LYRICS

Dizasta Vina Ft Baraka The Prince – Uwaridi Jeusi Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina Ft Baraka The Prince – Uwaridi Jeusi Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Uwaridi Jeusi, a number nine song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Waridi

Uwaridi Jeusi Lyrics by Dizasta Vina Ft Baraka The Prince

Williams Shakespeare said, speak low if you speak love
No, I speak loud because love is war
And war is really loud
I’ll tell you why — the course of true love never did run smooth
Love is rough, some Cupid kills with arrows
And some with traps, and the point is
You die at the end of the day

Yeah, nilishare chozi alipolia
Baridi ilipomfikia sikukimbia
Nilishare koti aliponiletea pozi
Niikamzoe nikamkosea
Akanuna, msamaha nikamwombea airport

Wafanyavyo wazungu, nikaonekana mpuzi mkuu
Dhahama mbele hadhara, uzushi tu
Upendo wa dhati ilikuwa script
Ilikuwa ni uchi, vyote ilikuwa movie tu

Nikajajua wamebaki kwenye simulizi
Wale wakubaki njia kuu
Najua nilisema hivi, nao wakanijia juu
Tofauti ya hayo maigizo na uhalisia huu
Kupendwa kwa hali na mali ni kwenye tamthilia tu

Tulioana na picha ikaenda slow slow
Aliniambia ananipenda kweli, ndivyo
Alivyomwambia Fredy, kisha akamwambia Francy
Nami nikamwambia Betty, Fetty na Nancy
Tukaenda draw draw

Hakuna aliyejiforce, hakuna aliyejilazimisha
Kati yetu hakuna aliyemdoshea machozi mwenzie
Hakuwa yeye aliyeziwinda pochi za mashemu
Au mimi mwenye namba nyomi za mademu

Tukajua kuwa mahusiano sio kitu simple
Aliniumiza, nikamuumiza, tukaishi hivyo
Mwanzoni tulichorana mpaka matching tattoos
Leo wote ni washenzi, nafuu hatukuitikia wito

Chorus
Nikikumbuka huwa nataka kulia
Watoto na wakubwa wanaaga dunia
Kwa sababu wanaumia, mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya
Matajiri walisaza dunia
Hata masikini wanaotanga na njia
Wako ndani wanaumia, mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya

Ukweli hakuwa mbali kuujua
Kati yetu hakuna aliyekuwa tayari kukua
Niliokota vidonge vya kutoa mimba nikauchubua
Akakuta condom kwenye nguo zangu kila alipofua

Tukaacha kufanya kwa siri, kufanya salama
Kila akitaka aishike hatamu
Alilala na rafiki yangu Rashidi, bosi wangu kazini
Nikalala na dada yake wa damu

Mapenzi noma, nakuhusia
Shangazi, wajomba wanajutia, niulize mimi
Mapenzi kidonda utaumia
Yalimtesa kocha wa dunia, Mwijuma Muumini

Hii game ikikushinda buni yako
Wanandoa wanafunga ndoa, hawafungi mlango
Wakimaanisha yeyote anaingia
Nakumbuka hata nikimshika, nikimbusu kwa hisia
Hafumbi macho

Mapenzi karaha, nyie msije hata kusikia
Nishaona wajanja wanaziacha career
Ninapoona wanafunzi nao wanataka dandia
Haki ya mama huwa nataka kulia

Nishaona na mke wangu ana pete kidoleni
Akiwa na mshefa pembeni, anasaini lodge anatimba ndani
Anaingia, mi natoka mwili hoi
Pembeni nikiwa na mrembo ananiita honey

Akivua pete kwenye milango ya bar
Sikuchukia, mi mwenyewe nina mipango kando kadhaa
Ngoja niwaambie wale wa true love, msitaanie
Kumpenda binadamu ni ushujaa, nyie

Kila alichofanya dhidi yangu nililipa
Twende sawa, mchongo ndo huo
Alichukua mababa, mpaka wenye umri wa dingi yangu kuniumiza
Nikachukua vitoto vya chuo

Aliingilia kushoto, niliingilia kulia
Alipobuni uongo, nami uongo niliujulia
Alirudi nyumbani na tai za wanaume tilatila
Nikarudi nikiwa na love bite bila bila

Na umalaya wangu na koti la mtumba
Bendi nikakodi na maua rozi ya size kubwa
Nikampeleka mke wa mtu lodge
Nikazuga ka sijaoa na mishumaa
Ilibaki kidogo nichome nyumba

Hizi romance ni filamu tu
Mara nikikuona nasinzia, sijui napata homa ya dunia
Ni filamu tu
Kutembea slow motion hatuwezi
Ukimkiss kwenye mvua, mvua hainyeshi — ni filamu tu

Alishindwa kuuchukua moyo wangu auwekeze
Nilishindwa kumfanya awe wife anipendeze
Ujanja umeisha, uhalisia umeturudisha ndani
Tumeathirika, hatujui ndani kauleta nani

Ushauri kwa kina dada — mahusiano ni vita
Wanaume wasafi wapo kwenye vitabu vya kuandikwa
Ukiolewa na ndoa ikayumba, jiongeze
Mwanaume ni mchafu, ukitaka aliyetukuka, mtengeneze

Ushauri kwa kaka — mahusiano si hija
Wanawake wasafi wapo kwenye filamu za kuigiza
Kwa hiyo ndoa yako inapopinda jiongeze
Mwanamke shetani, ukitaka malaika, mtengeneze

Chorus (Repeat)
Nikikumbuka huwa nataka kulia
Watoto na wakubwa wanaaga dunia
Kwa sababu wanaumia, mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya
Matajiri walisaza dunia
Hata masikini wanaotanga na njia
Wapo ndani wanaumia, mama wanaumia
Wanaumia mapenzi mabaya

Dizasta Vina Ft Baraka The Prince – Uwaridi Jeusi Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment