Sababu 4 za Wanawake kupenda Wanaume Masharobaro
LIFESTYLE

Sababu 4 za Wanawake kupenda Wanaume Masharobaro

Sababu 4 za Wanawake kupenda Wanaume Masharobaro

Wanawake kuchagua wanaume masharobaro ama kwa lugha ya kimombo badboys kuwaliko wanaume wa kawaida si jambo geni na hutokea mara kwa mara. Jambo hili tumeliona likitendeka aidha katika vyuo, vilabuni, sinema, maktabani ama sehemu yeyote ile.

1. Hamu ya kufuata.
Kufuata kitu ambacho unakipenda huwa kuna msisimko fulani mtu hupata. Lakini msisimko zaidi hutokea wakati ambapo mtu anajaribu kufuata mtu ambaye hataki kujulikana mienendo yake ya kimaisha, kufuatwa ama kueleweka kimaisha. Haya ndio maisha anayoishi mwanamume sharobaro.

Wanawake wanapenda sana wanaume ambao hawaeleweki kimaisha (yaani hawatambuliki) ama kutakwa kujua maisha yao. Na wewe kama mwanaume unataka kutumia huu udhaifu kwa manufaa yako, wakati mwingine unafaa kumfanya mwanamke abaki na maswali chungu nzima kutaka kukujua zaidi. Kama unampenda, jaribu kadri iwezavyo kutojaribu kumuonyesha. Badala yake mpe pia yeye changamoto kwa kuweka ujanja wa kutoeleweka mara kwa mara. Hii ni njia moja murua ya kuhakikisha utaingia katika akili yake.

2. Kutaka kuwaGeuza tabia zao.
Kitu kingine ambacho wanawake huvutiwa kwa sharobaro ni kutaka nafasi ya kuwafunga fundo ama kuwajeuza tabia zao. Mwanamke kikawaida amezaliwa naturally na hisia za uzazi, yaani hutaka kujeuza mtu mwenye tabia ovyo kuwa na tabia nzuri. Hii huibua hisia halisi za uzazi ndio maana kama mwanaume unapaswa wakati mwingine kumsumbua mwanamke kihisia, kimawazo na kadhalika. Unafaa kuwa mpinzani lakini usiwe mhalifu. Unafaa kuwa hatari lakini usipitishe kiwango ambacho kitamwogopesha.

RELATED: Njia 7 za Kuuhepa Mtego wa Kuwa Rafiki na Mwanamke Unayempenda

3. Uanaume uliothabiti.
Wanaume masharobaro (na si wale feki) karibu nyakati zote huwashinda wanaume wa kawaida kwa sababu ya mambo mawili makuu. Kwanza ni kuwa ni wanaume majasiri na pili wanaudhibiti uanaume wao kwa kuwa ngangari kimaisha. Kutoogopa kwao kwa jambo lolote ndiko kunawafanya wanawake kuvutiwa nao.

4. Uoga wa kujitwika majukumu.
Wanaume masharobaro hupenda kuhepa majukumu yanayohusiana na mahusiano. Kwa wanawake ambao wana uoga huo huo wa kuwa na majukumu, masharobaro huwavutia sana na kuwaona kama hakuna wanaume wazuri kama hao. Wanawake aina hii hawatajitweka majukumu kwa kuwa hawana haja ya kujishughulisha na hisia za kimapenzi ambazo ni stress.

Pia ni habari njema kwa wanawake ambao wako tayari kwa uhusiano wa kimapenzi wa muda mfupi pekee. Lakini kama kawaida, mwisho wa siku lazima mwanaume sharobaro au mwanamke mtundu lazima kuna sehemu fulani ndani ya mawazo yake anatamani kuwa na mahusiano ya kudumu na pia kupendwa.

Njia 31 ambazo zitamfanya mwanamke akupende zaidi.

Leave a Comment