Dizasta Vina – Not a Hero Lyrics
Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled Not a Hero, a number two song from his album titled A Father Figure Album.
SIMILAR: Dizasta Vina – A Father Figure
Not a Hero Lyrics by Dizasta Vina
Nikiwa narudi kutoka kwenye sherehe za mahafali,
Nikakatiza kwenye mtaa wenye taa mbali,
Kwahiyo giza kubwa, nikiwa na tahadhari,
Huku nikitafakari.
Vipi maisha yatakuwa? shule nimeua, naingia mtaani,
Je, nitapata kazi au nitalamba nyasi?
Au nitaingia shambani ama nitaishika gun?
Mawazo kichwani kama nitaipata mali.
Mbele namwona Lily, tunaenda njia moja,
Maana tunakaa mtaa mmoja, just kona mbili.
Bado alikuwa amevaa joho la kuhitimu,
Na mkononi simu, akibofya nini…
Alitembea kulia kushoto, mwendo wa madaha,
Sometimes aruke kidogo kuonyesha furaha.
Aliyapiga majani kwa fimbo,
Nilisikia sauti kwa mbali akiimba wimbo.
Nilitamani kumwita, niliogopa,
Nilibaki nyuma, nilizuga sikumkaribia.
Maana kitambo ninamjua ila daily tu navunga,
Vile mazoea hatuna na namfagilia.
Haikutokea siku nidiriki kuthubutu hata,
Kumfata kumwomba contacts.
Japo tunajuana, tulisoma sekondari,
Msingi na vidudu, kumfuata niliona woga.
Moyoni napiga kelele, “Come and save me,”
Nazama kwenye bahari hii ya mapenzi.
Pengine pia alinihusudu ila sikuwa kamili,
Pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri.
Aligundua kuwa namfata kwa nyuma,
Aligeuka aliniangalia nikauchuna.
Alinipungia mkono, niliupunga pia,
Lakini bado nilivunga, sikumkaribia.
Hofu iliufunika upendo wangu,
Kila nikimwaza yeye, niliiwaza kesho yangu.
Nilitamani mrembo asimame nimsemeshe soga,
Labda mikono tushikane tutembee pamoja.
Alikuwa karibu pia alikuwa mbali,
Nilijua kuwa naye penzini ingekuwa zali.
Nilitamani kumfata nimweleze nilichowaza,
Nilishindwa ’cause…
(I’m not a Superhero)
Ile haikuwa filamu so, I was not (a Hero).
Ushujaa ni dhahania, uhalisia hauna (Hero).
(Yeah yeah yeah, I’m not a Superhero)
(Yeah yeah yeah).
Alitembea mbele, nilibaki nyuma,
Mimi na moyo wangu mpweke uliojaa ufa.
Nikifurahia jinsi asili ilivyomuumba,
Nikijua dhahiri hofu haitazaa tunda.
Niki-fantasize siku atakuwa wangu,
Nikiomba mizimu ya mapenzi isikie dua zangu.
Na baridi ilinipiga ila haikufua dafu,
Nilikuwa mkavu.
Nilizidiwa na mawazo, hisia nilikuwa nazo moyoni tele,
Masomo tumemaliza, nitakuwa simwoni daily.
Mawazo nilipoyarudisha ndipo hofu ikanishika,
Niligundua Malaika yule simwoni mbele.
Sikusogea karibu, nilishapagawa,
Hisia ziliniambia kuna kitu hakikuwa sawa.
Nikasikia purukushani, nikaingiwa hofu,
Nikavamia karakana chini ya gari bovu.
Nikajificha.
Nikaona vijana wamefura dhambi,
Mkononi mapanga, usoni wamekula Maski.
Wakamwingiza Lily kwenye karakana,
Hawamkumvua nguo zake, walizichanachana.
Nilimwona Lily, Lily aliniona mimi,
Tukagonganisha macho ila sikutoka chini.
Akijua kuwa nina mpango wa kumsaidia,
Niliogopa nikamvungia, akaanza kulia.
Maninja walimbaka mmoja mmoja,
Wakigombea kuanza, hawakutaka ngoja ngoja.
Nilitamani muda urudi nimsemeshe soga,
Labda asingevamiwa kama tungekuwa pamoja.
Akipiga kelele “Come and save me,”
Sauti yangu hata kutoka tu haiwezi.
Pengine yale yalinihusu ila sikuwa kamili,
Pengine nilikuwa na nguvu ila sikuwa jasiri.
Alininyooshea mkono, sikuunyoosha pia,
Alitamani nitoke niende kusaidia.
Hofu iliufunika upendo wangu,
Nilipoyaona mapanga, niliiwaza kesho yangu.
Alikuwa karibu, ila alikuwa mbali,
Kumtoka kumwokoa, pengine ingekuwa zali.
Nilitamani kumfata, nimwondoe kwenye mkasa,
Nilishindwa ’cause…
(I’m not a Superhero)
Ile haikuwa filamu so, I was not (a Hero).
Ushujaa ni dhahania, uhalisia hauna (Hero).
(Yeah yeah yeah, I’m not a Superhero)
(Yeah yeah yeah…)
Dizasta Vina – Not a Hero Mp3 Download
More hit songs from Dizasta Vina;
