Taaluma Iliyopotea Sehemu ya Kwanza
IMEANDIKWA NA: FRANK MUSHI
*********************************************************************************
Simulizi: Taaluma Iliyopotea
Sehemu ya Kwanza (1)
“Katika maisha yangu nilikuwa na mipango mingi sana kama kijana yoyote yule,,nilisoma kwa bidii na kumaliza masomo yangu mpaka shahada ya pili…LAKINI MAPENZI YALIPOZIDI SIKUWA NA THAMANI TENA WALA HESHIMA TENA,,,Dhuluma ya kisiasa ilinipeleka KUZIMU na kuzika kila nilichokitegemea,”,,ANDIKA HIVI:
Ilikuwa asubuhi tulivu jijini Antananarivo nchini Madagascar, anga ilipambwa na ndege weupe waliokuwa wakishangilia ujio wa siku mpya, sauti zao zilikuwa zikiimba nyimbo nzuri zilizowabembeleza na kurudisha tumaini kwa wale walioonekana kupoteza matumaini. Pilikapilika za kusaka maisha zilikuwa zikiendelea wale waliokuwa wakielekea maofisini walionekana ndani ya magari yao ya kifahari, wale waliokuwa wakielekea katika shughuli za kawaida za ujasilia mali nao hawakuwa nyuma. Katika jiji hili kulikuwa na makundi matatu ya watu kama ilivyo katika majiji mengine kote duniani, kundi la kwanza na lenye nguvu lilikuwa ni kundi la wenye fedha maarufu kama ‘the haves’ na kundi la pili lilikuwa ni lile la wenye maisha ya kati na kundi la mwisho ni la wale wenye maisha ya chini. Jiji hili lilikuwa na shughuli mbalimbali zikishirikisha watu kutoka nchi mbalimbali, Jiji hili lilikuwa ni tofauti sana na jiji la Dar es salaam huko nchini Tanzania kutokana na ukweli kwamba jiji hili halikuwa na utofauti mkubwa sana kati ya matabaka haya matatu kama ilivyo jijini Dar es salaam, pia mfumo wa utunzaji mazingira ndani ya jiji hili ulikuwa ni ule unaotumiwa na jiji la Stockholm nchini Sweden.
FRANK
‘FRANKLINE ADVOCATES’ lilikuwa ni bango kubwa lililokuwa mbele yangu, bango hili lilinikumbusha machungu ya maisha niliyoanza kuyasahau, niliweka lile kapu langu chini na taratibu machozi yalianza kunitoka, nilikumbuka sana kipindi nikiwa Chuo Kikuu cha
Mzumbe kule Morogoro nchini Tanzania, nilikumbuka jinsi nilivyoipenda na kuitukuza taaluma ya sheria, nilianza masomo yangu ya sheria na miaka minne mbele nilihitimu na kutunukiwa Shahada yangu ya kwanza ya sheria mwezi wa saba mwaka huo, nilijiunga na shule ya sheria mwezi wa tisa mwaka huo na kupata cheti cha uwakili mwaka mmoja mbeleni, hapo niliteuliwa kuwa wakili wa mahakama kuu,,mwaka huohuo nilijiunga na Chuo Kikuu cha Pretoria huko Afrika ya Kusini ambapo nilipata Shahada ya uzamili na ndipo niliporudi nchini ili kuendelea na kuwasaidia watu mbalimbali,,kusoma kote huku sikuweza kusoma kwa pesa yang tu,,masomo ya shahada ya kwanza pamoja na yale ya uwakili nilipata mkopo toka bodi ya mikopo na wizara ya katiba na sheria,,na shahada ya pili nilisoma kwa pesa yangu binafsi na mchango mkubwa ulitoka kwa Natasha…
–
Machozi yalizidi kunitoka pale nilipogundua kuwa hali yangu ya kimaisha haikufanana kabisa na elimu niliyokuwa nayo. Nilinyanyuka pale nilipokuwa nimeweka kapu langu na kuelekea katika shughuli yangu ya kutembeza samaki kwenye nyumba za matajiri waliokuwa wanaishi eneo la HERTON ambapo ni moja ya maeneo maarufu wanayoishi watu matajiri nchini humo. Nilifika nyumba namba 55 ambayo ndiyo niliyokuwa nikipeleka samaki kwa siku hiyo na baada ya kuwapa oda yao nilishika njia kuelekea Pradriga sehemu yalipokuwa makazi yangu, pamoja na biashara ya samaki niliyookuwa nikiifanya lakini pia nilikuwa nikiandika kitabu changu nilichokipa jina la ‘THE LOST PROFESSION’ kitabu ambacho kilikuwa kikielezea mustakabali mzima wa maisha yangu na taaluma niliyoipoteza. Nilikuwa pia nikijisomea kila mara nilipopata muda wa kufanya hivyo. Niliishi kwa kuuza samaki katika jiji hili na nilikuwa maarufu katika mtaa wa HERTON huku wakiniita fisherman, hakuna aliyejua chochote kuhusu maisha yangu wala asili yangu. Mara nyingi nilikuwa nikitumia mda wangu kufanya mambo ambayo yangenisahaulisha juu ya yaliyotokea katika maisha yangu,,,hii ilikuwa ni sehemu pekee ambayo pengine ningeishi kwa Amani na kufanya mambo yangu bila muingiliano wa aina yoyote,,nilikuwa na elimu lakini sikuwa na cha kunitambulisha kuwa nilikuwa msomi,,sikuwa na kitu chochote zaidi ya taaluma iliyoozea mikononi mwangu,,,niliamini kuwa binadamu ni kiumbe muharibifu pengine kuliko kiumbe yoyote katika dunia
Maisha yangu nchini Madagascar yalikuwa ni ya kubahatisha sana ila maisha yalianza kubadilika pale nilipopata kazi ya kuhudumia bustani nyumbani kwa bwana Aristide Rusevelto aliyekuwa akiishi katika ngome yake iliyopo HIKTALAF pembezoni mwa mji, niliishi vizuri sana na familia ya mzee Aristide hasa ukizingatia kwamba nilikuwa mchapakazi na wakati mwingine nilifanya kazi zaidi hata ya zile ambazo tuliingia nae mkataba. Niliipenda na kuheshimu kazi yangu, kila mara nilipokuwa nikimaliza kazi zangu za bustani nilijificha nyuma ya nyumba hiyo na kuendelea kuandika kitabu change.
“Hello Mr. Fisherman” (habari Mvuvi), ilkuwa ni sauti nyororo ya msichana Beatrice
Rusevelto mtoto pekee katika familia ya mzee Aristide mfanyabiashara maarufu jijini Antanarivo na mmiliki wa hoteli ya AMARTON.
“hello Pretty”(habari mrembo) niliitikia kwa adabu
“am not pretty but you are handsome” (mimi si mrembo ila wewe ni mtanashati) aliniambia huku akitabasamu.
“Mr. Fisherman where is your family?”(familia yako iko wapi?), swali hili liliniumiza sana nlirudi nyuma na kufikiria mipango yangu ya kuwa na familia lakini jambo hilo lilishindikanika.
“mmh! I’ve no family Beatrice, many things happened that couldn’t give me the chance to make a family.(sina familia Beatrice,kuna mambo mengi yametokea ambayo hayakunipa nafasi ya kuwa na familia)
“And what is that?”(Na ni nini hicho?)
“It’s a very long story Beatrice you will get to know it when time reach.”( ni hadithi ndefu
Beatrice, mda ukifika utafahamu)
“Okey,dady has instructed me to go with you to buy you some stuffs”(sawa, baba amenielekeza niende na wewe kuna vitu nikakununulie) aliongea Beatrice huku
akiniangalia kwa macho ya kurembua.
“okey” (sawa). Tuliondoka ndani ya gari aina ya Mercedes Benz new Model na kuondoka kuelekea Litropatria Market.
Tulipofika pale Sokoni tulishuka na kuelekea upende wa pili wa soko,,,mbele kidogo Beatrice alisimama na kuanza kuonyesha hali ya mashangao, nilimuuliza nini kinaendelea lakini nilishangaa kumuona machozi yakimtoka.
“Beatrice ni nini tatizo kwanini unalia” Nilimuuliza kwa lugha ya kingereza
“Angalia kule Fisherman” aliongea kwa sauti yenye mchanganyiko wa kwikwi. Na mimi kwa haraka nilitazama mbele na ndipo nilipoishiwa nguvu baada ya kumuona Petrove kijana ambaye ni mchumba wa Beatrice akiwa na msichana mwingine huku wakipigana mabusu mbele ya watu pale Sokoni,,,niliishiwa nguvu kwakuwa ni wiki mbili sasa toka Petrove amvishe pete ya uchumba Beatrice,,,sikujua ni nini cha kufanya nikamshika Beatrice mkono na kumvuta kuelekea kule alikokuwa Petrove nia yangu ikiwa ni Petrove ajue kuwa Beatrice alimuona na hii ingemuondolea mzigo wa mawazo Beatrice kwa kiasi Fulani,,tulimsogelea yule kijana na ghafla alipomuona Beatrice alimuachia yule msichana na kukaa pembeni kama hamjui,,nilikuwa wakwanza kumsemesha Petrove.
“Leo ni wiki ya pili tu toka umvishe mtu pete alafu unadanganya vipi ikiwa mwaka toka umuoe?” nilimuuliza huku nikimtazama machoni,,,hasira zilinitawala kama jambo lile nilifanyiwa mimi,,,niliona jinsi Petrove alivyokuwa akicheza na hisia za Beatrice nakukumbuka kilichonifanya mimi niwe mfanya kazi wa ndani sasa tena nchini kwa watu,,,nilimtazama tena Petrove na sasa machozi yalikuwa yakinitoka,,,tuko hili lilinikumbusha mlolongo wa matukio yaliyotokea nchini Tanzania kabla ya tukio la mwisho lililonipotezea kila kitu katika maisha yangu.
“samahani Beatrice, sijui ni nini kimenitokea,,sijielewi huyu ni rafiki yang utu Beatrice tafadhali” hiyo ndiyo sauti iliyonishtua toka kwenye lindi la mawazo na kufuatiowa na sauti kubwa ya mlio wagari na hapo yule msichana alikuwa ameshaondoka,,Petrove akiwa bado analia na kuomba msamaha pale chini, Beatrice aliivua ile pete ya ndoa na kumrushia na
kisha kunivuta mkono kuelekea kule tulikokuwa tumeegesha gari letu.
Safari ya Sokoni iliishia hapo na sasa tulianza safari ya kuelekea nyumbani,,,tulipofika nyumbani tulikutana uso kwa uso na mzee Aristide Rusevelto baba wa Beatrice na hapo mzee alichanganyikiwa baada ya kumuona mwanae akilia.
“my daughter why are you crying?”(binti yangu kwanini unalia?)lilikuwa swali la kwanza kuulizwa Beatrice, hakuweza kulijibu kwani kilio kilimzidi.
“Fisherman” niliitwa kwa sauti ya ukali
“yes Sir”(ndio mzee) niliitika kama nilikuwa napokea amri toka kwa amiri jeshi mkuu
“why is my daughter crying”(kwanini binti yangu analia) lilikuwa swali lililofuata,,,na mimi sikujivunga ili kulinda kazi yangu nilimueleza mzee kila kitu na kilichofata ni hasira na machungu kwa mzee Aristide. Haraka alinyanyua simu na kubonyeza namba na kasha nilisikia akiongea:
“Petrove don’t ever come to my house again nor even near my gate you son of a bitch, and If caught u spoiling my daughter’s life again I swear to god I will castrate you”(Petrove usije tena nyumbani kwangu usisogee hata karibu na geti langu na kama nikikukamata ukiyaharibu tena maisha ya binti yangu nakuapia nitakuhasi) hayo ndo maneno machache mazito yaliyotoka kinywani mwa mzee Aristide,,,na hapo alinigeukia mimi nakunionya juu ya kumruhusu Petrove kuingia ndani ya nyumba ile.
Maisha yaliendelea na mimi nikiendelea kufanya kazi kwa bidii na mapenzi ya Petrove na Beatrice yalifika mwisho, wakati huu wote nilikuwa nikimalizia kitabu change kiitwacho The Lost Profession..
“Fisherman” sauti nyororo ilisikika ikiniita, nilipogeuka nilikutana na Beatrice aliyekuwa amevaa kibukta kilichoyapa nafasi mapaja yake mazuri yaonekane,,,Beatrice alikuwa ni msichana mzuri sana mbegu yake ilikuwa ni mchanganyiko wa mtu mweusi na
Mfilipino,,Beatrice alikuwa na umbo kama vile wasichana wakibantu,,aliumbika vizuri na alikuwa akikonga nyoyo za wengi kwa sauti yake nyororo na yenye mvuto wa aina yake,,alikuwa na macho ya mviringo na maziwa mazuri kifuani japo sikuwahi kuyaona lakini mara nyingi nimekuwa nikimuona akiogelea kwenye bwawa la kuogelea lililokuwa pale nyumbani na hapo nilipata nafasi ya kumtazama na kumthaminisha.
“Beatrice” nilimuita.
“Mambo” alinisalimia huku akiona aibu,,Beatrice alikuwa ni msichana mwenye aibu hasa ukimtazama machoni wakati unaongea nae.
“Safi habari yako”nilimjibu huku nikimuonyesha hali ya kukubali uzuri wake
“nzuri” alijibu huku akitabasamu na ndipo mawazo yangu yalipohama,,,tabasamu lile lilinikumbusha juu ya Natasha,,,mar azote katika maisha yangu nilikuwa nikimkumbuka sana Natasha na kila nimuonapo msichana akitabasamu picha niliyokuwa nikiipata ilikuwa ya Natasha,,nilimpenda sana Natasha wangu na nilikuwa tayari kufanya chochote kwa ajili ya Natasha kilichoniumiza kichwa ni kwanini Natasha hakufikiri juu ya mimi,,kwanini
Natasha alikubali mimi niwe katika hali kama ile…
“Fisherman” nilishtuka
“Naam” niliitika kama mtu alishtuka toka usingizini
“una shida gani mbona nakuongelesha unanyamaza na unaonekana una mawazo”
“hapana niko sawa, tabasamu lako limenikumbusha mbali”..nilijikuta maneno yamenitoka na nikashindwa kuyarudisha tena.
“hahaa wewe ni mcheshi Fisherman” aliongea huku akiketi karibu na mimi
“hahaa hataa ni sana bali wewe hunifanya niwe mcheshi”
Alicheka na kunitazama kwa makini kama anayetaka kujua kitu kutoka kwangu
“nina kazi ya kufanya ya chuo nimepewa naona uvivu sana kuifanya” alizungumza Beatrice
6 | P a g e
“kalete tujadili wote pengine naweza kukuchangia chochote”
“hahaa Fisherman utaweza kunisaidia kujadili maswali ya sheria wakati we ni mvuvi tu,,ni magumu” aliniambia kwa sauti ya kitoto na yenye kudeka, meneno aliyoniambia yaliniuma kwakuwa niligundua thamani ya elimu yangu haikuonekana tena lakini bado nilimsisitiza Beatrice akalete tujadili,, Beatrice aliingia ndani na kutoka na kitabu na daftrari kasha alisoma swali lililosomeka “what is the scope of Private International Law?”,, Baada ya kulisoma alinitazama na kuanza kucheka
“umesema tujadili sasa anza kuadili kama unaweza,,hahaa” aliniambia huku akicheka
“unataka nikuonyeshe maajabu”nilimwambia huku nikimtazama
“ndio Mr. Fisherman” alijibu kwa madaha
“sawa,,hili swali linataka umuelezee ni upi wigo wa P.I.L,,anaposema wigo(scope) ni sawa na kusema iyo PIL inatawala vitu gani au inameza vitu gani ndani yake,,kwanza kabisa PIL ni sharia inayokuja kutatua kesi ambayo inajumuisha pande mbili zinazotoka katika nchi tofauti au sehemu zenye sharia tofauti au mamlaka tofauti za kimahakama,,hii hushughulika na mahusiano ya watu wa nchi na nchi,,sasa hapa PIL huwa inacover vitu vitatu kwanza kabisa ni chaguzi ya mamlaka ya mahakama,,hii ni pale ambapo pande katika kesi wametoka katika mamlaka mbili tofauti za kimahakama,,baada ya kuchagua mahakama yenye mamlaka ya kusimamia kesi hii PIL inakuelekeza tena kwenye chaguzi ya sharia inayofaa kufuatwa baada ya kukuambia utafuata sharia ipi basi inakoma kufanya kazi na hapo itarudi tena kukusaidia kuitambua na kuitekeleza Hukumu iliyoamuliwa na mahakama mamlaka ya nje ya nchi unayotaka kutekeleza Hukumu ile,,,swali lako limeisha”
Mpaka hapo nilimtazama Beatrice usoni alikuwa amepigwa na butwaa,,alinitazama mara mbilimbili na ghafla kwa ukali aliamka na kuniuliza.
“Wewe ni nani?” aliniuliza kwa sauti ya ukali iliyoonyesha kuhitaji jibu
“una maana gani Beatrice” nilimuuliza huku nikicheka
“umetumwa kupeleleza familia yangu” aliuliza akiwa ananitolea macho zaidi
“sikuelewi” nilinyanyuka na kuonyesha kushangazwa
“Baba” Beatrice aliita kwa sauti ya juu akimuita baba yake,,sikuelewa kwa haraka kwanini Beatrice alimuita baba yake,,na hapo baba yake haraka alifika pale
“baba kila mara nimekuwa nikikutahadharisha juu ya wafanyakazi unaoleta huku ndani,,baba ni mara ngapi watu wanatumwa kuja kukupeleleza lakini kila mara unawaleta tu” alimwambia baba yake kwa sauti ya ukali
“unamaana gani Beatrice”
“Huyu si mvuvi ni mpelelezi au mtu mwenye nia mbaya na familia hii,,mvuvi anajua sharia?
Tena sharia za kimataifa? Baba umeleta mtu mbaya ndani ya familia yetu.
“unasemaje” mzee alitahamaki na kuingia ndani,,niliona kama naota kwa kile kilichokuwa kikiendelea pale,,nilitaka kujitetea lakini mar azote sauti ya Beatrice ilikuwa ikininyamazisha kwa ukali,,,mzee Aristede alitoka tena nje na hapo nikaona akienda kufungua geti na gari nyeusi aina ya land cruise VX yenye vioo vyeusi iliingia na mabaunsa wanne walishuka na bila kuuliza walinifata na pale ndipo kichapo kilipoanzia,
“siku zote binadamu huwadharau wawaonao kwakuwa tu muonekano wao na kazi zao huwatambulisha kuwa watu wa kundi la chini,,wanasahau kuwa kila mtu anaweza kuwa msaada kwao,,ikiwa hakuna mtu wa kutunza bustani ambaye wewe bosi unamdharau basi wewe ambaye ni bosi itakubidi pia utunze bustani…USIMDHARAU MTU KWA MACHACHE UYAJUAYO KUHUSU YEYE”,,,HII NI SEHEMU YA PILI….ANDIKA HIVI.
Nilipigwa sana na sikujua kwa haraka kwanini nilipigwa vile,,hali hii ilinikumbusha Tanzania siku niliyopigwa mbele ya Natasha lakini hakufanya chochote zaidi ya kuwaambia waniue,,,safari hii ilikuwa ni kupigwa tena kwa kosa ambalo silijui,,,niliingizwa kwenye gari na kupelekwa Ravopass ambapo ni msitu ulioko kilomita 75 toka pale Hiktalaf,,ndani ya dakika 45 tulikuwa tumeshafika Ravopass,,njiani gari ilikimbizwa kuliko kawaida,, nilipofikishwa kule niliendelea kupigwa huku nikilazimishwa niseme mimi ni nani na nilikuja kwa mzee Aristide kufanya nini.
“mimi ni mvuvi tu”,,,nilizidi kujitetea kwa sauti yenye mchanganyiko wa maumivu na kulia
“ulijuaje juu ya maswali aliyokuuliza Beatrice” aliuliza mmoja wa wale watesaji wangu.
“niliwahi kusoma mahali” niliongea kwasauti ya chini lakini hakuna aliyenisikiliza kila mtu aliniona mimi ni muongo,,niliendelea kuteswa na kupigwa pale kwa muda wa masaa miwili mfululizo na sasa sikujua kilichoendelea kwakuwa tayari nilikuwa nimepoteza fahamu.
BEATRICE ANAHADITHIA*
Mara nyingi nyumbani kwetu tulikuwa tukijiwa na watu wa aina mbalimbali wakiomba kazi lakini hawakuwa na nia ya kufanya kazi,,wengi waliokuja walikuwa ni wapelelezi waliotaka kujua juu ya utajiri wa baba yangu ni kwavipi alikuwa tajiri kiasi kile na uhalali wa pesa zake,,hivyo mara nyingi tulikuwa tukishuhudia watu wa aina hiyo lakini kwa Fisherman ilikuwa tofauti,,,Nilianza kumwamini na kumpenda Fisherman hasa kwakuwa alikuwa karibu sana na mimi kipindi nina huzuni na machungu ya kutendwa na mchumba wangu,,pamoja na kwamba Fisherman hakuwa mtu mzuri na alikuwa pengine na nia mbaya kwenye nyumba yetu lakini alikuwa ni mtu mwenye busara na anayejua kumfariji mtu,,,nilimpenda kwakuwa alikuwa na maono ya mbali,,japo alikuwa ni mtu wa kawaida lakini alikuwa anajua kujenga hoja na kuchambua anachokisema,,alikuwa ni mtanashati anayefanya kazi zake kwa wakati na alikuwa tayari kwa kazi mda wowote,,sikujua historia ya maisha lakini haikunihusu kwasasa,,,nilimchukia kuliko kitu chochote siku niliyogundua kuwa alikuwa si yule niliyedhani ndiye,,alikuwa mtu asiyeeleweka na ninaamini ili kuzuia anachotaka kufanya ni vyema kabisa akaondoka duniani.
WIKI MBILI MBELE
Ilikuwa usiku wa saa tatu nikiwa sebuleni pale ndipo baba alipokuja na kuniambia tutoke,, sikujua tulikuwa tunaelekea wapi lakini aliniambia nitamuuliza nitakapokuwa kwenye gari, nilitoka tukaingia kwenye gari nakuelekea Mitropan kisha tulikamata njia ya kwenda msitu wa Ravopass,,nilishtuka nakumgeukia baba ambaye alikuwa akiendesha gari;
“kila kitu kipo sawa?” niliuliza kwa shahuku ya kutaka kujua kwanini tulielekea msituni usiku ule.
“kila kitu kiko sawa ila yule nguruwe amegoma kusema yeye ni nani na amejulia wapi hayo maswali uliyomuuliza,,nimejaribu kufikiri nikagundua huyu kijana sio mtu mzuri sana na kama tutamwachia bila kumjua anaweza kufanya jambo lolote lile” aliongea mzee huku akionekana kusumbuliwa sana na hilo jambo.
“sasa baba kwanini tusimpoteze kabisa au hata kumfanyia kitu kitakachopoteza fahamu zake kabisa” nilipendekeza jambo hilo japo sikuwa na hakika kwamba ni mimi nilipendekeza,,sikuwa mtu wa unyama lakini hapa lilikuwa ni swala la uhai wa maisha ya mzee wangu,,nilikuwa tayari kufanya lolote kulinda uhai na furaha yake..kwangu Fisherman alikuwa ni mpita njia tu mwenye nia mbaya,,alikuwa ni mtu tu ambaye kwenye akili yangu hakustahili kuishi wala kuonewa huruma,,,alikuwa nyoka ambaye kama angening’ata ingenichukua muda kupona,,na dawa ya nyoka ni kumponda kichwa, sikuwa na sababu ya kumuonea huruma,,ni hawahawa wanaokuja na kujifanya wafanya kazi wa nyumbani waliowahi kumwekea sumu mama yangu kama njia ya kumkomoa baba yangu na ni baada ya kumkodisha mpelelezi binafsi ndipo tulikuja kugundua kuwa aliyemuwekea sumu alikuwa ni kijana wa kazi aliyetumwa na wafanya biashara wenzake na baba yangu,,kwasasa sikuwa tayari hayo yote yatokee.
“pipiii,,,pipiii” nilishtuliwa na kelele za honi ya gari, na sasa nilirudi katika dunia ya kwaida toka kwenye lindi la mawazo,,,mbele yangu kulikuwa na geti jeusi na baada ya kupigwa ile honi geti lilifunguliwa na tukaingia ndani.
“shikamoo mzee” ilikuwa sauti ya kijana aliyekuwa tisheti iliyombana na kuonyesha umbo lake la miraba mine.
“Marahaba,,yuko wapi” aliuliza mzee na yule jamaa alituelekeza njia,,tuliingia kwenye lile gofu na chumba cha pili tu alifungua ule mlango na ndipo nilipomuona Fisherman,,nafsi yangu ilimuonea huruma jinsi alivyokuwa amekonda na kudhoofika lakini sikujali kitu kwakuwa hakuwa mtu mzuri,,nilimsogelea pale alipo na kumtazama vizuri,,alikuwa amechanika usoni na damu zilikuwa zimeganda kila sehemu ya mwili wake;
“Fisherman” nilimuita huku nikimtazama, yule jamaa alikuja na kumpiga teke zito
lililomfanya akae vizuri.
“naam” aliitika kwa shida huku akifumbua macho yake taratibu.
“umetumwa na nani, kufanya nini, kwa ujira wa kiasi gani na kwa malengo yapi” nilimuuliza maswali mchanganyiko lakini hakuweza kujibu hata moja zaidi ya kutikisa kichwa akimaanisha hapana,,,nilimtazama vizuri na kukumbuka baadhi ya filamu za kigaidi nilizowahi kuizona,,nilimwambia yule baunsa amuweke kwenye kiti na kisha ampige shoti za umeme ili tuone kama atasema,,,walimfanyia hivyo lakini hakusema chochote zaidi ya kuzungumza kwa sauti ndogo sana kuwa yeye ni mtu mzuri,,hajatumwa wala hajui chochote kati ya yale tuliyokuwa tunamuuliza. Sikumuamini hata kidogo kwakuwa nafahamu asingesema ukweli.
“Baba nadhani ipo haja ya kufanya jambo” nilimweleza mzee huku nikimtazama lakini kabla sijaongea yule baunsa aliingilia.
“Tumpoteze tu na tumzike hukuhuku mzee,,atatupotezea muda tu,,nimejaribu kumoa mateso yote lakini anasisitiza kuwa yeye alisoma hayo mambo kabla ya kuja kufanya kazi kwako ila alipata matatizo yaliyomfanya apoteze alichokisoma” aliongea yule baunsa.
“hana lolote huyu ni muuaji tu,,mzee kumbuka mama yangu alifariki kwa sababu ya mambo kama haya,,kama sio watu kama hawa leo hii mama angekuwa hai,,siko tayari kuona huyu mbwa anaishi,,siko tayari,,hakuna matatizo yaliyompata wala nini niuongo tu” niliongea kwa hasira na huku machozi yakinitoka,,,hasira za kufiwa na mama yangu kipenzi tena kwa yeye kupewa sumu zilinifika tena na sasa sikuwa tayari kumuona yeyote aliyehusika au niliyemuhisi kuhusika akibaki duniani kuendelea kuishi. Niliona baba akinyanyua simu na bada ya muda niligundua alikuwa akiongea na daktari bingwa wa magonjwa ya ubongo na baada ya muda aliondoka na kuniacha pale na yule baunsa,,niliendelea kuamrisha apewe mateso lakini bado aliendelea kusema kuwa alikuwa mtu mzuri na kwamba hakutumwa. Baada ya muda mfupi mzee alikuwa amesharudi na alitoa kichupa kidogo chenye dawa na sindano;
“Vuta dawa ijae kwenye ilo bomba la sindano kisha hakikisha zimefika CC 10 kisha angalia
mshipa wake wa damu hapo nyuma ya sikio uidunge iyo sindano na uhakikishe dawa inaingia,,iyo itatosha kuharibu kumbukumbu yake” aliongea na kumkabidhi yule baunsa ile dawa na yeye alifanya hivyo baada ya kumchoma Fisherman alianza kutoa povu ghafla na alikaa kimya tulijaribu kumgusa, na kugundua kuwa mapigo yake ya moyo yalikuwa hayaendi tena.
“mpakie kwenye gari” ilikuwa sauti ya baba akiwaambie wale vijana wake,,,walimpakia kwenye gari na kuondoka ila mimi waliniacha pale na baada ya kama nusu saa walikuwa wamesharudi.
“Mmempeleka wapi” niliuliza swali hilo lakini sikujibiwa zaidi ya kuambiwa niingie kwenye gari, gari liliwashawa na safari ya kurudi nyumbani ilianza,,baada ya mwendo wa lisaa limoja tayari tulikuwa tumeshaingia nyumbani na kabla sijaingia chumbani nilimuuliza tena mzee lile swali;
“baba naweza kujua mlikompeleka Fisherman” niliuliza tena kwa sauti ya msisitizo.
“amefariki na tulienda kumtupa porini” lilikuwa jibu fupi lisilokuwa na maelezo zaidi lakini hata hivyo nilihisi sihitaji maelezo kwakuwa nilikuwepo eneo la tukio.
Nilikwenda moja kwa moja hadi bafuni na kuoga kisha nilipanda kitandani na kuvuta shuka,,mida ya saa nane usiku nilishtuka na usingizi ulikatika,,,ghafla akili yangu ilirudi nyuma na kuanza kuwaza jinsi ambavyo Fisherman alikuwa mkarimu kwangu,,nilijitahidi kutowaza lakini sikuweza,,iliendelea kunirudia akilini mwangu mpaka nilianza kulia,,kiukweli pamoja na mapungufu na ubaya wa Fisherman ila alikuwa na uzuri wake,,,alikuwa mtu ambaye alinifanya kila nilipotoka chuo nisikae na marafiki zangu bali nilikuwa nikiwahi kuja nyumbani ili kuongea nae,,alikuwa na faraja ya ajabu na maono mazuri ya kibinadamu,,alinijua na alijua namna ya kucheza na akili yangu.
“kwani tatizo lake ni nini,,nani alimtuma,,inawezekanaje toka miaka yote anatembeza samaki mtaani kwetu asiweke sumu au chochote kibaya kwenye samaki anazoleta badala yake aje leo” nilijiuliza sana kichwani ila sikujua yapi yalikuwa majibu sahihi,,baada ya kuona nayashindwa maswali mengi yaliyokuwa yakinisonga nilienda mpaka kwenye jokofu
na kuchukua pombe kali kisha nilijaribu kunywa japo haikunisaidia sana,,niliendelea kuwa macho mpaka mida ya saa kumi na mbili asubuhi niliposhtuka na kujiandaa kwenda chuo.
Siku nzima chuoni sikuwa na raha kabisa na baada tu ya kumaliza vipindi vyote niliwasha gari yangu na kurudi nyumbani,,nilipofika kabla ya chochote nilikwenda mpaka chumba alichokuwa akiishi Fisherman nakutoa vitu vyake vyote nje kisha nilianza kukagua vyote nilivyovikuta,,,nilifanikiwa kukuta picha ya msichana mremo sana na nyuma ya iyo picha kuliandika NATASHA,,IF I HAVE TO DIE FOR YOU, THEN I AM READY (NATASHA, KAMA ITAHITAJIKA KUFA KWA AJILI YAKO, BASI NIKO TAYARI),,,kilichonishtua si hii picha bali ujumbe uliokuwamo nyuma ya ile picha,,maswali mengi yaliujaza ubongo wangu nisijue lipi jibu sahihi,,Natasha ni nani,,kwanini Fisherman awe tayari kufa kwaajili ya Natasha,,ni mpenzi wake au?anaishi wapi? Hayo yalikuwa ni maswali machache kati ya mengi niliyojiuliza,,nilendelea kupekua na nilikutana na biblia,,niliipekua na ndipo nilikuta baaadhi ya sehemu alizichora mistari kama alama ya msisitizo,,moja sehemu alizochora ilikuwa ni Isaya 25:4 iliyosema ‘maana umekuwa ngome ya masikini, ngome ya muhitaji katika dhiki yake, mahali pa kukimbilia wakati wa tufani, kivuli wakati wa hari’..nilitafakari sana juu ya maneno haya lakini sikuelewa kitu, niliendelea kupekua ile biblia nilikutana tena na sehemu iliyowekwa ile mistari,,hii ilikuwa zaburi ya 64:1 iliyosomeka ‘mungu uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu, unilinde uhai wangu na hofu ya adui’..sehemu nyingine iliyokuwa na ile mistari ilikuwa ni Yeremia 18:23 iliyosomeka lakini wewe bwana wajua mashauri yao juu yangu,ya kuniua, usiwasamehe uove wao, wala usifute dhambi yao mbele za macho yako. Bali wakwaze mbele zako, uwatende mambo mbele ya hasira yako,,mistari hii ilionekana kuashiria jambo Fulani lakini sikuweza kujua ni nini,,,niliendelea kuifunua ile biblia na mbele nilikutana tena na mistari mingine ni pamoja na Mathayo 11:28 uliosema ‘njooni kwangu nyinyi nyote msumbukao na kulemewa na mizigo name nitawapumzisha’,,mwingine ulikuwa ni zaburi ya 7: 3-5 iliyosomeka ‘bwana mungu wangu ikiwa nimetenda haya, ikiwa mna maovu mikononi mwangu, ikiwa nimemlipa mabaya yeye aliyekaa kwangu salama, hasha! Nimemponya yeye aliyekuwa mtesi wangu bila sababu, basi adui na anifuate, na kuikamata nafsi yangu, naam akanyage
uzima wangu, na kuulaza utukufu wangu mavumbini’,,,,baada ya kusoma mistari yote hiyo nilichanganinyikiwa na sikujua nini maana yake au ni kwanini aliandika mistari iliyoonekana kumaanisha jambo moja,,nilikuta pia picha yake akiwa amepiga na watu watatu na haikuwa na shaka kuwa ilikuwa ni baba yake, mama yake na mdogo ilionekana kuwa ni dada yake, picha hii ilionekana kupigwa zamani sana,,nilipekua zaidi kwenye ile biblia nikafanikiwa kukuta cheti kilichokuwa kimeandikwa kwa lugha ambayo sikuitambua,,nilikitazama kilikuwa na tarehe pale na nilipopiga mahesabu ilionekana cheti hicho kilitolewa miaka 34 iliyopita,,kilikuwa na jina Frank Munishi ingawaje sikuwa nimetambua lugha iliyokuwa imeandikwa pale lakini niliamini kile kilikuwa cheti chake cha ubatizo kwakuwa kilikuwa na nembo ya msalaba na viashiria vingine vilivyoviona,,niliweka ile biblia na zile picha pembeni na kisha kuchukua nguo na kila kitu kilichokuwa pale chumbani nikaenda kuvichoma,,baada ya kumaliza kuvichoma niliiingia tena kwenye gari na kuelekea kanisa la Mtakatifu Fransisco wa Asiz lililokuwa Isoraka pembeni kidogo ya Mji wa Antananarivo, hili lilikuwa jimbo kuu la kanisa katoliki kwa pale Isoraka na nilienda kukutana na Askofu Neville rafiki mkubwa wa marehemu mama yangu,,nilifika kanisani pale na baada ya ukaguzi niliruhusiwa kuingia kuonana na baba askofu.
“haya mwanangu niambie unashida gani” ilikuwa sauti ya Askof Neville akiniuliza mara tu baada ya salamu.
“Askofu nimekuja kwa shida moja tu,,nilitaka kujua juu ya maandiko Fulani ya biblia na je mtu ikitokea umekuta ameandika sehemu kuwa soma sehemu hizi atakuwa anamaanisha nini?” nilishindwa hata namna ya kuuliza swali langu kwakuwa nilikuwa nadanganya baadhi ya mambo,,nilimkabizi kile kitabu change kilichokuwa kikionyesha iyo mistari na yeye alichukua biblia na kuanza kuipitia kisha alivua ile miwani na kunitazama.
“unataka kufahamu nini juu ya haya maandiko” aliniuliza huku akinitazama machoni,,nilitetemeka kwakuwa nilijua yule alikuwa ni mtumishi wa mungu na nilihisi pengine amefahamu kuwa nimeshiriki kuua.
“niliikuta kwenye biblia ya rafiki yangu na ninahisi anamatatizo ndiyo maana anasoma mistari ya aina hiyo tu” nilijaribu kudanganya japo sikuwa na ujasiri sana.
“rafiki yako itakuwa ana maadui sana wanaomfuta kwa jambo lisilo la kweli, au pengine wapo wanaomshambulia kwakuwa tu hawataki kumuona au wanapindisha ukweli ili kumfanya ateseke au adharaulike,,hii ni mistari ambayo wengi wanoitumia ni wale wanaotaka maombezi na msaada wa karibu wa mungu katika kushinda maadui zao” alimaliza na sasa nilipata picha kamili kuwa Fisherman alikuwa na jambo alilolificha kabla ya kifo chake,,,niliondoka na kwenda kwenye mtandao kutafuta lile jina lake ila sikufanikiwa kulipata kwenye kila sehemu niliyotafuta, na mwisho niliamua kurudi nyumbani kwakuwa ilikuwa imeshafika usiku,,nilipofika nilikwenda mpaka chumbani nilipofika niliwasha taa lakini haikuwaka, kulikuwa na giza kiasi, niliwasha tena na ghafla alitokea mtu kwenye kona ya ukuta,,nilipiga kelele na kufungua mlango ila haukufunguka na ghafla alipotea, na taa iliwaka hapo hapo,,nilisimama nikitafakari kilichotokea sikujua, niliikumbuka tena ile sura ya mtu aliyetokea pale nikakurupuka na kwenda mpaka sebuleni, ilionekana hakuna mtu aliyenisikia nikiongea, akili ilizunguka huku na kule na kunituma nikumbuke tena sura ya niliyemuona,,nilichomoa ile picha ya Fisherman aliyopiga na wale watu na ndipo nilipogundua kuwa yule aliyenitokea alikuwa ni yule mama kwenye ile picha.
“Kila jambo hupangwa na mungu,,ikitokea jambo husika analokupangia binadamu sio lile alilokupangia mungu basi halitakufika,,kumuhukumu mtu bila kujali ukweli wa jambo husika ndio tabia ya sisi binadamu hasa ikitokea uelewa wetu wa mambo umesongwa na chuki au historia mbaya ya kipindi cha nyuma” HII NI SEHEMU YA TATU,,,,ANDIKA HIVI:
BEATRICE ANAENDELEA KUHADITHIA
Nilikaa pale sebuleni huku jasho likinitoka, sikujua kwanini nilitokewa na yule mama,,niliendelea kukaa pale na sikutaka kuongea na yeyote,,nikabeba chupa kubwa ya pombe kali na kurudi tena mpaka chumbani, niliinywa ile pombe mpaka usingizi uliponifika nakunichukua moja kwa moja.
MIEZI MIWILI MBELE
FRANK
“Paa,,paa” nilisikia sauti ya mlio wa bunduki na ndipo niliposhtuka na kujikuta nikiwa kitandani,,mbavu zilikuwa zikiniuma kwa mbali na nilipotazama mguu wangu ulikuwa umening’nizwa juu,,sikufahamu nilipokuwepo lakini kilichoniogopesha ni milio ya bunduki niliyoisikia nje ya nyumba ile,,nilijitahidi na kufungua ile kamba iliyokuwa imeufunga mguu wangu,,sikuelewa kabisa eneo lile nililokuwepo, baada ya kukaa pale kitandani sasa akili yangu ilinituma kunyanyuka na kusogelea kioo kilichokuwa mbele kabisa ya chumba kile, nilisogea taratibu huku nikichechemea na nilifanikiwa kukifikia kile kioo, nilijitazama na sikuelewa nini kilinipata,,nilikuwa nimefungwa kichwani na plasta kubwa,nilikuwa na majeraha kila sehemu ya uso wangu, wakati nimesimama pale bado nikijiangalia nakutafakari nini kimenitokea nilisikia mlango ule wa kile chumba ukifunguliwa, niligeuka na kutazama kwa woga ni nani alikuwa akiingia,,nilishtuka kuona mzee wa kizungu akiingia huku ameshika bunduki,,nilijivuta mpaka nyuma kabisa na kujaribu kujificha ila alinisemesha kwa lugha ya kingereza nakuniomba nisiogope, alitoka nje mda huo na aliporudi alikuwa hana ile bunduki;
“Nimefikaje hapa na wewe ni nani?” lilikuwa swali la kwanza kumuuliza kabla hata ya
salamu yoyote, mazungumzo yote yalikuwa ni kwa lugha ya kingereza.
“Naitwa bwana Russel, ni muwindaji katika msitu huu wa Ravopass na hapa ni nyumbani kwangu” alinijibu huku akifuta miwani yake.
“nilifikaje hapa” nilimuuliza tena.
“usijali utajua kila kitu lakini kwasasa inabidi nikuchome sindano ya mwisho ili kukusaidia kwenye ugonjwa wako” aliniambia hayo na kunyanyuka kisha akatoka nje,,sikujua nini kilikuwa kinaendelea na wala sikupata muda wa kuuliza maswali zaidi,,sikuwa na kumbukumbu ya jambo lolote lile,,aliporudi alikuwa na binti mmoja aliyeonekana kuwa na miaka kati ya 16 na 18 na mwingine alikuwa ni mwanamke ambaye alionekana dhahiri kuwa alikuwa ni mke wake. Waliingia pale na kibeseni kidogo kilichokuwa na maji ya uvuguvugu na mabomba mengine ya sindano na dawa,,yule mwanamke baada ya kunisalimia alianza kunisafisha kidonda kilichokuwa kwenye goti langu na yule binti mdogo alitoka na kurudi na chai kisha alinipa,,mzee Russel yeye aliendelea kuchanganya dawa pale na yote haya yalitokea kwa wakati mmoja. Nilitamani sana kujua ni nini kilikuwa kinaendelea pale lakini sikubahatika kujua kwakuwa hakuna mtu aliyeonekana kuhitaji kuulizwa swali,,kila mtu alikuwa makini kufanya kile alichokuwa anafanya na mimi niliamua kukaa kimya ili waendelee na mambo yao,,baada ya kumaliza ile chai nilichomwa sindano kwenye mshipa mkubwa wa mkono na nyingine shingoni na hapo nilipitiwa na usingizi.
“hey,,amka, umelala mda mrefu sana” nilisikia sauti kwa mbali ikiniamsha, nilijitahidi kufungua macho lakini bado usingizi ulinikumbatia.
“aah,,wewe nani”niliuliza nikiwa bado nimefumba macho.
“mimi Natasha” iliongea sauti ile na hapohapo nilikurupuka na kuketi,,usingizi wote ulikuwa umekwisha na sasa niliketi ili nimuone Natasha lakini haikuwa hivyo,,nilijisikia mzito sana na mbele yangu niliwaona watu wale wale niliowaona mara ya mwisho kabla sijalala.
“Yuko wapi Natasha” niliuliza lakini kila mmoja pale alionekana akiwa anatabasamu na hakuna aliyenijibu,,yule mwanamke alitoka pale na kurudi na kikombe cha chai, alinipa na nilipomaliza kukinywa alinipa taulo na kunionyesha bafu lilipo,,mara hii nilianza kukumbuka matukio yote yaliyowahi kutokea katika maisha yangu,,kuanzia nikiwa Tanzania mpaka siku nateswa kwa kosa ambalo halikunihusu,,,nilimaliza kuoga na kurudi mpaka pale walipokuwepo,,ilionekana kuwa ni jioni tulivu sana na walikuwa wakiota moto nje ya ile nyumba yao,,nilisogea mpaka pale na kuamua kuketi pamoja nao;
“unajisikiaje?” aliuliza yule mwanamke.
“Nahisi vizuri,,ila sijui nilifikaje hapa” niliuliza tena lile swali lililokuwa likisumbua kichwa changu.
“nilikuokota msituni ukiwa katika hali mbaya sana miezi miwili iliyopita, nilikuleta mpaka hapa na sisi kama familia tuliamua kukutibu hapa” aliongea mzee Russel.
“wewe ni daktari?” nilimuuliza.
“Ndio, nilikuwa daktari bingwa wa magonjwa ya akili miaka mingi iliyopita wakati nikilitumikia jeshi la Pakistan kabla ya kuacha na kuja kuishi huku” aliyasema huku
akinyanyuka na kuniambia nimfate kuelekea ndani, nilimfuata huku nikijivuta na alifungua mlango mmoja uliokuwa ndani ya nyumba chenye giza kule ndani na kisha aliwasha taa na ndipo niliposhuhudia maabara nzuri ya kisasa.
“sasa huwa unamtibu nani hapa” nilimuuliza.
“sina ninayemtibu ila niliamua kujenga maabara hii mara baada ya kuja kuishi huku msituni ili niendelee kufanya tafiti zangu za kisayansi na pia namfundisha binti yangu juu ya mambo mengi ya kitabibu katika maabara hii” alimaliza kunieleza na kunirudisha tena hadi pale nje.
“ilikuwaje mpaka ukapata majeraha makubwa namna hiyo” aliniuliza na kunifanya sasa nianze kumuadithia jinsi nilivyopata kipigo baada ya Beatrice kumuelezea baba yake kuhusu mimi.
“pole sana,,wangeweza kukuua kwakuwa sindano waliyokuchoma ilizidi kipimo na sasa ikasababisha moyo wako usimame kusukuma damu,,ila kwakuwa niliwahi kukuchukua pale na kugundua kuwa moyo wako ulikuwa haufanyi kazi ipasavyo niliamua kukuanzishia matibabu ya haraka ili kunusuru maisha yako” aliniambia hayo huku akinitizama kwa makini.
“kwani walinichoma sindano ya nini” niliuliza tena.
“walikuchoma sindano ya sumu inayoshambulia sana ubongo, kitaalamu tunaita
Encephalopathy, hii huwa ni sumu inayoshambulia sana mishipa iliyopo kwenye ubongo,,dalili zake huwa ni kama kupoteza kumbukumbu,,matatizo ya kuona, na ikiwa
katika sehemu ya juu kabisa huweza kusababisha ukichaa,,sasa nilifanikiwa kuondoa ile sumu kwa kiasi kikubwa na tukimaliza sindano zote utakuwa mzima kabisa”,,mpaka hapo sikuwa na la kusema kabisa, niliwaza sana kwa baya gani nililofanya mpaka nistahili kupewa adhabu kubwa na ya kinyama kiasi kile,,lakini nilishukuru mungu kwa kuwa sasa nilikuwa hai na kumbukumbu zangu zilirudi.
ITAENDELEA
Taaluma Iliyoptea Sehemu ya Pili
Also, read other stories from SIMULIZI;