Dizasta Vina – Hatia VI Lyrics
LYRICS

Dizasta Vina – Hatia VI Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Hatia VI Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Hatia VI, a number seventeen song from his album titled A Father Figure Album.

SIMILAR: Dizasta Vina – Fanani

Hatia VI Lyrics by Dizasta Vina

Salamu baba mi mwanao
Naandika waraka kwa maana hutaki vikao
Nahitaji majibu nikihisi ni haki yangu
Najisikia vibaya kusikia unaishi na sina ngao

Nimeshika kalamu haya maandiko
Yametoka mahala timamu palipo wito
Sijatumwa na wenzangu hii ni akili yangu mwenyewe
Waraka huu ni salamu zangu za mwisho

Nina akili najua mambo yanapokuwa mrama
Natambua uhalisia nazitambua njama
Pengine nitachokisema kitazua laana
Nitaibeba lawama kwa kujifanya najua sana

Ndugu zangu wanachosema sisawiri
Mpaka wanahisi nimeanza kuchezwa na akili
Hata wakitaka kunitenga sibadili
Ulinitenga jana siogopi kutengwa mara mbili baba

Majirani wanatamba kukuongelea
Wakisema sina baba na kazi ya kukusemea
Na ukweli ni kwamba ni utata sana kukutetea
Maana shida ilinibana na baba haukutokea je

Utachukia nikiegemea penye power
Au utanipa hatia mikono michafu niende nawa
Nipo mbele yako kamwe siigizi uwepo kama wewe
Basi jibu kero zangu twende sawa

Juzi nilikuhonga maua, Jana nikakuhonga na tena
Subira gani isiyo na heri shaabash
Nimechoka kuchomwa na jua
Jionyeshe leo nimechoka barua
Nimechoka barua

Barua zako zinahubiri ushindi
Kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki
Na cha ajabu maadui ni wa kurithi
Chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithi

Njoo ulee wagonjwa ndo’ uongee kuhusu upendo
Tuvae bendera moja ndio uongee kuhusu uzalendo
Msamehe aliyekufanya uondoke ndo’ uendeelee
Kuhubiri kutubu kuhifadhi na kusamehe

Jenga daraja baba mahusiano yanavunjika
Hamna faraja huoni wanao wamekaza ndita
Jenga imani tena kwa wote waliogadhibika
Jenga kama ambavyo uliijenga hii nyumba kwa siku sita

Haukuja tulipopita kwenye
Miaka 400 ya utumwa njaa maradhi vita giza nene
Nipe sababu moja vipi nikujali vipi nikupende
Sababu moja tu kukusikiliza wewe

Nyumba uliyotupa ina twiga ina ndovu
Majirani warembo wenye figa na vitovu
Vinavutia, kuna dhahabu kadhalika
Zinatutajirisha ila zinafanya tuwe waovu

Huu uchafu atatetea wakili gani
Siri ipi na asili zetu hazilingani
Japo akili mali sio siri asili ghali
Tunamwagana damu kugombea rasilimali

Tunaisha kwa wivu wetu
Tunasita kwa uvivu wetu
Tunazikwa na mbinu zetu
Tunapikwa na kinu chetu

Tunasita kushika insha
Tunapitwa na wapita njia
Umoja unavunjika huku
Tumeshikwa na simu zetu

Sina tofauti nna watoto kama wewe
Napata changamoto kama wewe
Kama soja kwa ajili yao napambana naposhindwa
Tunateseka pamoja Kwani sina roho ndogo kama wewe

Asante kwa ulezi dhanifu
Asante kwa kuniandikia sheria za kishenzi
Kwenye pegi nadhifu asante kwa kuniacha stendi
Nikisubiri mapenzi ya ahadi nakesha nikienzi wasifu

Asante kwakuwa mbali nami
Kiasi nina shaka kuwa haujui nina hali gani
Umeacha barua ndefu ambayo sijui kama yako
Au ya kufoji na bado inahitaji mkalimani

Ona Napanga mipango ya kijinga
Ona naghafirika nafanya uliyopinga
Ona napinda napika chuki wenzangu
Wenye nyumba ndinga maana mimi ngano tu inanishinda

Huko mbali umejitenga nashanga
Haujui kinachosemwa na jamaa
Haujui usafi ni ndoto, ndoto iliyotengwa na ridhaa
Haujui ni ngumu sana kuwa mwema ukiwa na njaa

Haujui kuhusu adha za dunia
Haujui kero maana maudhi yalipokupata ukakimbia
Haujui kuhusu kifo na magonjwa haujui kuhusu
Insha na maandiko haziwezi tibu hivi vidonda

Ndugu zangu umewajenga kwa vpaji
Wapo kadhaa umewapa pesa za mitaji
Wengine warembo wenye vyeo wenye hadhi
Sisi tusio na hali tulalamike kunyimwa haki

Imechafuka taswira inaenda slow focus
Pengine its all bogus
Pengine I’m mad
And I’m talking to my own conscious

Labda haupo ni hadithi tu
Na kama ulifikia kifo ufalme umefika mwisho
Haurudi tena so nawaza
Lini utakuwa mwisho wa uhanithi huu

Uzazi sio simple but I still care
Nina watoto shida zipo and I’m still here
Matatizo yanapokaba kwenye shingo sikimbii
Napambana mpaka mwisho like a real man

Sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo
SikujuI sura maana hauna picha Google
Nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma
bakshishi niwe ninajua kuwa zinafika huko

Wenye majoho rangi nyeupe na dhahabu
Wana barua zako za tafsiri za kiarabu
Wanasema wanakujua kuliko ninavyokujua
Nikiwatilia shaka wananiita mwanaharamu

Je ni kweli uliwapa uwakilishi
Ni ngumu kuwasadiki hasa ukiwadadisi
Kama wanaongea uhalisi au wanachonga sera
Sometimes hawafundishi wananiomba hela

Thibitisha hizi hifadhi si uwongo
Uliowaacha wana nishani za,,,,

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment