LYRICS

Dizasta Vina Ft G Nako – Utaliimba Jina Langu Lyrics

Dizasta Vina Ft G Nako – Utaliimba Jina Langu Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Utaliimba Jina Langu, Featuring G Nako.

SIMILAR: Dizasta Vina – Fanani

Utaliimba Jina Langu Lyrics by Dizasta Vina Ft G Nako

VERSE I

Sitauona uzuri wa mataa
Maua na uturi au usafi wa suti nitayoivaa
Mtajadili kama nilifunzwa chuki na hii njaa
Au msamaha niliomba baada ya kuivunja mioyo kadhaa

Mikono yangu haitaishika sayari
Historia nitakuwa nimeimaliza tayari
Naenda upande wa pili, asili itanipiga kabali
Nitakuwa nimeimaliza safari

Maombi hayatakidhi nisimame soja
Nanyi mtaijua hadithi hii ya upande mmoja
Pesa na ustaa hautanibeba
Itaandikwa “mwisho wa kila shujaa ni jeneza”

Siwezi kimbia udhuru hata nikibadili njia
Nakuwa huru dhidi ya kufuru za hii dunia
Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa ama mtaliimba jina langu?

Siku hii iwakumbushe kuwa kesho mbali
Iwakumbushe havina maana pesa, mjengo mkali
Vyeo, urembo na pesa nyingi
Ni kiburi cha hii pumzi, pumzi ambayo ni temporary

Sijui nitamwachia nani mama yangu
Ikiwa nitaacha dini, itikadi ya chama changu
Cheo changu hakitakuwa na maana tena
Nitalala gizani japo mtajua nimelala pema

CHORUS

Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli

Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia…

VERSE II

Nitalala sitahisia karaha zako
Sitasikia matusi, sitasikia msamaha wako
Sitasikia kicheko au kilio cha unafiki
Ubongo hautatafsiri mawimbi ya sauti yako

Nini maana ya chuki yako kwangu ikiwa
Siwezi amka hayafungukia macho yangu
Nitakuwa mbali peke yangu futi sita
Hata kivuli hakiwezi kuwepo kando yangu

Ufedhuli ni kibari cha hii nguvu
Ya nyama na mifupa ambayo ni mali ya wadudu
Ipo siku utaimbiwa pambio na wadau
Kisha ndugu watagawana salio na kusahau

So, nataka nikifa msinidai
Msilie, msherehekee niliyoyafanya nikiwa hai
I wonder kama mwangaza usipotimba himaya yangu
Je utafurahi nikifa ama utaliimba jina langu?

Minara yangu imara itadondoka nayo
Sauti yangu ya gharama nitaondoka nayo
Masikini roho yangu mimi
Itaenda wapi pindi mwili utakapogusa
Udongo mkavu chini

Mwangaza hautafika himaya yangu
Je mtafurahi nikifa ama mtaliimba jina langu?

BRIDGE

Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi…

CHORUS (Outro)

Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi ni dhaifu
Na kweli

Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia…

Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(Dunia inashindwa kunilinda)
Kwakuwa niko mbali na ukweli na mimi
(Ni dhaifu na kweli)

Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia inashindwa kunilinda
Dunia…

Dizasta Vina Ft G Nako – Utaliimba Jina Langu Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment