Yawezekana huna mpenzi au labda huna muda wa kutafuta mwenza, utakapoona mabadiliko haya mwilini mwako basi inabidi ufikirie kuanza kale kamchezo ketu.
Haya ni mabadiliko yanayoweza kutokea mwilini mwako utakapoacha kufanya mapenzi, na si mabadiliko mazuri kama namba hili la kwanza katika mabadiliko haya:
Kitakachompata mwanamke akiacha kufanya mapenzi
1. Unaweza kupata ndoto nyevu
Kama inavyomtokea mtoto wa kiume aliye kwenye balehe, wanawake wasiofanya mapenzi mara kwa mara, watajikuta wakipata ndoto nyevu wakiwa usingizini.
Hii itakutokeasio tu kwa kutokufanya mapenzi mara kwa mara bali hata unapoacha kupiga punyeto.
Wanawake wengi wanakosa uhakika kama wanapata ndoto nyevu kwa kuwa inategemea endapo atakumbuka, kwakuwa hakuna kumbukumbu nyepesi kuisahau kama kukumbuka ulichoota.
Haikuwa rahisi kwa watafiti kuwa na jibu kuhusu kusisimka kwa mwanamke akiwa usingizini, kwakuwa inabidi wapime mapigo ya moyo, kupima ubongo na kufatilia mabadiliko ya joto ukeni.
2. Unapoteza hamu ya kufanya mapenzi
Japokuwa usemi wa “usichokitumia kitapotea” unatumika kuelezea jambo kama hili, wanawake hawapotezi kitu chochote ambacho hakiwezi kurudi kwenye hali yake ya kawaida, walau wakiwa katika hatua za kuweza kupata watoto.
Ni kawaida sana kwa mwili wa mwanamke kuacha kuwaza kufanya mapenzi kama hakufanya kwa muda mrefu. Mwili unazoea hali ya kutopata hisia hizo.
Hamu ya kufanya mapenzi inaweza ikapotea, kitu ambacho sio kibaya sana kama unataka kufanya mambo mengine. Pia utaweza kuachana na mambo yanayotokana na hisia zako za mapenzi.
Kama hutaki kupoteza hamu ya kufanya mapenzi hata kwa muda kidogo, kujichua kunaweza kukusaidia hili.
Mshauri wa masuala ya kujamiiana Holly Richmond, ambaye ni Daktari wa Saikolojia ya ufanyaji kazi wa mwili wa binadamu anasema, “Watu ambao huwa wanapiga punyeto huwa wana uwezo mkubwa wa kufikiria na ni wakarimu kwa wapenzi wao,” kwahiyo mwanamke asione aibu kupiga punyeto!
Isikupite Hii: Maneno 14 ambayo mwanamke anatamani umwambie
3. Kuta za uke zinadhoofika
Inafahamika kwamba ukiwa na umri zaidi ya miaka 50 hivi wanawake wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kutopata raha kabisa wakati wanafanya mapenzi iwapo hawatakuwa wakijamiiana mara kwa mara.
Kwa kawaida, kuta za uke zinakuwa nyembamba na kudhoofika hadi mara nyingine kuanza kuchanika wakati unaingia kipindi cha ukomo wa hedhi, hali inayofanya tendo la kujamiiana liwe na maumivu makali sana.
Jambo pekee la kuzuia hili lisitokee kimsingi ni kuendelea kufanya mapenzi mara kwa mara hata katika umri wako wa kustaafu. Dkt. Streicher ameliambia jarida la Reader’s Digest kwamba kupungua kwa kuta za uke kunatokana na kutopata kwa damu ya kutosha, tatizo linaloweza kurekebishwa kwa kusisimuliwa kimapenzi na kujamiiana.
“Wanawake wenye umri mkubwa ambao hawafanyi mapenzi mara kwa mara wapo kwenye hatari kubwa zaidi ya kupungua na kufa kwa tishu za kuta za,” amesema. “Kisababishi kikubwa cha tatizo hili ni kupungua kwa mzunguko wa damu, na inajulikana kwamba kufanya mapenzi mara kwa mara kunaongeza mzunguko wa damu maeneo hayo.”
Na kama maumivu makali wakati wa kujamiiana yatakuwa hayatoshi, madhara yanayoletwa na kupungua kwa kuta za uke ni ugumu wa kutengenezwa kwa kilainishi asilia kwenye maumbile yako, jambo linalofanya kitendo cha kufanya mapenzi baada ya muda mrefu kusababisha ukavu wa hali ya juu.
Ili kuzifanya kuta za uke ziwe nene na zenye afya, angalau soma vitabu vya mapenzi kila mara, na angalau uwe unapiga punyeto.
Kwa muktadha kama huu ndio madaktari wakasema kuwa kama usipotumia kiungo fulani basi kitadhoofika, kwahiyo njia rahisi zaidi ya kuondoa tatizo hili ni kufanya mapenzi mara kwa mara!
Mtaalamu wa magonjwa ya wanawake, Dkt. Barb DePree anasema, “Ninamhudumia mwanamke mwenye umri wa miaka 75 ambaye anasema kuwa anafanya mapenzi mara mbili kila wiki,” kwahiyo hakuna sababu ya msingi ya kutofanya.
4. Unaongezeka uzito wa mwili
Kufanya mapenzi ni njia bora sana ya kuishughulisha moyo na misuli bila kupata maumivu unayopata ukikimbia au gym.
Unaweza usiwe unajua ni kiasi gani cha ‘kalori’ unakipunguza unapofanya mapenzi, lakini unaweza kugundua hilo baada ya kumaliza.
Jarida la “Woman’s Day” lilichapisha kuwa kiwango cha kawaida cha kalori unachopunguza wakati wa kuandaliwa, matokeo yaliyowastua wengi.
Ukiwa unapata mabusu ya kawaida tu, unapunguza kalori 68 kwa saa, lakini yanapofanywa kwa muda mrefu zaidi yanapunguza kalori zipatazo 476 kwa saa. Hii ni kwa sababu kiwango cha kupumua kinapoongezeka, kalori zinapungua kwa wingi zaidi!
Tendo la kufanya mapenzi linasaidia kuchoma kalori 144 kwa kiwango cha chini. Kiasi hiki kitaongezeaka zaidi endapo utakuwa na ushirikiano wa kutosha.
Hii inamaanisha utapunguza kalori angalau 1,200 kama utakuwa unafanya mapenzi mara tatu au nne kwa wiki, kiasi ambacho ni kikubwa sana kama utakuwa hufanyi kwa muda mrefu.
Kwahiyo, kama ukiacha kufanya mapenzi, utaona mwili ukianza kuongezeka uzito kidogo kidogo.
Isikupite Hii: SMS 10 za kubembeleza na kuchochea mahaba
5. Kudhoofisha mfumo wa kinga ya mwili
Kufanya mapenzi mara kwa mara kuna faida kubwa kiafya, na tunapoacha kwa muda mrefu tunajiweka kwenye hatari ya kuugua kirahisi zaidi!
Kwa mujibu wa wataalamu wa Kliniki ya Mayo nchini Marekani, kila mara mwanamke au mwanaume anapopandishwa hamu ya kufanya mapenzi, mwili unatoa homoni aina ya Dehydroepiandrosterone (DHEA).
Homoni hii inasaidia kuupa nguvu mfumo wa kinga ya mwili, ikiusaidia mwili kupambana na bakteria, virusi na vijidudu vingine vingi. Lakini faida hii itapatikana endapo mwenza wako ataweza kufika kileleni mara kwa mara.
Japo kutofanya mapenzi haina maana kwamba utapata magonjwa makubwa ghafla, kinachomaanishwa ni kwamba utakuwa unakosa faida hizi zinazotokana na kufanya mapenzi mara kwa mara.
Homoni hii ya DHEA pia inasemwa kuwa inasaidia kuondoa msongo wa mawazo, kung’arisha ngozi, kurekebisha tishu zilizoharibika kwa haraka zaidi na pia kuongeza kiwango cha uelewa na kujifunza.
Utafiti uliofanywa na wanafunzi wa vyuo vikuu pia umebaini kiwango kikubwa cha protini aina ya immunoglobulin A, kiambata muhimu sana katika kinga ya mwili – kwa wanaofanya mapenzi walau mara mbili kwa wiki ikilinganishwa na ambao hawafanyi!
6. Kuwa na msongo wa mawazo
Sio tu kwa sababu ya raha unayopata wakati wa kufanya mapenzi, mbegu za kiume ni moja ya vinavyopunguza msongo wa mawazo kwa mwanamke. Yawezekana ikaonekana hiki ni kitu ambacho mwanaume atasema ili alale na mwanamke, lakini ndio ukweli wenyewe!
Jarida la Psychology Today limeripoti kuwa katika utafiti uliohusisha wanawake 293 kuhusu tabia zao kwenye mahusiano, kama idadi ya kufanya mapenzi na iwapo wanatumia kinga au la. Kisha wakapimwa kujua viwango vyao vya msongo wa mawazo.
Ilibainika kuwa waliokuwa wanafanya mapenzi bila kinga hawakuwa na msongo wa mawazo ikilinganishwa na waliokuwa wanatumia kinga au ambao hawakufanya kabisa.
Viambata vinavyopunguza msongo wa mawazo vilivyopo kwenye mbegu za kiume vikinyonywa na kuta za uke, vinamfanya mwanamke itulie kabisa! Hii ndiyo sababu watu hupata msongo wakiachana na wapenzi wao.
Kwa mujibu wa jarida la “Psychology Today,” homoni za endorphin zinazotoka wakati wa kufanya mapenzi zinasaidia kuondoa wasiwasi. Kwahiyo, unapopita muda mrefu bila kufanya mapenzi, unaweza kuona unapata msongo wa mawazo.
Haijaelezwa endapo homoni hizi zinatoka iwapo utafikia kileleni au la, na ikiwa ndivyo, basi wanawake wengi hawapati faida hii kwakuwa wengi wao hawafiki.
Uzuri ni kwamba hata ‘mazoezi’ unayofanya wakati wa kufanya mapenzi husaidia kufikia faida hiyo.
Tafiti moja imeonesha kuwa kwa wanaofanya mapenzi baada ya kila wiki mbili wana uwezekano mdogo wa kupata shinikizo la damu ikilinganishwa na wasiofanya kabisa au wanaopiga punyeto au wanaofanya njia yoyote isiyohusisha kujamiiana.
Kwahiyo, hata ‘ukijihudumia’ mwenyewe haitasaidia sana kukupunguzia msongo wa mawazo. Kwa sababu hii, wanawake wanahitaji hasa kuwa na mwenza.
7. Unapunguza uwezekano wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, UTI na mimba usizotarajia
Mara nyingine maambukizi yanatokana na kutojikausha vizuri au kuwa na unyevu kwa muda mrefu au kuvaa nguo zinazobana sana, lakini kutofanya mapenzi inamaanisha hutakuwa na wasiwasi tena kuhusu kupata magonjwa ya zinaa na mimba zisizotarajiwa.
Ingawa kutofanya mapenzi kabisa ndio njia pekee ya uhakika ya kuepuka maambukizi ya VVU, watu wengi hawajui kwamba kuna magonjwa mengine ambayo unaweza kupata maambukizi ya bila hata kufanya mapenzi.
Maambukizi ya mfumo wa mkojo ni tatizo kubwa sana. Yanasababisha maumivu makali na yasiyoisha.
Je, umegundua kuwa mara zote ulizogundua umepata maambukizi ni baada ya kutoka kufanya mapenzi? Gazeti la New York Times limeripoti utafiti unaoonesha kuwa asilimia 80 za maambukizi ya UTI yanatokea ndani ya saa 24 tangu kufanya mapenzi.
Ni kawaida kwa mwanamke kupata maambukizi akifanya mapenzi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu.
Hata kipindi cha wiki mbili au tatu kinatajwa kuwa ni muda mrefu kutofanya mapenzi, kwahiyo, kwa wanawake kuwa mbali na wapenzi wao kwa muda kunawaweka kwenye hatari ya kupata UTI.
Faida pekee unayopata kwa kutofanya mapenzi muda mrefu ni kwamba unakuwa na hakika nani aliyekuambukiza, lakini ukianza tena kufanya mapenzi mara kwa mara, ni kama una uhakika wa asilimia kubwa kwamba upo mbioni kupata maambukizi. Ni kama mshale wenye ncha mbili, ya faida na hasara.
8. Kusahau mara kwa mara
Uwezo wa kiakili unapungua. Kusahau mara kwa mara ni tatizo kubwa ambalo mwanamke anapata asipofanya mapenzi mara kwa mara kwa sababu hii:
Kufanya mapenzi inasaidia kuchangamsha mishipa iliyopo kwenye ubongo inayoitwa hippocampus ambayo kazi yake ni kutawala hisia, kumbukumbu na mfumo wa fahamu, ambayo husaidia sana kuweka kumbukumbu, lakini utambue kwamba haihusiki na kumbukumbu zako zote.
Wakati unafanya mapenzi, seli mpya huwa zinatengenezwa kwenye mishipa hii, jambo linalosaidia kwenye kumbukumbu. Unapoacha kwa muda mrefu, kazi hii inakuwa haifanyiki na kusababisha kuzorotesha uwezo wako wa kumbukumbu.