Dizasta Vina – Wachezaji wa Timu Lyrics
LYRICS

Dizasta Vina – Wachezaji wa Timu Lyrics

ALBUM MP3 DOWNLOAD Dizasta Vina - A Father Figure MP3 DOWNLOAD
Dizasta Vina – Wachezaji wa Timu Lyrics

Tanzanian hip hop musician and producer from Tanzania Edger Vicent Mwaipeta famous as Dizasta Vina unlocks a new song titled Wachezaji wa Timu.

SIMILAR: Dizasta Vina Ft Kaa la Moto – Achia Jala

Wachezaji wa Timu Lyrics by Dizasta Vina

Wanasema duniani kuzimu
Kwanini ukeshe kushika protocol wakati
Ulaji muhimu
Watu wanachohifadhi ni mbinu
Kucheza kulia kushoto ila wote ila wote
Ni wachezaji wa timu
Chumba kilijaa njemba za kisasi
Walipanga vifaa ka’ wanakwenda kwenye kazi
Palikuwa jitu juu meza yenye glass
Limeshika tissue kusafisha chemba ya risasi
Walijaa na maninja na ma bouncer
Wamevimba wenye sura za kutisha
Wamekausha,
Wamegadhibika mpaka amani ilijificha
Nilihisi mkojo unatiririka kwenye trouser
Sura za kutisha nafuu devils
Crate zimemwaguka utadhani sikukuu kesho
Kulikuwa kumejaa camera full angles
Huku warembo waki-twerk twerk juu ya pool table
Huku watemi wa ngenga wameketi
Mwonekano wa Rostam Bakhresa na Mengi
Palikuwa na mabegi ya cheda na chenchi
Yalikuwa mengi hata wachache kubeba hawawezi
Walikuwepo mabinti wamefanya line up
Mfano wa dinner set Sura ziko innocent
Zikionyesha zina majuto ya kusign up
Na baadhi yao walikuwa wadogo yaani minors
Babake Jesca alisimama kwenye chanja
Ametingwa kuchanganya plama kwenye ganja
Nikamsalimia hakuijibu salamu yangu
Akavuta beri kisha akapiga chafya mara saba
Kabla muda wake wa kumaliza
Akanyonga jani akapaka mate kwenye Lizzla
Akasnap vidole kuonyesha alikuwa Taita
Kumwita Mrembo na mrembo akaja Na lighter
Mrembo akamwashia kipuri wakapiga Puff mbili
Wakatoa moshi wakaanza kukiss pasi siri
Ka’ wacheza ngono mbele ya Binti yake Jesca na mbele yangu kiasi nafsi ikakosa tafsiri
Baba’ake aka-struggle kukumbuka jina langu
nikamwambia jina langu naitwa Toni Glove
Akauliza umemjua vipi binti yangu
Nikamwambia mi na jesca tumekutana kwenye coffee shop
Akaisogelea glass, akanywa kilichomo kisha
Aka-scan majibu
Ili kuhakikisha ninachokiongea fact, akasema sikujui unatokea wapi
Nikamwambia nimezaliwa hapa Nonde Sua
Nyumba no 77 kwa mzee Kilua.Akasema ninapiga simu mbili tatu kama hawakujui
Nitakushauri tu uombe dua
Akaja mtu akani-snap kwenye IPhone
Design kama anafanya michongo ya passport
Akainua uso nikaona umeweka ndita
Akatikisa kichwa kisha akaendelea ku-type more
Mkono wa jesca begani ukinipeti peti
Huku moyo wangu ukienda lesi lesi
Board guard wake wakinichekicheki
Mara wani-search mifuko mara wani-search begi
Nikaletewa maji ili nipoze kiu
Design hamu ilinikata mzee
Wasaidizi wakingiza jina langu kwenye simu ya kimtandao
Kunifanyia background check
Babake Jesca
Akanipa face look kisha
Akaomba simu sikubisha
Akaanza kukagua photo Akalog in kwenye social kunikagua Facebook Twitter
Ghafla ukimya ukaitawala nyumba
Wakati akili ikiwaza kufa
Nikitushwa Na yale mandhari yanayofanana na nyumba ya mafia mkubwa
Kutoka Kuala Lumpur
Akauliza je nipige down town
Maana najua kila mtu kule ukinidanganya bure
Nitakukausha kama kau kau mpaka uta shout shout
Jesca akasema Daddy calm down
Mi na Tony tayari tumependana
Amekuja kutoa mahari ili tuishi ka’ mke na bwana
Anaomba kibali anataka kunioa
Na kama utakubali basi soon tutafunga ndoa
Baba Jesca akaegemea kwenye kiti mwisho
Akashusha pumzi kwa masikitiko
Kwanini unadate na mtu hatumjui
Na unajua style ya kuleta hawa wakati ringi
mwiko
Jesca unajua hadhi ya hii business
Equation ya ndoa haifiti into this case
Kwanini usitafute a guy from inside
Ipo time utaleta ma-spy au ma-witness
Jesca akajibu daddy Tony Doctor
PhD holder chuo kikuu cha oxford
Anamiliki migahawa kadhaa hapa town
Analipwa vizuri na kipato kinamtosha
Namfahamu Tony sio mnoko
Na kwao wana uwezo sana baba yake don sio kitoto
Tumejuana miaka kadhaa ameshanikaa
Maana penzi nililolihifadhi moyoni sio kidogo
Babake Jesca akanicheki amenuna
Nikawa nimevex nimechuna
Moyo unaenda resi kama duma
Mabaunsa yapo next yametuna
Yakisubiri mechi hii kubuma
Nikamwona mshikaji ameshika panga bisu
Alikuwa busy anapanga vitu
Sura yake ilikuwa tayari kuanza bifu
Jesca akaniambia yule kaka’angu na ana anger issues
Akaja ameshika vipisi vya kete
Kisha akanidadisi si kibwege
akashout naskia harufu ya polisi kwa huyu bwege
Jesca akamuwahi akasema we’ chizi acha usenge
Akatoa syringe kwenye small bag
Akauliza unapendaga cocaine
Nikamwambia huwa situmii hizo zaga
Kaka’angu alitumia akabwaga akajibu okay
Nilihisi harufu ya casket
Kaka’ake Jesca alihisi mi’ shushushu akani-suspect
Nikahisi napokwenda sio
Moyo wangu ukienda mbio
Babake Jesca nae anahamaki
Baada ya kugundua nina camera kwenye kifungo cha shati
Akatoa bunduki nikahisi uhai wangu unaishia
Ndipo polisi wenzangu wakavamia

Dizasta Vina – Wachezaji wa Timu Mp3 Download

More hit songs from Dizasta Vina;

Leave a Comment