Operation Entebe Sehemu ya Kwanza
KIJASUSI

Ep 01: Operation Entebe

Operation Entebe Sehemu ya Kwanza

IMEANDIKWA NA : THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi : Operation Entebbe

Sehemu Ya Kwanza (1)

Mossad-1-jpg.524078

OPERATION ENTEBBE

Jina mbadala: Operation Thunderstorm/Operation Yonatan

Watekelezaji: -MOSSAD

– IDF (ISRAEL DEFENCE FORCE)

Kitengo cha Weledi: Sayeret Matkal

Mwaka wa utekelezaji: July, 1976

Nchi: Israel/Uganda

Silaha za kukumbukwa: Lockheed C-130 Hurcules

Wahusika wa kukumbukwa: – Yonatan Netanyahu (kaka wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu)

-Ehud Barak (alikuja kuwa Waziri Mkuu miaka ya karibuni)

mossad-1-jpg.524078

Advertisements

REPORT THIS AD

MOSAD & IDF: OPERATION ENTEBBE

Siku ya tarehe 27 June mwaka 1976 ilianza kama siku nyingine yioyote ndani ya uwanja wa ndege wa kimataifa katika mji mkuu wa nchi ya Israel Tel Aviv, uwanja ujulikanao kama Ben Gurion International Airport. Moja kati ya ndege ambayo ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya elo ilikuwa ni ndege ya kampuni ya Air Frace ambao walikuwa na ndege yao ya Air France Flight 139 ambayo ni ndege aina ya Airbus A300B4-203 yenye namba ya usajili mkiani F-BVGG (c/n 019).

Ndege hii ilikuwa inafanya safari yake katika siku ya leo kutoka Tel Aviv na ilikuwa inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Charles DE Gaulle International Airport jijini Paris, Ufaransa. Baada ya taratibu na protokali zote za uwanja wa ndege kukamilika na abiria wote kukwea kwenye ndege, ndege iliruka kutoka kiwanjani ikiwa na abiria 190 ndani yake pamoja na ‘crew’ ya watu 12 (Marubani na wahudumu) ambamo asilimia kubwa ya abiria walikuwa ni raia wa Israel pamoja na watu wenye asili ya kiyahudi. Ndege iliruka kutoka Tel Aviv mpaka jijini Anthens, Ugiriki ambapo ilichukua abiria wengine wapatao 58. Baada ya hapo ndege iliruka pasipo kujua kwamba kati aya abiria hao 58 waliowachukua Ugiriki ndani yao kulikuwa na abiria wanne ambao walikuwa ni wanachama wawili wa kikundi cha Popular Front For The Liberation of Palestine – External Operations (PFLP-EO) kutoka Plaestina na wanachama wawili wa kikundi cha Revolutionary Cells kutoka nchini Ujerumani.

Baada ya abiria wote kukamilisha utaratibu na kupanda ndani ya ndege, ndege iliondoka uwanjani Athens mnamo amjira ya saa 6 na dakika 30 mchana kuelekea Paris, Ufaransa.

Dakika chache baada ya ndege kuruka rubani mkuu wa ndege ambaye ndiye alikuwa ameshikili ‘usukani’ Bw. Michel Bacos akasikia kelele nyuma ya ndege wanakokaa abiria (cabin). Ili kujiridhisha kwamba kila kitu kiko sawa, rubani Michel Bacos akamuagiza msaidizi wake mmoja wapo ambaye ndiye alikuwa injinia wa ndege aende kuangalia nini kilikuwa kinaendelea.

Mara tu baada ya msaidizi huyo kufungua mlango wa mbele wa chumba cha marubani, alikutana uso kwa uso na bastola usoni mwake iliyoshikiliwa na mtu ambaye mkononi alikuwa amebeba bomu la kurusha kwa mkono. Huku msaidizi huyo akiwa bado ameshikwa na bumbuwazi, mtu huyu mwenye bomu mkononi na bastola (jina lake anaitwa Wilfred Bose raia wa Ujerumani) alimsukuma yule injinia nakumrudisha tena ndani ya chumba cha marubani na kisha yeye mwenyewe pia kuingia.

Mara tu baada ya kufika ndani ya chumba cha marubani, akawaweka chini ya ulinzi marubani ambao bado walikuwa kwenye mshituko wa mshangao na kisha kumnyanyua rubani msaidizi kutoka kwenye siti yake na kukaa yeye. Baada ya kukaa kwenye siti ya rubani msaidizi kitu cha kwanza alichokifanya haramia huyu Wilfre Bose ni kuchukua microphone ambayo marubani huwa wanatumia kutoa matangazo kwa abria, na baada ya kuiweka microphone akatoa tangazo lake la kwanza, kwa sauti ya utulivu iliyojaa lafudhi nzito ya kijerumani, akawasema; *“..kuanzia sasa ndege hii inaitwa HAIFA 1, badala ya Flight 139..”*

Haifa ni eneo (mji) maarufu ulipo kaskazini mwa nchi ambayo abiria wengi waliopanda kwenye ndege hiyo walitambua kama Israel lakini watekaji hawa na watu wengine duniani wakitambua kama Palestina.

Mara tu baada ya tangazo hili kusikika kwenye vipaza sauti vya ndege, abiria wote licha ya kuwa kwenye mshituko mkubwa wa ghafla lakini moja kwa moja waling’amua ni nini kilikuwa kinaendelea. Flight 139 au Haifa 1 kama alivyoibatiza aliyetoa tangazo, ilikuwa imetekwa na maharamia.

Baada ya Tangazo hili, haramaia Wilfred Bose akamuamuru rubani Michel Bacos kuendesha ndege kuelekea mji wa Bengazhi, nchini Libya.

Baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Bengazhi nchini Libya, ndege ilitumia karbia masaa saba uwanjani hapo kwa ajili ya kujaza ndege mafuta. Katika masaa hayo saba kuna mwanamama Patricia Martel mwenye asili ya Uingereza lakini akiwa ameolewa nchin Israel miaka michache iliyopita alifanya ‘kituko’ ambacho kilikuja kuwa na manufaa sana baadae. Wakati ambao ndege inaendelea kujaza mafuta kwa masaa yote hayo, huyu mama ambaye ni nesi kwa taaluma, alianza kulalamika juu ya maumivu ya tumbo yaliyopitiliza. Aliwaeleza watekaji kwamba ana ujauzito. Maharamia haya yakaruhusu wahudumu wa ndege wamuhudumie mwananmke mwenzao kwa vile ambavyo wataweza kwa kuzingatia kwamba ana mimba. Baada ya kuhudumiwa kwa karibia saa nzima, Patricia akatumua ujuzi wake wa unesi akafanya alicho kifanya na ghafla akaanza kutoka damu kiduchu sehemu za siri. Baada ya damu hizi kidogo kuanza kumtoka na kulalamika kuwa maumivu yamemzidia ndipo hapa ambapo wahudumu wa ndege wakaripoti kwa maharamia kuwa mimba ilikuwa imetoka.

Kwa huruma na ili kuepusha taharuki ndani ya ndege maharamia hawa wakamuachia huru mwanamama Patricia Martel hapo uwanja wa ndege mjini Bengazhi ili aweze kupata uangalizi mzuri zaidi wa kidaktari.

Lakini ukweli ni kwamba Patricia hakuwa na mimba wala hakuwa na maumivu yoyote tumboni, alichokifanya ilikuwa ni uigizaji pamoja na kuchanganya utaalamu wake wa fani ya unesi na kuweza kuwahadaa maharamia hao.

Baada ya kuachiwa Patricia alikuwa ni mtu wa kwanza muhimu kutumiwa na Mossad kujua taarifa sahihi zaidi kuhusu nini hasa kilikuwa kinaendelea ndani ya ndege, kulikuwa na watekaji wangapi, jinsia zao, silaha zao na vingine vyote ambavyo alifanikiwa kuviona.

ITAENDELEA

Operation Entebe Sehemu ya Pili

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment