LYRICS

Dizasta Vina – A Confession of a Mad Father Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – A Confession of a Mad Father Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled A Confession of a Mad Father, a number three song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Top Shelf

A Confession of a Mad Father Lyrics by Dizasta Vina

Nilimwambia hakuna kitu ataniambia,
Nikifa hakuna kitu nitamwachia.
Nilimwambia anaitia aibu familia,
Nilipenda mtoto ila tangu nimzae nilijutia.

Nilimwambia anastahili fimbo,
Anastahili msiba mbaya usio na maziko.
Asikae mezani, asishike sahani au kijiko,
Asitumie jina langu la mwisho,
Nilimchukia sana.

Nilimwambia asiniite baba,
Aliponiita hata bahati mbaya nilimchapa.
Sikumpa mahitaji, hamu ya mtoto iliniisha ghafla,
Alianza shule sikulipa ada.

Waliponiuliza nilimkana hadharani,
Nikasema hata kufanana hatufanani.
Nilimwambia simpendi, ni bora ningezaa hata Nyani,
Nilitamani nimgawe kwa jirani.

Nilimpeleka kwenye misa za kilokole,
Nilimchapa viboko vya kutisha kwa Mkole.
Habari zake zilitambaa, nilipewa pole,
Nilihama mitaa kuepusha watu kuninyooshea vidole.

Nilimuwekea mifano kadhaa ya kubuni,
Kwamba kuliko yeye bora ningezaa hata Mhuni.
Nilimwambia namwona kama Chawa au Kunguni,
Alinipogusa bahati mbaya nilinawa kwa sabuni.

Sikumpenda, nilihamishia chuki kwa Mama yake,
Niliona laana kuleta mtoto wa aina yake.
Sikutaka kumwona wala kumjua katu,
Na nakiri, nilishajaribu kumuua mara tatu.

Hakuwa na marafiki, tulimtenga ndugu,
Tuliamini ilikuwa ni laana toka kwa Mungu.
Alinikimbia, sikutaka kusikia sauti yake,
Sikuwa tayari kuuafiki utofauti wake.

Tulimweka kwenye taasisi bila idhini,
Alelewe akifanyiwa uhakiki wa kidini.
Kilichofanya nimwone ni mzigo mara mbili,
Ni pale taasisi zilipomshindwa kumbadili.

Tofauti ya haiba na hisia,
Sikuwa tayari kamwe kuukubali uhalisia.
Achana na vipigo vikali, kumnyima chai,
Ilibakia kidogo nimzike akiwa hai.

Nilikomaza chuki kwa kutumia jadi na dini yangu,
Au itikadi ya jamii yangu.
Nilifurahi kuona hana mahala pa kwenda,
Maana sio marafiki hata ukoo ulimtenga.

Hawakutaka wakae naye,
Vitabu vya Mungu vilishauri auwawe.
Nilikesha kuomba Mungu aibadili tabia yake,
Alipopita karibu nilimtemea mate.

Nilimwita majina ya kutosha ya kishezi,
Mara boga, mara mboga, mara shoga, mara ndezi,
Mara mzoga, nyoka asiye nyooka kwa malezi,
Nilitamani hata nafsi ingemtoka niimbe tenzi.

Niliamua kufanya maamuzi magumu,
Nikamfunge porini kisha nimnyweshe sumu.
Nikaandaa nyezo, nikanunua na kamba,
Nikaenda chumbani nikakuta barua kwenye kitanda.

Inasema:
“Mi ni mtumwa wa maumbile kiasili,
Iliyonizidi nguvu kihisia, kiakili.
Natamani ingekuwa rahisi kubadili,
Na kwa bahati mbaya Baba hukuwa tayari kujadili.”

“Nisamehe sana Baba,
Muda hautoshi kukuomba msamaha mara saba.
Kwakuwa nimeshindwa kuwa jinsi we unataka,
Najitoa uhai ili nikuondolee dhihaka.”

Dizasta Vina – A Confession of a Mad Father Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment