Sifa 20 zinayoonyesha ukichaa wa mapenzi
- Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
- Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
- Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
- Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.
- Kusema wanawake wote sawa.
- Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.
- Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.
- Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!
- Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?
- Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!
- Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!
- Kumhonga mwanaume ili akuoe!
- Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!
- Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!
- Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!
- Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.
- Kumsomesha mtu ili uje umuoe!
- Kumng’ang’ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!
- Kuwaeleza mashosti zako ‘utam’ anaokupa mtu wako!
- Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..
Nimeipaste kama ilivyo kama imekugusa Nivumilie
Isikupite Hii: Maswali 9 Ya Kuzingatia Kabla Kuingia Katika Mahusiano