Red Butterfly Sehemu ya Pili
IMEANDIKWA NA: HALFANI SUDY
*********************************************************************************
Simulizi: Red Butterfly
Sehemu ya Pili (2)
Imma na Seif walikuwa nyuma yake na pikipiki za jeshi. Red butterfly akiwa katika mwendokasi mkali aligeuka hivyohivyo. Mkongojo wake ulikohoa mara mbili gizani, kikohozi kilichowafanya Imma na Seif wapate ajari mbaya sana, tairi za mbele za pikipiki zao zilikuwa hazina hewa. Mkongojo wa Red butterfly ulizipasua.
Red butterfly aliongeza mwendokasi wa pikipiki yake na kutokomea.
Kibibi kizee kilitumia risasi sita huku risasi zote sita zikifanya alichozituma.
Ilikuwa shabaha kali sana gizani!!
Idd ndiye aliyepiga simu kuomba msaada. Dakika kumi baadae Ambulance ya hospitali ya Hurbert Kairuki ilifika na kuwabeba majeruhi watano, huku Idd akiwa haamini uwezo wa bibi kizee yule. Alikuwa na shabaha ya uhakika, sio ya kubahatisha. Alikuwa na wepesi wa ajabu sana. Uwepesi wa Red butterfly…
“Yule bibi kizee ni nani? Shabaha yake akilenga ni nadra sana kukosa. Ana wepesi wa ajabu sana, niliona jinsi alivyogeuka kwa kasi na kumshambulia Mosha kwa risasi. Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua na risasi yake ilimpata Mosha pajani na kumsukumia mtaroni. Yule bibi kizee ni nani? Nimemwona vizuri taa za pikipiki za kina Adrian zilivyommulika wakati anakimbia, ni kizee haswa akiwa amevaa joho jeupe lenye picha ya kipepeo mwekundu kwa nyuma. Hakika yule ni Red butterfly kama alivyosema Daniel Mwaseba” Idd alikuwa anawaza wakati gari la wagonjwa la hospitali ya Kairuki likikimbia kwa kasi kuelekea hospitali.
Walifika hospitali na moja kwa moja wagonjwa waliingizwa katika chumba kilichoandikwa ’emergency’. Idd alibaki nje ya chumba kile akizungukazunguka huku mawazo tele kichwani.
“Hapa yapaswa nimpigie IGP John Rondo nimfahamishe kuhusu hili shambulio la Red butterfly na jinsi lilivyoleta madhara” Idd aliwaza huku akitoa simu yake mfukoni, alimpigia IGP John Rondo.
“Haloo Mkuu” Idd alisema baada ya IGP John Rondo kupokea simu.
“Eeeh nambie Idd mbona usiku sana” IGP John Rondo alisema kwa sauti ikiyoonesha alikuwa anatoka usingizini.
“Kuna tatizo mkuu. Tupo hospitali ya Kairuki hapa Mikocheni, wakina Daniel wameshambuliwa usiku huu na Red butterfly…. ” Idd alisema.
“Eeeh unasema? Nakuja hapo Kairuki sasa hivi” Sauti ya John Rondo ilijaa fadhaha.
Simu ikakatwa.
Nusu saa ilitosha kumfikisha IGP John Rondo katika hospitali ya Hurbert Kairuki. Alikutana na Idd na kusimuliwa kila kitu kilivyotokea kule nyumbani kwa Daniel. Ilikuwa ngumu sana kuamini kitu alichokifanya Red butterfly kwa maana John Rondo alikuwa anamuamini sana mpelelezi Daniel Mwaseba. Kupigwa risasi kwa Daniel kulimtambulisha John kwamba huyo Red butterfly alikuwa mtu wa kuotea mbali.
Kuna tatizo mkuu. Tupo hospitali ya Kairuki hapa Mikocheni, wakina Daniel wameshambuliwa usiku huu na Red butterfly…. ” Idd alisema.
“Eeeh unasema? Nakuja hapo Kairuki sasa hivi” Sauti ya John Rondo ilijaa fadhaha.
Simu ikakatwa.
Nusu saa ilitosha kumfikisha IGP John Rondo katika hospitali ya Hurbert Kairuki. Alikutana na Idd na kusimuliwa kila kitu kilivyotokea kule nyumbani kwa Daniel. Ilikuwa ngumu sana kuamini kitu alichokifanya Red butterfly kwa maana John Rondo alikuwa anamuamini sana mpelelezi Daniel Mwaseba. Kupigwa risasi kwa Daniel kulimtambulisha John kwamba huyo Red butterfly alikuwa mtu wa kuotea mbali.
IGP John Rondo alienda kukutana na daktari mkuu wa hospitali ya Hurbert Kairuki. Alimwelezea kila kitu kuhusu umuhimu wa watu waliolazwa katika chumba cha ’emergency’. Daktari mkuu alimwabarisha kwamba wagonjwa walikuwa wanafanyiwa upasuaji wa dharura wa kutolewa risasi ndani ya miili yao. Na watakuwa sawa baada ya muda mfupi tu.
Baada ya saa moja ndipo upasuaji wa dharura ulimalizika. Walifanikiwa kutoa risasi katika miili ya wale askari watatu, lakini wale askari waendesha pikipiki ilishindikana kuokoa maisha yao. Wote walifariki katikati ya matibabu.
Hali ya Daniel na Haji zilikuwa afadhali, lakini hali ya Mosha ikiwa ni ya hatari sana na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Risasi walizopigwa Daniel na Haji zilipita kwenye nyama tu, huku risasi aliyopigwa Mosha ilipasua mfupa. Ripoti hiyo ilikiwa mbaya sana kwa IGP John Rondo hasa akifikiria Daniel yupo kitandani wakati muuaji yupo mtaani. Alijua lazima ataendelea kuuwa!!
“Pole sana soldier” IGP John Rondo alimwambia Haji baada ya kufika kitandani kwake.
“Ahsante sana mkuu” Haji alisema kwa sauti ya maumivu.
“Pole na tunakuombea upone haraka” IGP John Rondo alisema.
“Nashukuru sana mkuu” Haji alijibu.
Alipotoka katika kitanda cha Haji alienda kitanda alicholazwa Daniel Mwaseba.
“Karibu sana mkuu” Daniel alisema alipoona tu sura ya IGP John Rondo.
“Pole sana Daniel” IGP John Rondo alisema.
“Ahsante mkuu, ndio kazi zetu zilivyo, waweza kupoteza maisha wakati wowote ule” Daniel alisema.
“Pole tena, Idd amenieleza kila kilivyotokea usiku nyumbani kwako. Nimeustaajabu sana uwezo wa Red butterfly. Uharaka wake katika kuamua na kutenda ni sio wa kawaida. Shabaha yake ni ya hatari sana” IGP John Rondo alisema.
“Ni kweli, Red butterfly ni mzimu ule. Anafanya mambo kwa uwezo wa ajabu sana. Nashindwa kuelewa yule mwanamke kizee katoka wapi na nini dhumuni lake la kufanya maajabu. Yaani alipiga bastola sekunde ileile nilivyoweka mguu wangu nje ya geti. Sikuwa hata nimeona risasi imetokea upande gari. Nilisikia maumivu makali sana na kuanguka chini huku nikilia. Nilimshuhudia wakati Red butterfly akirukia pikipiki isiyo na mlio. Nilielewa kwanini nilikuwa namkosa siku zote. Alikuwa anagonga na kwenda kwa kasi ya ajabu kule nyuma ambapo hakukuwa na kamera na kudanda katika pikipiki yake. Nilimwona jinsi alivyogeuka kimaajabu akiwa juu ya pikipiki na kuachia risasi mbili kwa kutumia mkongojo wake wa ajabu. Taa za kina Adrian zilimmulika kwa nyuma, alikuwa amevaa joho jeupe lenye nembo ya kipepeo mwekundu. Alitokomea wakati mimi nikiugulia maumivu ya miguu” Daniel alimwelezea IGP John Rondo.
“Pole kwa mara nyingine tena. Bila shaka aligundua u hatari kiasi gani ndomana aliwahi kukushambulia kabla hujaamua cha kufanya. Pamoja na uhodari wake lakini najua Red butterfly anakuogopa sana” IGP John Rondo alisema.
“Sidhani kama ananiogopa. Ninachohisi mimi anakuja kunigongea kila anapofaanya mauaji kwakuwa kuna ujumbe fulani ananiletea. Swali la kujiuliza ni ujumbe gani huo? Nina dhima ya kwenda kuutafuta huo ujumbe” Daniel alisema kwa hisia.
“Ni kweli tupu usemayo Daniel. Lakini wewe sasa u majeruhi. Kwa mujibu wa daktari itachukua zaidi ya wiki tatu kupona kabisa, na wiki moja ya mapumziko. Hizo ni wiki nne. Je Red butterfly hatofanya tena mauaji? Je atamuua nani safari hii? Ni ngumu sana kumruhusu Red butterfly kufanya mauaji mwezi nzima. Hatujui atauuwa wangapi? Lazima tufanye kitu Daniel kitachomzuia Red butterfly kufanya mauaji na hatimaye kumkamata” IGP John Rondo alisema.
Daniel alitulia akitafakari. Aliungalia mguu wake uliokuwa umefungwa kwa bendeji kubwa nyeupe. Mawazo yake hayakuwa kwenye mguu lakini. Alikuwa anamuwaza Red butterfly. Afanye nini kumzuia yule mwanamke wa ajabu kufanya mauaji tena? Lilikuwa swali gumu sana kwake kupata jibu la haraka. Baada ya dakika moja na sekunde arobaini, kichwani kwake lilipita jina moja tu, Elizabeth Neville. Ndio Elizabeth Neville anaweza kufanya kitu kwa kipindi ambacho yeye atakuwa anauguza jeraha lake la risasi.
“Mkuu, najua ukubwa na weledi wa majeshi yetu. Lakini mimi naamini majeshi yetu yanatumia nguvu zaidi ya weledi, utafiti na busara. Mtu atakayeweza kumfatilia Red butterfly anatakiwa awe na vitu hivyo, na mtu huyo ni mmoja tu kwasasa” Daniel Mwaseba alisema.
Daniel alitulia akitafakari. Aliungalia mguu wake uliokuwa umefungwa kwa bendeji kubwa nyeupe. Mawazo yake hayakuwa kwenye mguu lakini. Alikuwa anamuwaza Red butterfly. Afanye nini kumzuia yule mwanamke wa ajabu kufanya mauaji tena? Lilikuwa swali gumu sana kwake kupata jibu la haraka. Baada ya dakika moja na sekunde arobaini, kichwani kwake lilipita jina moja tu, Elizabeth Neville. Ndio Elizabeth Neville anaweza kufanya kitu kwa kipindi ambacho yeye atakuwa anauguza jeraha lake la risasi.
“Mkuu, najua ukubwa na weledi wa majeshi yetu. Lakini mimi naamini majeshi yetu yanatumia nguvu zaidi ya weledi, utafiti na busara. Mtu atakayeweza kumfatilia Red butterfly anatakiwa awe na vitu hivyo, na mtu huyo ni mmoja tu kwasasa” Daniel Mwaseba alisema.
“Ni nani huyo Daniel?” IGP John Rondo aliuliza kwa wahka.
“Ni Elizabeth Neville” Daniel alijibu kwa kujiamini.
“Unamaanisha mke wako Daniel?” IGP John Rondo aliuliza.
“Ndio, mke wangu ana uwezo mkubwa sana wa kupeleleza kisa hiki cha Red butterfly na kukifikisha mwisho. Zaidi ya kuwa mke wangu, Elizabeth Neville ni jasusi hatari sana. Najua unajua mkuu. Ukimpa kazi ya kumsaka Red butterfly atakuletea yule mwanamke. La msingi we mtafute, muelezee na umuamini tu” Daniel Mwaseba alisema.
“Kwani kwa sasa yupo wapi mkeo?” IGP John Rondo.
“Alisafiri kwenda China kufatilia mambo ya biashara zake. Anarudi leo jioni. Akifika hapa na kuambiwa kilichotokea atakuwa tayari kumsaka aliyenifanya hivi. Hapo nitakukutanisha nae na uumpe ABC amini Utakuwa mwisho wa mauaji ya Red butterfly” Daniel Mwaseba alisema.
“Nitafanya hivyo, nitaenda kuonana na mkeo airport jioni” IGP John Rondo alisema.
Baada ya mahojiano yaliyodumu takribani dakika kumi mkuu wa Polisi wa Tanzania aliondoka. Baada ya kupanga mipango na Daniel Mwaseba na mipango kupangika.
SURA YA PILI
Saa kumi na moja jioni IGP John Rondo alikuwa katika uwanja wa Julius Nyerere. Ndege moja tu kutoka China ilikuwa inawasili muda huo. Na ndani ya ndege hiyo iliaminika kwamba mke wa Daniel Mwaseba, Elizabeth Neville alikuwemo humo.
IGP John Rondo akiwa na askari sita nyuma yake walikuwa mahali pa kusubiria wageni waliokuwa wanawasili. Walishuka abiria sitini na tano, macho kumi na nne ya askari yaliyoenda uwanja wa ndege kumpokea Elizabeth Neville hayakumuona. Wote walishikwa na mfadhahiko, Elizabeth alikuwa wapi wakati waliambiwa na Daniel kuwa anarudi na ndege ile na kwa muda ule. Iweje wafike muda uleule na Elizabeth Neville asiwepo, cha kushangaza zaidi katika mfumo wa abiria waliotakiwa wawemo katika ndege hiyo jina la Elizabeth Neville lilikuwepo. Yalikuwa maajabu ambayo hayakuingia kabisa katika kichwa cha IGP John Rondo.
“Atakuwa wapi huyu mwanamke?” IGP John Rondo aliuliza.
“Kuna utata juu ya ujio wa Elizabeth Neville, rekodi zote zinaonesha alitakiwa kuwepo kwenye hii ndege. Jina lake lipo sasa sijui kimetokea nini mpaka mwenyewe hayupo.” Inspekta Adrian alisema.
“Cha kufanya hapa ni kwenda kumueleza Daniel kilichotokea. Daniel ni mtu mwenye kutafakari sana, atajua tu kitu gani kimetokea” John Rondo alisema.
Walikubaliana. Kutoka Uwanja wa ndege moja kwa moja walienda Mikocheni ilipo hospitali ya Hurbert Kairuki. IGP John Rondo mwenyewe ndiye aliyemueleza Daniel kila kitu kilichotokea kule uwanja wa ndege. Daniel akiwa kitandani aliwaza sana, kisha akauliza.
“Mnadhani mke wangu atakuwa wapi?”
“Kusema kweli hatuelewi kabisa. Tumeona tuje kukwambia wewe kilichotokea kule uwanja wa ndege labda utakuwa na mawazo yoyote” IGP John Rondo alisema.
Baada ya kufikiria kidogo Daniel alisema “Hapo cha kufanya ni kuwasiliana na watu wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China watueleza je Elizabeth Neville alipanda katika hiyo ndege?” Daniel alisema.
“Wazo zuri sana Daniel. Tutafanya hivyo sasahivi tujue kama Elizabeth Neville alipanda ile ndege” IGP John Rondo alisema.
“Na endapo kama hakupanda basi kuna mchezo fulani umechezwa. Kama alikuwepo basi utakuwa ni mtihani wa mwaka, iweje Elizabeth apotelee hewani?” Daniel alisema.
“Ngoja tufatilie hilo tujue. Nitakuja tena hapa kukwambia majibu ya huko China” IGP John Rondo alisema.
IGP John Rondo aliaga kwa miadi ya kurudi baada tu ya kupata majibu.
Nusu saa baadae IGP John Rondo alirudi wodini kwa Daniel Mwaseba. Sura yake ikiwa yenye wingi wa mawazo. Daniel aliiona sura ya IGP John Rondo tangu kule mlangoni. Sura yake ilimwambia kuna kitu.
Baada ya salamu John Rondo alisema.
“Tumewasiliana na watu wa uwanja wa ndege kule China. Hata wao wameoneshwa kushangazwa sana na tukio hili. Hata huko China jina la Elizabeth Neville limeonekana katika orodha ya watu waliotakiwa kuondoka kutoka leo kule China kuja Dar es salaam, lakini Elizabeth Neville mwenyewe hakuwepo, nao bado wanafanya uchunguzi kimetokea nini..” Wakati anaongea mara siku yake iliita.
“Kuna taarifa mpaya tumeipata mkuu” Simu kutoka China ilisema “Ndege yetu ilitakiwa kuondoka na watu sitini na nne, na kweli iliondoka na watu sitini na nne, lakini cha kushangaza katika orodha yetu ina watu sitini na tano. Kwa mantiki hiyo inaonesha kuna mfanyakazi wetu aliongeza jina la mtu ambaye hajasafiri, na huku akiirudia namba ishirini mbili mara mbili katika orodha, na bila shaka mtu huyo ni Elizabeth Neville. Bado tunafanya uchunguzi ni nani kafanya hivyo na kwa malengo gani?” Yule mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China alisema.
“Nimekuelewa Maxi Lee. Fanyeni uchunguzi, nasi twachunguza huku tujue kitu gani kimetokea. Ukipata lolote usisite kuwasiliana na mimi” IGP John Rondo alisema.
“Sawa mkuu” Maxi Lee alijibu na siku ikakatwa.
“Daniel haya mambo yanazidi kuwa na utata. Yule mtu wetu anayetupa taarifa kutoka kule anasema ndege ilitakiwa kuondoka na abiria sitini na nne. Lakini katika orodha kulikuwa na abiria sitini na tano ila kuna namba moja ilirudiwa mara mbili. Hivyo kwa mwonekano wa kawaida inaonekana kama orodha ni ileile sitini nne kumbe wamezidi. Kwahiyo ndege ilikuja na abiria sitini na nne ila mkeo aliyekuwa anatengeneza idadi ya watu sitini na tano hakuwepo ndani ya ndege. Swali la kujiuliza ni, Yuko wapi?” IGP John Rondo alisema.
Wakati Daniel Mwaseba yupo kitandani, mkewe Elizabeth Neville hajulikaki alipo..
“Kuna utata juu ya ujio wa Elizabeth Neville, rekodi zote zinaonesha alitakiwa kuwepo kwenye hii ndege. Jina lake lipo sasa sijui kimetokea nini mpaka mwenyewe hayupo.” Inspekta Adrian alisema.
“Cha kufanya hapa ni kwenda kumueleza Daniel kilichotokea. Daniel ni mtu mwenye kutafakari sana, atajua tu kitu gani kimetokea” John Rondo alisema.
ITAENDELEA
Red Butterfly Sehemu ya Tatu
Also, read other stories from SIMULIZI;