Maana ya upendo wa kweli
LIFESTYLE

Maana ya upendo wa kweli

Maana ya upendo wa kweli
Maana ya upendo wa kweli

Upendo wa kweli ni hisia ya mapenzi, shauku, urafiki na kujitolea kwa kweli kwamba mtu mmoja anahisi kwa mwingine.

Upendo wa kweli ni dhana inayoenezwa na fasihi ya kimapenzi na ya kufikiria. Wawakilishi wake kwa mfano ni:

mwandishi wa Kiingereza William Shakespeare (1582 – 1616) na Romeo na Juliet,

mshairi wa Chile Pablo Neruda (1904 – 1973) na wake Mashairi ishirini ya mapenzi na wimbo wa kukata tamaa,

mwandishi wa Colombia Gabriel García Márquez (1927 – 2014) na wake Upendo wakati wa hasira,

mwandishi wa Kijapani Haruki Murakami (1949) na trilogy yake 1Q84, kati ya zingine.

SIMILAR: Biashara ya Juice

Hii Ndio Maana halisi ya Mapenzi katika mahusiano ni wengi tunapenda ila wa kweli ni wachache akupendae kwa dhati ni yule anaekupenda kwa dhati, kukujali, kukuthamini bila kujali vile ulivyo, maisha yako yalivyo , mapungufu yako ila upendo wake wa dhati anakujengaje katika mapenzi na maisha yake, anajengaje mapenzi furaha yake kwako anajengaje mapenzi furaha yako kwake bila kuangalia uwezo wake uzuri wake uwe handsome wake ila mapenzi yake ya kweli katika mapenzi na maisha yake

Siri ya mapenzi ya dhati Katika mahusiano ya furaha yote utendayo ufanyao fanya kwa upendo palipo mlango sahihi na ufunguo wa upendo na mapenzi yako pata funguka kwa mapokeo na majibu ya mapenzi ya dhati yaliyo katika hisia , upendo na fikira za pamoja mwaachie kwa upendo Kama ulivyo mpokea kwa upendo usitafute Sababu ya kutengana ni vizuri iende kwa upendo Kuna kesho unaweza penda tena ulipopenda ukapendwa.

Maana 3 Tofauti za Upendo Katika Mahusiano
Kujali

Kuna wanaoamini kuwa kujali tuu inatosha kuonyesha kuwa unampenda fulani, au fulani kuonyesha anakujali basi hiyo ndio maana halisi ya upendo. Wengi hujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta zawadi na surprises za ‘nguvu’ kama sehemu kuu ya kuonyesha upendo wao. Aina hii ya upendo inahusika sana hasa kwa watu waliopo mashuleni na vyuoni. Wengi wanaoamini maana hii ya upendo, husisitiza sana kuogopwa/kunyenyekewa kama sehemu ya kuonyeshwa kuwa nao wanapendwa.

Kujitoa kafara

Katika maana hii, upendo ni swala la jinsi gani unavyojitoa kwa mwingine ili kuona anakuwa na furaha na ajihisi kuwa salama kutokana na uwepo wako. La msingi katika aina hii ya upendo ni kupenda kumfahamu vema mwenzi wako, kujua shida zake, na ndoto zake, na kujitoa kwa hali na mali kuhakikisha anaona uwepesi katika shida zake, na kuwa anakuwa na matumaini ya kuwa ndoto zake zitatimia. Upendo wa namna hii huwa na subira, na huonekana zaidi kwa waliokomaa kifikra, na wenye kujiheshimu wao wenyewe.

Kuvutia

Kwa wengine upendo ni namna gani wanavyovutiwa kimapenzi na mtu husika, au vile wanavyojisikia kuwa salama mbele ya mtu fulani. Utakuta mtu anasema anampenda kaka fulani kwakuwa tuu amevutiwa na uhodari wa kijana husika katika masomo, kujiheshimu kwa kijana husika, sifa au umaarufu alionao mhusika. Na kwa upande mwingine, mtu anaweza kuvutia kwa uzuri wa sura au umbile la mtu fulani. Kutokana na mvuto wa hisia kama hizo na wakati mwingine hisia hizi za mvuto huwa kali sana, basi mtu akadhani hiyo ndiyo maana halisi ya Upendo. Wenye tafakari hii ya upendo wengi wao hawana subira na ukichukua muda mrefu kutafakari hisia hizi, unaweza kukuta ni za muda mfupi tuu.

Leave a Comment