Operation Entebe Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Operation Entebe

Operation Entebe Sehemu ya Pili

MEANDIKWA NA : THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi : Operation Entebbe

Sehemu ya Mbili (2)

Baada ya hapa Bose akamuamuru tena rubani Michel Bacos kurusha tena ndege angani pasipo kumueleza kuwa wanaeelekea wapi.

Wakiwa angani ndipo alianza kumpa maagizo wapi hasa anataka waelekee. Upande wa abiria kwenye cabin ambao nao walikuwa wamewekwa chini ya ulinzi na maharamia wengine waliosalia, wao hawaku wanafahamu hata ni wapi walikuwa wanaeleke. Ndege ilikuwa inaruka angani kwa karibia masaa 24. Abiria wengi walianza kuhisi labda ndege ilikuwa inaruka kuelekea China au labda Siberia, na vichwani mwao walikuwa wanajiuliza kwa nini walikuwa wanapelekwa huko.

Lakini laiti kama wangelijua mahali ambako walikuwa wanapelekwa basi wangetamani ndege hiyo ielekee kweli china.

Baada ya ya takribani masaa 24 ndege kuwa angani tangu iruke kutoka Bengazhi nchini Libya, hatimaye abiria walisikia ndege ikitua na kugusa Runway ya kiwanja cha ndege mahali fulani dunia walipowasili lakini wakiwa hawafahamu ni mwapi hasa walikuwa.

Baada ya matairi ya ndege tu kukanyaga lami za runaway na abiria kufungua ‘pazia’ (shutters) kwenye vioo vilivyopo pemnbeni mwa siti zao na kuangalia nje, mara moja wakaelewa wako wapi. Nje uwanjani kwenye lami, kulikuwa kumesimama lijitu la miraba minne lenye ngozi nyeusi tiiii likiwa na walinzi wa kijeshi na wengine waliovalia nguo za kiraia likiwa limezungukwa pande zote na walinzi hao. Mtu huyu mwenye umbo la kutisha kwa kipindi hiki alikuwa anajulikana ulimwenguni kote kutokana na matendo yake na ukatili wake. Kwa kutupa jicho mara moja tu haukuweza kukosea kujua kuwa pale kwenye lami uwanjani, alikuwa amesimama Generali Nduli Idd Amin Dadaa, ‘Field Marshal’. Swali lilokuwepo vichwani mwao lilikuwa limejibiwa tayari, wamepelekwa kwenye ardhi ya moja ya watawala ‘watemi’ na katili kuwahi kutokea juu ya uso wa dunia. Walikuwa nchini Uganda.

Baada ya ndege kusimama abria wote 248 ambao wengi wao walikuwa ni raia wa Israel na wayahudi, walishushwa kutoka kwenye ndege na moja kwa moja kupelekwa ‘terminal’ ambayo kwa wakati huo ilikuwa haitumiki. Mpaka muda huu wakang’amua kwamba hawakuwa ‘abiria’ tena kama ambavyo waliondoka Tel Aviv, bali sasa walikuwa ni mateka wa maharamia haya ya kijerumani, palestina na jeshi la Uganda.

entebbeairport-jpg.524095

Uwanja wa ndege wa Entebbe siku ya utekaji

Wakati huo huo…

Nchini Israel katika jamii ya masuala ya usalama walikuwa wako kwenye bumbuwazi kuu, matukio ya dizaini hii huwa ni ya kushtukiza na yanatokea kipindi ambacho ‘haujajiandaa’. Pia kwa kipindi hiki bado Idara ya Ujasusi ya Mossad hawakuwa na Intelejensia ya kutosha za nchi nyingi za kiafrika, akili yao na nguvu yao yote ilikuwa kwenyekudhibiti juhudi za nchi za kiarabu kufuta Israel kutoka kwenye eneo hilo walilopo. Kwa hiyo kitendo cha raia wao wengi kiasi hiki kutekwa na kupelekwa Africa kilikuwa si tu na changamoto ya namana gani wanawaokoa bali pia kulikuwa na changamoto ya uwepo wa Intelijensia ya kutosha kuhusu eneo la Entebbe, Uganda kuweza kufanya oparesheni yoyote ya kijeshi.

Ndipo hapa ambapo waziri mkuu wa kipindi hicho wa Israel Yitzhak Rabin akaitisha kikao cha maafisa wa ngazi za juu wa jeshi na Mossad na kuwauliza swali moja tu, *“…tunafanayeje?”*

Itaendelea…

THE BOLD

SEHEMU YA PILI

Tayari zilikuwa zimepita siku tatu tangu ndege ya Air France Flight 139 kuondoka Tel Aviv na hatimaye kutekwa baada ya kuruka jijini Athens iliposimama kuchukua abiria. Lakini pia zilikuwa zimepita siku mbili tangu ndege hii kutua katika uwanja wa ndege wa Entebbe nchini Uganda. Katika siku zote mbili hizi tangu ndege hii itue uwanjani hapa, rais wa Uganda Idd Amin Nduli Dadaa alikuwa anafika uwanjani hapo kila siku “kuwajulia hali” mateka hao.

Kwa muda wa siku hizi zote mbili tangu ndege itue uwanjani hapo, magaidi hawa walioiteka ndege kwa kushirikiana na jeshi la Uganda kuchunguza majina ya kila abiria kama ambavyo yalikuwa yameandikwa kwenye pasport. Lengo lao la kufanya hivi ilikuwa ni kujaribu kufahamu uraia wa kila mateka waliye naye. Baada ya kufanya uchambuzi huu wa passport zote, hatimaye siku hii ya tatu, yaani tarehe 29 June 1976 kiongozi wa magaidi hawa Wilfred Bose akiwa na karatasi mkononi aliingi ndani ya terminal ambayo walikuwa wanaitumia kuwahifadhi mateka na kisha akaanza kusoma majina ya kila abiria. Alichokuwa anakifanya ni kusoma majina ya mateka ambao passport zao zilionyesha walikuwa ni raia wa Israel. Lakini pia alisoma majina ya mateka wengine ambao licha ya passport zao kuonyesha kuwa hawakuwa raia wa Israel lakini walikuwa na majina ya kiyahudi. Pamoja na hao pia mateka wote ambao walikuwa na uraia pacha na uraia huo mmojawapo ukiwa ni Israel basi nao waliunganishwa kwenye list hii.

ITAENDELEA

Operation Entebe Sehemu ya Tatu

Isikupite Hii: Jinsi Ya Kumfanya Mwanamke Akupende Kwa Mara Ya Pili

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment