The Kingmakers Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: The Kingmakers

SIMULIZI The Kingmakers
The Kingmakers Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA THE BOLD

************************************************************************

Simulizi: The King Makers 

Sehemu ya Pili (2)

Sasa, kabla sinaeleza ni namna gani familia ya Lee imeifanya Korea Kusini kama mali yao binafsi, na namna gani ikaja kuzuka skendali iliyopelekea kuondolewa madarakani Rais Park na kupelekea CEO wa Samsung Jay Y. Lee kukamatwa juzi, ni vyema kueleqa kwanza ni namna gani mfumo wa umiliki wa Samsung ulivyo complex na unavyowafanya Lee Family kuwa na ‘absolute power’ ya kampuni.

Wengi wetu tukisikia Samsung tunaelewa kwamba ni kampuni ya Utengeneza simu, TV, na vitu vingine vya elektroniki.

Lakini uhalisia ni kwamba, Samsung Electronics ni kikampuni kimoja ndani ya kampuni 78 zilizo chini ya Samsung Group.

Mfano ndani ya Samsung group kuna Chiel Industries (kampuni ya utengenezaji nguo), Samsung C&T (kampuni ya ujenzi na Trading), Samsung Life (kampuni ya Bima), Samsung Heavy Industries (kampuni ya kutengeneza meli), Samsung Electronics (Kampuni ya kutengeneza simu n.k), Samsung Securities (kampuni ya biashara za hisa), Samsung Card, Samsung Fire & Marine na kadhalika na kadhalika.. Kama nilivyosema jumla ziko kampuni 78.

Sasa kampuni hizo kwa pamoja ndio zinaunda Samsung Group.

Umiliki wa kampuni hizi ni moja ya mifumo tata zaidi na complex katika nyanja ya biashara.

Kuelewa kwa undani juu ya namna makampuni ya Samsung yanavyomilikiwa inahitaji labda kuandika makala nzima na zaidi.. Lakini hapa nitajitahidi kueleza japo kwa muhtasari ili kuweka msingi imara wa mjadala tunavyoendelea huko mbele..

Kwa hiyo nitajaribu kuonyesha ni namna gani Lee Family wananufaika na mfumo huu complex ili kuendelea kuwa na absolute power ya kuimiliki na kuiongoza Samsung.

Cheil Industries ndio ‘holding company’ katika Samsung group.

Familia ya Lee inamiliki 31% ya hisa zaChiel Industries.

Sasa tuchukue kwa mfano Samsung Electronics, moja ya ‘lulu’ za Samsung group (inachangia 70% ya mapato ya Samsung Group). Cheil wanamiliki 4% ya Samsung Electronics. Pia Samsung Life wanamiliki 7% ya Samsung Electronics. Wakati huo huo Samsung Fire & Marine wanamiliki 1.3 ya Samsung Electronics.

Hii inawapa Lee Family jumla ya 12-13% ya umiliki wa Samsung Electronics.

Ukijumlisha na 3.44% ya umiliki wao wa moja kwa moja wa Samsung Electronics unawapa jumla ya umiliki wa 18% ya Samsung Electronics.

Kwa kuzingatia kwamba Samsung Electronics wana “Hisa hazina” (Treasury shares) ambazo hizi kawaida hazina haki ya kupiga kura kwenye maamuzi ya kampuni, kwahiyi hii inazifanya 18% ya umiliki wa Samsung Electronics wa Lee family kuwapa 22% ya kura kwenye maamuzi ya kampuni (22% voting shares).

Mtindo huu huh pia unatumika kumiliki makampumi mingine ndani ya Samsung Group.

Tuchukue mfano wa ‘lulu’ nyingine ndani ya Samsung Group, kampuni ya bima ya Samsung Life. Lee Family yenyewe inamiliki 20% ya Samsung Life. Wakati huo huo Cheil Industries (ambayo inamilikiwa 31% na Lee Family) wanamiliki 19% ya Samsung Life.

Ukijumlisha na hisa zinazomilikiwa na Samsung cultural Institute, jumla unapata 47% ya umiliki wa Samsung Life uko kwa Lee Family.

Au tukichukua mfano mwingine, Samsung Fire & Marine, Lee Family wenyewe hawamiliki hata 1% ya hisa wao kama wao lakini Cheil Industries (ambayo 31% inamilikiwa na Lee Family) wanamiliki 15% ya Samsung Fire & Marine.

Sasa turudi kwenye mfano wa Samsung Electronics ambayo ndio lulu ya Samsung Group. Tuseme kwamba maamuzi yanataka kufanyika kuhusu jambo Fulani na kura inabidi ipigwe.

Lee family wenyewe tayari wana 22% ya ‘voting shares’ kama nilivyoeleza.

Papo hapo pia kuna Mamlaka ya Huduma za Mafao (NPS – National Pension Services) wanamiliki 8% ya Samsung Electronics. Sasa NPS ni Idara ya serikali ambao ni vibaraka wa Lee Family, kwa hiyo kwenye maamuzi yoyote lazima wawe upande wa Lee Family.

Hii inafanya Lee family kuwa na 30% ya voting shares na 70% inayobakia inakuwa kwa mamia ya wanahisa wengine.

Kwa hiyo ni wazi kuwa Lee family ndio pekee wenye Sauti kubwa ya pamoja kwenye maamuzi yoyote yale.

Mfumo huu tata ndio umekuwa ukitumiwa na Lee Family kuiendesha Samsung Group tangu enzi za babu yao Lee Byung-chul, na sasa baba Lee Kun-hee na mtoto anayetaka kurithishwa Lee Jae-yong (Jay Y. Lee).

Mfumo huu umekuwa ukifanywa uwe complex zaidi kila mwaka na Lee Family.

Ndipo hapa tunafika mwaka 2014 ambapo Baba mtu Lee Kun-hee akapata mshtuko wa moyo na ikaanza kuwekwa mipango ya kumrithisha Jay Y. Lee.

Ndipo hapa ambapo ukapensekezwa mpaka wa kuunganisha (merger) kampuni ya Cheil Industries na Samsung C&T ili kuweza kumpa Jay Y.

The Kingmakers Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment