LYRICS

Dizasta Vina – Chupa Moja ya Ziada Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Chupa Moja ya Ziada Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Chupa Moja ya Ziada, a number six song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Mbuzi

Chupa Moja ya Ziada Lyrics by Dizasta Vina

Kalala chini, ubongo na fuvu vimetengana,
Hatoi sauti, hana hata nguvu ya kulalama.
Macho yetu yanagongana, ya kwangu yanaona haya,
Natamani kufumba maana naona uchungu kumtazama.

Ni butwaa, siwezi eleza hali yake,
Mifupa imezagaa kadhaa haipo mahali pake.
Waungwana wamejaa, wanauliza ka’ mi’ timamu,
Damu nyingi, nataka niamini ni filamu.

Hata nikifumba macho, naona jambo hili hili,
Nafsi yangu inahofu, na inatukana kwa siri siri.
Ameumia, siwezi kumtazama mara mbili mbili,
Mguu mmoja umetengana na kiwiliwili.

Kweli nimeamini utu wa mtu ni uhai wake,
Mja amelala, watu wamewahi karai lake.
Wengi wanatabiri tanzia bila kuficha,
Wema wanalia, na mabazazi wanapiga picha.

Amechanika nyama, kuonyesha nyama si tunu,
Anapata maumivu kabla hajaikumbata huru.
Anaonyesha kuwa mwili ni kasha lisilodumu,
Na kujua siku ya uhai kutoka ilivyo sumu.

Mtoto wake analia, ameisoma ajenda,
Kuwa baba uhai umetoka, na roho yake ishakwenda.
Anahitaji uthibitisho, na picha inajieleza,
Ananiona mimi, nami sina ninachokiweza.

Natamani niamke, nigundue picha nicheke,
Au labda naota ndoto ya kutisha nikeshe.
Huku wapita njia wakipiga kelele,
Kuona mtoto anakuwa yatima milele.

Chupa moja ya ziada,
Chupa moja ya ziada.

Nilipigiwa simu ikisema njoo baa,
Maana mtungi wa nyumbani haunogi.
Nikalewa kisha nikataka kuondoka,
Mpumbavu mwingine akasema “one for the…”

Chupa nikazipanga panga,
Mfuko ulipokauka wakanijaza.
Nikanywa nikijitapa kama mjanja,
Wana wakipiga kelele kuniita — mwamba, mwamba.

Sikio la mlevi likashika habari,
Sifa walizonipa zikanishika hatari.
Sikuwaza kuwajibika, kuwa nani nitamuumiza,
Nilikuwa mbinafsi kiasi, nilishindwa kujali.

Labda ningebakia kwenye kijiwe nongwa cha Biafra,
Ninywe kahawa nikisikiliza soga za siasa.
Ningekunywa kidogo labda nisingerudia,
Nimeua mpita njia sababu ya chupa moja tu ya ziada.

Nimefanya kosa, na muda unakwenda hasa,
Hasa nitaongea kipi? kipi nitaeleza sasa?
Sababu chupa moja tu ya ziada,
Mke anamkosa mume aliyempenda,
Mtoto anampoteza baba.

Maji yameshamwagika, nani wa kunifundisha lugha?
Niseme kwa nani, ama nani wa kuunganisha nyufa?
Nani wa kuujuza umma kuwa nami najuta nafsi?
Nani asimamishe siku, kisha akaurudisha muda?

Malipo gani yakurudisha pumzi kwenye mwili?
Uamke tena? uhai hata kwa hela tu haukopwi.
Adhabu gani itamfaa mpuuzi kama mimi,
Asiyejua maana ya pumzi?
Maana hata jela tu hainitoshi.

Hata nikiamua kufunga na kuuungama,
Siwezi kuzuia uuma wa watu wakiungana.
Kuamua kumwaga damu kwa mja nilie na laana,
Nife nilipe deni kwa hii dhuluma niliyoifanya.

Muda umesimama, moyo unaingia baridi,
Nimemgonga na gari, picha inanijia saa hizi.
Mja anakata roho, picha inayoingia zaidi,
Ni kuona vibaka wanaiibia maiti.

Chupa moja ya ziada,
Ziada, ziada, ziada, ziada, ziada…
Chupa moja ya ziada.

Dizasta Vina – Chupa Moja ya Ziada Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment