Jinsi Ninavyo Tengeneza Matangazo Ya Kulipia Facebook Na Instagram (Sponsored Ads)
LIFESTYLE

Jinsi Ninavyo Tengeneza Matangazo Ya Kulipia Facebook Na Instagram (Sponsored Ads)

Jinsi Ninavyo Tengeneza Matangazo Ya Kulipia Facebook Na Instagram (Sponsored Ads)
Jinsi Ninavyo Tengeneza Matangazo Ya Kulipia Facebook Na Instagram (Sponsored Ads)

Hatua kwa hatua Namna ya Kufanya Matangazo ya Kulipia Mtandaoni (Facebook sponsored Ads)

HATUA YA 1: SELECT A GOAL (KUCHAGUA LENGO LA TANGAZO LANGU)

More profile visits:

Hapa kupitia tangazo lako utakua unaelekeza watu wafike moja kwa moja kwenye ukurasa wako wa matangazo ili waweze kuona huduma/bidhaa ambazo unazitangaza,hapa utawapa uwezo wa wao kupitia huduma/bidhaa zako.

More website visitors:

Hapa ni kwa wale amabo tayari wana tovuti za biashara watakua wana waongoza wateja waweze kufika moja kwa moja kwenye tovuti zao na kuweza kuona huduma ambazo amewaandalia na hapo wateja wanaweza kufanya manunuzi ya bidhaa ambazo tayari wamependezewa nazo.

More messages:

Hapa utaweza kuwaongoza wateja waweze kufika moja kwa moja kwenye uwanja wako wa meseji wa FACEBOOK, INSTAGRAM au WHATSAPP kwa kupitia bidhaa hiyo ambayo umeifanyia tangazo.

HATUA YA 2: DEFINE YOUR AUDIENCE (KUCHAGUA AINA YA WATU AMBAO NATAKA TANGAZO LIWAFIKIE)

Automatic:

Ukitumia chaguo hili utaweza kuacha instagram/facebook kuweza kukuchagulia watazamaji wa kuliona tangazo lako wakiwemo wafuasi wa ukurasa wako.

Create your own:

Ukitumia chaguo hili utaweza kutengeneza aina ya watazamaji ambao unahitaji waweze kuliona tangazao lako kwa kuchagua jinsia zao, umri, na eneo la kijiografia unalotaka tangazo lako liweze kuonekana.

HATUA YA 3: BUDGETS & DURATION (BAJETI NA MUDA)

Hapa ndipo ambapo utachagua kiasi gani cha fedha unahitaji kukitumia kwenye tangazo lako na kwa mda gani mfano: dolla 5 kwa siku 10 inamaana kwamba unatakiwa uweze kua na kiasi cha dolla 50 sawa na shilingi 118,500/= kuweza kutangaza tangazo lako kwa siku 10.

HATUA YA 4: REVIEW YOUR AD (KUKAGUA TANGAZO)

Hapa utaweza kulikagua tangazo lako kua tayari limekidhi vigezo ambavyo unavihitaji, likiwa limeshakizi vigezo tayar unaweza kubofya kitufe cha BOOST POST.

Tangazo lako litapitia kwenye ukaguzi wa META kwa mda usiozidi masaa 24.

HATUA YA 5: KUFUATILIA MATOKEO YA TANGAZO.

Baada ya tangazo langu kuruhusiwa (approved), ni muda sahihi wa kuanza kuangalia na kufuatilia muenendo wa tangazo langu kwa ukaribu.

👉Endapo Unahitaji Ufafanuzi zaidi/Maoni/Una swali Kuhusiana na Biashara

Tuwasiliane: WhatsApp 0766 422 168
Email: [email protected]
Instagram: kichwadesign
USHAURI ni BURE

Get More Business Idea;

Leave a Comment