Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Pili
KIJASUSI

Ep 02: Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034

SIMULIZI Vipepeo Weusi Mkakati Namba 0034
Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Pili

IMEANDIKWA NA: THE BOLD

*********************************************************************************

Simulizi: Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034

Sehemu ya Pili (2)

“Hahaha! Ok, aaaahh kuna malaya nimenpiga hela” nikaongea kwa lugha ya kihuni ila moyo uliuma kwa mbali niliposema ‘malaya’, kwasababu huyo malaya ninayemsema ni Cheupe wangu.

“Duh! Kama shi ngapi hivi” kauliza kwa udadisi.

“Kidogo tu! M mbili kasoro”

Nikasikia watu kadhaa wametoa miluzi ya ‘appreciation’.

“Daaaaaahh! Mwana wewe ni nyok*, ko huyo malaya ni demu wako unamaanisha si ndio?” Akauliza tena yule dogo

“Yeah! Ni demu wangu”

“Daaahh kwahiyo kumtomb* unamtomb* na hela umepiga” akaongea huku anatabasamu kwa furaha kabisa.

Sikujibu kitu nikatabasamu tu. Yule dogo akainuka kikomedi komedi na kuanza kutembe tembea huku anaongea kama muhubiri, kikomedi kimedi.

“Daaahh! Kweli ulimwengu umeisha! Watoto wa watu kuwatomb* mnawatomb* na bado hela zao mnawaibia.!! Ama kweli katika nyakati hizi ni bora ya wali nyama kuliko walimwengu”

Watu wakaangua kicheko zaidi. Na mimi mwenyewe nikajikuta naanza kucheka. Mpaka mahabusu wa selo ya karibu yetu nao nikawasikia wanacheka.

Akiwa amesimama vile vile kama muhubiri akaendelea kuongea.

“Haya unayoyaona yote majambazi haya yanaenda motoni, tena mengine yatachomwa na moto wa gesi.”

Watu walikuwa hawakereki niliona wanacheka na kufurahi. Nilihisi wanafurahi hizi ‘show’ za dogo kwasababu walau anawasahaulisha matatizo yao kwa muda mchache.

Dogo akaanza kueleza kwa utani kesi ya mtu mmoja mmoja na anaelezea mpaka jinsi hayo matukio walivyoyatenda kana kwamba alikuwepo. Kila kesi aliyoielezea vicheko vilizidi zaidi.

Sikukariri kesi zote kumi na mbili za mahabusu niliowakuta mle lakini nilifanikiwa kukariri kesi nne.

Kuna jamaa anaitwa Raphel huyu alikuwa sharobaro flani hivi, alikuwa amevaa koti la leather, yeye alikuwa kesi ya ‘Wizi wa mtandaoni’. Pia kulikuwa na jamaa mtu mzima wa makamo anaitwa Luambano ambaye kazi yake ni Ulinzi huyu alikuwa na kesi ya ‘Kutishia kuua’. Kwa mujibu wa maelezo ya dogo jamaa alikuwa amemsaidia binti mmoja kusoma sekondari A-level na binti akafanikiwa kufaulu na sasa ni mwanafunzi Jordan University lakini baada ya kufika Chuo binti kapata ‘sharobaro’ na hamtaki tena Luambano. Kwahiyo jamaa akawaapia kuwa lazima awavizie awakate kate mapanga wote wawili, ndio kwa kuokoa maisha yao binti na Huyo sharobaro wakamshitaki polisi.

Keshi nyingine ambaye niliishika kichwani ni ya jamaa anaitwa Majuto, huyu kwa mujibu wa dogo ni kwamba alikuwa na kesi ya ‘robbery’.

Ilipofika zamu ya kueleza kesi yake kwanza ndipo nikafahamu jina lake ambalo watu wote walimuita, Godi. Kesi yake ilihusu wizi wa laptop za wafanyakazi wa NMB tawi la Wami, lililopo katikati ya mji. Lakini jinsi alivyoelezea kesi yake ilikuwa kana kwamba hakuna jambo lolote lililotumia akili duniani kushinda kesi yake.

Baada ya hapo wote tukaendelea na stori za hapa na pale na stori nyingi mahabusu wenzangu walisimulia kwa fahari jinsi walivyotekeleza matukio yao ya nyuma ya wizi.

Ilipofika mida ya saa kumi nambili kama na nusu hivi, geti la selo likafunguliwa na askari akatuwekea sinia kubwa lililojaa ugali. Pembeni yake kulikuwa na bakuli kubwa la ‘mboga’ ambayo ilinichukua karibia dakika tano kufahamu ni mboga gani. Walikuwa ni dagaa lakini kwa muonekano wake yalikuwa ni kama maji yaliyooshewa dagaa na hata tulipokula sikumuona mtu aliyechovya na kutoka na dagaa hata mmoja.Baada ya wote kunawa na kuanza kula nilipomaliza kumeza tonge la kwanza na kurudisha mkono kwenye sinia kumega tonge lingine nikakutana na sinia tupu na mahabusu wenzangu walikuwa wanainuka. Kitu kishaisha. Nikaelewa kweli hapa niko mahabusu.

Baada ya chakula kama nusu saa baadae selo zote zikafunguliwa. Mahabusu wote tukatoka nje ya selo zetu na kukaa kwenye korido. Baada ya hapo tukahesabiwa wote na askari kisha akajaza vitabu vyake na kutufungia tena.

Ndani ya selo stori zikaendelea mpaka mida ya karibia saa tano usiku hivi.

Yule dogo, Godi walau kidogo stori zetu ziliendana. Maana mahabusu wengine kila mmoja niliona maluwe luwe tu. Majuto yeye stori zake ni kujisifia ujambazi alioufanya. Yule Luambano yeye kila sekunde analalamika jinsi gani hupaswi kuwaamini wanawake. Sharobaro Raphael yeye stori zake zilikuwa ‘kudiscuss’ mbinu mpya za kuwaibia ‘maboya’ mitandaoni.

Dogo, Godi pia alikuwa ni mwizi sana tu ila alikuwa na wizi wa tofauti. Huwa naamini kuna wezi wa aina mbili. Kuna watu wanaiba ili kutajirisha maisha yao wawe na hali nzuri kuliko walivyo sasa, lakini kuna watu wanaiba kwasababu ya kuiba tu. Yani wanaamini wako duniani ili wawe wezi.

Sasa Godi, alikuwa ni mwizi wa aina ya kwanza. Anaiba ili awe na hali nzuri kuliko sasa. Wezi wa namna hii wanaweza kubadilika wakipewa mwongozo sahihi.

Ikipofika mida ya saa tano watu wakaanza kulala. Wengine wakalala juu ya Yale mabenchi ya zege. Wengine, chini ya uvungu wa yale mabenchi na wengine kwenye ile nafasi katikati.

Lakini kabla ya kulala nikashangaa wanafanya kitu cha ajabu kilichonishangaza. Walikuwa wanachukua chupa tupu za maji safi Kilimanjaro za lita moja na nusu na kuzijaza maji. Godi nae akajaza chupa mbili na kunipa moja.

“Ya nini?” Nikamuuliza kwa mshangao.

“Mto huo wa kulalia!” Akanijibu huku anacheka.

Nikaweka ile chupa chini kwenye sakafu alafu nikajaribu kuilalia. Wooow, hakika ilikuwa inaleta nafuu sana. Ni tofauti na maumivu unayoyapata kichwani ukilalia sakafu hivi hivi. Huu ‘mto’ angalau ulifanya mahabusu alale mifupa ya mwilini ikiugulia maumivu ya sakafu lakini walau kichwa kilikuwa kinapata raha.

“Wow! This is genius” nikajikuta nimeropoka kingereza.

“Umesemaje?” Godi akaniuliza.

“Aaah nasema wazo poa sana hili” nikamjibu

“Oyaaaa acheni vingereza vyenu hivyo basi! Au mnatutukana” akafoka Majuto huko mahabusu wengine wanacheka.

“Don’t worry about it man” nikaendeleza utani.

“Kum*nina zako, mwenyewe” Majuto akendelea kufoka mahabusu wengine wakiangua kicheko zaidi.

Ghafla kukawa kimya kila mtu akiutafuta usingizj.

Nikajilaza pale sakafuni nikimuwaza Cheupe wangu atakuwa na hali gani huko nyumbani. Pia nikawaza kama kesho kukicha nikipelekwa mahakamani maana yake usiku kama huu kesho sitakuwa kwenye lockup ya polisi, bali nitakuwa ndani ya gereza. Nikawaza na kuwazua ni namna gani nitaweza kumshawishi kaburu aongee na mimi kama nikifanikiwa kuingia gerezani.

Nikawaza mambo mengi sana mwishowe usingizi ukanipitia.


Nikishtuka takribani majira ya saa kumi na mbili asubuhi baada ya kusikia purukushani ya watu kuamka.

“Amkeni waseng* nyinyi mnadhani mko Nyumbani hapa” alifoka askari aliyevalia kiraia na mwenye mwili mkubwa kweli kweli ambao umekolea mazoezi.

Watu wote walikuwa wameamka na wamesimama kimya kwa woga.

Yule askari akapepesa macho akimuangalia kila mmoja wetu.

“Wewe, wewe na wewe! Twendeni huku” alikuwa ametunyooshea kidole mimi, Godi na Majuto kuwa tumfuate.

Nikabaki nimeduwaa tu. Tukatoka wote nje mpaka kwenye korido. Hapo tukakuta mahabusu wengine kama kumi na tano wa selo nyingine.

Lile geti kubwa la nondo likafunguliwa tukatolewa nje kwenye korido karibu na reception. Hapo kulikuwa na askari wengine kama sita hivi na wawili walikuwa na bunduki. Hofu yangu ikazidi kuwa kubwa. Nikaanza kutetemeka mpaka jasho linatoka.

“What the **** man” nikaongea kwa kunong’ona nikimuuliza Godi.

“Usiongee!” Akanijibu kwa mkato akinong’ona.

Tukapelekwa kwenye chumba Fulani hivi kama stoo. Kisha tukapangwa mistari miwili. Hapa ndipo nikahesabu vizuri! Jumla tulikuwa ishirini.

Baada ya kutupanga wale askari wakatulia tu kana kwamba kuna mtu wanamsubiri. Kila nilipowaangalia wale maaskari walioshika bunduki hofu yangu uliongezeka mara dufu.

Baadae kidogo, akaingia RCO Goodluck Sweya. Huyu namfahamu vizuri sana kutokana na kumuona mara kadhaa kwenye televisheni akitoa taarifa kuhusu uchunguzi wa matukio makubwa makubwa ya uhalifu.

Alikuwa amevaa kiraia na ameongozana na mama mmoja wa Kiarabu pamoja na askari mwingine aliyevaa sare.

Wale maaskari wote wakampigia saluti RCO, naye akawaitikia.

“Ndio hawa?” RCO akauliza.

“Ndio hawa Mkuu” yule askari ‘mbavu’ aliyetuamsha akaitikia.

“Ok! Nataka hili zoezi lifanyike haraka nikatoe taarifa kwa RPC” RCO akaongea kwa kifupi tu na kwa mamlaka.

Ingawa nilikuwa sijui nini kinataka kufanyika, nilijisikia kama nataka kuzimia. Nilishikwa na hofu shati lote lililowa tepetepe kwa jasho.

Macho yangu yakaganda kwenye zile bunduki za askari wawili.

Nikabaki najiuliza kimoyo moyo, “wanataka kutufanya nini hawa”

Baada ya RCO Sweya kuingia na yule mama wa kiarabu na kuwaamuru maaskari waliomo mule ndani kwamba “anataka zoezi lifanyike haraka apeleke taarifa kwa RPC”, nikaona wale maaskari wamesogea mbele kidogo kuelekea mahali sisi mahabusu tulipokuwa tunesimama.

Tulikuwa tumepangwa mistari miwili.. Kila mstari ulikuwa na mahabusu kumi. Mimi nilipangwa mstari wa nyuma na mbele yetu kama hatua mbili kwenda mbele walipangwa mahabusu wengine kumi tuliokuja nao.

Kilichokuwa kinanikera zaidi rohoni ni kwamba kila nikiwatazama wenzangu, nao walikuwa wanahofu kama mimi lakini nyuso zao zilikuwa zinaonyesha kuwa wanafahamu nini kinachoendelea. Nilitamani nimnong’oneze mahabusu wa pembeni yangu nimuulize lakini nikakumbuka onyo la Godi, “Usiongee”..

Nikajikaza kiume na kushusha presha yangu, walau kwa nje nionekane niko kawaida ingawa ndani nilikuwa na hofu karibu nipoteze fahamu.

Mara yule mama wa kiarabu akiwa ameongozana na RCO wakaanza kutembea kuanzia mstari wa mbele. Alipokuwa anapita alikuwa anamuangalia kila mahabusu kuanzia juu usoni mpaka chini miguuni.

Akafanya hivyo kwa mstari wote wa mbele yetu na kisha akaanza kukagua kwa namna ile ile kwa mahabusu wa mstari wetu.

Akakagua kila mahabusu lakini alipofika mbele yangu akatumia muda mwingi zaidi. Sikujua kama alikuwa ananiangalia mimi au mahabusu wa pembeni yangu, nahisi ni kutokana na hofu niliyokuwa nayo ilinifanya nisifikiri sawa sawa.

Yule mama wa kiarabu akatumia muda mrefu zaidi mpaka RCO nikaona naye anakuwa makini zaidi kwa kusogea karibu na sisi na kutuangalia kwa makini zaidi. Nikabaki nimemtumbulia macho yule mama huku nimejikaza kweli kweli nionekane niko kawaida.

“Huyu hapa!”

Akaongea yule mama wa kiarabu na kugeuka kumuangalia RCO. Kwa mbali nikaanza kusikia mkojo unanibana. Nikaanza kutamani niropoke kwa nguvu kuwa niko hapa katika mission yenye maslahi kwa usalama wa taifa. Ingawa ukweli ni kwa maslahi yangu, na cheupe na baba yake.

“Una hakika ni yeye?” RCO akamuuliza.

“Yes ni yeye” yule mama wa kiarabu akamuhakikishia RCO Sweya huku ananyoosha mkono kumgusa huyo anayemsema. Akamgusa lakini nikashtuka hakunigusa mimi kama nilivyokuwa nahisi. Nikageuza shingo kuangalia ni nani aliyekaa pembeni yangu.

Ni majuto!

Nikamuona Majuto anatoa tabasamu la hasira anashindwa aseme nini?

Mara maaskari wawili wakasogea alipo majuto na wakamshika msobe msobe na kumuondoa ndani ya kile chumba.

Kimya kimya RCO Sweya na yule mama wa kiarabu nao wakatoka kwenye chumba. Tukabaki sisi mahabusu, yule askari mbavu aliyevaa kiraia na maaskari wengine watatu.

“Haya twendeni” akaongea kitemi yule askari Mbavu aliyevaa kiraia.

Wakatuongoza moja kwa moja kuturudisha mahabusu. Lakini kitu cha ajabu tulipofika kwenye korido ya kuingilia kwenye selo zetu mahabusu wengine wakawa wanashangilia au sijui niseme wanapiga kelele..

“Manchester, manchesteeeerrr, manchesterrrr”

Wanapiga kelele huku wanacheka kweli kweli mpaka wakawa wanaudhi. Nikaanza kumuona yule askari anaanza kuchukia. Akageuka kwenye selo inayotazamana na selo yetu namba mbili. Hii ilikuwa ni selo namba moja. Akageuka kwa hasira kweli kweli.

“Weweeee Mbelwa acha useng, kum wewe! Usijifanye umezoea sana humu fala wewe, humu hakuzoeleki boya wewe” akamfokea mahabusu mmoja ambaye alikuwa anapayuka sana “manchester” kipindi tunaingia.

“Usimaindi sana Bitozi, usimandi mwanangu! Amani kaka” huyo mahabusu akamjibu yule askari ambaye nikafahamu kuwa wanamuita jina la utani Bitozi.. Alikuwa anamjibu huku anacheka! Nikaelewa huyu lazima amezoea sana humu mahabusu kumekuwa kama Nyumbani kwake.

Bitozi akafungua milango ya selo kwa hasira tukaingia kisha akaifunga tena kwa hasira na kuondoka.

Tukaingia ndani ya selo na kuketi. Godi nilimuona ule uchangamfu wake umepotea kabisa amejiinamia kuna kitu anawaza.

“Nani wamemsukumia fuko la mavi?” Mahabusu yule sharobaro anayeitwa Raphel akamuuliza.

“Majuto!” Godi akajibu kwa kifupi tu.

Nikaona wote wamekaa kimya.

“Godi, sijaelewa kilichotokea?” Nikamuuliza kwa shauku. Mahabusu wenzangu wote walionekana wanajua nini kimetokea na nini kinaendelea. Nachukia sana kuwa gizani wakati wenzangu wote wanafahamu nini kinaendelea.

“Oya kwani hujasikia watu wanavyopiga kelele ‘manchester'”.

Godi akanijibu kwa hasira.

“Nimesikia ila sijaelewa” nikamjibu na mimi huku nimekereka.

“Gwaride la utambuzi” akadakia yule mahabusu mtu mzima wa makamo anayeitwa Luambano.

“Nini?” Nikamuuliza huku nikigeuka kutoka kumuangalia Godi na kumuangalia yeye Luambano.

“Huko mlikopelekwa na kile kilichofanyika linaitwa gwaride la utambuzi.! Si unaona vile mlivyopangwa mstari? Kama vile wachezaji mpira wanapiga picha kabla ya mechi kuanza, ndio humu mahabusu tunaita jina la utani manchester” Luambano akanifafanulia na walau kuanza kunitoa gizani. Kwa mbali nilianza kuelewa nini kilichotokea ila nikahitaji uhakika zaidi.

“Ok, lengo lake ni nini hasa hilo gwaride la utambuzi” nikauliza huku kichwani nikiwa na nusu ya jibu la swali nililouliza.

“Chukulia kwa mfano kuna tukio la uhalifu limetokea mtaani na wahaisi labda moja wapo ya watekelezaji wa tukio hilo yuko humu mahabusu kwamba alikamatwa kutokana na kuhusika na tukio hilo au alikamatwa kwenye tukio lingine lakini ni baada ya tukio hilo wanalolilenga kufanyika. Kwahiyo wanachokifanya wanamleta moja ya watu ambaye alikuwepo wakati tukio linafanyika na akikutambua maana yake kwamba unaunganishwa kwenye kesi hiyo ya uhalifu na huo utambuzi wa huyo mtu aliyeletwa unatumika kama ushahidi mahakamani ukishtakiwa kwamba shahidi wa Jamuhuri alikutambua wewe ukiwa katika kundi la watu wengi hiyo maana yake ana uhakika wewe ulihusika kufanya tukio!! Hilo ndio gwaride la Utambuzi”

Luambano akanifafanulia.

“****! Sasa kama huyo shahidi waliyemleta akikosea, akakupointi mtu kumbe haukuwepo” nikaukiza kwa kukereka.

“Ndio inakuwa imekula kwako! Yani ndio usenge wa huku mahabusu, unaweza kuja na kesi ya kuiba simu ukajikuta unasukumiwa fuko la mavi la kesi ya mauaji!” Godi akadakia na kuongea kutoka kwenye mawazo aliyokuwa nayo.

“Yule uliyemuona pale ni mke wa Singa Singa wa masika pale si unamjua?” Godi akaniuliza..

“Yes! Namjua Singa Singa mwenyewe” nikamjibu.

“Sasa kama siku tatu zilizopita limefanyika tukio la ujamabazi nyumbani kwake pale pale masika na Singa singa mwenyewe ameuwawa kwa kupigwa risasi! Kwa hiyo leo mke wake amemtambua Majuto kuwa aliwepo kwenye tukio.. So ukiacha kesi yake Majuto inayomkabili iliyomleta huku tayari pale ameshasukumiwa fuko la mavi la kesi ya robbery na mauaji! Jambo la kujiuliza ni kwamba majuto yupo humu mahabusu karibu mwezi mzima, sasa anawezaje kufanya tukio uraiani siku tatu zilizopita?”

Godi akaongea huku uso wake ukiwa serious tofauti na kawaida.

“Hii mingine inakuwaga ni michongo tu Shahidi wanamtonya mapema mtu atakaye kaa mstari gani na amevaaje ndio ampointi” akaongea luambano kwa sauti ya kulalamika.

“Ndio maana sipendagi kukaa mahabusu, bora ya gerezani aisee” akaongea Godi huku anainuka na kuanza kutembea kikomedi kama kawaida yake. Kwa mbali uchangamfu wake ulikuwa unarudi kadiri tulivyokuwa tunajadili hii mada.

“Ndio maana hupendagi?? Ina maana mwenzetu wewe Nyumbani hapa” nikamuuliza kwa uchokozi.

“Humu lockup nishakaa karibia mara kumi na gerezani nishakaa mara mbili! Mara ya zote mbili nilienda kwasababu ya kushindwa masharti ya dhamana sio kufungwa”

“Duuuh hongera! Vipi kukoje gerezani” nikamuuliza nikishindwa kuficha shauku yangu ya kutaka kujua. Kimoyo moyo nilikuwa natamani sana nipate details za kutosha kwasababu leo kama nitapelekwamahakamani kuna uwezekano mkubwa nitaenda gerezani kwa “kukosa dhamana” kama nilivyokuwa nimepanga na wenzangu cheupe na Issack.

“Mbona unauliza kwa hamu kubwa sana, vipi wanakupeleka ngomeni nini leo?” Godi akaniuliza, nahisi aliona shauku yangu kwenye swali langu.

“Yeah! Leo nitapelekwa mahakamani nadhani na sina wadhamini so naweza kupelekwa ‘ngomeni'” nikamjibu na nikasikia mahabusu wengine kwenye selo yetu wakipiga miluzi ya taratibu.

“Duuuh! Wala usijali, nitakuwa mshenga wako.. Nitakutafutia bahasha mzuri mwenye hela tukikutana jela” akanijibu huku anaongea na kutembea kikomedi kama jana. Mahabusu wengine wakaanza kucheka.

Nikatambua kuwa hapa sitopata detail yoyote kuhusu jela! Jehanum inayonisubiri huko nitaikuta huko huko jinsi ilivyo.

Mara nikasikia geti kubwa kule nje kwenye korido linafunguliwa. Ilikuwa tayari karibia saa mbili asubuhi.

“Godfrey Nandonde, Godfrey Nandonde, Godfrey ……” Askari alikuwa ameingia huku anaita jina akipita kila sell kwa nje.

“Nipoooooo” Godi akaitikia kwa sauti huku anaelekea kwenye mlango wa selo.

“Umefika muda wangu wa kwenda kusulubiwa” Godi akaongea huku anageuka kutuangalia alipofika mlangoni.

Baada ya kugeka akainua mikono kufanana na jinsi Picha ya Yesu alivyosulubiwa msalabani. Kisha akalaza shingo yake begani. Watu wakaanza kucheka chini chini wakisubiri kituko anachotaka kukifanya.

“Naondoka naenda jela! Jela ni pazuri, naenda kuwaandalia makao ili nilipo mimi na nyinyi muwepo” akaongea kwa sauti kama ya kwenye filamu ya Yesu.

Watu wakaangua kicheko kikubwa kweli kweli. Aliongea kwa sauti kubwa hivyo mpaka selo nyingine tukawasikia nao wanacheka.

Mara mlango ukafunguliwa na Askari akamchukua na kuondoka naye Kwenda “kusulubiwa” mahakamani.

Kwa kiwango Fulani nilijisikia kumuhurumia kuwa hakuwa na wadhamini na atapelekwa jela kwa kushindwa masharti ya dhamana lakini nakiri kuwa kuna upande mwingine nilifurahi kuwa walau nikifika gerezani nitakuwa na “mwenyeji”.

Tukaendelea tena na stori na wale mahabusu wengine. Lakini stori zilikuwa hazinogi kwa kuwa “ze komedi” hayupo.

Nikavumilia hivyo hivyo kumsikiliza Luambano akilalamika kuhusu wanawake mpaka ilipofika majira ya saa nne asubuhi alipofika Sajenti Bidebu yule askari anayesimamia kesi yangu ambaye alinichukua na kwenda ofisini kwake.

Ofisini kwake akachukua makaratasi kadhaa akayashika mkononi tukatoka nje ya Jengo la Polisi makao makuu ya Mkoa wa Morogoro.

Siku hii kwa mara ya kwanza nikajua ni kiasi gani hewa ya uraiani ni tamu. Nilijikuta nafumba macho na kuvuta hewa nyingi ndani na kuitoa. Hakika huwa vitu vingi tunavichukua “for granted” kwa kuwa tu tumevizoea. Nimekaa lockup kama masaa ishirini na nne pekee lakini nilijikuta nimepamiss uraiani kuliko nilivyokuwa nafikiri nilivyokuwa ndani mahabusu.

Tukiwa hapa nje ya geti la Jengo la Polisi tukasimama kidogo mwanzoni sikujua anasubiri nini lakini kama dakika mbili baadae nikaelewa.

Kuna askari mwenzake alimuomba akamchukulie pingu.

Alipokuja nazo akanivesha “bangili” na tukanza kuondoka tukitembea kwa mguu.

Uzuri au ubaya ni kwamba, Jengo la Polisi na Mahakama ya Mkoa haviko mbalimbali sana. Ni kama kutoka kituo cha ‘Fire’ Morogoro Road mpaka Sekondari ya Azania.

Lakini hapo kati kati kulikuwa na maduka na migahawa, kwahiyo kila mtu alikuwa anatukodolea macho jinsi ninavyopelekwa na askari huku nimeveshwa pingu.

Nikajikuta namlaani kimoyo moyo Sajenti Bidebu kwa “kunidhalilisha” namna hii. Lakini mwenyewe alionekana wala hajali wala hana habari. Nikahisi hii itakuwa ni kawaida tu kuwapeleka washatakiwa namna hii. Lakini haijunipunguzia kukereka kwangu na jinsi raia walivyokuwa wananiangalia kwa macho ya tahadhali na kuniogopa. Mpaka mimi mwenyewe nikaanza kujihisi “muhalifu”

Kama dakika saba, tukawa tumefika mahakama ya Mkoa. Nikajishangaa kwa jinsi nilivyo shukuru kimoyo moyo kwa kufika mahakamani. Walau sasa naweza kuepuka kuangaliwa kwa macho ya kuogopwa na “raia wema”.

Mahakama ilikuwa imejengwa katika mtindo ambao, ukiingia tu getini mkono wa kushoto kuna Jengo lenye ofisi za mahakimu. Kisha mbele yake kidogo mkono wa kushoto kuna ‘Open court’ na mkono wa kulia kuna ‘open court’ nyingine. Na mbele yake kidogo katikati kuna kichumba kidogo cha mraba kama cha mita 2 x 2 chenye madirisha makubwa ila yako juu juu, hiki kilikuwa chumba cha kuwahifadhi washtakiwa kabla ya kupandishwa kizimbani.

Tukaenda moja kwa moja kwenye hicho kichumba nje ambapo kulikuwa na askari watatu wamekaa na mmoja ana bunduki.

“Mshtakiwa mpya huyu muweke tunduni” Sajenti Bidebu akaongea huku anamkabidhi askari mmoja karatasi Fulani na akimaanisha askari huyo aniweke kwenye kile kichumba cha washtakiwa.

“Mahabusu wa magereza naona hawajafika bado, wacha nimpeleke moja kwa moja kwa muheshimiwa nadhani ameshamaliz kusikiliza civil”

Akaongea askari mmoja huku akiinuka. Nikamuelewa kuwa muheshimiwa huyo anayetaka kunipeleka ameshamaliza kusikiliza kesi za madai kwahiyo anaweza kusikiliza yangu wakiwa wanawasubiri mahabusu kutoka magereza.

Sajenti Bidebu akaagana nao na kuondoka. Kisha yule askari akaanza kuniongoza kuelekea kwenye Jengo la ofisi za mahakimu. Kimoyo moyo nikakariri alichokisema Godi, “mda wangu wa ‘kusulubiwa’ umefika”

Tulipokaribia kuingia kwenye ofisi za mahakimu, nikatupa jicho kwenye geti la kuingilia, nikamuona cheupe na Issack wanaingia. Hii mahakama imezungushiwa ukuta mfupi, kwa hiyo unaweza kabisa kuona nje. Na kule nje nikamuona Baba Bite akiwa na dada mwingine ambaye simfahamu.

Moyo wangu ukapasuka, paaaaaahh!

Nikatupa tena jicho kwa Cheupe na Issack, kisha nikatupa jicho kwa Baba Bite na yule dada ambao tayari nao walikuwa getini wanaingia. Nikajiuliza hawa wamekuja wote au vipi??

Cheupe na Isaack nikagundua kuwa walikuwa wanakwepesha macho na mimi. Hawataki macho yetu yakutane kwahiyo wakawa wanajifanya kama hawajaniona. Baba Bite yeye aliingia getini huku ananiangalia na tukakutanisha macho, kama kawaida yake akatabasamu.

Nikaanza kuchanganua akili nini kitakuwa kinaendelea kwa hawa watu?

Nikakariri tena sentesi ya Godi, “siku yangu ya kusulubiwa imefika”!

Tulipifika nje ya mlango wa Ofisi ya hakimu, yule askari nikamuona amechungulia ndani ya ofisi kidogo na kutoka nje. Dakika moja baadae kuna mama wa makamo akatoka nje mpaka pale mlangoni tulipokuwa tumesimama.

“Nimeleta fresh” yule askari akaongea huku anamkabidhi makaratasi aliyopewa na Sajenti Bidebu yule mama ambaye baadae nilikuja kumfahamu kuwa ni Karani wa hakimu.

Mama akayachukua Yale makaratasi na kurudi tena ndani ya Ofisi.

Tukabaki tumesimama pale koridoni nje ya mlango wa ofisi ya hakimu na askari.

Kama dakika tano baadae yule karani akarudi na kutuita tuingie ndani.

Tukaingia huku askari amenitanguliza na yeye ananifuatia kwa nyuma.

Ndani ya ofisi kulikuwa na meza kubwa kiasi ya kiofisi mbele kabisa na nyuma ya meza hiyo alikuwa ameketi Muheshimiwa Hakimu Gertrude Mwasota. Alikuwa ni “binti” mdogo kuliko ambavyo nilitegemea nilipokuwa naingia humo. Kichwani nilikuwa nimejenga picha nyingine kabisa.

Kwa kumtazama kwa haraka nilimkadiria kuwa alikuwa na umri kati ya miaka 34 hadi 36 na alikuwa ni mrembo haswa.

Alikuwa amevalia miwani ya macho ya fashion ya kisasa.

Juu alikuwa amevaa kikoti maridadi cha suti cheusi ambacho alikivaa juu ya blauzi ya rangi nyeupe.

Nilitamani asimame kidogo nione amevaa sketi ya rangi gani, na nione ‘vitu vingine’! Daammnn.. Nikajikuta jicho langu moja kwa moja limetua katika kiganja chake cha mkono wa kushoto! Nikaona pete ya ndoa! “Shiiiiitt”… Nikajisemea kimoyo moyo.!!

‘Male instinct’ ilikuwa inachukua nafasi yake, kwa kiasi fulani kiduchu nikajikuta nakuwa disappointed. Akili zetu wanaume ni sisi wanaume pekee labda ndio tunazielewa. Haijalishi una mwanamke mzuri kiasi gani na unampenda kiasi gani, lakini bado sehemu fulani ya nafsi yako inatamani kummiliki kila mwanamke mwingine mzuri unayemuona mbele yako. Au hata kama sio kummiliki walau unajisikia faraja ukimuona yuko ‘available’, lakini sio kuona ‘pete ya ndoa’. Haijalishi mme wako au boyfriend wako anakupenda kiasi gani, lakini hata siku moja asikudanganye, hakuna mwanaume anayemuona mwanamke mrembo akiwa na pete ya ndoa na kufurahi.

Muheshimiwa Getrude Mwasota, alikuwa ananiangalia toka naingia mpaka nasimama mbele yao wote waliokuwa ndani ya ile ofisi.

Mbele ya meza ya hakimu kulikuwa na meza nyingine ndefu kiasi ambayo upande wa kushoto alikaa yule mama karani na mkono wa kulia walikaa watu wawili ambao nilikuja kuelewa kuwa ni waendesha mashitaka wa serikali.

Mmoja alikuwa ni mwanaume na mwingine mwanamke. Wote walikuwa vijana, ingawa yule mwanaume alikuwa anaweza kukaribia labda miaka 38 hivi tofauti na yule mwenzake wa kike ambaye nilikadiria hawezi kuwa zaidi ya miaka 34.

Wote walikuwa wamevalia suti nyeusi na shati nyeupe kwa ndani.

Kwa hiyo nilikuwa nimesimamishwa mbele yao wote. Kwa kiasi fulani nilishukuru kwa kuwa kesi yangu itakuwa inaendeshwa huku “chamber court” walau itaniondolea aibu ya kusimamishwa mbele ya kadamnasi ya kusimamishwa kizimbani kama kesi ingelisomwa “open court”.

Lakini kilichokuwa kinakera huku chamber court ni jinsi unavyokuwa umekaribiana na hawa “waheshimiwa” kiasi mpaka unajisikia aibu.

Yule askari aliyenileta alikuwa amesimaa mlangoni na nilipoangalia nje ya mlango niliwaona Cheupe na Issack na pembeni yao kidogo wamesimama Baba Bite na yule Dada ambaye nilikuwa bado sijamfahamu mpaka sasa. Wote walikuwa wamesimama koridoni lakini wamekaribia kabisa mlango wakiwa wanafuatilia kinachoendelea huku ndani.

Baada ya kama dakika nne hivi wote mle ndani ya ofisi ya hakimu walikuwa wameacha kunitazama na wameinama wanaandika kwenye makaratasi juu ya meza zao, hakimu akaanza kuongea.

“Mwendesha mashtaka” Hakimu akaongea kwa kifupi huku ameinama anaandika katika makaratasi yake.

Mwendesha mashtaka yule wa kiume akasimama na kuanza kuongea “Muheshimiwa Hakimu shtaka lililoko mbele yako ni shtaka la jinai namba 264 la mwaka 2016 ambapo Jamuhuri inamshtaki Bwana Rweyemamu Charles Kajuna kwa makosa matatu” akanyamaza kidogo.

Nikamuona hakimu anaandika kwa haraka haraka kwenye makabrasha yake.

“Endelea” Hakimu akamueleza muendesha mashtaka bila kumtazama akiwa anaendelea kuandika kwenye makabrasha yake.

“Shtaka namba moja” muendesha mashtaka akaanza kusoma huku ananitazama na kuangalia kwenye makabrasha yake na kunitazama tena. “Siku ya tarehe 23 Novemba 2016, kinyume na sheria za adhabu ya makosa ya jinai namba 333 na 335 (a) ya mwaka 2002, akijua kabisa ni kinyume cha sheria Rweyemamu Charles Kajuna alitumia kadi za benki mali ya Bi. Hasnati Jaffar Kumbea kuiba fedha katika mashine za fedha za Benki ya Barclay’s kiasi cha shilingi milioni moja na laki sita”

Mwendesha mashtaka alinisomea shtaka.

Hakimua aliandika andika kwa sekunde kadhaa baada ya muendesha mashata kunyamaza kisha akaniangalia na kuniuliza, “Mshtakiwa kweli ama si kweli?”

“Si kweli!” Nikamjibu

Akainama na kuandika tena kwenye karatasi zake.

“Mwendesha mashtaka?” Hakimu akaongea huku akimuangalia muendesha mashtaka.

Muendesha mashtaka akaendelea tena kunisomea mashtaka..

“Shtaka la pili, Kinyume na Kifungu cha sheria namba 271 ya adhabu ya makosa ya jinai ya mwaka 2002, Rweyemamu Chrles Kajuna akijua kabisa ni kinyume cha sheria alitumia nguvu kumuibia simu ya mkononi Bi. Hasnat Jaffar Kumbea katika mtaa wa mazimbu FK, wilayani Morogoro Mjini, Mkoa wa Morogoro”

Akanyamaza tena kidogo.

“Mshtakiwa kweli ama si kweli?” Hakimu akaniukiza safari hii bila kuniangalia alikuwa anaandika kwenye makaratasi yake.

“Si kweli” nikajibu

“Mwendesha mashtaka” hakimu akaongea akimuangalia muendesha mashtaka.

“Shtaka la tatu, kinyume na kifungu namba 337 cha adhabu ya makosa ya jinai, Rweyemamu Charles Kajuna katika eneo la Mazimbu FK, Wilani Morogoro Mjini, mkoa wa morogoro akijua kabisa ni kosa kisheria alimshambulia na kumpiga Bi. Hasnat Jaffar Kumbea na kumsababishia maumivu Makali”

Nikasomewa tena shtaka la tatu.

“Mshtakiwa kweli au si kweli?”

“Si kweli.!”

Hakimu akaandika tena kwenye karatasi zake.

“Mwendesha mashtaka?” Akamuuliza na kumuangalia mwendesh mashtaka.

“Muheshimiwa hakimu upelelezi bado unaendelea na upande wa Jamuhuri hauna pingamizi juu ya dhamana” akaongea mwendesha mashtaka na kukaa chini.

Hakimu akatumia muda mrefu zaidi safari hii kuandika. Alitumia karibia dakika mbili nzima kisha akainua kichwa na kuniangalia.

“Mshtakiwa unatakiwa uwe na wadhamini wawili na wote watasaini karatasi ya dhamana ya shilingi milioni moja kila mmoja, je una wadhamini ndugu mshtakiwa?”

Hakimu akaniuliza na nilikuwa najiandaa kumwambia hapana lakini kabla sijasema chochote nikasikia mtu anaingia ndani ya ofisi ya hakimu na kuongea kwa kupayuka.

“Tupooo muheshimiwa.!”

Wote tukageuka kuangalia mlangoni. Alikuwa ni Baba bite ameongozana na yule dada nisiyemfahamu. Mikononi wameshika makaratasi. Wakaingia haraka haraka na kunyoosha mkono kumkabidhi karani makaratasi yao.

“Muheshimiwa hawa watu siwafahamu.!” Nikajikuta naropoka kwa nguvu..

“Relax Ray, wacha tukusaidie”

Baba bite akaongea kwa tabasamu na ikanikera zaidi..

“Nooooo siwajui…!”

“Order please!!” Hakimu akafoka na kutukatisha mabishano yetu..

“Mahakama iko inaendelea nawataka muheshimu” akaongea huku anatuangalia mimi na Baba Bite.

“Enhe mshtakiwa unasemaje?”

“Muheshimiwa hawa watu siwajui na wala siko tayari kudhaminiwa nao kulinda usalama wangu!” Nikaongea kwa jazba.

“Ray mimi na wewe tunakaa nyumba moja unawezaje kusema….”

Baba bite akaongea kwa sauti ya juu lakini Muhesgimiwa hakimu akamkatisha.

“Naomba uheshimu mahakama, sijakuruhusu uongee na wala sijakuruhusu kuingia humu ndani… Karani mpe karatasi zake na naomba uondoke kabisa eneo la mahakama”

Muheshimiwa hakimu akaongea kwa hasira na kwa mamlaka.

Baba bite akachukua makaratasi yake huku anatabasamu kwa kujiamini kisha akanigeukia na kutikisa kichwa kwa kunisikitikia.

“Nahahirisha mahakama kwa muda na mahakama itarejea baada ya dakika kumi.” Hakimu akaongea baada ya Baba bite na mwenzake kutoka nje.

Kila mtu akasimama na kuanza kuchukua makaratasi yake kutoka nje.

Askari naye akaanza kuniongoza ili kutoka nje.

“Mshtakiwa naomba abaki” hakimu akamuamuru yule askari.

“Sawa muheshimiwa” askari akaitikia na kutoka nje.

Nikabaki nimesimama pale pale nilipokuwa. Ndani ya ofisi ya hakimu tulibaki mimi na yeye tu. Mwanzoni nilipokuwa naingia kwa kiasi Fulani nilivutiwa na Urembo wake lakini sasa baada ya kumshuhudia akidhihirisha mamlaka aliyokuwa nayo, nikawa nimebaki na mtazamo wa kumuheshimu kwa hali ya juu.

“Kaa kwenye kiti mahakama imehairishwa” Hakimu akaongea huku ananiangalia kana kwamba anamuangalia mtoto mdogo.

“Sawa muheshimiwa” nikaongea kwa heshima.

Akachukua mkoba wake wa kike ambao alikuwa ameuwek chini kwenye sakafu na kuuweka juu ya meza. Akaufungua ndani na kuanza kutafuta kitu. Akakipata na kukitoa.

Kilikuwa ni kikaratasi cheupe kimekunjwa. Akanyoosha mkono kunipa.

Nikamtumbulia macho tu nikijiuliza kama ni sahihi nilivyowaza kuwa alikuwa ananikabidhi kikaratasi au ni mawazo yangu. Akaendelea tu kuninyooshea mkono kunikabidhi kikaratasi.

Nikanyoosha mkono na kukipokea.

Baada ya kukipokea nikagundua kuwa kinafanana kabis na vile vikaratasi ninavyoletewaga kutoka kwa Dr. Shirima.

Nikainua kichwa na kumuangalia Hakimu, na yeye alikuwa ananiangalia huku amenikazia macho.

Nikakikunjua kikaratasi. Na ndani kilikuwa kimeandikwa.

“KESHO BISHOP RESIDENCE 4:00 PM

D.S. #14″

Nikakisoma kikaratasi kwa kukirudia rudia. Nikainua macho kumuangalia Hakimu. Bado alikuwa amenikazia macho.

Nilielewa kuwa hiki kikaratasi kimetoka kwa Dr. Shirima na anataka tufanye kikao chetu cha 14 na kikao changu mimi naye safari amepanga kitakuwa katika makazi ya Askofu!

Sikuweza kung’amua mara moja kama huyu Hakimu mrembo naye ni mmoja wa wanachama wa The Board, au ni kibaraka kama nilivyokuwa mimi au wamemtumia tu siku ya leo.

Nikakikunja kikaratasi na kukiweka mfukoni.

Waendesha mashitaka walikuwa mlangoni wanaingia, dakika kumi zilikuwa zimeisha. Wakaingia na kuketi.

Baada ya Hakimu kuandika andika katika makaratasi yake akaanza kuongea.

“Mahakama imerejea tena na kabla ya kuihairisha tulikuwa tunazungumza kuhusu dhamana ya mshtakiwa… Aaahh sasa ni kwamba… aahh baada ya mahakama hii kutafakari kwa kina imeafikia maamuzi kwamba, kwa kuwa mshtakiwa Rweyemamu Charles Kajuna ni mtu anayefahamika na mwenye heshima katika jamii hivyo basi kwa kutumja kifungu cha Sheria namba …..… (sikukishika kichwani kifungu alichotaja) hivyo basi mahakama hii inamruhusu mshtakiwa ajidhaimini yeye mwenyewe.”

Nilishtuka na nikagundua sio mimi pekee niliyeshtuka. Hata waendesha mashataka walikuwa wameshtuka zaidi yangu. Wakawa wanaangaliana na kwa haraka yule mwendesha mashtaka wa kiume akainuka.

“Muheshimiwa hakimu….”

Kabla hajamaliza hakimu akamkatisha.

“Kaa chini mwendesha mashtaka sijakuruhusu uongee.. Mshtakiwa?”

Hakimu akaongea kwa mamlaka akinipa mimi nafasi niongee na kumuamuru mwendesha mashtaka akae chini.

Nikapatwa na kigugumizi kwa karibia dakika nzima. Sikujua nisemeje. Inapaswa niwe makini sana kukubali hii “ofa” ya mahakama kwamba nijidhamini mwenyewe. Nilihisi huu ni mtego.

Nikahisi huyu Hakimu anatumiwa na The Board, kwa hiyoThe Board wanataka niwe uraiani. Kwanini??

Nikafikiri haraka haraka. Nikaamua kwamba busara ni kufanya kinyume na The Board wanachokitaka.

“Muheshimiwa hakimu kwa kuzingatia tukio lilitokea na kwa kuzingatia usalama wangu mimi mwenyewe binafsi siko tayari kujidhamini”

“Unaweza kuieleza mahakama unahofia nini?”

“Muheshimiwa nashukuru mahakama yako kwa kuniamnini, lakini naomba mahakama yako ifahamu kuwa siko tayari kujidhamini”

Ule mshangao ambao waendesha mashtaka walikuwa nao mwanzoni uliongezeka mara kumi zaidi. Nahisi walikuwa wanahisi kama wako ndotoni kwa hiki kilichokuwa kinaendelea.

Muheshimiwa nikamuona ameshikwa na hasira. Akanikazia macho kwa takribani dakika mbili pasipo kusema chochote.

“OK.! Mshtakiwa ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo mshtakiwa utaenda mahabusu gerezani na kesi imehairishwa mpaka tarehe 8 mwezi wa 12”

Hakimu akaongea akiwa serious zaidi huku anaandika. Waendesha mashataka wao bado walikuwa wameduwaa tu hawaelewi wala kuamini nini kimetokea.

Yule askari akaja akanishika mkono na kuniongoza kutoka nje. Moyo wangu ukajaa giza nikifikiria kitakachofuata mbele yangu dakika chache zijazo..

Nilikuwa katika kile kichumba ambacho wenyewe wanakiita tunduni, kichumba ambacho mahabusu wanawekwa wakiwa wanasubiria kupandishwa kizimbani.

Niliporudishwa na askari kutoka ofisini kwa hakimu niliwakuta mahabusu wengine watano humu ndani ya kichumba ambao wao walikuwa wameletwa kutoka gerezani kuja kusikiliza kesi zao.

Uzuri kesi zao zote zilikuwa zimekuja kutajwa tu siku ya leo. Kwahiyo walikuwa wanachukuliwa na kupandishwa kizimbani, kisha kesi inatajwa na kuhairishwa kisha wanarudishwa tena humu tunduni. Hii ili maanisha kuwa muda si mrefu zoezi la kutajwa kesi litaisha na tutapelekwa gerezani.

Nilikuwa nimesimama tu naangalia nje ya tunduni kupitia dirisha. Akilini mwangu mawazo kadhaa yalikuwa yanapita kichwani.

Cha kwanza niliwaza kuhusu The Board. Ni dhahiri kuwa walikuwa hawataki niende gerezani na hii nilihisi kuwa walikuwa wamefahamu au wamehisi mpango wangu kuwa nina lengo la kuonana na Eric Kaburu. Kwahiyo kichwani mwangu niliamini kuwa labda walikuwa na hofu ni kitu gani Kaburu atanieleza kama nikifanikiwa kumshawishi kuongea na mimi.

Ilikuwa ni ajabu kupata kikaratasi cha kunitaka tuonane kutoka kwa Dr. Shirima kwa muda mfupi hivi toka tuonane. Ni takribani wiki tatu pekee toka tuonane pale kwenye parking ya Nashera Hotel na kwa kawaida ingepita miezi mitatu au hata minne ndio niletewe kikaratasi kingine cha kunitaka tuonane. Hivyo ni dhahiri kuwa hii ilikuwa ni ’emergency’. Na nilitafsiri kuwa walikuwa wanahofia mimi kuonana na Kaburu.

Upande mwingine ni Idara ya Usalama wa Taifa. Kwanini nao hawataki niende gerezani? Je, wanahofia usalama wangu? Au labda wamehisi nina mpango gani na wanaona si mpango sahihi?

Sikupata jibu zaidi ya kujua tu kwamba nao hawataki niingie gerezani. Rohoni mwangu nikazidi kuamini kwamba ninachokifanya ni sahihi kabisa ndio maana The Board hawataki nikifanye, na ndio maana Usalama wa Taifa nao hawataki nikifanye.

Nikiwa bado nachungulia nje ya dirisha, nikamuona Baba Bite akiwa anaingia tena getini. Alikuwa amebeba briefcase na alipoingia akatembea kwa haraka sana kuja huku tunduni. Nikamfuatilia kwa macho na nikamuona ameenda mpaka nje ya hiki kichumba mahala ambapo maaskari wanaotulinda wamekaa.

Alipofika nikawaona kama wanasalimiana kisha akaingiza mkono mfukoni na kutoa kitu kama kitambulisho hivi mfukoni na kuwaonyesha. Ghafla wale maaskari wote nikawaona wamesimama kwa ukakamavu na kupiga saluti.

Kisha maaskari wawili, yule aliyenipeleka ofisini kwa hakimu kusomewa shtaka na mwingine mwenye silaha wakaongozana na Baba Bite mpaka mlangoni mwa hiki kichumba na kufungua.

“Haya tokeni nje” yule askari ambaye hakuwa na silaha akaamuru.

“Wewe baki ndani” akaninyooshea kidole mimi.

Wale wenzangu wote wakatoka nje nikabaki mimi peke yangu. Kisha nikamuona Baba Bite ameingia na briefcase yake na mlango ukafungwa.

“Ray, sijawahi kuona mtu mpuuzi kama wewe” Baba bite akaongea akiwa serious.

“Nilishawaambia nikijua chochote nitawasiliana na nyinyi, haya ni maisha yangu na nafanya kile ninachokiona sahihi” nikamjibu kwa kujiamini.

“Hivi unafahamu kuwa The Board hawawezi kuruhusu upate hizo taarifa unazozitaka? Na wanaweza hata kuua kabla haujazipata?” Akaniuliza huku anafungua briefcase yake.

Nikakaa kimya, sikujibu chochote.

Alipomaliza kufungua briefcase akatoa karatasi nyeupe ya A4 yenye maandishi yaliyo chapwa. Akanikabidhi mkononi.

“What is this?” Nikapokea karatasi na kumuuliza.

“Hicho kilichopo humo kitakusaidia labda kukuepusha na kifo ukiwa ndani gerezani” akanijibu

“Hakikisha unaificha isionekane ukiwa unaingia gerezani”

“Nitaifichaje wakati nasikia kabla hujaingia gerezani unasachiwa” nikamuuliza.

Baba bite akatabasamu. Tabasamu fulani hivi kama ananicheka .

“Well, wenzako wafungwa wazoefu huwa wanaficha vitu katikati ya makalio ila wanaingiza kwa ndani kidogo” akaongea huku anatabasamu zaidi kama ananicheka.

“****!!” Nikasikia kinyaa. “Na kwanini wewe na wenzako kwenye Idara mjisumbue kiasi hiki kutaka kulinda Usalama wangu gerezani, napata hisia kuwa kuna kitu haukisemi”

“Ray, bado kuna mambo mengi tunahitaji utusaidie… So wewe ni asset kwetu na kila binadamu ana haki ya kulinda asset yake” akatabasamu.

“Bullshit!” Nikamjibu kwa kukereka.

Baba bite akagonga mlango na askari aliyekuwepo nje akafungua.

“Hey, alafu mshtakiwa anataka kwenda kujisaidia.. Mpelekeni tafadhali kabla hajaenda ngomeni” Baba bite akaongea na kunikonyeza kwa kunicheka.

Nikajikuta nacheka kichini chini nikikumbuka ushauri alionipa jinsi ya kuficha ile karatasi.

“Sawa mkuu, twende mshtakiwa” yule askari akajibu.

Akanisindikiza mpaka chooni ambavyo vilikuwa karibu tu na tunduni. Akabaki nje ya mlango wa choo na mimi nikaingia ndani.

Nilichokifanya huko ndani kuficha ile karatasi siwezi kusimulia.

Nikatoka chooni baada ya kama dakika tano hivi. Wote walikuwa wananisubiri mimi. Tukapandishwa katika difenda ya polisi na safari ya kuelekea magereza ikaanza.

Gari ikanyoosha moja kwa moja mpaka ’round about’ ya mnara wa mashujaa, tukapinda kulia barabara ya ‘Old Daresalaam Road’, tukaenda kidogo kama tunaelekea kilakala na dakika kama kumi hivi tulikuwa tumeshafika Gereza Kuu la mkoa wa Morogoro.

Kwa miaka mingi niliyokuwa naishi Morogoro nimekuwa nikipita njia hii na kuliona jengo hili lenye muonekano wa kuogofya.

Jengo hili la magereza kwa muonekano wa nje lilikuwa limejengwa kwa mawe yenye rangi kama nyeusi hivi iliyo changanyika na kijani lakini imepauka sana na lilikuwa na kuta ndefu sana zilizopanda juu sana na zimewekewa nyaya za miiba. Ukiwa nje unaona miembe miwili mikubwa imechomoza ikiwa ndani ya gereza.

Nimeliona jengo hili la kutisha kwa miaka mingi lakini leo linaenda kuwa makazi yangu.

Geti kubwa likafunguliwa. Tukaingia ndani wote sita.

Pale ndani kulikuwa na kama kibaraza hivi, na mkono wa kushoto kuna chumba kile ambacho watu wanaingia wakienda kuwaona wageni na mkono wa kulia kulikuwa na mlango ambao bado sikujua kazi yake lakini nitaijua mda mchache ujao.

Tulipoingia tu hapo kwenye kama hicho kibaraza. Wenzangu wote wakachuchumaa chini. Na mimi nikachuchumaa. Kisha mmoja wa yule askari tuliyekuja naye akamkabidhi makaratasi mmoja wa maaskari magereza tuliowakuta pale.

“Kuna fresh mmoja” yule askari akamueleza yule askari magereza. Kisha akapewa likitabu fulani hivi akaandika andika na mwishoni nikamuona anatia saini.

Baada ya kukamilisha hizo taratibu yule askari tuliyekuja naye na wenzake wakaondoka. Tukabakia na maaskari magereza watatu mbele yetu.

Akachukua zile karatasi na kuanza kuita majina. Alikuwa anaita katika mfumo ambao, anasoma jina lako la kwanza pekee alafu wewe unamalizia jina lako ka kati na la mwisho na unayatamka kwa kupayuka kwa nguvu kweli kweli kisha unasimama.

Akasoma majina ya wenzangu wote watano, na jina langu mimi lilikuwa la mwisho.

“Rweyemamu!” Akasoma

“Charles Kajunaaaaaaa” nikapayuka kama wenzangu walivyofanya na kusimama.

“Wewe ndio fresh?” Akaniuliza.

“Ndio” nikajibu

“Ingia huko”

Akanionyesha ule mlango wa mkono wa kulia.

Nikafungua na kuingia ndani. Ilikuwa ni ofisi na nilimkuta askari magereza kijana wa kama makamo yangu hivi ameketi.

“Karibu” yule askari akanikaribisha.

Huyu jamaa kwa kiasi fulani alikuwa tofauti na wale maaskari magereza wengine. Akikuwa ana mwonekano fulani hivi na ‘swaga’ ya kisomi somi flani hivi. And alikuwa na kiwango kikubwa sana cha ustaarabu pengine kuzidi hata jinsi askari magereza anavyotakiwa awe.

Akanikabidhi makaratasi ya kujaza. Nikajaza majina yangu kamili, namba yangu ya kesi, kesi yangu inahusu nini, ninakoishi, jina kamili la ndugu wa karibu, anuani yake na namba yake ya simu na mwishoni nikasaini.

Akaichukua ile karatasi, akaipitia kwa makini kisha akaniuliza.

“Hivi wewe si ndiye mwenye ile nini inaitwa… Aaahh Sote! Yeah sote hub? Si ni wewe?”

“Yeah ni mimi” nikamjibu kwa kiasi fulani huku najisikia aibu.

“Aisee, pole sana kiongozi yataisha haya! Ndio maisha”

“Nashukuru sana”

Akanionyesha nifungue mlango mwingine wa kutokea tofauti na ule niliotumia kuingilia. Nikafungua na kutokea kwenye chumba kingine na sekunde chache wale mahabusu wengine wakiwa na wale maaskari magerez nao wakaingia.

Hiki chumba kilijuwa kimeungana chumba kingine lakini hakukuwa na mlango kati kati.

Yaani kilijengwa katika mtindo ambao kulikuwa na vyumba viwili vinavyopakana lakini havikuwa na mlango wa kufungua, unapita tu na kuingia chumba kinachofuata.

Tukiwa pale kwenye kile chumba cha kwanza nikaona wenzangu wanaanza kuvua nguo. Na mimi nikafuatisha. Tukavua nguo zote na kubaki uchi kabisa.

Ingawa wote tulikuwa wanaume lakini hakuna kitu kinachokera kama kuwa kwenye kundi la wanaume wenzako mkiwa uchi. Inakera haswa.

Wengine sijui hawajanyoa wana miezi mingapi, wengine maumbile makubwa kama waigizaji wa filamu za ngono, wengine maumbile madogo yamesinyaa utadhani nyanya chungu za juzi. Ili mradi ni kero tu. Nilitamani kujifunika uume wangu kwa mikono kama mtoto.

Wenzangu walikuwa kawaida tu, inaonekana wamezoea hili zoezi.

“Haya twende” askari mmoja akaamuru.

Nikaona mahabusu mmoja ameingia kwenye kile chumba kinachofuata kisha baada ya muda sauti ya mlango huko kwenye chumba hicho unasikika unafunguliwa na huyo maabusu anaondoka. “Mwingine” anaita huyo mtu aliyeko kwenye chumba cha pili.

Wote wakafuata utaratibu huo na mimi nikawa wa mwisho.

Nikaingia uchi na nguo zangu nimeshikilia mkononi. Kwenye hicho kichumba kulikuwa na askari kijana tu ila ana sura chungu kweli kweli ya kibandidu amekaa kwenye kiti na kuna meza mbele yake. Chumba kizima hakukuwa na kabati la ofisi wala taka taka yoyote ile. Kulikuwa na kiti na meza ndogo tu na huyu askari aliyekaa. Nikafika nimesimama tu namwangalia.

“Unashangaa nini wewe , lete nguo hizo” akafoka yule askari.

Nikaweka nguo zangu juu ya meza. Akaanza kuzikagua. Akasachi mifukoni, akakagua kwenye pindo za nguo, kisha akaikung’uta kung’uta mara kadhaa, alipomaliza akazitupa sakafuni.

“Geuka” akaniamuru.

Nikageuka.

“Inama” akaniamuru tena.

Nikasita. ‘Huyu ukaguzi gani huu’! Nikajisemea kimoyo moyo.

Sikutaka matatizo. Nikainama.

Alikuwa bado amekaa pale kwenye kiti nyuma ya meza. Nikamchungulia kwa chini nikiwa nimeinama. Nikamuona yuko makini sana “kunikagua”.

“Panua matako” nikamsikia ananiamuru.

Nikajikuta ghafla nimeshikwa na hasira iliyochanganyika na hofu. Pia nikakumbuka huko ninakoambiwa nipanue nimeficha karatasi niliyopewa na Baba Bite. Nisipofanya kitu hapa nitaumbuka na kujiingiza kwenye matatizo mengine

Nikainuka kwa hasira.

“Huku sio kunisachi sasa, huu ni udhalilishaji!!” Nikaongea kwa hasira kwa sauti ya juu.

Yule askari akainuka haraka kutoka kwenye kiti akiwa amefura kwa hasiara.

“Unasemaje wewe !!” Akafoka.

“Huu udhalilishaji, sio ukaguzi huu” nikavimba.

“Skia we , hii jela! Unaskia, usiniletee usenge usenge wako wa haki za binadamu, hii jela!! Nikikwambia lala unalala, nikikwambia kaa chini, unakaa chini, nikikwambia simama unasimama, nikikwambia panua matako, una panua matako!!” Yule askari akafoka kwa hasira huku amefura ananisogelea pale niliposimama.

Moja wapo ya mbinu za kumkabili adui ni kamwe kutokumuonesha hofu yako. Kwa hiyo na mimi nikamvimbia. Sikusogea hata hatua moja nyuma. Nikamtazama usoni kwa hasira huku ‘nimevimba’.

“Unaskia we , nikikwambia panua matako unafanyaje?” Akaniuliza kwa kufoka.

“Ukinambia panua matako nakwambia panua wewe kwanza!!” Nikamjibu kwa hasira na kufoka kwa sauti ya juu.

Akanishtukiza kwa kofi zito shavuni. Lilikuwa kofi kali mpaka nikajiinamia kwa maumivu. Mara nikasikia ‘kifuti’ kikali amenipiga mbavuni. Nikadondoka chini kuugulia maumivu.

“Nitakuumiza wewe **** wewe! Nitakuumiza!!” Akafoka kwa hasira huku ananipiga mateke ya mbavuni pale chini nilipo lala.

Nikasikia maaskari wengine wanaingia.

“Hey, hey, hey, hebu muacheni” nikasikia askari mmoja ana waamuru.

“Mseng* huyu hataki kukaguliwa anatuletea ujuaji!!” Akafoka yule askari bandidu aliyenipiga.

“Ni mgeni hajui utaratibu! Hebu tokeni nitamkagua Mimi msije kuleta balaa hapa” yule askari mwingine akawamuru.

Nikamuangalia vizuri, alikuwa ni yule askari mwenye “swaga za kisomi” aliye niandikisha maelezo yangu kwenye chumba kingine kile.

Wale askari wengine wakaondoka kwa hasira. Nikajiinua na kukaa sakafuni. Bado niko uchi.

“Inuka uvae” yule askari akaniamuru.

Nikasimama huku naugulia maumivu na kuanza kuvaa.

“Dogo, hii sehemu hatari sana! Usijifanye mjuaji utaumia!!”

“Sorry! Nashukuru kwa kuniokoa kiongozi” nikamjibu kwa sauti ya maumivu huku navaa.

“Usijali! Unasaidia vijana wengi huko uraiani kwahiyo wewe ni asset na asset inapaswa kulindwa!”

Nilikuwa nafunga mkanda nikajikuta nimeganda kama sanamu. Hii ilikuwa ni bahati mbaya au ameongea sentesi hii kwa makusudi? “wewe ni asset na asset inapaswa kulindwa”!!

Nusu saa iliyopita Baba bite ametoka kunambia sentesi inayofanana kabisa na hii. Na huyu anakuja kuniokoa na kutamka sentesi kama hiyo! Ni bahati mbaya au amefanya kusudi?

Nikainua kichwa kumtazama. Tukakaziana macho kama sekunde thelathini hakuna aliye pepesa macho.

Kisha akatabasamu. Pembeni ya hiki chumba kulikuwa na mlango mkubwa kama geti. Akaenda mpaka hapo mlangoni na kunifungulia.

“Kilala kheri” akaongea akinionyesha ishara nitoke kwenye chumba na kuingia rasmi gerezani.

Sikujibu chochote. Nikamuitikia kwa kichwa tu. Nikapita mlangoni na kutokea upande wa pili. Gereni kwenyewe. Sasa nilikuwa nimekanyaga rasmi gerezani.

Watu wanaona jinsi gereza linavyoogopesha kwa nje ukilitizama, lakini kitu wasichofahamu ni kwamba hakuna kitu chenye kuogofya kama muonekank wa gereza kwa ndani.

Nikavuta pumzi kubwa ndani na kuitoa nje. Sasa umefika wakati wa kuikabili ‘jehanum’ iliyoko mbele yangu.

Nilibaki nimesimama pale nilipo kwa dakika kadhaa nikiangalia kilichopo mbele yangu.

Nilikuwa ndani ya gereza kwa mara yangu ya kwanza kwenye maisha. Nilihisi kama niko ndotoni.

Mbele yangu niliona vyumba vikubwa kama ‘halls’ vitatu. Moja kilikwa mkono wangu wa kushoto na vingine viwili mbele yangu. Kati kati kulikuwa na uwanja mkubwa. Pia mbele yangu kulia kidogo kulikuwa na chumba kingine kikubwa ambacho kutokana na moshi pamoja shughuli zilizokuwa zinaendelea nikaelewa kuwa lilikuwa ni jiko.

Nikajiuliza wafungwa na mahabusu wako wapi?

Maana mbele yangu pale katikati kwenye nafasi kubwa kama uwanja ambao chini imemwagwa sakafu ya zege kulikuwa na Nguo nyingi zimetandazwa chini zimeanikwa. Kulikuwa na sare za kifungwa na nyingine nguo za kiraia, lakini mbele yangu niliona kama wafungwa na mahabusu 15 pekee wote wakiwa bize kufanya shughuli hii ama ile pale jikoni.

Ila mkono wangu wa kulia kulikuwa na liukuta likubwa sana la mawe lenye mlango mdogo ambao ulikuwa wazi.

Nikarudisha tena macho yangu kwenye ‘jiko’. Moshi mzito wa kuni ulikuwa unatoka na kutengeneza kama wingu zito na ‘wapishi’ wenyewe walikuwa hawajali, inaonekana wamezoea hali hii. Walikuwa wanakohoa na kuendelea na wanachokifanya.

Nikajiuliza tena. Wafungwa na mahabusu wako wapi.

“Hahahahahah siamini macho yangu”

Nikasikia mtu upande wangu wa Julia anacheka. Nikageuka kumuangalia.

Godi.

“Siamini macho yangu kama umekuja huku”

Godi akaongea na kunifuata mpaka pale nilipokuwa nimesimama.

“Nilikuwaa yard huko, niliposikia watu wamerudi kutoka mahakamani, nikasema ngoja nije nione kama kuna mgeni na kama yuko ninaye mfahamu, lakini sikutegemea uwe ni wewe aisee hahahah”

Godi akaongea na alikuwa ameshafika pale nilipokuwa nimesimama.

“Karibu sana gerezani, jisikie uko nyumbani!”

“Asante, ila nyumbani kwetu hakuna jiko la namna hii kama tuko karne ya 18” nikamjibu kwa utani huku namuonyesha kidole kule jikoni.

“Ooohh usijali kila mtu siku ya kwanza analionaga hilo jiko lina kera kama liko miaka 100 nyuma lakini baada ya wiki tu utaanza kuliona kama Sheraton” Godi akaongea huku anatabasamu.

“Wafungwa wako wapi? Mbona sioni mtu zaidi ya wale jikoni sijui ndio wapishi” Nikamuuliza.

“Ooh hili eneo haliruhusiwi kukaa mida hii. Wafungwa wote na mahabusu wako yard mda huu” akaongea akinionyesha kidole kile kimlango kidogo kwenye lile liukuta likubwa mkono wetu wa kulia.

“Ile pale unayoiona” akanyoosha kidole moja vyumba vikubwa vile kama ‘hall’ mkono wetu wa kushoto, “ile ni selo ‘namba moja kubwa’ au tunaiutaga reception. Humo wanalala wagonjwa wa akili lakini pia na wageni kama nyinyi mkija siku za kwanza kwanza. So nisipofanya miujiza yangu leo maana yake utapangiwa kulala mle.”

Akaongea huku anatabasamu kwa kujidai.

“Ile pale ni ‘selo namba mbili kubwa'” akaoonya kidole kwenye chumba kikubwa sana kati ya vile vitatu.

“Hii tunaiita ‘selo ya waislamu’. Hii ndio moja ya selo za kistaarabu zaidi lakini wanaolala humo wengi ni waislamu so kila mda wa swala inabidi mjumuike kuswali”

Akanielezea huku tumeanza kutembea kuelekea kwenye kile kimlango kidogo kwenye liukuta likubwa.

“Ile pale ni ‘selo namba tatu kubwa’ au tunaiita selo ya walokole” akanionyesha chumba kikubwa cha Tatu ambacho kimepakana na jiko.

“Humo wanaolala wengi ni walokole, kwahiyo usiku mapambio kwa sana na kunena kwa lugha hahahah” akaongea huku anacheka. Tulikuwa tume karibia kabisa kile kimlango kwenye liukuta.

“Hizo selo nilizokuonyesha kila moja wanalala wafungwa kama 40 hivi, lakini pia huku yard tunakoenda kuna ‘selo ndogo’ kama 70 hivi na kila selo moja wanalala wafungwa watano”

Akanieleza na tulikuwa tumefika kwenye kile kimlango kwenye liukuta.

Tukaingia kwenye kile kimlango na kutokea upande wa pili.

Kulikuwa na kama uwanja mkubwa ambao chini pia ulikuwa na sakafu ya zege. Uwanja huu ulikuwa umezungukwa na vyumba vidogo vidogo vilivyo ungana na kutengeneza umbo la ‘U’. Lakini kwa hesabu ya haraka haraka vile vyumba vilikuwa havifiki sabini kama Godi alivyonieleza.

“Hii ni yard ya kwanza! Ya pili iko nyuma huko” akaongea akinionyesha ishara kuwa nyuma ya msululu wa selo zilizo kuwa mbele yetu kuna yard nyingine.

Katikati ya huu uwanja uliozungukwa na selo, au yard kama wenyewe wanavyoita humu gerezani, kulikuwa na mwembe mkubwa katikati. Nikakumbuka huu ni moja ya miembe ambayo inaonekana ukiwa nje ya gereza.

Kuna watu kadhaa walikuwa wameketi kuzunguka huu mwembe. Kuna mzee mmoja wa makamo nilimuona yeye kuna vitu anashona shona na sindano ya mkono, siku za baadae nikaja kuelewa kuwa ndio alikuwa “fundi cherehani” wa gereza ingawa hakuwa na cherehani.

Pembeni yake walikuwa wameketi wafungwa kadhaa wanacheza drafti.

Sehemu ya mbele kabisa ya hii yard kulikuwa na televisheni imewekwa juu ya meza na kulikuwa na wafungwa wengi wamejikusanya wamekaa chini sakafuni wanaangalia.

Katika kila karibia mlango wa hizi selo ambazo zote niliona zilikuwa zimefungwa, kulikuwa na wafungwa wamekaa chini wanapiga stori.

Kitu kingine nilichokigundua kwa haraka kwenye hizi selo ni kwamba hazikuwa na madirisha.

Zilikuwa na milango ya Chuma iliyopakwa rangi ya kijani na katika hiyo milango ndio kulikuwa na vidirisha vidogo sana.

Nyuma kabisa ya hii yard kulikuwa na wafungwa na mahabusu ambao kwa muonekano walikuwa ni ‘mabandidu’ haswa wamekalia ndoo za maji wanapiga stori na baadhi yao ‘wanatuchora’ mimi na Godi anavyoniongoza kwenye hii ‘tour’.

Tukaondoka kutoka kwenye hii yard na kwenda kuangalia yard nyingine ambayo iko kwa nyuma.

Tukaenda mpaka nyuma kabisa ya yard walipokaa wale ‘mabandidu’ kuna uchochoro mpana sana ambao pia unatumika kama ‘bafu’ tukapita hapo na kutokea yard ya pili iliyoko nyuma.

Hii ilikuwa inafanana kabisa na ile yard ya kwanza. Ilikuwa na uwanja mpana wenye sakafu ya zege, katikati kulikuwa na mwembe mkubwa. Pia, Selo za vyumba vidogo vidogo vilivyoungana kutengeneza umbo la herufi ‘U’.

Lakini yard hii haikuwa na televisheni kule mbele. Badala yake pale mbele kulikuwa na ukuta wenye geti la kijani.

“Kule kuna nini?” Nikamuuliza Godi nikimuonyesha ule ukuta mbele ya yard wenye geti.

“Ooh kule ni kondemu (condemn)”

“Kama ikitokea mahabusu akihukumiwa kifungo cha maisha au kunyongwa, anatengwa na mahabusu na wafungwa wengine unao waona hapa. Anafungiwa kule ndani kwenye lile geti unaloliona, ndani yake kuna selo kama tano hivi. Kwahiyo anakuwa anahifadhiwa humo mpaka atakapokuja kuchukuliwa kupelekwa kwenye gereza lao maalumu liko dodoma linaitwa Isanga.”

Godi akanieleza huku tuna tembea tembea pale kwenye yard.

“Kwahiyo ikitokea hakuna aliyehukumiwa kifungo cha maisha au kunyongwa, hizo selo zinakaa hivyo tu hata mwaka mzima?” Nikamuuliza.

“Hapana! Pia huwa wanawahifadhi mahabusu na wafungwa maalumu! Uliwahi kusikia wale watu waliokamatwa kilombero wakihusishwa na ugaidi kwamba wameweka kambi msituni wanajifunza ugaidi?” Akaniuliza.

“Yes! Nakumbuka nilisikiaga” nikamjibu.

“Sasa mahabusu maalumu kama hao ambao hawatakiwi wachanganyike na wengine wanawekwa kule kondemu. Pia kuna mahabusu kama hawa akina shehe Juma Kassim pia wanawekwaga huko”

Akanieleza akinipa mfano wa sheikh Juma Kasimu ambaye mihadhara yake imekuwa ikimfanya aingie kwenye mgogoro na serikali mara kwa mara na kumfanya awe na kesi mfululizo zisizoisha. Kiasi nikawa nimemuelewa Godi anachonieleza.

“Vipi umekujaje humu mwenzangu?” Godi akanieleza huku tunatembea tembea pale yard.

“Kujaje kivipi?” Nikamuuliza.

“Hujaficha hata hela kidogo kuingia nayo?”

Akaniuliza. Lakini alipotaja kuhusu kuficha hela nikakumbuka karatasi ‘niliyoficha’.

“Hapana sijaficha hela yoyote! Kwani tunahitaji hela humu? Maana sijaona duka wala soko! Alafu tumbo silielewi elewi hebu nielekeze chooni” Nikamjibu huku nikidanganya kutaka kwenda kujisaidia ili nikatoe ile karatasi niliyoificha.

“Unahitaji hela humu kuliko unavyohitaji oksijeni! Na hiyo haja yako hebu ibane mpaka tukiingia selo kulala! Vyoo vya nje huku majanga tupu, kwanza vichafu alafu na hivi wanakujua mgeni wanaweza kukuweka mtu kati wakakufanyia kitu mbaya”

Godi akaongea huku anapepesa macho pale yard huku na huko kama kuna mtu anamtafuta.

“Mpaka mda wa kulala? Yani nikae na haja mpaka usiku mda wa kulala? Acha utani?” Nikamjibu kwa mshangao nikishangazwa na na pendekezo lake ati nisubiri mda wa kulala.

“Hahahaha! Humu kulala ni saa kumi kijana, na kwa makisio hii inakaribia kabisa saa tisa” akanijibu bila kuniangalia huku anaendelea kupepesa macho pale kwenye yard.

“Jesus Christ! Saa kumi? Hata usingizi unakuja kweli? Unatafuta nini alafu mbona unatazama tazama?”

“Nimekumbuka inabidi nifanye miujiza yangu tupate sehemu nzuri ya kulala. Hebu nisubiri hapa nakuja dakika sifuri!” Akaongea akinionyesha nikae chini kwenye mwembe kisha akaondoka kulekea yard ya kwanza kule tuliyotoka.

Nikakaa chini kwenye sakafu ya zege pale kwenye mwembe.

Nikatafakari mambo kadha wa kadha. Jambo moja ambalo lilikuwa linanitatiza kichwani ni kwamba tumetembea kwenye yard zote mbili lakini sikufanikiwa kumuona Eric Kaburu. Kwanini? Yuko wapi?

Kingine kilichonitatiza ni jinsi gani nitakavyoweza kumshawishi anipe siri nzito ambazo naamini kuwa anazo kuhusu The Board. Hivi nikionana naye nitamweleza kitu gani?

Nikawaza pia kama Isaack na Cheupe wataweza kupata kitu chochote kwenye uchunguzi wao wa Kaburu ambacho kitaweza kunisaidia kumshawishi aongee na mimi.

Pia nikawaza hiki kikaratasi nilichopewa na Baba bite kinahusu nini??

Nikawaza na kuwaza.

Nikaanza kumuwaza Cheupe wangu. Ni Mungu pekee ndiye anajua kiasi nilichommiss.. Nilitamani nimchukue twende tukaishi kwenye sayari nyingine kabisa kuepuka hizi heka heka, migogoro na mkanganyiko.

Dammmnn nimemiss Cheupe wangu.

Nikafumba macho kwa hisia kumuwaza cheupe.

“Oyo! Twende huku!” Godi alinishtua kutoka kwenye kutafakari kwangu.

Nikainuka na kumfuata. Tukaelekea mpaka kwenye uchochoro ule mpana tuliotumia kuingilia huku yard ya pili.

Hapo tukamkuta jamaa fulani hivi mrefu na ana mwili mkubwa wa mazoezi. Alikuwa amevaa Nguo za kifungwa lakini tofauti na wafungwa wengine yeye alikuwa na mkanda kiunoni.

Ingawa hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuingia gerezani lakini nikaelewa kuwa huyu atakuwa ni Nyapala.

“Huyu ndo mwenzako?” jamaa akauliza kitemi.

“Ndio huyu” Godi akamjibu.

“Kwahiyo mnataka selo namba mbili kubwa si ndio?” Akaukiza tena.

“Ndio hivyo Mkuu” Godi akajibu tena kistaarabj tofauti kabisa na kawaida yake.

Jamaa hakuongea tena chochote. Mkononi alikuwa na kifuko fulani hivi cheusi. Akatoa vipande kadhaa vya sabuni akanikabidhi mimi vitano Godi akampa vitano.

Sasa wadogo zangu ole wenu hiyo jumapili nisipate hiyo elfu kumi ndio mtajua uchungu wa jela” jamaa akaongea serious huku anaondoka.

“Utapata mkuu usijali” Godi akajibu tena kistaarabu kabisa kiasi sijawahi kumuona.

Tukaondoka tena na kurudi yard ya pili.

“Whaaaatt!! Are you crazy?? Tunaitoa wapi hiyo elfu kumi sina hata shilingi mia” nikammaindi.

“Wewe nawe hebu niachie vingereza vyako, ndio uchekeche akili sasa ujue tunaipataje?” Godi akanijibu kwa kutojali hatari ya alichokifanya kama kawaida yake.

“Kwanza sabuni zote hizi za nini umemwambia atupe? Mimi sihitaji sabuni zote hizi nguo pekee nilizonazo ni hizi nilizo vaa, misabuni yote hii ya nini?” Nikaongea kwa kekereka.

“Acha ubwege. Hizo sabuni ni sawa na hela humu! Humu jela unanunua kitu kwa kutumia hela yenyewe au unatumia sabuni. Mfano hapa wote hatujala tumechelewa msosi wa jela umetupita, so itabidi tufanye mpango baadae tutumie sabuni kadhaa kununua belenge moja la ugali.!” Godi akaongea.

“Belenge? Ndio kitu gani”

“Tuliza mshono mtoto wa kike! Utaona hapo hapo”

“****!”

“Mwenyewe”

Tukajikuta tunacheka tu na ile taharuki ikayeyuka. Tukaendelea kidogo na stori, mara ghafla tukamuona yule nyapala anapita anapayuka….

“Kaba selooooooooo! Kaba selooooooooo”

Watu wakaanza kunyanyuka na kutembea haraka haraka huku na huku.

“Muda wa kulala huo!” Godi akaongea huku anatabsamu.

“Ndio inaitwa ‘kaba selo'” nikamuuliza huku nanyanyuka.

“Yeah! Ukisikia wanatangaza ‘kaba selooooo’ unatakiwa ukasimame mbele ya selo yako.” Godi akaongea huku anamuigiza kikomedi yule nyapala anavyopayuka ‘kaba selooooo’.

Tukainuka na kuelekea yard ya kwanza kisha tukatoka na kile kimlango kidogo mpaka upande uke mwingine wa gereza wenye jiko.

Kwa mujibu wa Godi hapa ndipo wageni inabidi msubirie nyapala aje kuwapangia selo ya kulala.

Wafungwa na mahabusu ambao walikuwa wanalala kwenye ‘selo kubwa’ zilizoko upande huu wa gereza nao tuliwakuta wamejipanga nje ya selo zao namba moja kubwa, mbili kubwa na selo namba tatu kubwa. Wote walikuwa wamevua mashati na kuchuchumaa.

Kama dakika kumi baadae yule nyapala akaja pale tuliposimama na kutuambia twende selo namba mbili kubwa.

Hakukumbusha chochote kuhusu ‘hela yake’ Godi aliyoahidi jumapili tutampa. Alituongelesha kana kwamba hatujaongea kabisa hapo kabla.

Tukaenda kupanga mstari na kuchuchumaa nje ya selo namba mbili kubwa tukiwa tumevua mashati kama wenzetu.

Tukiwa tumechuchumaa pale pale chini nikaona nimuulize Godi swali lililokuwa linanitatiza kichwani.

“Oi! Kuna mtu nimejaribu kupepesa sana macho lakini sijamuona na nina fahamu yuko gereza hili”

“Nani?” Godi akaniuliza.

“Eric Kaburu” nikamjibu.

Godi hakusema chochote akabakia kimya tu.

“Yupo humu kweli?” Nikamuuliza.

“Yupo! Una shida naye gani?” Godi akajibu bila uchangamfu na kwa kiasi fulani alikuwa na wasi wasi kwa mbali.

“Nimeuliza tu” nikamjibu.

Hakusema chochote. Akakaa kimya tu. Ila nilihisi jinsi hofu fulani ilivyomuingia nilipomtajia jina la Eric Kaburu.

Kule mbele ya mstari askari magereza alikuwa anatuhesabu na kisha ukishahesabiwa unainuka unaingia ndani ya selo. Ni kama vile ng’ombe wanavyohesabiwa jioni wakirudi zizini.

Nami nikahesabiwa. Nikasimama na kuingia ndani ya selo.

Siku ilikuwa imeisha. Sasa yanipasa niwe na mkakati wa kumsaka Eric Kaburu kesho na nijaribu kuzungumza naye.

Sikujua kwanini lakini ile hofu niliyoiona usoni kwa Godi nilipomtajia jina la Eric Kaburu, ilinitisha. Nikamuomba Mungu awe nami.

GEREZA KUU LA MKOA, MOROGORO.

SIKU YA KWANZA

Ilikuwa yapata saa kumi na mbili asubuhi. Mda mchache uliopita waumini wa kiislamu ndani ya selo walikuwa wamemaliza kuswali na sasa watu walikuwa wamekaa kwenye magodoro wanapiga stori tunasubiri kuja kufunguliwa selo tuelekew yard ili kuanza siku nyingine ndani ya gereza.

Selo yetu ambayo ni ‘Namba 2 kubwa’ ilikuwa na urefu wa takribani kama mita nane kwa urefu na mita tatu upana.

Jana jioni saa kumi tulivyoingia nilimuona nyapala wa selo amendika mlangoni 53. Akimaanisha kuwa jumla ya wafungwa na mahabusu 53 siku hiyo tumefungiwa ndani ya selo namba mbili kubwa.

Wafungwa na mahabusu wote isipokuwa manyapara tulikuwa tunalalia godoro moja watu wawili. Godoro lilikuwa na ukubwa wa kama inch tatu kwa tank hivi.

Mimi na Godi tulishea godoro moja na staili rasmi ya wafungwa wote kulala ni ‘mzungu wa nne’.

Usiku wa jana nilikuwa nimeenda chooni kilichopo ndani ya Selo na kuitoa ile karatasi niliyopewa na Baba Bite. (Kwa mara nyingine, siwezi kamwe kuelezea namna nilivyoitoa).

Nilisoma kilichopo ndani, na ingawa siku kielewa lakini yanipasa kukifanyia kazi kama Baba Bite alivyonieleza kuwa “itanisaidia kusurvive humu ndani.”

Toka jana mda tunaingia ndani ya selo nilipomuuliza Godi kuhusu Eric Kaburu, kwa kiasi fulani alikuwa amenichunia na hataki kabisa maongezi na mimi.

Watu walikuwa wanapiga soga kila upande lakini mimi na Godi tulikuwa kila mtu yuko kwenye dimbwi la mawazo.

Nikaona nivunje ukimya.

“Braza naona toka jana nikutajie jina la Kaburu, umebadilika kabisa! Ingekuwa poa ukinidokeza hata kidofo hofu yako ni nini badala ya kuninunia kama mtoto wa kike” nikamueleza kwa sauti ya kihuni Fulani hivi, jela ilikuwa imeanza kunikaa kwenye damu.

“Sitakueleza hofu yangu ni nini, ila nitakuonyesha!” Godi akaongea akiwa serious kweli kweli bila kuniangalia usoni.

“Una maana gani??” Nikamuuliza kwa mshangao.

Hakunijibu chochote akaendelea kukaa kimya tu anaangalia pembeni.

Mara nikamsikia Nyapara wa selo anaongea kama anatangaza kwenye kipaza sauti, “kaa kwenye mstari weweeeeeee, kaa kwenye mstariiiiiii.”

Wafungwa wote na mahabusu tukainuka na kupanga mstari kuelekea mlangoni.

Kisha akaja askari magereza akasimama kule mbele mlangoni baada ya kuufungua. Na kama jana jioni tukaanza kuhesabiwa tena kama ng’ombe tunatoka zizini.

“Mda wa mazoezi ya viungo huu na mchakachaka, tukimakiza kabla ya kunywa uji nitakuonyesha kwanini sitaki kumuongelea Kaburu!” Godi akaongea huku anatembea bila kuniangalia mara tu tulipotoka ndani ya selo.

Tukaelekea mpaka kule kwenye yard ya pili, kwenye uwanja mkubwa ambako hakuna TV. Tukawakuta wafungwa wanaolala selo ndogo wote wameshafunguliwa milango na wako yard wanakimbia mchaka mchaka kuuzunguka mwembe.

Utaratibu ni kwamba ukifika tu pale na wewe ‘unaunga tela’ kukimbia mchaka mchaka. Mbele alikuwa ametangulia askari magereza anaimbisha na wafungwa wanaitikia.

Yule askari alikuwa anaimbisha wimbo ambao ulinikumbusha mbali sana, enzi za utoto.

“Zaina zainaaaaaaa”

“Zainaaaaaaaaaaaa” wafungwa wanaitikia.

“Zainabu wanguuuuuuu”

“Zainaaaaaaaaaaaa” wafungwa wanaitikia tena.

“Mtoto wa kihayaaaaaaaaa”

“Zainaaaaaaa! Lete raha zainaaaaa!!” Wafungwa.

“Ukimuona zainaaaaaaa”

“Zainaaaaaaaaaaa”

“Mtoto ziwa konziiiiiiiii” askari magereza anaweka mbwembwe. Na wafungwa wanaitikia kwa furaha “lete raha zainaaaaaaa.”

Mimi, Godi na wafungwa wenzetu tunaolala selo kubwa tulifika pale yard yapata kama saa kumi na mbili na dakika kumi hivi na tukaungana na wenzetu kwenye mchaka mchaka huo kwa takribani dakika ishirini hivi tukizunguka pale yard na kuuzunguka mwembe.

Baa ya hizo dakika ishirini za mchaka mchaka wote tukakusanyika mbele ya ule mwembe ambapo kulikuwa na kama ‘kibaraza’ hivi kimejengwa kimeinuka juu kidogo na yule askari akapanda pale juu ya kibaraza na kuanza kuimbisha nyimbo za “kijeshi”.

Alipokuwa anaimbisha tulikuwa tumejipanga kama vile wanafunzi wako ‘assemble’ na tulikuwa tunaimba huku tunaruka kama wanajeshi kweli kweli.

Kukupa picha kamili, niseme kwamba naamini umewahi kuona jinsi wanajeshi wale ‘makomando’ kwenye sherehe za Uhuru pale uwanja wa taifa wakimaliza ‘show’ yao ya kuvunja mawe kwa kichwa na kulala juu ya misumali (sijui ukomando wa wapi huu?? Kama mazingaombwe!!) Huwa wanapita mbelw ya rais na wageni waalikwa jukwaa kuu wakiruka ruka kama wanakimbia. Basi hicho ndicho nasi tulikuwa tunakifanya hapa jela kwenye haya mazoezi. Tulikuwa tunaruka ruka kama makomando wa uwanja wa taifa huku nyimbo za halaiki zinaimbwa na yule askari magereza.

“Arereeeeeeeeeeee”

“Haiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii” wafungwa wanaitikia

“Arereeeeeeeeeeee”

“Haiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii”

“Chini kuna motooooo”

“Kanyagaaaaaaaaaaa” wafungwa wanaotikia.

“Chini kuna motooooooooo”

“Kanyagaaaaaaaaaaaa”

Hiyo mkiimba “kanyagaaaaa” unatakiwa unyanyue mguu juu kweli kweli kama komando kweli. Uzuri mimi ni mtu wa mazoezi kwahiyo nikawa nanyanyua mguu karibu ufike kidevuni.

Wakati huo maaskari wengine wanakuwa wanapita pita huku na huko kuangalia wafungwa wanaotegea. Kwahiyo kila baada ya sekunde chache unasikia “paaaaaaaaahh”. Mtu amepigwa “salala” kama wanavyoita gerezani, kofi la haja la mgongoni mpaka unasikia kama ngozi inabanduka.

Nilichokuja kugundua muda huu wa mazoezi ndio moja ya muda unaopendwa sana na wafungwa. Kwani kwa kuangalia tu nyuso za watu walikuwa na furaha na kwa muda mchache walikuwa wamesahau kuwa “hawana maisha” kwa maana ya maisha. Na mimi nikaanza kusikia kifuraha fulani hivi kinaniingia na sikupenda kabisa, lakini nilishindwa kujizuia. Aliyeanzisha huu mfumo wa mchaka mchaka na mazoezi gerezani ni ‘genius’ anastahili nishani ya heshima. Msongo unaondoka kwa mfungwa bila mwenyewe kutaka.

Baada ya yule askari kumaliza kutuimbisha kijeshi akapanda askari mwingine mfupi hivi mwenye mbwembwe kibao na alivyopanda tu wafungwa wakaanza kushangilia. Huyu askari nilikuja kumfahamu hapo baadae kuw anaitwa jina la utani ‘Msauzi’ na alikuja kunisaidia sana huko mbeleni kutimiza azma yangu iliyonileta humu gerezani.

Msauzi akaanza mbwembwe zake.

“Wiiiiiiiiiiiiiiiii”

“Waaaaaaaaaaaaaaa” wafungwa wakaitikia.

Akaanza kuimbisha nyimbo zake za “kihuni”.

“Ptruuuuuuuuuu wekaaaa”

“Wekaaaaaaaaaaaaa” wafungwa wakalipuka na kujibu kwa sauti.

“Niweke vodaaaaaa??”

“Wekaaaaaaaaa” wafungwa wanaitikia.

“Niweke zeniiiiiiiiiii??”

“Wekaaaaaaaaaaa”

“Niweke tigoooooooo??”

“Aaaaaaaaaaaaaaahh” wafungwa wanakataa kuitikia kwa utani.

Kisha anaanza tena mwanzo. Akaimbisha hizi nyimbo za “kihuni” kwa karibia robo saa, na kwakweli nilisikia raha sana. Umepita mda mrefu tangu nijihisi kufanya “uhuni” walau kidogo. Roho yangu ikasuuzikasijakaa,

Baada ya ‘mchaka mchaka’ na mazoezi kuisha watu wakaanza kujiandaa kwenda kunywa uji.

Tukarudi mpaka kule jikoni upande wenye selo kubwa. Nikachukua kikombe cha bati kama wenzangu na kupanga foleni, kisha nikawekewa uji wangu wa dona, na ninaposema dona ni dona kweli kweli, uji hata rangi yake sijui ni rangi gani. Chukua njano changanya na nyeusi rangi utakayopata ndiyo hiyo hiyo niliyokuwa naiona kwenye kikombe changu cha uji.

Baada ya kuwekewa uji nikarudi yard namba mbili kule kutafuta sehemu ya kukaa niburudike na kifungua kinywa chabgu huku kichwani nikipanga nifanye mini.

Nilipofika yard kabla sijakaa chani, ghafla nikamuona Godi anakuja kwa kasi pale nilipo.

“Twende” akaongea huku anatembea haraka haraka bila kuniangalia.

“Twende wapi?” Nikamjibu bila kunyanyua hatua hata moja.

Akagueka na kunifata kwa kasi mpaka pale nilipo.

“Uliniuliza kwanini nilikuwa na hofu uliponitajia jina la Kaburu, nikakwambia sitakwambia kwanini Bali nitakuonyesha! So twende nikuonyeshe kwanini sitaki kusikia hill jina” akaongea kwa hasira huku anageuka na kuanz kuondoka.

Nikaweka kikombe cha uji chini na kuanza kumfuata.

Tukaelekea mpaka kwenye ule ‘uchochoro’ ambao ukipita unatokea yard ya kwanza, uchochoro ambao pia unatumika kama bafu.

Tulipofika hapo akasimama. Tulikuwa peke yetu.

“Umeona pale!” Akanionyesha mahali Fulani ukutani.

“Sioni kitu naona ukuta tu na ukungu wa kijani” nikamjibu. Nilijitahidi kukaza macho ukutani lakini kitu pekee nilichokiona ni ukungu wa kijani uliotokana na watu kuoga mahali hapo.

“Angalia pale juu kidogo”

Nikatazama kwa umakini zaidi. Kuna sehemu ilikuwa na kama alama kubwa nyekundu ambayo imebadilika kiasi na kuwa kama nyeusi kutokana na kukaa muda mrefu.

“Yeah nimeona kama damu hivi nahisi”

“Sio unahisi, hiyo ni damu! Damu ya binadamu” akanijibu huku ananiangalia kwa hasira. “Sogea cheki na hapa” akanionyesha sehemu nyingine kwenye kona ya ukuta inapokutana na ukuta mwingine.

“Umeona hapa?” Akanionyesha.

Sehemu ya chini kidogo kulikuwa na alama kubwa ya kama kitu kimechuruzika ukutani.

“Nahisi ni damu pia”

“Pimbi wewe, sio unahisi! Hiyo ni damu! Damu ya binadamu!” Akanijibu tena huku ananiangalia kwa hasira.

“Unaweza ukanambia kwanini unanionyesha damu za binadamu?” Nikamuuliza kwa hofu.

“Ile damu pale juu maiti ya mfungwa ilikutwa hapa mwaka mmoja uliopita! Inaonekana kuna mtu alimuinua juu juu na kumbamiza Kisogo ukutani mpaka akafa!” Akaongea kwa jazba. “Hiyo damu hapo chini miezi mitatu au minne iliyopita nikiwa humu humu jela, mfungwa mwingine alikutwa amechinjwa na mzoga wake umeegemezwa hapo hapo ukutani!! Unajua wote kosa lao lilikuwa nini?” Akauliza huku amefura kwa hasira.

“Walikuwa na kosa gani?” Nikamuuliza kwa hofu na unyonge.

“Walikuja humu gerezani wakaanza kumuulizia na kuchunguza chunguza kuhusu Eric Kaburu! Na hiki ndicho kilichowapata na kwa mujibu wa magereza waliotemnda hayo mambo ‘hawajulikani’ mpaka leo hii” Godi alikuwa na hasira mpaka anatetemeka.

“Kwahiyo nakuambia hivi! Kuanzia sasa sitaki unisemeshe wala kunijua jua humu jela! Endelea na using* wako kumuulizia Kaburu sitaki unijue” akaongea kwa hasira huku anaondoka, lakini ghafla akageuka na kunifuata tena kama kuna kitu amekumbuka, “na kwa kuwa umedhamiria kufa wacha nikusaidie! Ukitaka kuonana na Kaburu muda pekee unao weza kumuona ni muda wa uji pekee anakuwa yuko yard ya kwanza! Baada ya hapo huwezi kumuona mpaka muda wa kaba selo.! So nakushauri uende sasa ukajichimbie kaburi” akaongea nan kutoa kicheko cha dharau chenye hasira ndani yake na kuondoka.

Nikabaki nimeduwaa pale nimepigwa na bumbuwazi. Kwa dakika kadhaa sikuweza kutingishika nikabaki nimekodolea macho zile sehemu zenyw damu nilizoonyeshwa na Godi.

Nikakumbuka sentesi yake ya mwisho “ukitaka kumuona Kaburu muda pekee unaoweza kumuona na muda wa kunywa uji anakuwa yard ya kwanza.”

Nikajikaza kiume. Nikatembea kutola kwenye uchochoro huo mpaka nikatokea yard ya kwanza.

Niaanza kupepesa macho kumtafuta Kaburu ni wapi alipokaa. Nikamuona ameketi mbele kabisa kwenye yard mahali wanapoangalia TV akiwa amekaa na kikombe chake cha uji mkononi.

Nikakumbuka usia niliopewa na Godi kuhusu jinsi watu walivyouwawa kwa kumfata fata Kaburu na kumuulizia. Nikakumbuka pia maneno niliyoambiwa na kaburu mwenyewe siku ya kwanza tulipoonana alinambia “usije tena hapa kwa usalama wako na wangu.”

Nikajiuliza nifanyeje? Niachane na mpango wa kuonana nae na kuzungumza naye? Nikifanya hivyo tabu yote hii niliyoipata mpaka kuingia jela itakuwa na faida gani??

Hapana, nimekula ng’ombe mzima wacha nimalizie mkia.! Liwalo na liwe..

Sikujua niongee nae nini au nitasema kitu gani lakini nikaamua kuwa huu ndio muda wa mimi kumkabiri Kaburu.

Nikatembea kumfuata pale alipo na kusimama nyuma yake.. Kaburu hakugeka ila nilikuwa na hakika alikuwa amehisi nimesimama nyuma yake! Akaweka chini kikombe cha uji.. moyo ukanipasuka!!

Nikatembea mpaka kufika pale alipokuwa amekaa Kaburu lakini nikasimama nyuma yake. Nilikuwa na uhakika kabisa kuwa alikuwa anajua kuwa kuna mtu amesimama nyuma yake lakini hakugeuka aliendelea tu kunywa uji.

“Sijawahi kuona mtu mpumbavu kama wewe!” Kaburu akaongea huku ana simama na kunigeukia.

“Toka kuzaliwa kwangu, nimeona watu wajinga na wapumbavu! Lakini hao wote hawafikii upumbavu wako kijana” akaongea huku akiwa amesimama na kuniangalia usoni.

“Shikamoo mkuu” nikamuamkia.

“Sikudhani kama utarudi tena toka nikupe lile onyo siku ile kwamba unahatarisha usalama wako na usalama wangu kwa kuja kuongea na mimi! Lakini kudhihirisha ulivyo mpumbavu umejileta jela makusudi uendelee kunifuata fuata” akaongea kwa hasira bado akiwa ananiangalia usoni.

“Sikuwa na jinsi.! Sina chaguo lingine zaidi ya kufahamu ukweli kuhusu The Board” nikaongea kwa kujitutumua na kujiamini.

“Na kinachokufanya uhisi kuwa nitakwambia hicho unachokitaka ni mini?” Akaniuliza huku anatabasamu kwa dharau.

“Trust me! Utanieleza ninachokitaka utake usitake” nikaongea kwa kujiamini kabisa. Nimeishi uswahilini maisha yangu yote utotoni. Na moja ya vitu muhimu nilivyojifunza uswahilini ni kutokumuonyesha adui hofu yako na kujua namna ya kupiga mikwara.

Nikamuona kaburu alivyoduwaa ghafla baada ya kuona kujiamini kwangu.

“Ok! Tuseme kwa mazingaombwe yako ukawa na njia ya kunifanya nikupe hiyo taarifa! Nakuhakikishia kuwa utakuwa ushafukiwa kaburini siku nyingi kabla ya kuifanyia Nazi” akaongea akiwa na uhakika usoni wa anachokisema.

“Unadhani unavyoua watu ndio suluhisho la wewe kuwa Salama?” Nikamuuliza kwa hasira.

“Sio mimi nitakaye kuua kijana! Humu ndani kuna watu wa hao unaowasema,The Board na nina hakika kuna watu wa Usalama wa Taifa. Hao ndio watakaoshughulika na wewe” akaongea huku anageuka mkono wake wa kushoto kuna mahabusu akawa anawaangalia.

Nikageuka kuangalia kule mkono wa kushoto. Kulikuwa na mahabusu watatu wamesimama wanatufuatilia maongezo yetu.

Nikagundua kuwa wawili kati yao walikuwa ni moja katika wale mahabusu kadhaa jana waliokuwa wamekaa nyuma kabisa ya yard ‘wakituchora’ mimi na Godi jana wakati ambapo Godi alikuwa ananionyesha mazingira ya humu ndani.

Hawa wajamaa walikuwa na miili iliyojengeka kiasi na mmoja wao alikuwa amevaa nguo za kifungwa za rangi ya chngwa na mwingine alivaa nguo za kawaida ikimaanisha alikuwa mahabusu kama mimi.

Nikageuka kumuangalia tena Kaburu. Alikuwa ananiangalia huku anatabasamu kisha akaanza kutikisa kichwa kama ananisikitikia.

“Umebakisha siku chache sana za kuishi mdogo wangu” akaongea huku anaanza kuondoka pale yard.

Nikageuka tena kuwaangalia wale mahabusu waliokuwa wanafuatilia maongezi yetu muda wote. Bado walikuwa wamesimama wananiangalia huku usoni wakiwa wako serious haswa.

Kaburu alikuwa ameshaondoka kutoka yard hivyo na mimi nikageuka na kuondoka kwenda yard namba mbili.

Nilipofika yard nikaangaza macho huku na huko lakini sikumuona Godi.

Nikasogea na kwenda kukaa chini karibu na muembe nikiwaza mambo kadhaa.

Kitu cha kwanza nilichokuwa nakifikiria sana ilikuwa ni taarifa niliyoambiwa na Godi na baadae Kaburu mwenyewe kuithibitisha kwamba watu wengi walioingia humu jela na kuanza kumfuata fuata wamekuwa wakiuwawa.

Moja kwa moja nikaamini kuwa lazima The Board watakuwa wanahusika na mauaji hayo, yani kwamba wamepandikiza watu humu gerezani kufuatilia nyendo za Kaburu na wakiona kuna mtu anakuwa naye na ukaribu sana basi wanammaliza haraka.

Hii ilinifanya nielewe kwamba kuna taarifa ambazo Kaburu alikuwa nazo na The Board walikuwa wanahofia mtu mwingine yeyeote asizifahamu.

Lakini swali kubwa zaidi nililokuwa najiuliza kichwani ni kwanini The Board wasimmalize Kaburu mwenyewe ili kuondoa kabisa hofu yao ya taarifa kuvuja?? Kwanini walimuacha aishi kama wanahofia kuvujisha taarifa zao?

Moja kwa moja nikaanza kuhisi kwamba labda pengine kuna taarifa nyeti sana za The Board na mtu pekee ambaye anazo hizo taarifa ni Kaburu ndio maana wanahofia kumuua. Nilikuwa na hakika kabisa lazima kutakuwa na siri nzito kuhusu The Board ambayo Kaburu alikuwa anaitumia kama ‘insurance’ kumuwezesha kuepuka kumalizwa na The Board.

Kitu kingine nilichojiuliza na ambacho nilikuwa natakiwa kukifahamu haraka sana ni kuhusu anakoshinda Kaburu humu gerezani. Nikikumbuka kauli ya Godi alinieleza kwamba muda pekee ninaoweza kumuona Kaburu ulikuwa ni muda wa kunywa uji na baada ya hapo sitoweza kumuona mpaka muda wa ‘kaba selo’.

Niko humu gerezani ili niweze kumshawishi Kaburu anipe taarifa kuhusu The Board, na ili niweze kumshawishi ninatakiwa niwe na muda wa kutosha wa kuongea naye. Kwahiyo yanipasa kufahamu anakoshinda mida wa mchana na nione ni namna gani nitaweza kwenda hapo alipo na kuongea naye.

Nikiwa bado nimekaa pale chini ya mwembe nikiwaza na kutafakari, nikamuona mahabusu ambaye hapo baadae nilikuja kufahamu jina lake la utani humu gerezani wanamuita Sinyorita, alikuwa anatembea kuja pale nilipokuwa nimekaa.

Huyu kijana alikuwa na umri wa kama miaia 24 hivi na alikuwa na ‘swaga’ Fulani hivi kama mwanamke.

Kwanza kabisa alikuwa na umbo fulani hivi namba 8 ambalo mtoto wa kiume hapaswi kuwa nalo na kwa jinsi alivyokuwa mshenzi alikuwa anavaa vibukta vifupi vinavyombana.

Pia alikuwa ‘amejaaliwa’ rangi nyeupe pee kabisa mpaka kwenye visigino.

Siku za huko mbeleni nilikuja kufahamu kuwa Sinyorita alikuwa moja ya ‘makaka poa’ wa ‘hadhi ya juu’ humu gerezani. Yani kwamba humu gerezani kulikuwa na mahanisi wengi tu ambao kila mmoja wao alikuwa na hadhi yake. Kuna wale ambao walikuwa na hadhi ya kufanana na malaya wa uwanja wa fisi. Kulikuwa na wengine wenye hadhi ya kama machangu wanajiuza barabarani sinza. Kukikuwa na wengine wenye hadhi ya kufanana na wale machangu huku mtaani wa “laki moja kwa goli”!

Alafu kulikuwa na mahanisi first class wenye hadhi kama ya wale wanajiuza Serena Hotel kwa mfano. Na Sinyorita humu gerezani alikuwa na hadhi hiyo. Alikuwa ni pumziko la ‘madoni’ wa gereza.

Moja ya vitu nilivyokuja kuvigundua humu gerezani tofauti na stori za mitaani ni kwamba watu wanaofirw* humu, wengi wao wanafanya hivyo kwa hiari yao kabisa. Yani kiasi fulani ni kama ilivyo mtaani, kuna watu humu gerezani wana hela kweli kweli na wanatumia hizo hela kushawishi wafungwa wenzao au mahabusu na kuwageuza wake zao.

Japokuwa kulikuwa na matukio machache ya watu kubakwa au kufirw* kwa lazima, lakini hiyo ilikuwa ni moja kati ya makosa ambayo ukiyatenda humu jela na likifika kwa Askari magereza, basi wewe mbakaji utatamani ardhi ipasuke ukimbilie jehanum.

Wenyewe maaskari magereza walikuwa na msemo wao kuwa “jela ikitulia, ikiwa na amani na sisi kazi yetu inakuwa rahisi na tunafurahi kuifanya.”

Hivyo ishu ya kubaka ilikuwa moja ya vitu vinavyokemewa vikali humu ndani, lakini hawakuwa na time wala kujali wale wanaofiran* kwa hiari yao.

Kwahiyo, japokuwa bado gerezani ni sehemu ya hatari, iliyojaa uonevu na ukatili ila ikitokea mtu ameenda jela na ukasikia wenzake wamemgeuza mke wao, ujue kuna asilimia kubwa alifirw* kwa hiari yake kutokana na tamaa ya kutaka kuishi jela kama yuko uraiani kwa kula vizuri na kulala vizuri.

Sinyorita alitembea mpaka pale nilipokuwa nimekaa, alafu akasimama mbele yangu. Nikainua shingo na kumuangalia.

“Mambo!” Akanisalimia kwa sauti kama anabana pua.

Sikuitikia, nikaendelea tu kumwangalia.

“Naweza kukaa hapa?” Akaniuliza tena bado akiongea kikike kike.

Sikumjibu kitu, lakini akakaa pale pale nilipokaa mimi akiwa amenisogelea kabisa.

“Mambo vipi?” Akarudia tena kunisalimia kikike kike baada ya kukaa.

Kuna mda huwa mtu anafanya kitu cha Ainu kiasi kwamba wewe wa pembeni yake unajisikia aibu kuhusu anachokifanya kuliko hata yeye mwenyewe. Hivyo ndivyo nilivyokuwa najisikia muda huu.

“Unataka nini?” Nikamjibu kwa ukali na kukereka.

“Ai jamani kwani ugomvi” akaendelea kuongea kwa deko.

“Nimekuuliza unataka nini?” Safari hii nikamjibu huku nimekunja uso namtazama usoni mwake.

“Heee! Basi bwana yaishe, nimetumwa na blaki anakuita”

“Blaki ndio nani?”

“Yule pale!”

Akanionyesha kule nyuma ya yard mahali ambapo kuna ule uchochoro wa kutokea yard namba moja.

Alikuwa ni mmoja wa wale wajamaa walikuwa watuangalia mimi na Kaburu tulipokuwa tunaongea. Moyo wangu ukapasuka kwa hofu.

“Mwambie niko bize siwezi kwenda” nikamjibu kwa mkato.

“Nyoko zako uko bize na nini wakati uko jela humu! Hebu waulize mbwa wenzako nini kitakukuta Blaki akikuita na ukikataa kwenda” Sinyorita akaongea kama vile wanawake wanasutana.

“Anataka nini?” Nikauliza tena kwa kifupi.

“Hebu nenda bwana utajua huko huko anachokuitia msyuuuuuuu” akaongea na kumalizia na kusonya.

Baada ya hapo akainuka na kuanza kuondoka huku anatembea kwa madaha kama kawaida yake.

Nikatazama kule nyuma ya yard kwenye uwazi wa uchochoro, Blaki alikuwa amesimama ananiangalia.

Kiasi fulani nilishikwa na hofu lakininkwa upande mwingine nilishikwa na moyo wa ushujaa. Kwamba tayari nimeshaingia jela, sipaswi kuogopa chochote humu ndani. Maji nimeshayavulia nguo, sharti niyaoge.

Nikainuka na kuanza kueleke kule alipo Blaki. Nilipofika pale akasogea kidogo kama ananipisha nipite. Nikapita.

Baada ya kuingia pale uchochoroni nikakuta kuwa wako watu watatu. Blaki, yule mwenzake anayevaa nguo za kifungwa na mahabusu mwingine.

Nipoingia tu kwenye uchochoro, mwenzake mmoja akakaa kwenye uwazi wa kutokea uchochoroni mkono wa kulia mwingine akakaa mkono wa kishoto na Blaki mwenuewe akasimaa mbele yangu kama hatua tatu hivi kutoka pale nilipo.

Tukabaki tunaangaliana tumekaziana macho kwa takribani dakika nzima. Nikaanza kukumbuka stori za Godi aliponileta hapa asubuhi kuhusu watu waliouwawa hapa, pia nikakumbuka kauli ya Kaburu aliposema “umebakiza siku chache sana za kuishi”. Nikahisi hiki ndicho nilichoitiwa hapa.

Jambo la ajabu ni kwamba, japokuwa presha ilikuwa imenipanda na jasho lilianza kunitoka lakini sikuwa na hofu kabisa moyoni mwangu badala yake nilijisikia hasira ya kiwango cha juu.

“Dogo una dakika moja kunieleza ni nini ulichofiata huku jela” Blaki akaongea huku amefura.

“Kabla sijajieleza chochote kwanza nadhani ujieleze wewe kwanza, wewe nani na unataka nini?” Na mimi ‘nikamdindia’ huku nimefura.

“Narudia tena una dakika moja kujieleza ulichofuata huku jela” Blaki akaongea huku

Nikaona ngoja nimjaribu.

“Niko jela kwasababu kuna mtu nimemuibia na nimekosa dhamana, unaweza kunieleza unataka nini kuniuliza maswali ya ajabu ajabu?”

Ghafla nikamuona Blaki amefura zaidi kwa hasira. Akaingiza mkono mfukoni. Akatoa kisu. Nikasikia roho imepasuka kwa hofu, pwaaaaaaaa. Jasho likaanza kunitirika.

Gerezani hawaruhusu wafungwa kuwa na visu, kwahiyo wanachokifanya wanachukua kijiko na kukichonga kwa kukisugua sana mpaka kinatengeneza ncha kali kama kisu na upande mwingine wanafunga na mpira wa kuvutika ili kutengeneza kama mpini hivi.

Hicho ndio aina ya kisu ambacho Blaki alikuwa amekitoa kutoka mfukoni.

Akakishikilia kisu mkononi na kuanza kunisogelea taratibu. Mapigo yangu ya moyo yakaongezeka kwa kasi ambayo nikahisi moyo unataka kuchomoka.

“Wewe fala nakuuliza mara ya mwisho! Umefata nini jela??” Blaki akafoka kwa hasira mpaka jasho lilianza kumtoka. Pepo la uuaji lilikuwa limeshampanda kichwani.

Nikaanza kurudi nyuma taratibu.

“Fikiria kwa makini hicho kitu unachotaka kufanya, mimi sio huyo mtu mnayemfikiria” nikajitetea huku narudi nyuma mpaka nikafika ukutani. Blaki tayari alikuwa mbele yangu na “hasira” ilikuwa imempanda mpaka jasho linamtoka.

Ghafla nikakumbuka ile karatasi niliyopewa na Baba bite kuwa itanisaidia kusurvive humu gerezani. Jana usiku niliisoma lakini sikuielewa kwa asilimia zote lakini nakumbuka kabisa jina la “Blaki” limetajwa mara kadhaa mle ndani kwenye maelezo ya Baba Bite.

Kila nilipojitahidi kukumbuka haraka haraka kujua ni nini kilichoongelewa kuhusu Blaki, kumbukumbu ilikuwa haiji. Nadhani ni kutokana na kuwa katika paniki mda huu na pia kwakuwa sikuyaelewa Yale maelezo toka jana wakati nayasoma.

Nikanyoosha mkono wangu mpaka kwenye mifuko ya suruali ili nitoe hicho kikaratasi ili nikisome au walau nimuonyeshe Blaki. Sidhani kama nimewahi kuwa ‘desperate’ kiasi hiki kwenye maisha yangu kama jinsi ambavyo nilikuwa najisikia muda huu.

Nikanyoosha mkono na kupapasa mifuko ya suruali, lakini jambo la ajabu ni kuwa ile karatasi haikuwepo. ‘What the ****??’, nikajikuta najiuliza kichwani. Karatasi imeenda wapi wakati nakumbuka kabisa baada ya kuisoma niliiweka mfukoni na hata asubuhi milipoamka bado nilikuwa nayo mfukoni.

Siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Huu msemo haukuwa tu msemo, bali kwa wakati huu ndio ulikuwa uhalisia uliopo mbele yangu.

Nikajiuliza labda nipigane nao? Lakini nikaona uhalisia kabisa, kisu kilichopo mkononi mwa Blaki kitakuwa kimeshafika tumboni mwangu kabla hata sijarusha ngumi ya kwanza.

Macho yangu yakaanza kuangalia pale juu kwenye damu iliyovilia ambayo alinionyesha Godi asubuhi, kisha macho yakahamia kuangalia pale chini kwenye kona kwenye michirizi ya damu iliyovilia ambayo pia Godi alinionyesha asubuhi. Nikahisi kama moyo wangu umeacha kudunda.

Nikamuona Blaki anageuza kisu mkononi na kukishikilia vizuri na kwa nguvu zake zote! Alikuwa amefura kwa hasira. Jasho linamtiririka, pepo wa kuua amempanda.!!

Nikajua kinachofuata! Nikafumba macho kwa hasira, uchungu na hofu.!!

Nikiwa bado nimefumba macho kwa uchungu na hasira iliyochanganyika na hofu, kitu pekee nilichokuwa nakiona katika ufahamu wangu ni giza lililotanda ambalo niliamini kuwa leo yaweza kuwa siku yangu ya mwisho duniani.

Lakini ghafla..!!! Nikasikia mtu anafoka..

“Ole wako umguse hata shati.”

Nikashtuka kutoka katika hofu yangu na uchungu na kufumbua macho. Blaki naye nikagundua ameshtuka na kugeuka kuelekea upande sauti ilipotoke.

Kushoto mwa uwazi wa kuingilia kwenye uchochoro alikuwa amesimama Godi. Mkononi ameshika kipande cha karatasi.

“Narudia ole wako umguse hata shati” Godi akaongea kwa kujiamini huku anaingia kwa nguvu kumpita yule mahabusu mwingine aliye kaa pale kwenye uwazi wa kuingilia uchochoroni.

“Unasemaje wewe mseng*” blaki akafoka kwa hasira huku anamsogelea Godi kwa shari.

Godi akapiga hatua moja mbele kwa kujiamini huku anaongea.

“Kama unataka RCO Sweya ajue kuwa maiti ya askari wake imefukiwa nyumbani kwenu nyuma ya nyumba, basi mguse huyo au niguse mimi! Pia kama unataka taarifa za bunduki mlizoficha nyumbani kwa bimkubwa wako kihondo zimfikie RPC basi niguse au mguse huyo! Naamini kesi iliyokuleta humu ni kesi ya kijinga tu ya kukutwa na kiroba cha bangi! Sasa kama unataka kesi ya mauaji ya askari pamoja na ujambazi wa silaha zikukute basi jaribu kutugusa!! Naamini Bimkubwa wako pia hawezi kuwa Salama kwenye hizo kesi.. So kama unajiona wewe ndio kidume pekee mwenye pumb* basi tuguse.”

Godi aliongea kwa kujiamini na kwa utulivu wa hali ya juu kana kwamba yuko juu ya kilele cha dunia.

Akasogea hatua nyingine mbele na kukaribiana kabisa na blaki, kisha akaendelea kuongea.

“Na usidhani nakutania, chukua hii karatasi ukajisomee ushaidi wa hiki nilichokueleza”

Godi akaongea huku anakunja karatasi aliyokuwa ameishika mkononi kisha akamuwekea Blaki kwenye mfuko wa suruali. Wakati anaikunja kunja karatasi niliitazama kwa makini na kugundua kuwa ilikuwa ni karatasi ile niliyopewa na Baba Bite ambayo ghafla nilikuwa siioni kwenye mfuko wangu wa suruali.

Blaki alikuwa amefura kwa hasira lakini ameganda kana kwamba ni sanamu ya barafu. Niliwatazama na wale ‘wapambe’ wake, nao macho yalikuwa tamewatoka kweli kweli na wamegubikwa na mshtuko usoni.

Ilikuwa kana kwamba ni mnyama swala amemulikwa na tochi kali usoni nyakati ya usiku. Licha ya ujanja wa swala uliotukuka muda wa mchana, lakini hakuna mnyama mjinga kama swala umshitukize usiku kwa kummulika na tochi kali usoni. Anabaki ameganda ameduwaa hajui afanye nini.

Ndicho kilichokuwa kimemkuta Blaki muda huu. Aliganda ameduwaa ingawa bado alikuwa amefura kwa hasira.

Walikuwa wamesogeleana na Godi kwa ukaribu bado kidogo pua zigusane na Godi wamekaziana macho wanaangaliana.

Wakaganda hivyo kwa takribani dakika moja nzima hakuna anayepepesa macho.

Ghafla Blaki akageuka na kuanza kuondoka kutoka kwenye uchochoro. Wapambe wake wakamfuata. Wakaondoka kuelekea yard namba moja.

“Oooooooooopppssss” Godi alihema kwa kutoa pumzi ndefu nje na kukaa chini.

“Wewe mseng* unajua leo tungekufa wote hapa??” Godi akaongea kwa akiwa ana hema na kukaa chini vizuri.

“****! Asante kwa kuiba karatasi yangu na asante kwa kuniokoa” nikaongea huku nahema kwa nguvu pia na kuingizia utani kwa mbali lakini bado paniki ilikuwa haijaisha ndani yangu.

“Sihitaji asante yako wala ujinga wowote! Ninachotaka unambie wewe ni nani na nini kinachoendelea” Godi akaongea huku ananyanyuka pale chini akijishikilia ukutani kana kwamba amechoka kwa kukimbia umbali mrefu.

“Hapa sio mahala sahihi kuongea hayo mambo” nikamjibu na wote tukaanza kutembea haraka kutoka hapo uchochoroni.

Tukaelekea yard namba mbili na kutafuta sehemu ya peke yetu na kuketi.

“Tangu siku ya kwanza nilihisi kuna kitu unaficha! Unaongea uongo” Godi akafungua maongezi mara tu tulipoketi chini.

” Jana nilipokuwa nimekupokea humu gerezani na kukuonyesha mazingira unakumbuka baada ya hapo ni kitu gani cha kwanza uliniomba?” Akaniuliza.

“Kitu gani?”

“Uliomba kwenda chooni.!” Akaongea huku ana tabasamu.

“Kwahiyo ndio nini sasa?” Nikamjibu nikijifanya sielewi anachoongea.

“Skia kijana, nina uzoefu sana na jela.! Mahabusu akitoka huko nje alafu akirejea humu na kitu cha kwanza akielekea chooni, humu jela tunaita anaenda ‘kudownload’! Yani kuna vitu amevificha nyuma huko labda hela, bangi au chochote so anataka kwenda kukitoa” akaongea huku anatoa tabasamu Fulani hivi la mzaha. “Sasa Jana uliniambia unaataka uende chooni na nikakufanyia kusidi tu kukwambia usubiri mpaka tukiingia selo ili nione utafanyaje na cha ajabu tulivyoingia tu selo kitu cha kwanza ukaenda chooni! So nikajua kuwa ulienda kudownload.. Tukipokuwa tumelala nikakusachi mifukoni nijue ulicho enda kudownload chooni ndio nikakuta karatasi. Sikuisoma wala nini na nikairudisha tena mfukoni mwako coz nilijua asubuhi ukiikuta haipo utajua ni mimi na ilipofika asubuhi kwenye wakati tumepanga mstari tunafunguliwa kutoka selo nikakuchomoa tena hiyo karatasi na nikaenda kuisoma na kukuta hayo niliyoyakuta. Sasa humu jela watu wanaingiza bangi, wanaingiza hela na vitu kama hivyo lakini wewe umeficha karatasi na ulikuwa na shauku ya kujua taarifa za Kaburu so moja kwa moja hii ina maana lazima wewe utakuwa mtu wa ‘system’ na humo humu kwa kazi maalumu!! Una swami lolote kwanza mpaka hapo”

Godi akaongea kwa madaha kabisa, ni dhahiri alikuwa anainjoi jinsi alivyonibananisha.

“Endelea!” Nikamjibu kwa kifupi tu kwa kukereka lakini niko makini.

“OK!” Akakaa vizuri na kuendelea, “baada ya mazoezi nikakuonyesha Kaburu alipo na nikafuatilia kwa mbali mlivyokuwa mnabishana, nikafuatilia ulivyorudi yard huku, nikafuatilia Sinyorita alivyokuja kukuita na nikakuona ulivyoelekea uchochoroni kuonana na kina Blaki, so ikanibidi nitumie uzoefu wangu wa kitaa na taarifa niliyosoma kwenye karatasi yako na nikajitoa kuwa ‘Yesu mtoto’! Nikatoa maisha yangu ili niokoe maisha yako!!” Akaongea huku akimalizia na utani kama kawaida.

“Na kilichokufanya uhatarishe maisha yako kuokoa maisha yangu ni nini?” Nikamuuliza kwa shauku kwasababu ingawa nilimshukuru sana moyoni kwa kuniokoa lakini bado moyoni nilokuwa najiuliza kwanini alijihatarisha kiasi kile kuniokoa. Hatukuwa tumeshibana kiasi kwamba awe tayari kufanya ‘chochote kwa ajili yangu’.

“Jibu lake simpo tu” akaongea huku ana tabasamu, “wanakwambia ukikaa karibu na waridi lazima unukie! Sikufichi Ray, hii kesi niliyonayo safari hii lazima itanifunga na nahisi nitafungwa namba ndefu sana.. So, nimekuokoa namna ile nadhani haitakuwa vibaya kama ukiongea na hao wenzako kwamba msinisahau katika ufalme wenu na kunisaidia niepuke kifungo! Hiyo ndiyo sababu na bila kusahau nimefanya vile kwa upendo pia hahahaha” akaongea hoja yake ya kweli kwanini ameniokoa kisha akamalizia kwa kuingiza utani tena.

“Wow! Una mikakati mizuri ila ulichokosea tu ni kwamba mimi sio mtu wa ‘system’! Mimi raia kama wewe”

“Ucha ufala basi! Nimekuokoa sekunde chache zikizopita alafu unashindwa kuniheshimu kusema ukweli.. Acha mambo ya kiseng* aisee” Godi akafoka na mzaha ukaondoka kabisa usoni mwake.

“Ok ok ok! Labda niseme kwamba mimi ni raia kama wewe ila nashirikiana na ‘system’ kuhusu masula fulani”

“Masuala gani?”

“Siwezi kukwambia!”

“Sihitaji unambie nataka angalau unitoe tongo tongo usoni!”

Nikajifikiria kwa sekunde kadhaa nimueleze nini? Haitakuwa uungwana kwangu kumficha kabisa ukizingatia kuwa ameniokoa kutoka kwenye kifo dakika chache zilizopita. Lakini pia nikagundua kutokana na uzoefu wake wa jela, Godi anaweza kuwa ‘asset’ kwangu.

“Ooooops! Ok, ulisikia kuhusu kifo cha Waziri Josephat Kipanju?” Nikamuuliza.

“Kila mtu amesikia kuhusu hilo!”

“Ok! Ni kwamba tunaamini kuwa Kaburu anafahamu taarifa kuhusu muuaji wa Waziri Kipanju” nikamweleza kwa kifupi.

“Duuuuhh!” Akaguna, “na umesema wewe ni raia kama mimi sasa uchunguzi wa mauaji ya Viongozi wa serikali wewe unakuhusu nini?”

“Kwa kifupi tu labda niseme kuna mtu wangu wa karibu amesukumiwa fuko la mavi kuhusishwa na kifo hicho kwahiyo nisipozipata taarifa za muhusika halisi wa tukio like kutoka kwa Kaburu basi ndugu yangu nitampoteza!” Nikamfafanulia.

“Aiseeeee!! Una Bahati mbaya aisee, maana huyo Kaburj mwenyewe kwanza huwezi kumpata muda wa mchana na hata ukimpata sijui utamweleza nini ili atoe hizo siri” Godi akaongea huku anainuka.

Wote tukainuka, makalio yakianza kuuma kwa kukaa chini mda mrefu. Tukainuka na kuendeleza maongezi huku tunatembea tembea pale yard.

“Kaburu huwa ana shinda wapi mchana?” Nikamuiliza.

“Ofisini kwa mkuu wa gereza!” Akanijibu.

“Whaaaat?? Anafanya nini ofisini kwa mkuu wa gereza??”

“Humu jela kila mfungwa anapangiwa kazi ya kufanya! Ndio maana wengine unawaonaga huko nje wanapelekwa shamba, wengine wapishi humu ndani jikoni kule, wengine kutunza mifugo kwenye mazizi ya magereza na kadhalika.! Sasa Kaburu yeye kazi yake anazifanya ofisini kwa mkuu wa gereza!”

“Aisee! Ilikuwaje mpaka apangiwe kazi ya kibishoo hivyo? Na anafanya nini hasa uko ofisini?”

“Kuhusu alipataje hilo shavu la kushinda ofisini kwa mkuu wa gereza labda ukamuilize mkuu wa gereza mwenyewe.. Lakini kwa ninavyofahamu kazi anayoifanya huko ni kusidi kazi za kiofisi hasa nyaraka za wafungwa na mahabusu.!! Yani kwa mfano nyaraka za hukumu za wafungwa zikiletwa zinakuwa zimeandikw kingereza kwahiyo yeye anazichapa kwa kishwahili, au mahabusu wenye kesi kubwa wakiletewa mienendo ya kesi zao kutoka mahakama kuu pia inakuw kwa kibgereza na yeye anawasaidia kuzichapa kwa kiswahili au mfano wafungwa humu wakitaka kukata rufaa wanaandika rufaa zao na yeye anasaidia kuzichapa zikae kwenyw standard ya kiofisi! Hicho anachokifanya kila siku huko anakoshinda ofisini kwa mkuu wa Gereza” Godi akanifaanulia.

“Fuuuucck!! Kwa stahili hiyo inabidi nitafute namna ya kumfanya aisende huko ofisini kwa angalau hata siku tatu ili nipate mda mzuri wa kumshawishi aniambie ninachotaka”

“Na utafanyane hayo mazingaombwe kusafanya Kaburu asiende ofisini kwa siku zote Tatu hizo?”

“Inabidi kutafuta namna hakuna jinsi!”

“Sidhani kama…….”

Nikamkatisha aisongee.

“Quite! I’m thinking!”

“Unazemaje?” Akaniukiza akiwa amekereka na kingereza changu kama kawaida.

“Nyamaza kidogo niwaze nini cha kufanya”

Hakusema chochote akakaa kimya tu. Yukawa tunatembea tembea pale yard tuko kimya kama mabubu.

Huu ndio ulikuwa wakati wa mimi kutumia akili zangu zote nilizojaaliwa tangu nazaliwa. Nikawaza na kuwaza kwa dakika kibao. Hatimae nikapata wazo.

“Yeeeesss! I got it.. Nahisi najua cha kufanya” nikamuambia kwa msisimko baada ya kuhisi nina wazo la kufanikisha kumuondoa Kaburu ofisini kwa mkuu wa gereza.

“Kitu gani” Godi akaniuliza kwa shauku.

“Subiri utaona! Hivi Sinyorita ana kesi gani humu?” Sikumjibu swali lake badala yake nikamtwanga swali langu.

“Ana kesi ya robbery!” Akanijibu

“Robbery?? Hivi Sinyorita anaweza kumtosha hata nzi??” Nikashangaa.

“Stori ndefu sana! Hebu nidokeze hicho unachokiwaza” Godi bado alikuwa na shauku kujua ninachokipanga kichwani.

“Relax! Utaona.. Unafahamu askari anayewapangia zamu za ulinzi maaskari magereza wenzake humu?” Nikamuuliza tena bila kumjibu swali lake.

“Askari flani hivi bishoo tunamuitaga Obama”

“Ndio yupi huyo” nikamuuliza.

“Ulipokuja naamini kuna chumba cha ofisi ulipelekwa kuandikisha taarifa zao? Ndio huyo jamaa mwenyewe!” Akanijibu.

Nikamkumbuka. Ni yule askari magereza mstaarabu aliyeniokoa na kipigo kutoka kwa askari mwenzake wakati nasachiwa kabla sijaingia humu.

“Ok ok! That’s , gud.. Nisubiri hapa nakuja” nikamjibu huku naanza kuondoka.

“Unaenda wapi?” Godi akaniuliza kwa mshangao.

“Kuna jambo nataka kwenda kuongea na Obama!”

“Umechanganyikiwa au??” Godi akauliza kwa mshangao mkubwa sasa hivi.

“Nipe dakika chache narudi.! And hakikisha umemtafuta Sinyorita nikirudi nataka niongee naye” nikamjibu na kuondoka yard.

Godi akabaki ameduwaa tu ananiangalia ninavyoondoka. Nilitamani nimueleze nikichokipanga kichwani lakini ili nitekeleze kwa uzuri hiki nilichokipanga ni bora tukifanye akiwa haelewi ninacholenga aje kujua mwishoni baada ya kuona mtokeo ya mpango wangu kama ukifanikiwa.

Nikaelekea uoande ule wenye jiko amabo umeungana na ofisi.

GEREZA KUU LA MOROGORO

SIKU YA PILI

Kengere ya kuashiria muda wa chakula cha mchana Ilikuwa imepigwa tayari na wafungwa na mahabusu walikuwa wanaondoka yard kuelekea upande wa gereza wenye jiko.

Wakati wenzetu wanaelekea jikoni kuchukua chakula mimi na Godi tulibakia yard namba mbili.

Tukasubiri kama dakika tano tukiwa peke yetu kabisa yard yote, kisha ndio tukamuona Obama, yule askari magereza mstaarabu akija pale tuliposimama.

“I really hope unajua unachokifanya la sivyo wote tutaongia kwenye matatizo” Obama akaongea huku ananikabidhu funguo.

“Usijali mkuu, kila kitu kitaenda sawa!” Nikamjibu huku napokea funguo kwa kuificha kiganjani na kuiweka mfukoni. “Msauzi umempanga lindo pale nilipokueleza?” Nikamuuliza.

Obama akaitikia kwa kichwa kisha akageuka haraka na kuondoka.

“Ray, ungenidokeza japo kidogo huu mpango wako labda inaweza kusaidia! Usisahaunkuwa nina uzoefu mkubwa wa jela kuliko wew” Godi akaniuliza kwa shauku huku tunatembea kuelekea yard namba moja.

“Tatizo ni kwamba nikikwambia hauwezi kukubaliana nao” nikamjibu huku natembea kwa haraka.

“Unasemaje????” Godi akahamaki. “Kama una uhakika siwezi kukubaliana nao maana yake huo mpango wa wa hovyo”

“Ni kweli ni mpango wa hovyo lakini Nina hakika utafanikiwa, na bora kuwa na mpango wa hovyo kuliko kutokuwa na mpango wowote” nikamjibu.

“Na Obama umefanikiwaje kumshawishi hicho ulichoenda kumshawishi mpaka amekubali kukuletea funguo!!”

“Nitakuambia usijali” nikamjibu kwa mkato huku bado tunatembea kwa haraka na tahadhari kuelekea yard namba moja.

“Unaonaje ukiniambia sasa?” Akaniukiza huku ananishika bega nipunguze mwendo.

“Shiiiittt!! Una mpango mwingine wowote wa namna gani tunaweza kumfanya Kaburu asitishe kwenda ofisini kwa mkuu wa gereza???” Nikamuuliza kwa kufoka huku namtazama usoni. Godi hakujibu chochote. Nikaendlea kuongea, “sasa kama huna plani yoyote, unaonaje ukiacha kubwabwaja na kuniuliza maswali na badala yake ufanye kile ninachokueleza?” Nikaongea kwa kufoka.

“Ok! Poa..” Akajibu kwa kifupi.

Tulikuwa tumeshafika yard namba moja, ambapo napo yard yote tulikuwa peke yetu, wafungwa wote na mahabusu wameenda kula.

“Ok! Selo ya Blaki iko wapi?” Nikamuuliza Godi.

“Selo namba 46, ile kule mwishoni” akanijibu huku tunatembea kuifuata selo ilipo.

“Una uhakika bangianazowauzia wafungwa anaziweka humu ndani??” Nikamuuliza tukiwa tayari tumefika nje ya selo namba 46.

“Nisingekuwa na uhakika nisinge kwambia! Blaki ni kama kiwanda humu ndani unaweza kukuta ana kete hata mia tano humo ndani” Godi akaongea.

“Ok!!” Nikajibu kwa kifupi huku nafungua kufuli kubwa la Chuma lilikuwa linaning’inia selo namba 46.

Nikalifungua haraka haraka kisha tukaingia wote wawili. Ndani ya selo kulikuwa na magoro matatu yamepangwa pembeni na upande mwingine kulikuwa na mabegi ya mgongoni kama matatu hivi na yote kwa muonekano wa haraka haraka yalionekana yalikuwa na nguo ndani.

Nikang’amua kwamba begi mojawapo kati ya hayo atakuwa ameficha misokoto yake ya bangi anayouza humu jela ila amechanganya na Nguo ili isionekane kwa urahisi. Hatukuwa na muda wa kusachi kwa hiyo tukayabeba mabegi yote matatu na kuondoka nayo.

Tukatoka nje na kuanza kuondoka.

“Umesahau kufunga mlango!” Godi akageuka na kunionyesha mlango ambao niliuacha wazi.

“Sijasahau! Nataka ubaki hivyo” nikaongea huku natembea kwa haraka.

Tukarudi tena yard namba mbili na mabegi yetu.

“Ok! Selo ya Bokela iko wapi?” Nikamuuliza huku napepesa macho huku na huku.

“Ile kule nayo iko mwoshoni namba 75” akanijibu kwa haraka na tukaanza kutembea haraka haraka kuifuata.

“Kwa hiyo hawa ndio madoni wa kuuza bangi humu jela” nikamuiliza tukiwa tunaikaribia selo namba 75.

“Ndio hawa! Wote ndio madoni wa bangi humu lakini Blaki ndio nyoko zaidi, ana wapambe karibia ishirini humu ambao ni kama misukule yake akiwaambia chochote wanatekeleza bila kuuliza! Bokela yeye kwa hesabu ya haraka haraka wapambe wake hawavuki kumi” Godi akaongea tukiwa tumefika nje ya sell namba 75.

“Ok naomba kibiriti!” nikaongea huku naweka mabegi chini nje ya selo namba 75.

“Nimepata kibiriti ila ujue kwamba kibiriti ni bidhaa adimu humu, so nilicbofanikiwa kupata ni hiki” Godi akaongwa huku ananikabidhi njiti moja ya kibiriti na kipande cha karatasi cha kibiriti ile sehemu ya kahawia ya kuwashia.

“Itatosha! Good job” nikavipokea

Tukaangaza macho huku na kule pale yard kuhakikisha hakuna aliyerudi kuona na kutubamba tukifanya hiki tunachokifanya.

Nikaanza kuiwasha ile njiti kwa umakini sana huku Godi amezungusha mikono kuzuia upepo usiizime pindi ikiwaka.

Hatimaye ikawaka na nikachukua karatasi kidogo pembeni na kuiwasha pia ili kupata moto mkubwa kisha nikaanza kuyaunguza yale mabegi kwa chini moja baada ya jingine.

Tulipoona mabegi yameanza kushika moto, tukainuka kwa haraka na kuondoka yard na kuyaacha mabegi pale pale nje selo namba 75.

Tukaelekea upande wa mbele wa gereza kule jikoni na kupanga foleni ya chakula.

Kwakuwa tulikuwa tumechelewa kuja huku kwahiyo tukajikuta tuko mwisho kabisa foleni. Lakini kitu kilichomshangaza Godi ni kwamba tuliyemkuta nyuma kabisa ya mstati kabla yetu alikuwa ni Sinyorita.

Godi akageuka kwa mshangao na kuninong’oneza.

“We mseng* umepanga nini kitokee?? Na huyu choko uliongea naye nini jana nilipokuitia?” Akauniliza kwa kuninong’oneza ili Sinyorita asisikie.

“Utaona ndani ya dakika chache! Relax” nikaongea huku natabasamu kwa wasi wasi.

Magereza mengi ya Tanzania hayana ‘mesi’ ya kulia chakula. Hivyo gereza hili la Morogoro walikuwa na utaratibu kwamba ukishachukua chakula unasubiri mpaka watu waishe kwenye foleni au kubakia kidogo kisha mnaeuhusiwa mrudi yard na vyakula vyenu mkale.

Wakati tunafika kwenye foleni kulikuwa na kama watu thelathini hivi, lakini sasa tulikuwa tumebaki kama kumi hivi.

Afande Msauzi akafungua geti na kuruhusu watu waanze kurudi yard wakalw chakula.

Dakika kama tatu baadae baada ya watu kuruhusiwa kurudi yard ambapo kwenye foleni tulikuwa tumebaki kama watu watano hivi, ghafla tukaanza kusikia kelele kubwa za kishindo zinasikika kutoka yard.

Zilikuwa kelele kubwa hasa kama vile watu wanashangilia au kama wako kwenye uwanja wa vita wanapambana. Kelele zilizidi kila sekunde zilivhokuwa zinasonga,n ghafla tukasikia askari magereza aliyepo yard anapiga filimbi ya kuashiria hatari. Kadiri filimbi ilivyokuwa inapigwa na kelele zilizidi kuwa kubwa zaidi.

Wale wenzetu tuliokuwa nao kwenye foleni wakasahau ghafla hata swala la chakula wakakimbilia yard kwenda kushuhudia kinachoendelea.

Kwahiyo kwenye eneo hili tulibaki mimi, Godi, Sinyorita, Msauzi na wapishi jikoni.

Filimbi ya hatari ilipulizwa kwa nguvu zaidi na kishindo cha kelele kilizidi kuwa kikubwa.

Ghafla akatokea askari magereza kutoka kwenye ule mlango wa kwenda maofisini alikuwa anakimbia huku amebeba bunduki begani anaelekea yard.

Alipopita tu pale mlangoni kunakoelekea yard, Msauzi akaniangalia. Nikampa ishara kwa kumuitikia kwa kichwa. Akafunga geti kisha na yeye akakimbia kwenda yard.

Kwa hiyo katika eneo hili kwa sasa tulibaki mimi, Godi, Sinyorita na wapishi wa jikoni.

Kama sekunde kumi baada ya yule askari mwenye bunduki kupita na Msauzi kumfuata, tukasikia mlio mkali wa risasi. Mlio huo mkali ulisikika kwa kishindo mara tatu. Risasi tatu zilikuwa zimepigwa hewani. Wote kwa haraka tukajirusha na kulala chini mikono kichwani.

Hiyo ndiyo ilikuwa protokali ya magereza Tanzania. Kukitokea hatari askari anaoiga filimbi ili mlale chini, kama msipotii basi zinapigwa risasi hewani.

Baada ya hapo askari anaruhusiwa kumpiga risasi mgungwa yeyote ambaye atakuwa bado amesimama.

Kwahiyo kwa haraka sana tukalala chini, mpaka wapishi kule jikoni nikawaona nao wamejirusha kulala sakafuni.

Nikaangaliana na Sinyorita na kumpa ishara kwa kichwa.

Sinyorita akainuka kwa haraka na kukimbia kwa kunyata kuelekea kule kwenye mlango wa kuingia kwenye maofisi ya magereza. Akapita mlangoni ambao ulikuwa umeachwa wazi na yule askari mwenye bunduki na akatokomea huko ndani kwenye maofisi.

Tukiwa tumelala chini pale pale Godi akanigeukia na kuniangalia kwa mshangao.

“Kumanina zako! Nishaelewa ulichokilenga” akaongea na kutabasamu.

Kama dakika tatu baadae Msauzi akarejea kwenye eneo hili lenye jiko na akaongea kwa mamlaka na kwa kufoka.

“Wafungwa, mahabusu wote kwenda yard namba moja!! Wote yard namba moja” akaongea huku anatembea.

Wote tuliokuwa hapa, mimi, Godi na wapishi tukainuka na kuanza kukimbia kuelekea Yard namba moja.

Zaidi ya mimi na Godi, hakuna mwingine aliyekuwa anajua kuwa Sinyorita ameingia kule kwenye maofisi.

Tulipofika yard namba moja tukawakuta wafungwa wote na mahabusu wamejaza kwenye eneo hili.

Kwa kawaida wafungwa wakiwa wametapakaa yard ya kwanza na ya pili unaweza kuhisi gereza lina watu wachache sana. Lakini tulipokuwa tumekusanywa hapa na kujazana ndio nikapata picha halisi jinsi tulivyo kuwa wengi.

Watu wote walikuwa wamekalishwa chini kitako.

Mbele kabisa ya yard walisimama maaskari kama watano hivi na yule mmoja mwenye silaha. Pembeni yao kulikuwa na watu kama kumi na tano wamepigishwa magoti na karibia wanane kati yao walikuwa wanavuja damu kutokana na majeraha kichwani. Hawa walikuwa ni Blaki, Kobelo na wapambe wao.

“It’s namba kuanzia mwisho huko” askari mmoja akafoka.

Wafungwa wakaanza kuhesabu namba kwa kutamka kwa sauti.

Ilichukua karibia dakika kumi nzima zoezi hili la kuhesabu namba kukamilika.

Baada ya kukamilika yule askari akafoka tena.

“Haya anzia hapa mbele kwenda nyuma”

Tukaanza tena kuhesabu namba safari hii kuanzia sisi tuliokaa mbele na kushia kwa wale waliokaa nyuma.

Mara zote mbili hesabu iliyopatikana ilikuwa ni 314.

“Bado wafungwa wawili hawapo” afande mwingine aliyekuwa ameshika daftari na kalamu akaongea.

“Umejumlisha vizuri walioko nje shambani”

“Nimefanya hivyo mkuu, walioko shamba ni 22 nikiwajumlisha hapa bado watu wawili hawapo hapa” akaongea yule mwenye peni na karatasi.

“Nani hayupo hapa” yule askari mwingine akajliza kitemi kwa sauti ya juu.

Watu wakaanza kugeuka geuka kuangaliana usoni.

“Kaburu hayupo!!” Kuna mfungwa akaongea kwa sauti..

“Yes mjumlishe na Kaburu yuko ofisini” yule askari akaongea akiwa kama amekumbuka kitu cha wazi kabis walichokisahau Kumjumlisha Kaburu aliyeko ofisini.

“Nani mwingine” akauliza tena.

Watu wakaanza kugeukiana na kuaangaliana.

“Daudi hayupo” kuna mfungwa akapayuka.

“Daudi yupi?” Yule askari akauliza kwa shauku.

“Sinyorita” Yule mfungwa akapayuka tena.

Wale maaskari wakashtuka kidogo na kuangaliana.

“Kwahiyo Kaburu na Sinyorita hawapo hapa” yule askari akaongea kwa hasira.

Wakaangaliana tena na maaskari wenzake. Kisha maaskari wawili wakaondoka kutoka pale yard na kuelekea kule eneo la jiko.

Yard ilikuwa kimya kabisa. Godi alikuwa anageuka na kuniangalia kisha anatabasamu kichini chini.

Tulikaa tukiwa tumetulia vile karibia robo saa nzima.

Mara tukaona watu kadhaa wameongozana wanaingia Yard.

Mbele alikuwa ametangulia mkuu wa gereza na pembeni yake kulikwa na maaskari wawili. Nyuma yao walikuwa ni Kaburu na Sinyorita ambao nyuma yao nao kulikuwa na maaskari wengine wawili.

Walipoingia pale yard wafungwa wote na mahabusu tukashikwa na mshangao mkubwa hatukuamini tulichokuwa tunakiona.

Au niseme wengine wote isipokuwa mimi walishikwa na mshangao.

Sinyorita alikuwa ameletwa yuko uchi wa mnyama ameshikilia nguo mkononi.

Walipofika pale mbele maaskari wote wakapiga saluti, kisha wakasogea pembeni kumpa nafasi mkuu wa gereza azungumze.

Kaburu na Sinyorita wakapiga magoti baada ya kukuta wenzao wengine akina Blaki waliokuwa pale mbele wamepiga magoti.

“Simameni hivyo hivyo msipige magoti nataka wenzenu wote wawaone mashetani nyinyi” Mkuu wa gereza akaongea kwa hasira.

“Naona mmeanza kutupanda kichwani sasa!” Akaongea mkuu wa gereza huku anatuangalia wafungwa wote na mahabusu.

“Yani mnaingiza taharuki kwenye gereza langu kwa kugombea misokoto ya bangi??” Akaongea kwa hasira na kutoa macho.

“Naona mmejisahau kuwa mko gerezani labda tumewapa Uhuru sana ndio maana. Sasa kesho asubuhi hakutakuwa na mazoezi badala yake tutafanya msako wa selo kwa sell, ole wako tukukuta na bangi, ole wako tukukute na sigara, ole wako tukukute na ugoro, ole wako tukukute na kisu, ole wako tukukute na begi limejaa Nguo!! Nasema ole wako tukukute na kitu chochote tulichokikataza.” Mkuu wa gereza akahutubia kwa hasira.

“Na wewe Blaki umeshakuwa kero humu gerezani, kuanzia kesho akuweka solo mpaka utakapobadilika” akaongea huku anamuangalia Blaki na wapambe wake.

Baadae nilikuja kuelewa kuwa aliposema anamuweka ‘Solo’ alimaanisha kuwa atamuweka kwenye “solitary confinement”. Ni ile sehemu yenye selo zilizojitenga ambazo Godi alinieleza kuwa huwa wanawekwa mahabusu na wafungwa ‘maalum’.

“Sasa kwa kuwa nyinyi mnajifanya vidume, mimi nitawaonyesha ni kidume zaidi yenu wapumbavu nyinyi” akaongea huku anatuangalia wafungwa wote na mahabusu.

“Kaburu nilikupa heshima sana ndio maana nikakupangia kazi ofisini mwangu! Lakini unathubutu kuingiza mashetank wenzako ofisini kwangu ili mfirane!! Ofisi yangu mimi, ofisi yangu mnatumia kufirana, ofisi yangu mimi.!!” Mkuu wa gereza akaongea kwa hasira na hisia huku anapiga piga kifua.

“Afande nataka hawa mashetani wote! Kuanzia hawa waliokuwa wanafirana, na hawa waliokuwa wanagombea bangi.. Nataka muwapeleke ofisini kule mpige virungu mpaka wajute kuzaliwa! Mkimaliza hawa mbwa Blaki na wenzake wafungieni ‘solo’ kule na huyu firauni Kaburu nataka kuanzia jumatatu aanze kwenda shamba simuhitaji tena ofisini kwangu” akaendelea kuongea kwa hasira.

Nikajikuta natabasamu niliposikia maneno “simuhitaji tena ofisini kwangu”!! Nikajipongeza, ‘goal achieved’ nikajisemea kimoyo moyo.

“Saa ngapi hapo” akamuuliza askari wa pembeni yake.

“Saa nane na robo Mzee” askari akajibu kwa heshima.

“Sasa nadhani mlikuwa mnakula, lakini kutokana na ujinga huu mlio ufanya nahairisha kila mlichokuwa mnakifanya na mtafungiwa selo sasa hivi saa nane mlale badala ya saa kumi” akaongea kwa hasira kubwa na kumalizia, “vijana msitake kunijaribu, mimi sijaribiwi! Mtaiona jela chungu”

Akamaliza na kuanza kuondoka.

“Kaba seloooo” askari mmoja akapayuka kitemi.

Wote tukaanza kuinuka kwa unyonge tumelowa kama tumemwagiwa maji ya barafu.

Tukaongozana na Godi kuelekea selo yetu namba mbili kubwa.

“Kumamae wewe ni kichwa!! Saluti” akaninongoneza kwa kufurahi.

“Kwahiyo nini kifuatacho ITV??” Akaniliza kwa shauku.

“Well, tumeshafanikiwa kumuondoa ofisini kwa mkuu wa gereza! Lakini umesikia pale ameamuru kuwa jumatatu aanze kupelekwa shamba. Maana yake ni kwamba tuna siku ya kesho ijumaa, jumamosi na jumapili!! Tuna siku tatu tu kuhakikisha tumeongea nae na ametupatia taarifa tunayohitaji” nikaongea kwa sauti ya chini huku tunatembea kuelekea selo.

“Woooww!! Daaahh nilikuwa nakuchukulia poa sana.. Kumbeee daaahh! Sakuti aisee!” Akaongea kwa utani huku ananipigia saluti.

Nikatabasamu tu. Sikusema chochote.

Siku hii ya pili imeisha kwa mafanikio. Nina siku tatu mbele yangu kuhakikisha nakamilisha ‘mission’ iliyonileta humu.

Nikajipa moyo. ‘Inyeshe mvua, au liwake jua’ lazima kieleweke.

GEREZA KUU LA MKOA MOROGORO

SIKU YA NNE.

Moja kati ya vitu ambavyo vinanikera kuhusu kukaa ndani ya gereza ni kutokujua muda.

Kwa namna nilivyojizoesha katika maisha ya uraiani kutokana na ratiba zangu nyingi ni kuangalia saa kila baada ya muda mchache.

Gerezani mfungwa hauna hata ‘access’ ya kujua muda. Kwahiyo ili kujua muda inatakiwa utumie uzoefu wako wa kulisoma jua na kuhisi muda.

Na katika hisia zangu, hii ilikuwa yapata saa tatu asubuhi.

Tulikuwa tumemaliza kunywa uji takribani masaa mawili yaliyopita. Sikujua ni kwanini lakini siku za jumamosi na jumapili hakuna mazoezi gerezani.

Siku za ‘weekend’ ni siku zinazopendwa zaidi humu gerezni, kwasababu ni siku ya kutembelewa na ndugu, jamaa na marafiki.

Wafungwa wenyewe wanaitwa siku za ‘Vistazi’.

Mimi na Godi pia tulikuwa tumekaa tukiwa na shauku kubwa na siku hii. Nilikuwa na tumaini leo kuna uwezekano Cheupe na Issack wanaweza kuja kuniona na labda wanaweza kuwa na taarifa muhimu kuniwezesha kumshawishi Kaburu kunipa taarifa ninazohitaji.

Siku ya Jana Ijumaa ilikuwa imepita bure pasipo kufanikisha jambo lolote la maana kuhusu kilichonileta humu.

Siku ya jana Kaburu alitumia karibia muda wote katika zahanati ya magereza. Hii ilikuwa ni moja ya visanga vilivyokuwa vinanichekesha na kunishangaza kuhusu magereza. Ni juzi tu ambapo maaskari magereza walifuata amri ya Mkuu wa gereza na kuwashushia kipigo cha virungu Kaburu, Blaki, Bokela na wapambe wao, alafu kesho yake wafungwa hao wakashinda zahanati ya magereza kutibiwa majeraha na maumivu.

Siku ya jana kitu pekee labda cha maana nilochokifanya ni kuendeleza mazungumzo yangu ya makubaliano na Sinyorita na Msauzi japokuwa sikufanikiwa kuonana na Obama.

Kwa kawaida muda wa watu kuja kutembelea ndugu zao hapa magereza ni saa nne asubuhi na ilikuwa imekaribia tayari, zilikuwa zimesalia dakika kadhaa tu.

“Naomba Mungu wasisahau mapocho pocho ya kula, kudadeki maana hili dona la jela lishanikinai aisee” Godi akaongea kwa msisitizo na kukereka. Tulikuwa tumekaa chini ya mwembe kule yard ya pili ambayo tunaipenda.

“Daah!! Ndio unachowaza tu fala wewe.. Badala ufikirie unatokaje jela, unawaza kula tu” nikamjibu kwa ‘dongo’. Jela ilokuwa imenza kuniingia kwenye damu. Maana kuongea lugha ya maudhi nilikuwa naiongea bila hata kushtuka.

“Kutoka jela nataka na ni lazima, lakini kipindi nasubiria muujiza wa kutoka humu ndani sio dhambi roho yangu ikifurahi walau hata kidogo.” Akaongea huku anajinyoosha. “Na sio misosi tu! Usisahau tunadaiwa buku kumi na nyapala”.

“Oooopps! Tuombe Mungu” nikamjibu huku nainuka.

Tukainuka na kuanza kunyoosha miguu pale yard.

Kuna muda kwa kiasi fulani nilitamani kama siku zote humu gerezani ziwe za utulivu kama siku ya leo.

Siku amabayo hakuna mipango ya siri, hakuna pilika pilika za kuchoma moto vitu vya watu, hakuna mipango ya kuhatarisha maisha.

Lakini si sahihi kuruhusu hisia hii ya kutamani utulivu initawale. Sikuja humu ndani gerezani ili niwe na utulivu.

Lakini bado nikiri kuwa kuna muda nilitamani utulivu kama wa siku hii ya leo uendelee.

“Faridi Mkudeeeeeeeee! Eeeee faridi mkudeeeeeeee”

ITAENDELEA

Vipepeo Weusi : Mkakati Namba 0034 Sehemu ya Tatu

Also, read other stories from SIMULIZI;

Leave a Comment