Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Sehemu ya Kwanza
KIJASUSI

Ep 02: Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse

SIMULIZI Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Ep 1
Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi: Top Secret: Nyaraka Namba 12333 Kutoka Whitehouse

Sehemu Ya Kwanza (1)

Kwahiyo; kwa kuzingatia vigezo vyote hivi ambavyo Allan Dulles mkurugenzi wa CIA aliviainisha, akawaeleza Rais Eisenhower na kaka yake John Dulles waziri wa mambo ya nje kuwa ni idara moja tu katika vyombo vyote vya ulinzi na usalama ndani ya Marwkeani yenye weledi, uwezo, watu, ufanisi na ruhusa ya kisheria kutekeleza mkakati wa dizaini hii.

Idara hiyo ni kitengo maalumu ndani ya CIA kinachojulikana kama SAD (Special activities Divisio).

Special Activities Division ni kitu gani??

Kutokana kuongezeka kwa changamoto za kimataifa , ambazo nyingine zinatishia usalama au maslahi ya mrekani lakini marekani haiwezi kuchukua hatua zozote kutokana kujiepusha na lawama kutoka jamii ya kimataifa ndipo hapo ikaonekana kuna umuhimu wa kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya suala hili.

Ndipo hapa ambapo serikali ya marekani ikaagiza shirika la kijasusi la CIA kuanzisha kitengo maalumu ndani yake ambacho kitakuwa na maafisa (wanajeshi) ambao wanaweza kutekeleza oparesheni yoyote ya kijeshi kwa kujitegemea pasipo kuhusisha serikali ya marekani.

CIA wakaanzisha idara maalumu ndani yake na kuuita Special Activities Division au kwa kifupi SAD ambayo idara yenyewe ilikuwa na maafisa wa siri ambao hawabebi vitambulisho na majina yao ni siri kubwa hayawezi kupatikana hata kwenye orodha ya maafisa wa CIA.

Lengo kubwa la kuanzishwa kwa idara hii ni kutekeleza oparesheni maalumu za kijeshi au proaganda na iikitokea wakakamatwa au kushitukiwa basi serikali ya marekani wanawakana kuwa si maafisa wao.

Kwahiyo kitengo hiki kilikuwa kinafanya kazi kwa niaba ya serikali ya marekani lakini kulikuwa hakuna uwezekano wowote wa adui kuunganisha uhusika wa kikosi hiki na serkali ya marekani.

Ndani ya Idara hii ya SAD kuna vitengo vidogo viwili;

Kitengo cha kwanza kinaitwa Political Action Group: kitengo hiki kazi yake kubwa ni kufanya ushawishi wa kisiasa (political influence), oparesheni za kisaikolojia (psychological operations) na vita za kiuchumi (Economic Warfares). Pia kutokana na maendeleo ya kiteknolojia, kitengo hiki kimeongezewa jukumu la vita za kimtandao (cyberwarfares).

Tuchukulie kwa mfano; katika nchi fulani kuna serikali au mwenendo wa serikalin unatishia maslahi ya Marekani basi kitengo hiki kinaingia kwa siri kubwa na kufanya mojawapo ya mambo ambayo nimeyaorodhesha hapo juu.

Moja ya matukio ambayo kitengo hiki kimehusika sana na CIA wamekiri kwenye nyaraka zilizowekwa wazi mwaka 2013 ilikuwa ni kueneza propaganda ambayo ilichangia kupinduliwa kwa Rais wa Iran mwaka 1953 ambapo kisa hiki nitakieleza kwa kina katika makala hii.

Pia kitengo hiki kilitumika kuzuia chama cha kikomunisti cha Italia kushinda uchaguzi mwaka 1960.

Pia kitengo hiki kimewahi kufanya oparesheni ya siri iliyoitwa Operation Mockingbird katika taifa la marekani. Oparesheni hii ilikuwa na lengo la ‘kucontrol’ habari zinazoandikwa na Vyombo vya habari nchini humo.

Oparesheni hii imekuja kupingwa vikali siku za karibuni na baraza la seneti kwa kuwa sheria hairuhusi CIA kufanya oparesheni yeyote ndani ya ardhi ya marekani.

Kitengo cha Pili kinaitwa Special Oparatins Group (SAG); na kazi yake ni kama ifuatavyo;

Kitengo hiki kinajumuisha wanajeshi wenye weledi wa hali ya juu kutekeleza malengo ya kivita pasipo kujulikana uhusika wa serikali ya marekani.

Ili kulinda utambulisho wao, wanajeshi wa kikosi hiki maalumu hawavai sare za jeshi wala kubeba vitambulisho.

Inaelezwa kuwa hiki ndio kikosi maalumu cha oparesheni za kijeshi chenye usiri mkubwa nchini marekani.

Maafisa wa kitengo hiki wanapatikanaje??

Maafisa wote wanaojiunga katika kitengo hiki maalumu cha SAD wanachaguliwa kutoka katika vikosi vingine vya weledi vya jeshi la marekani mfano Army Rangers, Combat controllers, Delta Force, 24TH STS, US Army Special Forces, SEALs, Force Recon n.k.

Wakishakuchaguliwa wanapelekwa katika kituo maalumu cha mafunzo ya CIA kilichopo Virginia kinachojulikana kama Camp Peary (au maarufu kama ‘The Farm’) ambapo miezi 18 ya kwanza wanafundisha kuhusu intelijensia na ushushushu.

Baada ya miezi 18 hiyo wanapelekwa kwenye kituo kingine cha CIA kilichopo California ambacho kinajulikana kama ‘The Point’.

Hapa wanafundishwa mafunzo ya hali ya juu ya kijeshi ambayo hayapatikani kwa kiwango hicho katika vikosi vingine vya marekani.

Mfano wanafundishwa; mapigano ya ana kwa ana ya kiwango cha juu zaidi (special hand to hand combat), kutumia karibia aina zote za silaha na milipuko ya jeshi la marekani na nchi za kigeni, ufuatiliaji adui (tracking), Kukabiliana na hali ngumu kwenye mazingira ya kawaida na nyikani ( extreme survival and wilderness train ing), Kumkwepa aduia, kuzuia adui na kutoroka adui (evasion, Resistance and escape – SERE) na pamoja na mafunzo hayo anaongezewa kozi maalumu ya kutambua fiziolojia ya binadamu (Udaktari).

Afisa ambaye anafuzu mafunzo haya kwa muda wa miezi 36 anakabidhiwa katika idara ya SAD ndani ya CIA na anatambulika kama “Afisa Mwenye Mbinu Maalumu” (Specialized Skills Officer).

Katika oparesheni zao maafisa hawa huwa wanazitekeleza katika vikundi vya watu wachache sana wasiozidi sita na oparesheni nyingine zinatekelezwa na Afisa mmoja pekee.

Katika Ofisi za CIA zilizopo kitongoji cha Langley jijini Virginia kuna ukuta wa majina ya Maafisa wa CIA waliotunikiwa tuzo za heshima kutoka na utumishi wao uliotukuka ( Distinguished Intelligance Cross na Intelligence Star). Majina ya maafisa wengi kwenye ukuta huo ni ya wale waliotumikia kitengo cha SAD ndani ya CIA.

ITAENDELEA

Top Secret Namba 12333 Kutoka Whitehouse Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment