Dizasta Vina – The Last Confession Lyrics
Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania, Dizasta Vina unlocks a new song titled The Last Confession, a number nineteen song from his album titled A Father Figure Album.
SIMILAR: Dizasta Vina Ft Benno Mwampamba – Get Better
The Last Confession Lyrics by Dizasta Vina
“Baba, let me get this clearly, ni wewe kweli umefanya hivi?
Na kama ni wewe, ni kwanini ulifanya hivi?
Unajua, hatuwezi kukusaidia.
Sio dada Mori au kaka Levo, ikiwa hatutajua the real story.”
Nilipozaliwa nilijua ulimwengu ndio utanionyesha dira
Sikujua dini wala kabila
Sikuwa na itikadi, desturi wala mila
Wala chama, niliujua upendo kabla ya hira
Nilionyesha tabasamu hata kwa ambaye simjui
Kabla ya ulimwengu haujanipa maadui
Kabla sijajifunza kuchagua
Niliujua umoja na ulimwengu ndo’ ulionifunza kubagua
Nafsi haikuweza kutamani
Nilifundishwa pesa ina thamani
Kabla ya utu, nilijali nilimpenda Mkyuba na Mjerumani
Hata kubagua rangi nilifunzwa tu ukubwani
Sikutunza kisasi nilipofanyiwa njama
Ya dunia yalinighasi nikamkimbilia mama
Jamii ilizembea walimwengu wakashindwa kunikanya
Na wazazi wakanitishia laana
Sikuujua uongo, sikuujua ufitini
Nilifunzwa na hii dunia sikuwa mchoyo kwa idhini
Dunia ilinipa ndugu wakanidhamini
Kabla kunifundisha utu wakanirithisha dini
Niliigawa thamani kwa kuzingatia upendo
Kabla dunia haijanifunza kuutamani urembo
Wakati mdogo sikuijua mipaka ya wahisani
Nilivunja nikaenda kucheza mpaka kwa jirani
Eeh!! sikuona ishu aisee
Kumbe jirani alikuwa na bifu na mzee
Mzazi alinipa kula sikuweza kuihoji haki
Bila hatia nikashiriki ugomvi wa wazazi
Ndipo nilipoijua chuki
Nikajua maana ya mipaka ya Marekani na Urusi
Sikujua kuongea nikapewa lugha ya matusi
Na kabila la Kihutu ili nimtukane Mtutsi
Nikamjua ndugu wa upendo anaitwa wivu
Nikayajua majivuno, kisha hasira, kisha bifu
Nikafichwa ustaarabu, nikafichwa haya
Nikapewa nguvu za miguu niende kuutimiza ubaya
“Ah Baba, unajua unaweza kwenda jela miaka mingi sana?
Hivyo kuwa direct basi.
Ukiweka pembeni falsafa zako, tunahitaji utuambie ukweli.
Why? why uliamua kufanya hivyo? kwanini?”
Asili imenipa macho nashukuru
Nione mabaya matamu, nione mazuri yanayonidhuru
Wazuri wanaojiremba niwapende
Ili nitoe jasho kisha nije niwape pesa wanitende
Ujirani uko wapi? siku hizi hatuchezi pamoja
Hatupigi soga, tunawekeana mageti
Hakuna kuombana chumvi
Kwakuwa kuna fensi, ukuta mkubwa na vihunzi
Tunafuga vikosi vingi vya kininja
Mbwa na majeshi na walinzi kujilinda
Mwanzo niliogopa simba
Sasa nafunga mlango maana hata binadamu ananiwinda
Nimekubuhu nimekinai maudhi
Naona mstari mwembamba kati ya uhai na mauti
Sikuchagua hasira au kinyongo kunishika
Nikalambisha udongo watu sita
Wa kwanza nilimpiga risasi mara tatu
Sikuuliza maana hakuvaa gwanda kama langu
Kiongozi akasema nisipigwe na bumbuwazi
Kutoa uhai wakati wa vita si uuaji
Nikajuana na mtu wa pili
Mungu wa dini yangu alimwita huyu kafili
Tulichukiana kiasi alitaka kunipiga
Nikamuwahi maana imeandikwa vita ni vita
Wa tatu alisahau chake changu
Njaa yake ilimleta kwenye shamba langu
Nikamkamata nikamziba mdomo asilete methari
Nikamfungua macho na sikio aujue ubepari
Wa nne na wa tano waliniletea ushenzi
Cheo kilikuwa kidogo wakati tulikuwa wengi
Ili wasije kufukua maiti, nikamuua wa sita
Alikuwa shahidi
Dizasta Vina – The Last Confession Mp3 Download
More hit songs from Dizasta Vina;
