariff, habari za siku kadhaa zilizopita?”
“Habari ni njema kabisa karibu sana?” Alijibu Mohammed Aboushariff huku akimkaribisha na kuongozana na mgeni wake wakielekea kile chumba ambacho alielekea yule mwanamke. Walifika kwenye chumba kingine hiki kilikuwa kikubwa zaidi huku kikiwa na madirisha makubwa yaliyofunguliwa vioo sambamba na mapazia yake kusogezwa pembeni. Chumba kile kilikuwa na watu watatu yaani yule mwanamke aliyeingia na Mohammed bwana wa mtindo wa ‘O’ wa ndevu zake akiwa na bwana mmoja mnene aliyevaa suti za rangi ya kijivu aliyefahamika kwa jina la Zabuni Usambo na kijana mwingine mrefu zaidi njorinjori anayekwenda kwa jina la Mathew Bangile. Idadi yao sasa ilifikia watano na wote walikutana kwenye meza kubwa ya mstatiri iliyozungukwa na viti vya idadi yao. Yule mzee alikwenda kukaa upande mmoja wa meza ile na huyu Mohammed akakaa upande mwingine wa meza hiyo wakabaki wakitazamana huku hawa watatu wakikaa bavuni mwa meza ile. Walizunguukwa na bilauri zilizojaa maji baridi. Kimya cha muda kikashika hatamu kisha Zayd akaanza kwa kujikohoza kidogo kabla ya kuanza kuzungumza.
“Taarifa kutoka kwako…?” Alisema hayo huku akimtazama Mohammed Saloom. Mohammed akawatazama wote kwa namna ya pekee akajiweka sawa kitini na kuanza kuzungumza.
“Hakuna asiyejua kuhusu kinachofanyika hapa jijini, kila mmoja wetu anajua namna utendaji wa kazi unavyokwenda labda kama kuna tofauti.”
“Tofauti hakuna mpango unakwenda vilevile kama ambavyo ulipangwa. Juzi shinda jana, tumeliteketeza kontena jingine ambalo lilisheheni bidhaa zenye sumu. Kama ambavyo huwa tunafanya kwa makontena ya namna hii, huwa tunawaagiza watu wetu wenye uwezo wa kuyasogeza mahali pazuri pa kuyateketezea na ndivyo ilivyokuwa. Ilikuwa ni rahisi sana.” Alieleza huyu njorinjori Mathew kama ambavyo hupenda kufanya siku zote. Kimya kikazoa taarifa zote pale na kuzifutika kibindoni kwa muda na kuwaacha watu wale wakiwa wanatazamana huku baadhi yao wakijipatia maji kulainisha makoo yao baada ya taarifa nzuri kuwafikia.
“Vipi kuhusu nchini Kenya kuna sababu zozote za kuweka uangalizi au kutuma Ua kule…?” Zayd yule mzee aliuliza tena akifanikiwa kuufukuza ulimya. Macho ya wote pale yakamgeukia yule bwana aliyevaa suti ya rangi ya kijivu.
Kwanini yeye…?
Huyu bwana alikuwa ni afisa mkubwa kwenye ngazi za kijeshi nchini Kenya alikuwa anamiliki cheo cha Luteni na huyu bwana ndiye pekee aliyekubali kuwa mtoa siri wa mipango ya jeshi ambayo ilikuwa ikiundwa na majeshi ya nchi mbili ili kuweza kukabiliana na ugaidi katika nchi hizo. Unaweza kujiuliza ni kwanini huyu bwana amekubali kulihujumu taifa lake na jeshi lake kwa ujumla na kusababisha vifo vya wanajeshi wa ngazi za juu jeshini? Jibu hutakuwa nalo kwa kuwa hakuna ufumbuzi wa wazi kuhusiana na jambo hilo hata hivyo ukweli unasimama kuwa huyu bwana anayebeba jina la Zabuni Usambo ni mtu hatari kuliko watu wanavyomdhania ni nyoka ambaye huweza kumuua mtu mara mbili na zaidi kama akiamua na kuna baadhi ya vifo yeye ndiye msababishaji na amefanya hivyo makusudi tu ili aendelee kujilinda na asijulikane kama yeye ni msaliti. Kuna mambo mengi ya kutisha yapo nyuma yake na ndiyo sababu akawa hapa nchini akisheherekea kifo cha afisa mwenzake wa jeshi huku akizidi kutakiwa kuziweka wazi siri za taifa lake. Kwanini anashirikiana na magaidi na kwanini yuko radhi kuwaondoa maafisa wenzake wa ngazi za juu jeshini? Je, ni huyu tu Leous Mipango au wapo wengine kwenye orodha yake ambao watatakiwa kuuawa huku mratibu wa vifo hivyo akiwa amepata amri kutoka kwake? Inatisha hii.
Zabuni Usambo aliuvuta mgongo wake kutoka kwenye foronya safi ya kiti alichokalia na kuikingama mikono yake mezani huku macho yake makubwa na mekundu yakiwatazama wenzake.
“Kenya kuko shwari hakuna shaka kabisa bali shida iko huku.” Akasema na kuzidi kuyazunguusha macho yake kama mamba mwenye njaa.
“Kwanini useme hivyo na inajulikana kuwa tayari kuna vifo viwili vya maafisa wa jeshi tumevisababisha sisi wenyewe kimoja kikiwa kimetokea ndani ya ukumbiwa wa Hoteli ya Serena Nairobi huku kingine kikiwa kimetokea huko Kismayo nchini Somalia?” Aliuliza Zayd Aboushariff akiwa na mashaka kidogo na kauli ya Zabuni.
“Kwanini useme hivyo na inajulikana kuwa tayari kuna vifo viwili vya maafisa wa jeshi tumevisababisha sisi wenyewe kimoja kikiwa kimetokea ndani ya ukumbiwa wa Hoteli ya Serena Nairobi huku kingine kikiwa kimetokea huko Kismayo nchini Somalia?” Aliuliza Zayd Aboushariff akiwa na mashaka kidogo na kauli ya Zabuni.
SONGA NAYO…
“Kenya ni nchi yangu na mimi nikiwa kama afisa mkubwa wa jeshi nchini humo. Mipango ya siri ya kijeshi yote hainipiti na vile vile ni mshawishi mkubwa sana kwa Jenerali hata Rais wakati mwingine, kwani mbali na kazi mimi na hawa watu ni marafiki wa siku nyingi na tuliotokea kwenye kabila moja. Wanasikiliza hoja zangu, ushari wangu na hata michango yangu hasa pale wanapotaka kufanya jambo. Tambua kuwa mimi nalinda maslahi ya upande wangu nadhani mnajua hivyo siwezi kuona kazi hii inafanywa kuwa kubwa. Hadi hapa nafikiri mtakuwa mmenielewa kile ambacho namaanisha.” Akaweka tuo na kuwatazama wenzake kwa mtindo ule ule wa utazamaji kimya cha uelewa wa kile anachokizungumza kilipokuwa kimeendelea kutuama, Zabuni akaendelea.
“…mpanngo wa wana usalama wa taifa la Kenya ulikuwa umepanga kushirikiana na nchi hii kuhakikisha wanawaadabisha wale waliosababisha mauaji ya wajumbe wao sambamba na utekaji wake, nadhani mnajua kama vyombo nyeti vya kiusalama vya nchi hizi vikiamua kuungana nini kinatokea maana yake ni kwamba kazi hii ingekuwa ngumu na kubwa kiasi kwamba ingetuvuruga au kutupotezea wakati wetu mwingi bure. Nikakinga kifua pale baada ya kupokea ujumbe kwa njia ya barua pepe na wasuka mipango kuwa nihakikishe napunguza makali. Kazi haikuwa ndogo na pengine kama nisingetumia akili nyingi wangeweza hata kuniwekea alama ya uchunguzwaji kuonekana kama nimekuwa Nyumbu ama kuna jambo nalikingia kifua. Mimi nilipoona wanakuwa wabishi kuelewa, nikamvuta Jenerali pembeni pamoja na afisa mkuu kabisa wa shirika la kijasusi nchini mule na kuongea nao kwa kutumia mazungumzo na makibaliano ya kikao cha kwanza cha majeshi mawili haya mara yalipokutana Nairobi. Nyinyi wenyewe mnajua kwa kuwa niliwapa nyaraka zile za kwanza kwa uchache tu kwa kuwa zilibanwa sana na hata upatikanaji wake ulikuwa wa nyeti mno. Kila mmoja akaona jinsi Tanzania ilivyokuwa ikitaka kujitenga kwao na kujiona kuwa wao hawakuwa na matatizo ya kigaidi nchini kwao huku wakijiweka mbali zaidi. Nikajaza chumvi na nikawaambia kuwa kama isingelikuwa maafisa wa jeshi wa Kenya kuwapigia magoti wasingetuma wajumbe kuja kutoa maadhimio na maadhimio yenyewe hayakuwa ya moja kwa moja…mnaona sasa…! Hoja hii ikawa imewaingia watu hawa… Hah hah hah haaa…! Ndiyo iliwaingia maana nilihakikisha hawachomoki kwenye kazi yangu ya kupunguza makali kama ambavyo nilitakiwa nifanye. Wakaingia mkenge nami nikagongelea msumari wa moto kwa kuwambia kuwa, hakuna kukubali kushirikiana na watu ambao hawajali shida za wengine maana viongozi wa sasa si kama alivyo mwalimu Julius Kambarage Nayerere ambaye alijali shida za majirani zake kama za kwake na kufikia kuwasaidia wenzake wengi wa bara hili la Afrika kujikomboa toka mikononi mwa ukoloni. Unadhani kama si Nyerere Afrika ya kusini ingetoka mikononi mwa makaburu mapema? Kama si Julius Kambarage Nyerere; Msumbiji ingejinasua toka mikononi mwa wareno? Kama si Nyerere vipi kuhusu Uganda, Zimbabwe na Namibia…? Nchi hizi zingechelewa sana pengine kutoka mikononi mwa makoloni yaliyokuwa yamewashikilia. Na haikuwa hivi hivi tu kwa vyama kama Zimbabwe African National Union (ZANU) na Zimbabwe African People’s Union (ZAPU) vya Zimbabwe; African National Congress (ANC) cha Africa ya kusini; South West African People’s Organizatio (SWAPO) cha Namibia na kile cha Msumbiji Frente de Libertação de Moçambique (FRELIMO), kuweza kujipatia uhuru wake kirahisi. Vyama hivi vyote vilikuwa chini ya chama cha Tanu ambacho kilikuwa chini ya Jasusi aliyeacha historia kubwa duniani Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vikapewa mbinu, nguvu na motisha ya kujipatia uhuru navyo kwa kujiongeza kwao vikapata morali na wakafikia hatua ya kupigania uhuru wao ndipo Afrika ya kusini na wenzake wakawa huru. Unadhani hayo yote yangeweza kufanywa na viongozi wetu wa leo…? Wapii!” Zabuni Usambo alizidi kubwata huku akiwa anajiona ni moja ya washindi wakuu sana kwa kufanikisha lile. Hakuishia hapo la! Aliendelea;
“…kwanini nimezunguuka huku kote…?” Akasema. “…nimezunguuka huku ili kuwapa picha halisi ya kile ninachokizungumza kwao na kikubwa nilichotaka kuwamaliza kabisa ni kuhusiana na hoja yangu ya kuwa kwa sasa hakuna viongozi wenye kupenda ushirikiano wa kweli kabisa, ushirikiano wa shida zangu ni zako na shida zako ni zangu, hakuna…nakataa kabisa hakuna. Ushirikiano niliouona hapa ni ule wa shida zangu ni zako na shida zako ni zako mwenyewe. Nilipofikia hapa nikawaona wale mabwana wakishusha pumzi nzito sana na kuvifanya vifua vyao vipoe. Walinielewa. Pamoja na kuwa walinielewa hata hivyo hawakuacha kuuliza kuhusu vifo vya wanajeshi wao tena wa ngazi za juu…!” Akatabasamu Zabuni Usambo alipofika hapo. Watu wote pale mezani wakajiweka sawa kumsikiliza zaidi ili kujua namna alivyojibu maana hilo ndilo lililokuwa swali la wengi ijapokuwa liliulizwa na mzee yule mwenye nywele nyeupe aliyeonekana kuwa ndiye kiongozi; Zayd Aboushariff. Zabuni akaendelea mara baada ya kutua kutoka kwenye kuangua kicheko kikali cha sifa alipoona wenzake wamevutiwa na uhodari wake wa ushawishi.
“…mnajua niliwajibu nini sasa…! Heh heh hee! (Akamalizia kicheko), niliwaambia kuwa…!” Hapa Zabuni aliweka umakini na kusogeza masikhara pembeni.
“Niliwaambia kuwa lazima Tanzania itaingilia kati hili suala na haitakubali kamwe kuona wanajeshi wao wanauawa bila mpangilio na watakapoingilia kati kwa eidha kuwatumia majasusi wao ama vinginevyo sisi itaturahisishia kujua wabaya wetu ni akina nani maana unaambiwa uwakapo moto mdogo msituni fuata moshi. Hivyo nikawatanabaishia kuwa kazi yetu kubwa itakuwa ni kufuata moshi uliko. Yule mkuu wa kitengo cha ujasusi nchini Kenya akaonekana kupingana na kauli yangu na kuniuliza kuwa ina maana tutegee? Nikamjibu hapana, hata hivyo inawezekana pia. Lisikilizeni jibu langu kwa umakini. Nilimjibu hivi, huoni Korea na Marekani walivyokuwa wakizitumia hizi mbinu, mbinu za jogoo. Mbinu pekee za kumsubiria fulani aanze na kwa kuwa kila mmoja alikuwa na hofu na mwanzake kukawa hakuna wa kuanza hadi walipoamua kuita mkutano wa usuluhishi. Hoja yangu akaielewa, akatulia na kuona nilikuwa na maana kubwa sana ndani yake basi kwangu ikawa rahisi ili sisi tuweze kutimiza azimio letu nchini hapa kwani ndiwo mpango husika.” Alimaliza kuzungumza Zabuni na kuurudisha mgongo wake kwenye foronya laini ya kiti ambayo ilimpokea na kuuhifadhi mgongo huo kwa starehe akiwatazama wenzake ambao waliachia matabasamu ya ushindi. Walikuwa na haki ya kutabasamu kwa kuwa kila kitu walikiona kikienda vema kwa upande wao. Maandalizi ya muda mrefu kuhusiana na kile walichokikusudia kiwe ndiyo hasa yanayowapa ushindi mnono. Hata hivyo ingawa walikuwa na imani ya kila kazi iliyofanyika, bado walikuwa macho kila mahali kuhakikisha hakuna baya ambalo litakwenda kuwaharibikia kabla hawajafika mbali, hawakutaka kujipa imani moja kwa moja kuwa nchi ya Kenya italubali kutulia kimya pasipo kufanya juhudi zozote kuhusiana na wanajeshi wao waliouawa. Zayd Aboushariff akawatazama wenzake akiomba utulivu, kimya kilipopata nafasi akawaambia;
“Tusijisahau na kujiona washindi kiasi tukaacha dhamira yetu. Nchi hii tukiiamulia ni ndogo sana na haifurukuti. Huu ni mwanzo tu wa kuwaonesha kuwa sisi si watu wa kuchezea sharubu zetu hivyo basi tuwe ngangari huku macho yetu makali yakiwa wima kila kona ya mji huu. Ningependa kujua nini kinachoendelea hadi sasa na nilishawaambia kuwa ule mwili tangu kutoweka kwa giza la jana ambalo lilindoka na mwili wake hadi sasa ule nwili uko hospitali unaendelea kufanyiwa uchunguzi hilo mnalifahamu. Ninachotaka kujua si uchunguzi wa mwili huo lah! Nataka kumjua mtu atakayejitokeza kupokea huo uchunguzi na kutaka kuufanyia kazi. Hatuogopi wala kutishwa na wachunguzi bali shida yetu ni uchunguzi huo utaingia mikononi mwa nani hilo ndilo suala la msingi…!”
“Lakini mimi naona hata kuruhusu huu mwili ufanyiwe uchunguzi ni hatari sana, kwanini tumeruhusu hili lifanyike…?” Akawahi kuuliza Mohammed Saloom akiwa amemkatia kwa mbele yule mzee.
“Hofu yako nini…? Kama ni kuhusu kujulikana namna marehemu alivyouliwa si tatizo kwani si mara ya kwanza kugundua, watakuwa wameweza kugundua kwa mara ya pili kwani hata miili ile ya wajumbe waliouawa kwenye ukumbi wa Serena Hoteli; Nairobi iliuawa kwa aina hii ya kifo na ilifanyiwa uchunguzi na kama ilifanyiwa uchunguzi unafikiri kuna maana gani nyingine tofauti, hakuna…tayari wanazo taarifa za kifo ama vifo vyote. Sasa wewe hofu yako ni nini?” Akatoa majibu Zayd Aboushariff kwa mapana zaidi kisha akahoji mwishoni.
“Ninavyoijua nchi hii wakishagundua sababu inayoendeleza vifo vya wakuu wao vinavyotokea kila uchao na uchwao, lazima watalivalia njuga hili…!”
“Enhee! Hapo ndipo pazuri na patakapo maliza kazi yetu kwani mimi nilikuwa naongea kitu gani jamani…?” Akauliza Zayd akiikata kwa mbele kauli ya Mohammed huku akiwa ameinyoosha mikono yake kwa kuitawanya mithili ya mtu atoaye umbea. Alipoona wenzake wakiwa wanamtazama kama picha ya mnato akaendelea.
“…maana yangu ilikuwa ni hiyo na kama ungenipa muda wa kumalizia kuzungumza hadi mwisho na kunisikiliza kwa umakini mkubwa, ungenielewa au niseme ungeielewa maana yangu. Watakapo jifanya kulivalia njuga watatukuta sisi tukiwa imara zamani sana hivyo ndiyo maana nikasema nataka kujua ni namna gani watu wetu wako na wamejipanga kwa vipi…!”
“Sasa nimeelewa…!”
“Umeelewa eeenh…! Safi, hah hah hah haaa…! Sasa hebu tupeni utaratibu ulivyo? Je, vipi kuhusu maendeleo ya maua yalilopandwa kona zote za jiji hili ili kumnasa nyuki, yameshaanza kufanya mambo yake?” Akauliza Zayd baada ya kufurahishwa na uelewa wa watu wake.
“Hadi sasa hakuna nyuki aliyepata harufu yake ingawa yanachanua kwa kasi na yanaendelea kutoa harufu nzuri kwenye kila pembe ya mji huu,” akajibu Mathew (njori njori) akiwa mpole kabisa.
“Unataka kuniambia kuwa hakuna mpuuzi yoyote aliyeingia hapa jijini?” Aliuliza kwa hamaki na mshangao mkubwa Zayd.
“Mbona una wahaka mkuu!” Aliuliza Mohammed Saloom.
“Lazima niwe na wahaka maana ni jambo lisilowezekana kirahisi kuwa pamoja na hili kubwa kutokea uambiwe bado hakujaingia mdudu hata mmoja zaidi ya hawa polisi wanaorandaranda kutwa kucha. Kha!” Akahamaki Zayd. Mathew akaingilia kati na kuwatoa wasiwasi wenzake kwa kuwaambia kuwa wasitie shaka kwani hadi wakati huo wakiwa wanaongea tayari kila upande ulikuwa ukiimarisha ulinzi vya kutosha hivyo kama kumetokea taarifa ya kuwa hakuna mdudu aliyeingia si kwamba jambo hilo limeongelewa tu alimradi liongelewe la! Bali aliyeliongea alikuwa na uhakika mkubwa kwa kuwa yeye ndiye mwenye kuwaongoza vijana wote muhimu ambao wanahakikisha ulinzi unakuwa imara zaidi. Kidogo imani kwao ikajengeka kikao hicho kikawa kimefika tamati wakatawanyika wakikubaliana kukutana tena hasa pale itakapolazimika kuwa hivyo.
Mathew akaingilia kati na kuwatoa wasiwasi wenzake kwa kuwaambia kuwa wasitie shaka kwani hadi wakati huo wakiwa wanaongea tayari kila upande ulikuwa ukiimarisha ulinzi vya kutosha hivyo kama kumetokea taarifa ya kuwa hakuna mdudu aliyeingia si kwamba jambo hilo limeongelewa tu alimradi liongelewe la! Bali aliyeliongea alikuwa na uhakika mkubwa kwa kuwa yeye ndiye mwenye kuwaongoza vijana wote muhimu ambao wanahakikisha ulinzi unakuwa imara zaidi. Kidogo imani kwao ikajengeka kikao hicho kikawa kimefika tamati wakatawanyika wakikubaliana kukutana tena hasa pale itakapolazimika kuwa hivyo.
SONGA NAYO…
WAKATI KIKAO KILE KILICHOKALIWA HUKO RASKAZONE KINAFIKA TAMATI, asubuhi hiyo mambo yalikuwa yakiendelea kama ilivyopangwa na wapangaji. Alan alikuwa kwenye maegesho ya magari ya Hospitali ya Bombo akikatiza eneo hilo huku akiyatazama magari yaliyoko eneo hilo kwa umakini mkubwa lengo lake kuu lilikuwa ni kutazama gari ambayo alishapewa maelekezo yake tayari. Aliona gari nyingi zikiwa zimeegeshwa hapo nyingi zikiwa za wafanyakazi wa hospitalini hapo na chache zikiwa zinamilikiwa na hospitali hiyo. Katika pitapita yake aliweza kuona gari ambayo hisia zake zilimwambia kuwa hiyo ndiyo ambayo alipaswa kuitumia kwa kuwa mkuu wake alishamwambia namna gari hizo zilivyo. Ilikuwa ni Toyota Harrier yenye rangi ya maziwa ikiwa imetulia tuli gurudumu zake imara zikiwa mpya kabisa zikampa hamasa ya kupenda kuitumia gari hiyo. Akatoa kikasha kidogo kilicho na fuguo ambazo ndizo zinazotumiwa na gari hizo alizoambiwa atakutana nazo hapa jijini, akaminya kitufe kilichopo kwenye kikasha kile kilichobeba funguo na kweli gari ile ikaitika kwa kutoa kengele. Alijiridhisha na ukaguzi wake akaondoka na kuelekea ndani kabisa ya Hospitali ile akiwa amekamata ujia mmoja upande wa kushoto wa Hospitali. Akanyoosha hadi mbele kabla yajafika kwenye jengo la zamani ambalo lilitumika kama ofisi akaingia upande wa kulia kisha akauacha ujia uliokuwa ukielekea kwenye wodi za kawaida na kuukamata ujia uliokuwa ukielekea kwenye wodi ya Cliff. Hatua zake za haraka haraka zilimpeleka hadi ulipo mlango mkubwa wa kuingilia kwenye vyumba vya wodi ile, akaichunguza mandhari ya pale kwa haraka na umakini mkubwa akatazama na alipotoka kwa namna ya pekee alipohakikisha hakuna aliyekuwa akimfuatilia ndipo akaingia. Alifika hadi sehemu ya kupumzikia wagonjwa na wauguzaji wa wagonjwa aghalabu hasa nyakati za mchana, akatazama upande wa kushoto ambako kulikuwa na ofisi ya wauguzi huku upande wa kulia kukiwa na viti safi vyenye foronya laini kwa ajili ya mapumziko. Akachungulia dirishani baada ya kumuona muuguzi akitokea kwenye chumba kimoja kilichopo nyuma ya mlango wa kuingilia kwenye ofisi hiyo na alipoutazana vizuri ule mlango akagundua kilikuwa ni chumba ambacho walikitumia wauguzi kubadilishia nguo. Alipotazama kwa ndani zaidi ya ofisi ile upande wa mbele wa macho yake akaona kulikuwa na mlango mwingine hata hivyo huo haukuwa umeandikwa chochote.
“Habari yako kaka…?” Alisalimia Alan huku macho yake yakiwa yanatazama kila mahali kwa umakini mkubwa.
“Salama.” Alijibu yule muuguzi huku akiwa anachukua boksi hili na lile akitoa dawa hii na ile akiwa hamtazami Alan usoni. Hali hiyo ya kutokutazamwa usoni ikawa inampa Alan nafasi ya kuweza kulitazama lile jengo vizuri na kuona namna muundo wake ulivyo. Alikuwa akishindana na nafsi yake kwa wakati huo juu la hitaji lake, alikuwa akijiuliza kama aulize ama lah! Binafsi alikuwa akikifahamu hadi chumba ambacho madaktari aliotakiwa kukutana nao wamepewa kama ofisi hadi pale uchunguzi wao utakapofika tamati kwani maelezo yote alikuwa nayo. Akiwa hapo bado huku akiendelea kumtazama muuguzi yule namna anavyojishughulisha na hamsini zake, akauona ule mlango wa upande wa mbele ya macho yake mule ofisini mwa wauguzi ukifunguliwa. Akaweka umakini zaidi kuona kama anayetoka ndani ya chumba kile ndiye anayemuhitaji au ni vinginevyo. Hakuwa amekosea, mlango ulipofunguliwa kabisa sura ya Dokta Limo ikaonekana ikijitoa mule ndani.
“Karibu, nikusaidie nini sijui…?” Yule muuguzi hatimaye akauliza baada ya ukaribisho kwa mara nyingine hata hivyo Alan alimpuuza na kujifanya kutokumsikia, yule muuguzi alimtazama Alan kwa mara ya kwanza, Alan aliyekuwa akilitegemea lile akageuza sura yake na kumpa muuguzi yule shavu hivyo kumfanya muuguzi yule asimuone sawia kisha akakamata sinia lililosheheni dawa. Wakati akiwa anataka kutoka Dokta Limo akawa anapita pale na kumpita akawahi kuwa wa kwanza kutoka nje.
“Dokta?” Aliita Alan baada ya kumuona Dokta Limo akiwa amechukua uelekeo wa upande wa nyuma wa jengo lile baada ya kuifuata korido ile. Dokta Limo aligeuka kwa kasi na kutazama sauti ilipotokea kisha akajipa utulivu mara baada ya kuona sura ambayo hakuwahi kuiona machoni mwake. Alan alizivuta hatua zake hadi alipomkaribia akamsabahi na kumuomba watoke mbali na pale. Walichukua uelekeo ambao Dokta aliuchukua wakafungua mlango wa kutokea nyuma ya lile jengo wakatoka na kuurudishia mlango nyuma yao. Walipokelewa na nyasi fupi zilizokatwa kwa mashine maalumu, miti mingi iliyoweka kivuli cha kutosha huku wakiifurahia hewa safi iliyokuwa ikitokea baharini.
“Wewe ni nani kijana?” Akauliza Dokta Limo akiwa anamtazama Alan usoni moja kwa moja. Alan aligeuka kutoka alikokuwa akitazama na kumtazama Daktari huyo.
“Jina langu ni Iddialan Simion…!” Alijitambulisha sambamba na kumkabidhi Daktari huyo karatasi fulani ambayo ilisomwa vema, aliirudisha ile karatasi na kumtazama tena usoni kisha akasema.
“Nilishangaa sana kusikia mtu ananiita maana hakuna mtu anayeweza kuniita nikiwa siko kwenye mavazi ya kidaktari kama ambavyo wewe umeweza kuniita niliamini ni lazina atakuwa ni mtu anayenifahamu vizuri.”
“Ni kweli Daktari na utambulisho niliopewa kukuhusu wewe na Dokta Lumoso usingeweza kunipoteza hata kidogo.” Alisema Alan. Kimya kikachukua mamlaka yake, utulivu ukatawala huku upepo mwepesi ukiitikisa miti kwa madaha na kuifanya hali ya hewa ya mahali hapo kuzidi kuleta hamasa ya kuendelea kuwepo.
“Vipi kuhusu kazi…?” Akauvunja ukimya ule Alan, akameza mate na kuendelea na ulizo lake.
“…nini ambacho mmeweza kukigundua kwenye mwili wa marehemu?”
“Hakuna tofauti na ule mwingine uliotokea Nairobi tukiachana na ule wa meja Deus Macha ambao umezikwa tayari. Nadhani tusiandikie mate wakati wino ungalipo, twende kwenye chumba cha uchunguzi ambako Dokta Lumoso anafanya uchunguzi wa mwisho maana tumepokea amri kuwa jioni hii mwili unatakiwa uwe tayari kwa kuchukuliwa ili kesho uweze kufanyiwa mazishi.” Alisema Dokta Limo huku wakiwa wanazunguuka lile jengo kuweza kuondoka eneo lile na kuelekea chumba cha uchunguzi ambacho kimetengwa maalumu kwa ajili ya uchunguzi huo wa kina.
“Unadhani kulikuwa na ulazima wa kufanya uchunguzi wa mwisho ikiwa kila kitu unasema kinafanana na kile kilichoonekana awali?” Akauliza Alan.
“Hakukuwa na ulazima wa kufanya hivyo hata hivyo kama madaktari huwa tunapenda kufanya mambo katika ubora mkubwa sana kwani endapo kutatokea dosari itakuwa ni fadhaa kubwa sana kwetu na hatutaaminika tena kama ambavyo tunaaminiwa sasa. Lazima tujitofautishe na madaktari wengine kwa kuwa sisi tunatazamwa zaidi ya mara mbili.”
“Hakika usemalo.” Alijibu Alan. Walikuwa wakizipanda ngazi za jengo moja la ghorofa kisha wakaifuata korido ndefu ambayo ilikuja kuwatoa kwenye ujia wa juu kwenye jengo lile la juu na kushuka tena ngazi kwa upande mwingine. Waliufuata ujia wa chini baada ya kushuka zile ngazi, walikuwa wakipishana na watu tofauti tofauti wakiwemo wagonjwa, wauguzi na madaktari wachache. Hakuna aliyekuwa akijishughulisha na mwenzake kila mmoja alionekana kuwa na jambo lililomtinga kichwani mwake. Walikuja kuingia kwenye jengo moja dogo lililojengwa kwa madirisha ya vioo hata hivyo madirisha yale hayakuwa ya kumfanya mtu aweze kuona ndani kwani yalitengenezwa kwa juu. Waliingia ndani ya jengo lile baada ya Dokta Limo kuusukuma ule mlango, walipokewa na korido nyembamba na fupi ambayo waliiacha baada ya muda mfupi na kuingia kwenye chumba kimoja. Hiki kilikuwa ni chumba cha kubadilishia mavazi, walivaa mavazi ya kiuchunguzi sambamba na maski za kuziba pua na kinywa kisha wakatoka na kuingia kwenye chumba kilichokuwa kikitazamana na walichotoka. Chumba hiki kilikuwa kimya sana, hakikuwa na vurugu na makorokoro mengi zaidi kilikuwa na kitanda kimoja meza moja na kiti kimoja usawa wa dirisha huku kikiwa na sinia moja la wastani lililobeba vifaa vya kupimia na zana mbalimbali ndogondogo za kiupasuaji kama viwembe, pamba, chupa za dawa, sindano, mikasi midogo na kadhalika. Kulikuwa na mtu mmoja aliye katika mavazi kama ambayo walivaa wao. Akiwa karibu na kitanda ambacho kilikuwa na mwili uliofunikwa shuka hadi kifuani ukiwa umewekwa pamba sehemu za wazi. Kimya kilitanda maradufu mule ndani huku mzizimo wa kiyoyozi ukiichagiza hofu iliyomo. Walisogea hadi hapo alipo huyo mtu na huo mwili Alan na Dokta Limo. Waliutazama kwa pamoja ule mwili kana kwamba wanaufanyia maombezi uamke ungali hai.
“Huu ndio mwili wa Luteni Jenerali Leous Mipango…!” Akasema Dokta Limo akiwa amesimama nyuma ya Dokta Lumoso kisha kuufunua ule mwili pale kitandani kutokea kifuani lilipoishia lile shuka jeupe hadi kiunoni. Alan alikuwa makini sana kuhakikisha anaona kila kitu kwa dhahiri si pichani tena kama alivyouona wa Luteni Usu Makame Daudi. Dokta Lumoso akageuka kama aliyeshtuliwa baada ya Dokta Limo kutoa ile sauti ya maelekezo hata hivyo kabla hajauliza chochote Dokta Limo akaendelea.
“Nadhani unaweza kujionea kwa macho ya kawaida namna hali ilivyo kabla hatujakupeleka kwenye majibu ya uchunguzi.” Bado Dokta Lumoso Papi Mmbai alikuwa akiwashangaa pasipo kuzunguamza chochote. Alan aliutazama ule mwili kwa kitambo kifupi na kuwatazama madaktari wale wawili ambao hasa ndiwo waliohusika na uchunguzi wa mwili huo.
“Huyu ni mpelelezi ambaye ametumwa na Mr. Dao kuja kujua juu ya hiki tukichunguzacho.” Dokta Limo akatoa utambulisho kwa Daktari mwenzake ambaye sasa alimtazama Alan akiwa na tabasamu pana baada ya kulisikia jina la Mr. Dao. Hakuwa na shaka tena na Alan aliporidhishwa na utazamaji wake. Dokta Lumoso akaufunika ule mwili gubigubi kisha akachukua pini na kadi moja ndogo akaibandika juu ya lile shuka akabana pini wote wakatoka mule chumbani na kuingia kwenye kile chumba cha kubadilishia mavazi ambako waliacha mavazi yao na kuingia kwenye mlango mwingine kwa humo ndani. Huko walikaa kwenye meza ya pamoja na kuzungumza mengi yahusuyo vipimo.
“Kama ambavyo Daktari amekuelekeza kijana kuwa mwili huu haukuwa na tofauti na mwili wa marehemu Makame Daudi aliyeuawa jijini Nairobi. Tumegundua matundu mawili ya risasi ambayo yameacha majeraha mabaya sana upande wa nyuma zilikotokea risasi. Tundu moja likiwa kwenye paji la uso na tundu jingine likiwa shingoni. Yaani ni kama kifo kile kimehamishiwa huku hakuna tofauti yoyote ile. Alama tatu za kitu chenye ncha kali kama kucha za mnyama jamii ya paka pia huku zimeonekana na si kuonekana tu bali hata madhara yake yamejitokeza…”
“Dokta unataka kuniambia hata kwenye mwili huu sumu ile imejitokeza?” Akauliza kwa kudakia Alan macho yake makali akiwa kayatoa.
“Ndiyo,” alijibu Dokta Lumoso akaweka pozi kidogo na kuendelea tena.
Yaani ni kama kifo kile kimehamishiwa huku hakuna tofauti yoyote ile. Alama tatu za kitu chenye ncha kali kama kucha za mnyama jamii ya paka pia huku zimeonekana na si kuonekana tu bali hata madhara yake yamejitokeza…”
“Dokta unataka kuniambia hata kwenye mwili huu sumu ile imejitokeza?” Akauliza kwa kudakia Alan macho yake makali akiwa kayatoa.
SONGA NAYO….
“Ndiyo,” alijibu Dokta Lumoso akaweka pozi kidogo na kuendelea tena.
“…VX Nerve Agent hata huku imejitokeza tena kwenye mwili huu sumu hiyo imeonekana kusambaa mwilini kwa kiasi kikubwa hata kuliko ule wa awali.”
“Hiyo inamaana gani?”
“Maana yake ni kwamba mwili huu uliondoshwa maisha yake na sumu hii kisha risasi zikafuata.” Alijibu kwa utaratibu Dokta Lumoso kama ilivyo ada yake. Majibu haya yalimpa wakati mgumu sana Alan, kifo cha kwanza kilionesha kuwa risasi zilitangulia na kufuatiwa na sumu, hii ilikuwa ni taarifa ambayo kwake hakutakiwa kuichukulia kiwepesi hata kidogo. Alizungumza mengi na madaktari wale akiwahoji hiki na kile kuhusiana na mambo ya kitaalamu alipomaliza mazungumzo nao aliichukua nakala ya ripoti ile na kusimama akiwa pamoja na Dokta Lumoso Papi Mmbai wakatoka wakizungumza lile na hili huku wakizirusha hatua zao kwa utaratibu hadi nje ya jengo lile ambalo walilitumia kwa ajili ya kufanyia uchunguzi. Walikuwa kwenye kivuli kikubwa cha miti ya miembe ambayo ilitawala hospitalini hapo, bado walionekana wakizungumza huku wakiwa wanatembea na kusimama kwa namna fulani. Hatua zao ziliwafikisha kwenye mapumzikio ya wanaosubiri huduma au wanaosubiri majibu ya huduma zao hapa wakaacha ule ujia waliokuwa wakionekana kuufuata na kushika ujia mwingine ambao ulikuwa ukielekea maabara. Hata hivyo hawakufika mbali Dokta Lumoso alimfinya Alan mara baada ya kuona kitu chenye kuushtua moyo wake. Alikuwa ni msichana mrembo sana aliyevaa suruali ya jeans yenye rangi ya kibuluu iliyoiva ambayo ilimkaa vilivyo yule binti, alivaa viatu virefu vilivyoongeza urefu wake kwa kiasi kikubwa, alivaa kishati kidogo cha rangi nyekundu akiwa amezifunga nywele zake kwa nyuma alizozinyongorota zikawa ndefu pamoja kama mkia wa Ngedere. Alikuwa akitembe mwendo wa haraka huku akiyatikisa maungio yake ya nyuma kwa namna ya kuvutia sana, machoni alivaa miwani ya kirembo iliyomfanya aonekane wa kipekee mno.
“Si kama namuona kwa mara ya kwanza huyu mwanamke, ni mara ya tatu au niseme tangu tumefika hapa amekuwa ni mtu wa kufika hapa mara kwa mara.” Aliongea Dokta Lumoso huku akimtazama yule msichana ambaye alikuwa akinyoosha njia akitokea kwenye lango kubwa la kuingilia hospitalini mule. Alan alimtazama vizuri na kumuweka kwenye alama yake ya kiuchunguzi vema.
“Hujawahi kujua anafuata nini hasa?” Akauliza.
“Huwa anafika hadi kwenye jengo la Cliff na kuingia kwenye wodi moja ya mwisho kabisa kule kuna mgonjwa huwa anakwenda kumuangalia…!”
“Wodi ya mwisho…?” Akauliza kwa hamaki Alan kwa kuwa wodi hiyo ambayo Dokta Lumoso anaizungumzia ni ile ambayo waliipita akiwa na Dokta Limo na kutokea upande wa nyuma wa jengo hilo la Cliff. Kuna mgonjwa wake huko? Akawaza Alan kisha akageuza shingo kwa haraka sana na kutazama upande wa mbele ambako ndiko uliko ujia wa kuelekea jengo la Cliff, alimuona huyo mrembo akiwa ananyoosha akielekea huko kitu kilichoamsha hisia zake za wazi ni kwamba alimuona akiwa anatazama kila upande kama mtu anayechunguza kama kuna mtu yeyote aliyekuwa akimfuatilia.
“Wanajua uwepo wenu hapa?” Akauliza Alan huku akizidi kutazama kwenye ule ujia.
“Wanajua kuwa tupo hapa nadhani…!” Alijibu Dokta Lumoso kisha akamtazama Alan. Alan akasema;
“Kazi imekwisha mnatakiwa kuondoka haraka sana na ni muda huu…!” Wakati anamaliza kuongea, Dokta Limo akawa tayari amefika akasema kuwa kila kitu ameshakabidhi mahali husika hadi ripoti ya uchunguzi. Kuna gari inawasubiri nje hivyo wametakiwa kuondoka haraka sana. Kauli ile ya Dokta Limo ikamfanya Alan amtazame sana Daktari huyo kisha akatoa simu yake kubwa na kutazama kama kuna ujumbe ulitumwa kwake. Hakika kulikuwa na ujumbe ambao ulimwambia kuwa kazi imekwisha ya wataalamu wale kuwapo hapo jijini kwani ni hatari kubwa kama wataendelea kuwapo. Alielewa maana hivyo hakusubiri maana zaidi ya hiyo, akawaruhusu madaktari wale kuondoka. Akalitazama lile eneo kwa namna ya kulichunguza ili kuona kama kungekuwa na macho ya watu wasio wa kawaida alipoona hakuna na kila mtu yuko na hamsini zake, akachepuka na njia moja akaifuata njia hiyo huku akiwa anatembea kwa haraka sana. Alikunja kona fulani hadi akafika kwenye mlango wa jengo la Cliff hata hivyo hakuingia ndani alilizunguuka lile jengo na kutokea upande wa nyuma. Akatembea kwa tahadhari kubwa hadi alipolikaribia dirisha la chumba kile cha mwisho ambapo Dokta Lumoso alisema kuwa ndipo msichana huyo anapoingia. Alitega mahali ambapo pasingempa wakati mgumu kuweza kusikia maongezi yaliyokuwa yakiendelea kwa upande wa ndani.
“Sijajua kama ni nyuki amependa harufu ya Ua lakini yuko karibu sana na Ua husika…!” Ilisika sauti kwa ndani na ilikuwa ni sauti ya kiume.
“Vipi kuhusu madaktari wanasemaje kuhusu afya yako?” Sauti ya kike ilizungumza na Alan akainyaka vema kabisa.
“Afya yangu haitatanishi kwani ugonjwa huu si mara ya kwanza kuugua nilishaugua hapo awali na dalili zake ni zilezile hivyo wapo kwa ajili ya kunitibu hata hivyo sijajua itakuwa ni tiba ya aina gani?” Sauti ya kiume ilisikika. Alan alishtuka sana kwa namna watu hao walivyokuwa wakizungumza, haikuwa lugha ya kawaida hata kidogo ilijaa mafumbo sana lugha hiyo. Hapa alipata picha ya jambo fulani.
“Kuna umuhimu wa kuonana na Dokta sasa?” Sauti ya kike iliuliza.
“Ikibidi ili aniambie anataraji kutumia tiba gani kunitibu maana hawa madaktari wengine siona kama wanatija…!”
“Ok, nitarejea kukupa taarifa.”
“Ok,” maongezi yale yalikoma kisha mlango kufunguliwa Alan alikuwa na hamu kubwa ya kuonana na huyo mgonjwa haraka iwezekanavyo hivyo alitazama kila mahali kama kuna mtu yeyote alikuwa akimfuatilia pale alipokuwa amesimama akifuatilia mazungumzo hayo ya mafumbo, hakuona. Akainama chini ili kivuli chake kisionwe na mtu aliyeko ndani akapita chini ya dirisha pasipo kufanya kelele yoyote na kuibukia upande ulipo mlango wa nyuma wa lile jengo kwani jengo hili lilikuwa na milango mitatu. Mlango wa kwanza ulikuwa ni wa mbele ambao ndiwo hutumiwa zaidi na kila mtu, kulikuwa na mlango wa upande aliyopo ambao huu ulitumiwa na wagonjwa waliopata nafuu au ndugu zao waliopo kwa ajili ya kuwauguza. Waliutumia mlango huu kwa ajili ya kupunga hewa kwa kuwa eneo hili la nyuma lilikuwa na miti mingi ya Miarobaini na mikoko kwa ipande wa chini kwa kuwa jengo hilo halikuwa umbali mwingi kutoka bahari ya hindi ilipo. Mlango wa mwisho na wa tatu ni ule ambao aliutumia yeye na Dokta Limo mara ya kwanza walipotoka huko nyuma na sasa alikuwa akitaka kuutumia tena kwa lengo la kuingia. Akili ya Alan ilimwambia kuwa kwa muda ule bado mlango ule uko wazi haukuwa umefungwa. Akachungulia kupitia nondo za mlango ule na kumuona yule msichana mrembo akiwa anatoka kwa mwendo wa haraka sana akizipa shida nyama zake za makalio kwa namana anavyozitikisa. Alinyanyua mkono uliobeba saa Alan na kutazama majira. Ilikuwa ni saa sita tayari na dakika ishirini. Alikuwa amesaliwa na dakika arobaini pekee kabla hajatafutwa simuni na Maisara yule dereva teksi aliyepeana naye miadi ya kukutana kwa ajili ya kupata chakula pamoja. Aliufungua ule mlango taratibu mara baada ya kuhakikisha yule msichana amepotelea nje tayari. Ulikuwa haukufungwa kama alivyojiaminisha na sasa akawa amefanikiwa kuufungua akaingia na kukikabili kile chumba cha mwisho ukitokea mlango wa mbele au cha kwanza kwa mlango ule alioingilia yeye ambacho kwa juu kiliandikwa Cliff no. 04. Akajishika kiunoni akiitazama kama silaha yake ilikuwapo alipojihakikishia kuwa ipo, aliusukuma mlango na kuingia ndani. Kulikuwa na vitanda viwili vya chuma ndani ya kile chumba upande wa kushoto ukiingia, upande wa kulia kulikuwa na kijiboksi kidogo cha mbao chenye droo tatu pana kwa ajili ya kuwekea vifaa vya wagonjwa pia kulikuwa na chumba cha kubadilishia nguo kwa upande huo wa kulia. Juu ya kitanda kimoja kulikuwa na mtu aliyejifunika shuka hadi kifuani, alikuwa ametulia kimya juu ya hicho kitanda jicho lake likimtazama yeye. Alan alifanikiwa kuuona wasiwasi uliojiunda machoni mwa yule mtu pale kitandani. Akatazama dirishani Alan ambapo aliona pazia lililo kusanywa mahali pamoja na kubanwa na mkanda maalumu kisha akayarudisha macho yake kwa mgonjwa aliyekuwa ameanza kujivuta ili kuketi kwa kuwa ugeni alioupokea pengine si ule alioutarajia.
“Vipi hali yako mgonjwa…unaendeleaje?” Alisabahi Alan.
“Sija…sijambo kiasi namshukuru Mungu…!” Alijibu yule jamaa pale kitandani akiwa anatoa sauti ya kusuasua kama mgonjwa ambaye kweli alikuwa akianza kupata unafuu. Hapa akapata picha nyingine kuwa hawa watu walikuwa wapo hapa Hospitali kwa kazi maalumu na si vinginevyo. Sauti aliyokuwa akiizungumza huyo jamaa ilikuwa ni tofauti kabisa na aliyokuwa akiizungumza akiwa na yule binti.
“Pole sana je, madaktari wanasemaje kuhusu afya yako kwa sasa…?”
“Imebadilika sana, si sawa na nilivyoingia hapa kwa kweli wanajitahidi sana na huduma zao ni nzuri mno.” Alijibu yule jamaa mgonjwa. Wakati yule jamaa anajibu, Alan akili yake ilikuwa mbali sana kifikira, alikuwa akiwaza namna watu hawa walivyoweza kulitumia hilo jengo na kukitumia hicho chumba cha kulazia wagonjwa bila shida yoyote na kilikuwa kimefanyiwa usafi wa hali ya juu huku kukiwa na makasha kadhaa ya dawa kama geresha. Hadi hapo alikuwa na hakika kuwa mbele yake hakuwa na mgonjwa hilo hakuwa na shaka nalo. Swali lake kuu ni je, kama hawa watu wanakaa kwenye chumba cha kulazia wagonjwa na ikiwa si wagonjwa, kuna nini kimejificha? Na imekuwaje wazipate taarifa za madaktari waliotumwa na kitengo cha usalama mapema kiasi kile? Moja kwa moja akajua kuna mtu aliyekuwa akizitoa hizi taarifa na huwenda mtu huyo alikuwa ni kiungo muhimu sana kwao kwa kuwa wanahakika anazipata taarifa mapema. Ili kujua yote hayo ilikuwa ni lazima ashughulike na huyo jamaa mgonjwa.
“Wewe ni nani…?” Yule jamaa mgonjwa akauliza akiwa na tashwishi isiyojificha usoni mwake. Alan hakujibu kwanza alikitazama kitambulisho kilichokuwa kikining’inia kifuani mwake hiyo ilitosha kumfanya yule jamaa akisome vema kile kitambulisho. Abasi Mgizu alitambulika kwa jina hilo akiwa kama mwandishi wa habari wa gazeti la serikali. Alan alirudi nyuma huku akiwa makini na kuufunga kabisa ule mlango. Kitendo kile kikawa kimesababisha sintofahamu kwa yule jamaa hivyo kwa kasi ya ajabu akaupindua mto na kutoka na bastola hata hivyo bastola ile haikupata makazi ya kudumu kwenye mikono yake, kwa kasi ya umeme Alan ajizungusha na teke kali ambalo liliupiga mkono uliokamata bastola na kuitupilia ukutani ambako ilijibabatiza na ukuta kisha ikapotelea uvunguni.
NILISEMA MIMI KUWA HAPA HOSPITALI NINA MASHAKA NAPO, ONA SASA NA HUWENDA KUKAWA NA MAKUBWA ZAIDI? MH! HEBU NGOJA TUONE.
Abasi Mgizu alitambulika kwa jina hilo akiwa kama mwandishi wa habari wa gazeti la serikali. Alan alirudi nyuma huku akiwa makini na kuufunga kabisa ule mlango. Kitendo kile kikawa kimesababisha sintofahamu kwa yule jamaa hivyo kwa kasi ya ajabu akaupindua mto na kutoka na bastola hata hivyo bastola ile haikupata makazi ya kudumu kwenye mikono yake, kwa kasi ya umeme Alan ajizungusha na teke kali ambalo liliupiga mkono uliokamata bastola na kuitupilia ukutani ambako ilijibabatiza na ukuta kisha ikapotelea uvunguni.
SONGA NAYO….
“Mbona unanipa mashaka rafiki yangu inamaana hutaki rafiki humu ndani unapenda kuwa mwenyewe tu. Nimekuja kukujulia hali kama kawaida yangu ya kupenda kufanya hivyo japo kuna habari huwa naokota humu hata hivyo ninapenda kutembelea wodi mbalimbali kuwapa salamu wagonjwa na kuwajulia hali…?”
“Muongo mkubwa…niambie wewe ni nani?” Alipayuka yule jamaa akiwa na hofu tayari baada ya kasi ambayo aliitumia Alan au Abasi Mgizu kama kitambulisho chake cha mwanahabari cha kughushi kinavyomtambulisha. Alan alikenua tabasamu huku akimuangalia yule jamaa kwa umakini mkubwa.
“Huyu mwanamke aliyetoka humu ndani ni nani?” Akauliza Abasi akilipuuza swali la yule jamaa.
“Yupi…? Huyu aliyetoka…? Ah! Si kama wewe tu ulivyoingia, mimi simjui alikuja kunijua hali…!” Alijibu huku akijitahidi kwa namna moja ama nyingine kuificha hofu yake hata hivyo iligoma kuondoka. Alijawa na hofu kuu.
“Usinifiche maana kunificha haitakusaidia kitu nataka kujua yule dada ni nani kabla sijakuuliza kuhusiana na Ua?” Aisee! Yule jamaa alichanganyikiwa waziwazi na kujikuta akimeza funda kubwa la mate ya hofu.
“Sijui…!” Alijibu hata hivyo alitoa sauti za maumivu baada ya Alan kumtandika ngumi moja nzito ya mwamba wa pua. Damu nyepesi zikaanza kumtoka puani. Akaanza kuhema kwa nguvu akiwa na hofu ya wazi kabisa.
“Natumai unajua, ninamaswali mengi sana rafiki hata hivyo yanategemea namna ambavyo utanijibu…!”
“Sina majibu mimi…!” Akajibu akiwa na hasira kali iliyokuwa ikimtetemesha mwili.
“Majibu ya maswali yangu unayo na ndiyo maana nikaja kwako, utanijibu tu japo inategemea na utakavyopenda unijibu.” Akasema Alan huku akiichomoa bastola yake toka kiunoni ambayo ilikuwa kwenye kiwambo cha kukinga sauti tayari. Mshtuko mwingine ukamkuta yule jamaa.
“Yule msichana ni nani?” Akauliza Alan akijifanya kutokuuona mshtuko wa yule jamaa.
“Ni mtu aliyekuja kunijulia hali kama wewe bwana mbona hunielewi…!” Alijibu kwa ukali yule jamaa huku ile sauti yake ya ugonjwa ikiondoka na kuwa na sauti halisi. Alan alimtandika yule jamaa teke moja kali sana la mbavu na kumnyooshea bastola barabara.
“Kuwa na huruma na mwili wako maana naona jinsi utakavyo kwenda kuumia pasipo sababu za msingi, sema tu ukweli. Jamaa alikuwa akilia kwa maumivu makali hata hivyo hakusema kitu. Alan akatazama saa yake tena akaona muda ambavyo ulikuwa ukimtupa mkono. Hakujua kama kitendo kile cha kutazama saa kilikuwa kikisubiriwa kama kosa kwa yule jamaa. Ghafula bila kutaraji Alan alimuona yule jamaa alijifyatua kutokea pale kitandani kama mshale na kumvaa kwa mapigo makali ambayo yalipelekea bastola ya Alan kuhama mikononi huku akikubali kupokea kichapo cha sekunde kadhaa kilichombabatiza na ukuta. Yule jamaa alikuwa mwepesi sana na mwerevu wa mapambano ya ana kwa ana hata hivyo Alan hakuwa na budi zaidi ya kupambana vikali na jamaa huyo. Jamaa aliendelea kumpa Alan mapigo makali ambayo yalimpa wakati mgumu kuyakwepa hata hivyo Alan naye alirusha ngumi yenye shabaha iliyompata jamaa mdomoni kiasi cha kumfanya agumie kwa ndani huku akitema damu baada ya pigo lile kumsababishia kujiuma mdomo wake kwa juu. Kitendo kile kikawa kimemchanganya yule jamaa na kuanza kumfuata Alan kama Mbogo. Hakufua dafu kwa mara hiyo alimkuta Alan akiwa imara zaidi. Ngumi mbili za mbavu zikamnyong’onyeza na ngumi moja ya tumbo ikampa kichefuchefu hata hivyo alizuiwa kutapika baada ya pigo kali lililotua kwenye koo lake akatapatapa hadi kitandani kwa mara nyingine anakuja kukaa sawa, bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti ilikuwa mikononi mwa Alan kwa mara nyingine na punde ikateuka risasi moja iliyolichangua goti la huyo jamaa.
“AAAAGH…!” Akapiga yowe kali la maumivu na kubingiliana akaporomokea chini ya kile kitanda.
“Nadhani umegundua kuwa sina utani sasa. Haya niambie yule mwanamke ni nani?” Akauliza Alan akiwa amemnyooshea bastola bado yule jamaa. Jamaa badala ya kujibu akaanza kucheka huku akilia kwa wakati mmoja alipokuja kunyamaza akasema;
“Niuwe tu, niuwe maana najua hutaweza kuniacha hai, niuwe ili uondoke hapa kabla hujakutwa maana utakufa bure…!”
“Unaongea upuuzi gani wewe…? Unadhani utakufa pasipo kuniambia chochote? Sahau, lazima unijibu maswali yangu niliyokuuliza ndipo ufe…!”
“Siwezi kusema chochote na unajisumbua sana kupambana na hawa jamaa, usidhani unapambana na kikundi kidogo cha panya ambacho kinaweza kusambaratishwa na wewe kinda dogo kabisa la paka. Huu ni mtandao mkubwa sana ambao unamalengo maalumu hapa nchini na malengo yake hayawezi kufumbuliwa kirahisi na Ngedere wa kufugwa kama wewe.” Akasema yule jamaa huku akiugulia maumivu. Alan akamtazama huyo jamaa huku akiyafikiria maneno yake kwa upana zaidi. Yalikuwa na ukweli wowote ama? Akajiuliza akilini hata hivyo akaona kumbe huyo jamaa anaweza kumueleza mengi kama atambana vizuri.
Hakujua Alan, hakujua hata kidogo.
“Kwahiyo huo mtandao unahusiana vipi na wewe sambamba na yule mwanamke au…!” Hakufika mwisho wa sentensi yake Alan kwani yule jamaa alijitikisa kidogo tu kisha kwa kasi kubwa akachomoa kisu kutoka kiunoni hata hivyo hakufanikiwa kukirusha risasi moja ikapenya kwenye kifua chake upande wa moyo na kumfanya atapike damu. Lilikuwa ni shambulio la ghafula sana ambalo Alan hakulitegemea ambalo pengine lingemletea madhara makubwa sana. Akamtazama kwa ghadhabu ya kutokupata chochote kutoka kwake. Hakika akaona jinsi kazi yake itakavyokuwa ngumu kwani mwanzo wake tu ulikuwa mgumu kiasi hicho. Hakujua nini kingetokea kama huyo jamaa angemruhusu kukirusha hicho kisu na kuingia mwilini mwake, bado alikuwa akiikumbuka sumu iliyoyaondoa maisha ya maafisa wale wa jeshi. Umakini kwake lilitakiwa kuwa ni jambo la kwanza kabla ya yote na hivyo ndivyo ilivyokuwa, risasi yake ilifanikiwa kuwa na kasi kuliko kisu na ikafanikiwa kumzima huyo jamaa mgonjwa.
“Kufa tu maana kifo ulikitaka, nadhani nitapata mengi nikimpata yule malaya mwenzako.” Aliongea kwa ghadhabu ya wazi kabisa Alan. Akampindua yule jamaa na kumpekuwa kwenye mifuko ya suruali, hakukuta kitu hata kimoja, akageuza mito na kutazama chini ya godoro pia patupu. Akaichukua ile simu na kuitoa ile bastola iliyoangukia uvunguni na kuichunguza. Ilikuwa ni bastola aina ya Gsh-18 iliyobeba risasi tatu tu. Alimtupia bastola yake akaitia ile simu mfukoni akiwa na lengo la kuondoka nayo. Hata hivyo wazo la kuwa azipekuwe zile droo likamjia. Akaanza na droo za upande ule wa kulia, alizipekuwa zote hata hivyo hakuambulia kitu. Akarudi kwenye hizi droo za pembeni ya kitanda alichokuwa kalalia huyo jamaa nazo zilikuwa tupu ila wakati anazirudishia, kukaanguka kipande kidogo cha karatasi ambacho kilikuwa cheupe kisichoandikwa kitu kwa upande wa juu. Akakitazama kwa kitambo kifupi kabla ya kukiokota na kukigeuza. Alishangaa Alan, upande mmoja wa ile karatasi hakukuwa na maandishi ya aina yoyote ile zaidi ya Ua moja dogo lililochorwa vizuri lenye rangi kama ya pinki hivi. Ua hili lilikuwa likijulikana kwa jina la Bee Balm (Bee Balm flower). Alilitazama sana hili uwa na hakujua sababu ya kuwepo mahala pale. Kila alivyojaribu kuunda matukio kichwani mwake alishindwa kuelewa, alilitia mfukoni mwa suruali yake na kutoka mule wodini akiurudishia ule mlango. Alizirusha hatua zake hadi ilipo ofisi ya wauguzi huku mawazo ya kufikiria namna ya hawa watu walivyoweza kupata nafasi kwenye Hospitali hii hadi kupewa chumba cha kulazwa huku kukiwa hakuna mgojwa, yakijijenga kichwani mwake upya. Alipofika kwenye ile ofisi alipiga jicho moja ndani ya ile ofisi na kumuona muuguzi mmoja akiwa amevaa mavazi yake ya kazi akivua glovu za mipira na kuzitupia mezani. Alikuwa akitoka kutoa huduma kwa wagonjwa waliomo kwenye wodi nyingine za jengo hilo, aliitazama ile korido ambayo ingeweza kumtoa nje kisha akatazama alikotoka, kulikuwa kutupu hakuna mtu wa aina yeyote. Akausukuma mlango na kuingia ndani ya ile ofisi ya wauguzi, yule muuguzi wa kike akashtuka sana na kumtazama Alan usoni akiwa na sura yenye tashwishi.
“Habari yako dada?” Alisalimia Alan akiwa anamtazama muuguzi huyo usoni.
“Salama, vipi unahusika na humu ndani?” Alijibu salamu yule dada huku akiwa anamtzama Alan usoni bado.
“Hapana, ila niko na shida muhimu inayohitaji msaada wako.”
“Kwanini usingeizungumza shida yako ukiwa hapo dirishani na ukaamua kuingia moja kwa moja humu ofisini ni hatari sana hii na ni kinyume na utaratibu wa kawaida unaweza hata kuniharibia kibarua changu.”
“Najua…!” Alan alijibu akiwa na tabasamu huku utulivu ukiwa kwa kiasi kikubwa sana moyoni mwake. Akaendelea.
“…namuulizia mgonjwa wa wodi ya mwisho yaani wodi namba nne…?”
“Nimekuona unatokea huko ni ndugu yako au yuko na shida inayohitaji msaada wa haraka?”
“Hapana, hayuko na shida yoyote…!”
“Ila…?”
“Uko na taarifa za yule mgonjwa tangu amefikishwa hapa?” Aliuliza Alan. Hili swali likamfanya yule muuguzi kumtazama Alan kwa macho ya mshangao yenye alama ya kuuliza.
SOMA HADI MWISHO ILI UJUE NAMNA YA KUMUUNGA MKONO MWANDISHI.
“Najua…!” Alan alijibu akiwa na tabasamu huku utulivu ukiwa kwa kiasi kikubwa sana moyoni mwake. Akaendelea.
“…namuulizia mgonjwa wa wodi ya mwisho yaani wodi namba nne…?”
“Nimekuona unatokea huko ni ndugu yako au yuko na shida inayohitaji msaada wa haraka?”
“Hapana, hayuko na shida yoyote…!”
“Ila…?”
“Uko na taarifa za yule mgonjwa tangu amefikishwa hapa?” Aliuliza Alan. Hili swali likamfanya yule muuguzi kumtazama Alan kwa macho ya mshangao yenye alama ya kuuliza.
SONGA NAYO….
Swali hili hakuwa akiliwaza kama angeulizwa maana ni kweli tupu kuwa tangu mgonjwa yule amefikishwa pale hakuwahi kuruhusiwa kuingia mule ndani ispokuwa kulikuwa kukiingia dokta mmoja tu ambaye alikuwa ni mganga mkuu wa hiyo Hospitali.
“Hapana sina taarifa zake…!” Alijibu akiwa na wasiwasi mkubwa na hakumuelewa kabisa huyo kijana ni kwanini amemuuliza swali kama hilo.
“Wakati ukiwa unaingia zamu, hukuwa ukienda kumuhudumia?” Alizidi kuhoji Alan.
“Hapana, huwa tunapewa maelekezo ya wagonjwa wote wanaotakiwa kuhudumiwa ila huyo sikuwahi kupewa maelezo yake.” Alijibu yule muuguzi. Alikuwa mrefu mweupe aliye zilaza nywele zake kwa nyuma, macho yake madogo yanayo ng’aa yaliongeza ziada ya urembo wake aliojaaliwa na muumba. Alan alinyanyua mkono uliobeba saa kisha akatoka mule ndani na kusimama dirishani, wakati anasimama hapo dirishani akapita muuguzi mmoja ambaye alinyoosha moja kwa moja akiifuata ile korido na kwenda kuingia kwenye wodi ya pili kutoka pale upande wa kushoto. Alan alimtazama alipoona amepotelea ndani ndipo akamtazama yule muuguzi.
“Ni kawaida kuzuiwa kutoa huduma kwa baadhi ya wagonjwa?” Akamuuliza. Yule muuguzi akasita kujibu kisha akainamia karatasi moja iliyokuwa na maelezo ya dawa ambayo alitakiwa kumpatia mgonjwa kisha akayainua macho yake na kumtazama huyo kijana.
“Kwani wewe ni nani unayeuliza haya…?” Hatimaye yule muuguzi aliamua kuuliza. Alan akatabasamu kidogo huku akiwa anajua alibakiwa na muda mchache sana wa kukutana na Maisara kule kwenye chumba cha Hoteli ya Maua Inn muda wa saa saba adhuhuri. Alikuwa ameshakula muda wa kutosha sana.
“Mimi ni mwandishi wa habari huwa naandika makala mbalimbali ambayo kabla ya yote huwa nafanya kwanza uchunguzi. Kuna matatizo mengi huwa yanajitokeza hasa kwa wagonjwa mbalimbali hivyo ni wajibu wetu kama wanahabari kuhakikisha matatizo hayo yanakuwa bayana na jamii inajua. Nina siku tatu tangu nifike hapa nikichunguza habari fulani ambayo ningependa kuiandikia makala hata hivyo huwa napata fursa ya kutembelea wagonjwa na kuwajulia hali huku nikiwapa pole. Siku zote nikiwa hapa nimeona wauguzi wakijishughulisha na kuingia kwenye wodi zote isipokuwa wodi namba nne. Hii imenijengea maswali mengi sana na nilijaribu kuwauliza baadhi ya wauguzi hata hivyo hawakunipa ushirikiano wa kutosha sijui kwanini wanakuwa wazito kutoa ushirikiano kuhusiana na hili linalohusu afya ya mtu. Nimeona wewe uko tofauti na wengine, ni mpole, na pengine usiye na makuu hivyo nikatamani kuuliza japo machache hivyo nategemea huwezi kuniangusha.” Alan aliamua kutumia uwongo mwingi sana ili kuweza kumuingiza yule dada kwenye nafasi aitakayo. Hakika alifanikiwa hata hivyo muuguzi yule alikuwa na wasiwasi mkubwa na kila wakati alikuwa akitazama saa yake ya mkononi. Alan alikuwa ni jasusi mjuzi na anayejua alama nyingi za hatari hivyo kwa muonekano huo wa huyo binti alijua fika ipo sababu ya kuwa hivyo.
“Unahitaji kwenda kutoa huduma kwa wagonjwa?” Akabadili swali Alan huku akijua hilo wala halikuwa chanzo cha huyo binti kuwa hivyo.
“Yaa, ndiyo, ndiyo…! Nina wagonjwa wananisubiri na muda unakimbia sana.” Alijibu yule muuguzi. Jibu lake lilipwaya kuonesha kuwa halikuwa jibu la kweli bali alisumbuliwa na jambo fulani kichwani mwake. Alan alitumbukiza mkono mfukoni na kutoa kadi ya biashara inayomtambulisha kama muandishi wa habari ambayo ilikuwa na namba za simu na baadhi ya taarifa za kughushi.
“Unaishi wapi kwa hapa mjini?” Aliuliza Alan akiwa mpole sana huku tabasamu la kumvunja binti yoyote nyonga likiwa usoni mwake. “Kuwa huru tafadhali hakuna ubaya kukufahamu.” Akaongezea.
“Naishi Makorora nyumba namba 120, ni nyumba iliyopo barabarani na inatazamana na duka moja kubwa la vyakula la Mpemba.” Alijibu yule dada huku akikichukuwa kile kikaratasi alichopewa na kukitia kwenye mfuko wa vazi lake la kiuguzi.
“Unaitwa nani?”
“Naitwa Zaituni.”
“Asante Zaituni, naweza kuwa mgeni wako leo usiku au kuna shemeji na haitafaa mimi kukutembelea usiku wa leo?” Alichombeza Alan huku akizidisha tabasamu ambalo lilizidi kuziharibu hisia za Zaituni na kwa namna moja ama nyingine akiiona hofu aliyokuwa nayo moyoni ikiyeyuka na kumuacha umbali mrefu, pumzi nyingi zikamshuka akatabasamu katika namna ya kuwa na matumaini.
“Hakuna mtu wa kunizuia nisipokee wageni wangu, unaweza kuja wakati wowote na unakaribishwa sana. Ukija usiku kwa wiki hii ni sawa tu maana natoka hapa kazini saa mbili usiku hivyo kuanzia saa tatu nakuwa nyumbani hii ni hadi juma pili ndio nabadilisha zamu.” Alieleza kwa undani Zaituni. Alan akamshukuru na kumuaga akimuahidi kumtembelea au anaweza kumpigia simu kama ataona anachelewa kufika kwake. Waligana.
Hakukutana na yule mwanamke tena wala hakukuwa na dalili zake, njia zote alizopita zilikuwa nyeupe kabisa hii ilimfanya kujenga mashaka makubwa sana kwake na pengine ingempa wakati mgumu kuweza kumpata yule dada ambaye aliamini angeweza kumpa maana ya lile Ua ambalo alilikuta kwenye zile droo mule wodini. Hata hivyo wazo hilo la kumtafuta huyo dada akaliondoa kichwani mwake mara tu alipokumbuka kuwa alikuwa na simu ya yule jamaa aliyemuangamiza kule kwenye wodi za Cliff. Akapata nguvu mpya akiamini ni lazima yule mwanamke angepiga simu kwani kupitia mazungumzo yao aliweza kuamini kurejea kwake kama alivyosema anakwenda kumuita Daktari kwa ajili ya kuangalia afya ya mgonjwa wake kama imetengemaa kisha atarejea baadaye. Hata hivyo hakumuona akirejea hadi anatoka kwenye lile jengo. Alikuwa akiifuata njia ambayo ilikuwa ikimpeleka yalipo maegesho ya magari. Alipofika akatoa kikasha cha funguo na kuchagua funguo moja akaizamisha kwenye kufuli la mlango la Toyota Harrier. Loki ya mlango ikaachia akaufungua na kuingia ndani ya ile gari. Alijituliza kwa muda huku akiichunguza ile gari ambayo aliwekewa hapo kwa ajili ya shughuli zake. Gari ilikuwa salama kabisa isiyo na shaka lolote na ilionekana kuwa nzima kabisa. Alitazama nje kupitia vioo vya gari ile ili kuona kama angeweza kumuona yule msichana akirandaranda hata hivyo kulikuwa kimya sana. Alikata shauri na kuamua kuwasha gari na kuondoka mahala hapo hata hivyo alichelewa kidogo kufanya maamuzi. Mtetemo wa simu kutokea kwenye moja ya mifuko yake ya suruali ikamgutusha. Akaitoa ile simu na kuona jina la mtu aliyekuwa akipiga kwenye ile simu ‘Bee Balm’. Loh! Lilikuwa ni jina la lile Ua. Akajilaumu sana kwa kutokuipekuwa hiyo simu na kuona ina nini. Damu zikamkimbia Alan na nywele kumsimama. Akili yake ikafanya kazi ya haraka akajua kuwa yule huwenda alikuwa ni yule mwanamke. Akaipokea ile simu kisha kuiweka sikioni na kusikiliza ili kujua kama sauti itakayozungumza ni ya kiumbe wa aina gani. Mtu wa upande wa pili wa simu naye hakuzungumza chochote ni kama alishtukia mchezo uliokuwa ukichezwa.
Walitegeana.
Hali ya kutegeana ilidumu kwa muda mfupi sana huku kilichokuwa kikisikika ni sauti ya upepo na mikwaruzo mingine ya mpapaso wa simu hata hivyo hakukusikika kitu kingine hadi pale mtu wa upande wa pili alipoikata ile simu.
“Pumbavu kabisa huyu!” Alitukana Alan akiwa anahakika huwenda yule mwanamke amejua kitu tayari. Kwanini alikuwa haongei? Au kulikuwa na namna ya walivyojiwekea utaratibu wa kuzungumza na yeye hakujua? Aliwaza sana Alan hata hivyo haikusaidia kitu. Alikwama kuweza kumjua mpigaji. Akajaribu kuipiga ile namba hata hivyo ilileta majibu ya kukera ikidai kuwa namba ile imefungiwa kabisa. Akapiga ngumi kwenye Dashi bodi ya gari yake kwa ghadhabu kisha akaliwasha gari mara baada ya kukumbuka miadi yake na Maisara kule hotelini kwake. Akaondoka.
Ilikuwa imeshatimu saa saba na dakika tano wakati Alan akiwa anawasili kwenye maegesho ya magari ya Maua Inn Hoteli. Aliegesha gari lake na kuteremka. Hakutaka kuonekana kwa wepesi kuwa amefika hapo akiwa na gari, aliingia kwenye ukumbi wa Hoteli ile na kuukagua katika namna ya kumtafuta mtu hata hivyo hakuona sura ya mtu anayemfahamu, sura zote zilikuwa ngeni kwenye mboni za macho yake. Hakusubiri kutokana na kuwa na uhakika wa kupigiwa simu kama mtu huyo angefika hapo mapema, akapiga hatua mbili kisha akasita kujishauri kama aendelee na safari ya kuelekea chumbani kwake ama arudi ukumbini amsubiri Maisara. Akiwa anajishauri namna ya kufanya, simu yake ya mkononi ikaita akaitoa ba kutazama mpigaji. Ilikuwa ni namba mpya iliyokuwa ikimpigia. Akaipokea na kuiweka sikioni.
“Jabir Azakia!” Iliita sauti ya kike upande wa pili wa simu katika namna ya kutania.
“Nipe habari Maisara?” Akaitika Alan ikiwa ni baada ya kuikumbuka sauti ya mpigaji wa simu hiyo.
“Nimechelewa sana mpenzi kuna kazi zimenibana sana kiasi kwamba hadi sasa siwezi kufika kwenye miadi yetu, najisikia vibaya sana kwenda kinyume na makubaliano hata hivyo natumai unajua shughuli zetu zilivyo, kazi zinakuja ukiwa huna matarajio.”
“Najua najua, usijali Maisara nayafahamu vizuri sana mambo ya kazi hasa hizi ambazo ni za kusafirisha watu unaweza usimpate mteja pale unapotegemea kumpata kila siku na akaja wakati ambao hukudhani.”
“Nisamehe sana mpenzi wangu…unisamehe mno.” Aliomba sana radhi Maisara kisha akaahidi ifikapo usiku watakuwa wote.
“Nimechelewa sana mpenzi kuna kazi zimenibana sana kiasi kwamba hadi sasa siwezi kufika kwenye miadi yetu, najisikia vibaya sana kwenda kinyume na makubaliano hata hivyo natumai unajua shughuli zetu zilivyo, kazi zinakuja ukiwa huna matarajio.”
“Najua najua, usijali Maisara nayafahamu vizuri sana mambo ya kazi hasa hizi ambazo ni za kusafirisha watu unaweza usimpate mteja pale unapotegemea kumpata kila siku na akaja wakati ambao hukudhani.”
“Nisamehe sana mpenzi wangu…unisamehe mno.” Aliomba sana radhi Maisara kisha akaahidi ifikapo usiku watakuwa wote.
SONGA NAYO….
Walimaliza kuongea na simu kukatika. Alan aliachana na mawazo ya kukutana na Maisara kwa wakati huo tena, alichoamua kukifanya ni kuutumia muda huo kuitafakari kazi iliyoko mbele yake. Alimfikiria yule jamaa aliyepambana naye kule hospitalini kisha kumuondosha. Mapambano yake na yule jamaa yalimpa picha kuwa watu ambao anapambana nao hawakuwa watu wadogo. Iweje waweke watu wanaojua kupambana wafanye uchunguzi dhidi ya madaktari wale na ni ipi sababu? Aliwaza Alan kwa kina sana. Jibu alilolipata lilikuwa ni la dhani kwani hakukuwa na uhakika wa moja kwa moja hata hivyo hakulipuuza jibu lake. Aliamini huwenda kulikuwa kuna mpango siri ambao hawa jamaa walikuwa wanapanga kuufanya hapa nchini. Pia aliyakumbuka maneno ya yule jamaa wakati walipokuwa wakifanya mahojiano. Hasa pale aliposema kuwa hataweza kupambana na watu wale hata kidogo ambao wamejizatiti kila kona ya jiji hili. Kauli hii ya yule jamaa ilikuwa si ya kupuuzwa hata kidogo. Alipomaliza kutafakari juu ya hayo, aliachana na mawazo hayo kwa kuwa hajaona hatua ambayo alipiga, hatua yake imeishia njiani ikiwa butu. Mtu pekee wa kumjuza mengi alikuwa ni yule mwanamke hata hivyo wakati mwanamke yule anapiga simu hakuwa muongeaji zaidi ya mtegeano. Hadi hapa Alan alichoka kiakili. Alikuwa amejituliza ndani ya chumba chake cha Hoteli ukimya ukiwa mkubwa sana. Alitafakari mengi akayaacha baada ya kutokumpa ufumbuzi wowote. Akawaza hili na lile hadi alipomfikiria marehemu Leous Mipango aliyeuawa kinyama hotelini. Kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango ndicho kilichomfanya yeye kufika hapa jijini hivyo ilikuwa ni lazima aujue undani wa kifo hicho ili ajue anapeleleza kesi ya namna gani. Aijue kwanza familia yake, mahali alipokuwa akiishi na mitaa aliyokuwa akipenda kutembelea. Kwanza kabla ya yote ni kujua mahali alipokuwa akiishi, angepajuaje? Hilo ndilo swali alilokuwa akijiuliza. Hata hivyo hakungoja sana, alishapata wazo akilini mwake na hakuona sababu ya kuendelea kukaa hapo chumbani kwa masaa mengine zaidi. Alitoka kwa hatua za taratibu akakifunga chumba chake vizuri kisha akatoka hadi nje ya Hoteli ile. Hali ya hewa ilikuwa ni ya mawingu kiasi, jua lilifichwa kwa namna fulani na kusababisha joto kali. Kilikuwa ni kipindi cha mvua za vuli hivyo isingestaajabisha hali ile kubadilika na kuwa ya mawingu mazito. Njaa ilikuwa ikimsumbua sana kwa majira hayo na kila akifikiria muda ambao alikula hakukumbuka zaidi ni kwamba aliahidiana na Maisara kukutana kwenye ukumbiwa wa chakula wa Maua Inn Hoteli na kutokutokea kwake ikawa imeharibu hata ratiba yake ya kula. Aliwasha gari yake akaliondoa taratibu maegeshoni hapo akiifuata barabara ya nane kisha akaja kuikamata barabara ya Taifa ambayo ilikuwa inakwenda hadi kituo cha zamani cha mabasi, bado mwendo wake ulikuwa ni wa taratibu sana hadi alipofika karibu na kituo hicho cha mabasi zamani, akapunguza mwendo wa gari yake baada ya kuvutiwa na gazeti moja kwenye ubao wa muuza magazeti. Akaliegesha gari lake pembeni kidogo mwa barabara hiyo kisha akateremka akalifuata na kulinunua. Akarudi garini na kuondoka hadi alipoufikia mzunguuko wa barabara wa Mabanda ya papa akazunguuka hadi alipoikamata barabara iliyokuwa ikielekea ilipo ofisi ya mkuu wa mkoa. Alikanyaga mafuta kwa mwendo wa wastani akaja kuegesha gari lake nyuma kidogo ya kiwanda cha utengenezaji wa samani mbalimbali cha Burhani au mkabala na ofisi ya mkuu wa mko. Alitazama usalama wa hapo na kule alikotokea kote kulikuwa kimya hakukuwa na dalili zozote za kufuatiliwa. Alan alipaona mahala hapo panamfaa kuweka kikao cha muda mfupi kwa kuwa hapakuwa na kelele nyingi na pia hapakuwa na usumbufu wa ufuatiliaji wa uegeshaji wa magari. Mbele yake hatua kama tatu za mtu mzima kulikuwa na mama mmoja wa kimasai akiwa anauza dawa za asili na shanga hivyo hivyo kwa upande wa nyuma yake halafu kwa mbali kutokea hapo kulikuwa na kijana mwingine wa kimasai akiwa anauza viatu na upande wa pili wa barabara kukiwa na maskani moja ya vijana ikiwa imepangiliwa matairi kama vikalio. Aliporidhishwa na uchunguzi wake huo, alilitoa lile gazeti na kulifungua ukurasa wa tatu ambako kulikuwa na habari ambayo ndiyo iliyomvutia kuweza kulinunua gazeti lile. Habari hiyo ilikuwa ni ya kifo cha Luteni Jenerali Leos Mipango. Si kama alitaka kujua namna alivyouawa lah! Alichotaka kukijua kwa wakati huo ni wapi mtu huyo alikuwa akiishi. Ilikuwa ni habari ndefu iliyojaa dhania nyingi huku sehemu chache zikiwa na ukweli. Luteni Jenerali alikuwa na familia ya mke na watoto watatu; wakike walikuwa wawili na wa kiume mmoja. Aliishi maeneo ya Nguvumali. Hii ndiyo ilikuwa habari aitakayo hata hivyo bado kulikuwa na kazi nyingine ya ziada kwani Nguvumali ilikuwa kubwa kujua mahali alipokuwa akiishi huyo mtu ilikuwa ni kazi kubwa sana na hakuamini kama mtu mkubwa kama yule angekuwa akiishi aina moja ya maisha lazima kuna utaratibu wa kimaisha ambao ulikuwa ukimhusu. Aliwasha gari na kuitia barabarani kwa kasi kubwa huku lile gazeti akilitupia kwenye kiti cha pembeni. Akaongeza mwendo wa gari yake akaiacha barabara ya Chuda akanyoosha na kuipita reli hadi mzunguuko wa Kwaminchi akaishika barabara ya Mombasa. Alinyoosha na barabara hiyo hadi alipoukuta msikiti wa hapo Kwaminchi akaupita kisha baada ya mwendo mfupi akakunja kushoto akiifuata barabara iliyokuwa ikielekea Kisosora. Mbele kidogo akaiacha barabara hiyo na kuishika ile ya Nguvumali. Haukuwa mwendo mrefu sana punde alikuwa New Kwetu Hotel Nguvumali. Akapita mitaa ile na hii akaja kusimama kwenye kibanda kidogo cha kuuzia mbogamboga, kabla ya kutoka garini alilichunguza kwanza hilo eneo aliporidhika nalo ndipo alishuka na kutembea kwa mwendo wa miguu akipita hapa na pale. Isingempa tabu kuifahamu nyumba ya Luteni Jenerali Leous Mipango kwa kuwa kipindi hiki kilikuwa ni kipindi cha msiba japo alikuwa na taarifa zote kuwa mwili huo usingefikishwa nyumbani kwake bali ungesafirishwa hadi Handeni ambako ndiko kwenye chimbuko lake. Alitaka kufahamu tu nyumbani kwake kwanza ili aweze kujua namna ambavyo angeichimbua sababu au kile kilichopelekea kifo chake.
ITAENDELEA
Simulizi : Mikono Ya Jasusi
Sehemu Ya Nne (4)
Hatua za Alan zilimfikisha kwenye maskani moja ya fundi pikipiki, akawasabahi vijana aliowakuta hapo na kumuamkua mzee mmoja kati ya vijana wale kisha akaketi kwenye fomu moja akiwa karibu kabisa na yule mzee.
“Mzee wangu habari za hapa?” Alan aliukusanya muda kwa kuendeleza maamkizi ya kiswahili.
“Habari za hapa ni nzuri kabisa kijana wangu sijui za huko utokako?” Yule mzee naye akaijibu salamu ile kwa ukarimu mkubwa; hii ndiyo raha ya u-Tanzania. Salamu hanyimwi mtu.
“Aah! Mimi ni mgeni mzee wangu…!” Akaendelea Alan kisha akaweka pozi dogo la tafakuri kishapo akaendelea.
“…ni mgeni na nilikuwa nauliza nyumba ambapo upo msiba wa yule jamaa aliyekuwa mwanajeshi…!”
“Nyumba ya msiba ya jamaa aliyekuwa mwanajeshi…?” Mzee akainukuu kauli ile kwa mshangao wa kuuliza.
“Ndiyo,” Alan akajibu huku akiwa makini na macho ya mzee yule ambayo yalikuwa mekundu kiasi huku jicho moja likinyemelewa na tongotongo kutokana na ubovu wa macho ya kiutu uzima.
“Kwani wewe unatokea wapi hadi usimjue mtu huyu maarufu, alikuwa ni mwanajeshi kweli tena mwenye cheo kikubwa jeshini…alikuwa Luteni Jenerali, ndiyo. Hata hivyo hakuwa mtu wa majivuni, aliwapenda sana vijana wa hapa tangu kuhamia kwake hapa Nguvumali. Nashangaa kuwa humfahamu labda kama si wa hapa mjini Tanga…ni wa wapi wewe?” Akauliza yule mzee huku akiliweka sawa vazi lake la saruni.
“Huwezi kuamini mzee wangu naishi hapahapa mjini hata hivyo sikuwa nikizijua kwa undani sifa za huyu bwana.” Alijibu Alan huku akijenga ukaribu na huyu mzee kwa kuangua kicheko kidogo. Kabla yule mzee hajaendelea na mazungumzo alipita bwana mmoja akiwa na birika lake la kahawa na kashata. Alan akamuuliza yule mzee kama ni mtumiaji wa kahawa. Mzee yule akasema hakuna mwenyeji wa pwani halafu akawa si mpenzi wa kahawa. Ilimbidi Alan ampungie mkono yule kijana asogee mahala pale. Alikuwa na uzoefu mkubwa na wazee wa mkoa huu kwanza walipenda sana kujipa sifa ya u-alwatani, wajuaji wa mambo na watu wa kujikweza na ilhali pengine hawana kitu aghalabu ni watu wa kushinda vijiweni tu. Kijana yule alisogea na kutakiwa kuhudumu, bwana mwingine naye alisogea baada ya kuona pananyweka naye akajumuishwa kwenye huduma ile huku yule kijana akitakiwa kulichochelea mkaa birika lake kwani bado watu hao walikuwa katika uhitaji wa kinywaji hicho.
“Kijana…!” Akaanza yule mzee. “…unahusiana vipi na marehemu…?” Akauliza, hili lilikuwa ni swali la kidadisi.
“Bwana mkubwa una kashata?” Alan akamuuliza muuza kahawa lengo lake si kwamba anywe kahawa na kasha lah! Lengo lake kuu lilikuwa ni kulipotezea lile swali la yule mzee na kujifanya hakuwa amelisikia.
“Ndiyo ninazo ziko humu kwenye mfuko.”
“Wazee kuleni na kashata msiwe na shaka lolote.” Akasema Alan na wazee wakajisevia huku akichomekea na swali hapo hapo.
“Umesema ni mtu anayefahamika sana hivyo msiba wake utahusisha watu wengi sana na hapo kwake hapata tosha?”
“Mmh! Unadhani msiba uko hapa Nguvumali, wapi! Msiba umesafiri yule bwana chimbuko lake ni Uziguani. Vijana ni wengi sana waliokwenda hata hii maskani imepwaya sana wengi hapa wamekwenda kwa kutumia gari ya kukodi.”
“Aisee! Kweli, hata hivyo kifo chake ni tata sana mzee wangu unajua huku kuachiwa kwa wanajeshi kuishi mitaani na raia nako si kuzuri sana?”
“Sanaa, sana na wala si kidogo…!” Walijibu kwa pamoja.
“Inakuwaje kwa mtu kama yule…?” Alan akauliza huku akiacha mtego mbele. Alikuwa akiwatazama wazee wale kwa macho ya udadisi.
“Unajua yule bwana alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana na huwa akitoka kazini nyakati za jioni au mwishoni mwa juma hakosi kunitembelea…!”
“Ndiyo…!” Alan alidakia huku akijiweka sawa na kumtazama yule bwana aliyejisogeza baada ya kuona kunanyweka. Alikuwa akikitua kikombe chake cha kahawa kikiwa kitupu na tayari alishamimini viwili kinywani mwake chapuchapu kama yu kwenye ligi hata hivyo alivutiwa sana na maongezi ya huyu bwana. Wakati yule muuza kahawa akikimimina kahawa nyingine, yule bwana akaendelea.
“…kifo chake kimesababishwa na mwanamke yule bwana wazi kabisa…!”
“Wee!” Alan akaonekana kushtuka hata hivyo yule mzee alikuwa mkavu kabisa akiendelea kumumunya kahawa na kubendua kipande cha kashata na kukitafuna.
Alikuwa akikitua kikombe chake cha kahawa kikiwa kitupu na tayari alishamimini viwili kinywani mwake chapuchapu kama yu kwenye ligi hata hivyo alivutiwa sana na maongezi ya huyu bwana. Wakati yule muuza kahawa akikimimina kahawa nyingine, yule bwana akaendelea.
“…kifo chake kimesababishwa na mwanamke yule bwana wazi kabisa…!”
“Wee!” Alan akaonekana kushtuka hata hivyo yule mzee alikuwa mkavu kabisa akiendelea kumumunya kahawa na kubendua kipande cha kashata na kukitafuna.
SONGA NAYO….
“Alaa! Nakuambia tena…!”
“Kivipi yaani?” Alisema yule bwana na Alan akadakia kwa swali.
“Pamoja na kuwa yule bwana alikuwa na mke na watoto hata hivyo alikuwa hajatulia, alikuwa kicheche mno. Vibinti vidogo na wanawake wa marika tofauti hakuacha kuwasarandia, sasa wanasema tabia ikikua hukuza kidonda. Bwana akapata mwanamke mmoja mzuri sana huyu ndiye aliyemuondoa.”
“Unataka kuniambia mwanamke ndiye amefanya yale maana kifo chake wanasema ni cha kupigwa risasi sasa mwanamke atawezaje?” Alizidi kuukusanya muda Alan huku kichwani mwake kukiwa na mvurugano mkubwa sana hasa baada ya kusikia kuwa mwanamke ndiye aliyefanya balaa lile. Haraka sana moyo wake ukapiga kwa kasi baada ya ubongo wake kuruka alipomkumbuka yule mwanamke kule Bombo Hospitali. Hakika maneno haya aliyokuwa akiyaongea huyo mzee yalikuwa na ukweli ndani yake alijipa utulivu kusikiliza.
“Yule bwana hakuwa akinificha kitu na ndiyo maana nimejua haya…!”
“Anayokuambia huyo bwana si uwongo, bwana yule hata mimi alikuwa akitaka ushauri sana hasa akimtaka binti hapa mtaani. Pabaya nilimtahadharisha ila pazuri nilimwambia awe makini kwa kuwa dunia ya leo si enzi za ukuaji wetu.” Yule mzee alidakia na Alan akatulia zaidi kuweza kusikiliza.
“Hazikuwa siku nyingi tangu aliponiambia amepata chombo kikali sana na amekielewa.” Yule bwana alisema akatua kidogo akinywa kahawa na kumega kashata akasendelea. “…alisema kuwa huyo mwanamke ni balaa kwa urembo na amempenda mno. Sikuwa nikishangaa kwa kuwa tabia zake nazijua. Siku tatu kabla hili halijatukia akaniambia anataraji kutoka na yule mwanamke mwishoni mwa juma hivyo huwenda mimi naye tusionane. Basi ikawa hivyo hatukuonana kweli hadi napokea taarifa ya kifo chake na ni mwishoni mwa juma hilohilo unadhani ni nani aliyehusika.” Aliongea bwana huyo.
“Daah! Kweli ukistaajabu ya Musa utachoshwa na ya Firauni, dunia tambara bovu jamani hadi wanawake wanakuwa na roho za kinyama namna hii…hakuwahi kukuambia jina la huyo mwanamke?” Aliongea Alan kisha akauliza mwishoni huku akikisogeza kikombe chake cha kahawa kwa muuzaji ili aongezwe. Yule bwana akaguna mh! Akiwa anapiga funda dogo la kahawa ile ya moto aliyotoka kuongeza punde. Akakitua kikombe na kuvuta kimya akitafakari.
“Isabela…! Alisema msichana huyo anaitwa Isabela nakumbuka aliniambia. Hakuniambia jinsi alivyo na wala sikumuuliza sana maana angeniona mchimbifu sana wa mambo yake na unavyojua tabia za wanajeshi tena.”
“Ndiyo.” Alan alijibu huku lilile jina akilihifadhi kwenye memori ya ubongoni mwake. Waliendelea kuongea lile na hili huku akiwa tayari ameoneshwa nyumba hiyo ilipo hata hivyo alisema hakuna sababu ya kwenda wakati msiba haukuwepo hapo. Alan aliuliza kiasi cha pesa anachodaiwa akaambiwa ni shilingi elfu mbili na miatano. Alitoa waleti yake iliyotuna na kutoa noti ya shilingi elfu tano akamkabidhi yule bwana kisha akarudishiwa shilingi elfu mbili na ile mia tano akiiacha wazee wale waweze kuimalizia. Aliwashukuru wale wazee na kuondoka huku wazee wale wakimtakia baraka nyingi kwa kuweza kuwanunulia kahawa.
Alan alitembea kwa mwendo wa miguu kurudi mahali alipoegesha gari yake kichwani mwake jazanda kubwa la kile alichokipata pale kwa wale wazee likiundika upya. Akaunganisha matukio na kuona namna yanavyoundika kwa uzuri. Huyo mwanamke ni nani na kwanini ahusike kwenye kifo cha Luteni Jenerali Leous Mipango? Au ni yule yule ambaye nilimuona kule Hospitali ambaye aligoma kuzungumza simuni? Aliwaza Alan akiwa analikaribia gari lake. Alilikagua eneo lile kwa namna ya kulichunguza na alipoona shwari akazitupa hatua zake na kujiweka garini. Ilikuwa tayari ni saa moja kaso robo usikua. Akafungua mahali kwenye dashibodi ya gari yake na kutoa simu aliyokuwa akiitumia yule jamaa aliyemuangamiza kule Hospitali. Lengo lake lilikuwa ni kuipiga tena ile namba ambayo ilihifadhiwa kwa jina la Bee Balm. Aliipiga ile namba hata hivyo hakukuwa na mabaliko yoyote zaidi ni kwamba namba ile ilikuwa haipo kabisa. Akachanganyikiwa Alan na kuona namna anavyokwenda kugonga mwamba. Aliipekuwa ile simu kwa upande wa kuhifadhia namba hakukuwa na jina lolote lililohifadhiwa humo zaidi ya lile moja la Bee Balm. Akaachana na upande huo na kuingia kwenye bahasha ya ujumbe mfupi wa maneno nako hakukuwa na kitu. Akakereka sana na kuamua kushusha kioo cha gari yake na kuitupia ile simu upande wa nje akiwa ameiharibu vya kutosha pamoja na lile gazeti kwani hakutaka kulitumia tena. Akaondoka eneo hili huku akitafuta mahali aweze kutia kitu tumboni mwake kwani njaa ilikuwa imefikia kiwango kikubwa sana. Alikuwa akiisubiria simu ya Maisara tu kwa wakati huo na si mtu mwingine. Alichanganyikiwa sana na umbo la Maisara na kujikuta akimtamani kwa kiwango cha juu sana. Aliona jinsi ambavyo atakwenda kuufurahia usiku huo akiwa na mtoto huyo wa kike mwenye urembo wa daraja la juu.
Wakati Alan akiisubiria simu ya Maisara akiwa chumbani kwake hotelini, upande wa pili wa shilingi hali ilikuwa ni ya kuzizima sana. Ukimya ulikamatia hatamu kwa kitambo kirefu. Meza ilikuwa imezunguukwa na watu wale wale wakiwa katika sintofahamu kuu.
“Mnadhani nini hiki kilichotokea?” Aliuliza kwa sauti yenye kupwaya Zayd Aboushariff akifanikiwa kuufukuza ukimya ule.
“Kuna kiumbe cha hatari kiko hapa mjini lile tukio tusilichukulie kama gonjwa la degedege. Tumepoteza mtego wetu tulioutega na mbaya zaidi mtego umeharibika bila kukamata tulichokitega.” Alizungumza Mohammed Saloom.
“Mbona imekuwa rahisi sana kama kumvua chupi kahaba?” Akazidi kuuliza Zayd.
ITAENDELEA
Mikono ya Jasusi Sehemu ya Nne
Also, read other stories from SIMULIZI;